Saturday, 23 November 2019

SIMBA SC YAIADHIBU RUVU SHOOTING.... MADENGE ATUPIA MAWILI.MBRAZIL AKIUA MOJA

Mabingwa watetezi, Simba SC leo wameiadhibu Ruvu Shooting baada ya kuichapa mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

Nyota wa mchezo wa leo alikuwa ni mshambuliaji Miraji Athumani ‘Madenge’ aliyefunga mabao mawili, huku lingine likifungwa na beki Mbrazil, Tairone Santos da Silva.

Na kwa ushindi huo, Wekundu wa Msimbazi wanafikisha pointi 25 katika mchezo wa 10 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu ikifuatiwa na Kagera Sugar yenye pointi 23 za mechi 11, wakati Ruvu Shooting inabaki pointi zake 15 baada ya kucheza mechi 12.

Miraj anayefahamika pia kwa jina la utani Sheva akifananishwa na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Ukraine, Andriy Mykolayovych Shevchenko alifunga bao la kwanza dakika ya 39 kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kulia Shomari Kapombe.

Beki Mbrazil, Tairone Santos da Silva aliye katika msimu wake wa kwanza tangu asajiliwe kutoka Atletico Cearense ya Daraja la Nne nchini kwao akafunga bao la pili dakika ya 47 akimalizia mpira wa kona wa kiungo Mkenya, Francis Kahata kutoka kulia.

Miraj aliyeibukia timu ya vijana ya Simba, maarufu kama Simba B kabla ya kwenda kujikomaza kisoka Mwadui FC ya Shinyanga, Toto African ya Mwanza na Lipuli FC ya Iringa kisha kurejea nyumbani msimu huu, alifunga bao la tatu kwa shuti dakika ya 74 akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenzake, Mnyarwanda Meddie Kagere.

Kikosi cha Ruvu Shooting kilikuwa; Mohamed Makaka, Omary Kindamba, Kassim Simbaulanga, Renatus Ambroce, Rajab Zahir, Zuberi Dabi, Emmanuel Martin, Shaaban Msala/Moses Shaaban dk73, Saadat Mohamed, Said Dilunga/Fully Maganga dk58 na Edward Christopher/Abdulrahman Mussa dk61.

Simba SC; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Tairone Santos, Pascal Wawa, Gerson Fraga ‘Viera’, Hassan Dilunga/Deo Kanda dk63, Muzamil Yassin, Meddie Kagere/Ibrahim Ajibu dk75, Miraji Athuman ‘Madenge’ na Francis Kahata/Sharaff Eldin Shiboub dk79.
Chanzo - Binzubeiry blog
Share:

Ajari Ya Lori Yaua Watu Watatu Jijini Dar

Jumla ya watu watatu wamefariki Dunia papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya, baada ya kugongwa na Lori la mafuta lililoacha njia na kuparamia watembea kwa miguu, maeneo ya Mlimani City, lililokuwa likitokea Ubungo kwenda Mwenge.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mussa Taibu, amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 5:20 asubuhi, ambapo mara baada ya ajali hiyo kutokea, dereva alikimbia na kutoweka kusikojulikana.

"Dereva aliacha njia na kugonga watembea kwa miguu, kati ya watu wanne waliogongwa watatu walifariki papo hapo na mmoja ni majeruhi amepelekwa hospitali, mmoja aliyefariki ametambulika kwa jina la Daniel Mushi ni fundi umeme na mkazi wa Kimara - Temboni, ni uzembe tu wa dereva maana aliacha njia na kuparamia watembea kwa miguu" amesema Kamanda Taibu.

Kwa mujibu wa Kamanda Taibu, miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali hiyo na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kufanya juhudi za kumsaka dereva huyo popote alipo.

Share:

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI WATANO IKULU CHAMWINO JIJINI DODOMA. NOVEMBA 23, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Maj. Jenerali Anselm Shigongo Bahati kuwa
Balozi wa Tanzania Nchini Misri, Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Novemba 23, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Mohamed Abdallah Mtonga kuwa Balozi wa
Tanzania Nchini Abu dhabi (UAE) , Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini
Dodoma. Novemba 23, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Dkt. Jilly Elibariki Maleko kuwa Balozi wa
Tanzania Nchini Burundi , Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma.
Novemba 23, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Jestas Abouk Nyamanga kuwa Balozi wa
Tanzania Nchini Ubelgiji , Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma.
Novemba 23, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Ali Jabir Mwadini kuwa Balozi wa Tanzania
Nchini Saud Arabia , Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Novemba
23, 2019.
Mabalozi wapya watia sahihi hati za kiapo cha Maadili kwa
Watumishi wa Umma kilichoongozwa na kamshna wa Tume ya Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli . Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Novemba 23, 2019. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu na Waziri Mkuu Mhe.
Kassim Majaliwa , Katibu Mkuu Kiongozi Balozi wa John Kijazi, Waziri wa Mambo
ya nje Profesa Palamagamba Kabudi ,Waziri wa TAMISEMI Seleman Jaffo, Waziri
wa Ardhi William Lukuvi, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi wakwanza kushoto pamoja na Mabalozi wapya mara baada ya tukio la uapisho Ikulu chamwino jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akiwagawia Vitafunwa wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho ya Mabalozi iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Novemba 23, 2019.
Mabalozi wapya wakila kiapo cha Maadili kwa Watumishi wa Umma
kilichoongozwa na kamshna wa Tume ya Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli . Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Novemba 23, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza mara baada kuwapisha Mabalozi watano
walioapishwa kuiwakilisha Tanzania katika Nchi za Burundi, Abu Dhabi (UAE)
,Ubelgiji, Misri pamoja na Saud Arabia katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino
jijini Dodoma. Novemba 23, 2019.
PICHA NA IKULU
Share:

Tapeli akamatwa na kadi 23 za benki Akiwa Amezificha Sehemu za Siri

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM KUIMARISHA ULINZI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika kwa amani na utulivu.
 
Ndugu wana habari, tarehe 24/11/2019 ni siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji hivyo basi sisi kama Jeshi la Polisi tutaimarisha ulinzi maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam, katika vituo vya kupigia kura, ofisi zote za vyama vya siasa na ofisi zote za watendaji wa kata.
 
Aidha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa onyo kali kwa mtu yeyote au kikundi chochote cha watu watakao jaribu kuvuruga amani jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA WIZI WA FEDHA KWENYE MASHINE ZA KUTOLEA FEDHA (ATM) NA ATM KADI 23
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Bi Halima Juma (23)Mkazi wa Chalinze kwa tuhuma za wizi wa fedha kwenye mashine za kutolea fedha (ATM)
 
Mnamo tarehe 19/11/2019 katika benki ya CRDB tawi la Mbagala akiwa katika ATM hizo, aidha alimtilia mashaka binti huyo aliyekuwa kwenye chumba cha ATM ya benki hiyo akijifanya kuwasaidia wazee na wastaafu wasiojua kutumia ATM mashine vizuri, lakini lengo lake ni kuchukua namba za siri za wastaafu na wazee hao na kisha kuwabadilishia ATM kadi zao na baadaye kuwaibia fedha kwenye akaunti zao kwa kutumia kadi halisi za wahusika baada ya kuwabadilishia kadi na kuchukua namba za siri.
 
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari wanaolinda Benki hiyo na alipopekuliwa alikutwa na ATM kadi 23 za watu mbalimbali za benki tofauti tofauti zikiwa katika pochi yake huku akiwa amezificha katika sehemu zake za siri ukeni.
 
Kadi hizo ni kama ifuatavyo;
1.CRDB kadi 07
2.NMB kadi 06
3.NBC kadi 02
4.AMANA kadi 02
5.POSTA BENKI kadi 02
6.ACB kadi 01
7.STANIBIC kadi 01
8.DTB kadi 01
9.EQUITY kadi 01
 
Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani hivi karibuni.

TAHADHARI YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA JIJINI DAR ES SALAAM.​

Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam linapenda kutoa tahadhari kwa wakazi wa jiji la Dsm wote kuwa makini kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha ili kuepukana na majanga yanayoweza kuepukika. 

Hivyo wananchi wote wanatakiwa kuwa makini na watoto wadogo wanaohitaji uangalizi wa karibu, pia kujiepusha kupita kwenye maji ya mito midogomidogo au madimbwi ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wao.
 
Aidha hadi sasa zimepokelewa taarifa za watu wawili kufariki dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

LAZARO .B. MAMBOSASA – SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.

Share:

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Kupokea Madaktari Bingwa Kutoka China

Share:

Wagombea 1,851 wa vyama vya upinzani kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Mkoani Rukwa.

Wagombea wa vyama vya upinzani wapatao 1,851 kushiriki katika nafasi mbalimbali za uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika nchini tarehe 24.11.2019 ili kuwapata wawakilishi katika ngazi ya kijiji, mtaa, kitongoji pamoja na wajumbe mchanganyiko na wajumbe wa viti maalum katika ngazi hizo.

Taarifa kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa inasema kuwa wagombea hao hawatakuwa na uwezo wa kuweka mawakala kisheria kwasababu mawakala hao wanatakiwa kuwa na kiapo cha kisheria pamoja na utambulisho kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi na kuongeza kuwa ni isipokuwa mgombea mwenyewe ndiye anaweza kuwa wakala.

Aidha, ametahadharisha kuwa endao kutatokea vurugu katika maeneo ambayo kwasababu nembo ya chama cha upinzani imetumika wakati mgombea amejitoa ambapo yawezekana alijitoa kwa kuchelewa au aliamua kutosumbuka kujitoa,Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya zitaimarisha ulinzi katika maeneo ya kupiga kura.

Idadi ya wagombea wa vyama vya upinzani waliobakia Mkoani Rukwa baada ya mwisho wa tarehe ya kujitoa 16.11.2019 saa 10 jioni ni katika vijiji 67 (19.7%), Vitongoji 348 (19.1)%, mitaa 9 (5.4%), wajumbe mchanganyiko 876 (11.8%) na wajumbe wa viti maalumu 551 (19.1%). Mkoa una jumla ya vijiji 339, vitongoji 1,817, mitaa165. Wajumbe mchanganyiko 7,420 na wajumbe wa viti maalum 2,875.

Share:

Nafasi 200 za Kazi Zilizotangazwa Wiki Hii....Zipo za Umoja wa Mataifa, WHO, Benki Mbalimbali za Tanzania Na Zingine

1. Job Opportunity at PwC | Environmental Specialist

2. Job Opportunity at PwC | Procurement Specialist 

3. New Jobs At The National Electoral Commission (NEC), Tanzania | Nafasi Mpya Za Kazi Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi

4. Senior Finance & Accounting Officer at Lifewater International 

5. Job Opportunity at Reliance Insurance | Assistant Accountant

6. Job Opportunity at RTI International | Extramural Advisor

7. Job Opportunity at TradeMark East Africa (TMEA) | Transport Director, Logistics

8. Job Opportunity at TradeMark East Africa (TMEA) | Transport Director

9. Job Opportunity at World Vision | Sponsorship & Program Facilitators

10. Job Opportunity at U.S. Embassy | Administrative Assistant OSC

11. Job Opportunity at U.S. Embassy | Electrician

12. 22 Job Opportunities at Startimes Tanzania Company Limited

13. Job Opportunities at Tanga UWASA | Drivers II 

14.Job Opportunity at Tanga UWASA | Customer Service Manager 

15.Job Vacancy at Geita Gold Mining (GGML) | Superintendent UG Planning 

16.Job Opportunity at Tanzania Revenue Authority (TRA) | Assistant Lecturer 

17.Job Opportunity | Estate Officer At Mbeya University November 

18.Artisan II Jobs (Masonry-2 And Plumber-1) At Mbeya University 

19.Technician II Jobs (Civil) At Mbeya University

20
.New Job Opportunity at Institute of Adult Education (IAE) | Deputy Director (Academic, Research And Consultancy) 

21.Airport Services Duty Officer at Qatar Airways  

22.Job Opportunity at ICAP | Strategic Information (SI) Specialist, Tanzania 

23.Job Opportunity at ICAP | Project Director for Health Information Systems (HIS), Tanzania 

24.Job Opportunity at ICAP | Zonal Project Manager 

25..Job Vacancy at Kazini Kwetu Limited | Depot Accountants 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬   

Share:

Tanzania Ya Kwanza Kutoa Mafunzo Ya Kutumia Afya Moja Kutathimini Hatari Ya Vimelea Hatarishi Vya Magonjwa

KWA mara ya kwanza Barani Afrika, Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kufanya mafunzo katika ngazi ya mkoa na Halmashauri kwa kutumia dhana ya Afya moja  kuwajengea uwezo wadau wa Afya moja juu ya namna ya  kufanya tathmini ya vimelea hatarishi vya magonjwa. 

Mafunzo hayo yamewakutanisha wadau wa Afya moja na wataalam kutoka sekta za afya ya binadamu, wanyama pori, mifugo, kilimo na mazingira. Wadau hao na wataalam kutoka sekta hizo za afya wamepata mafunzo ya namna ya kufanya tathmini hiyo kwa magonjwa ya Kichaa cha mbwa, Kimeta na Ugonjwa wa Brusela (Ugonjwa wa Kutupa mimba kwa wanyama).

Kufuatia nchi ya Tanzania kuwa imepiga hatua katika uratibu wa  masuala  ya Afya moja, ambayo ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo, kilimo na  mazingira katika kujiandaa, kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu. 

Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa  (FAO) imeratibu mafunzo hayo  yaliyotolewa na wakufunzi wa hapa nchini waliojengewa uwezo  na wataalamu kutoka Makao makuu ya  Shirika la Afya Duniani (WHO), Makao makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa  (FAO), pamoja na Shirika linaloshughulika na Afya ya Wanyama (OIE).

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo tarehe 22 Novemba 2019,Jijini Arusha, Mkurugenzi wa Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, amebainisha kuwa ushirikiano wa wadau wa Afya moja na wataalam na sekta za Afya  kwa kutumia dhana ya Afya Moja hivi sasa ni agenda ya dunia nzima. 

Aidha amefafanua kuwa  dhana hiyo inapunguza gharama katika kushughulikia tishio la magonjwa  yanayotokana na vimelea vyenye uwezo wa kutoka kwa wanyama na kwenda kwa binadamu na hata mimea (mazingira) na kusababisha magonjwa na hata usugu wa vimelea vya magonjwa.

“Wadau wa afya moja wanawajibika kupanga mikakati mbalimbali ya udhibiti, ulinzi na usalama katika kuzuia, kujiandaa na kukabali magonjwa ambukizi. Moja ya mkakati ulioibuliwa Kitaifa na kimataifa ni kujiandaa kwa kuwafundisha  wataalam wa sekta mbalimbali za  afya jinsi ya kufanya tathmini ya  hatari ya vimelea vya magonjwa ambukizi kwa ushirikiano.” Amesema . Kanali Matamwe.

Kwa upande wake, Mwezeshaji wa Mafunzo hayo kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa  (FAO), Tanzania, Bi. 

Niwael Mtui amefafanua kuwa Shirika hilo moja ya kipaumbele chake ni kupunguza umasikini na kuongeza kipato cha wananchi, hivyo Shirika hilo linashirikiana na serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, katika kujenga uwezo wa  ndani ya nchi kwa kuwafundisha wataalam wa sekta za Afya katika kudhibiti magonjwa ambapo uwezo huo utasaidia kuimarisha afya ya binadamu na mifugo na hatimaye kipato kitaongezeka na umasikini utapungua

Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo  hayo wamebainisha kuwa  wamekuwa wakifanya tathmini za vimelela hatarishi vya magonjwa hapa nchini lakini tathmini hizo zimekuwa ni za kisekta kwani hazikuwa zinazingatia ushirikiano kwa maana ya dhana ya Afya moja. 

Aidha walifafanua kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kutumia Dhana ya Afya moja kwa kuwa inapunguza gharama katika kushughulikia tishio la magonjwa  yanayotokana na vimelea vyenye uwezo wa kutoka kwa wanyama na kwenda kwa binadamu na hata mimea (mazingira) na kusababisha magonjwa na hata usugu wa vimelea vya magonjwa.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Afya moja nchini. 

Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa  (FAO) na wadau waliandaa na kuratibu mafuzo hayo, ambapo wataalamu wa sekta za Afya na Wadau wa Afya moja kutoka Halmashauri nne za mkoa wa Arusha (Halmasahauri ya Arusha, Monduli, Ngorongoro na Karatu) walishirki mafunzo hayo

MWISHO

Share:

Aliye Jifanya Afsa Usalama Wa Taifa Akamatwa Mkoani Kagera.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera.
Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linamshikilia  bw.Erasto Matembo  mwenye miaka 30 mkazi wa Kinondoni mkoani Dar Es Salaam kwa tuhuma za kujifanyaAfisa Usalama wa Taifa na kuwanyanganya  wananchi mali zao.
 
Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Revocatus K.Malimi wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake Novemba 22/2019 na kusema kuwa mtu huyo amekamatwa kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama  na kuongeza kuwa alikuwa akijitambulisha kwa wananchi akiwapa huduma kuwa ni Afsa Usalama wa Taifa .
 
Kamanda Malimi amesema kuwa mnamo Novemba 18 mwaka huu akiwa katika kijiji cha Mugoma wilayani Ngara mtuhumiwa alimkamata mtu mmoja  kwa kile alichoeleza kuwa  anazo taharifa za mtu huyo kumiliki siraha ya kivita isivyo halali na kwamba  siraha hiyo anaitumia katika ujambazi  ndipo alipompeleka katika kituo cha polisi  wilayani humo.
 
Ameongeza kuwa mara baada ya Polisi kuanza  kumhoji huyo mtu aliyekuwa amemkamata ,lakini pia kulingana na uzito wa tuhuma yake na uzito wa ofisi ya mkamataji waliamua kushiriana na mkamataji  pamoja na ofisi yake ya Wilaya. 
 
Kamanda ameongeza kuwa alifikishwa kituoni na kujitambulisha  kuwa ni  Afsa Usalama wa Taifa mnamo Nonemba 19 mwaka huu  na walipomfanyia mahojiano alikiri kwa kinywa chake kuwa si mtumishi wa serikali bali amekuwa akitumia kama mbinu ya kujunufaisha .
 
Ameongeza  kuwa alisalimisha siraha mbili aina ya Bastola ambazo amekuwa akizimiliki na kuzitumia katika kutaperi wananchi .
 
Aidha  Kamanda amesema kuwa kijana huyo alihama  kutoka Dae es salaam na kuja kuishi katika kijiji cha Kirusha kata ya Mgoma,Wilaya ya Ngara  kwa kumfuata mke wake ambaye ni mwalimu katika shule ya msingi ya Kishura na mda wote alimwaminisha mke wake kuwa mtumishi serikalini katika idara ya usalama wa Taifa.
 
 Kamanda Malimi ameongeza kuwa taratibu za uchunguzi zikikamilika  atafikishwa mahakamani ili kujibu ntuhuma hizo pia amewaomba wananchi  ambao wamewai kukutana naye na kuwafanyia kitando chochote cha dhuruma kujitokeza ili kupata ushuhuda wao.

Share:

Aliyeikamata Ndege ya ATCL Afrika Kusini Kaikama Tena Huko Canada

Ndege  nyingine ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombadier ambayo ilikuwa ikijiandaa kuja Tanzania imekamatwa nchini Canada, ambapo aliyefanya hivyo ni yuleyule (Hermanus Steyn, raia wa Afrika Kusini) ambaye aliikamata ndege kama hiyo nchini Afrika Kusini miezi michache iliyopita lakini Serikali ya Tanzania ikamshinda mahakamani.

Hayo yamesemwa leo, Jumamosi Novemba 23, 2019 na Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, wakati akihutubia baada ya Rais John Magufuli kuwaapisha mabalozi wateule watano watakaoiwakilisha Tanzania nchi mbalimbali ambapo hafla hiyo ya imefanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Mabalozi walioapishwa leo Ikulu Dodoma ni;
  1. Mhe. Mej. Jen. Mstaafu Asleim Bahati, Balozi wa Tanzania Misri
  2. Mhe. Jestas Nyamanga, Balozi nchini Ubelgijji
  3. Mhe. Mohammed Mtonga, Balozi wa Tanzania, UAE
  4. Mhe. Jilly Maleko, Balozi nchini Burundi
  5. Mhe. Ali Mwadini, Balozi nchini Saudi Arabia.
Profesa Kabudi amesema kuendelea kwa vitendo hivyo ni hujuma za mabeberu wasiofurahishwa na maendeleo nchini.
 
“Tulikwenda mahakamani tukamshinda (Afrika Kusini) akakata rufaa na wiki iliyopita tukamshinda tena, huyohuyo sasa amekimbilia Canada amekamata ndege ya Bombardier Q400 ambayo ilikuwa ifike nchini.

“Jambo linalosikitisha ndege zilizokuwa zinatoka Marekani aina ya Dreamliner mbili hazikukamatwa zimefika lakini kila ndege inapotakiwa kuondoka Canada tunashangaa hao matapeli wanajuaje na ndege zinakamatwa.”
Amesema Profesa Kabudi.
 
Amesema Balozi wa Tanzania nchini Canada aliitwa nchini na kuelezwa jinsi nchi isivyofurahishwa na kukamatwa kwa ndege zake kila zinapokaribia kuja kuondoka nchini humo.
 
“Jana nimemuita Balozi wa Canada, nimeongea naye kinagaubaga na kumwambia, haturidhishwi na tumechukizwa na tabia inayoendelea ya ndege zetu kukamatwa kila zinapotaka kutoka Canada, Mheshimiwa rais tunafikiri kukushauri kuhusu suala la kununua ndege Canada, si wao pekee wanaotengeneza ndege, hata Brazil wanatengeneza.

“Wanasingizia hali ya hewa, wanasimamisha safari zake, kisha wanaikamata. Kule Afrika Kusini tulimshinda kesi ya msingi na rufaa sasa hivi amekimbilia Canada, tayari tumeshapata wanasheria kule Canada na taratibu zote za kutetea ndege yetu zimeanza.

“Hoja yetu kubwa ni kuwaeleza watu wa Canada kwamba amekenda kwenye mahakama za nje ameshindwa na sasa amekimbilia Canada. Sasa tumeelewa kuwa kila unapoleta maendeleo wapo mabeberu wa nje na wengine wa ndani wanaotuhujumu. Wanakesha wakiunguruma ili wairarue nchi hii,” amesema Prof. Kabudi.

Kushikiliwa kwa ndege hiyo kunarejesha kumbukumbu ya ndege nyingine ya Tanzania aina ya Bombardier Q400-8 iliyozuiwa nchini Canada mwaka 2017 kutokana na madai ya Sh87.3 bilioni zilizokuwa zikidaiwa na kampuni ya kikandarasi.

Share:

Hifadhi Tatu Mpya Zatangazwa Rasmi

Share:

KAMPUNI YA BUSINET AFRICA YADHAMIRIA KUENDELEZA ZAO LA ALIZETI MKOANI SINGIDA

 Meneja wa Mradi wa Kampuni ya BusinetAfrika Irene Njovu, akizungumza na waandishi wa habari mjini Singida jana, katika kikao cha wadau wa zao la alizeti kilichofanywa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
 Kikao kikiendelea .
Meneja wa Mradi wa Kampuni ya BusinetAfrika Irene Njovu, Irene Njovu, akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.

Na Waandishi Wetu, Singida

KAMPUNI ya BusinetAfrica imedhamiria kuwasaidia Wakulima Mkoani Singida namna ya Kutengeneza maandiko ili waweze kupata mikopo kwenye Mabenki itakayowasaidia katika shughuli za kilimo. 

Kampuni hiyo imewakutanisha pamoja viongozi wa vyama vya ushirika kutoka kila wilaya za mkoa huo, wakulima wa zao la alizeti na wasindikaji wa zao hilo kwa lengo la kuwaunganisha  na taasisi za Kifedha ili waweze kufanya kazi kwa pamoja. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kikao hicho Meneja wa Mradi wa Kampuni hiyo,  Irene Njovu alisema kampuni hiyo imekuja na mradi wa kuwasaidia wakulima wa zao la alizeti  kupata mikopo kwa kuwaunganisha na Benki ya Kilimo na Maendeleo Tanzania (TADB) kuwaelekeza taratibu zinazotakiwa ili waweze kupata mikopo. 

"Tumekuja na mradi wa kuendeleza zao la Alizeti Mkoa wa Singida na tumeamua kuwaunganisha wakulima na taasisi za kifedha hususani benki yao ili waweze kupata mikopo katika msimu huu wa kilimo". alisema  Njovu. 

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika 'SIFACU' Mkoa wa Singida, Yahaya Hamis alisema kutokana na wakulima wengi pamoja na Viongozi wa vyama vya ushirika kutokujua kuandika maandiko ili kupata mikopo,  kwa kupitia mradi huo watakuwa na ufahamu na kuanza kuandika maandiko yatakayosaidia kupata mbegu bora na kuongezeka uzalishaji wa zao hilo. 

Hata hivyo wakulima wameshukuru kwa hatua hiyo lakini hofu yao wameona mradi huo umechelewa, hivyo wameomba taasisi za kifedha hususani Benki ya Kilimo na Maendeleo Tanzania (TADB) ambayo ndio wameunganishwa nayo kutoa mikopo mapema ili waweze kupata mbegu bora kwa wakati kabla msimu haujaisha, huku wasindikaji wakiwa na matumaini ya kupata malighafi ya kutosha baada ya mradi huo kuwafikia. 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger