Saturday, 23 November 2019

Serikali Yasisitiza haiwezi kupanga bei elekezi ya mchele ama mahindi

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa serikali haiwezi kupanga bei elekezi ya mchele ama mahindi hivyo amewataka wakulima kote nchini kupandisha bei ya mazao hayo kadri wawezavyo kulingana na mahitaji ya soko.

Akizungumza wakati alipotembelea kikundi cha wanawake wajasiriamali wauzaji wa mchele katika eneo la Vwawa Mkoani Songwe juzi tarehe 21 Novemba 2019 alisema kuwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya nafaka ambayo ni mahindi na mchele katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 waendelee kunufaika na biashara ya mazao hayo kulingana na mahitaji ya soko.

Alisema kuwa wakati bei ya mazao hayo inaposhuka sokoni serikali haiingilii kupandisha bei ya mazao hayo na wananchi hufurahia kushuka kwa bei, hivyo basi wakati bei ikipanda pia wakulima wanatakiwa kuendelea kufurahia na kununua kwa wingi mazao hayo.

“Kuna watu wananipigia simu wakidai mishahara iongezwe kwa watumishi kwakuwa bei za mahindi na mchele zimepanda, na mimi nimekuwa nikiwajibu wakati bei ikipungua mbona hawajawahi kunipigia wakiniomba mishahara ipunguzwe” Alihoji Mhe Hasunga

Juzi Novemba 20, 2019 akizungumza na wananchi wa Gairo Mkoani Morogoro wakati akiwa safarini kuelekea Jijini Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliwataka wakulima na wafanyabiashara kupandisha bei ya mahindi kutokana na hali ya soko huku akisisitiza kuwa serikali anayoiongoza haitopanga bei elekezi ya mahindi.

Alisema serikali anayoiongoza haiwezi kupanga bei elekezi ya mahindi kwani kufanya hivyo itakuwa imefilisika kiutawala, hivyo mahindi yatajiendesha kulingana na soko kwani huu ni mwaka wa wakulima hivyo wapandishe tu bei kadri wawezavyo kulingana na soko.

Mhe Rais alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa kwa mwananchi yeyote atakayeona mahindi yamekuwa ya bei ya juu aende akalime ya bei ya chini.

Aidha, Waziri wa Kilimo amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kumkomboa mkulima ili kunufaika na jasho lake hivyo imnaendelea kuimarisha kitengo cha masoko ikiwa ni mkakati maalumu wa kuhakikisha kuwa wakulima wanajipatia kipato kizuri kwa kuwa na soko la uhakika la bidhaa za kilimo ndani na nje ya nchi.

MWISHO


Share:

Waziri Wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Azindua Msimu Wa Kilimo Mwaka 2019/2020

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 22 Novemba 2019 amezindua msimu wa kilimo Kitaifa mwaka 2019/2020 ambapo amewataka wakulima kote nchini kulima mazao ya chakula na biashara kwani serikali inaendelea kuimarisha masoko ya mazao ndani na nje ya nchi.

Katika uzinduzi huo wa msimu wa kilimo uliofanyika katika eneo la Vwawa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe amewahakikishia wakulima kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imeanzisha kitengo cha masoko chini ya wizara ya Kilimo ambacho moja ya kipimo chake kiutendaji ni kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ndani na nje ya nchi.

Alisema serikali imeweka msisitizo katika kuimarisha mazao mbalimbali ya chakula, biashara pamoja na mazao ya mbogamboga na matunda hivyo wakulima hawapaswi kuwa na wasiwasi na masoko ya mazao yao kwani yataendelea kuimarika maradufu.

Mhe Hasunga ameitaka Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuhakikisha kuwa inasimamia utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanauza mbolea kwa bei elekezi ili kuwanufaisha wakulima kwani mbolea ni miongoni mwa Pembejeo muhimu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wakulima wanalima mazao yenye tija.

Alisema kuwa mfanyabiashara yeyote atakayebainika kuuza mbolea zaidi ya bei elekezi anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni ya kufanya biashara hiyo.

Kuhusu Mbegu za mazao, Mhe Hasunga ameitaka Taasisi ya Udhibiti wa mbegu nchini (TOSCI) kuhakikisha kuwa mbegu zinazopelekwa kwa wakulima nchini zinakuwa katika ubora unaostahili huku akiagiza wauzaji wa mbegu feki kuchukuliwa hatua.

“Vilevile naagiza Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kuhakikisha kuwa wanazalisha mbegu za kutosha na kuzifikisha kwa wakulima kwa wakati ili katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020 kuwa na uzalishaji mkubwa na tija kwa wakulima” Alisema

Kwa upande wa Viuatilifu, Waziri Hasunga ameiagiza Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa Viuatilifu ukanda wa Kitropiki (TPRI) kuhakikisha wanafanya ukaguzi nchi nzima ili kubaini na kuondoa viuatilifu feki vyote sokoni.

Ameongeza kuwa TFRA inapaswa kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima kote nchini kuhusu matumizi sahihi ya Viuatilifu ili kuondoa dhana ya wakulima kuwa na malalamiko mengi kuhusu viuatilifu.

Aidha, Mhe Hasunga amesisitiza kuwa serikali inayoongozwa na Dkt Magufuli haitawapangia bei ya mazao yao wakulima hususani mazao makuu ya chakula na biashara kwani wakulima wanapokuwa wanalima mazao yao hakuna watu wanaowasaidia hivyo wakati wa kuuza pia wanapaswa kuamua bei kulingana na soko.

Mhe Hasunga pia amewataka wakulima kujihusisha zaidi na kilimo kinachozingatia hifadhi ya udongo (Climate Smart Agriculture) kwa kuchimba mashimo na kupanda mbegu kuliko kilimo kinachoharibu udongo kilichozoeleka.

MWISHO


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi November 23




Share:

Friday, 22 November 2019

Waziri Mabula Aagiza Kufuatiliwa Deni La Zaidi Ya Bilioni 1.9 Ya Kodi Ya Ardhi Kwa Taasisi Za Serikali

Na Munir Shemweta, WANMM KILOMBERO
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro kuzifuatilia taasisi za serikali zinazodaiwa kodi ya pango la ardhi kwenye halmashauri hiyo zaidi ya bilioni 1.9 ili ziweze kulipa deni hilo.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo jana alipokutana na uongozi wa wilaya ya Kilombero pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri za wilaya ya Kilombero na ile ya Mji wa Ifakara  wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro.

Agizo hilo la Dkt Mabula linafuatia kuelezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Injinia Stephano Kaliwa kuwa miongoni mwa wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika halmashauri yake ni taasisi za serikali zinazodaiwa zaidi ya bilioni 1.9.

Alizitaja taasisi hizo kuwa ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linalodaiwa zaidi ya bilioni 1.7 katika maeneo yake inayomiliki ya Kidatu shilingi 1,007,452.00, Kihansi 996,957,750.00 pamoja na Mlimba 29,826,650.00. Pia taasisi ya The Trustees of TANAPA nayo inadaiwa jumla ya shilingi milioni 12,819,550.00.

Hata hivyo, Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Remigi Lipiki alimueleza Naibu Waziri Mabula kuwa, TANESCO imetaka kufanyika uhakiki kwanza wa deni lake kwa madai kuwa baadhi ya maeneo inayomiliki yalishachukuliwa na taasisi nyingine na kutolea  mfano wa eneo la Kidatu.

Dkt Mabula alisema, halmashauri ya wilaya ya Kilombero lazima ihakikishe inazifuatilia taasisi hizo ili ziweze kulipa madeni ya kodi ya ardhi kwa kuwa taasisi hizo zimekuwa zikitenga fedha kwa ajili ya malipo ya huduma mbalimbali ikiwemo kodi hiyo ya pango la ardhi.

‘’Taasisi zinashindwa kulipa madeni na hazijachukuliwa hatua, haiwezekani deni lifikie zaidi ya bilioni moja, fuatilieni suala hili na mchukue hatua za kisheria.’’ alisema Dkt Mabula

Hata hivyo, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero alieleza changamoto kubwa inayoikabili halmashauri yake kuwa ni ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa baadhi ya wawekezaji wa Mashamba kutokana na kutokamilika taratibu za uhaulishaji mashamba hayo ambayo wamiliki wake hawana nyaraka.

Aliataja baadhi ya wamiliki wa mashamba hayo kuwa,  ni Kampuni ya Mufindi Paper Mills yenye hekta 10,000 , Green Resource Limited hekta 25,000, Hiragro Ltd hekta 1500 na Sygen yenye ekari 30,000.

Kwa mujibu wa Kaliwa, kutokana na kutokamilika mchakato wa uhaulishaji wa mashamba hayo kumekuwa na upotevu wa makusanyo ya kodi ya jumla ya shilingi 132,865,031.00 kila mwaka.


Share:

Spika Ndugai atoa neno kwa Mbunge atakaye kataa bajeti ya serikali


Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema mbunge anayekataa bajeti ya Serikali bungeni ni mpuuzi.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo wakati akiahirisha Bunge la sita la Vijana la mwaka 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa, mjini Dodoma.

"Kuna mambo matatu katika bajeti, kusema ndio, hapana au kukaa kimya ambako ni ishara ya kuwa hujakataa au  kukubali lakini unasema hapana kwa sauti kubwa hivi unamwelewa mtu huyo kweli," amesema Ndugai.

Spika amesema bajeti zinazokataliwa na wapinzani huwa zimebeba mishahara yao na watumishi wengine,  fedha za miradi ya maendeleo na kwamba kusema hapana ni sawa na kutaka kila kitu kisipelekwe.


Share:

UNDER THE SAME SUN YAKUTANA NA WANAWAKE WENYE UALBINO,WANAWAKE WENYE WATOTO WENYE UALBINO MWANZA


Na George Binagi-GB Pazzo, Mwanza

Shirika la Under The Same Sun linaloshughulika na utetezi wa haki za watu wenye ualbino Tanzania limetoa mafunzo kwa wanawake wenye ualbino pamoja na wanawake wenye watoto wenye ualbino mkoani Mwanza ili kuwajengea uwezo kuhusu hali ya ualbino.
Mafunzo hayo ya siku tatu yameanza Novemba 22, 2019 jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Mfuko wa Kanada kwa ajili ya Mipango ya Kijamii (Canadian Fund for Local Initiative- CFLI) unaotekelezwa katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga.

Mratibu wa mradi huo, Grace Wabanhu amesema matarajio baada ya mradi huo wa miezi minne kufikia tamati ni wanawake hao kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu hali ya ualbino na hivyo kuwa na ujasiri wa kuielimisha jamii inayowazunguka ili kuondokana unyanyapaa na ukatili dhidi ya watu wenye ualibino na hatimaye kuleta usawa katika jamii.


Naye Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino (TAS) Mkoa Mwanza, Alfred Kapole amesema akina mama ni jeshi kubwa hivyo baada ya kuelimishwa kupitia mradi huo watakuwa mabalozi wazuri wa kutoa elimu katika jamii kuanzia ngazi ya nyumbani na hatimaye kusambaa hadi vijijini.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo mama mwenye mtoto aliye na ualbino, Shika Madebe kutoka wilayani Misungwi wameahidi kuitumia vyema elimu watakayoipata kwa kuwaelimisha wanajamii wengine ambao bado hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na ualibino na hivyo kuondokana na unyanyapaa dhidi ya watu wenye ualibino ambao wamekuwa wakiitwa majina mabaya.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Tazama Video hapa chini

Share:

MOE: Stipendium Hungaricum Scholarships to eligible Tanzanian Nationals 2020/2021

THE STIPENDIUM HUNGARICUM SCHOLARSHIP TENABLE FOR THE ACADEMIC YEAR 2019/2020. MOE: Stipendium Hungaricum Scholarships to eligible Tanzanian Nationals 2020/2021 1.0 Call for Application The General public is hereby informed that the Government of Hungary has opened new Stipendium Hungaricum Scholarships to eligible Tanzanian Nationals to pursue undergraduate and postgraduate studies at Universities in Hungary for the academic year… Read More »

The post MOE: Stipendium Hungaricum Scholarships to eligible Tanzanian Nationals 2020/2021 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

BABU WA MIAKA 71 ATANGAZA KUOA MKE WA 9...ATAFUNGA NDOA FEBRUARI 2020


 Babu Ron Sheppard akiwa na mke wake wa nane.

Ron Sheppard (71) kutokea nchini Uingereza, ni maarufu kwa jina la Muingereza ambaye mpaka sasa ameshaoa mara nane na wake zake wote ameachana nao na sasa anajipanga kuoa kwa mara ya tisa.

Ndoa hiyo ya tisa anatarajia kuifunga Februari 2020, na mwanamke anayejulikana kwa jina la Rose Hans, mwenye miaka 30, ambaye amemaliza kozi ya udaktari nchini Ghana, na anajipanga kuhamia nchini Uingereza.

Kupitia mtandao wa The Sun Online, Babu huyo amesema "Najua Rose ni mmoja wao haijalishi kama tumekutana wapi ila nachoweza kusema tuna muunganiko mzuri, umri ni namba tu sijali kama ni nusu ya miaka yangu au zaidi ana mapenzi na mimi na nampenda yeye" .

Historia yake inasema kwa sasa ni Baba wa watoto nane na ndoa yake ya kwanza alifunga akiwa na miaka 19, ilikuwa 1966, ambayo ilidumu kwa miaka miwili na kupata watoto watatu, ndoa ya pili alifunga 1973-1974, ndoa ya tatu ilikuwa 1976 na ilidumu kwa miaka mitano, ndoa ya nne ilifanyika mwaka 1982-1986.

Ndoa ya tano 1986-1997 na alipata watoto wawili wa kiume ya sita ilikuwa 1999 na alichana baada ya kumsaliti mkewe 2003, ndoa ya saba ilidumu kwa miezi 8 tu, ndoa ya nane alifunga mwaka 2004 na ilidumu kwa miaka 11 hadi kufikia 2015.

Source by The Sun Online.
Share:

Rais Magufuli awapa polisi ofisi Ya Makao Makuu Dodoma Yenye Ghrorofa Nne

Rais Dk. John Magufuli, amewapa ofisi jeshi la polisi jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya jeshi hilo na serikali kuhamia jijini humo.

Akizungumza katika uzinduzi wa ujenzi wa nyumba za polisi eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo Ijumaa Novemba 22, amesema anawakabidhi jengo la ghorofa nne lililokuwa linatumiwa na Uwasa ambapo yatakuwa makao makuu ya jeshi hilo.

“IGP nimefurahi umesema umehamia hapa Dodoma, ningeshangaa kuona mimi nimehamia hapa wewe bado hujahamia, ningeteua IGP wangu wa hapa Dodoma.

“Lakini kwa sababu umewahi umehamia hapa nakushukuru na kwa sababu umehamia kufanya hivyo kwa sababu askari hasubiri nyumba nimeamua kuwapa zawadi, siyo hela mimi sitoagi hela nimeamua kwa vile mmeshatekeleza wito wa kuhamia hapa na sitaki kujua mmehamia wapi inawezekana  mnakaa kwenye miembe kwenye nini, lakini jukumu lenu mmelifanya la kuhamia hapa nimewamua kuwapa jengo moja kubwa lenye ghorofa nne lilikouwa linatumiwa na Uwasa.

“Sasa ndiyo yatakuwa Makao Makuu ya Polisi na ninakupa picha zenyewe ni matumaini yangu leo nitaona makao makuu ya polisi kwenye jengo hilo,” amesema Rais Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli amesema serikali imeshahamia Dodoma hakuna lugha nyingine kwamba watahamia, hapa ndiyo makao makuu hakuna jingine na watabanana hapa hapa kwa wagogo hakuna namna.

“Dodoma inapendeza, Dodoma inavutia. Na katika miaka michache ijayo jiji hili litaipita hata jiji la Dar es Salaam na majiji mengine,”- amesema.


Share:

LIVE: Ziara Ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli Jijini Dodoma .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 22 Novemba, 2019 ataweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru katika eneo la Maduka Chamwino, ataweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 118 za askari polisi katika eneo la Nzuguni, ataweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma katika eneo la Nzuguni, ataweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Soko Kuu la Dodoma katika eneo la Nzuguni na kisha atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.


Share:

Nafasi Mpya Za Kazi Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi-NEC

Kwa  Nafasi mbalimbali  za Kazi kama hizi <<INGIA HAPA>. Kupata Ajira  Yako sasa

Kwa  Nafasi mbalimbali  za Kazi kama hizi <<INGIA HAPA>. Kupata Ajira  Yako sasa


Share:

Head; Compliance at NMB Tanzania

Head; Compliance   Reporting Line: Chief, Risk and Compliance Job Purpose Asses the adequacy of efforts made by Management and operational staff in complying with regulatory requirements and support management in building a robust compliance culture based on ethical standards of behavior and thus contributing to effective corporate governance. Introduce, review, seek approval and implement all compliance related policies.… Read More »

The post Head; Compliance at NMB Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Human Resources Officer (HRO) at Lifewater- November 2019

Position Title:                             Human Resources Officer (HRO) Managers Position:                   Country Director Direct Reporting Positions:      None Position Location:                     Shinyanga, Tanzania (with regular travel to the project areas) Lifewater is… Read More »

The post Human Resources Officer (HRO) at Lifewater- November 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Jinsi Ya Kuandika CV Nzuri Ambayo Itamvutia Mwajiri na Kukufanya Upate KAZI Kirahisi

WATU wengi nchini wamekosa ajira  kwa sababu ya makosa wanayoyafanya wakati wa kuandika CV zao.

Kumbuka,  makampuni  karibia yote yanayotangaza nafasi za kazi hupokea wastani wa maombi 200-500 ya kazi kwa tangazo moja la kazi. 

Hivyo, CV yako lazima ikae vizuri ili kumshawishi mwajiri. Utaratibu wa kuomba kazi unaweza ukawa tofauti kati ya makampuni na mashirika, ila yote yatahitaji uwatumie CV.

CV ni nini?
CV ni maelezo ya ujumla kwa kiundani ya historia yako ya kazi na shule. Kawaida, inatumika kwenye maombi ya kazi ya nafasi za kati, za juu na za utafiti.

Mambo yafuatayo yatasaidia kuifanya CV yako iwe bora na hivyo, kukusaidia kupata interview za kazi.

👉Soma na kuelewa maelezo ya kazi
Una ujuzi gani? Mwajiri anatafuta mfanyakazi wa aina gani? Maswali haya ni muhimu kujua kama utaiweza hiyo kazi au la. Pia, ni vizuri kujua nini hasa ni muhimu kwa muajiri na kufanya maombi yako yaendane zaidi na mahitaji ya mwajiri.

Kwa mfano, kama kazi inaweka umuhimu kwenye ujuzi wa kutumia mitandao ya kijamii kwa matangazo, hakikisha CV yako ina kazi zote zilizohitaji matumizi ya mitandao ya kijamii.

👉Andika maneno muhimu yaliyotumika kwenye maelezo ya kazi, uyatumie kwenye CV
Usichukue sentensi nzima kutoka kwenye maelezo ya kazi na ukaitumia vile vile kwenye CV yako. Ila, tumia lugha na baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye CV.

👉Fanya utafiti juu ya kampuni iliyotangaza kazi
Pamoja na kuchambua maelezo ya kazi, ni muhimu kufanya utafiti juu ya kampuni yenyewe. Kama wana tovuti au wapo kwenye mitandao ya kijamii, jaribu kujua ni kazi gani na sekta ipi wanayohusika nayo. 

Pia, ikiwezekana jaribu kuwajua wafanyakazi/meneja wa kampuni hiyo. Hii itakusaidia kujua maadili na muelekeo wa kampuni. Hii itakusaidia kuweka maombi yako ya kazi yaendane na kampuni hiyo.

👉Orodhesha ujuzi wako wakufanya kazi
Hapa, usiweke kazi zote ulizozifanya maishani mwako ila, weka zile ambazo zilikuongezea ujuzi utakayo kusaidia kufanya kazi unayoomba.

==>Format/Staili inayotumika zaidi kwenye kuandika CV:
   1. Lengo la CV na ujuzi wako
    2.Ujuzi wako wa kazi
   3. Mafanikio maalum
   4. Elimu
   5. Ujuzi muhimu binafsi

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Angalizo:
  1.  Tumia maandishi ya kawaida ya Times New Roman
  2.  Tumia size 9 – 12 ya herufi
  3.   Hakikisha unatumia staili moja ya kuandaa CV kote
  4.   CV isiwe zaidi ya ukursasa 2
  5.   Usitumie sentensi ndefu
  6.  Hakikisha CV yako inasomeka kiurahisi na inawasilisha   mafanikio yako kwa uwazi.
  7.  Anza na kazi yako ya sasa hivi au ya hivi karibuni alafu rudi nyuma.
   ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 
   ==>.Hakikisha Yafuatayo:
1.Ukiwa unaandika jina la kampuni uliyo fanya kazi, andika jina la kampuni kikamilifu. 
2.Eleza kwa ufupi kampuni yao inahusika na nini. 
3.Tatu, weka muda uliyofanyakazi hapo (mwezi na mwaka).  
4.Baada ya hapo, orodhesha kazi na majukumu yako kwenye hiyo kampuni.
5.Usidanganye

👉Maandalizi ya Mwisho

1.Pitia kila kitu kwa mara ya mwisho
 -Print CV yako alafu ipitie. Hii huwa inasaidia kuona makosa yako.

2.Mpe Rafiki  yako apitie CV
-Muombe rafiki yako apitie CV yako. Macho manne ni bora zaidi ya mawili!

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

Hatua ya kwanza kwenye kupata kazi unayotaka ni kutuma maombi. Tunatumaini kwamba maelezo yaliyoelezwa humu yatakusaidia kuandaa CV bora kwa ajili ya mwajiri.

👉Sasa, kwa kuwa umeshajua jinsi ya kuandika CV nzuri, anza kutafuta kazi unayoitaka kwa kubofya hapo chini.

AU 



Share:

Senior Finance & Accounting Officer at Life water International

Senior Finance & Accounting Officer at Life water International Position Title:      Senior Finance & Accounting Officer Manager Position:   Country Director Direct Reporting Positions:  Accounts Assistant Position Location:       Shinyanga, Tanzania (with regular travel to the project areas) Lifewater International (Lifewater) is a Christian water development organization dedicated to effectively serving children and families by partnering with… Read More »

The post Senior Finance & Accounting Officer at Life water International appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Mkuu wa Mkoa Aamuru Mkandarasi Manispaa ya Bukoba na Mkuu wa Shule Wakamatwe na Kuwekwa Ndani

Na avitus benedicto kyaruzi,Kagera
Mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Marco Elisha Gaguti amemuagiza Kamanda wa polisi mkoani humo Revocatus Malimi kuwakamata na kuwaweka ndani mara moja mkandarasi wa manispaa ya Bukoba, Mkandarasi wa  Kampuni ya Mzinga Holding Company ambaye pia ni msimamizi wa ukarabati wa Shule ya Sekondari Kahororo, mkuu wa shule ya Sekondari Kahororo pamoja na kaimu mkuu wa shule ya  Bukoba secondari kutokana na kushindwa kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya shule hizo kwa wakati uliopangwa.
 
Hayo yamejili  Novemba 22,2019 baada ya Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na kamati ya  Manispaa ya Bukoba Mkoani humo ilipofanya ziara mbalimbali ili kukagua baadhi ya miradi kwa upande wa manispaa ya Bukoba ikiwemo elimu, afya,pamoja na miundombinu ya barabara.
 
Waliokamatwa ni Mhandisi wa manispaa ya Bukoba bw,George Geofrey, Mkandarasi wa  Kampuni ya Mzinga Holding Company ambaye pia ni msimamizi wa ukarabati wa Shule ya Sekondari Kahororo,bw Festo Talimo ,Mkuu wa Shule ya sekondari kahororo bw Omary Ogambage pamoja na makamu mkuu wa Shule ya Sekondari Bukoba bw,Phocus Siasa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wasimamizi wa miradi hiyo mkuu wa mkoa wa kagera Brigedia Gaguti amesema kuwa miradi hiyo kwa ujumla mpaka hivi sasa haifanyi vizuri na kutoa msisitizo kwa watu wanaosimamia miradi hiyo kukamilisha kwa wakati na muda uliopangwa pasipo  kuomba muda wa nyongeza.
 
“ Watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia miradi hiyo  wasimamie ili iweze kukamilika kwa muda uliopangwa lakini pale ambapo kuna uzembe tuliokuwa tukiuona  katika baadhi ya maeneo tutachukua hatua sitahiki ”
 
Ameongeza kuwa ataendelea kuchukua hatua stahiki kwa watendaji wa miradi hiyo watakaoshindwa kukamilisha kwa wakati  miradi hiyo na hakuna mkandarasi atakayeondoka mkoani Kagera kabla ya kukamilisha mradi anao simamia.
 
Kadhalika Brigedia Gaguti amesema kuwa miradi hiyo imepokea shilingi bilioni 12 kutoka fedha za serikali kuu kwa mwaka wa fedha kwa upande wa manispaa ya Bukoba mkoani humo na kuwataka wakandarasi kuongeza kasi ili wasije kulipa dhamana yao kwa uchungu huku akihaidi ushirikiano wa kutosha kwa wasimamizi wa miradi hiyo pale watakapo kuwa wamekwama.


Share:

Waziri Wa Kilimo Afanya Ziara Ya Kushitukiza Kukagua Bei Na Upatikanaji Wa Mbolea Mkoani Songwe

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)  tarehe 21 Novemba 2019 amefanya ziara ya kushitukiza ili kujionea hali ya upatikanaji wa mbolea katika baadhi ya vijiji mkoani Songwe.

Katika ziara hiyo Mhe Hasunga kadhalika amekagua na kujionea kama wafanyabiashara wanauza mbolea kutokana na maelekezo ya serikali iliyopanga bei elekezi na kuitangaza hivi karibuni.

Akiwa katika ziara hiyo ya kikazi katika kijiji na Kata ya Ipunda katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mhe Hasunga amempongeza mfanyabiashara wa pembejeo kijijini hapo Ndg Lukas Simkonda kwa kuuza mbolea kwa gharama ya chini kuliko bei elekezi.

“Wewe ni miongoni mwa wafanyabiashara tunaowataka, serikali imepanga bei elekezi lakini wewe umeamua kuuza chini ya bei elekezi ili kuwanufaisha zaidi wakulima, jambo hili sisi kama serikali tunaliunga mkono na kukupongeza kwa dhati kwa kazi ya kizalendo unayoifanya” Alisisitiza Mhe Hasunga

Katika hatua nyingine Wafanyabiashara wa mbolea nchini wametakiwa kuuza bidhaa hiyo kwa kufuata bei elekezi zilizotangazwa na Waziri wa Kilimo hivi karibuni kwani lengo la serikali ni kuhakikisha wakulima wanapata mbolea ya uhakika na kwa bei nafuu.

Aliitaja sababu ya kuwa na bei elekezi ya mbolea kuwa ni kukuza kilimo na kuongeza mavuno ya mazao ambayo ndio malighafi kuu inayohitajika wakati huu ambapo serikali inatekeleza mipango ya ukuaji wa viwanda, kama msingi mkuu wa uchumi.

Katika ziara hiyo Mhe Hasunga akiwa katika zahanati ya Ipunda katika Jimbo lake la uchaguzi la Vwawa amewapongeza wakazi wa kijiji hicho kwa kujitokeza kwa wingi kupima Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwani amesema kupima afya ni msingi wa uimarishaji wa afya zao.

Vilevile Mhe Hasunga amewataka wakulima kula chakula kizuri chenye mchanganyiko wa mbogamboga na matunda. “Wakulima wangu mnaniangusha maana ninyi mnalima na kuzalisha chakula cha kutosha lakini ajabu ninyi ndio mnaongoza kutokula vizuri jambo hili sio sahihi kabisa, mnapaswa kuimarisha afya zenu kwa kula vizuri” Alisema Mhe Hasunga

Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amewapongeza wajasiriamali Wilayani Mbozi kwa kuanzisha viwanda vidogo vya ubanguaji wa karanga kwani vitaongeza uwezekano wa wakulima kuongeza uzalishaji wa karanga kwakuwai nyenzo za kubangua zitakuwepo kutokana na teknolojia hiyo ya kisasa.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ameanza ziara ya kikazi ya siku 6 mkoani humo ambapo pamoja na mambo mengine anakagua hali ya upatikanaji wa mbolea pamoja na kukagua kama wafanyabiashara wanauza mbolea kutokana na bei elekezi iliyowekwa na serikali.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger