Sunday, 26 May 2019

MTAJI WA BENKI YA BIASHARA MKOMBOZI WAFIKIA SHILINGI BILIONI 20.62 MWAKA 2018

 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, Beatus Kinyaiya, akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Kumi wa Wanahisa wa Benki ya Biashara Mkombozi uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Thomas Enock na Kaimu Mwenyekiti wa bodi, Profesa Marcellina Chijoriga.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara Mkombozi, Thomas Enock, akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Kumi wa Wanahisa wa Benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, Beatus Kinyaiya na Mwenyekiti wa bodi, Profesa Marcellina Chijoriga.


 Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu.


 Wanahisa wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wanahisa wakijisajil kabla ya kuanza kwa mkutano huo
 Mmoja wa Wanahisa akiuliza swali kwenye mkutano huo
 Mwanahisa akichangia jambo kwenye mkutano huo



Na Dotto Mwaibale

MTAJI wa Benki ya Biashara Mkombozi umeongezeka kutoka shilingi za kitanzania bilioni 6.01 mwaka 2009 na kufikia shilingi za kitanzania bilioni 20.62 mwaka 2018.

Hayo yalisemwa na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Profesa Marcellina Chijoriga wakati akitoa taarifa kwenye mkutano mkuu wa kumi wa wanahisa
wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

" Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita tangu kuanzishwa kwa benki yetu mwaka 2009 tumeshuhudia ukuaji wake kutoka hadhi ya benki ndogo mpaka kufikia benki ya hadhi ya kati kwa mantiki ya rasilimali, amana za wateja, shughuli za uendeshaji na faida" alisema Chijoriga.

Alisema mpaka sasa benki hiyo imeweza kufungua matawi 10, manne katika mkoa wa Dar es Salaam, moja katika mikoa ya Morogoro, Moshi, Mwanza, Kagera na hivi karibuni Iringa na Dodoma.

Aliongeza kuwa rasilimali za benki hiyo zimekua kutoka shilingi za kitanzania bilioni 8.69 mwaka 2009 na  kufikia shilingi za kitanzania bilioni 178.82 mwaka 2018.

Alisema Amana za wateja nazo zimeongezeka kutoka shilingi za kitanzania bilioni 2.19 mwaka 2009 na kufikia shilingi za kitanzania bilioni 136.47 mwaka 2018 huku mikopo ikikua kutoka shilingi bilioni 37 mwaka 2009 na kufikia shilingi bilioni 99.04 mwaka 2018.

Alisema benki hiyo imefanikiwa kulipa gawio kwa wanahisa la thamani ya shilingi za kitanzania bilioni 0.41 mwaka 2016 na shilingi bilioni 0.52 mwaka 2017.

Akitaja mafanikio ya benki hiyo kwa mwaka 2018 alisema licha ya matatizo ya kiuchumi na mazingira ya soko benki hiyo iliweza kupata faida baada ya kulipa kodi ya shilingi za kitanzania milioni 806.04 na kuwa changamoto kubwa waliyokuwa nayo ilikuwa ni kuanza kwa matumizi ya Kanuni namba 9 ya Kanuni za Kimataifa za Uwasilishaji wa Taarifa za Fedha inayojulikana kitaalamu kama Internatipnal Reporting Standard (IFRS 9)

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma, Beatus Kinyaiya ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa benki hiyo aliwaomba wanahisa wa benki hiyo kwa kipindi hiki kutochukua hisa zao kwani hali ya soko duniani sio nzuri hivyo wasubiri hali itakapo kuwa nzuri ndipo wachukue kwa faida kubwa.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili May 26




Share:

Saturday, 25 May 2019

ILE ALMASI KUBWA KULIKO ZOTE YAUZWA BILIONI 3.2 SHINYANGA


Joseph Temba, mchimbaji mdogo wa madini mkoani Shinyanga leo Jumamosi Mei 25, 2019 ameuza jiwe la almasi kwa Sh3.2bilioni katika soko la madini la Mkoa wa Shinyanga.


Mauzo ya almasi hiyo yenye uzito wa Kareti 512.15 yamefanyika jana katika soko la madini Mkoa wa Shinyanga na kushuhudiwa na naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma.

Akizungumzia mauzo hayo, Nyongo amesema kutokana na mauzo hayo Serikali itapata Sh238milioni.

Amebainisha kuwa lengo la Serikali ni kuwezesha shughuli za wachimbaji wadogo na wadau wote wa sekta ya madini kufanyika kwa utaratibu unaoeleweka kwa faida yao na ya Serikali.

“Nimpongeze Joseph ameuza almasi yake hapa kila kitu kinakuwa wazi mbele ya Serikali, polisi, watu wa usalama na wawakilishi wa Benki ya CRDB tena bila usumbufu wowote na hiki ndicho tunachokitaka,” amesema Nyongo.

Kwa upande wake Temba ameishukuru wizara hiyo kwa utaratibu waliouweka katika kutoa mwongozo na usimamizi wa namna ya mauzo ya madini unavyotakiwa kufanyika.

“Natoa wito kwa wachimbaji wadogo hakuna sababu ya kuyakimbia masoko yaliyoanzishwa na Serikali yana faida nyingi ikiwemo usalama, ulinzi, uwazi na utambuzi wa thamani halisi ya madini kitu ambacho ni nadra sana kwenye masoko yasiyo rasmi,” amesema Temba.
Share:

Picha : DC MBONEKO AMWAGA VIFAA VYA SHULE KITUO CHA KULEA WATOTO WENYE UALBINO, AWASIHI WASOME KWA BIDII

Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, ametoa msaada wa vifaa vya shule kwenye kituo cha kulea watoto wenye ulemavu ualbino Buhangija Jumuishi kilichopo manispaa ya Shinyanga, kwa ajili ya kuwapatia hamasa ya kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.

Mboneko ametoa msaada huo leo Mei 25, 2019 akiongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, pamoja na Ofisa Maendeleo ya Jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone, kwa kutoa msaada huo wa vifaa vya shule kwa watoto hao.
Amesema msaada wa vifaa hivyo vya shule ameshirikiana na marafiki zake wa kituo Cha Computer Digital Women cha Jijini Dar es salaam, ambapo wameguswa na watoto hao wenye ualbino, na kuamua kuwasaidia vifaa hivyo,ili kutoa hamasa kwao ya kusoma kwa bidii.
“Vifaa hivi vya Shule nimeshirikiana na marafiki zangu wa kikundi cha Computer Digital Women cha jijini Dar es salaam, ambapo wameguswa  na ninyi na kuamua kuwasaidia ili msome kwa bidii na kutimiza ndoto zenu,”amesema Mboneko.
“Vifaa vya shule ambavyo nitawapatia ni madaftari, Counter Book, kalamu za penseli na wino, vifutio, vichongeo, rula, soksi, nguo za ndani kwa watoto wa kike na wa kiume, pamoja na zawadi zingine kama pipi na biskuti,” ameongeza.
Pia aliwapongeza walezi wa kituo hicho kwa kwahudumia watoto hao vizuri  na kuwalea kama watoto wao, huku akiwataka waendelea kuboresha hali ya usafi  kituoni hapo ili kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko.
Naye mkuu wa kituo cha Polisi Shinyanga Mjini (OCS) Grace Salia, aliwahakikisha ulinzi na usalama watoto hao kwenye kituo hicho, ambapo siku zote wamekuwa wakilindwa na askari.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija Seleman Kipanya ambaye ndiye mlezi mkuu wa kituo hicho, akizungumza kwa niaba ya watoto hao alimpongeza mkuu huyo wa wilaya kwa kutoa vifaa hivyo vya shule pamoja na marafiki zake, ambavyo vitawasaidia katika masomo yao.
Alitaja jumla ya watoto ambao wanalelewa kwenye kituo hicho kuwa wapo 230, wasiosikia 74,Wasioona 36, pamoja na wenye ualbino 140 ambao ndiyo wengi zaidi, na kutoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitokeza ili kuwatatulia baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwataka watoto wenye ualbino wanaolelewa kwenye kituo cha Buhanghija Jumuishi Shinyanga Mjini wasome kwa bidii ili kutimiza Ndoto zao. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Askari Alphonce Bandya (ASP) kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga (RPC) Richard Abwao, akiwasisitiza watoto hao kupenda sana elimu ambayo ndiyo itakuwa mkombozi wa maisha yao.
Mkuu wa kituo cha Polisi Shinyanga Mjini (OCS) Grace Salia, akiwahakikisha ulinzi na usalama watoto hao wenye ualbino.
Watoto wenye Ualbino wakisikiliza nasaha za viongozi juu ya kusoma kwa bidiii.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akigawa vifaa vya shule kwa watoto wenye ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.

Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akigawa vifaa vya Shule kwa watoto wenye Ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akigawa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto  likiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule likiendelea kwa watoto hao wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule likiendelea kwa watoto hao wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule likiendelea kwa watoto hao wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule likiendelea kwa watoto hao wenye Ualbino.
Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akigawa vifaa vya Shule kwa watoto wenye Ualbino.
Watoto wenye Ualbino wakiangalia Madaftari waliyopewa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko .
Watoto wenye Ualbino wakiangalia Rula ambazo wamepewa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Watoto wenye Ualbino wakionyesha vifaa vya Shule ambavyo wamepewa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Watoto wenye Ualbino wakionyesha Soksi kwa ajili ya kuvalia kwenye viatu vya shuleni.
Watoto wenye Ualbino ambao wapo darasa la Saba wakiangalia Kaunta Book walizopewa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akifungua boksi la biskuti kwa ajili ya kuzigawa kwa watoto wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji Piki na Biskuti likiendelea.
 Muonekano wa vifaa vya shule.
 Awali watoto wenye Ualbino wakimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wakati akiwasili kwenye kituo chao kwa ajili ya kuwapatia vifaa vya shule.
 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwaaga watoto hao wenye Ualbino mara baada ya kumaliza kutoa zawadi ya vifaa vya Shule na kuahidi Serikali itaendelea kuwa nao pamoja katika kuwatatulia changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili.
 Mwalimu mkuu wa Shule ya Buhanghija Selemani Kipanya ambaye pia ndiye mlezi mkuu wa watoto hao wenye Ualbino akishukuru kwa msaada huo wa vifaa vya shule ambavyo vitawasaidia watoto hao katika masomo yao.
 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, mkono wa kushoto akiwa na Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone wakikagua mahali ambapo wanalala watoto hao wenye Ualbino na kukuta hali ya usafi inaridhisha.
 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko katikati akiwa na Mkuu wa kito cha Polisi Shinyanga Grace Salia mkono wa kulia, huku mkono wa kushoto ni Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone, wakipiga picha ya pamoja na watoto wenye Ualbino.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Share:

Namba Za Simu Kuhusu Katazo La Mifuko Ya Plastiki

Kufuatia Katazo la Matumizi ya Mifuko ya Plastiki kuanzia tarehe 1Juni 2019, Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa namba maalumu za simu kwa ajili ya wananchi kuuliza maswali na kutoa maoni, ushauri ama taarifa yoyote.

Mwananchi hataingia gharama kupiga simu katika namba hizi ambazo zinapatikana masaa 24, ukiwa na swali, maoni, ushauri ama taarifa yoyote usisite kuwasiliana nasi au kutuma ujumbe mfupi (SMS) au Ujumbe wa Whatsapp kwa namba zifuatazo:

KUPIGA BILA MALIPO                    SMS/WHATSAPP
(0800 110 115)                          +255 737 796 253
(0800 110 116)                         +255 737 796 252
(0800 110 117)                         +255 737 796 249
(0800 110 118)                         +255 737 796 250
(0800 110 119)                         +255 737 796 251

•    Namba hizi zitaanza kutumika rasmi siku ya Jumatatu 27/05/2019

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
25 MEI 2019


Share:

Dc Wa Ruangwa Awapiga Stop Mangariba Na Waganga Wa Jadi Wasio Na Vitambulisho Vya Wajasiriamali.

Na Bakari Chijumba, Lindi.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, Hashim Mgandilwa amepiga marufuku wamiliki wa viwanja vya kucheza unyago kutumia Mangariba wasio na vitambulisho vya wajasiriamali wadogo.

Amesema hayo 23 Mei 2019, wakati wa kikao cha mangariba(Wanaotahiri watoto), waganga wajadi na wamiliki wa viwanja vya kuchezea unyago kilichofanyika ukumbi wa CCM Ruangwa mjini.

Mgandilwa amemtaka kila waganga wa jadi kuwa na kitambulisho cha mjasiriamali mdogo kama anataka kuendelea kutoa tiba katika Wilaya ya Ruangwa.

Mkuu huyo wa wilaya amesema wamiliki wa viwanja vya unyago wanapaswa kuzingatia ratiba ya kufunga na kufungua shule ili mtoto anafanyiwa unyago asikose haki ya kupata elimu.

"Msitafute shida,Halmashauri ikianza kutoa vibali vya sherehe hizo nitafuatilia kama umepokea watoto siku husika ya tarehe 8 mwezi wa 6 na kumaliza tarehe 6 mwezi wa  7 ikifika tarehe ya mwisho  watoto wote wawe wametoka Jando" amesema Mgandilwa.

Aidha Mgandilwa amewataka wazazi na wahusika wa shughuli za unyago, kuhakikisha watoto wanapokuwa jandoni wanalazwa kwenye vyandarua ili kuepusha maradhi na pia amesisitiza umuhimu kuzingatia usafi wa  maeneo ya viwanja vya unyago.

"Mnapofanya shughuli hizi zingatieni msingi ya afya kila mwenye kiwanja awe na uhakika na daktari ni vyema tukaangalia usalama wa watoto wetu" amesema  Mgandilwa

Mgandilwa amewataka pia wanaohusika  na shughulia za jando, kuzingatia  mafunzo  wanayotoa kwenye jando na unyago  yaendane na maadili ya kitanzania na umri wa watoto wanaopewa hayo mafunzo.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger