Saturday, 25 May 2019

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 25,2019





Share:

SERIKALI KUWAJENGEA UWEZO MAFUNDI SANIFU (MAJENGO) NA MAFUNDI MICHUNDO KUPITIA MIRADI INAYOTEKELEZWA NCHINI.

Na. Paschal Dotto-MAELEZO 

Serikali Kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, imesema kuwa itaendelea kuwajengea uwezo na uzoefu mafundi sanifu na mafundi Michundo, ili waendelee kutekeleza kazi zao kwa ufanisi na kuongeza wataalam katika kada hiyo kwani fani hizo zina watu wachache. 

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wasanifu Majengo na mafundi Michundo, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Dkt. Elius Mwakalinga alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imejikita katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa miundombinu unafanikiwa kwa kiasi kikubwa. 

“Serikali imedhamiria kujenga miundombinu ili kuwezesha ukuaji wa Sekta ya Viwanda nchini, hivyo Mafundi sanifu wanategemewa sana katika kuwezesha miundombinu hii, ili Tanzania iweze kufikia ndoto ya kuwa kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda, na katika kutekeleza hilo mwaka wa Fedha 2019/2020, Wizara ya Ujenzi imejikita katika ajenda tatu ikiwemo kuwajengea uwezo wasanifu na wahandisi wote nchini”, Alisema Dkt. Mwakalinga. 

Dkt. Mwakalinga alisema kuwa Serikali inahakikisha watalaam chini ya Taaluma ya Uhandisi, Usanifu Majengo, Ukadiriaji Majenzi na kada zingine katika sekta ya ujenzi wanaongezeka kiidadi na kujengewa ujuzi mahsusi ili kuwa na uwezo na kumudu mahitaji ya nchi ya wataalam hao. 

Aidha, Dkt. Mwakalinga aliwathibitishia kuwa serikali inaendelea kushirikiana na bodi mbalimbali za taaluma za kihandisi kwa kutoa miradi inayotekelezwa nchini ili kuwawezesha watalaam hao kupata uzoefu na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kazi hiyo itaanza rasmi mwaka wa fedha 2019/2020, Julai Mosi. 

“Napenda niwadhihirishie kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya uongozi wa Rais Magufuli, inayo dhamira ya dhati ya kuendeleza fani ya usanifu kwa kutumia miradi yake inayotekelezwa, kama vile ujenzi wa Reli ya kisasa, SGR, Ujenzi wa Interchange Ubungo, Ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha umeme mto Rufiji, na ujenzi wa Daraja la Selander, kwa hiyo miradi hii itaweza kutoa uzoefu mkubwa kwa wataalum wetu”, alisema Dkt. Mwakalinga. 

Katika kuongeza uzoefu wa watalaam hao, Dkt Mwakalinga amesema ni lazima kuwepo na maarifa na vitendea kazi ambavyo kwa sasa ni uwepo wa miradi ya kimaendeleo ambayo inatekelezwa na Serikali na sasa mafundi sanifu wanahitajika ili kuiwezesha miradi hii kutekelezwa pasipo gharama kubwa. 

Akaongeza kuwa Serikali inapoendelea na zoezi la kuwapa uwezo watalaam hao inawaomba wawe waadilifu, wenye kujituma na wenye weledi mkubwa maana kazi yao hiyo ni kubwa sana kuliko kazi zingine za kihandisi. 

“ Kama nilivyosema hapo awali tutaendelea kuwajengea uwezo watalaam wetu kwa kutumia miradi tuliyonayo, lakini kujenga uwezo kuna uhusiano mkubwa na masuala ya kujituma, kuijitoa kwa moyo kwa taifa, kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa, hii ndiyo itakuwa tiketi ya kupata kazi na tutachagua watalaam kulingana na vigezo hivyo,”Alisisitiza Mwakalinga. 

Akizungumzia kuhusu changamoto za uhaba wa wataalam hao, Dkt. Mwaklinga aliainisha kuwa, kwa takwimu za Shirika la kazi duniani, ILO, zinabaini kuwa Mhandisi mmoja anapaswa kufanya kazi na Mafundi Sanifu watano, na Mafundi Stadi 25, na kuongeza kuwa hiyo inaonyesha umuhimu wa wasanifu na mafundi stadi katika sekta ya ujenzi. 

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), Prof. Ninatubu Lema, alisema kuwa Wasanafi wanahitajika kijituma ili kuanzisha viwanda vidogovidogo vya kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kuuzwa nchini. 

“Mnatakiwa Mafundi Sanifu kuwa wabunifu katika kujenga na kutengeneza uwezo kwa kufanya wajasiriamali wa kujenga viwanda vidogovidogo, ili mtu mmoja aajiri watu watano, watu sita au watu 10 na kutengeneza vitu vidogovidogo vya kuuzwa hapa nchini, … tuko tayari kuratibu na kwenda kwenye nchi za wenzetu kama India, China kutazama hivyo viwanda vidogovidogo.”, Alisema, Prof.Lema.


Share:

Friday, 24 May 2019

MUHAS: Short Course on Traditional Medicine Development Level I & II

muhas prospectus, muhas login, muhas saris, muhas admission, muhas online application, muhas saris 2 muhas library muhas diploma courses

Short Course on Traditional Medicine Development Level I

The Institute of Traditional Medicine (ITM) is advertising five days short course on Traditional Medicine Development level I starting from 9th to 15thSeptember 2019. The applications are open from 30th April, 2019 and the closing date for receiving application and payment is 15th August, 2019. Download the Advert and Application Form.

Short Course on Traditional Medicine Development Level II

The Institute of Traditional Medicine (ITM) is advertising five days short course on Traditional Medicine Development level II starting from 16th to 22ndhSeptember 2019. The applications are open from 15th April, 2019 and the closing date for receiving application and payment is 15th August, 2019. Download the Advert and Application Form.

 

More details: https://www.muhas.ac.tz/

The post MUHAS: Short Course on Traditional Medicine Development Level I & II appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

SUA: Higher degree application 2019/20

sua admission login, sua admission contacts, sua login, sua university, sua university online application, sua entry requirements, sua online application

APPLICATIONS FOR ADMISSION INTO NEW HIGHER DEGREE PROGRAMMES FOR THE ACADEMIC YEAR 2019/2020


Applications are hereby invited for admission into newly approved Higher Degrees Programmes at Sokoine University of Agriculture (SUA) for the academic year 2019/2020. Candidates for Master and PhD Degree programmes with course work are admitted once every year for an academic year that starts in October of each year. Successful candidates will be notified immediately after approval of their applications is made and they will be expected to embark on studies in October, 2019. Candidates meeting the prescribed minimum qualifications are invited to apply for admission in the following Master and PhD degree programmes tenable at SUA:

A. MASTER DEGREE PROGRAMME 
Hosted by College of Agriculture
Master Programmes by Coursework and Dissertation

  1. MSc. Aquaculture  (New)

B. PhD DEGREE PROGRAMMES
PhD Programmes by Coursework and Dissertation

  1. PhD Agro ecology (New)

GENERAL MINIMUM ADMISSION QUALIFICATIONS
1. Master Degrees

  1. A candidate shall either hold an undergraduate degree with GPA of at least 2.7 of SUA or a qualification from an approved institution of higher learning with a GPA of 2.7.
  2. Candidates who hold unclassified degrees (e.g. BVM) should have an average of B grade in the subject of intended Master’s degree.
  3. Candidates with Pass degree will be considered for admission if their undergraduate performance in the proposed subject of study was a B grade average or above.
  4. Candidates with Pass degree will also be considered for admission if they have satisfied the relevant College/School Postgraduate Studies Committees that they have exhibited academic potential through extensive fieldwork/research experience of at least three years and/or additional professional development courses of duration of at least three months.
  5. Master degree programmes are tenable for two years for full time students and three years for part time students. In the case of full time students, the first year is dedicated for coursework, while the second year is for research and dissertation writing.

PhD Degree Programmes
Applicants for PhD programmes should possess Master’s degree of SUA or relevant Master’s degree of equivalent standing from another approved university   in the relevant field. Applicants should submit a research concept note along with the application documents. PhD studies by Research and coursework is tenable for 3 to 4 years for studies. The duration for part time students is a maximum of six years.

MODE OF APPLICATION AND PAYMENT
Candidates can apply for admission into SUA degree programmes through either of the two options:

(a) Application forms can be downloaded from our website:
http://www.sua.ac.tz/postgraduate-application-forms. Application forms can also be requested from the Director’s Office through drpgs@sua.ac.tz or postgraduate.students@sua.ac.tz. Such dully-filled forms can be returned physically or mailed to the undersigned together with evidence of payment of Tanzanian Shillings TZS 50,000/= or US$ 20 for international students as application fee (normal application submitted by 31st May, 2019) or TZS 80,000/= or US$50 for international students (for all late applications submitted after 31st May, 2019).
Payments should be made through A/C NO. 0150076769860 CRDB Bank: Swift Code No CORUTZTZXXX.

(b) Online application through http://suasis.sua.ac.tz:9092/index.php/welcome. Make sure that all relevant academic and financial documents are attached before final submission is made.

DEADLINES FOR APPLICATIONS
The deadline for applications are scheduled as follows:
a) Normal application without penalty: 15th September, 2019
b) Late Application with penalty: 15th October, 2019

In all programmes, female applicants are highly encouraged to apply.

For further information, please contact

The Director,
Directorate of Postgraduate studies, Research, Technology Transfer and Consultancy
Sokoine University of Agriculture,
P.O. Box 3151, Chuo Kikuu,
Morogoro, Tanzania.
Telephone:+255 023-2640013,
Fax: +255 023 2640013
E-mail: drpgs@sua.ac.tz/postgraduate.students@sua.ac.tz
Website: http://www.dprtc.sua.ac.tz/
Twitter: @DPRTC_SUA

 

You may also like

SUA : Revised Undergraduate-programmes Admission and examination Requirements 2019

The post SUA: Higher degree application 2019/20 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Picha : ICS NA SERIKALI YA MKOA WA SHINYANGA WAANZA KUTENGENEZA MPANGO MKAKATI WA KUTOKOMEZA UKATILI KWA WANAWAKE NA WATOTO




Shirika la Kimataifa (ICS) linalojishughulisha na masuala ya kuboresha malezi na makuzi bora ya watoto na kuwaimarishia ulinzi na usalama,kuimarisha uchumi wa kaya,masuala ya UKIMWI kwa vijana na afya ya uzazi, kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Shinyanga limefadhili kuanza kutengenezwa kwa mpango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.



Mpango mkakati huo umeanza kutengenezwa leo Mei 24, 2019 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga, kwa kuhusisha maofisa maendeleo, ustawi wa jamii, dawati la jinsia na watoto, wachumi, wanasheria, waratibu wa afya ya uzazi, maofisa elimu, pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo washiriki hao wanatoka katika halmashauri zote sita za mkoa huo.

Akizungumza kwenye kikao hicho,Meneja wa Shirika hilo la ICS Tanzania Kudely Sokoine Joram, alisema mwaka jana (2018) walishirikiana na serikali ya mkoa wa Shinyanga kuunda kamati ya mkoa ya ulinzi na usalama kwa watoto na wanawake, ambapo ilipewa mafunzo ya siku tatu na wizara ya afya kwa kushirikiana na ICS juu ya masuala ya MTAKUWWA, kwa ajili ya kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto.

Amesema baada ya kutolewa mafunzo hayo ndipo ikaazimiwa kutengenezwa mpango mkakati wa mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kushughulikia masuala hayo ya kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto ili kufanikisha mpango wa Serikali (MTAKUWWA) wa kutokomeza ukatili huo kutoka asilimia 37 hadi asilimia 10 ifikapo 2022.

“Kikao cha leo ni cha kwanza ambacho tunatengeza mpango mkakati wa kutokomeza masuala ya ukatili kwa wanawake na watoto mkoani Shinyanga pamoja na kuunda timu ya wataalamu itakayo kwenda kuanza kazi ya kukamilisha utengenezaji wa mpango mkakati mara moja ili kutokomeza ukatili huo,”amesema Kudely.

“Mbali na kushirikiana na Serikali ya mkoa wa Shinyanga pia tumehusisha na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo ni SAVE THE CHILDREN, AMREF, JHPIEGO, TVMC, AGAPE, WORDVISSION, NA JSI ,kwa lengo la kuunganisha nguvu ya pamoja kutokomeza masuala ya ukatili kwa wananawake na watoto mkoani hapa,”ameongeza.

Naye mgeni rasmi kwenye kikao hicho katibu tawala msaidizi utumishi na utawala mkoani Shinyanga Amos Machilika, akimwakilisha katibu tawala wa mkoa huo, alisema mpango huo mkakati utaleta matokeo chanya ya kupungunza ukatili mkoani humo dhidi ya wanawake na watoto likiwamo na suala la mimba na ndoa za utotoni.

Aidha amesema mkoa wa Shinyanga bado unaongoza kwa masuala ya ndoa za utotoni kwa asilimia 59,ikifuatiwa Tabora 58, na Dodoma 51, ambapo pia kwa mwaka jana kuanzia Julai hadi Disemba jumla ya matukio 31 ya ndoa za utotoni yaliripotiwa.

Pia ametaja takwimu za mimba za utotoni mkoani Shinyanga kuwa ni asilimia 34 kwa mujibu wa takwimu za viashiria vya hali ya kiafya nchini (TDHS) ya Mwaka 2016, ikitanguliwa na Katavi 45, Tabora,43, Dodoma 39, na Mara 37, ambapo wastani wa kitaifa ni asilimia 27, huku kwa kipichi cha miaka mitatu jumla ya wanafunzi 351 walipewa ujauzito na kuacha masomo mkoani humo.

Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakiwasilisha mada akiwamo Afisa Ustawi wa Jamii Kahama Mji Ibrahimu Nuru, amesema ili kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto mkoani humo kuondoa kwanza tatizo la mila na desturi Kandamizi pamoja na kuimarisha uchumi wa kila Kaya.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Meneja wa Shirika la kimataifa ICS Tanzania Kudely Sokoine Joram, akizungumza kwenye kikao cha mpango mkakati wa kupanga kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto mkoani Shinyanga.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Meneja wa Shirika la kimataifa ICS Tanzania Kudely Sokoine Joram, akisisitiza ushirikiano uwepo wa kuunganisha nguvu ya pamoja kati ya mashirika yasiyo ya kiserikali na Serikali ya mkoa wa Shinyanga, kwa ajili ya kupambana kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Afisa ustawi wa jamii wa halmashauri ya Kahama Mji Ibrahimu Nuru, akiwasilisha mada ya mpango mkakati wa Serikali wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) kwenye kikao hicho, na kubainisha moja ya changamoto ambayo inatakiwa kushughulikiwa ili kufikia malengo yake ni kutokomeza mila na desturi kandamizi pamoja na kuimarisha uchumi wa kaya.

Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale, akielekeza washiriki wa kikao hicho namna ya kuandaa taarifa zinazohitaji katika kuunda mpango mkakati wa mkoa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Meneja wa Kanda kutoka Shirika la JSI Anthony Mwendamaka akichangia mada kwenye kikao hicho cha mapango mkakati wa kutomoze ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.

Kaimu mkurugenzi wa Shirika la Save The Children Mkoani Shinyanga Alex Enock akichangia mada kwenye kikao hicho cha kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.

Washiriki wakiwa kwenye kikao cha kupanga mpango wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.

Washiriki wakiwa kwenye kikao cha kupanga mpango wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.

Washiriki wakiwa kwenye kikao cha kupanga mpango wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.

Washiriki wakiwa kwenye kikao cha kupanga mpango wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Kikao kikiendelea.

Washiriki wakiendelea na kikao cha kupanga mpango kazi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.

Kikao kikiendelea.

Washiriki wakiwa kwenye makundi ya kila halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga wakiandaa mpango mkakati wa mkoa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Washiriki wakiwa kwenye makundi ya kila halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga wakiandaa mpango mkakati wa mkoa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Washiriki wakiendelea kupanga mapango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.

Washiriki wakiendelea kupanga mapango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.

Washiriki wakiendelea kupanga mapango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.
Washiriki wakiendelea kupanga mapango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.

Washiriki wakiendelea kupanga mapango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.
 
Washiriki wakiendelea kupanga mapango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.

Washiriki wakiwa kwenye makundi ya kila halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga wakiandaa mpango mkakati wa mkoa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.

Picha zote na Marco Maduhu-Malunde 1 Blog
Share:

Picha : RAIS MAGUFULI ATUA AFRIKA KUSINI KUHUDHURIA SHEREHE YA UAPISHO WA RAIS MTEULE CYRIL RAMAPHOSA


Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa OR Tambo Nchini Afrika Kusini kwaajili ya kuhudhuria Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa nchi hiyo Mhe.Cyril Ramaphosa ambaye anatarajiwa kuapishwa Mei 25,2019. Picha na Ikulu




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kuingia kwenye ndege ya Shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) walipokuwa wakielekea Nchini Afrika Kusini kwaajili ya Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa nchi hiyo Mhe.Cyril Ramaphosa ambaye anatarajiwa kuapishwa Mei 25,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa kwenye ndege ya Shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) wakielekea Nchini Afrika Kusini kwaajili ya Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa nchi hiyo Mhe.Cyril Ramaphosa ambaye anatarajiwa kuapishwa Mei 25,2019.

Picha na Ikulu
Share:

Usikubali Kupitwa na Habari Zote Kali : Pakua App ya Malunde 1 blog Leo ili Tuwe Tunakutumia kwenye simu yako Bure Kabisa

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:

WAZIRI UMMY ATOA RAI KWA VIONGOZI WA DINI PAMOJA NA WAZAZI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTOA ELIMU JUU YA MALEZI YA WATOTO


 Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,jinsia Wazee na Watoto  Mhe.Ummy Mwalimu ametoa Rai kwa viongozi wa Dini,Taasisi pamoja na wazazi kushirikiana na Serikali  kutoa Elimu juu ya Malezi bora ya Watoto ili kupunguza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto vinavyofanywa na watu wa karibu ikiwa ni pamoja na ulawiti. 


Mhe.Ummy ametoa Rai hiyo,Leo Mei 24,2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la  Nyongeza la Mbunge wa Rombo Joseph Selasini aliyehoji kuwa watoto wananyanyaswa kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kulawitiwa ni lini serikali itatembelea mashuleni ili kuweza kutoa elimu dhidi ya unyanyasaji na kulawitiana kwa watoto. 


Katika majibu yake,Waziri Ummy amesema pamoja na majukumu ya kila siku kwa wazazi wanatakiwa kuwakagua mara kwa mara watoto wao huku akiomba viongozi wa dini kusaidia kuhubiri kwani sheria peke yake haiwezi kumaliza tatizo hilo. 


Aidha ,Waziri Ummy amesema serikali imekuwa ikifanya mikakati mbalimbali katika kudhibiti vitendo vya  Ukatili kwa wanawake na watoto kwa kutoa elimu ambapo pia kuna namba ya bure ambayo ni 116 husaidia kwa watu wanaofanyiwa vitendo hivyo kuwasiliana na mamlaka husika na kuna zaidi ya madawati  ya kijinsia 350   hapa nchini. 


Hata hivyo,Waziri Ummy amesema kuanzia Tarehe 16 Juni,2019 ambayo ni siku Muhimu ya Mtoto wa Afrika serikali itazindua ajenda ya kitaifa kuhusu wajibu wa Mzazi katika Malezi ya Mtoto.

 


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger