Saturday, 12 October 2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi October 12





















Share:

Friday, 11 October 2019

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya Yatengua Hukumu ya Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi (Sugu)

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya leo tarehe 11 October 2019 imetengua Hukumu,Mwenendo na Kifungo alichohukumiwa Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi aka Sugu kwa kile ambacho Mahahaka Kuu imeeleza kuwa ni ubatili wa mwenendo katika kesi hiyo. 

Akisoma Uamuzi wa Rufaa Nambari 29 ya Mwaka 2018 iliyowasilishwa na Sugu kupitia Mawakili Peter Kibatala na Faraji Mangula,Jaji Utamwa amesema kwamba kulikuwa na Makosa yasiyotibika katika mwenendo wa shauri hilo,hasa pale ambapo aliyekuwa Hakimu Mwandamizi Mteite wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mbeya aliposhindwa kuwasomea Mashtaka Washtakiwa katika hatua ya usikilizaji wa awali (Preliminary Hearing). 

Katika Hukumu yake iliyosomwa na Naibu Msajili wa Mahaka wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Jaii Utamwa alisema kwamba hakubaliani na hoja za upande wa Serikali ambao ni Wajibu Rufaa kwamba mapungufu hayo yanatibika, na badala yake Jaji Utamwa amesema kwamba makosa hayo yanaathiri mwenendo mzima wa kesi iliyopelekea kufungwa kwa Sugu na mwenzake Emmanuel Masonga.
 
Jaji Utamwa ametengua Hukumu, Mwenendo mzima wa kesi na adhabu ya kifungo waliyohukumiwa Sugu na Masonga.


Share:

WAZIRI WA ULINZI DK HUSSEIN MWINYI AKERWA NA USIMAMIZI USIORIDHISHA UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA USHETU


Waziri wa Ulinzi Dk Husein Mwinyi akipokea maelezo ya mradi kutoka kwa mkandarasi kampuni ya Mzinga Holding Meneja wa shirika la Mzinga na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mzinga holdings Meja Jenerali Seif Makona.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akimuongoza Waziri wa Ulinzi Dk Husein Mwinyi kuelekea eneo la Mradi
Mafundi wakiendelea na kazi katika eneo la ujenzi wa jengo hilo

Na Salvatory Ntandu - Malunde 1 blog
Waziri wa Ulinzi, DK Husein Mwinyi amezitaka pande tatu zinazohusika na usimamizi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa wakati uliopangwa kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata huduma.

Waziri Mwinyi ametoa leo agizo hilo katika kikao cha pamoja kilichowakutanisha, Wakala wa ujenzi Tanzania (TBA), Halmashauri ya Ushetu, na mkandarasi Mzinga holding baada ya kubaini upande hizo kulaumiana katika utekelezaji wa ujenzi huo na kusababisha mpaka sasa ujenzi huo kufikia asimia 27 badala ya asilimia 50 kwa mujibu wa mkataba.

Amesema Serikali haitavumilia kuona ujenzi wa jengo hilo ukiendelea kwa kusuasua hali ambayo inaweza kusababisha kutokamilika kwa wakati kama mkataba unavyoelekeza huku wasimamizi wakuu wa mradi huo wakiendelea kulaumiana bila sababu ya Msingi.

Waziri Mwinyi amesema serikali imebaini kuwepo kwa utolewaji wa vibali vya ujenzi kutoka kwa wakala wa Ujenzi TBA usioridhisha sanjari ucheleweshwaji wa utolewaji wa fedha kutoka Halmashauri hiyo kwenda kwa Mkandarasi Mzinga holding ambayo ipo chini ya wizara yake.

Kwa upande wake mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amesema utendaji kazi wa TBA katika mradi wa ujenzi huo hauridhishi na umesababisha kusuasua kwa mkandarasi katika ujenzi huo licha ya serikali kutoa shilingi bilioni 9.1 lakini wao kama wasimamizi wakuu wa mradi huo wamekuwa hawaonekani katika eneo la ujenzi na kusababisha mkandarasi kushindwa kufanya kazi.

Naye Kaimu meneja wa TBA mkoa wa Shinyanga Mhandisi Sobe Makonyo amesema wameshakubaliana na kampuni ya Mzinga Holdings kujenga jengo hilo kwa saa 24 na ujenzi wake utamilka kwa wakati kama vile mkataba unavyoekeza na watahakikisha wanaweka watumishi wao katika eneo la maradi.

Awali akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Atanas Lucas amesema halmashauri hiyo ilipokea fedha kutoka serikali kuu shilingi bilioni 1.9 za wali ili kutekeleza mradi huo ambao unatajia kutumia shilingi bilioni 5.2

Atolea Ufafanuzi kuhusiana na Ujenzi huo Meneja wa shirika la Mzinga na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mzinga holdings Meja Jenerali Seif Makona amesema watahakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati na kuiomba TBA na Halmashauri ya Ushetu kutokwamisha vibali vya ujenzi na Malipo kwao.

Ujenzi wa jengo hilo unatarajia kutumia shilingi bilioni 5.2 na Mpaka sasa ujenzi huo umefikia asilimia 27 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 2 mwaka 2020.

Share:

JACOB ZUMA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU MASHITAKA YA RUSHWA


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya rushwa baada ya mahakama kutupilia mbali ombi lake la kutaka kesi hiyo isitishwe kabisa. 

Uamuzi huo wa leo una maana kuwa kutakuwa na uchunguzi zaidi kuhusu mpango wa ununuzi wa silaha wa mwaka wa 1999 ambao Zuma anatuhumiwa kwa kupokea rushwa kutoka kwa kampuni ya kutengeneza silaha ya Ufaransa Thales. 

Tuhuma hizo ziliibuliwa zaidi ya muongo mmoja uliopita lakini zikaondolewa, na kurejeshwa tena baada ya Ofisi ya Mashitaka kutangaza kuwa kuna ushahidi wa kutosha wa kumfikisha Zuma kizimbani. 

Alikuwa rais kutoka mwaka wa 2009 hadi 2018, wakati alipolazimishwa kujiuzulu na chama tawala cha African National Congress ANC kutokana na madai mengine tofauti ya rushwa. Zuma anaweza kukata rufaa uamuzi huo wa leo wa mahakama.


Share:

Scholarships for Tanzanian Students | Ufadhili Kusoma Nje

📚 FURSA ZA UFADHILI  WA KUSOMA NJE YA NCHI

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

    🎓 Tanzanian Scholarships

Kama wewe ni Mtanzania mwenye Ndoto ya Kusoma nje ya Nchi lakini hukuwa na uwezo, basi hii ni Nafasi yako. Kuna Nafasi Nyingi sana za Ufadhili zimetangazwa (Scholarships)

*📌 PHD
*📌 MASTERS
*📌 UNDERGRADUATE

 

ZIKO WAPI😳😳
✈(1)Zipo za Hong Kong
🛩(2) Marekani
✈(3)Uingereza
🛫(4)Canada

 Zote Hizo ni Full Funded( Unalipiwa kila Kitu) Japo kuna zingine utachangia kidogo
. _______________________
Bado hujachelewa, Deadline ni kuanzia Mwezi huu wa kumi mwishoni hadi Mwakani-2020
._______________________ 

Bofya hapo chini kujua zaidi
👇👇👇👇👇👇👇👇


http://ajirazote.com/scholarship/


Share:

Bashe: Tunahitaji Tafiti Bora Za Mbegu

Na Bashiri Salum, Wizara ya Kilimo,Morogoro
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo  Hussein Bashe jana (10/10/2019 ) aemeshauri Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine na Wakala wa Uzalishaji Mbegu Tanzania (ASA) kushirikiana kuzalisha mbegu bora ili kukidhi mahitaji ya wakulima.

Amesema taasisi za Serikali zinapasa kuwa mdau wa kwanza katika kuhakikisha mbegu bora na za kutosha zinapatikana.

“Usalama wa Chakula utakuwa endelevu endapo hatua madhubuti zitachukuliwa kuona taifa linazalisha mbegu za kutosha na zinazohimili magonjwa” alisema Naibu Waziri

Bashe yupo mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi kukagua shughuli za uzalishaji mbegu ambapo alifanya mikutano na wakuu wa Viongozi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine,Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) pamoja na Wakala wa Mbegu (ASA)

Bashe alisitiza kuwa uchumi hauwezi kukua kama hakutakuwa na uwekezaji mzuri  kwenye kilimo kwa kutumia utaalam unaopatikana kwenye taasisi za kitaaluma.

Naibu Waziri alibainisha kuwa ni lazima kilimo kiangaliwe  kwa jicho la kibiashara ili kiweze kumvutia mkulima na wawekezaji hivyo ni wakati wa wataalamu wa kilimo  kuchochea mabadiliko chanya.

“Ni muda muafaka sasa tafiti nyingi za SUA zitokane  na matatizo ya wakulima ili waweze kuzitumia na kubadilisha kilimo chao kuwa chenye tija” alisema Bashe

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Prof Raphael Tihelwa Chibunda amesema chuo chake kipo tayari kufuata maelekezo kwa kuwa tafiti zao zote zinalenga mahitaji ya jamii ya watanzania.

Prof Chibunda amesema pamoja na kuongeza uzalishaji wa mbegu lakini ni muhimu kama nchi kuimarisha huduma za ugani ili kuleta matokeo mazuri pindi wakulima watakapotumia mbegu bora za kilimo

Hata hivyo amemweleza Naibu Waziri kwamba imefika wakati nchi kuondokana na kuweka vikwazo zadili (regulatory) badala yake iwe na mikakati ya  promosheni kwa kuwa bado hatujawa na utoshelevu katika mbegu.


Share:

Utiaji Saini Mkataba Wa Ukarabati Mkubwa Wa Ujenzi Wa Jumba La Baitul El Ajaib Wafanyika Zanzibar

Na Miza Kona Maelezo 11/10/2019
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Oman imetiliana saini mkataba wa Ukarabati wa ujenzi Jengo la Urithi wa Mji Mkongwe Beit el -Jaibu.

Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale baina ya katibu Mkuu wa wizara hiyo Bi Khadija Bakar Juma na Katibu Mkuu wa Mambo ya Urithi na Utamaduni wa Serikali ya Oman Bwana Salim Mohammed Mahrouk.

Akizungumza katika Utiaji saini huo Waziri wa Habari na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo amesema Zanzibar ni nchi ya 10 katika nchi zenye Miji ya Urithi wa dunia hivyo imeamua kulifanyia ukarabati jengo hilo ili lisiondoke katika nchi zenye urithi huo na kuongeza hadhi ya miji yenye vivutio vya uasili.

Amesema kuwa jengo hilo litakarabatiwa bila ya kubadilishwa na kuondosha uhalisia wake wa zamani  ili liweze kudumu kwa muda mrefu na urithi mzuri wa vizazi vijavyo na kuwa vivutio kwa watalii.

Waziri Mahamoud amefahamisha serikali itayafanyia ukarabati majengo ya kihistoria yaliyochakaa na kuyarejesha katika hali yake ya zamani ili kuongeza hadhi ya miji yenye historia na vivutio kwa wageni.

Ameeleza kuwa serikali ya Oman imekuwa ikisaidia Zanzibar katika Nyanja mbali mbali kwa lengo la kuleta maendeleo na kudumisha mashikiano makubwa yalipo.

Nae katibu Mkuu wa Mambo Urithi na Utamaduni wa Oman Bwana Salim Mohammed Mahrouk amesema serikali ya Oman itaendelea kuisaidia Zanzibar katika kuimarisha Utamaduni na Urithi na kuleta maendeleo zaidi

Mapema Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Mji Mkongwe Issa Sarboko Makarani amesema watahakikisha kuwa jengo la Beit-el Jaibu linakwenda sambamba kushajihisha wananchi kuyafanyia ukarabati majengo yao yaliyomo mji mkongwe  

Ujenzi huo ni wa miaka miwili ambao unaokarabatiwa na kampuni ya Gilardi kutoka Itali ambao utagharimu jumla ya sh bilioni 14 hadi kumalizika kwake.   


Share:

HESLB: NOTICE TO LOAN APPLICANTS WITH INCOMPLETE LOAN APPLICATIONS

This is to inform loans applicants with ‘Incomplete Applications’ in the academic year 2019/2020 to visit their online accounts in http://olas.heslb.go.tz and complete applications by uploading missing attachments or filling required information. This notice is applicable to applicants with ‘Incomplete Status’ only who are now required to upload ‘Signatures and Declarations’ pages (2&5). To upload or fill missing information, kindly follow the following steps: Visit… Read More »

The post HESLB: NOTICE TO LOAN APPLICANTS WITH INCOMPLETE LOAN APPLICATIONS appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waziri Mkuu Azindua Mradi Wa Kitalu Nyumba Kwa Vijana Kwa Nchi Nzima

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano imeamua kupambana na ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kuanzisha programu za kuongeza na kurasimisha ujuzi.

“Mwelekeo wa Serikali hivi sasa ni kuendeleza viwanda na viwanda hivi vinahitaji malighafi kutokana na mazao. Tumeamua kuongeza malighafi kupitia kilimo, lengo ni kuwafanya vijana waweze kuajiriwa kwenye sekta hii kubwa ya uzalishaji,” alisema.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Oktoba 10, 2019) wakati akizindua mradi wa kitaifa wa mafunzo ya ujenzi na kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ya kitalunyumba (greenhouse) kwenye viwanja vya maonesho vya Ngongo, mjini Lindi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa kwa mwaka 2019.

“Nataka vijana muondokane na dhana ya kwamba kuwa na ajira ni lazima uwe umekaa mezani na umeshika kalamu. Ajira ni kazi yoyote ya halali inayompatia mtu kipato iwe ni biashara ndogondogo, mamalishe au bodaboda.”

Akifafanua kuhusu teknolojia ya kitalunyumba, Waziri Mkuu alisema: “Programu hii inasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Serikali inayoongozwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeweka msisitizo kwenye kilimo lakini tunaangalia na aina ya kilimo tulichonacho.”

“Maeneo mengi nchini hayana mvua za kutosha. Kwa hiyo tumeanzisha kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone na siyo kwa kuchimba mifereji. Kitalunyumba kinahitaji nafasi chini ya robo eka, na humo ndani kuna matuta manne tu. Kwa kutumia tenki la maji, unatumia maji kidogo sana kwa kila mche, kwa sbabu yanatoka kwa matone,” alisema.

Alisema mtu yeyote mwenye eneo la kutosha anaezaa kutumia teknolojia ya kitalunyumba wakiwemo wafanyakazi ili wapate mazao ya kujiongezea mapato. “Unaweza kulima mahindi ukala mwaka mzima, unaweza kulima vitunguu au mboga za majani ukauza na siyo nyanya peke yake, hawa wamepanda nyanya kwa sababu ni mfano tu,” alisisitiza.

Akitaja faida zake, Waziri Mkuu alisema mche wa kwenye kitalunyumba unadumu kwa muda mrefu, haupati magonjwa na unazaa kwa wingi. “Mche mmoja unaweza kuzalisha kilo 30 na ndani ya kitalunyumba kimoja kuna miche 580. Nimeambiwa nyanya tisa tu, zinajaa kilo moja. Hii ni fursa ambayo kila mmoja anaweza kulima akiwa nyumbani kwake,” aliongeza.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi huo, Waziri wa Nchi OWM - Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama alisema Serikali ilifanya utafiti na kubaini kwamba asilimia 56 ya nguvukazi nchini ni vijana lakini wanakabiliwa na changamoto ya kukosa ajira.

“Katika utafiti mwingine wa Serikali, tulibaini kuwa kundi kubwa la vijana linaajiri na kuajiriwa lakini pia vijana hawa wanakosa ujuzi unaotambulika rasmi ndiyo tukaja na mkakati wa Taifa wa uwezeshaji wa vijana kwa kuboresha mazingira na kuwapa stadi na ujuzi mbalimbali unaohitajika katika soko la ajira. Stadi na ujuzi huu utawawezesha kujiajiri na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.”

Alisema mradi wa kitalunyumba ni mradi wa kiprogramu ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umelenga kuwapa vijana stadi za kilimo ili waweze kujiajiri au kuajiri wenzao. “Ofisi yako kupitia programu hii inatekeleza mradi wa kilimo cha kisasa kupitia teknolojia ya kitalu nyumba (greenhose) kwa vijana.”

“Mradi wa kitalunyumba ni ujuzi kwenye shamba wa kuwasaidia vijana kulima mazao ambayo yatawasaidia vijana kupata masoko, yatawasaidia wajiajiri ama kuajiri wenzao na kuongeza pato la Taifa,” alisema.

Alisema uzinduzi uliofanywa katika viwanja vya Ngongo unawakilisha vitalunyumba vyote nchini chini ya mradi utakaohusisha vijana 18,000 ambapo kila Halmashauri ina vijana 100 wanaoshiriki kwenye mradi huo ambao watanufaika na mafunzo ya kilimo cha kisasa.

Alisema hadi Septemba 2019, jumla ya vijana 8,700 kutoka katika Halmashauri 83 za mikoa 12 wamepatiwa mafunzo ya ujenzi na kilimo ndani ya kitalunyumba. Mikoa hiyo ni Mwanza, Iringa, Ruvuma, Shinyanga, Geita, Mbeya, Lindi, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Kagera na Simiyu. Alisema maandalizi ya kutoa mafunzo kwa vijana kutoka katika Halmashauri 102 zilizobaki za mikoa 14 yamekamilika, na yataanza kutolewa kabla ya Novemba, 2019.

Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu imetoa zabuni za kuendesha mafunzo hayo kwa kampuni zinazomilikiwa na vijana wa Kitanzania wenye taaluma za kilimo ambao ni wahitimu wa elimu ya juu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA). Kampuni zilizopewa kazi ya kufundisha vijana wenzao ni Sokoine University Graduates Corporation (SUGECO), Royal Agriculture Ltd na Holly Green Agriculture  Group Ltd.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Video za Ngono Zamponza Menina, Aitwa BASATA

Baada ya kusambaa kwa picha na video zisizo na maadali (za ngono) za msanii Menina, Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limemtaka msanii huyo kufika katika ofisi zake jijini Dar es Salaam.


Share:

Picha : RC TELACK AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI UTEKELEZAJI WA MTAKUWWA....'HALI BADO SI SHWARI MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI'


Imeelezwa kuwa licha ya kuwepo kwa taasisi nyingi na jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali kwa kushirikiana na serikali bado hali ya ndoa na mimba za utotoni si shwari mkoani Shinyanga.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Oktoba 11,2019 na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack wakati akifungua Kikao cha Mwaka cha Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kilichohudhuriwa na viongozi wa dini,wajumbe wa MTAKUWWA na wadau wanaotekeleza afua za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia nyenzo ya MTAKUWWA.

Mkuu huyo wa mkoa alisema hali ya mimba na ndoa za utotoni bado si shwari mkoani Shinyanga kutokana na kwamba vitendo vya kuozesha watoto wa kike vinaendelea kwa usiri mkubwa na watoto wa wanaendelea kupewa mimba katika umri mdogo kutokana na mila potofu zinazochangiwa na ukosefu wa elimu.

“Naomba mtumie fursa ya kikao hiki kujadili kwa kina na kudadavua sababu zinazotukwamisha kushindwa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni na kuweka mikakati inayotekelezeka.Kikao hiki kiwe na tija na manufaa ya kumsaidia na kumkomboa mtoto wa kike”,alisema Telack.

Aidha aliwataka wadau zikiwemo taasisi na mashirika,viongozi wa dini na jamii kwa ujumla kuongeza kasi ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa Mkoa amesema bado kuna changamoto ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia ambapo wanawake na watoto ndiyo waathirika wakubwa kutokana na uwepo wa mila na desturi gandamizi dhidi ya wanawake hali ambayo kikwazo kikubwa cha kuwanyima fursa wanawake na watoto katika kufanya maamuzi kuhusu maisha yao.

Telack ameziagiza mamlaka zote zinazohusika katika kuzuia na kupinga ukatili wa kijinsia kuendelea kuelimisha jamii kwa kutoa ufafanuzi wa athari za unyanyasaji na ukatili wa kijinsia,kusimamia haki,kuharakisha utekelezaji wa mashauri ya kesi zinazohusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Hata hivyo,Telack alisema kutokana na umuhimu wa kutatua changamoto za ukatili dhidi ya wanawake na watoto hususani mimba na ndoa za utotoni,Mkoa wa Shinyanga umeandaa Mpango Mkakati wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto utakaozinduliwa rasmi mwishoni mwa Mwezi Oktoba 2019 ili kukomesha matukio ya aina zote za ukatili.

Kwa Upande wake,Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao alisema miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni kesi za ubakaji kuchelewa kufikishwa kwenye madawati ya jinsia na watoto na kukosa ushirikiano hususani kwenye matukio ya kubakwa ambapo kwenye hatua za mwanzo ushirikiano huwa unakuwepo lakini baadaye wahusika kugeuka na kumaliza kesi kifamilia.

"Kesi nyingi za ukatili wa kijinsia zimekuwa zikikwama kutokana na wahanga kuficha ushahidi,kuwakataa watu waliowafanyia ukatili mfano wabakaji na watu wanaowapa mimba watoto,familia kutorosha mashahidi,kesi kumalizwa kifamilia hali inayochangia vitendo vya ukatili kuendelea katika jamii",amesema.

"Baadhi ya viongozi ngazi ya jamii wakiwemo wa vitongoji,vijiji na kata wamekuwa wakiongoza maridhiano kwenye familia kuhusu matukio ya ubakaji. Tunawaomba wawe wanatoa ushirikiano ili tusafiri kwa pamoja katika kukomesha vitendo vya ukatili katika jamii",ameongeza Kamanda Abwao.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akifungua Kikao cha siku mbili cha Mwaka cha Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kilichohudhuriwa na wadau wanaotekeleza afua za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia nyenzo ya MTAKUWWA. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akiwasisitiza wadau kuendelea kushirikiana na serikali kupiga vita vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela,kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akizungumza katika kikao cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akizungumza wakati wa kikao cha Mwaka cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza wakati wa wakati wa kikao cha Mwaka cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akiongoza kikao cha Mwaka cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Richard Abwao akizungumza wakati wa kikao cha Mwaka cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Richard Abwao akizungumza wakati wa kikao cha Mwaka cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Shinyanga,Victoria Maro akizungumza wakati wa kikao cha Mwaka cha  Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).
Viongozi wa dini na wadau mbalimbali wanaotekeleza afua za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia nyenzo ya MTAKUWWA wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Wadau wanaotekeleza afua za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wanaotekeleza afua za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Kikao kinaendelea.
Kikao kinaendelea.
Kikao kinaendelea.

Kikao kinaendelea.
Share:

Madson Property Limited Inakuletea Mkopo Wa Viwanja Usio Na Riba Wala Dhamana

MADSON PROPERTY LIMITED
inakuletea Mkopo wa Viwanja usio na riba wala dhamana
✅Maeneo yapo GOBA, BOKO, BAGAMOYO, KIBAHA NA VIGWAZA.

📌Goba kinzudi- 35,000
📌Goba njia nne- 38,000
📌Goba mpakani- 32,000
📌Goba Kulangwa-30,000
✅ BOKO viwanja vipo karibu na St Joseph University- 32,000
✅KIBAHA- 11,000
✅BAGAMOYO-13,000
✅ Vigwaza-mashamba 2M kwa hekari moja.
 
NB: Bei hizo ni kwa sqm moja na Viwanja vyetu vimepimwa na Hati zipo tayari.
 
Karibuni ofisi zetu zipo Mwenge Tower Opposite na Mlimani city

Contact: 0718 65 71 89


Share:

Kabudi: Hakuna Mwenye Uwezo wa Kubadili Ukomo wa Rais wa Awamu Mbili

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema hakuna mtu yoyote mwenye uwezo wa kubadili ukomo wa urais wa awamu mbili huku akisisitiza hilo haliwezekani katu.

Profesa Kabudi amesema hayo jana wakati akifungua kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere ambapo mada kuu ilikuwa inasema miaka 20 baada ya Mwalimu.Profesa Kabudi alikuwa amemuwakilisha Rais Dk.John Magufuli ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.

Wakati anatoa hotuba yake Profesa Kabudi alisema kuwa hakuna wa kubadili awamu mbili za uongozi wa urais."Tutaendelea na vipindi viwili vya ukomo wa urais, na kesi iliyofungulia na moja ya raia wa Tanzania kuhusu ukomo wa Rais, isihusishwe na Rais wa sasa."

Alifafanua kwamba vipindi vya urais ni sehemu ya tunu iliyoachwa na Mwalimu Nyerere na hivyo kila mmoja wetu analojukumu la kuilinda tunu hiyo ambayo imeweka utaratibu mzuri kuhusu ukomo wa Rais.

Profesa Kabudi ametumia nafasi hiyo kuelezea pia uamuzi wa Mwalimu Nyerere katika mfumo wa vyama vingi ambao aliuruhu lakini katika mfumo wa kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa na umoja, amani na mshikamano.

Ambapo katika eneo hilo la vyama vingi mbali ya kuwa sehemu ya kumuenzi Mwalimu Nyerere, ametumia kuhimiza Watanzania wa kada mbalimbali kusoma sheria mpya ya vyama vya siasa ambayo kwa sehemu kubwa imefanyiwa marekebisho.

"Moja ya marekebisho ndani ya sheria ya vyama vingi, inazungumzia umuhimu wa vyama vya siasa kufanya uchaguzi za ndani kwa ajili ya kubadilishana uongozi na wanawake kushirikishwa.

"Pia katika sheria hiyo imezungumza kwa kina suala la uwazi kuhusu vyanzo vya fedha pamoja na matumizi yake ambayo yanatakiwa kuwa wazi na kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.Pia sheria hiyo inapiga marufuku kuwa na vyama vya siasa vyenye muelekeo wa udini, kuligawa taifa na fujo na kueneza chuki miongoni mwetu,"amesema Profesa Kabudi.

Aliongeza kuwa sheria hiyo pia inatoa maelekezo mafunzo na itikadi zinazofundishwa ndani ya vyama vya siasa lazima Msajili wa Vyama vya Siasa apewe taarifa na kushiriki kwenye mafunzo hayo.

Profesa Kabudi wakati anazungumzia mambo ya kumuenzi Mwalimu Nyerere amegusia suala la utaifa na hasa katika kuhakikisha lugha ya Kiswahili inaunganisha wananchi wote bila kujali makabila zaidi ya 120 yaliyopo nchini.

"Kuna mambo mengi ambayo nchi yetu inaendelea kufanya kama sehemu ya kuenzi misingi ambayo wengine wanaita tunu iliyoachwa na Mwalimu Nyerere.Hata hivyo Rais wetu Dk.Magufuli kuna mambo mengi anafanya kwa ajili ya kumuenzi kwa vitendo Mwalimu Nyerere,"amesema Profesa Kabudi.

Alitaja baadhi ya mambo ya hayo ni utekelezwaji wa miradi mikubwa nchini ambayo inafahamika kama miradi ya kimkakati ukiwemo uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano kuhamia rasmi Dodoma kwani huo ulikuwa mpango wa Mwalimu lakini hakufanikiwa kuutekeleza.Pia ujenzi wa mradi wa umeme katika bwawa la Mto Rufiji ambalo kwa sasa linafahamika kama Mwalimu Nyerere Hydro Power Project utakaozalisha megawati 2115 na utagharimu zaidi ya Sh.trilioni 7 fedha ambazo ni za ndani.

Pamoja na hayo Profesa Kabudi amezungumzia ujenzi wa reli ya kisasa ambayo awamu ya kwanza ya ujenzi imeanza Dar es Salaam hadi Dodoma."Mwalimu Nyerere aliwapenda sana Watanzania na hivyo alikuwa na ndoto ya kuona wanakuwa na uchumi wa kati , hivyo Rais Magufuli ameibeba ajenda hiyo kwa vitendo ambapo ndani ya miaka minne ya uongozi wake amehakikisha amejenga na anaendelea kujenga miradi mbalimbali ya kimandeleo.

"Na katika hilo Serikali imeamua kwa vitendo kuboresha huduma za afya kwa kujenga vituo 352 na kwa ujenzi wa kila kituo umegharimu Sh.milioni 500 tofauti na hapo awali ambapo gharama za ujenzi zilikuwa kubwa sana na mkapaka sasa kuna maombi ya ujenzi wa viwanda nane vya dawa nchini,"amesema.

Ameongeza kuwa katika kumuenzi Mwalimu Nyerere ambaye alihakikisha watu wake wanapata elimu, Rais Magufuli ameamua kutoa elimu bure huku akifafanua kuwa kama Watanzania wanakumbuka Rais baada ya kuapishwa alikaa miezi mitatu bila ya kuwa na baraza la mawaziri ili fedha za kuwalipa zitumike kusomesha watoto.

"Uamuzi wa Rais kutoa elimu bure, umeongeza idadi ya uandikishwaji wa wanafunzi kwa asilimia 20.1 .Hali hiyo imeongeza pia idadi ya watoto wanaojiunga na masomo ya sekondari,"amesema Profesa Kabudi.

Katika eneo la maji Profesa Kabudi amesema kuwa ni moja ya changamoto kubwa lakini Serikali imeendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha wananchi wake wanapata maji safi na salama.

"Nilikuwa kwenye ziara ya Rais, tukiwa huki tumekutana na changamoto ya uhaba wa maji.Nakumbuka siku za karibuni nilikuwa Marekani ambako huko nilikuwa nalala kwenye hoteli ya hadhi ya nyota tano lakini baada ya kurudi na kuungana na Rais kwenye ziara nimelala gesti ya kawaida ambayo maji ya kuoga tunateka kwa ndoo,"amesema.

Kuhusu mikataba Profesa Kabudi amesema kuwa iliyopo sio kwamba haikuwa halali lakini Rais Magufuli kwa mapenzi mema aliyonayo kwa wananchi wake ameona ni vema ikapitiwa ili kuleta tija kwa watu wote tofauti na awali.

"Ndio maana Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kupitia upya mikataba ya madini na leo hii wote tunaona faida yake.Pia mkataba wa Kampuni ya simu ya Airtel ambao umepitiwa upya na sasa tunanufaika na uwepo wa kampuni hiyo.Niwaambie tu pamoja na Serikali kuwa na hisa bado kila mwezi tunapata Sh.bilioni moja kutoka kampuni hiyo na itakuwa hivyo kwa kipindi cha miezi 60,"amesema Profesa Kabudi.

Hata hivyo amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuenzi mambo ya msingi ambayo yameachwa na Mwalimu Nyerere kwa maslahi ya Taifa letu la Tanzania.

Credit: Michuzi


Share:

Tanzania Kupokea watalii zaidi ya 1000 kutoka nchini Israel

Tanzania inatarajia kupokea watalii zaidi ya 1000 kutoka nchini Israel ambao wanakuja nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii mwezi huu wa Oktoba.

Kundi la kwanza lililokuwa na zaidi ya watalii 200 liliwasili nchini kuanzia tarehe 05 Oktoba na kundi la pili lenye zaidi ya watalii 520 linatarajiwa kuwasili nchini tarehe 12 na kundi la tatu lenye watalii zaidi ya 200 litawasili nchini tarehe 13 Oktoba kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Watalii wengine zaidi wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi huu baada ya Makampuni ya Uwakala wa Utalii kukamilisha taratibu za safari zao.

Watalii hao wanatarajiwa kutembelea Visiwa vya Zanzibar, Hifadhi za Taifa za Serengeti, Tarangire na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Ujio wa watalii hao unatokana na jitihada za kuitangaza nchi zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Israel kwa kushirikiana na wadau wa utalii  wa ndani na nje ya nchi.

Tanzania imejipanga kuwapokea na kuwatembeza watalii hao katika vivutio vya utalii vilivyoko nchini. Serikali inawakaribisha watalii hao kutembelea vivutio hivyo vya utalii ambavyo nchi imebarikiwa kuwa navyo ili wakawe mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania nchini kwao na kwingine watakakokwenda.

Imetolewa na:
Dkt. Faraji K. Mnyepe
Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
DODOMA


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger