Monday, 14 October 2019

WAZIRI MPINA ASHIRIKI ZOEZI LA KUJIANDIKISHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KIJIJINI ISANGIJO WILAYANI MEATU MKOANI SIMIYU NA KUSISITIZA UMUHIMU WA UCHAGUZI

 MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akijiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu. Kulia ni Afisa Mwandikishaji Sospeter Mseya.(13. 10.2019)
 MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akiwa kwenye mstari kwa ajili ya kuingia kwenye kituo cha kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu. .(13. 10.2019)
 MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akisalimiana na Waasisi wa Chama cha TANU muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu. .(13. 10.2019
 MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akizungumza na wananchi muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu. Kushoto ni Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Maswa, Constantine Sement Shillingi  (13. 10.2019)
MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akisisitiza umuhimu wa kuchagua viongozi bora watakaoweza kusimamia mipango ya Serikali kwenye vitongoji na vijiji muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu (13. 10.2019)
Share:

Waziri Mhagama Awataka Vijana Kuenzi Mchango Wa Baba Wa Taifa

Na; Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewataka vijana nchini kuenzi na kuziishi fikra na mitazamo za Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuendeleza umoja uliopo nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Mkoani Lindi Oktoba 13, 2019, Waziri Mhagama alisema kuwa vijana wanapaswa kuendeleza mambo mema yote aliyoyafanya Baba wa Taifa enzi za uhai wake ili waendelee kujivunia juu ya misingi ya amani na umoja iliyopo nchini.

“Vijana mna kila sababu ya kujivunia amani na umoja ulipo katika taifa letu kwa kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi aliyewapenda watu wote bila kujali imani zao wala itikadi zao, alikuwa mzalendo na alitaka watanzania wote waishi kwa umoja,” alisema Mhagama.

Aidha alifafanua kuwa, Amani na umoja zilikuwa ni miongoni mwa tunu na falsafa kuu za Baba wa Taifa ambayo ndiyo matokeo ya umoja na mshikamano wa taifa uliopo sasa.

Aliongeza kuwa miongoni mwa mambo muhimu ambayo Baba wa Taifa alikuwa akisisitiza katika kuwaunganisha watanzania ni pamoja na kulijengea uhuru taifa na watu watu wake, kudumisha amani, upendo, umoja, uzalendo, mshikamano na  kuandaa sera za kukabiliana na ujinga, umaskini na maradhi.

Pamoja na hayo alisisitiza pia vijana na wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kuendeleza maono ya Baba wa Taifa ikiwemo mageuzi ya kiuchumi yenye manufaa kwa taifa.

Akitolea mfano sekta ya elimu ambayo serikali ya awamu ya tano imekuwa ikitoa elimu bure ilikuwa ni falsafa ya Mwalimu katika kuwajenga watanzania fikra ya kujitegemea ili waweze kuukabili umasikini.

Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo pia kuwahimiza wananchi kuendeleza maudhui ya Mwenge wa uhuru ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kuwaunganisha watanzania na kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi alisema kuwa Mwalimu Julius Nyerere ataendelea kukumbukwa na Watanzania kwa mchango wake aliojitolea katika kulijenga taifa.

MWISHO


Share:

Waziri Hasunga Aviagiza Vyama Vya Ushirika Kushiriki Katika Ununuzi Wa Mbolea Kwa Pamoja (BPS)

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Katavi
Kutokana na kuwepo kwa mfumo wa ununzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) serikali imeviagiza Vyama vya ushirika vya msingi (AMCOs) na vyama vikuu (FCU) kuanza kushiriki kwenye ununzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) ili kuhakikisha upatikanaji wa mbolea kwa bei nafuu na kwa wakati.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mbolea Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika leo tarehe 13 Octoba 2019 katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili Wilayani Mpanda mkoani Katavi.

Amesema kuwa ili kuongeza matumizi ya mbolea nchini, Wizara ya kilimo kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha mbolea inapatikana kwa wakati na kwa bei nafuu ikiwemo mfumo wa unuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS).

Pia, imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoa elimu kwa njia tofauti kwa lengo la kuongeza uelewa wa umuhimu na kuongeza matumizi ya mbolea nchini hivyo ili tija na uzalishaji viongezeke vyama vya ushirika havina budi kushiriki kwenye ununuzi wa mbolea ili kuwarahisishia wanachama wao ambao ni wakulima kupata mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu.

Mhe Hasunga ametoa mwito kwa wafanyabiashara wa mbolea kuuza mbolea kwa bei elekezi iliyopangwa na serikali na wazingatia bei hizo kwa mbolea za kupandia (DAP) na kukuzia (UREA) ambazo zinaingizwa nchini kwa mfumo wa Uingizaji wa Mbolea kwa Pamoja yaani Bulk Procurement System BPS.

“Kama mnavyofahamu, Serikali imeendelea kuratibu utoaji wa mikopo yenye riba nafuu kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (Tanzania Agriculture Development Bank-TADB), Benki ya Uwekezaji (Tanzania Investment Bank TIB) na Mfuko wa Pembejeo wa Taifa. Hivyo, nitoe wito kwa wakulima wote wa Mkoa wa Katavi na Mikoa mingine kujiunga katika ushirika ili kuweze kutumia fursa zinazotolewa na taasisi hizi ili kujiletea maendeleo” Alikaririwa Mhe Hasunga

Waziri Hasunga amesema kuwa ili kuwa na matumizi sahihi ya mbolea, ufahamu juu afya ya udongo ni muhimu; hivyo, ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kutoa taarifa ya afya ya udongo kwa wakulima na wadau wengine ili matumizi ya mbolea yaendane na mahitaji ya zao na udongo husika.

Niwakumbusha wafanyabiashara wakubwa kuwa mbolea zinahitajika zaidi mikoani; hivyo ni wakati muafaka wa kuanza kusambaza mbolea mikoani haraka iwezekanavyo. Pia ni wakati sahihi wa kufungua matawi ya mauzo na maghala mikoani badala ya mbolea nyingi kurundikana kwenye maghala yaliyoko Dar es salaam ambako mahitaji yake ni madogo.

Ameongeza kwa kusema kuwa ili mbolea iweze kuwafikia wakulima kwa wakati, amelitaka shirika la reli Tanzania (TRC) kutoa kipaumbele katika usafirishaji wa mbolea kwa mikoa ya Tabora, kigoma na Katavi huku akiitaka Mamlaka ya udhibiti wa mbolea (TFRA) kuhakikisha inasimamia ubora wa mbolea kuanzia bandarini inapoingia hadi kwa muuzaji anayemuuzia mkulima.

Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni ‘matumizi sahihi ya mbolea kwa uhakika wa chakula na uchumi wa viwanda’. Ambapo lengo la maadhimisho ya siku ya mbolea duniani nchini Tanzania ni kupata wigo mpana zaidi kwa Wadau kuelezea masuala mbalimbali katika tasnia ya mbolea.

Masuala hayo ni pamoja na mafaniko ya tasnia ya mbolea nchini, kuwahabarisha wadau wa mbolea hususani wakulima na wafanyabiashara wa mbolea mifumo mbalimbali ya upatikanaji na usambazaji wa mbolea; pia kutoa elimu kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia tasnia ya mbolea.

Siku ya mbolea duniani ilianza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza tarehe 13 Oktoba, 2016 huko nchini Uingereza. Siku hii ilianzishwa mahsusi kwa lengo la kuhamasisha Wadau wa tasnia ya mbolea duniani kote kutambua jukumu kubwa walilonalo la kuhakikisha kuwa wakulima wanatumia mbolea bora na sahihi ili kuleta mapinduzi ya kijani kwa uhakika wa chakula.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera amesema kuwa tayari serikali imetangaza bei elekezi ya mbolea hivyo wafanyabiashara watakaokiuka na kuanza kuuza kwa bei zaidi ya hiyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Amesema kuwa serikali inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kuwanufaisha wakulima kwenye sekta ya kilimo hivyo kukiuka maelekezo ya serikali kwa wafanyabiashara wa mbolea hawana tofauti na wahujumu uchumi.

Akizungumzia kuhusu uzalishaji wa mazao ya chakula amesema kuwa mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo utahamasisha wakulima kulima mazao mengi kwa tija ili kuongeza uzalishaji utakaoimarisha usalama wa chakula nchini.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt Steven Ngailo amesema kuwa mbolea kwa ajili ya kukuzia na kupandia tayari imewasili nchini hivyo wakulima wana fursa mahususi kabisa ya kujitokeza na kuendeleza sekta ya kilimo katika kuongeza uzalishaji wa chakula kwa ajili ya biashara.

Ameitaja kuwa siku ya mbolea Duniani ni kumbukizi ya maadhimisho ya uvumbuzi wa mbolea aina ya Amonia uliofanywa na Bwana Fritz Haber mwaka 1908. Uvumbuzi huo ulichochea mapinduzi ya kijani katika karne ya 20 yaliyowezesha kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao kutokana na matumizi ya mbolea yaliyosaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa janga la njaa na kuleta uhakika wa chakula katika nchi nyingi duniani.

MWISHO


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu October 14























Share:

Sunday, 13 October 2019

Picha : SIMBA SC YATUA KWA KISHINDO KIGOMA KUKIPIGA NA MASHUJAA FC NA AIGLE NOIR YA BURUNDI


Mashabiki wa timu ya simba waliojitokeza kuipokea timu yao ilipowasili leo Mkoani Kigoma kwaajili ya mechi ya kirafiki kesho na timu ya Mashujaa FC.Picha zote na Na Editha Karlo - Malunde 1 blog Kigoma
Baadhi ya wachezaji wa timu ya simba wakiwasili Mkoani kigoma tayari kwa mechi ya kirafiki na timu ya,mashujaa FC kesho kwenye uwanja wa Lake Tanganyika
Baadhi ya wachezaji wa timu ya simba wakiwasili Mkoani kigoma tayari kwa mechi ya kirafiki na timu ya,mashujaa FC kesho kwenye uwanja wa Lake Tanganyika
Baadhi ya wachezaji wa timu ya simba wakiwasili Mkoani kigoma tayari kwa mechi ya kirafiki na timu ya,mashujaa FC kesho kwenye uwanja wa Lake Tanganyika
Kocha wa timu ya Simba Patrick Aussems akisaini kitabu cha wageni baada ya kuzindua tawi jipya la Tanganyika la wanasimba
Na Editha Karlo - Malunde 1 blog Kigoma
TIMU ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara klabu ya simba sc imewasili Kigoma kwa ajili ya mechi ya kirafiki   dhidi ya Mashujaa fc na  Aigle Noir ya nchini Burundi. 

Akizungumza baada ya kuwasili mkoani Kigoma, Kocha wa Simba Patrick Aussems amesema amefurahi kwa timu yake kuwasili mkoani humo na kwamba wamejipanga kupata ushindi katika michezo hiyo.

Amesema mechi hizo za kirafiki ni maandalizi ya kujiweka tayari na mchezo unaofuata  dhidi ya Azam fc katika ligi kuu.
 
Mara baada ya kuwasili walifungua tawi la mashabiki wa Simba tawi la Tanganyika lililopo eneo la Ujiji.

Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Kigoma KFA mkoani Omary  Gindi amesema mikakati ya chama hicho ni kuwa timu ya mashujaa iweze kupanda ligi kuu msimu ujao.

Amesema katika mchezo huo viingilio vitakuwa sh.5,000/= kwa viti vya kawaida na VIP itakuwa sh.10,000/=.

Kikosi hicho kimewasili mkoan Kigoma baada ya miaka 18 ya kucheza na timu ya reli.
Share:

WANANCHI KAGERA WASHAURIWA KUJENGA MAJENGO IMARA ILI KUEPUKA MAAFA

Mwenyekiti wa kamati ya maafa mkoa wa Kagera ambaye pia katibu Tawala mkoa Kagera Profesa Faustin Kamuzora

Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Wananchi mkoani Kagera  wameshauriwa kujenga majengo yaliyo imara kwa kufuata taratibu zote za ujenzi ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.


Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 13, 2019 na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya mkoa wa Kagera ambaye pia ni katibu Tawala mkoa wa Kagera Prof. Faustin  Kamuzora wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa Duniani.

"Sisi kama mkoa tunatumia siku hii kuwataka wananchi kujiepusha na maafa mbali mbali na pia Halmashauri ziboreshe sheria ya majengo imara ili kujikinga na madhara", alisema Kamuzora.

Amesema wananchi kabla ya kujenga watafute sehemu sahihi kwa kujiepusha kujenga sehemu za mabondeni.

Profesa Kamuzora amesema kutokana na madhara makubwa ambayo yamekuwa yakiukumba mkoa wa  Kagera  ikiwemo tukio la Septemba 2016 la tetemeko la Ardhi lenye mkubwa 5.9 katika vipimo vya Richter na mengine mengi wananchi wanapaswa kutumia siku hii kujenga majengo yaliyo imara kwa kufuata taratibu zote za ujenzi ili kuepuka na maafa ambayo yamekuwa yakijitokeza.

Amesema mkoa wa Kagera umechukua hatua endelevu kupunguza uharibifu wa maafa katika miundo mbinu na kuendelea kuelimisha wananchi kujenga majengo imara na kufuata taratibu za ujenzi.

Aidha amezitaka Halmashauri za mkoa huo kusafisha mifereji kila wakati ili kuruhusu  Maji kupita na kutiririka kuelekea sehemu husika kuepuka mafuriko yanayoweza kuleta maafa.

Hata hivyo amesema mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watahakikisha wanatoa elimu zaidi kwa wananchi ili waweze kupambana na maafa.
Share:

WAZIRI JAFO AONGEZA SIKU TATU UANDIKISHAJI DAFTARI LA ORODHA WAPIGA KURA SERIKALI ZA MITAA

Na Oscar Job, Kisarawe
Waziri  wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ameongeza siku tatu kwa wananchi kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 Mwaka huu.

Akizungumza kabla ya kujiandikisha Kijijini kwake Kimani,Kisarawe mkoani Pwani , Waziri Jafo alisema kuongezwa kwa siku tatu hizo kumetokana na sababu mbalimbali ambazo kimsingi zimesababisha wananchi kuikosa fursa hiyo.

Alisema kimsingi siku za uandikishaji huo zilizoongezwa kutoka leo hadi Oktoba 17, kumesabishwa na tatizo la mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali na hivyo kuleta shida kwa wananchi wengi kujiandikisha.

Aliitaja sababu nyingine kuwa ni pamoja na uwepo wa zoezi la wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, hali iliyoleta dhana  kwa baadhi ya wananchi kuwa kitambulisho cha mpiga kura kitawawezesha kupiga kura katika uchaguzi huo wa Serikali za mitaa.

“Kutokana na sababu hizo na kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2019 na matangazo ya Serikali Na 371,372,373 na 374 ya Mwaka 2019 Waziri mwenye dhamana na Serikali za mitaa ana mamlaka ya kutoa miongozo mbalimbali kuhusu uchaguzi wa  Serikali za Mitaa”  alisema Jafo

Alisema kutokana na kanuni hizo na changamoto zilizojitokeza Wizara yake imeona vyema kuongeza siku hizo tatu ili kuwapa nafasi wananchi kujiandikisha na hivyo kutumia fursa yao ya kikatiba kuwachagua viongozi wanaowataka.

Aidha alisema tangu kuanza kwa Oktoba 8 hadi Octoba 12 Mwaka huu wananchi zaidi ya Milioni 11 walikuwa tayari wamejiandikisha nchi nzima kushiriki uchaguzi huo huku akilitaja zoezi hilo kuwa lenye mafanikio makubwa ikilinganishwa na kipindi kingine chote.

Alisema kufuatia mabadiliko, ratiba ya uandikishaji wa orodha ya wapiga kura na matukio yanayohusu uandikishanji yatakuwa na mabadiliko fulani fulani ikiwemo kubandikwa kwa orodha ya wapiga kura litakalofanyika kuanzia Oktoba 18, utoaji wa pingamizi kuhusu uandikishaji wapiga kura litakalofanyika Oktoba 14 hadi 24.

Mabadiliko mengine ni pamoja na uamuzi kuhusu pingamizi litalofanyika kuanzia Oktoba 24 hadi 25,marekebisho ya orodha ya wapiga kura kuanziaa Oktoba 25 hadi 25 pamoja na ukataji wa rufaa dhidi ya uamuzi wa pingamizi utakaofanyika Oktoba 24 hadi 26 sambamba na ukataji wa rufaa utakaofanyika Oktoba 24 hadi 29 Mwaka huu.

Aidha alisema matukio mengine yote zikiwemo kampeni za wagombea zitaendelea kubaki kama kawaida huku akiwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuwa na sifa ya kupiga kura katika uchaguzi huo.


Share:

Makonda aagiza maduka yote Dar kesho yafunguliwe saa 5 asubuhi Ili Kutoa Nafasi Kwa Wananchi Kujiandikisha Kwenye Daftari La Wapiga Kura.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Paul Makonda amesema, siku ya kesho maduka yote mkoani humo yatafunguliwa kuanzia saa 5 asubuhi ili kupisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuenzi miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa

Makonda ametoa agizo hilo leo Jumapili Oktoba 13, 2019 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.
 
RC Makonda amesema kwakuwa kesho ni Siku ya Kumbukumbu ya Miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ameona ni vyema Wananchi wote wakamuenzi Baba wa Taifa kwa kuhakikisha wanapata Nafasi ya Kutosha ya Kujiandikisha ili waweze kuchagua Viongozi wa mitaa wanaoweza kutatua matatizo yao.
 
Aidha RC Makonda amewasihi Wamachinga, Bodaboda, Makondakta, madereva, Viongozi wa Taasisi, wafanyakazi wa Bar, Saloon, wamiliki na wafanyakazi wa Sehemu za Starehe kuhakikisha wanajiandikisha kwenye Ofisi za Serikali ya Mtaa, Shule za Msingi,  sekondari na sehemu zilizowekwa mahema maalumu ya kujiandikisha.


Share:

Ongeza Nguvu Za Kiume, Maumbire Madogo Pamoja Na Tiba Mbalimbali

MASISA 3 POWER nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoazaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wara kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20-40

SUPER MONGERA  Hurefusha na kunenepesha maumbile madogo yaliosinyaa. Matatizi haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguluma na kujaa gesi,ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia ninadawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

Ni DR CHIPUPA  pekee mwenye uwezo wa kumrudisha mume , mke ,mchumb.

Kwa nini uhangaike na matatizo ya uzazi;   ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,

 wasiliana na DR. CHIPUPA 

Call+255 0620510598

watsap +255 0758840958

Huduma hii inakufikia popote ulipo


Share:

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.



Share:

Dawa Komesha Ya Maumbile Madogo , Nguvu Za Kiume Na Magonjwa Mengineyo

*NGETWA MIX*/
√Hii ndio dawa bora ya mitishamba kiboko ya maumbile Madogo(KIBAMIA) Hurefusha na kunenepesha maumbile  mafupi pia  yaliyoingia ndani kutokana na kitambi ama kuathirika na punyeto

*📌SUPER MORINGA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
🔖(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri   ilio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
🔖(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
🔖(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
🔖(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
🔖(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
🔖(3)Ngiri/
🔖(4)Kama umejichua sana punyeto/
🔖(5)Kisukari/
🔖(6)Presha ya kupanda na kushuka/
🔖(7)Vidonda vya tumbo,/
.
Na haya yote husababisha/
📍Kuishiwa kwa nguvu za kiume 📌/
. _______________________
Bado hujachelewa dawa hizi ni mpya kabisa  ni tofaut na ulizo wahi kutumia pia zimeonesha mafanikio kwa watu wengi sana/

Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
DR .SELEMANI OMARY ANAPATIKANA  DAR ES SALAAM , PIA UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO  NDANI NA NJE YA NCHI .SIMU NO:/
*📞+255788468114*


Share:

Waziri Lugola Aagiza Polisi Kuwakamata Wanaowapotosha Wananchi Uandikishaji Uchaguzi Serikali Za Mitaa

Na Felix Mwagara, MOHA, Mwibara
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini, kuwakamata na kuwafunguliwa mashataka watu ambao wanawapotosha wananchi kutokujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Lugola amesema watu hao wanawarubuni wananchi kwa njia za mitandao ya kijamii, kuwafuata majumbani kwao, wakiwapotosha kususia uchaguzi huo, pamoja na kuwadanganya kuwa walishajiandikisha kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hivyo watatumia vitambulisho hivyo hivyo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 24, 2019.

Akizungumza na wananchi Jimboni kwake Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, mara baada ya kujiandikisha katika kituo cha Sokoni, Kata ya Kibara, alisema taarifa hizo amepewa na viongozi wa Serikali ya Kijiji pamoja na vyanzo mbalimbali, kuwa kuna kundi la wananchi wanapita mitaani kuwapotosha wananchi na pia kuwatisha wasifike vituoni kujiandikisha wakiwa na lengo la kuvuruga uchaguzi.

“Wananchi Kibara, wacha niwaambie, Serikali ya awamu ya tano si ya kuchezewa, watu hao ni wapotoshaji na lengo lao wanataka kuvuruga uchaguzi ambao ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi, sasa naagiza polisi kuwasaka na kuwakamata watu hao, ili wawe mfano,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, Wizara yake inalinda amani katika uchaguzi huo, hivyo haiwezi kukaa kimya kuwaacha wapotoshaji hao wakiendelea kuharibu na kutamba mitaa jambo ambalo Serikali haiwezi ikawaacha.

Pia aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika vituo mbalimbali nchini kujiandikisha ili waweze kuwachagua viongozi wao na kuiletea maendeleo nchi.

“Leo mmejitokeza wengi, nawapongeza, nafikiri wengi wenu mmekuja labda baada ya kuniona mimi mbunge wenu nimefika, lakini bado siku hazijaasha, waambieni wananchi wajitokeze kuja kujiandikisha leo, pamoja na Kesho, viongozi msichoke, fanyeni kazi kwa nguvu zote, kwa maendeleo ya jimbo let una nchi kwa ujumla,” alisema Lugola.

Alisema kupitia uchaguzi huo, viongozi wa vijiji na mitaa watasaidia Wizara yake baada ya kuwapata viongozi hao ambao pia wataunda Kamati ya ulinzi na usalama ya Kijiji na usalama wa eneo husika unaimarishwa zaidi kutokana na uwepo wa viongozi hao.

Aidha, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibara B, Laurent Mafwili Mnyaga, alikiri kuwepo kwa tatizo hilo kijijini kwake, lakini agizo alilolitoa Waziri Lugola litasaidia wananchi kujitokeza kwa wingi na pia litawasaidia viongozi wa Kijiji chake kuwahamasisha wananchi waende kujiandikisha kwa wingi zaidi, kwasababu wapotoshaji hao wanawajua na Serikali ya Kijiji hicho watahakikisha wanawapeleka polisi.

“Nimefurahi sana kumuona Mbunge wetu kufika Mwibara na kutuhamasisha zaidi, lakini alilolisema ni sahihi kabisa, baadhi ya wananchi wamepotoshwa wasije kujiandikisha, wakidanganywa kuwa kadi za zamani zitatumika kapigia kura uchaguzi wa Serikali za Mitaa jambo ambalo si sahihi,” alisema Mafwili.

Aliongeza kuwa, licha ya kukabiliwa na changamoto ya wananchi kupotoshwa, kutishwa na watu mitaani wenye nia ovu na serikali, lakini Mwenyekiti huyo alisema utoaji wa elimu kuhusu uandikishaji haukua na nguvu kiasi kilichosababisha wananchi kutokujitokeza kwa wingi.

Waziri Lugola tayari amejiandikisha katika Kijiji hicho na kupongezwa na wananchi hao, ambao wengi wao walijitokeza baada ya kumuona Mbunge wao kujitokeza katika kituo hicho.


Share:

Hazina Saccos Kuwekeza Mradi Wa Bilioni 52 Dodoma

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
CHAMA cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Saccos kimeazimia kujenga kitega uchumi cha kisasa kwa gharamaya  Shilingi bilioni 52 kupitia mradi wa Njedengwa katika Jiji la Dodoma ili kukuza uchumi wa mkoa wa Dodoma na Taifa kwa kupitia kodi.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi wa chama hicho cha Ushirika Bw. Aliko Mwaiteleke  wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka  uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Hazina,  na kuongeza kuwa mradi huo upo katika hatua za mwisho za utekelezaji wake.

Mwaiteleke alisema mpaka sasa upembuzi yakinifu wa mradi huo utakaojengwa kwa njia ya ubia kati ya Hazina Saccos na mwekezaji kwenye neo lenye ukubwa wa ekari 22  kupitia utaratibu wa Jenga, Endesha na Hamisha (Build, Operate and Transfer - BOT) ambapo mwekezaji atagharamia ujenzi wote na kuendesha kwa muda ambao utakubaliwa ndani ya mkataba.

Alisema mradi huo unasimamiwa na Kamati ya watu Saba wakiongozwa na Profesa Esta Eshengoma kutoka Chuo Kiuu Cha Dar es Salaam na wajumbe wake kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru),  Bodi ya Manunuzi ya Umma (PSPTB), Kituo Cha Uwekezaji (TIC), na Chuo Kikuu cha Ardhi ambao kwa sasa wanafanya kazi ya kusaka mwekezaji ili kufanikisha mradi huo.

Bw. Mwaiteleke alifafanua kuwa Mradi wa Njedengwa upo mbioni kuanza  na unategemewa kuwa chachu ya maendeleo ya chama hicho kwa kukiingizia kipato kutokana na shughuli zitakazokuwa zikifanyika kupitia mradi huo.

Alifafanua kuwa  mradi huo utahusisha ujenzi wa hoteli ya kisasa, kumbi za  mikutano, majengo ya Ofisi,  Viwanja vya Michezo na bwawa maalum la kuogelea.

Aidha alisema Chama hicho cha Hazina Saccos ambacho kina wanachama 5,600 kina mtaji mtaji wenye thamani ya shilingi bilioni 10 ikiwa ni fedha taslimu na mali wanazozimiliki ikiwemo ardhi ambazo zimekuwa na manufaa makubwa kwa wanachama..

"Mwaka jana pekee kupitia akiba na mikopo  tulipata faida ya shilingi milioni 64 na kila mwanachama alipewa gawio la asilimia 20 kulingana na hisa zake"alisema Mwaiteleke.

Alisema faida nyingine waliyopata kupitia Hazina Saccoss ni kununua viwanja 150 katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Dar es Salaam na Pwani na kuwakopesha wanachama wao kwa bei nafuu ambapo wanalipa kidogo kidogo kwa miezi 60.

"Pia Dodoma tumenunua viwanja 897 katika maeneo ya Ihumwa Ngaloni, Iyumbu  (maeneo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambavyo tumevigawa kwa wananchi na viwanja vya Nzuguni tutaanza kuvigawa baada ya taratibu za Halmashauri ya Jiji la Dodoma kukamilika ili kuwawezesha wanachama wetu waliohamia Dodoma kupata maeneo ya kujenga makazi yao” alisema Bw. Mwaiteleke

Naye Meneja wa Hazina Saccos Bw. Festo Mwaipaja, alisema Saccoss hiyo sio ya wafanyakazi wa Wizara ya Fedha peke yake bali watumishi wote wa serikali wanaruhusiwa kujiunga na chama hicho isipokua vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo ni jeshi, Polisi, na Usalama wa  Taifa.

Alisema kwa mtumishi wa umma kujiunga na chama hicho cha ushirika mbali na kuwa muajiriwa pia atapaswa kulipa kingilio cha shilingi 20,000 na kununua hisa kuanzia 20 ambazo kila hisa moja ni shilingi 10,000 na kufanya thamani ya hisa zote kuwa shilingi 200,000.

Aidha alisema kuna mchango wa shilingi 20,000 kila mwezi na kuwataka watumishi wa umma kutoka taasisi na idara zote za serikali kuchangamkia fursa ya kujiunga na ushirika huo ili kujiinua kiuchumi

Kuhusu viwanja, Bw. Mwaipaja alieleza kuwa Chama hicho kimetumia zaidi ya shilingi bilioni 4 kununua viwanja katika Jiji la Dodoma na kuchangia eneo hilo kuwa na mzunguko mkubwa wa fedha kwa wenyeji na kwamba hayo ni mafanikio yanayoihusu jamii.

Akifungua Mkutano Mkuu huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mary Maganga, ameipongeza Hazina Saccos kwa kuwapatia viwanja wanachama wake na kuwataka wanachama waliopata fursa ya kupata viwanja hivyo waviendeleze haraka ili kuodokana na changamoto ya malazi kwa kuwa baadhi walipata viwanja hivyo tangu mwaka uliopita, 2018.

Aidha, ameipata kongole Hazina Saccos kwa hatua waliyofikia ya kutafuta mwekezaji katika mradi wa Njedengwa ambao utaongeza mapato ya Ushirika na kuwataka viongozi na wanachama kuhakikisha wanazingatia taratibu Sheria na Kanuni ili kufanikisha mradi huo muhimu.

Mwisho


Share:

Serikali Kuzipatia Ruzuku Kaya Zote Maskini Nchini Baada Ya Kuridhishwa Na Maendeleo Wanufaika Wa Tasaf

Na James K. Mwanamyoto-Nyasa
Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imeahidi kuzinufaisha kaya zote maskini nchini baada ya kuridhishwa na namna wananchi katika vijiji vilivyonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini walivyoboresha maisha yao na kujikwamua katika lindi la umaskini liliokuwa likiwakabili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati akizungumza na wanufaika na wananchi wa kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa akiwa katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango huo wilayani humo.

Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, iwapo wanufaika wasingetumia ruzuku vizuri kuboresha maisha, Serikali isingesita kusimamisha utekelezaji wa Mpango huu wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.

“Hongereni wanufaika wa TASAF kijiji cha Nangombo na maeneo mengine kwa kutumia ruzuku kuboresha maisha yenu, kujenga nyumba bora, kununua vifaa vya shule kwa ajili ya watoto na kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi,” Mhe. Mkuchika amepongeza.

Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano imeridhika na mafanikio yaliyopatikana, hivyo itaendeleza vita dhidi ya umaskini, lengo likiwa ni kuboresha maisha ya kaya zote maskini nchini.

Akiwasilisha taarifa ya kijiji cha Nangombo kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Afisa Mtendaji wa kijiji hicho, Bw. Joseph P. Ngogi amesema watoto 66 wa shule wananufaika na ruzuku inayotolewa hivyo imeongeza mahudhurio shuleni na kliniki kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, aidha kaya 65 zimeboresha makazi yao kwa kujenga ama kukarabati na kuezeka kwa bati.

Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa TASAF kijiji cha Nangombo, Bi. Mariana Mkwaila amesema ruzuku anayoipata imemuwezesha kuwanunulia watoto wake sare za shule, viatu na madaftari ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba kubwa ambayo anatarajia kuizeka kwa bati hivi karibuni.

Naye, Bi. Elizabeth Damian amesema, alikuwa akiishi maisha ya kimaskini kwenye nyumba ya nyasi kabla ya kuingizwa kwenye Mpango, lakini baada ya kuanza kupokea ruzuku ameweza kufuga kuku, mbuzi na kufyatua tofali zilizomuwezesha kujenga nyumba iliyoezekwa kwa bati.

Mhe. Mkuchika amehitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma kwa kuitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo.


Share:

Jamii Yaaswa Kushiriki Kuzuia na Kupunguza Athari za Maafa

Na Mwandishi Wetu
Jamii imeaswa kushiriki kikamilifu katika kuzuia na kupunguza athari za maafa pale yanapotokea katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
 
Aklizunmgumza leo Oktoba 13, 2019 Jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Upunguzaji wa Athari za Maafa Duniani ambapo alikuwa mgeni rasmi, Katibu mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko amesema suala hilo linahitaji ushirikiano wa jamii nzima.
 
“Tumekutana leo hapa tukishirikiana na wenzetu Duniani kote kukumbushana mbinu na mikakati ya kupambana na maafa ikiwemo kuweka mikakati ya kupunguza maafa yanapotokea katika maeneo yetu”Alisisistiza Bi Mwaluko
 
Akifafanua amesema kuwa, Wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) wanaosomea Shahada ya udhibiti wa maafa katika mazingira washiriki kikamilifu katika kutoa elimu kuhusu maafa katika shule za Sekondari na msingi zilizopo hapa Dodoma  kupitia chama cha udhibiti wa maafa katika chuo hicho.
 
Aliongeza kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kuwa chachu katika kutoa elimu kuhusu maafa ili kupanua wigo wa elimu na kuagiza chama hicho kuhakikisha kuwa kinawasilisha mpango wake wa utoaji elimu katika Ofisi yake.
 
Aidha, Bi Mwaluko ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kujiandikisha ili waweze kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa na kuchagua viongozi watakaosaidia katika kuleta maendeleo kwa kusimamia kikamilifu rasilimali zinazotolewa na Serikali kwa maslahi ya wananchi.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri mkuu, Kanali Jimmy Said amesema kuwa Sera ya Maafa inaelekeza kikamilifu majukumu ya kamati za maafa katika ngazi zote ili kurahisisha mawasiliano na kuimarisha utendaji .
 
Aliongeza kuwa kila mwananchi anapaswa kutimiza wajibu wake katika eneo lake ili kupunguza athari za maafa pale yanapotokea.
 
Siku ya maafa huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 13, ya kila mwaka ili kuwaleta pamoja wadau kujadili na kuweka mikakati ya pamoja katika kupambana na maafa.




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger