Saturday, 26 October 2019

LIVE: Hafla Ya Mapokezi Ya Ndege Mpya Boeing 787-8 Dreamliner Ya Air Tanzania

LIVE: Hafla Ya Mapokezi Ya Ndege Mpya Boeing 787-8 Dreamliner Ya Air Tanzania


Share:

WATU NANE WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI KUTUMBUKIA MTONI TANGA




Watu nane wamefariki dunia wilayani Handeni mkoani Tanga, baada ya gari walilokuwa wanasafiria, kutumbukia mtoni kutokana na daraja kukatika. 

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu, leo tarehe 26 Oktoba 2019, Edward Bukombe, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, amesema anafuatilia tukio hilo. 

Kamanda Bukombe amesema yuko njiani kuelekea eneo la tukio, na kwamba atatoa taarifa kamili kuhusu tukio hilo, pindi atakapofika eneo la tukio.

“Hizo taarifa nimezipata na sasa hivi niko barabarani naelekea eneo la tukio, nikifika nitawajulisha kilichotokea. Maana kwa sasa niko mbali na tukio,” amesema Kamanda Bukombe.

Chanzo- Mwana Halisi Online
Share:

Mvua yasababisha mafuriko wilayani Korogwe.....Mamia ya abiria wakwama

Mamia ya abiria waliokuwa wanasafiri kutoka Arusha, Kilimanjaro na nchi jirani na waliotoka Dar es Salaam kuelekea mikoa mbalimbali wamekwama tangu jana mchana Ijumaa Oktoba 25, 2019 wilayani Korogwe na Handeni Mkoa wa Tanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea kuimarisha usalama kwa abiria wote, waliokwama kuendelea na safari baada ya maji kujaa juu ya daraja ili kuepusha madhara makubwa hususani wale ambao watalazimisha kuvuka.

Kauli hiyo ameitoa leo ambapo amesema kuwa abiria ni wengi kwani wanaongezeka kila muda na kwamba wameshindwa kupata idadi kamili ya watu waliokwama kwa hizo pande zote mbili.

"Bado njia haijafunguka kule Handeni tulikokuwa tunapategemea kupita daraja lilishakatika kabisa kwahiyo hakuna mawasiliano na hii ya Segera - Korogwe na yenyewe bado maji yanapita juu, kwahiyo tunasubiri maji yapungue ili tuone uimara wa daraja na gari kama zinaweza zikapita", amesema Kamanda Bukombe.

"Tunachokifanya kwa sasa ni kuimarisha ulinzi ili yasiwepo madhara ya kuibiwa na wale ambao huwa wanataka kuvuka kwa kutumia nguvu'', ameongeza.

Inakadiriwa kuwa abiria zaidi ya 5,000, kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na hata nchi jirani na wale waliokuwa wanatoka Dar es Salaam kwenda katika mikoa hiyo wamekwama siku ya jana ya Oktoba 25, 2019, wilayani Korogwe na Handeni, kufuatia mvua kubwa inayonyesha na kupelekea maji kujaa juu ya daraja na huku lingine likisombwa na maji.
 


Share:

Wizara ya Afya: Call for replacement Jobs-Ajira za Afya 2019

Wizara ya Afya: Call for replacement Jobs-Ajira za Afya 2019 The Office of the President – Regional Administration and Local Government (OR-GOVERNMENT) wishes to notify applicants of the various health cadres who have submitted applications from 22/07/2019 to 05/08/2019 for the process of organizing work centers completed in the second phase. This phase is for the filling of… Read More »

The post Wizara ya Afya: Call for replacement Jobs-Ajira za Afya 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Watatu Kizimbani kwa Kukutwa na Tausi wa Ikulu

Watu watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la  kukutwa na ndege watatu aina ya tausi waliokuwa Ikulu wenye thamani ya zaidi ya Sh3.4milioni.

Washtakiwa hao wanaokabiliwa na kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 116/2019 ni David Graha, Mohamed Hatibu na Mohamed Ally.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alisema  Juni Mosi 2015 na Oktoba 14, mwaka huu jijini Dar es Salaam, washtakiwa walijihusisha na mtandao wa uhalifu ambapo wanadaiwa kuratibu genge la uhalifu wakijihusisha na biashara ya ndege aina ya Tausi bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Katika shitaka la pili, Nchimbi amedai katika tarehe hizo washitakiwa walikutwa na ndege watatu aina ya tausi wenye thamani ya USD 1,500 ambazo ni sawa na Sh milioni 3.4 mali ya serikali bila kuwa na kibali.

Pia Oktoba 14, mwaka huu maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Ally alikutwa na ndege watatu aina ya Tausi wanaopatikana Ikulu, ambao aliwapata kwa njia zisizo halali huku katika shtaka la tano, washtakiwa i Graha na Hatibu katika tarehe hizo hizo walijipatia Sh 300,000 huku wakijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la wizi.

Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo waliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na kuzingatia kwamba mashitaka hayo hayana dhamana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 7 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa walirudishwa rumande kwa sababu mashitaka hayo hayana dhamana.


Share:

198 Ajira za mkataba taasisi ya Benjamini Mkapa Octoba 2019

Benjamin Mkapa Foundation (BMF) The Benjamin William Mkapa Foundation is trust, non-profit making organization, established and incorporated under the Trustees Incorporation Ordinance, CAP 375. We aim to supplement and complement the development efforts of the Government of the United Republic of Tanzania.The Foundation was established after the launching of its first initiative known as the “Mkapa Fellows Programme”… Read More »

The post 198 Ajira za mkataba taasisi ya Benjamini Mkapa Octoba 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Ndege ya pili Boeing 787-8 Dreamliner yaondoka Marekani....Kutua nchini leo mchana

Ndege mpya ya pili aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imeondoka nchini Marekani jana Ijumaa, Oktoba 25, 2919 kuja Dar es Salaam Tanzania.

Ndege hiyo kubwa yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo mchana Oktoba 26, 2019.

Ndege hiyo itapokelewa na wananchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Hii inakuwa ndege ya 8 kati ya ndege 11 zilizonunuliwa na Serikali kwa lengo la kuimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kukuza utalii na uchumi.


Share:

Tatizo la Uhaba wa vitabu kwa wanafunzi katika shule za msingi katika Halmashauri ya Mji Kahama kuwa historia

NA SALVATORY NTANDU
Katika Jitihada za kukabiliana na uhaba wa vitabu vya Masomo ya sayansi na hisabati katika Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinayanga Idara ya elimu Msingi imegawa vitabu elfu 88,652 vya darasa la awali hadi darasa la tano katika shule za msingi 72 zilizopo Halmashauri hiyo ili kukuza  kiwango cha taaluma.

Hayo yamebainishwa jana na  Afisa Elimu, Vifaa na Takwimu Mwalimu Sadick Juma,wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema kuwa Vitabu hivyo ni vya masomo ya Hesabu, Kiswahili, kingereza, Sayansi, Uraia na Maadili, Maarifa ya jamii ambavyo ni maalumu kwa  wanafunzi wa darasa la awali hadi tano.

Amesema hapo awali kulikuwa na tatizo la uhaba wa vitabu ambapo wanafunzi watatu walikuwa wanatumia kitabu kimoja hivyo upatikanaji wa vitabu hivyo utakuwa suluhisho kwani kwa sasa kila mwananfunzi atakuwa anatumia kitabu chake mwenyewe.

Vitabu hivyo vimegawanyika katika makundi yafuatayo  Kiswahili darasa la tatu vitabu 2676,kusoma darasa la kwanza 4133,kuhesabu darasa la kwanza 4133,sayansi darasa la tatu 2676,hisabati darasa la tatu 2676,kiingeza darasa la tano 300.

Kiswahili darasa la nne 2739,uraia na maadili darasa la nne 2672,maarifa ya jamii darasa la tatu 114,hadithi darasa la awali 24,kifaransa hatua ya kwanza kwa darasa la kwanza hadi la tatu 277 na darasa la nne hadi la saba 277, na hisabati darasa la tatu 376

Amefafanua kuwa mbali na kugawa vitabu hivyo kwa  wanafunzi wa darasa la awali hadi latano, pia Halamshauri hiyo inatarajia kupokea vitabu vingine kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la sita na la saba huku asilimia kubwa ya vitabu hivyo vikiwa vya masomo y sanyansi na hisabati.

Katika Hatua nyingine Mwalimu Juma  Hata amesema  kuwa, mbali nakutoa vitambu hivyo bado wanakabiliwa na  uhaba wa walimu katika shule za msingi ambapo mwaka jana wa 2018 Halmashauri ya mji wa kahama ilipokea walimu 20 wapya  ambapo wanauhitaji wa walimu zaidi ya 600.

Mwalimu Juma alitolea mfano Shule ya msingi Mhungula inawanafunzi 4000uhitaji wawalimu 88 na walipo 39, na Shule ya Msingi majengo inajumla ya wanafunzi 2800 na inauhitaji wa walimu 64 na walipo ni 36 laki shule hizi zimeonekana kufanya vizuri katika mtihani mbalimbali ya kitaifa.

Amesema Katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu ,shule tatu kati ya shule za msingi 72 za serikali zilizopo Halmashauri ya mji wakahama zimefanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba ambazo ni shule ya msingi Kinaga iliyoshika nafasi ya kwanza katika Halmasghauri hiyo,Kilima B, Majengo pamoja na Kahama B,na shule zilizofanya vibaya ni shule ya msingi Bukooba, Mpera, Bujika na Shule ya msingi Nyandekwa.


Share:

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Ahudhuria Mkutano Wa Mawaziri Wa AU Mjini Addis Ababa

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega yuko nchini Ethiopia ambapo anahudhuria mkutano wa mawaziri wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wanaohusika na Kilimo, mifugo, uvuvi, mazingira, maji na Maendeleo Vijijini.

Mkutano huo ulioitishwa na Kamisheni ya Afrika kupitia Shirika lake la kusimamia Maendeleo ya Rasilimali za Wanyama Barani Afrika (AU-IBAR), unafanyika kwa siku mbili mjini Addis Ababa ambapo mbali na mambo mengine mkutano huo utapokea ripoti na maazimio mbalimbali kutoka kwa wataalam wa sekta hizo kujadili na kuyapitisha ili waweze kupeleka Halmadhauri Kuu ya AU kwa maamuzi na utekezaji.

Moja ya mikakati, ripoti na maazimio na mapendekezo yanayotarajiwa kujadiliwa na kuridhiwa na baraza hilo la mawaziri wa AU wa sekta ya mifugo, uvuvi, kilimo, mazingira na maji ni ripoti ya miaka miwili ya Tathmni ya Azimio la Malabo (Malabo Declaration) lenye lengo la kuondoa njaa katika bara ka Afrika ifikapo Mwaka 2025 na ripoti ya Tathnimi ya kuwasiliana na Majanga ya asili kama mafuriko na ukame.

Maazimio na mapoendekezo mengine ni ripoti ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabia nchi, juhudi za nchi wanachama kuzuia matumizi ya bidhaa za plastiki, mkakati wa kupanda mazao yenye viini lishe vya kutosha na mkakati wa kukabiliana na upotevu wa mazao ya mimea na samaki baada ya kufunga (Post harvest Loss).

Katika kikao hicho pia kitajadili mkakati wa kupambana na magonjwa na vimelea sugu kwa mifugo, mpango wa kuanzisha maabara za kupima ubora wa chakula katika bara la Afrika, mpango wa pamoja wa kuwa na kusimamia na kuweza katika wazo la uchumi wa bahari (Blue economy), mpango mkakati wa miaka 10 kuendeleza uvuvi mdogo mdogo (small scale fisheries) na mpango mkakati wa miaka 10 wa kuendeleza sekta ya ukuzaji viumbe maji.

Mkutano huo ulifunguliwa na Balozi Bi. Josefa Correia Sacko Mkuu wa Kamisheni ya Afrika ya Kilimo na maendeleo vijijini, ambapo zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi 49 za bara la Afrika wanahudhuria wakiwepo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa kama FAO, WWF, Benki ya Dunia na NEPAD.

Mwisho.


Share:

Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Magufuli Katika Mkunao Wa 18 Wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Oktoba 26, 2019 anatarajiwa kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 18 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) kutoka Afrika na kwingineko duniani utakaofanyika Baku, Azerbaijan.

Mkutano huo unalenga kujadili namna ya kutatua changamoto za kisiasa, kiuchumi na kijamii zinazokabili nchi wanachama wa NAM katika nyakati za sasa, pamoja na na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maslahi ya nchi wanachama wa umoja huo.

Waziri Mkuu aliwasili nchini Azerbaijan jana (Ijumaa, Oktoba 25, 2019) na alipokelewa na Naibu Waziri Mkuu wa Azerbaijan, Bw. Ali Ahmadov pamoja na viongozi wengeine wa Serikali hiyo. Mapokezi hayo yalifanyika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heydar Aliyev.

Ajenda za mkutano huo ni kupokea ripoti za mkutano wa maandalizi wa Mawaziri, kupokea ripoti ya mkutano wa maandalizi wa Maafisa Waandamizi, uchaguzi wa nchi zitakazokuwa wajumbe katika ofisi ya uratibu wa shughuli za NAM, New York kwa kipindi cha mwaka 2019-2022.

Mbali na ajenda hizo, pia ajenda nyingine za mkutano huo ni kupokea ripoti za shughuli za umoja huo zilizotekelezwa chini ya Mwenyekiti wa NAM, Venezuela, mjadala mkuu, pamoja na kupitisha maandiko yatokanayo na mkutano.

Mheshimiwa Majaliwa ameambatana na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Damasi Ndumbaro na Balozi wa Tanzania Nchini Urusi ambale pia ni Balozi wa Azerbaijan, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Mumwi.

Awali, Waziri Mkuu alikuwa Sochi nchini Urusi ambako pia alimwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika Mkutano wa Uchumi kati ya Urusi na Afrika (Russia - Africa Economic Forum) na baadae Mkutano wa wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Mataifa ya Afrika uliofunguliwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, OKTOBA 26, 2019


Share:

Meli Mpya Ya MV Victoria Tayari Imeanza Kujengwa .....Wananchi Kagera Kunufaika Tena

Na: Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera
Wakati Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli inaendelea kujenga miradi mikubwa ya kimkakati ya kuelekea katika uchumi wa kati bado Mkoa wa Kagera haujasaulika bali sasa wananchi wake wanakumbushwa kujiandaa kikamilifu kwa kuchapa kazi za kilimo na biashara wakati nchi inaelekea katika mapinduzi makubwa ya kiuchumi ili kutembea na kasi ya uchumi wa kati.

Ni baada ya meli ya MV Victoria meli kongwe na maarufu kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera  kukamilika ukarabati wake ifikapo Machi 2020 na kurejea katika Ziwa Victoria kwa kufanya kazi kati ya bandari za Mwanza, Bukoba na Kemondo  kusafirisha abiria zaidi 1000 pamoja na mizigotani 200 ambapo kutakuwepo na nafuu kubwa ya bidhaa za viwandani pamoja na usafiri wa wananchi kati ya Bukoba na mwanza.

Uhakika wa meli ya MV Victoria kukamilika ukarabati wake mwakani Machi 2020 pia na ujenzi wa meli mpya ulishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti pamoja na Kamati ya amani ya Mkoa wa Kagera iliyowajumuisha viongozi wa dini watatu Askofu Methodius Kilaini Askofu msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba, Askofu Dk. Abednego Keshomshahara  Askofu wa (KKKT) Jimbo la Kasikazini Magharibi na Sheikh Haruna Kichwabuta Sheikh wa Mkoa wa Kagera.

Mkuu wa Mkoa Gaguti akiwa katika ziara hiyo ya kutembelea na kujionea maendeleo ya ukarabati  na ujenzi wa Meli mpya pamoja na cherezo katika Bandari ya Mwanza Kusini alisema kuwa anampongeza Rais Magufuli  kwa kuleta mradi huo kwa ajili ya ukombozi wa kiuchumi  wa wananchi wa Kagera kwani utaweka usafiri wa uhakika pia alitoa wito kwa wananchi wa Kagera kujielekeza katika kazi zenye tija za kilimo na biashara na kujiandaa kutumia maboresho ya usafiri kuinua uchumi wa mkoa.

Askofu Msaidizi Methodius Kilaini baada ya kuiona miradi hiyo mitatu alisema kuwa anamshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kutekeleza maajabu katika miradi ya ujenzi na ukarabati wa meli, aidha alisema kuwa Mkuu wa Mkoa Gaguti amewafanyia jambo jema sana la kuwafanya wao kama viongozi wa dini wapate nguvu ya kuleta tumaini na uelekeo kwa watu na kuufanya Mkoa wa Kagera kusimama tena kiuchumi.

Askofu Dk. Keshomshahara mara baada ya kujionea ujenzi wa meli mpya na cherezo na ukarabati wa Meli ya MV Victoria alisema kuwa sasa wao kama viongozi wa dini wamepata neno la kuwaeleza waamini wao na kuwahamasisha kujiandaa kwaajili ya kuitumia fursa ya Meli hizo zikikamilika . Sheikh Haruna Kichwabuta naye alisema kuwa Rais Magufuli alihaidi wakati wa kampeini sasa ametekeleza bila ahadi hewa hasa kwa wananachi wa Mkoa wa Kagera.

Bw. Eric B. Hamissi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za meli nchini alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti kutembelea miradi hiyo ya ujenzi na ukarabati wa meli na kutoa wito kwa wananchi na viongozi wengine nchini kwenda kutembelea miradi hiyokujionea maendeleo ya ujenzi wa meli mpya na cherezo pia na ukarabati wa meli za zamani.

Bw. Eric alisema kuwa mradi  unatekelezwa na Kampuni ya JV of Gas Entec  CO. Ltd  Kang Nam Corporation na SUMA JKT  ambapo kwa ujumla utagharimu jumla ya shilingi bilioni 152 na tayari Serikali imetoa shilingi bilioni 60 wakandarasi wanadaiwa kazi hawaidai Serikali aidha, mradi umegawanyika  katika sehemu kuu nne. Kwanza ni ujenzi wa meli mpya ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba tani 400 Abiria 1200 ikiwa na urefu wa meta 92.6, urefu kwenda juu meta 11.2 (sawa na ghorofa nne) na upana wa meta 17 na gharama yake ni shilingi bilioni 90.

Mradi wa pili ni ujenzi wa cherezo ambacho kitakuwa na uwezo wa kubeba meli zenye uzito wa tani 4000 ambapo meli mpya itakuwa na uzito wa tani 3500 tu aidha, cherezo kama  hicho hakuna katika nchi za Afrika Mashariki na Kati  na kikikamilika kitaiingizia Serikali Mapato kama kitatumika kwa kujenga meli zenye uzito mkubwa hasa kutoka nje ya Tanzania.  Mradi wa cherezo utagharimu shilingi bilioni 36 na ujenzi wake umefikia asilimia 52.

Mradi wa tatu ni ukarabati wa Meli ya MV Victoria ambao utagharimu shilingi bilioni 22.8 na ukarabati wa meli hiyo umefikia asilimia 50 ambapo inakarabatiwa ikiwa ni pamoja na kubadilishwa mfumo wake wa zamani na kuwekewa mfumo wa kidigitali. Mradi wa wa nne ni ukarabati wa meli ya Butihama ambapo mradi huo nao utagharimu shilingi bilioni 4.9 na ukarabati wake umefikia asilimia 40.

Kwa msaada wa ofisi ya mkuu wa mkoa


Share:

MCHUNGAJI RWAKATARE 'MAMA KISULISULI' ASEMA VIJANA HAWATAKI KUOA KUKWEPA MAJUKUMU,WENGI NI MARIOO


Mama wa upepo wa kisulisuli na Askofu wa Kanisa la Mlima wa Moto Dkt Getrude Rwakatare, ameeleza sababu ya wanawake wengi kushindwa kuolewa ni kutokana na vijana wengi kukwepa majukumu yao.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital,Askofu Dkt Getrude Rwakatare, amesema kila mtu lazima aolewe na kuoa sio vijana kukwepa majukumu na kukimbilia kuwa Marioo.

"Tatizo la wanawake kukawia kuolewa ni tatizo la kidunia, ulimwenguni kote kuna tatizo kama hilo kwa sababu Wanawake tupo wengi kuliko wanaume, lakini tatizo hili limekuwa kubwa zaidi kwa sababu vijana wanakwepa majukumu yao ndiyo maana inakuwa shida" amesema Mama Rwakatare.

"Vijana wa sasa hivi wengi wanakwepa majukumu hawataki kujiingiza kwenye shida wengi wao ni "Marioo" wanataka kuolewa na majimama hii mbaya sana na ndoa ni mipango ya Mungu" ameongeza.

Aidha Mama Rwakatare, amesema ndoa hazidumu kwa kuwa watu wanakaa mwaka mmoja, mitatu au wengine ni miezi sita kisha zinakufa kwa sababu maadili hakuna na sasa hivi watu wanaoana kwa 'fashion'.
Chanzo - EATV
Share:

MVUA YABOMOA NYUMBA 20 KATAVI


Zaidi ya nyumba 20 katika kijiji cha Kamsanga B, kilichopo Kata ya Mnyagala Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, zimebomoka huku zingine zikiwa zimeezuliwa mapaa, kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali na kujeruhi watu watatu.

Akizungumzia tukio hilo Mtendaji wa Kijiji hicho Mwikobe Saimon, amesema mpaka sasa nyumba 17 zimebomoka na nyumba 20 zimeezuliwa mapaaa.

"Jana majira ya jioni mvua iliyoambatana na upepo mkali ilianza kunyesha na ikaezua mapaaa na tulifika kuangalia namna ya kuwanusulu ila nyumba ishirini mapaa yake yalikuwa yamedondoka na nyumba 17 ndiyo zilikuwa zimebomoka kabisa" amesema Mtendaji wa Kijiji hicho Mwikobe Saimon.

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika, Salehe Mhando, amefika kijijini hapo na kutoa pole kwa waathirika wa upepo huo, ambapo amesema kuwa Serikali itaandaa utaratibu maalum wa kuwasaidia.

"Kwenye suala la ujenzi inabidi tuendelee kuelimishana ili tuweze kuweka vizuri, mfano nyumba ikiwa haijafungwa lenta ikipata misukosuko inabomoka" amesema Mkuu wa Wilaya.
Share:

Jeshi la Polisi Lazuia Mkutano wa Mchungaji Peter Msigwa

Jeshi la Polisi mkoani Iringa, limezuia mkutano wa Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, kwa madai ya kutokuwapo kwa askari wa kutosha wa kulinda mkutano huo.

Taarifa za kuzuiwa kwa mkutano huo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikionyesha barua ya zuio kutoka polisi. Mkutano huo ulikuwa ufanyike katika viwanja vya Mwembetogwa.

Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Juma Bwire, alisema marufuku hiyo ilitokana na kutokuwapo kwa askari wa kutosha kwa kuwa wako kwenye usimamizi wa mitihani ya kidato cha nne, kidato cha pili na darasa la nne pamoja na kuwapo kwa taarifa za kiintelijensia juu ya kutokea vurugu na kusababisha uvunjifu wa amani.

Kamanda huyo amesema sababu nyingine ni dalili za kuanza kampeni mapema za kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa kabla ya kalenda ya kampeni kuanza.

Kamanda huyo amebainisha kuwa sababu nyingine ni barua ya mkutano huo kutoweka wazi dhumuni la mkutano ikiwa ni kinyume cha kifungu cha 43(1)(b) cha Sheria ya Polisi na Polisi wasaidizi sura 322 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

 
Akizungumzia kuhusu kuzuiwa mikutano yake, Msigwa alisema hiyo ni kinyume cha sheria kwa kuwa Mbunge hutakiwa kutoa taarifa ili kuhakikisha usalama wa mikutano yake na si kuomba ruhusa kwa jeshi hilo.

"Mimi ni mbunge na ile ndiyo kazi yangu. Sasa kazi yao ni kulinda mikutano yangu ili pasitokee vurugu na si kuzuia." alisema Msigwa.


Share:

HUKUMU YA JAMAL MALINZI NA WENZAKE WATATU KUTOLEWA MWEZI UJAO

Hatima ya Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka (TFF), Jamal Malinzi na wenzake watatu kurudi uraiani au la itajulikana Novemba 7,mwaka huu watakaposomewa hukumu.


Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335.

Uamuzi huo ulisomwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, baada ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde aliyesikiliza kesi hiyo kuwa na udhuru.

Hakimu alisema baada ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi wa pande zote mbili, mahakama yake itatoa hukumu mwezi ujao.

Wakili wa Serikali Ester Martin alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kupanga tarehe ya hukumu na kwamba upande wa Jamhuri uko tayari.

Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itasomwa hukumu tarehe iliyopangwa na kuamuru washtakiwa warudishwe mahabusu.



Share:

Kilele Cha Wiki Ya Kisheria Wananchi 1018 Wapatiwa Msaada Kisheria

Na Stella Kalinga, Simiyu RS
 Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi amesema  takribani wananchi 1018  wamepata huduma ya msaada wa kisheria katika maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria tangu Oktoba 21, 2019 mpaka Oktoba 25, 2019, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Mushi ametoa taarifa hiyo katika Kilele cha Maadhimisho hayo, Oktoba 25, 2019 ambapo amebainisha kuwa asilimia kubwa ya matatizo ya kisheria yalihusu migogoro ya ardhi na yameshafikishwa mahakamani  na yako katika hatua mbalimbali.

Amesema huduma walizopata wananchi katika wiki ya msaada wa kisheria ni pamoja na huduma za usuluhishi, ushauri wa kisheria, kuandaa nyaraka na maelekezo ya sehemu  sahihi ya kwenda pindi wanapopata migogoro.

“Mbali na huduma kwa wananchi mafunzo yametolewa kwa makundi mbalimbali ya watumishi wa umma wapatao 1300 wakiwemo, wajumbe wa menejimenti ya sekretarieti ya mkoa, wajumbe wa kamati ya parole, wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji, wajumbe wa kamati ya maadili ya mahakimu, askari polisi na magereza, wajumbe wa kamati za shule na watendaji wa vijiji na kata, “ alisema Mushi.

Kwa upande wake Hakimu Mary Nyangusi akimwakilisha Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio, ametoa wito kwa wananchi kuandika wosia ili kupunguza migogoro ya ardhi ambayo mingi inatokea mara nyingi wanaume( baba) wanapofariki na wake(mke) na watoto kudhulumiwa haki zao.

Adam Kisinza ni Mmoja wa wananchi waliofika kupata msaada wa kisheria katika maadhimisho hayo amesema, “nashukuru nimeelewesha ninachotakiwa kufanya maana kule kwetu baba mwenye mji anapokuwa amefariki wakabaki watoto na mama, wanakuwa hawana mamlaka juu ya mali iliyoachwa maana kila mtu anataka achukue chake wakati mzee hakuacha hata  wosia”.

Akifunga Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni vema wizara ya katiba na sheria ikaona umuhimu wa kupeleka maadhimisho ya wiki ya msaada wa huduma za kisheria katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo, ili wananchi wapate uelewa wa masuala ya kisheria na kupata matokeo yatakayoonekana.

Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Kitaifa mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu:- “Msaada wa Kisheria kwa Maendeleo Endelevu”ambapo kilele cha maadhimisho haya kimeenda sambamba na uzinduzi wa Jarida la Msaada wa Kisheria, ambalo limezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.


Share:

Waziri Wa Kilimo: Makamishna Wa Tume Ya Maendeleo Ya Ushirika Hawatekelezi Majukumu Yao Ipasavyo, Ubadhilifu Umekithiri

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.

Amesema kuwa Mali zinaibiwa za wananchi, watu wanauziana viwanda huku Ubadhilifu ukiwa umekithiri kuliko kawaida lakini bado kuna tume ya Maendeleo ya Ushirika.

Mhe Hasunga ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Makamishna wa Tume hiyo katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo tarehe 25 Octoba 2019.

Waziri Hasunga amesema kuwa jumla ya Bilioni 124 zimeibiwa kwenye vyama vya ushirika lakini hakuna hatua zilizochukuliwa, "Mnataka mpaka kuwe na posho ndipo kamati ikutane kuona ulazima wa kusimamia fedha na Mali za ushirika" Alihoji Mhe Hasunga

Aliongeza kuwa wizi wa mali na fedha hizo za ushirika ni ishara ya makamishna kutofanya majukumu yao ipasavyo hivyo jambo hilo linapelekea Wanachama kuendelea kuteseka.

"Nasikitika sana Watu walioaminiwa na kupewa dhamana wameshindwa kutekeleza majukumu yao, kwenye zao la ufuta pekee zimeibiwa Bilioni 2.5 lakini wahusika wanadunda mtaani kadhalika mazao kama ya korosho na Pamba ambapo hakuna Ushirika badala yake kuna madalali tu" Alisema

Mhe Hasunga ameongeza kuwa hakuna sababu ya kuwa na Tume ya Ushirika isiyotekeleza majukumu yake ipasavyo huku akiongeza kuwa serikali inataka kujenga ushirika lakini kuna watu kazi yao ni kubomoa, na kuweka urasimu katika utendaji.

Waziri Hasunga amemtaka Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya ushirika Dkt Titus Kanani kuchukua hatua za haraka kwa watendaji wote wa Tume hiyo ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Mhe Hasunga amesema kuwa endapo ushirika utasimamiwa vizuri wananchi watakuwa na maendeleo maradufu yatakayopelekea Taifa kuendelea mbele kiuchumi.

Kadhalika ametoa nafasi ya ziada kwa Tume hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuonyesha matokeo makubwa ya uwajibikaji vinginevyo ametishia kuivunja tume hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt Titus Kamani amempongeza Waziri wa Kilimo kwa kukubali kushiriki katika kikao hicho huku Kamishna wa Tume hiyo Mudhihir M. Mudhihir akizungumza kwa niaba ya Makamishna wengine amehakikisha kuwa Tume hiyo itatekleza majukumu yake kwa weledi mkubwa.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger