Friday, 11 October 2019
4th Round: Undergraduate Multiple Selected Applicants 2019_2020
Undergraduate Multiple Selected Applicants 2019_2020 and not confirmed The Tanzania Commission for Universities (TCU) is a body corporate established on the 1st July 2005, under the Universities Act 2005 (Chapter 346 of the Laws of Tanzania) with mandate to recognise, approve, register and accredit Universities operating in Tanzania, and local or foreign University level programmes being offered by… Read More »
The post 4th Round: Undergraduate Multiple Selected Applicants 2019_2020 appeared first on Udahiliportal.com.
Rais Magufuli awaonya wakimbizi wanaojihusisha na ujambazi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amewataka wakimbizi kutoka nchini Burundi ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kigaidi hapa nchini kuacha mara moja.
Rais Magufuli ametoa onyo hilo alipokuwa akizungumza na wananchi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi baada ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Mpanda hadi Tabora na kuzindua kituo kipya cha mabasi kilichopewa jina la Waziri Mkuu msataafu, Mizengo Pinda.
“Katika mkoa huu kuna wenzetu kutoka Burundi na maeneo mbalimbali ambao tuliwakaribisha katika nchi yetu kama Tanzania ilivyo na ukarimu kwa watu kutoka nje lakini pamejitokeza baadhi ya changamoto watu wako kambini baadhi yao wakawa wanashiriki katika masuala ya ujambazi kulifanya eneo hili lisiwe salama kwasababu ya ukarimu wetu,
“Hauwezi ukakaribishwa kwasababu ya shida ulizozitengeneza huko kwenu uje uzilete hapa hivyo nitoe wito kwa ndugu zetu ambao walikuja hapa tukawapokea kwa upole wasije wakalifanya eneo hili likawa la hatari,
“Hamuwezi mkakaribishwa halafu baadhi yenu wanashiriki kuwaonea raia wema na saa nyingine kupitisha silaha kupitia Ziwa Tanganyika ninawaomba waache na kutokana na mienendo hiyo ambayo haifurahishi tumeona tulichunguze hili suala la kuwapatia uraia watoto wao kwasababu wanaweza wakaleta watu wakasema ni watoto wao kumbe ni majambazi kwani wamekuwa na tabia ya kukaribisha wenzao wiki hii yuko hapa wiki inyokuja yuko Burundi na kadhalika,
Aidha amewataka Watanzania kuacha kuishi na raia hao wa kigeni kwa misingi kwamba wanawasaidia katika kazi kwasababu wao wanakuwa wanawasoma halafu usiku wanakuja, Tanzania ni nchi ya amani na palipo na amani kunakuwa na kila kitu,” amesema Rais Magufuli.
WAKILI LUTAINULWA : WANANCHI ACHENI KUKIMBILIA MAHAKAMANI MIGOGORO MIDOGO MIDOGO
Wakili wa kujitegemea Jovin Rutainulwa
Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Wananchi mkoani Kagera wameshauriwa kujiepusha na masuala ya kukimbilia mahakamani badala yake wamaliza migogoro yao midogo midogo kwa kutumia wana familia, na vyombo vya kidini ili kukwepa kupoteza muda wa kufanya shughuli za kimaendeleo katika jamii.
Ushauri huo umetolewa jana Oktoba 10, 2019 na Wakili wa kujitegemea Jovin Rutainulwa wakati akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake zilizopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ikiwa ni siku ya kupinga adhabu ya hukumu ya kunyongwa duniani.
Wakili Rutainulwa amesema wananchi wanapaswa kuepukana na masuala ya kukimbizana mahakamani kwa migogoro midogo midogo badala yake watumie wanafamilia, na vyombo vya kidini ili kurahisisha migogoro hiyo kuisha kwa haraka kwani kesi hutumia muda mwingi na kusababisha shughuli za ki maendeleo kukwama.
"Mahakama hujaza kesi ambazo nyingine hupaswa kuishia katika ngazi ya jamii. Utakuta kesi nyingi hazina msingi ni za kupoteza gharama na kujenga chuki zisizokwisha, wananchi acheni kukimbilia mahakamani tafuteni njia mbadala za kutatua migogoro yenu labda pale inaposhindikana ndiyo mahakama ihusike’’, alisema wakili Rutainulwa
Aidha Amezipongeza mahakama mkoani Kagera kwa kutenda haki ipasavyo na kuhakikisha kila mtu anapata haki yake licha ya changamoto nyingi.
Ametoa wito kwa mahakama kuendelea na mfumo walio nao wa kupunguza mashauri mahakamani kwa njia ya usuruhishi na kusikiliza kesi kwa haraka huku akitoa pongezi Wanasheria wa serikali na wa kujitegemea kwa kazi wanazofanya katika kuhakikisha wateja wao wanapata haki zao kwa muda kwa mujibu wa sheria.
KIKWETE AKERWA NA WANAOTAFSIRI VIBAYA HOTUBA YAKE

Ofisi ya Rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, imewataka baadhi ya watu kuacha kutoa tafsiri isiyo sahihi, kuhusu alichokizungumza katika kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere.
Taarifa hiyo iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Oktoba 11, imeeleza masikitiko yake kuhusu upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu, kuhusu hotuba aliyoitoa Oktoba 8, 2019, katika Kongamano lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kivukoni.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa katika kongamano hilo Rais Mstaafu, alieleza namna alivyokuwa akimfahamu Hayati Baba wa Taifa, lakini kilichowashangaza ni kujitokeza kwa baadhi ya watu wachache wanaopotosha ukweli kuhusu maneno aliyoyasema kwa kujaribu kuweka maneno ambayo hakuyatamka kinywani mwake kwa madai ya kuwa anawasema baadhi ya viongozi waliopo sasa.
Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, Dkt Kikwete, hakufanya ulinganifu wowote kati ya Mwalimu Nyerere na marais waliopo na waliomaliza muda wao na kwamba huo ni uzandiki, fitna na uchonganishi.

MISITU YA TFS YAONGEZA UZALISHAJI WA ASALI NCHINI
Afisa Nyuki wa wakala wa huduma za misitu(TSF) wilaya ya Shinyanga,Franael Sumari akionesha asali na nta waliyozalisha mwaka huu
Afisa habari na uenezi wa TFS kanda ya Magharibi,Karimu Solyambingu akionesha mtambo wa kutengeneza Nta katika misitu ya TFS Shinyanga.
Mlinzi ofisi za TFS Nzega akionesha baadhi ya mizinga ambayo inaendelea kusambazwa katika wilaya hiyo.
*************
Na Mwandishi wetu, Arusha
Uzalishaji wa Asali na nta chini, umeongezeka katika Misitu inayosimamia na Wakala wa huduma za Misitu Tanzania(TFS) kutokana na kuboresha uhifadhi wa mazingira na wananchi wengi kupata elimu ya kufuga nyuki.
Afisa Habari na uenezi wa TFS Kanda ya Magharibi, Karimu Solyambingu akizungumza na waandishi wa habari, alisema ongezeko la uzalishaji huo wa asali pia limechangia udhibiti wa uhabifu wa mazingira katika hifadhi za misitu unaendelea kufanywa na TFS maeneo mbalimbali nchini.
"katika misitu ya hifadhi inayosimamiwa na TFS kanda ya Magharibi, katika wilaya za Sikonge, Shinyanga, Nzega na hata eneo la Manyoni uzalishaji wa asali na nta umeongezeka sana"alisema
Ramadhani mzirai Meneja wa TSF wilaya ya Shinyanga alisema,uzalishaji wa asali katika misitu ya TFS katika wilaya hiyo, umeongezeka kutoka kilo 130 mwaka 2017/19 hadi kufikia kilom 700 mwaka 2018/19.
"ongezeko hili halijawahi kutokea katika misitu yetu kwani pia tumepata zaidi ya kilo 15 za nta na tumeweza kuwa na mizinga 140 ambayo inazalisha lakini pia wananchi 264 kutoka vijiji 13 tuliwapa elimu na wanafuga nyuki kisasa"alisema
Bibi nyuki wa kituo cha TFS wilaya ya Manyoni, Jackline Leshabari alisema alisema uzalishaji wa asali umeongezeka wilayani Manyoni,kutoka tani 1.7 mwaka 2017/18 hadi kufikia tangi 3.2 mwaka 2018/19.
"ongezeko hilo limetokana pia na kiasi cha mvua cha wastani ambacho kilinyesha msimu uliopita ambacho kiliwezesha nyuki kupata maua kwa wingi na maji kwa ajili ya kutengeneza asali "alisema
Mkuu wa TFS wilaya ya Sikonge, Haji Abdalah alisema kumekuwepo na ongezeko kubwa la uzalishaji wa asali katika misitu iliyohifadhiwa katika wilaya hiyo na mwaka 2018/19 hadi kufikia tani 100.
"katika misitu hii sasa kuna zaidi ya wafugaji 1000 wanaendesha ufugaji wa kisasa lakini pia sisi kama TFS tumekuwa tukishirikiana nao katika kuandaa mizinga na kuwapa elimu ya ufugaji nyuki "alisema
Yuda Zebedayo ambaye ni mmoja wa wafugaji wakubwa wa nyuki wilaya ya Sokonge alisema mwaka huu anatarajia kuwa na asali zaidi ya 120 kutokana na kuwepo msimu mzuri katika misitu ya wilaya hiyo.
Katika wilaya ya Nzega Katibu wa mbunge wa jimbo la Nzega vijijini, Basirio Lazaro alisema uzalishaji wa wilaya hiyo, inaendelea kuongezeka hasa baada ya TFS kuwapa mizinga mipya 300 katika vikundi vya ufugaji nyuki.
Lazaro alisema kila kikundi kimepewa mizinga 20 na sasa wameanza kuvuna asali na wanatarajia mwishoni mwa mwaka huu, kuwa na mavuno makubwa.
"tunapongeza TSF na Waziri wa Maliasili na Utalii, ambaye ni mbunge wetu, Dk Hamis Kigwangalla kwa kazi nzuri ambayo wanafanya hapa nzega kuwahakikisha maisha bora wananchi kupitia asali badala ya kutegemea kilimo pekee"alisema.
JAJI MKUU: SHERIA ITUMIKE IPASAVYO KUDAI TAARIFA
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na Mwenyekiti wa MISATAN Tanzania, Bi. Salome Kitomari (hayupo pichani) pindi ujumbe kutoka Taasisi hiyo ulipomtembelea Ofisini kwake, Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa MISATAN-Tanzania, Bi. Salome Kitomari akizungumza jambo na Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani).
Mhe. Jaji Mkuu akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe, wa kwanza kushoto ni Katibu wa Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Adrian Kilimi, kulia ni Maafisa kutoka MISATAN na Mahakama.
Maafisa kutoka MISATAN-Tanzania, (kushoto), Mwenyekiti, Bi. Salome Kitomari na Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi hiyo, Bi. Neema Kasabuliro kwa pamoja wakinukuu masuala yaliyokuwa yakitolewa na Mhe. Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka MISATAN-Tanzania na baadhi ya Watumishi wa Mahakama walioshiriki katika mazungumzo hayo, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa MISATAN Tanzania, Bi. Salome Kitomari, wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe, wa kwanza kushoto ni Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi hiyo, Bi. Neema Kasabuliro na wa kwanza kulia ni Salum Tawan, Mkutubi-Mahakama ya Tanzania. (Picha na Mary Gwera, Mahakama)
Na MISA Tanzania
Ujumbe wa taasisi ya MISA Tanzania ukiongozwa na Mwenyekiti wake Bi. Salome Kitomari umemtembelea na kufanya mazungumzo na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo, Bi. Kitomari ameitambulisha MISATAN pamoja na kuelezea majukumu yake mbalimbali kwa Mhe. Jaji Mkuu ikiwemo kutetea na kufanya uzengezi kuhusu utoaji na upataji taarifa nchini.
Mwenyekiti wa MISA amezungumzia uhusiano mzuri uliopo baina ya taasisi yake na Mahakama ya Tanzania. Uhusiano huo umejikita ktk kuimarisha na kutetea haki ya utoaji na upatikanaji wa taarifa zenye maslahi kwa umma. “Katika hili, MISA kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania tumeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi zaidi ya 300 wa kada mbalimbali za Mahakama kuhusu namna bora ya kuwahudumia wateja na mbinu za utoaji wa taarifa kwaumma” alifafanua Bi. Kitomari.
Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na MISA Tanzania, mafunzo haya yameongeza weledi kwa washiriki na kuleta mabadiliko chanya katika utoaji wa taarifa za Mahakama hapa nchini. Aidha, Mwenyekiti wa MISA alisisitiza haja ya kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya taasisi hizi mbili
pamoja na kuhusisha taasisi nyingine za kihabari ili kupanua wigo wa utoaji na upatikanaji wa taarifa za kimahakama zenye maslahi ya umma.
Bi. Kitomari ameshauri kufanyika mikutano kati ya MISA TAN, Mahakama ya Tanzania na taasisi nyingine za Habari ili kuimarisha ushirikiano, imani na uwajibikaji katika mchakato mzima wa utoaji na upatikanaji wa taarifa kwa wananchi. Pia, ameshauri kuwepo kwa mafunzo endelevu ya huduma kwa mteja na upatikanaji wa taarifa kwa kuhusisha viongozi wa juu wa Mahakama wakiwemo Majaji, Mahakimu na afisa tawala.
Kwa upande wake, Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Tanzania ameipa changamoto MISATAN na taasisi nyingine za Habari nchini kuitekeleza ipasavyo Sheria Namba 6 ya Upatikanaji wa Habari ya mwaka 2016 katika kudai taarifa zenye maslahi kwa umma na taifa. “Sheria hii inatoa shurti ya kutoa taarifa zinazotakiwa na umma, hivyo sio Fadhila bali ni amri. Hivyo ni vyema kuangalia ni kwa namna gani tunatumia sheria hii kushurutisha utoaji wa taarifa sahihi kwa wananchi” alisisitiza Mhe. Jaji Mkuu.
Aliongeza kwamba ni wajibu wa kila mmoja kutimiza wajibu wake kikamilifu katika kutekeleza sheria hii ipasavyo. “Kwa kufanya hivyo tutakua tumetekeleza takwa la Kikatiba na kisheria” amehimiza Mhe. Jaji Mkuu.
Kwa upande mwingine, Mhe. Prof. Juma amevitaka vyombo vya Habari kuzingatia weledi katika kuhabarisha umma ili kuepusha mifarakano katika Jamii. Amewahimiza waandishi wa habari nchini kujikita zaidi katika kuandika habari za kiuchunguzi badala ya kutegemea habari za matukio. “Habari za kiuchunguzi huhusisha utafiti na ushahidi wa jambo. Kuripoti habari hizi kutapunguza malalamiko na mifarakano katika jamii” amehitimisha Mhe. Jaji Mkuu.
MKURUGENZI MTENDAJI WA TIGO, SIMON KARIKARI ASIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WATEJA WA TIGO KATIKA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA
Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja (Tigo)Bi. Mwangaza Matotola -, akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mawasiliano Tigo Bw. Simon Karikari pamoja na viongozi wa idara mbalimbali katika kituo cha kisasa cha huduma kwa wateja. Tukio hilo liliambatana na ukataji wa keki.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano TIGO Bw. Simon Karikari akimuongoza mteja katika duka la Tigo Mlimani City kukata keki ya kusherehekea wiki ya Huduma Kwa Wateja pamoja na kushiriki katika kutoa huduma kwa wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari, akijibu na kutatua maswali ya wateja wa Tigo katika kituo cha cha kisasa cha huduma kwa wateja , zoezi hilo limefanyika katika wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari, akijibu na kutatua maswali ya wateja wa Tigo katika kituo cha cha kisasa cha huduma kwa wateja , zoezi hilo limefanyika katika wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya mawasiliano TIGO Bw. Simon Karikari ametembelea duka la Tigo Mlimani City na kupata nafasi ya kushiriki katika wiki ya huduma kwa wateja na wateja wa Tigo waliokuwa wakiendelea kupata huduma.
Watumishi wa umma, Watanzani jitokezeni kujiandikisha-Kailima
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhan Kailima, ametoa wito kwa watumishi wa umma na Watanzania kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili kutumia fursa hiyo kuchague viongozi wenye sifa karika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Kailima aliyasema hayo Mjini Dodoma jana asubuhi baada ya kujiandikisha katika daftari hilo kwenye kituo kilichopo Mtaa wa Chimuli, Kata ya Makole.
Alisema uzoefu unaonyesha kuwa, kuna mwamko mdogo kwa kundi la watumishi wa umma kujiandikisha, kushiriki uchaguzi huo ili waweze kuchagua viongozi wenye sifa.
“Uchaguzi wa Serikali za Mitaa una umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla, uandikishaji huu umeanza Oktoba 8-14, mwaka huu.
“Kampeni zitafanyika kwa wiki moja kuanzia Novemba 17-23, mwaka huu, uchaguzi utafanyika Novemba 24, mwaka huu…ni muhimu jamii kutambua kuwa, mshindi katika uchaguzi huu atapatikana kwa idadi ya wapiga kura sio asilimia,” alisema.
Kailima alisema ni muhimu Watanzania wakashiriki uchaguzi huo uli watumie fursa hiyo kuchagua kiongozi anayestahili, wasiposhiriki atachaguliwa Mwenyekiti wa Serikali ama mjumbe ambaye jamii kubwa haitapenda achaguliwe.
“Nawaomba wananchi wahudhurie kampeni, waulize maswali kwa wagombea, watumie fursa hiyo kuchagua viongozi ambao ni waadilifu na waaminifu.
“Rushwa ni adui wa maendeleo, wananchi mjiepushe kupokea rushwa, Wizara yangu kupitia taasisi zake za ulinzi na usalama ziko imara, tutaimarisha ulinzi wakati wa kampeni, upigaji kura na utangazaji matokeo,” alifafanua.
Aliwapongeza waandikishaji, wasimamizi wa zoezi hilo kwa kufika mapema kwenye vituo vya uandikishaji wapiga kura.
Alisema vituo hivyo viko sehemu barabarani, mitaani ambapo uandikishaji huo hauna vikwazo kwani hauhitaji kitambulisho cha uraia, cheti cha kuzaliwa.
“Ukifika kituoni utaulizwa majina yako kamili, umri wako, eneo unaloishi…kama eneo lako la kujiandikisha sio hilo utaelekezwa eneo la kwenda kujiandikisha,” aliongeza.
Kwa upande wao, mwandikishaji wapiga kura katika kituo hicho, Peter Ititi na mjumbe wa Serikali ya Mtaa huo, John Fundi walimshukuru Kailima kwa wito alioutoa ili jamii ione umuhimu wa kushiriki uchaguzi huo.
Thursday, 10 October 2019
Habinder Singh Seth Kaandika Barua Kwa DPP Kukiri Makosa Yake
Mfanyabiashara maarufu , Habinder Singh Seth ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha.
Wakili wa Seth, Michaele Ngalo, ameiarifu Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Oktoba 10 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Seth pamoja na mfanyabiashara mwenzake James Rugemalira, kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 wanayodaiwa kuyatenda jijini Dar es Salaam, Afrika Kusini, Kenya na India.
Washtakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama hiyo Juni 19, 2017 na hadi sasa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Miongoni mwa mashtaka hayo ni kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi na kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara ya Dola milioni 22 na Shilingi za Tanzania bilioni 309.
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amethibitisha kuwa wamepokea barua ya Seth wanaifanyia kazi na majibu yatatolewa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 24, 2019
Kadi Ya Mpiga Kura Haitatumika Kwenye Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi kwa wananchi juu ya mazoezi mawili tofauti yanayoendelea Nchini ya kuandikisha wapiga kura na kuwatahadharisha kwamba Kadi ya Mpiga Kura inayotolewa na Tume haitatumika kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwenzi ujao.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo (10.10.2019), Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Dkt. Wilson Mahera Charles amesema kwamba uandikishaji unaoendelea ambao ulianza tarehe 08, Oktoba 2019 unahusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 24 Novemba 2019 ambao hausimamiwi na Tume.
“Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwataarifu wananchi kuwa uandikishaji unaofanyika kuanzia tarehe 08, Oktoba 2019 hadi tarehe 14, Oktoba 2019 na kusimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI) kupitia Halmashauri mbalimbali kote Nchini unahusika na uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 24 Novemba 2019. Mwananchi asipojiandikisha hataweza kupiga kura katika uchaguzi huo,” amesema Dkt. Mahera.
Aliongeza kwamba mwananchi ambaye hatajiandikisha kwenye uandikishaji unaofanywa na OR-TAMISEMI hatapata fursa ya kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24 mwaka huu, hata kama atakuwa na Kadi ya Mpiga Kura inayotolewa na Tume na kwamba uchaguzi huo hausimamiwi na Tume bali unasimamiwa na OR-TAMISEMI
Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi hilo la kujiandikisha ili wapaete fursa ya kuwachagua viongozi wa mitaa yao siku hiyo ya tarehe 24 Novembe 2019.
Aidha, Dkt. Mahera amesema kwamba Tume kwa mujibu wa Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ina jukumu la kuandikisha Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani kwa Tanzania Bara.
“Uandikishaji huo (wa OR-TAMISEMI) ni tofauti na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaofanywa na Tume kwenye mikoa mbalimbali Nchini. Uboreshaji huu unahusu Uchaguzi wa Rais, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani wa Tanzania Bara utakaofanyika mwakani 2020,” amesema.
Dkt. Mahera ameeleza kwamba zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linaendelea kwa sasa katika mikoa ya Tabora, Katavi na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma ambako uboreshaji utafanyika kuanzia tarehe 14 Oktoba hadi tarehe 20 Oktoba mwaka huu.
Ameongeza kwamba zoezi hilo litaendelea kwenye mikoa ya Songwe, Dodoma na Singida kuanzia tarehe 26 Oktoba hadi tarehe 01 Novemba 2019.
“Wanaostahili kujiandikisha ni wale ambao wana miaka 18 na wale ambao watafikisha miaka 18 mwakani (2020) kabla ya uchaguzi, lakini pia zoezi linawahusu wale ambao kadi zao zimeharibika au zimepotea ili wapate fursa tena ya kuwepo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,” alismema Dkt. Mahera.
Mwisho
Taasisi Za Umma Zapigwa Marufuku Kutumia Kampuni Binafsi Katika Masuala Ya Tehama
Serikali imepiga marufuku taasisi za umma nchini kutumia fedha za Serikali kuilipa taasisi binafsi ili kupatiwa huduma ambazo pia zinazotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) ametoa agizo hilo kwa watumishi wa umma na waajiri Serikalini, wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kilichofanyika wilayani humo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.
Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, Serikali imebadili Wakala ya Serikali Mtandao kuwa Mamlaka kwa sababu hivi sasa ina wataalamu wa kutosha wa TEHAMA hivyo hakuna ulazima wa kuilipa kampuni binafsi ili kupata huduma ya TEHAMA.
“Kama Serikali ina chombo chenye uwezo na weledi wa kutosha wa kutoa huduma za TEHAMA ikiwemo mifumo ya kielektroniki ya utoaji huduma, ni nini kinachoshinikiza Taasisi za Umma kuendelea kuomba kupatiwa huduma hiyo na kampuni za watu binafsi?,” Mhe. Mkuchika amehoji.
Mhe. Mkuchika yuko katika ziara ya kikazi mkoani Ruvuma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani humo.
Tembelea Ivigo Herbal Clinic: Kituo Cha Tiba Asili Na Tiba Mbadala Kwa Magonjwa Ya Binadamu
IVIGO HERBAL CLINIC ni Kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa Magonjwa ya Binadamu ikiwemo Kisukari, presha, Nguvu za Kiume, Vidonda vya Tumbo, Tambazi, MATATIZO ya Uzazi, BAWASIRI, Muwasho sehemu za siri, Miguu kuvimba, UVIMBE Tumboni, Tezi Dume, SHINGO ya KIZAZI kwa Akinamama ,Meno bila kung'oa, Maumivu ya Mgongo na kiuno , Kuborsha Maumbile ya Kiume pamoja na MATATIZO Mbalimabali ya Kimaisha.
Kwa Huduma zetu Tembelea Vituo vyetu ulichokaribu nacho. MBEYA tupo barabara ya ISANGA kabla hujafika Darajani simu 0744687649, Mbarali KITUO KIPO IGAWA STAND YA BARABARA KUU YA KWENDA MBEYA SIMU 0767007704, DODOMA KITUO KIPO CHANG'OMBE STAND simu 0746906010 na Makao Makuu NJOMBE simu 0767944041.Nyote Mnakaribishwa IVIGO HERBAL CLINIC kwa Tiba Bora







































