Saturday, 10 August 2019

Ufugaji wa nguruwe : Gharama na Faida Zake

 Utangulizi
Nguruwe ni mnyama amabaye hutumika kama chakula / mboga na pia ni zao la biashara kwa mfugaji, mjasirimali na mfanyabiashara.
 
NGURUWE HUTEGEMEA SANA MAMBO YAFATAYO
1 . Banda imara na rafiki kwake
2. Usafi ni muhimu sana katika banda la Nguruwe
3 Mchaganyo bora wa chakula
4. Tiba bora na kinga
5. Maji na Lishe ( access ya vyakula Muhimu kwake )
 
CHANGAMOTO
KATIKA UFUGAJI WA NGURUWE KUNACHAGAMOTO ZAKE LAKINI ZAWEZA KUTATULIWA KWA KUFATA MAMBO KADHAA.
Katika ufugaji wa nguruwe kunachagamoto ya vifo vya nguruwe wachanga ambao hupunguza faida ya biashara ya nguruwe kwa kupunguza idadi ya nguruwe wazima wa kuuzwa lakini utunzaji mzuri wa nguruwe wachanga huepusha vifo vinavyotokana na shida kama:
 
Matatizo ya kupumua
Ni kifo kinachosababishwa na mama anapomlalia nguruwe mchanga.chagamoto hii inaweza kutatuliwa kwa kuwatenga au kuwa na mabanda makubwa ya kulelea watoto.
 
Baridi
Nguruwe wachanga huathiriwa na baridi haswa katika majuma mawili au matatu ya mwanzo. Hii ni kwa kuwa wana kiwango kidogo cha utando wa mafuta wa kuwakinga.
 
Unashuriwa kuwaweka katika hali ya joto, wape matandiko na utumie vipasha joto kama vile kuwasha globu za joto kama utakuwa umewaweka kwenye mabanda ya kuta au nyumba yenye sakafu baridi.
 
Namna bora utunzaji wa nguruwe wachanga
Nguruwe moja wa kike ana uwezo wa kuzaa watoto 12. Namna ifuatayo itasaidia kupunguza idadi ya vifo vya nguruwe wachanga:
1.Pale nguruwe awapo na kidonda nyunyizia dawa ya ayodini 5% kwenye kovu ili kuzuia kuambukizwa kwa magonjwa.
2.Wawekee matandiko (nyasi kavu au maganda ya miti) mahali pa mapumziko ili wapate joto au utumie globu za joto.
3Wadunge sindano ya madini ya chuma (iron) siku ya tatu baada ya kuzaliwa ili kuzuia upungufu wa damu.
3. Yalainishe meno ya vichaga kabla ya masaa 24 ili kuzuia uharibifu wa matiti wakati wanaponyonya.
4. Watie vibandiko au utoboe masikio ili uwatambue na uhifadhi rekodi zao kama kuna umuhimu kama vile wafanyavyo wafugaji wa ng’ombe.
5. Wapime uzani wanapozaliwa na uhifadhi rekodi hiyo itakusaidia kujua ukuaji wao na maendeleo yao
6. Wahasi wale wa kiume juma la tatu, wale ambao hawafai katika kuendeleza kizazi kwa kutumia mtindo wazi (open method) kama unaona inafaa.
7. Wapatie dawa ya kuzuia minyoo pia zipo dawa za asili kama unga wa mkaa na majivu pia zipo za kitaalamu, wasiliana na wataalamu wa mifugo
8.Waachishe kunyonya katika juma la nane au wafikapo kilo 14 hadi 20 hii itasaidia kujitegemea na kukua kwa haraka.
 
Nguruwe Walioachishwa Kunyonya
1.Walioachishwa kunyonya wawekwe makundi ya 10 hadi 12 kulingana na uzito au ukubwa wao kwenye eneo ambalo watajitosheleza.
2.Watenganishe wakubwa kwa wadogo ili kuzuia kupigana.
3.Wakati wa kuwaachisha kunyonya mwondoe mama yao kutoka kwa watoto ili kupunguza usumbufu.
4Watoto wa nguruwe wa mama tofauti wasiwekwe pamoja maana hii husababisha mapigano kati yao na
5.Unapowachanganya watoto wa mama tofauti wapake mafuta ya gari yaliyotumika kwenye ngozi yao au mafuta ya kula ili kuiondoa harufu ya kutambulika ili wasipigane
 
FAIDA YA UFUGAJI WA NGURUWE
Faida kuu ya nguruwe ni zao la chakula lakini pia ni zao la kukuongezea kipato ukiwa kama mjasirimali / mfanyabiashara.
Lengo langu nikueleza namna unavyoweza kufuga na kutupa faida, Steps zifatazo ni muhimu kuzigatia.
 
JIPE MTAJI WA MILLION 4 / 3.5 KWA NGURUWE 50
UANDAAJI WA BADA WEKA MAKADILIO YA LAKI TANO (800,000/=) .
Hapo nazugumzia banda lenye heru U yenye mstatili ikiwa na kitako kirefu
Eneo lenye ukubwa wa mita 50 kwa 50 litafaa zaidi ili kuhakikisha usalama wa nguruwe wako na ukuaji bora.
1. Tafuta mabati used kwa bei ya 5000 mfano mabati 20 ya futi 10 /10 = 100,000/=
2. Tafuta mabazi ya futi 10 kwa 2000 kila moja utapata mabazi pic 100 = 200,000/=
3. Tafuta miti ya nguzo na kechi ya 1000 na 2000 miti ya 1000*70 na 2000*3 = 120,000/=
4. Tafuta chagalawe / moramu trip 10*3000 =30000/=
5. Cement mifuko kwa ajiri ya sakafu na mashimo ya kulishia 5 *18000 = 90,000/=
6. Misumari ya aina 4, nch 6 kg5,nch 3 kg5 nch 5 kg10 na nch4 kg10, Bawaba na komeo =100,000/=
7. Malipo ya fundi 75000 fundi uashi na 75000 fundi seremala =150,000
JUMLA HAPO INAKUWA 790,000/= MAKADILIO INAKUWA 800,000/=
 
UNUNUZI WA NGURUWE WA KUANZIA .
Nguruwe wadogo wadogo ni vinzuri zaidi kuanza nao kwa sababu watakuzalia watoto wengi na kwa muda mrefu . Chukua mfano MILLION 2.5 . Nguruwe wadogo wa dogo wanauzwa 50000 au 40000 inategemeana na mahala na maelewano . Milioni 2.5 inakupa vitoto 50 au 55 . Hivyo unawexa kuwa na vitoto jike 50 na vidume 5. baadaye ukaongeza madume matano ya kuazima au kukondi kwa ajiri ya kupandishia
 
MAANDALIZI YA CHAKULA
Mchaganyiko wa chakula cha nguruwe na gharama zake tunaweza ukadilia kujitosheleza kwa laki tatu kwa mwenzi mmoja kwa nguruwe hao 50, kwa 300,000/= , ambapo itajumuisha tiba / kinga, lishe, vyakula vya nguruwe vinaweza kuwa pumba ya mpunga ile laini,pumba ya mahindi, mashundu, mabaki ya magada ya vianzi amba mabaki ya chakula yaliyosalama
 
MALIPO YA MSIMAMIZI NA ENEO LA KUWEKEZA
Katika kipengele hiki makadilio ya juu ama ya chini kwa msimamizi wa kazi yako waweza mlipa 100,000/= ama chini yake pia kwa mwenye eneo huwa nimaelewano tu aunaweza pata kwa fair au kukakodi kwa laki tatu, 300,000/= kwa mika miwili.
 
HIVYO JUMLA YOTE YA GHARAMA ZA UAZISHAJI UWEKEZAJI WA NGURUWE 50 ZITAKUGHARIMU MILLION 4 AMA MILLION 3.5 KWA MAANA KUWA HAPO JUU NIMETUMIA MAKADILIO YA JUU NA UKIINGIA KWENYE UHALISIA KAMA MJASIRIMALI LAZIMA IPUNGUE NA KUFIKIA 3.5

KIPATO AU FAIDA YA UFUGAJI NGURUWE
Nguruwe wanafaida ya haraka na nimradi wa uhakika kabisa, ukipitiia mchanganuo hapo juu wa nguruwe 50 utatupa faida kama ifatavyo
 
Nguruwe huzaa Mara mbili kwa mwaka na huzaa watoto zaidi ya watanoyaani huzaa watoto 12 ama nane .
Basi chukua nguruwe 50 * vitoto 5 yaani ufanye kuwa nguruwe wako 50 wakupatie vitoto vitano vya uhakika
Nguruwe 50*5 = 250 ukijumlisha na wale 50 wa mtaji umakuwa nao 300 . Chukua zao la nguruwe la 250 na uza kwa 200000 kwa kila nguruwe yaan bei ya kawaida kabisa. Utapata Million 50.

Hivyo zao la kwanza ndani ya robo tatu ya mwaka inakutegenezea million 50 pia na mienzi sita ijayo inakupa tena 50 na zaidi ili kukamilisha uzao wa pili hii inkupa uhakika wa kutegeneza million 100 za uakakika ndani ya mwaka mmoja na nusu ama miaka miwili ukijipa timeframe work lakini kumbuka hapo tumefanya kwa hesabu ya uzao wa chini kabisa ambapo tumeangalia na hasara ya vifo kama vifo visipotokea na uzao ukawa mkubwa utakuwa na uhakika wa kutegeneza million 150 kwa miaka miwili.

Kwenye hesabu ya kuwale unaweza kuwaza sana kuwa itaongezeka na kukughalimu sana jibu ni hapana mpka kufikia kuuza hawatokugharimu zaidi ya million 7 je million 7 kwenye million 150 ni kitu kisicho nafaida ?
 
NB . jambo lolote linahitaji umakini naa dhamira ya dhati pia kushirikisha wataalamu na wenye uzoefu ili kufikia leng Ewe ndugu kila kitu kinawezekana UTAYARI WAKO / UTHUBUTU WAKO, UAMINIFU .NA MAAMZI YAKO.
 


Share:

Jeshi la Polisi Lataja idadi kamili ya marehemu na majeruhi wa ajali ya moto mkoani Morogoro.

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Lebaratus Sabas,  ameitaja idadi ya watu waliofariki katika ajali ya gari iliyoanguka nakupelekea kulipuka kwa moto leo Agosti 10,  imefikia 62.
 
Ameeleza kuwa kati yao wanaume ni  58 na wanne ni wanawake ambapo mmoja katika wanawake hao ni mtoto.

Kwa upande wa idadi ya majeruhi imefikia  72, wanawake wakiwa 8 na wanaume 64 ambapo wote wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hosptali ya rufaa ya Morogoro.

Ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi katika eneo la Msamvu Mkoani Morogoro na hadi sasa Jeshi la polisi,  limekwishakamata lita takribani 206 za mafuta ya petroli , zilizokuwa zimefichwa katika mabanda pembezoni mwa eneo la ajali ilipotokea.

''Pia katika eneo la  tukio zimepatikana pikipiki zilizoungua kwa moto zipatazo 26 na baiskeli 6, pia yamaeonekana mabaki ya madumu na ndoo za plastiki zilizoungua'' amesema Kamishna Sabas.

Aidha Kamishina Sabas amewataka wananchi wanaoishi kandokando  ya barabara kutokuwa na tamaa na kujiepusha na ajali ambazo zinaepukika, pamoja na kuwataka wale wote waliopata majeraha madogomadogo na  kutokomea wasisite kwenda hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.


Share:

Ajali ya Moto Morogoro: Lugola Akatisha Ziara Yake Mkoani Rukwa

Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola  ameamua kuahirisha  ziara yake Mkoani  Rukwa  kutokana na ajali ya moto iliyotokea eneo la Msamvu Mjini Morogoro.

Ajali hiyo imetokea leo tarehe 10 Agosti, 2019 majira ya saa 2 asubuhi ambapo lori hilo lililokuwa linatoka Dar es Salaam limepinduka jirani na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu baada ya dereva wa lori kumkwepa mwendesha pikipiki na kisha mafuta yaliyokuwa yakimwagika kushika moto na kuunguza watu waliokuwa wanayachota.

Waziri huyo ameanza safari kuelekea eneo la tukio.


Share:

Huawei Waamua Kuachana na Android....Watengeza Program Yao

Kampuni ya Huawei imeweka wazi jina la programu endeshaji mpya kwa ajili ya simu na vifaa vya kisasa vya kielektroniki ambayo itaanza kutumika badala ya Android.

Mfumo huo wa Huawei-HarmonyOS unalenga kupunguza utegemezi wake kwa kampuni za Marekani.

HarmonyOS utakuwa tayari kuwekwa katika skrini za samart kwenye bidhaa kama vile Televisheni, saa za smart , na magari baadae mwaka huu, amesema Richard Yu, Mkurugenzi mkuu wa wa kitengo cha walaji cha Huawei katika mkutano wa ubunifu.
 
Katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Huawei,kampuni ambayo ni ya pili kwa ukubwa duniani ya mauzo ya smartphone ,  imesema itaangalia jinsi ya kuuweka mfumo wa HarmonyOS kwenye vifaa zaidi zikiwemo simu zake za mkononi aina ya smartphones.
 
Kampuni ya Huawei inasema kuwa imeazimia kuendelea kutumia Android ,lakini HarmonyOS utatumika kama mpango mbadala kama mambo yataenda kombo

Tangazo hilo la Huawei limekuja miezi kadhaa baada ya serikali ya Marekani kuweka masharti ya kibiashara nchini Marekani yanayoilenga kampuni hiyo pamoja na kampuni nyingine washirika .

Serikali ya Marekani imeishutumu Huawei kwa kuiba siri za kibiashara , na ikasema inaleta hatari kwa usalama wa taifa.

Baada ya shutuma hizo , Google, Intel,na makumpuni mengine yanayochangia  kwa kiasi kikubwa katika teknolojia na utatuzi wa matatizo ya smartphone walisitisha biashara na Huawei


Share:

Korea kaskazini Yarusha Makombora Zaidi

Korea kaskazini imerusha makombora 2 ya masafa mafupi katika bahari  ya mashariki.

Taarifa zilizotolewa na jeshi la Korea kusini inasema majaribio ya makombora mawili yalifanyika mashariki mwa Korea kaskazini. 

Makombora hayo yaliyofikia kimo cha kilomita 48 baada ya kusafiri umbali wa kilomita 400 yalianguka bahari ya mashariki.


Share:

Kutana na Sheikh Omary Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali za Matatizo Yako Na Kutafsiri Ndoto kwa kutumia Vitabu vya QUR-AN

Sheikh Omary Ni bigwa wa kutatua matatizo kwa haraka, ni mtu aliye jaliwa kubuli Shufaa pia anatoa Duah  za Ruhia. Ukija na Maradhi yanaondoka hapo hapo bila kungoja kesho,  UKIPEWA MKONO  na Sheikh Omary .
 
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
 
Sheikh Omary ni Mtaalamu wa Nyota za Binadamu  Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
 
Je una NUKSI  zisizo kwisha.!? JE umekimbiwa na Mume/Mke na Anaishi na Mtu Mwingine..!? Muone Akutatulie,
 
Una kosa bahati ya wanaume au mume wa kukuoa..Unataka nyota ing'ae Au huna hamu na Mkeo/ Mumeo.
 
Jini mahaba. Kama Unakasirika ovyo ukiwa na bwana au mwanamke wako na  kumchukia Mpaka  kushindwa kufanya nae tendo la ndoa.
 
Njoo umuone Sheikh Omary  na ujuwe  yanayo kusibu.Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN

Mawasiliano: Sheikh Omary 0673531992. WhatsApp/Call
Tembelea Page ya @Mtabibu_Omar  @Mtabibu_Omar
Usome Makala Tofauti Tofauti Kama.


Share:

Waziri Mkuu: Bodi Ya Mikopo Tafakarini Vigezo Vya Kutoa Mikopo Kwa Wanafunzi

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutafakari namna ya kurekebisha baadhi ya dosari zilizopo likiwemo suala la kuwanyima mikopo wanafunzi kwa kutumia kigezo cha kusoma katika shule binafsi.

Amesema kuna baadhi ya wanafunzi ambao wamefaulu vizuri kidato cha nne na wamekosa nafasi katika shule za Serikali na wanatoka katika familia zisizokuwa na uwezo, hivyo wanatafuta wafadhili ambao wanawasomesha kwenye shule binafsi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Agosti 10, 2019) wakati akifungua mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) kwenye ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Amesema kitendo cha bodi hiyo kuwanyima mikopo baadhi ya wanafunzi kwa kigezo cha kusoma katika shule binafsi bila ya kujiridhisha kama wanatoka kwenye familia zenye uwezo au zisizokuwa na uwezo kinawanyima wanafunzi hao fursa za kuendelea na masomo.

 Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaonya wakuu wa vyuo vikuu ambao wanatumia vibaya fedha za mikopo ya wanafunzi kwa kuzipeleka katika miradi mbalimbali baada ya kuzipokea kutoka HESLB na kuwacheleweshea wanafunzi stahiki yao.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa vyuo vikuu kuimarisha mafunzo kwa njia ya vitendo kwani tafiti nyingi zinazohusu mambo ya ajira zimebainisha umuhimu wa mafunzo ya vitendo katika kumuwezesha mhitimu kuwa na uelewa na ujuzi mpana wa kile alichokisoma kwa njia ya nadharia.

“Vyuo viongeze umakini na ufuatiliaji wa karibu wa vijana wetu wanapokuwa kwenye elimu kwa vitendo ili kuhakikisha kwamba wanapata maarifa na ujuzi uliokusudiwa katika mitaala yao. Pia natoa wito kwa waajiri wa sekta ya umma na binafsi watoe ushirikiano wa dhati kwa wanafunzi wanaotafuta nafasi za kufanya mafunzo kwa njia ya vitendo kwenye taasisi zao.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAHLISO, Bw. Peter Niboye amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanafunzi wa elimu ya juu ni ucheleweshwaji wa mikopo kwa baadhi ya vyuo licha ya HESLB kuwasilisha fedha hizo mapema, hivyo ameiomba Serikali kuwasaidia katika kutatua tatizo hilo.

Kadhalika, Mwenyekiti huyo wa TAHLISO, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa ushirikiano mkubwa inaoipatia jumuiya hiyo hivyo kurahisisha utendaji wake.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bw. Patrobas Katambi alimkabidhi Waziri Mkuu hati ya kiwanja kilichoko katika eneo la Mtumba jijini Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za TAHLISO, ambapo baada ya kupokea hati hiyo, Waziri Mkuu aliikabidhi kwa Mkwenyekiti wa jumuiya hiyo Bw. Niboye.

Mkutano huo umehudhuriwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Godfrey Chongolo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Bw. Kisare Makori pamoja na viongozi kutoka vyuo mbalimbali nchini vinavyounda TAHLISO.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,        
JUMAMOSI, AGOSTI 10, 2019.


Share:

Waziri Mkuu Awalilia Waliofariki kwa Ajali ya Lori Morogoro

Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa ametumia dakika moja kuwaombea dua majeruhi na watu waliopoteza maisha yao kwenye ajali ya moto iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Msamvu- Mkoani Morogoro.

Akitoa salamu za pole kabla ya kuanza hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (Tahliso) unaofanyika katika ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo Jumamosi, Majaliwa amesema ajali hiyo inasikitisha.

"Mpaka sasa kuna majeruhi zaidi ya 63 hali zao sio nzuri sana, tunawaombea kwa Mungu ili wapone haraka. Ajali hii imetokana na lori na ndugu zetu hawa walienda kujipatia mafuta," amesema Majaliwa.

Akizungumzia mkutano huo, Majaliwa amesema amani na utulivu vilivyopo kwenye vyuo vya elimu ya juu nchini vinaonyesha kuna watu wanatekeleza wajibu wake ipasavyo.

Amempongeza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kwa kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi wa elimu ya juu.


Share:

DC Ndejembi : Waliofanya Ubadhilifu Wa Fedha Ujenzi Wa Kongwa Sekondari Watazitapika.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mkuu wa wilaya  Kongwa jijini Dodoma Deo Ndejembi amesema wahusika wote waliofanya ubadhilifu wa fedha za ujenzi katika Shule ya Sekondari Kongwa mkoani Dodoma Watazitapika.
 
Ndejembi amesema hayo Agosti 9,2019  alipofanya ziara shuleni  hapo kwa lengo la  kuangalia mwenendo wa  ujenzi wa Shule ya Sekondari Kongwa Dodoma   unaogharimu  zaidi ya  Tsh.Milioni 290 fedha zilizotolewa na Serikali.
 
Mkuu huyo wa wilaya ametaja miundombinu inayojengwa katika shule hiyo ni pamoja na mabweni mawili ambapo  kila moja lilitengewa  Tsh.Milioni 75 lakini hayatakamilika kutokana na fedha kuisha,Bwalo lilitengewa milioni 100 lakini nalo pia halitakamilika kutoka na kubaki mifuko ya saruji 40 pekee .
 
Hata hivyo, amebainisha kuwa kwa upande wa Madarasa yatakamilika kwa milioni 36 huku  fedha zilizobaki kwenye akaunti ni milioni 74  pekee ambazo hazitaweza kutosheleza katika ukamilishaji wa miundombinu yote na zilizobaki nje ya akaunti laki moja na nusu pekee.
 
Mhe.Ndejembi amesema sababu zilizosababisha majengo hayo kutokamilika licha kutengewa fedha nyingi ni kutokana na kutofuata maelekezo ya Serikali ya kutumia Force akaunti ambapo walitangaza tenda hali iliyosababisha ununuzi wa vifaa vya ujenzi kununuliwa kwa bei kubwa tofauti na ilivyo kawaida na ameshangazwa kwa maeneo mengine hapa nchini yamekamilika.
 
Hivyo Mkuu huyo wa wilaya ameagiza TAKUKURU kufuatilia bei ya Manunuzi ya Bidhaa hizo za Ujenzi ,milioni 74 zilizobaki kwenye akaunti zisitume mpaka uchunguzi ukamilike  na wale  wote waliohusika katika ubadhilifu huo wanachukuliwa hatua kwa kumdanganya  na kumdharau Rais,Waziri wa TAMISEMI pamoja na yeye.


Share:

Ujumbe Wa SADC Watembelea Viwanda Kikiwemo Kiwanda Kikubwa Cha Kuzalisha Malumalu Afrika Mashariki Na Kati

NA.Mwandishi Wetu-MAELEZO.
Wawakilishi wa Ujumbe wa SADC wametembelea viwanda Vitatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na Chalinze kikiwemo kiwanda kikubwa za kuzalisha malumalu(Tiles) kwa Afrika Mashariki na Kati cha KEDA. 
 
Akizungmza katika ziara hiyo Mwakilishi wa Ujumbe wa SADC,Genoveva Kilabuka, alisema kuwa ujumbe kutoka SADC umefurahishwa kuona Tanzania inasonga mbele kwenye utekelezaji wa ujenzi wa viwanda kwani ndiyo azma kubwa kwa nchi pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC.
 
Lengo kubwa la ziara hiyo ni kujifunza namna ya uzalishaji wa bidhaa kwa kutumia malighafi mbalimbali za ndani ili kuongeza thamani ya malighalifi hizo kwa kuchakata na kuzalisha bidhaa zilizobora kwa masoko ya ukanda wa Kusini mwa afrika hususani katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
 
“Kwa kweli tumefarijika kuona Tanzania ya Viwanda inasonga mbele sawasawa na mikakati yetu ya kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi za ndani, huu ni mkakati mkubwa wa nchi na SADC ambao unasisitiza ujenzi wa viwanda  ili kutengeneza ajira kwa vijana wengi, kwa hiyo tumeendana kabisa na kauli mbiu ya mwaka huu ya Wiki ya viwanda SADC, “ kwa hiyo viwanda hivi ni moja ya alama kubwa Nchini kwetu”, Alisema Genoveva.
 
Alisema kuwa katika kutekeleza mikakati ya kufanya  viwanda kuwa endelevu Jumuiya ya SADC ni muhimu kwa soko la bidhaa zinazozalishwa nchini, SADC inajikita zaidi kusisitiza ujenzi wa Viwanda na ikiwa Wilaya ya Bagamoyo ina takribani viwanda 65 vikiwemo viwanda vikubwa vilivyotembelewa na wajumbe kutoka SADC, viwanda hivyo ni Elven Agri, SAYONA na kiwanda kikubwa Afrika Mashariki na Kati cha kuzalisha Malumalu cha KEDA, na mkakati huo unalenga zaidi kuzalisha ajira kwa vijana wa nchi wanachama SADC.
 
Genoveva alitoa rai kwa wazalishaji wa viwanda nchini kuchangamkia Fursa zilizoko SADC ili kuweza kupanua masoko kwa bidhaa zao kwenye nchi mbalimbali zilizoko Ukanda huo wa Afrika, kwani shughuli za Jumuiya hiyo sasa zitahamia Tanzania ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa SADC kwa muda wa mwaka mmoja.
 
“Ni rai kwa wenye viwanda kama hiki cha KEDA kinachotoa ajira za moja kwa moja kwa watanzania 1,000, na ajira ambazo siyo za moja kwa moja 3,000, tumieni fursa hii ambayo Tanzania tutakuwa wenyeji wa Jumuiya ya SADC kwa muda wa Mwaka mmoja  ili kujitangaza na kupata soko, kwani shughuli nyingi za Jumuiya hii zitafanyika Tanzania”, Alisisitiza Genoveva.
 
Kwa Upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo, Kasrida Mgeni kuwa ni fursa kubwa kutembelewa na Ujumbe wa SADC kwani ujio wao utafungua mtandao mkubwa wa kujua masoko ya kupeleka bidhaa zao kwenye nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ya kusini mwa Afrika.
 
Mgeni alisema kuwa kati ya mikoa ambayo ina viwanda vingi, Mkoa wa Pwani moja wapo huko halmashauri ya Bagamoyo ikiwa na viwanda takribani 65 huku viwanda 6 vikiwa ni vikubwa na ugeni huo ulipata kutembelea viwanda vitatu vikiwemo Elven Agri, SAYONA na kiwanda cha kuzalisha  Malumalu cha KEDA.
 
“Ujumbe huu ni muhimu sana kwetu, na kama mnavyofahamu Mkoa wetu wa pwani una viwanda vingi na Wilaya yetu ya Bagamoyo tuna takribani viwanda 65,na  viwanda 6 kati ya hivyo ni vikubwa kwa hiyo ugeni huu utaweza kufungua Fursa ya kupata masoko kwa Nchi wanachama wa SADC”, Alisema Mgeni.
 
Mgeni alisema kuwa wawakilishi hao kutoka SADC, wataiwezesha Serikali, Wananchi pamoja na wawekezaji kupat fursa kubwa ya masoko na kutengeneza faida kubwa itakayowezesha ujenzi wa viwanda vingine na kutengeneza ajira kwa vijana nchini.
 
Naye Afisa Masoko kutoka kiwanda cha Alven Agri, Salumu Kabuluta alisema kuwa ugeni wa SADC katika kiwanda hicho siyo tu fursa kwa nchi bali utawezesha uzalishaji kuimarika na kuweza kutimiza kikamilifu ujenzi wa Tanzania ya Viwanda kama Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza kuwa na uchumi wa viwanda.
 
“Tukiendana na sera ya Serikali ambayo inataka Tanzania iwe na viwanda vingi na tukihusianisha na hii wiki ya viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika SADC, sisi kama kampuni ya kitanzania tuahakikisha zaidi suala la viwanda linafanikiwa na sasa nchi yetu inaenda kuwa wenyeji wa SADC kwa hiyo masoko ambayo yapo kwenye nchi hizi 15 tutaweza kuyafikia kwa kirahisi.
 
Alisema kuwa mpaka sasa bidhaa zao zimefika nchi hizo zikiwemo Zambia, Congo DRC, Malawi na Botswana na Mkutano wa SADC itakuwa ni kichocheo zaidi ya Bidhaa zao kuweza kuenda kwenye nchi hizo 15 ili kukuza masoko ambayo hapo awali hayakuwepo.
Mwisho.


Share:

Rais Magufuli atoa salamu za rambirambi kufuatia vifo vya ajali ya lori la mafuta Morogoro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu zaidi ya 60 na majeruhi takribani 70 walioungua kwa moto baada ya lori lililokuwa na shehena ya mafuta kupata ajali na kisha kulipuka moto Mjini Morogoro.

Ajali hiyo imetokea leo tarehe 10 Agosti, 2019 majira ya saa 2 asubuhi ambapo lori hilo lililokuwa linatoka Dar es Salaam limepinduka jirani na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu baada ya dereva wa lori kumkwepa mwendesha pikipiki na kisha mafuta yaliyokuwa yakimwagika kushika moto na kuunguza watu waliokuwa wanayachota.

Mhe. Rais Magufuli ametoa pole kwa familia, ndugu, marafiki na wote waliopoteza jamaa zao katika ajali hii na pia amewaombea majeruhi wapone haraka.

“Nimeumia sana kusikia idadi kubwa ya Watanzania wenzetu waliopoteza maisha katika ajali hii, natoa pole kwa wote walioguswa na vifo hivi hasa familia za Marehemu wote, nawaombea Marehemu wapumzike mahali pema peponi na majeruhi wote wapone haraka” amesema Mhe. Rais Magufuli na kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe kufikisha salamu zake za pole kwa familia na wote walioguswa na vifo hivyo.

Mhe. Rais Magufuli ameagiza Wizara zote zinazohusika kushughulikia ajali hii na ametaka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhakikisha majeruhi wote wanapatiwa matibabu ili kuokoa Maisha yao.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo vya watu kuvamia magari yanayopata ajali kwa lengo la kujipatia bidhaa mbalimbali zilizobebwa na magari hayo na ametaka vitendo hivyo vikome.

“Baadhi ya magari haya yanabeba mafuta ambayo ni hatari kama ilivyotokea Morogoro, yapo magari yanabeba kemikali za sumu, yapo magari yanabeba milipuko nakadhalika, nawaomba sana tuache tabia hii” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Agosti, 2019


Share:

TAASISI YA TIA KUBORESHWA KUENDANA NA MPANGO WA MIAKA MITANO


Mhadhiri wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Bw. Burkadi Haule, akitoa ufafanuzi wa ramani ya majengo ya taasisi hiyo, katika maeneo mbalimbali nchini, kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, wakati wa ziara ya kutathimini utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2018/19, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, akieleza nia ya Wizara ya Fedha na Mipango ya kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania-TIA, ili kwenda sambamba na lengo la Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya TIA, Bi. Luciana Hembe (kushoto) na Mhadhiri wa taasisi hiyo, Bw. Burkadi Haule, wakisikiliza maagizo ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani), katika Taasisi ya TIA, jijini Dar es Salaam
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania- TIA- jijini Dar es Salaam wakisikiliza maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani),  kuhusu kufanya kazi kwa weledi na maadili kwa ajili ya maendeleo ya Taifa .
Mtaalam wa masuala ya Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Msabaha Msabaha, akihoji kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2018/19 na changamoto zake, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani), katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania- TIA- jijini Dar es Salaam.
Moja ya ramani ya majengo ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania- TIA, ambayo yanatakiwa kujengwa ili kuwezesha upatikanaji wa wahasibu wakutosha kulingana na mpango wa maendeleo wa miaka mitano.
(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)Na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam
Serikali imeahidi kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) ili kuongeza udahili wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na  kupatikana kwa wahasibu wa kutosha kama mpango wa Taifa wa miaka mitano ulivyoelekeza.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipang,o Dkt. Khatibu Kazungu, wakati wa ziara yake ya kikazi katika taasisi hiyo iliyochini ya Wizara ya  Fedha na Mipango  kubaini changamoto za utekelezaji wa Bajeti ya taasisi hiyo kwa mwaka 2018/19.
Dkt. Kazungu alisema kuwa Taasisi ya TIA inakabiliwa na changamoto kubwa ya ufinyu wa bajeti jambo lililosababisha baadhi ya miundombinu yake kutokamilika kwa wakati na hivyo kupunguza kiwango cha udahili wa wanafunzi.
“Lengo la Mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano ni pamoja na taifa kuzalisha wahasibu wa kutosha ili kuleta chachu katika maendeleo ya uchumi na nyanja zingine za maendeleo, malengo yanayotegemewa kwa kuimarishwa kwa miundombinu ya taasisi hii”, alieleza Dkt. Kazungu
Alisema kuwa miundombinu inayoangaziwa kwa mwaka huu wa fedha ni pamoja na Mabweni ya wanafunzi, vyumba vya madarasa na ofisi za watumishi, aidha kuangalia uwezekano wa kuongeza wahadhiri kulingana na kozi zinazotolewa jambo litakalokwenda sambamba na ongezeko la wanafunzi.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji wa Taasisi ya TIA Bi. Luciana Hembe, alieleza  kuwa, hatua ya viongozi wa juu kutembelea taasisi wanazoziongoza na kuona uhalisia wa mambo, unaongeza morali ya kiutendaji ya watumishi kwa kuwa hutatua changamoto nyingi hususani za kibajeti.
Alisema kuwa Taasisi ya TIA imejipanga kikamilifu kuhakikisha wahitimu wake wanakuwa na weledi wa kutosha katika kuhimili ushindani wa soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Mwisho.
Share:

Utupaji Holela wa Taka Kudhibitwa

Na Lulu Mussa,Mwanza
Serikali imezitaka halmashauri zote nchini, kutenga maeneo maalumu mbali na makazi ya watu yatakayotumika kujenga madampo ya kisasa ili kuzingatia hifadhi ya mazingira.
 
Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa dampo la kisasa linalojengwa eneo la Buhongwa Jijini Mwanza.
 
Alisema ujenzi wa huo wa dampo la kisasa utasaidia juhudi za Serikali za kutotumia fedha nyingi kwenye ununuzi wa vifaa tiba kwa kuwa taka zitakazolishwa katika Jiji la Mwanza zitapelekwa dampo kwa wakati na kunusuru magonjwa ya mlipuko.

“Huwezi kutenganisha afya na mazingira, mradi huu ni mkubwa sana na kwa namna utakavyotekelezwa hatutaraji kuona taka mjini zinazagaa.Tunatarajia kuona taka zote zinakuja hapa,” alisema Sima.

“Natoa rai kwa halmashuri zingine ambazo zinatekeleza miradi ya kimkakati kutoa kipaumbele kwa ujenzi wa madampo ya kisasa”.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba alisema dampo hilo lina ukubwa wa hekta 34 na linatarajia kukamilika desemba mwaka huu na kwa sasa ujenzi upo asilimia 78 ukigharimu Sh bilioni 16.6, ukienda sambamba na ujenzi wa barabara.

“Dampo hilo litakuwa na chemba sita za kuhifadhi taka na mabwawa ya kuhifadhi maji taka, barabara za kisasa zenye urefu wa kilomita 1.9, taa za nishati ya jua na maabara maalumu ya kupima maji taka” Kibamba alisema

Kukamilika kwa dampo hilo la kisasa litakuwa na uwezo wa kuteketeza taka mara baada ya kufikishwa kwenye eneo hilo na,litaongeza  mapato katika jiji hilo

Kwa mujibu wa Kibamba, tani 33 hadi 36 zinatarajia kupelekwa katika dampo hilo mara baada ya ujenzi kukamilika na linatarajia kudumu kwa zaidi ya miaka 15


Share:

RPC Morogoro Kasema Zaidi ya Watu 56 Wamefariki Dunia Katika Ajali ya Lori Lililowaka Moto

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema karibu watu 56 wamepoteza maisha baada ya lori la mafuta ya petroli kupinduka eneo la Msamvu mkoani Morogoro na kuwaka moto

Ajali hiyo imetokea leo Jumamosi August 10, 2019  umbali wa mita 200 kutoka kituo kikuu cha mabasi Msamvu ukitokea Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa , baada ya lori hilo kupinduka, watu walianza  kujazana  wakigombania kuchota mafuta ambapo mmoja wa waliokuwa wakichota mafuta hayo alianza kuvuta betri ya gari na ikawa ndo chanzo cha moto kulipuka


Share:

SBL YAZINDUA KAMPENI YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA ,KUOTESHA MITI 1000 KILIMANJARO

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Sara Cooke akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti  alipotembelea Kiwanda cha Bia cha Serengeti cha Moshi mkoani Kilimanjaro,katikati ni Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha Biashara ,Andrew Rosendell.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mark Ocitti akiwaongoza wageni wake ,Balozi wa Uingereza nchini Tanzania ,Sara Cooke na Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha Biashara ,Andrew Rosindell walipotembelea kiwanda cha Bia cha Serengeti Moshi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mark Ocitti  (wa pili kushoto) akiwa na wageni wake ,Balozi wa Uingereza nchini Tanzania ,Sara Cooke (wa kwanza kulia) na Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha Biashara ,Andrew Rosindell wakijiandaa kuotesha miti katika kiwanda cha Bia cha Serengeti -Moshi.
Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha Biashara ,Andrew Rosindell  akizungumza wakati wa zoezi la kuotesha miti katika kiwanda cha Bia cha Serengeti ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa kuotesha miti katika mkoa wa Kilimanjaro .
Balozi wa Ungereza nchini Tanzania ,Sara Cooke akiotesha mti katika kiwanda cha Bia cha Serengeti mjini Moshi .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti ,Mark Ocitti akimwagia maji mti alioutosha katika kiwanda cha Bia cha Serengeti cha mjini Moshi ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuotesha miti 1000 katika mkoa wa Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mark Ocitti  (kulia )akiwa na wageni wake ,Balozi wa Uingereza nchini Tanzania ,Sara Cooke (kushoto)  na Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha Biashara ,Andrew Rosindell(katikati) 

Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV

KATIKA kukabiliana na uharibufu wa Mazingira pamoja na mabadiliko ya tabia nchi Kampuni ya Bia ya Seerengeti (SBL) kwa kushirikiana na taasisi ya The Kilimanjaro Project wamezindua kampuni ya kuotesha miti 1000 kwa mkoa wa Kilimanjaro.


Zoezi la uoteshaji miti linakuja huku kukiwa na wito kutoka jumuiya ya kimaitafifa juu ya kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa kuongeza juhudi za uhifadhi wa misitu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuweka mazingira katika hali ya usalama kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Akizungumza mara baada ya zoezi la kuotesha miti katika kiwanda cha SBL kilichopo Pasua katika wilaya ya Moshi ,Mkurugenzi Mtendaji wa SBL ,Mark Ocitti amesema SBL imeamua kuongeza jitihada za uhifadhi wa mazingira sit u katika maeneo yaliyo chini ya SBL bali katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

“Huu ni uthibitisho tosha kwamba SBL imejidhatiti na iko tayari kushirikiana na wadau wengine katika kutekeleza miradi yenye kuleta tija kwa jamii zetu”alisema Ocitti.

Zoezi la uoteshaji miti limehudhuriwa na ujumbe kutoka British High Commission akiwemo Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha Biashara Andrew Rosindell pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania  Sara Cooke waliotembea kiwanda cha Bia cha Serengeti Moshi .

Mpango wa SBL unaenda sambamba na sera ya kampuni hiyo katika kurudisha kwa jamii sehemu ya faida na umejikita zaidi katik autoaji wa huduma bora ya maji safi kupitia mradi uitwao Water of Life (WOL) .
 
Mpango mwingine ilionao SBL ni pamoja na kuwasaidia wanafunzi kupata ufadhili wa masomo ya elimu ya juu,kuwasaidia wakulima wa ndani husuani wa vijijini pamoja na mpango wa kuhamasisha unywaji pombe kistaarabu.

Mwisho .
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger