Monday, 27 May 2019

Rais Magufuli Apokelewa Na Mwenyeji Wake, Rais Hage Geingob Wa Namibia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa na Mwenyeji wake Rais Hage Geingob wa Namibia alipowasili katika Ikulu ya nchi hiyo, Jijini Windhoek leo Mei 27, 2019. Rais Dkt. Magufuli amewasili nchini Namibia kwa Ziara Rasmi ya Kikazi ya Siku
mbili.



Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521


Share:

Kesi ya Shamim Mwasha na mumewe Yapigwa Kalenda

Upelelezi wa Kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride   inayomkabili  mmiliki wa Blog 8020 Fashion, Shamim Mwasha (41) na mumewe, Abdul Nsembo(45) bado haujakamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Mkazi, Kelvin Mhina kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika, hivyo anaomba ahirisho.

Baada ya kueleza hayo Wakili utetezi, Charles Kisoka amedai kuwa shauri hilo halina dhamana hivyo wanauonba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.

Wakili Wankyo ameeleza kuwa amesikia kilichozunguzwa na upande wa utetezi, hivyo watawahimiza wenzao wa upelelezi wafanye haraka na tarehe ijayo wataeleza upelelezi ulipofikia.

Hakimu Kelvin Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi June 10, 2019, washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu kesi yao haina dhamana.

Washtakiwa hao wanatuhumiwa kusafirisha dawa hizo za kulevya, Mei 1,2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini  Dar es Salaam kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.


Share:

BINTI HUYU NI MGONJWA ANAHITAJI MSAADA WAKO... HANA PESA ZA MATIBABU


Happiness Stephen ambaye ni mkazi wa mtaa wa Busulwa kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga anaomba msaada wa matibabu kwa mtoto wake aitwaye Rogathe Cyprian Makala mwenye umri wa miaka 18, ambaye anayesumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa ngozi kwa muda wa miaka 16 sasa.
Anasema amehanghaika katika hospitali mbalimbali hapa nchini, lakini siku moja alikutana na Daktari Bingwa kutoka Apolo India katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ndipo akampima na kumgundua kuwa homoni zake ziko kwenye njia ya mkojo, hivyo anatakiwa apatiwe matibabu ndani ya miezi tisa kwa kupatiwa dawa kutoka India, ambapo kila mwezi inatakiwa shilingi 504,000 ambapo kwa miezi hiyo tisa ni sawa na shilingi milioni 4,536,000.

Kwa mujibu wa Daktari huyo,binti  huyo akifikisha umri wa miaka 20 ugonjwa huo wa ngozi utaweza kugeuka na kuwa kansa, na ataweza pia kuwa anazaa watoto wenye kisukari, na kichwa kikubwa na hata kuambukiza watu wengine kwa njia ya kuchangia choo.

Daktari huyo huwa anakuja kila baada ya mwezi hapa mkoani Shinyanga ambapo dozi ya dawa hiyo anatakiwa aanze Juni 2 mwaka huu ambapo itakuja na daktari huyo.

Mama wa binti huyo anasema yeye hana uwezo wa kumtibu binti yake, mume wake alishafariki kwenye ajali mwaka (2007) ambaye alikuwa Mhasibu wa shirika la umeme TANESCO mkoani Shinyanga.

Mama wa mtoto anasema mwanae huwa halali usiku kucha anashinda anajikuna tu na hata wakati wa jua kali huku vipele vikimtoka mwili mzima, na anatarajia kujiunga na kidato cha tano kwani amefaulu kidato cha nne.

Kwa yeyote atakayeguswa kumsaidia awasiliane kwa namba zifuatazo:

Vodacom : 0764206669 ukitaka kutuma kwa m-pesa jina litasoma Happines Makala

Halotel: 0626845953 jina litasoma Eliud Makala
Happines Stephen Makala (kushoto) akiwa na mtoto wake Rogathe Cyprian Makala (18) ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi na kuomba msaada wa matibabu.
Msichana Rogathe Cyprian Makala akionyesha namna ugonjwa huo wa ngozi unavyomsumbua na kutoka vipele mwili mzima na hawezi kulala usiku akishinda ana jikuna na kuomba msaada wa fedha za matibabu shilingi milioni 4.5
Kwa yeyote atakayeguswa kumsaidia awasiliane kwa namba zifuatazo: 

Vodacom : 0764206669 ukitaka kutuma kwa m-pesa jina litasoma Happines Makala

Halotel: 0626845953 jina litasoma Eliud Makala
Share:

Video Mpya : BHUDAGALA NG'WANA MALONJA - PESA


Hii hapa video mpya ya Bhudagala Ng'wana Malonja inaitwa Pesa

Share:

ZAMALEK WATWAA TAJI LA KWANZA AFRIKA TANGU WAVULIWE UBINGWA NA SIMBA 2003

TIMU ya Zamalek ya Misiri imefanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa penalti 5-3 kufuatia sare ya jumla ya 1-1 dhidi ya Renaissance Sportive Berkane, maarufu kama RSB Berkane usiku wa jana Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.

Bao pekee la penalti la beki Mmisri, Mahmoud Alaa Eldin dakika ya 55 liliipa Zamalek ushindi wa 1-0 ndani ya dakika 120 za mchezo wa jana Misri.

Na kufuatia RSB Berkane kushinda 1-0 pia, bao pekee la mshambuliaji Mtogo, Fo-Doh Kodjo Laba dakika ya 90 na ushei akimalizia pasi ya Hamdi Laachir liliipa RSB Berkane Uwanja wa Manispaaa ya Berkane Mei 20 mchezo ukahamia kwenye mikwaju ya penalti.

Zamalek ilipata penalti zake zote kupitia kwa nyota wake, Mmorocco mzaliwa wa Ufaransa, Khalid Boutaib, Mahmoud Alaa, Abdallah Gomaa, Youssef Obama na Ahmed Sayed ‘Zizo’. 
Lakini Hamdi Laachir akakosa penlati ya kwanza ya Berkane, wakati Ismail Mokadem, Mtoto Fo-Doh Kodjo Laba na Mburkina Faso, Issoufou Dayo walifunga.
Jana ilikuwa mara ya nne katika fainali 16, mikwaju ya penalti inaamua mshindi wa taji hilo, timu nyingine zilizowahi kutwaa Kombe hilo kwa matuta ni Hearts of Oak ya Ghana, Stade Malien ya Mali na MAS Fes ya Morocco.

Ushindi huo unamaliza ukame wa mataji ya Afrika wa miaka 16 kwa Zamalek mara ya mwisho wakishinda mwaka 2003 taji la Ligi ya Mabingwa ambalo walivuliwa na Simba SC ya Tanzania.

Wapinzani wao wa Jiji la Cairo, Al Ahly wanaongoza kwa kutwaa mataji mengi Afrika, 19 wakifuatiwa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mataji 11.

Kwa ushindi huo, Zamalek watapatiwa dola za Kimarekani Milioni 1.25, huku Berkane wakiambulia dola 625,000. 

'The White Knights' sasa watamjua mpinzani wao kwenye kuwania taji la Super Cup ya CAF 2019 wiki ijayo wakati Esperance ya Tunisia itakapomenyana na Wydad Athletic ya Morocco kufuatia kutoa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza mjini Rabat.
Share:

WAZIRI MKUCHIKA AZINDUA KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF


Waziri Mkuchika akimkabidhi zawadi ya saa yenye picha za
wajumbe wa kamati ya uongozi ya TASAF iliyomaliza muda wake Dr. Florens Turuka,wa kwanza kulia ni mwenyekiti mpya Dr. Moses Kusiluka na kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw.Ladislaus Mwamanga. 
Waziri Mkuchika akizindua Kamati ya taifa ya Uongozi ya TASAF katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Mfuko huo jijini Dar es salaam, kulia kwake ni mwenyekiti mpya wa Kamati Dr. Moses Kusiluka akifuatiwa na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dr. Florens Turuka . Kushoto kwa Mhe. Mkuchika ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga.
Waziri Mkuchika (aliyeketi katikati) katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati mpya ya uongozi ya TASAF na menejimenti ya Mfuko huob aada ya kuizindua Kulia kwake ni mwenyekiti mpya wa kamati hiyo Dr. Moses Kusiluka na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga. 
Waziri Mkuchika (aliyeketi katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya TASAF waliomaliza muda wao baada ya kuzindua rasmi kamati Mpya kwenye Ofisi ndogo ya TASAF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya menejimenti ya TASAF wakimsikiliza Waziri Mkuchika wakati wa uzindizi wa Kamati ya Taifa mpya kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo za Mfuko
huo jijini Dar es Salaam. 
Waziri Mkuchika (wa pili kushoto) akizungumza na Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uongozi ya TASAF, Dr. Moses Kusiluka (kulia )na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dr. Florens Turuka) wa kwanza kulia ,na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga (kushoto ) baada ya kuzindua kamati ya taifa ya uongozi ya TASAF jijini Dar es Salaam.

***
NA ESTOM SANGA-DSM 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteini Mstaafu George Huruma Mkuchika (MB) amezindua Kamati yaTaifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF na kuagiza kamati hiyo kuendelea kutilia mkazo suala la utendaji kazi kwa kuzingatia misingi ya uadilifu na uwajibikaji. 

Akizindua Kamati hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya TASAF jijini Dar es Salaam, Mhe. Mkuchika amesema Mfuko huo umetekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kujenga jina zuri na hivyo ameagiza sifa hiyo iendelezwe kwa maslahi ya taifa. 

Amesema majukumu ambayo TASAF imekabidhiwa yanagusa kwa kiwango kikubwa maisha ya wananchi ambao wanakabiliwa na umaskini na hivyo kutaka Kamati hiyo mpya ya Uongozi ya TASAF kushirikiana na watumishi wa Mfuko huo kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla. 

“mnalo jukumu kubwa mlilokabidhiwa na taifa la kusaidia serikali kupambana na adha ya umaskini na kuboresha maisha ya wananchi,jukumu ambalo ni lazima litekelezwe kwa nguvu na ufanisi zaidi”, amesisitiza Mhe. Mkuchika. 

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa kamati ya taifa ya Uongozi iliyomaliza muda wake Dr. Florens Turuka akizungumza kwenye hafla hiyo amepongeza hatua ya serikali ya kuendelea kuuamini Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kama njia mojawapo ya kuhamasisha wananchi kupambana na umaskini,na kuwapongeza Watumishi wa Mfuko huo kwa kufanyakazi kwa kujituma kwa manufaa ya taifa. 

Naye Mwenyekiti Mpya wa Kamati ya taifa ya Uongozi ya TASAF ,Dr. Moses Kusiluka amesema msingi imara uliowekwa na kamati iliyomaliza muda wake utaendelezwa kwa nguvu zaidi ili kukidhi matakwa ya serikali na wananchi wanaotegemea huduma za Mfuko huo unaogusa maisha ya wananchi wengi. 

Dr. Kusiluka pia ametumia fursa hiyo kuagiza uongozi wa TASAF na watumishi wake kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili mfuko huo unaohudumia wananchi wanaokabiliwa na kero ya umaskini waendelee kunufaika na huduma za Serikali kupitia Mfuko huo. 

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF ,bw Ladislaus Mwamanga , ameelezea mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa mfuko huo mwaka 2000 hususani katika sekta za elimu, afya, maji, miundobinu , kilimo,mifugo, uchumi na mapambano dhidi ya umaskini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao amesema umefanikiwa kuhudumia zaidi ya kaya milioni Moja na Laki Moja katika awamu yake ya kwanza ya utekelezaji kwa aslimia 70 ya mitaa/vijiji na shehia nchini kote.
Share:

Waziri Mkuu Awaonya Wamiliki Wa Vituo Vya Kulelea Watoto Yatima

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaonya baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa makao ya watoto wasiofuata taratibu za usajili wa watoto, wanaowatumia watoto kama mitaji au kwa maslahi binafsi na wanaoendesha makao hayo kwa minajili ya kidini na kikabila.

Amewataka pia wamiliki hao waache mara moja kuwalea watoto hao katika maadili yasiyofaa na yasiyo ya Kitanzania na kwamba maofisa ustawi wa jamii wahusike moja kwa moja katika usajili wa mtoto ili kuhakikisha kuwa ni watoto wanaostahili tu kuwekwa kwenye makao ndiyo wanasajiliwa.

Alikuwa akizungumza jana usiku (Jumapili, Mei 26, 2019) kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam alikokuwa mgeni wa heshima wakati wa futari ya pamoja na watoto yatima kutoka kwenye vituo sita vya kulea watoto yatima vya jijini humo.

“Nitoe rai kwamba watu mmoja mmoja, taasisi na makao wazingatie baadhi ya taratibu za msingi za uendeshaji wa makao kama vile mtoto kukuzwa katika mazingira ya familia, kuzingatia misingi ya kitaifa badala ya misingi ya tamaduni za kigeni.

“Mtoto kukuzwa kwa kuzingatia maslahi bora ya mtoto; kuzingatia umuhimu wa kuwa na mwendelezo katika dini ya mtoto na utamuduni wake; kutotenganisha watoto na ndugu na kuhakikisha watoto wote wanapata huduma stahiki, kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji; na kutunzwa na  kuendelezwa hadi kufikia kimo cha utimilifu wao,” alisema.

Waziri Mkuu alitumia hadhara hiyo pia kutoa maelekezo mahsusi kwa waendeshaji wa makao pamoja na wasimamizi wa sheria na taratibu za uendeshaji wa makao ya watoto yatima.

“Afisa Ustawi wa Jamii katika eneo yanakoanzishwa makao, ahusike moja kwa moja katika usajili wa mtoto ili kuhakikisha kuwa ni watoto wanaostahili tu kuwekwa kwenye makao ndio wanasajiliwa.

“Taasisi na makao zihakikishe kuwa kila mtoto anawekewa mpango maalumu wa kuondoka kwenye makao na namna ya kumuunganisha mtoto huyo na familia yake.

“Wamiliki wa taasisi na makao, waruhusuni maafisa ustawi wa jamii na maafisa wengine wa Serikali wafanye ukaguzi kwa mujibu wa sheria na wekeni utaratibu wa kuandaa taarifa za kila mwezi za watoto na taarifa ya mwaka wa fedha,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu pia alionya dhidi ya wale “wanaowabadili watoto dini kinyume cha sheria; wanaofanya vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto; wasiowaruhusu watendaji wa Serikali kufanya ufuatiliaji na usimamizi; wasioandaa mpango wa kuwaunganisha watoto na familia zao na hivyo, kusababisha watoto kukaa kwa muda mrefu kwenye makao na wale wote wanaondesha makao bila kuwa na leseni ya uendeshaji.”

Alisema Serikali haitowafumbia macho watu wa namna hiyo, na mara tu watakapogundulika kuanzisha au kuendesha makao bila kufuata taratibu, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Alisema tangu mwaka 2016 hadi sasa, kuna jumla ya watoto 24,067 wanaolelewa katika makao yaliyosajiliwa nchini yakiwemo makao 140 yanayoendeshwa na kumilikiwa na watu au taasisi binafsi. Kati yao wavulana ni 11,925 na wasichana ni 12,142.

Alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaratibu upatikanaji wa huduma za msingi kwenye makao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na kuwezesha upatikanaji wa Bima ya Afya kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi. “Hadi sasa, watoto 900 kutoka Dar es Salaam, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha wamepatiwa kadi hizo na zoezi hilo linaendelea,” alisema.

Waziri Mkuu alisema Serikali itaendelea kusimamia na kufuatilia kwa karibu uendeshaji wa makao ya watoto sambamba na kutoa elimu kuhusu malezi, makuzi, haki, ulinzi na usalama wa mtoto kwa mujibu wa sheria zinazosimamia haki na ustawi wa mtoto.

Mapema, akielezea azma ya kuandaa futari hiyo, Mkurugenzi wa Chocolate Princess na mwandaaji wa kipindi cha televisheni maarufu cha The Mboni Talk Show, Bi. Mboni Masimba alisema jumla ya watoto yatima 325 walikuwa wamealikwa kushiriki futari hiyo.

Watoto hao wanatoka vituo vya Ijango Zaida Orphanage Centre kilichopo Sinza, Alzama Orphanage Centre (Mbagala), Ashura Foundation (Vingunguti), Madina Orphanage Centre (Tandale), Hiyari Orphanage Centre (Mbagala) na Hisani Orphanage Centre (Mwasonga).

Futari hiyo iliandaliwa na Mboni Masimba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Asure Yetim Vafki, United Bank of Africa (UBA), Junaco, Mo Dewji Foundation, Lake Oil, ASAS, AZAM, Uncle K Catering, Zurii, Simply Special Decor na State Oil na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo Balozi wa Uturuki nchini, Bw. Ali DavutoÄŸlu, Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Taifa, Sheikh Issa Othman, masheikh, maimamu wa misikiti na viongozi wa taasisi zinazojihusisha na malezi ya watoto yatima.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,



Share:

Askari Magereza anaswa kwa utapeli Mwanza

Polisi  jijini Mwanza imemkamata askari magereza Kibemba Warioba (27) mwenye namba za usajili B.9205 WDR, akiwa na simu tano za aina tofauti na mitandao tofauti akijihusisha na makosa ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi saa nne na nusu asubuhi, ambapo polisi wa mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi la Mkoa wa Kagera walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa anafanya kazi wilayani Biharamulo mkoani Kagera na tayari amesimamishwa kazi kwa hatua zaidi za kisheria.

Kamanda Muliro alisema polisi walimbaini mtuhumiwa huyo akitumia njia ya mitandao hiyo ya simu ambapo alianzisha Saccos ‘Bandia,’ iliyojulikana kwa jina la Info Tell CCM, akilenga kuwatapeli wanachama wa CCM na wengine katika mikoa ya Mara na Kagera.

Alitoa onyo kwa wananchi wenye tabia ya kufanya vitendo hivyo vya uhalifu waache mara moja kwa kuwa ni kinyume cha sheria.


Share:

DC Nyimbi Afagiria Umahiri Wa Serikali Ya Magufuli Katika Kutekeleza Miradi Ya Maendeleo

Na  Amiri kilagalila
Kaimu mkuu wa mkoa Mwanza Dkt. Philis Nyimbi ambaye pia ni mkuu wa Wilaya Nyamagana amefagiria serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna ilivyoonesha umahiri mkubwa wa kuibua miradi inayotatua changamoto za watu wote katika nyanja ya elimu, afya, miundombinu ya barabara, anga, reli, bandari,  kilimo na mifugo.

Dkt. Nyimbi amebainisha hayo akifunga kongamano la  kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu tano katika miaka minne mkoani  Mwanza. 

Ambapo amepongeza umahiri wa uwasilishaji wa mada mbali mbali zilizotolewa katika kongamano, umakini  wa ichangiaji Mada kwa  washiriki wote. Dkt. Nyimbi akihitimisha kwa kuomba waandaji wa kongamano hilo taasis ya Sautu ya Jamii Tanzania mwaka ujao kuuongeza mada itakayo pima mafanikio kwa kuakisi usawa wa kijinsia.

Akitoa salamu za Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana, Bi Florah Magabe amepongeza umahiri wa uongozi wa Magufuli kwa kutekeleza ahadi zote alizozitoa katika Ilani yake ya Uchaguzi kwa zaidi ya 75%. 

Kadharika amesifia uongozi huu umewezesha wilaya ya Nyamagana kupata ongezeko ya 100% ya madawa na vifaa tiba, ujenzi wa Zahanati tano mpya pamoja na kituo cha afya chenye hadhi ya hospitali ya wilaya.

Bi. Magabe ameomba mwaka ujao kongamano hilo lifanyike wazi kuongeza idadi ya washiriki maana uongozi wa   Magufuli kwa kushirikiana na Mhe. Mabula wilayani Nyamgana serikali imewezesha  ujenzi wa madaraja mawili ambayo yalijengw enzi za ukoloni zitakazo unganisha wilaya ya Magu, Kwimba na Misungwi. 

Kadharika amefafanua namna ambavyo Nyamagana imejidhatiti kutatua uhaba wa maji kwa miaka 20 ijayo kwa serikali kwa kutoa fedha kwa miradi mikubwa ya miwili ya maji,  ujenzi wa barabara zote za mjini kwa kiwango cha rami pamoja na kujenga barabara za moramu na mawe.

Kongamano hilo la pili kufanyika kitaifa limeandaliwa ba taasis ya Sauti ya Jamii Tanzania na kuwakutanisha wadau wa maendeleo ambapo mada mbali zilitolewa ba TAKUKURU, TRA, NIDA, Taasis za fedha, Wanazuoni pamoja na mfuko wa Pembejeo.


Share:

RC Olesendeka aridhishwa na ukamilishwaji wa kituo kipya cha mabasi Njombe

Na Amiri kilagalila-Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amefanya ukaguzi katika kituo kituo kipya cha mabasi kitakachogharimu zaidi ya bil 9.6 Hadi Kukamilika Kwake pamoja na ujenzi wa mradi wa soko kuu mjini Njombe lenye hadhi ya kimataifa litalogharimu bil 9.3 na kuonyesha kuridhishwa na mwenendo wa ukamilishaji wa miradi hiyo inayofadhiliwa na benk ya dunia.

Pamoja na kuridhishwa na ujenzi unaoendelea akiwa katika kituo cha mabasi ambacho kilianza kufanya kazi Mei  11 kwa agizo la rais ,mkuu wa mkoa amepokea malalamiko kutoka kwa abiria,machinga,mama na baba lishe ambao wanasema wanashindwa kufanya biashara kama ilivyokuwa awali katika stendi ya zamani kwani halmashauri imezuia kufanya biashara ndani ya stendi hata kwa wenye vitambulisho vya mjasiriamali.

"Unapotoka toka pale ile lisiti waliyonipa wanachana natoka tena kuchukua abiria ninavyoingia nalipa tena mia mbili sasa kuanzia saa kumi na mbili ile asubuhi mpaka saa moja jioni ninakuwa nimelipa shilingi ngapi,lakini humu ndani hakuna mboga wala cha nini kuna mwingine anahitaji mboga mfano samaki aende nazo kijijini hamna haya chungwa hamna" walisema baadhi ya wajasiriamali ndani yastendi

Mara baada ya kusikiliza kero hizo Christopher Olesendeka anawataka Wajasiliamali Hao Kuvuta Subira Wakati Yakiwekwa Sawa Mazingira Ya Wao Kufanya Biashara Ndani ya Stendi Hiyo Baada ya Ujenzi Wake Kukamilika.

"Nataka niwahakikishieni mheshimiwa Rais ametoa fedha kwa ajili ya stendi hii na akaelekeza kituo hiki cha mabasi kikamilike haraka ili ninyi kina baba lishe na mama lishe muweze kufanya biashara katika maeneo mazuri zaidi,tunaendelea kukagua kuonamaeneo yaliyobaki ili stendi ikamilike vizuri halafu tuendelee kuungana na halmashauri yenu tuweke utaratibu rafiki ili kuona wanyonge wa Njombe ndio watakaonufaika na vibanda vilivyoko stendi na uendeshaji wabiashara katika eneo hili''

Katika hatua nyingine Olesendeka amekagua ujenzi wa soko kuu ambao Ameonyesha kuridhishwa na kasi na ubora katika ujenzi Huo  huku Mhandisi wa mradi huo Mboka Justin akidai mradi umefika asilimia 60 na kuahidi kukamilika ndani ya muda uliopangwa.


Share:

Auawa kwenye sherehe akigombea mwanamke

Mkazi  wa Mtaa wa Tagota Halmashauri ya mji Tarime mkoani Mara, Muniko Kinyunyi (30) amekufa kwa kuchomwa na kisu shingoni baada ya kutokea ugomvi na mwenzake ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.

Wawili hao wanadaiwa kuwa walikuwa wakigombea mwanamke katika sherehe iliyofanyika nyumbani kwa aliyekuwa mgombea ubunge mwaka 2015 Jimbo la Tarime Mjini, Michael Kembaki.

Kwa mujibu wa diwani wa Kenyamanyori, Ganga Mgendi tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa kuamkia jana nyumbani kwa Kembaki Tarime mjini.

Kembaki katika uchaguzi huo wa mwaka 2015 aliwania nafasi hiyo ya ubunge Tarime Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuangushwa na mbunge wa sasa, Esther Matiko (Chadema).

Mgendi alisema tukio hilo lilitokea wakati wa sherehe iliyofanyika nyumbani kwa mwanasiasa huyo aliyetembelewa na dada yake aliyekwenda na kikundi cha watu kuwasalimia mama na ndugu zake.

Alisema katika shamrashamra hizo ndipo kulipoibuka ugomvi kati ya Mniko na mtu ambaye hakufahamika mara moja jina lake wakigombea mwanamke hali iliyosababisha mtu huyo kumchoma Mniko kisu shingoni karibu na kifuani na kisha kutoroka wakati watu wakihangaika kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya Tarime ambapo alifariki kabla ya kupatiwa matibabu kutokana na kutokwa damu nyingi.

Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, Henry Mwaibambe alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji na kueleza kuwa Jeshi la Polisi linamsaka mtuhumiwa na kuwaomba raia wema kutoa ushirikiano ili kuweza kumkamta mtuhumiwa huyo aliyetoroka.

Credit: Habarileo


Share:

LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka Bungeni Dodoma

LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka Bungeni Dodoma


Share:

Vikosi Maalum Vikiongozwa Na Kamishna Operesheni Na Mafunzo Ya Jeshi La Polisi CP Liberatus Sabas, Wafanya Operesheni Mapango Ya Amboni Mkoani Tanga.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi La Polisi CP Liberatus Sabas, ameongoza Vikosi Maalum ya Kupambana na Uhalifu katika Operesheni iliyofanyika maeneo yote ya Mapango ya Amboni Jijini Tanga juzi baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kumeonekana baadhi ya watu wasiofahamika na baadhi yao ni wahalifu waliokuwepo kipindi cha nyuma ambao wengi wao walishakaatwa na Jeshi la Polisi na mwisho amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na taarifa katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama. (Picha na Jeshi la Polisi).



Share:

Wamiliki Tanzanite Wapewa Miezi Sita Kuboresha Miundombinu

Ofisa madini Mkazi wa Mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima amewapa miezi sita wamiliki na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani, kuboresha miundombinu ya migodi yao la sivyo itafutiwa leseni.

Ntalima aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na mameneja, wachimbaji na wamiliki wa migodi ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani.

Alisema ametoa miezi sita hadi mwezi Septemba kwani ikifika mwezi Octoba wataanza kuchukua hatua na wanaanza kuhesabu miezi sita hiyo kuanzia mwezi Aprili hadi Septemba.

Alisema hawezi kutoa muda wa mwaka mmoja kwani ni muda mrefu hivyo wamiliki wa migodi hiyo zaidi ya 800 wajitahidi kuboresha miundombinu yao kabla ya miezi sita kumalizika.

“Migodi yote inapaswa kuwekewa uzio wa ukuta wa matofali au mabati ili kuimarisha ulinzi na usalama mgodini na siyo senyenge mmiliki akishindwa hilo mgodi utafutiwa leseni,” alisema Ntalima.

Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoani Manyara (Marema) Tawi la Mirerani, Shwaibu Mushi alisema wachimbaji hao wanaiomba Serikali kuwapa muda mwaka mmoja ili waboreshe miundombinu ya migodi yao ikiwemo kuweka uzio.

Mushi alisema wengi wao uchumi wao ni mdogo hivyo wanaomba muda huo ili kutekeleza hilo kwani agizo hilo limekuja kipindi ambacho wengi wao wana hali ngumu.

“Wachimbaji wadogo bado wanahitaji kuwa wachimbaji wakubwa baada ya kupata madini, tuliomba tuongezewe muda wa mwaka mmoja ili tutekeleze hilo japo tunashukuru kwa kutuongezea miezi sita,” alisema.

Mwenyekiti wa kamati ya Tanzanite, Money Yousuph alisema wachimbaji wamegawanyika kwenye matabaka tofauti kiuchumi hivyo wanaomba mwaka mmoja wa kutekeleza hilo.

“Ofisa madini mkazi Ntalima wewe ni mlezi wetu na mchimbaji asiyekuwa rasmi mnamtambua na hamchukulii hatua kali na pia ukuta siyo kero ni tija tunaomba busara na hekima zako kwani sisi ni wasikivu,” alisema Yousuph.


Share:

Waziri Kivuli wa Nishati, John Mnyika Ataka Mikataba ya Stiegler's Gorge pamoja na mikataba yote ya bomba la gesi Mtwara Ipelekwe Bungeni

Waziri Kivuli wa Nishati, John Mnyika, ameitaka serikali iwasilishe bungeni mkataba wa utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa Stiegler's Gorge pamoja na mikataba yote ya bomba la gesi Mtwara na ripoti zote zilizotokana na kamati zilizoundwa kuhusu mafuta na gesi ili Bunge iipitie.

Pia ametaka serikali iwasilishe ripoti ya tathmini ya kimazingira iliyofanyika ya utekelezaji wa mradi wa Stiegler’s ili Bunge lione athari zake.

Mnyika aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa mikataba hiyo pamoja na ripoti hizo ziwasilishwe bungeni kesho wakati waziri akiwasilisha hotuba ya wizara yake.

Akizungumzia kuhusu mkataba wa Stiegler’s, Mnyika ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kibamba (Chadema), alidai umekuwa na mkanganyiko wa gharama zitakazotumika, hivyo ametaka upelekwe bungeni ili waone ni miujiza gani iliyofanyika kutoka utekelezaji wake wa miaka 12 awali hadi miaka mitatu sasa.

“Binafsi nimeshaandaa rasimu ya hotuba yenye kurasa 80 na aya 145 inayozungumzia mambo mbalimbali ya sekta ya umeme, gesi na mafuta,” alisema.

“Serikali ilileta bungeni muswada wa sheria unaohusu sekta inayogusa rasilimali za nchi, muswada mmojawapo ukiwa na kifungu chenye kutoa wajibu na haki kwa Bunge na wajibu kwa serikali kwenye mikataba mikubwa ya nchi inayogusa rasilimali za nchi.

“Mikataba hii ilikuwa na kifungu kwamba inabidi ipelekwe bungeni kwa sababu kumeshatokea utata wa mradi wa Stiegler's Gorge, wito wangu ni kwamba tarehe 28 (Jumanne) wakati waziri anasoma hotuba yake bungeni pamoja na hotuba ya serikali, awasilishe mkataba wa ujenzi wa mradi wa Stiegler's ili mbivu na mbichi zijulikane.”

Mnyika alisema serikali ilisema mkataba ambao umesainiwa na mkandarasi ni wa Sh. trilioni 6, lakini awali iliwahi kusema mradi mzima utagharimu Sh. trilioni 10.

“Uchambuzi mbalimbali ukianzia na wa serikali yenyewe ikiwamo Wizara ya Nishati na Madini wakati huo (mwaka 2016) ilifanya uchambuzi kuhusu gharama za mradi huu ambao ungetumia miaka 12 kujengwa, hii ni kwa tathmini ya wizara na tathmini ya wataalamu kuanzia mwaka 2012,” alisema.

Credit: Nipashe


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya May 27




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger