Sunday, 12 January 2020

WAZIRI DKT. KALEMANI AKAGUA TENA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA MAJI WA JULIUS NYERERE MW 2115, AAGIZA WAKANDARASI KUHAKIKISHA WAFANYAKAZI WAO WOTE WANAHAMIA ENEO LA MRAD



NA MWANDISHI WETU, RUFIJI

WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, amefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere Mw 2115 (JNHPP) uliotimiza mwaka mmoja tangu kuanza kwa utekelezaji wake.

 Dkt. Kalemani ameridhishwa na hatua mbalimbali ambazo mradi huo unaotekelezwa kwenye mto Rufiji kwenye mpaka wa mikoa ya Pwani na Morogoro umefikia tangu kuanza kwa ujenzi wa mradi. 

Aidha, alitoa maagizo kwa Wakandarasi kuhakikisha Wafanyakazi wao wote wanahamia eneo la mradi, huku akitoa mwezi mmoja kwa wafanyakazi wengine wa mradi wawe wamehamia. 

"Wafanyakazi wote wakae eneo la mradi, hii itaharakisha mradi kukamilika mapema na haraka", alisema Dkt. Kalemani. Pia, alisisitiza kazi zote zinazohusu utoaji huduma zifanywe na Makampuni ya kitanzania ikiwemo Wakandarasi wasaidizi. 

Mkataba wa ujenzi mradi wa Julius Nyerere ulisainiwa Desemba 12, 2018 Ikulu Jijini Dar ea Salaam ambapo Mkandarasi alikabidhiwa eneo la mradi Februari 14, 2019 na kuanza kazi za maandalizi ya ujenzi kwa kipindi cha miezi sita, ambapo mwezi Juni 2019 alianza rasmi kazi za ujenzi. Mradi wa Julius Nyerere unatarajiwa kukamilika 14 Juni 2022
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, (kushoto), akimsikiliza Mratibu wa ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius NyerereMw 2115 (JNHPP) wa mto Rufiji mkoani Pwani, Mhandisi Steven Manda wakati alipofanya ziara ya kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi  huo.
 Dkt. Kalemani (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kushoto kwa waziri), wakati wa ziara hiyo leo Januari 12, 2019.





Share:

YANGA YATANGAZA KOCHA MPYA

Share:

Nyalandu:Tutahakikisha Chadema Tunashinda Na Kuliongoza Jiji La Dodoma Mwaka Huu 2020

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA]kanda ya kati,Lazaro Nyalandu amesema katika mwaka huu wa Uchaguzi mkuu,2020 Chama hicho kimejipanga kushinda na kuliongoza jiji la Dodoma.

Akizungumza leo Januari,12,2020 jijini Dodoma na Waandishi wa habari Mhe.Nyalandu amesema Kipaumbele cha  CHADEMA kanda ya kati ni kuhakikisha jiji la Dodoma linakuwa mikononi mwa Chama hicho.

"Kipaumbe No 1 cha CHADEMA kanda ya kati ambapo mimi naongoza ni kuhakikisha tunaliongoza  jiji la Dodoma,ambalo ni makao makuu ya nchi yetu kama ilivyo desturi ya CHADEMA ni kuchukua kwanza eneo ambalo watawala wamekaa.Kama mnakumbuka mwaka 2015 jiji la Dar Es Salaam lilichukuliwa na CHADEMA"amesema.

Aidha,ameendelea kusema "Tutashinda kwa mbinu zinazojulikana na mbinu zisizo julikana hivyo Wanachama tuhakikishe tunaipa raha CHADEMA"amesema.

Pia Mwenyekiti huyo wa CHADEMA kanda ya Kati amesema kuna uhitaji mkubwa wa kuwa na tume huru ya Uchaguzi hali itakayoipa heshima Kubwa nchi ya Tanzania  na Kuisaidia CCM itakapokuwa Chama cha Upinzani.
 
"Kuna Msisitizo mkubwa sana ambapo pana uhitaji wa tume huru ya uchaguzi ,Demokrasia yetu itakuwa ya kuigwa Afrika Mashariki na ukanda wa SADC kwa ujumla"amesema.

Katika hatua nyingine Nyalandu amesema  mchakato wa kurekebisha daftari  la Mpiga kura lifanyike kwa ueledi kabla ya uchaguzi huku akiomba sheria ya vyama vya siasa kufanyiwa marekebisho hali itakayoruhusu wanasiasa  na asasi za kiraia kuruhusiwa  kushiriki kuhamasisha watu kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura huku pia akisisitiza vyombo vya Ulinzi na Usalama kutojihusisha na Masuala ya siasa.

Sanjari na hayo Nyalandu amesema CHADEMA sio chama cha kulalamika tu na kuwaomba wanaohusika na Masuala ya kilimo kuhakikisha wanasambaza pembejeo za kilimo katika kipindi hiki cha  Mvua ili wakulima walime kwa wakati hali itakayosaidia kupata chakula cha kutosha.


Share:

Naibu Waziri Bashe ataka wakulima wa mahindi wasiingiliwe kwenye uuzaji wa mazao yao

Na Amiri kilagalila-Njombe
Serikali imeendelea kuwapa uhuru wakulima wa zao la mahindi nchini kwa kuuza mazao yao sehemu yoyote na kwa bei yoyote bila kuwekewa vikwazo kama ilivyo kwa mazao mengine ya chakula na biashara.

Naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe akiwa mkoani Njombe wakati akizungumza na wakulima wa matunda ya parachichi na mahindi katika ukumbi wa Turbo mjini Njombe,amesema hakuna kiongozi wa serikali atakayempangia mkulima katika uuzaji wa mazao.

“Kama naibu waziri wa kilimo debe la mahindi hata muuze elfu hamsini hakuna mtu atakayewaingilia katika kuuza mazao yenu.lazima tuiheshimu sekta ya kilimo kama sekta zingine zozote”alisema Waziri Bashe

Aidha waziri Bashe amewataka wananchi watakaoshindwa kutumia unga wa mahindi kwa sababu ya ghalama wawe huru kununua zao jingine la chakula kama mchele au mihogo kuliko kumnyanyasa mkulima wa Mahindi,na kuingilia sekta ya kilimo huku akiwataka wakulima kuongeza uzalishaji.

Katika hatua nyingine ameagiza kuundwa ushirika wa wakulima wa parachichi mkoani Njombe kutoka mtandao wa wakulima wa parachichi ili waweze kukopesheka na kutanua kilimo hicho kutokana na uwingi wa wananchi walioweza kuhamasika .

“Nimefurahi sana kuona huu umati unaolima parachichi,tunataka huu mtandao ugeuke kuwa chama cha ushirika cha wakulima wa parachichi na TADB ili mkopesheke lazima muwe kwenye ushirika,na mkiwa kwenye ushirika tutatengeneza mradi wa kutengeneza soko la uhakika na kujenga miundombinu ya kuhifadhi mazao ili mnunuzi anapokuja kununua asinunue mazo yaliyoharibika”alisema Bashe

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amesema amekwisha weka utaratibu wa kuwashirikisha wakulima wa parachichi na na wanunuzi wa zao hilo ili kuweka utariatibu wa uuzaji wa parachichi utakaomuhakikishia mkulima  bei ya uhakika pamoja na kuwa tayari kushughulikia swala la uundaji wa ushirika.

Erasto Ngole ni mmoja wa wakulima wa parachichi mkoani Njombe amesema licha ya mkulima wa zao hilo kunyonywa na wanunuzi lakini ametoa shukrani zake kwa serikali kuendelea kupambana na kuwajali wakulima hao.


Share:

Serikali Na Wadau Wakutana Kuandaa Taarifa Ya Nchi Ya Utekelezaji Wa Mkataba Wa Kimataifa Wa Kutokomeza Aina Zote Za Ubaguzi Dhidi Ya Wanawake.

Na Mwandishi Wetu Morogoro
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo amewataka wadau wa haki na utetezi wa wanawake kuendeleza juhudi za Serikali ili kuhakikisha wanawake wanalindwa dhidi ya ubaguzi wa aina yoyote na kushiriki katika fursa za maendeleo na ustawi wao.

Bi. Chonjo alisema hayo wakati wa kuahirisha Kikao cha wadau wa Kitaifa waliokutana mjini Morogoro kwa lengo la kuboresha Taarifa ya Nchi ya Utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza aina zote za ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW).

Aidha Bi. Chonjo aliwapongeza wadau kwa kuweza kuainisha mafanikio yaliyofikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuzuia ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi 2019 akilitaja jambo hilo kuwa limetokana na utendaji wa pamoja.

’’Kazi hii ya kuandaa Taarifa ya Nchi ambayo mumeifanya kwa muda wa siku tatu itaboresha shughuli zilizofanyika na kuonesha jinsi Tanzania ilivyotekeleza masuala ya kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake na pia kuwawezesha kiuchumi, kisiasa na kijamii’’. Aliongeza Bi. Chonjo.

Aidha Bi. Chonjo pia alisema idadi ya wanawake nchini Tanzania ni kubwa ukilinganisha na idadi ya wanaume uku akitaja takwimu zinaonesha kuwa kuna takriban asilimia 51 ya wanawake ukilinganisha na wanaume na kati ya hao 80% wanaishi vijijini wakijiajiri katika shughuli za kilimo, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuwalinda wanawake dhidi ya ubaguzi na aina zote za ukatili wa kijinsia ili kushiriki nafasi za maendeleo

’’Tukitambua kuwa idadi ya Wanawake nchini ni kubwa kwa asilimia 51 ukilinganisha na idadi ya wanaume hoja hii inakuwa msingi wa kuwekeza katika kukuza ushiriki wa wanawake ambapo takriban asilimia 80 ya wanawake hao wanaishi vijijini wakiwa wamejiajiri katika sekta ya kilimo, hivyo kuna uhitaji mkubwa wa kupinga ubaguzi dhidi ya wanawake’’.Alisisitiza kiongozi huyo wa Wilaya.

Aidha Bi. Chonjo alizitaja juhudi za serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake  nni pamoja na kuanzisha Madawati ya Jinsia na Watoto 420 katika Vituo vya Polisi kwa lengo la kuwezesha kupata haki na huduma stahiki kwa wanawake na kuongeza kuwa  madawati haya yameongeza ari ya wananchi kujiamini na kuvunja ukimya katika utoaji taarifa za vitendo vya ukatili kwenye maeneo ya jamii.

Aidha Bi. Chonjo alivitaja Vituo vya pamoja vya  kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia kuwa  vimeanzishwa katika mikoa sita ya Tanzania Bara ambavyo ni Dar es Salaam, Pwani, Mwanza, Mbeya, Iringa na Shinyanga vimewesha utoaji wa huduma stahiki kwa waathirika akivitaja kuwa hatua muhimu iliyochokuliwa na serikali kupambana na vitendo vya ukatili hapa Nchini.

Bi. Chonjo alitaja hatua nyingine iliyochukuliwa na Searikali kupuna na vitendo vya ukatili kuwa ni kufanya marekebisho ya Sheria ya Elimu na kulifanya kosa la kumpa mimba au kuoa au kuolewa mwanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuwa kosa la jinai na pale inapothibitika adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 marekebisho haya yamesaidia kupunguza matukio ya mimba za utotoni.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bibi Mboni Mgaza ameeleza kuwa Taarifa hii ya Tisa ya Utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza aina zote za ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW)itawasilishwa Umoja wa Mataifa Mwezi Machi 2020 ikiwa imeunganisha taarifa ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.


                                              ---Mwisho.---


Share:

PICHA: Rais Wa Zanzibar Dk Shein Ahutubia Kilele Cha Miaka 56 Ya Mapinduzi Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride Maalum la Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza vla Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar
 Mgeni rasmi,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya sita Dk. Amani Abeid Karume alipowasili jukwaa kuu,katika Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.Pichani kati anaeshuhudia ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
VIJANA wa Maandamano Maalum ya kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa na Picha za Waasisi wa Mapinduzi, wakati wa hafla hiy0 iliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Vijana wa Chama cha mapinduzi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi ikiwa ni Ishara ya kutoa heshima katika maandamano ya maadhimisho ya ya Miaka 56 ya Mapinduzi yaliofanyika Aman mjini Zanzibar. 
WANACHAMA wa Chama cha CUF wakishiriki katika Maandamano ya kuadhimisha sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar
VIJANA wa payunia wakitowa salamu ya heshima kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein wakati wa maandamano ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vikosi vya Jeshi la Ulinzi na Usalama Vikipita mbele ya Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya Makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi yaliofanyika Aman mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akitoa hotuba ya kilele cha  Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi yaliofanyika Aman mjini Zanzibar.

PICHA NA IKULU PAMOJA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.


Share:

Serikali Yaonya Wananchi Wanaojenga Mijini Bila Kufuata Utaratibu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameonya wananchi wanaojenga mijini bila kufuata utaratibu.

Mhe. Lukuvi ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Ndachi Kata ya Mnadani jijini Dodoma wakati akikagua nyumba ambazo zimejengwa bila kufata utaratibu na kukosa vibali vya ujenzi.

Waziri Lukuvi alifikia hatua ya kusimamisha ujenzi kwa kuziwekea alama nyumba ambazo ujenzi wake umekiukwa na kuwaamuru wamiliki kusitisha shughuri zote hadi wafuate utaratibu.

Hata hivyo Mhe. Lukuvi amesema Serikali haina mpango wa kubomoa nyumba za wananchi isipokuwa wananchi wanatakiwa kujenga kwa kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kupata kibali cha ujenzi.


Share:

RAS SHINYANGA- Viongozi Wa Umma epukeni Migongano ya Kimaslahi katika vituo vyenu vya kazi

SALVATORY NTANDU
Mmomonyoko wa maadili na Migongano ya maslahi kwa Viongozi kwa baadhi ya viongozi wa mashirika na taasisi za Umma mkoani Shinyanga umetajwa kusababisha hasara kwa serikali kutokana na uwepo wa ufanisi mdogo  katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.

Hayo yalibainishwa Januari 10 mwaka huu na Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela wakati akifungua mafunzo ya siku mmoja ya  sheria ya maadili yaliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kujumuisha watendaji wakuu wa taasisi na mashirika ya Umma.

Alisema kuwa  Sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma inaelekeza majukumu ya viongozi wa taasisi na mashirika ya Umma, kusimamia sheria za Nchi, haki na utu ili kumsaidia Rais katika kutekeleza majukumu yake na hatimaye kutoa huduma bora kwa jamii na kuepuka kujiingiza katika migogoro isiyokuwana tija.

“Wapo  baadhi ya viongozi wa Umma wanaendekeza migogoro kwenye maeneo yao yakazi kwa kufanya kazi kwa makundi na kusababisha watumishi kutowajibika ipasavyo kinyume na viapo vyao,kama wapo humu hebu wajirekebisheni haraka kabla hatua za kinidhamu hazijachukuliwa dhidi yao, alisema Msovela.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kanda ya Magharibi inayojumisha mikoa ya Tabora,Shinyanga,Simiyu na Kigoma,kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma, Gerald Mwaitebele alisema kuwa endapo viongozi hao wataamua kubadilika malalamiko hayatajitokeza tena na wananchi watapata huduma za kijamii vizuri.

“Tangu tumeanza kutoa mafunzo haya katika mikoa yetu ya kanda ya magharibi tumeona mabadiliko makubwa hususani suala la maadili, uadilfu na vitendo vya rushwa limepungua na kutupa matumaini ya kuendelea kutoa elimu hii kwa ngazi zote kwenye jamii kama vile shuleni na kwenye mikutano ya hadhara ya vijji na mitaa” alisema Mwaitebele.

Nila Mabula ni Mshiriki wa Mafunzo hayo  ambaye pia ni Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Mkoa, ameiomba Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kutoa mafunzo hayo kwa watumishi wote wa umma ili kuzuia vitendo vya ukiukwaji wa maadili hususani pindi wanapokuwa wanatoa huduma kwenye jamii.

Mafunzo hayo yalijumuisha  Wakuu wa vyombo vya Usalama, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Makatibu Tawala wa Wilaya, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara na Vitengo, watendaji wa Mahakama na Wakuu wa Taasisi za Umma.

Mwisho.


Share:

TANGA UWASA KUJA NA TEKNOLOJIA YA UFUNGAJI WA MITA ZA MAJI ZENYE UWEZO WA KUJISOMA ZENYEWE

 Afisa Ankra wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Daudi Mkumbo  akizungumza katika mkutano wa wananchi wa Kata ya Duga Jijini Tanga kwenye zoezi la uelimishaji kuhusu huduma zao.
 Msimamizi wa Mtandao wa Maji Tanga Uwasa George Mbalai akitoa elimu ya usomaji mita kwa wananchi wa Mtaa wa Majengo Kata ya Duga wilayani ya Tanga wakati wa mkutano  wa kutoa elimu kwao kuhusu huduma zao
 AFISA Msaidizi wa Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa Mariam Mikidadi akisisitiza jambo kwa wananchi wa Mtaa wa Majengo Kata ya Duga Jiji Tanga wakati wa zoezi la uelimishaji kuhusu huduma zao.

 Msimamizi wa Mtandao wa Maji Tanga Uwasa George Mbalai akitoa elimu ya usomaji mita kwa wananchi wa Mtaa wa Majengo Kata ya Duga wilayani ya Tanga wakati wa mkutano  wa kutoa elimu kwao kuhusu huduma zao
 DIWANI wa Kata ya Duga (CUF) Khalid Rashid akizungumza wakati wa mkutano huo
Sehemu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo


Mmoja wa wananchi wa Mtaa wa Majengo Kata ya Duga Jijini Tanga akiuliza swali kwenye mkutano huo


MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imesema kwamba wanafikiria kuingia kwenye teknolojia ya ufungaji wa mita za maji ambazo zitakuwa na uwezo wa kujisoma zenyewe na kuzituma taarifa kwenye data base ofisini kwao.



Hayo yalisemwa na Afisa Ankra wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Daudi Mkumbo wakati akizungumza katika mkutano wa wananchi wa Kata ya Duga Jijini Tanga kwenye zoezi la uelimishaji kuhusu huduma zao.

Alisema kwani mita hizo zitakuwa zimefungwa chombo ambacho kitakuwa na uwezo wa kujisoma zenyewe na watu ambao wanashughulika na usomaji wa mita watakwenda kufanya kazi nyengine hali ambayo itarahisisha usomaji wake.



“Katika miaka ijayo tunafikiria kuanzisha mpango huo wa mita hizo lakini zile ambazo tunazotazamia kuzifunga mwaka huu ni kununua na kufungwa chombo ambacho kinaweza kupelekea mita kujisoma zenyewe na hao wasomaji waende kufanya kazi nyengine”Alisema



Afisa Ankra huyo alisema kwamba anaamini uwepo wa mita hizo utaondoa changamoto kwa baadhi ya wateja ambao wanadai kwamba wasomaji hawafiki kwenye maeneo yao kusoma mita.



“Kwa sasa kuna teknolojia ambayo mtu hataweza kusoma mita ya maji kwa umbali wa mita zaidi ya mita sita inamaana ndani ya mita sita ndio mtu anaweza kusoma maana yake kila mita ya maji itakuwa imefungwa kifaa hicho cha GPS ya eneo na ile mita ilipo atakuwa anatambulika na msomaji akifika ndani ya mita sita hawezi kudanganya”Alisema



Hata hivyo alishauri wananchi wa maeneo hayo kuacha tabia ya kutokuacha mabomba wazi wakati wanasubiri maji yakiwa yamekatika kwani hiyo ndio inaweza kuwa ndio chanzo kikubwa cha kupata bili kubwa ambayo haihusiani na matumizi ya wateja.



“Kwa sababu kipindi ambacho maji yamekatika kwenye bomba linajaa upepo hivyo wakati maji yanaporudi yakiwa na msukumo ule upepe ndio ambao unatangulia kabla ya maji unaozungusha mita na hiyo ndio chanzo kikubwa”Alisema Afisa Ankra huyo.



Hata hivyo alisema kwamba kama eneo ambalo ni Duga kuna changamoto ya miuondombinu chakavu aliwashauri kufunga maji na kutokufungua bomba mpaka wahakikishe maji yanatoka ili kuepukana na bili kuwa kubwa.



“Lakini ukifungulia maji wakati hamna maji kwani utasababisha bili kubwa wakati maji yanayorudi huo ni ushauri mpaka pale ambako yataweza kurekebisha miundombuni ili maji yaweze kutoka muda wote”Alisema



Hayo yanatokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi kwenye mtaa wa Majengo Kata ya Duga ambao walilamika kwamba wanapata bili kubwa wakati muda mwengine maji yanakuwa yamekatika.



Akizungumza mmoja wa wananchi hao Selemani Rashid alisema kwamba kwenye suala la usomaji wa mita wanaokwenda kufanya hivyo lazima wakutane na watu waliopo kwenye maeneo wanayokwenda.



“Lakini muweke utaratibu kwamba wasomaji wanapokwenda kusoma mita lazima wakutane na watu kwa lengo kwamba wakati wa usomaji wa mita hizo washughudie namna zinazosomwa ili kuonda dhana kwamba hawapiti kusoma maji”Alisema


Naye kwa upande wake mkazi mwengine wa mtaa huo Magreth Jeros alisema kwamba maji yanaweza kukatika asubuhi mpaka jioni hayatoki na sio siku moja hadi siku mbili lakini bili zinazokuja zinakuwa ni kubwa sana.
Share:

Mamia ya wananchi Iran Waandamana kulaani kuangushwa ndege ya abiria Ya Ukraine

Maandamano makubwa yameripotiwa usiku wa Jumamosi kwenye maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Iran Tehran, baada ya nchi hiyo kukiri kuwa kombora la kijeshi liliiangusha ndege ya abiria ya Ukraine. 

Mamia ya watu wameshiriki maandamano hayo ya usiku kuikosoa serikali ya nchi hiyo na hatua yake ya hapo kabla ya kupinga madai kuwa kombora lilikuwa chanzo cha ajali hiyo.

 Kulingana na shirika la habari la Isna waandamanaji nje ya chuo kikuu cha Amir Kabir wametaka wote waliohusika na kuangushwa ndege hiyo wajiuzulu..

 Wakati huo huo rais Donald Trump wa Marekani ameionya Iran dhidi ya kujaribu kufanya ukandamizaji wa maandamano hayo na kutoa wito kwa nchi hiyo kuruhusu makundi ya haki za kirai kufuatilia kile kinachoendelea. 

Ujumbe wa Trump umekuja baada ya polisi kuwatawanya wanafunzi waliokuwa wakitoa kauli kali kuwakumbuka wahanga wa ajali ya ndege iliyotokea Jumatano iliyopita.


Share:

Naibu Waziri Mabula Aagiza Wakuu Wa Idara Halmashauri Za Mkoa Wa Njombe Kuandikiwa Barua Za Kujieleza

Na Munir Shemweta, WANMM NJOMBE
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza Wakuu wote wa idara za Ardhi katika Halmashauri za mkoa wa Njombe kuandikiwa barua za kujieleza kutokana na kushindwa kusimamia uingizaji taarifa za viwanja kwenye mfumo wa Kielektroniki wa ukusanyaji kodi ya serikali.

Aidha, alitoa miezi mitatu kuanzia tarehe 11 Januari 2020 hadi April 12, mwaka huu kwa halmashauri za mkoa wa Njombe kumpatia taarifa ya kuingizwa viwanja vyote vya wamiliki wa ardhi kwenye mfumo wa kielektroniki katika mkoa huo.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo jana katika kikao chake na watendaji wa sekta ya ardhi wa halmashauri sita za mkoa wa Njombe akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi pamoja na kukagua miradi ya ujenzi inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Wakuu wa idara ya ardhi walioangukia mikono ya Dkt Mabula kuhusiana na kuandika barua za kujieleza ni kutoka Halmashauri za Njombe Mji iliyoingiza viwanja 7,301, Makambako 5,712, Njombe Wilaya 326, Wanging’ombe 375, Makete 2156 na Ludewa viwanja 3,793.

Uamuzi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi unafuatia kuelezwa kupitia taarifa ya mkoa wa Njombe pamoja na zile za halmashauri zote za mkoa huo kuwa, kuanzia kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 ni  viwanja 19,645 tu ndivyo vilivyoingizwa kwenye mfumo kati ya viwanja 40,961.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, utaratibu wa kuingiza viwanja kwenye mfumo wa kielektroniki ulianza mwaka 2017 lakini cha kushangaza hadi kufikia sasa hakuna jitihada za dhati zilizofanywa na baadhi ya halmashauri kuhakikisha viwanja vyote vinaingizwa kwenye mfumo huo ili kurahisisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia pango la ardhi.

Alisema, kuingiza viwanja kwenye mfumo wa kielektroniki siyo tu unarahisisha kutambua wamiliki wote wa ardhi bali unasaidia kuwafuatilia wamiliki wanaokwepa kilipa kodi ya ardhi jambo alilolieleza lisiposimamiwa kwa umakini litapunguza wigo wa ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi.

‘’Uingizaji viwanja kwenye mfumo wa kielektroniki ulianza tangu mwaka 2017 lakini bado hakuna kilichofanyika hatuwezi kulea uozo huu unaoweza kuwapa mzigo wateja kutokana na malimbikizo ya kodi’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri Mabula alisema, wizara yake inataka kuwa na malengo yanayoendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano na kuiagiza ofisi ya Ardhi ya Kanda kupitia takwimu za viwanja vilivyo katika mfumo kwa halmashauri za mkoa wa Mbeya na kusisitiza haiwezekani kuwa na Afisa Ardhi Mteule ama Mkuu wa idara ya Ardhi asiyefuatilia na kusisitiza katika suala hilo wizara yake haitakuwa na msamaha.

Akigeukia ukusanyaji mapato yatokanayo na kodi ya pango la ardhi, Dkt Mabula alionesha kutoridhishwa na makusanyo ya kodi hiyo kwa halmashauri za mkoa wa Njombe ambapo kufikia Desema 2019 halmashauri zote zilikusanya jumla ya shilingi 369,863,643.34 kiasi alichokieleza kiko chini ya asilimia 50 ya makusanyo ya kodi ya ardhi katika mkoa huo uliokuwa na lengo la Bilioni 1.2.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa kwa gharama ya takriban bilioni 2.7.

Dkt Mabula mbali na kuridhishwa na ujenzi wa jengo hilo amelitaka shirika la Nyumba la Taifa kuhakikisha jengo hilo linakamilika mapema iwezekanavyo kwa kuwa lilichelewa kukamilika kutokana na changamoto mbalimbali.


Share:

Kamishna Wa Operesheni Na Mafunzo Cp Liberatus Sabas, Aongoza Vikosi Maalum Katika Kufanikisha Kuwatafuta Watu Waliohusika Na Mauaji Ya Watu Wanne Wa Familia Moja

Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 33 waliohusika kwa namna moja au njingine katika kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara Petro Sagalika yaliyotokea siku ya tarehe 02, Januari mwaka huu katika kijiji cha Msambala wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Aidha Kamishna CP Sabas amesema Mzee Perto Sagalika alikuwa Mfanyabiashara wilayani Kasulu aliekuwa anamiliki vibanda sita vya biashara, watu hao walimfuata mida ya saa kumi na mbili jioni katika eneo lake la Biashara na kuanza kumkata kata kwa mapanga mpaka kupelekea umauti wake, wakati wananchi hao wakiendelea na adhima hiyo kijana wa Mzee huyo aliweza kupata taarifa kuwa baba yake kavamiwa alifika ili kuja kumsaidia ila nae aliuliwa pia kwa kukatwa katwa kwa Mapanga.

Baada ya hatua hiyo wananchi hao wenye hasira kali walielekea nyumbani kwa Mzee Petro Sagalika na walimkuta mkewe na mwanae wa kike wakiwa wamekaa na ndipo walijichukulia sheria mkononi tena kwa kuwaua kwa kuwakata kata na mapanga mpaka kusababisha vifo vya familia nzima ya Mzee huyo baada ya kuhakikisha wameisha ua familia nzima ndipo walichukua uamuzi wa kubomoa nyumba na vibanda vyote sita vya mfanyabiashara huyo na kisha kutoweka.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas, huku akisisitiza kuwa kwavile tukio lilitokea mchana hakuna atakaesalimika kwani wahusika wote watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria huku akiongezea mpaka sasa wamepatikana watuhumiwa 33 ila bado Operesheni inaendelea kwani hakuna jiwe litasalia juu ya jiwe.

Cp Sabas, amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi kwani ni kinyumea cha taratibu na sheria za nchi.


Share:

LIVE: Sherehe Za Miaka 56 Ya Mapinduzi Matukufu Ya Zanzibar

LIVE: Sherehe Za Miaka 56 Ya Mapinduzi Matukufu Ya Zanzibar


Share:

Soko La Mazao Ya Kilimo Kujengwa Longido

 Wizara ya Kilimo inatarajia kuanzisha ushirikiano na Wilaya ya Longido kwa ajili ya kufanya uwekezaji na uendelezaji wa eneo la kilimo lenye ukubwa wa ekari 50 katika mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga.

Kauli hii imetolewa jana (11.01.2020) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe alipofanya kikao na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Frank Mwaisombe ofisini kwake jijini Dodoma.

“Ni wajibu wa wizara ya kilimo kuhakikisha mazao ya kilimo yanapata soko la uhakika na kuongezwa thamani ili kuwanufaisha wakulima,hivyo uwepo wa soko la mazao
mpakani Namanga utasaidia serikali kuongeza mapato” alisema Mhandisi Mtigumwe.

Katibu Mkuu huyo alisema wizara kwa kuanzia itatuma wataalam kwenda Longido wiki ijayo ikiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko kuweka mpango mahsusi wa kuwezesha serikali na wawekezaji kutumia eneo hilo la kilimo.

Aliongeza kusema kuwa wizara ya Kilimo kupita ushirikiano hu inataka kuona eneo hili la mpakani linakuwa kituo kikuu cha uwekezaji kwenye kilimo,kwani ni jukuma la wizara kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima kupata masoko ya mazao yao.

“ Wataalam wakae chini baada ya kutembelea Longido na kuweka mpango wa uanzishwaji soko na maghala kwa ajili ya mazao ya kilimo mapema” alisisitiza Katibu
Mkuu huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisombe aliyeongozana na wataalam wa kilimo na ardhi wa halmashauri alisema ushirikiano na wizara ya kilimo unahitajika ili kujenga soko,maghala na viwanda vitakavyoongeza thamani ya mazao kabla ya kuuzwa.

Mwaisombe alisema uwepo wa soko na viwanda vya mazao ya kilimo mpakani Longido kutawanufaisha wakulima na wafanyabiashara kuuza mazao yao kwa bei nzuri na nchi
kupata pato zaidi.

“Tunayo fursa nzuri ya kushirikiana na wizara hii kuimarisha masoko ya mazao ya kilimo kabla hayajauzwa nje ya nchi,hivyo kuboresha maisha ya wakulima kama anavyoelekeza Mheshimiwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli” alisema Mkuu wa Wilaya ya Longido.

Wilaya ya Longido iliyoanzishwa mwaka 2016 ipo mpakani na nchi ya Kenya ambapo kwa mwaka zaidi ya shilingi Bilioni 54 zinakusanywa kama mapato toka ushuru
hususan mazao ya kilimo.

Aliongeza kusema Halmashauri ya Longido hukusanya kati ya shilingi milioni 300 kwa mwezi toka ushuru na tozo mbalimbali mpakani hapo,hivyo uwepo wa soko la kilimo utasaidia kuongeza wigo wa mapato toka mazao ya kilimo yanayopitishwa kwa wingi mpakani kwenda Kenya na Somalia.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya hiyo aliyataja mazao ya kilimo yanayongoza kupita mpaka wa Namanga kuwa ni mahindi,vitunguu,nyanya na mazao ya mbogamboga na matunda mengi yakiwa hayajaongezwa thamani.

Kikao hiki kimefuatia ziara aliyoifanya Katibu Mkuu Mhandisi Mtigumwe kutembelea halmashauri ya Longido mwanzoni mwa mwaka huu 2020 kwa mwaliko wa Mkuu wa wilaya hiyo Frank Mwaisombe ili kuona namna wizara itakavyosaidia kutumia fursa ya mpaka kukuza masoko ya mazao ya kilimo kwa manufaa ya wakulima nchini.


Share:

Rais Magufuli aweka jiwe la msingi ujenzi wa Sekondari ya Mwanakwerekwe na afungua Hotel Verde Zanzibar




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya January 12















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger