Friday, 24 May 2019

Dr. Mwakembye Avitaka Vyombo Vya Habari Kuweka Sera Madhubuti Katika Kutetea Na Kutangaza Mafanikio Ya Maendeleo Ya Afrika

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amevitaka vyombo ya habari vya Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania kutangaza na kuandika habari za kweli ili kujitofautisha na vyombo vya Nje ya Bara hilo ambavyo upotosha na kubeza kwa makusudi mambo mazuri yanayotekelezwa na yaliyotekelezwa na Nchi za Afrika.

Akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Mawasiliano Barani Afrika leo Ijumaa (Mei 24, 2019) Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe alisema vyombo vya Habari vya Afrika havina budi kuonyesha udhubuti kwa kuweka sera zinazoakisi maendeleo na kuyatangaza kwa Wananchi wake na wote waliopo nje ya Bara hilo.

Dkt. Mwakyembe alisema sehemu kubwa ya maudhui ya Vyombo vya Habari vilivyopo nje ya Bara la Afrika vinavyoongozwa na Wakoloni waliowahi kutawala katika Bara la Afrika hawapendi kuona Nchi za Afrika zinapiga hatua za Maendeleo kwa wananchi wake na badala yake hupenda kuripoti na kutangaza mambo mabaya yanayohusu Afrika ikiwemo njaa, magonjwa, vurugu za kisiasa, vita n.k.

Aidha Dkt. Mwakyembe alisema yapo mambo mazuri ya Maendeleo yanayofanyika katika Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania ambayo zimepiga katika kipindi cha miaka minne imepiga hatua kubwa katika Maendeleo ya kiuchumi, na miundombinu, jambo ambalo baadhi ya vyombo vya habari vya Mataifa ya Nje ya Afrika yamekuwa hayapendi kuyatangaza, hivyo ni wajibu wa vyombo  vya habari kutumia majukwaa yao kutetea na kutangaza mafanikio hayo.

“Wakati Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Kenneth Kaunda wa Zambia walipoamua kujenga Reli ya Tazara, walipingwa vikali sana Wakoloni waliotuwala na wengine waliita reli ile kuwa ni bamboo (mianzi) lakini ni taifa moja tu la Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China walitusaidia na leo hii reli ile ndiyo ndefu zaidi katika Bara la Afrika yenye urefu wa kilometa 1860” alisema Dkt. Mwakyembe.

Kwa mujibu wa Waziri Mwakyembe alisema Maendeleo ya Bara la Afrika yatatetewa na kupiganiwa na Wafrika wenyewe, hivyo ni wajibu wa vyombo vya habari vya Bara hilo kujitokeza na kutetea Maendeleo hayo na kamwe haitatokea siku moja chombo cha habari cha BBC au CNN vikatangaza mafanikio hayo kwani hawapendi kuona Mataifa waliyoyatawala yakifikia hatua kubwa za kimaendeleo.

Akifafanua zaidi Dkt. Mwakyembe aliwataka Vijana wa Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania kujifunza historia ya Bara lao ili kuweza kufahamu wapi walipotoka na wapi wanapoelekea badala ya kupenda kulalamika pasipo na kuweka mikakati ya namna bora ya kupiga hatua za kujietea Maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi.

Waziri Mwakyembe alisema ni wajibu wa Taasisi mbalimbali za Habari na Mawasiliano zilizopo katika Bara la Afrika kujenga mifumo imara ya mawasiliano ikiwemo kutumia vyema mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuchapisha habari zinazohusu masuala ya maendeleo badala ya kutumia majukwaa hayo kuandika mambo yasiyo na faida wala tija kwa mataifa yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, alisema Serikali imeendelea kuimarisha ushirikiano na taasisi za mawasiliano katika sekta binafsi ili kuhakikisha kuwa wanajenga daraja moja katika kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo ya sekta ya habari na Mawasiliano nchini.

Naye Rais wa Chama cha Maafisa Uhusiano wa Sekta binafsi Tanzania (PRST) Loth Makuza alisema, taasisi hiyo ni jukwaa huru linalotoa fursa na nafasi ya kujadili masuala mbalimbali ya mawasiliano nchini ikiwemo changamoto na utatuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya habari na mawasiliano nchini.

Anaongeza kuwa Taasisi hiyo kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano imeweza kutengeneza majukwaa mbalimbali yanayotangaza masuala mbalimbali ya kimaendeleo yaliyofikiwa katika Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania, lengo likiwa ni kubadili mtazamo hasi wa Bara la Afrika katika nyanja za kiuchumi, kijamii kupitia ngazi ya kimataifa na duniani kwa ujumla.


Share:

Sugu aitaka Serikali kupunguza tozo hotelini......Ashauri Hoteli Mpya Zipewe Miaka Miwili

Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi (Chadema) maarufu Sugu ameitaka Serikali kupunguza tozo kwenye Hotel kwani zimekuwa zikiwarudisha nyuma wafanyabiashara.

Mbilinyi ametoa kauli hiyo leo Mei 24 bungeni wakati akichangia Mjadala wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2019-2020.

Mbilinyi amesema tozo zinazotozwa kwenye hotel nchini zimekuwa nyingi hivyo ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iziondoe ili wafanyabishara wenye biashara zao ziweze kukuwa.

“Kuhusu Tozo zimekuwa nyingi, umekaa tu mara wanapiga hodi anasema anatoka sehemu fulani,amefuata tozo, hotel mpya mzipe miaka miwili bila tozo ili wakuze biashara zao.Niiombe Serikali itoe hizo tozo zimejaa sana ndio maana biashara hazikuwi,”amesema Mbilinyi.


Share:

Video Mpya:Harmonize - Never Give Up

Video Mpya:Harmonize - Never Give Up


Share:

Video Mpya: Masanja Mkandamizaji – Short And Clear

Video Mpya: Masanja Mkandamizaji – Short And Clear


Share:

Waziri Mkuu Wa Uingreza Theresa May Ajiuzulu

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ametangaza kuwa atajiuzulu Juni 7, 2019, baada ya kuliongoza taifa hilo kwa miaka 3. 

Kiongozi huyo ambaye ni mwanamke wa pili kushika wadhifa huo amekuwa akikumbana na upinzani mkali kuhusu makubaliano ya kujitoa ndani ya Umoja wa Ulaya (EU). 

Katika taarifa iliojaa hisia alioitoa huko Downing Street, Bi May amesema amefanya "kila awezalo" kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya mnamo 2016.

Amesema ni jambo linalosalia kuwa "na majuto mengi" kwamba ameshindwa kutimiza Brexit - Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya

Bi May amesema ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu wakati kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa chama cha Conservative.

Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7 na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada ya hatua hiyo.


Share:

WAZIRI MKUU KUJIUZULU JUNI 7

Theresa May kujiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative tarehe 7 Juni na kutoa fursa kuidhinishwa mchakato wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya Uingereza.

Katika taarifa iliyojaa hisia aliyoitoa huko Downing Street, Bi May amesema amefanya "kila awezalo" kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya mnamo 2016.

Ni jambo linalosalia kuwa "na majuto mengi" kwamba ameshindwa kutimiza Brexit - Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, ameongeza.

Lakini waziri mkuu mpya ndio suluhu " kwa manufaa ya taifa".

Bi May amesema ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu wakati kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa chama cha Conservative.

Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7 na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada ya hatua hiyo.
Theresa May Uongozini

Miaka 3 ahudumu kama waziri baada ya kuondoka David Cameron

Miaka 6 kabla ya hapo, waziri wa mambo ya ndani

Ashindwa katika uchaguzi mkuu 2017 , lakini alisalia waziri mkuu

Asaliampiga kura katika kura ya maoni ya EU mnamo 2016

Brexit iligubika muda aliohudumu 10 Downing Street BBC

Sauti yake ilittereka na alikuwa mwingi wa hisia alipomaliza hotuba yake akisema: "Nitaondoka katika wadhifa huu hivi karibuni lakini imekuwa heshima kubwa maihsani mwangu kuhudumu.

"Waziri mkuu mwanamke wa pili, na bila shaka sio wa mwisho.

"Nachukua hatua hii bila ya uovu wowote, bali na shukrani za dhati na kubwa kutokana na kupata fursa kuitumikia nchi ninayoipenda."
Chanzo - BBC
Share:

Wakaguzi wa mifuko ya plastiki hawaruhusiwi kuingia kwenye makazi ya watu, au kusimamisha magari, ili kutafuta mifuko ya plastiki.




Share:

Halmashauri Tatu Kupandishwa Hadhi na Kuwa Manispaa

Na.Faustine Gimu Galafoni,Kutoka Jijini Dodoma.

Bunge limeelezwa kuwa ,Serikali ipo katika mchakato wa kupandisha hadhi halmashauri 3 hapa nchini kutokana na kukidhi vigezo vya mapato kujitosheleza. 

Hayo yamesemwa leo Mei 24,2019 bungeni  jijini Dodoma na Waziri wa Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa TAMISEMI ,Mhe.Seleman Jafo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Msalala Kahama Ezekiel Maige aliyehoji,lini mji wa Kahama utapandisha kuwa hadhi kuwa Manispaa baada ya kutimiza vigezo vya mapato kujitosheleza  pamoja na Isaka kupandishwa hadhi ya Mji. 

Akijibu Swali hilo,Waziri wa TAMISEMI Mhe.Seleman Jafo amesema Serikali inatambua maeneo matatu hapa nchini ambayo serikali ipo katika mchakato wa kupandisha hadhi kuwa Manispaa kutokana na kukidhi vigezo vya kujitosheleza kimapato. 

Mhe.Jafo ameyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga,Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani na Halmashauri ya  mji wa Geita mkoani Geita na muda wowote kuanzia sasa maeneo hayo yatapandishwa hadhi kuwa Manispaa pindi mchakato utakapokamilika.


Share:

Rais Magufuli Aondoka Nchini Kuelekea Afrika Kusinj

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Mei, 2019 ameondoka nchini kwenda Afrika ya Kusini ambapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa.

Katika safari hiyo Rais Magufuli ameongozana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Philip Mangula na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi.

Wakizungumza kabla ya kuondoka Rais Mstaafu Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa CCM Mangula wamesema Tanzania na Afrika ya Kusini zina uhusiano mkubwa na wa kihistoria na kwamba Serikali na chama zina kila sababu ya kudumisha uhusiano na ushirikiano huo.

Viongozi hao wameondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Afrika ya Kusini, Mhe. Rais Magufuli atafanya Ziara Rasmi ya Kitaifa nchini Namibia ambako pia atazindua mtaa uliopewa jina la Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kutambua mchango mkubwa alioutoa katika ukombozi wa Taifa hilo.



Share:

Video : DAKIKA 11 ZA MASELE AKIWASHA MOTO BUNGENI DHIDI YA TUHUMA ZA SPIKA NDUGAI

Spika Job Ndugai na Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele.

Ukumbi wa Bunge jana ulikuwa wa moto. Hivi ndivyo unavyoweza kuelezea kile ambacho kilitokea bungeni wakati Spika Job Ndugai na Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele kutuhumiana.

Masele ambaye ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) alitumia dakika kumi na moja alizopewa na Spika Ndugai kuomba radhi, kutoa tuhuma mbalimbali dhidi ya kiongozi huyo wa Bunge baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumtia hatiani kwa makosa manne.

Masele, alisema barua ya Ndugai kwenda kwa Rais wa PAP, Roger Dang ingeweza kumng’oa huku akishangaa kwa nini hakutaka kumsikiliza kabla ya kuchukua hatua hiyo.

“Rais wa PAP aliitaka hii barua yako kutaka kunivua. Kwa kuzingatia barua yako Spika ninayekuheshimu, nilitafakari sana kwa maslahi ya wabunge, Taifa na kijana ninayekua katika uongozi. Nilifikiria haraka na busara yangu iliniongoza kama Spika ananisimamisha bila kunisikiliza, ndio sababu ya kukata rufaa na ndio sababu ya kuwasiliana na mwenyekiti wa CCM na mwenyekiti wa wabunge wa CCM bungeni ambaye ni Waziri Mkuu.”

Huku akishangiliwa na wabunge wa pande zote, Masele alianza kwa kumshukuru Mungu kisha kusema, “ninaomba kutumia fursa hii kukuomba radhi wewe (Spika) binafsi na familia yako kwa usumbufu wowote ulioupata kupitia sakata hili. Niwaombe radhi wabunge wenzangu kwa usumbufu mlioupata. Nitumie nafasi hii pia kuwaomba radhi viongozi wangu wakuu, mwenyekiti wa chama changu Rais John Magufuli, Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) ambaye ni mwenyekiti wetu wa wabunge wa CCM kwa usumbufu wowote walioupata kutokana na jambo hili,” alisema.

Alisema anaomba rekodi ibaki sawa kuwa, “makosa yaliyoorodheshwa katika shtaka langu, ningefurahi kama hansard ya kikao ingeletwa katika Bunge hili ili wabunge na Watanzania wajue ukweli.”

Alianza kwa kutoa barua ya mwaliko wa kuhudhuria kikao cha Bunge la PAP na kuionyesha akisema, “utaratibu wa Bunge, huwa hatuji kuomba kibali, bali tunatoa ‘notification’ kwa hiyo mheshimiwa Spika nilileta notification katika ofisi ya Katibu wa Bunge. Tuhuma zinasema nimesafiri bila kibali, sisi tuko wanne, kwa nini Masele ninaadhibiwa mimi na wabunge wenzangu wasichukuliwe hatua?”

Huku ukumbi wa Bunge ukiwa kimya kumsikiliza, Masele alisema barua ambayo Spika alimwandikia Mei 16, aliipata saa 11 jioni ikimtaka awe amefika Tanzania Jumanne ya Mei 17 saa 4:00 asubuhi jambo ambalo lingekuwa gumu kutokana na kubadili tiketi ya ndege na hakuwa na fedha za kulipia hoteli na Bunge kutowalipa posho za kujikimu.

Alisema barua hiyo ilitaka kutumiwa na Rais wa PAP ambaye ni raia wa Cameroon kumng’oa kwenye wadhifa huo wa Makamu wa Rais wa PAP na mjumbe wa Bunge hilo.

Alisema alifikiria haraka na busara yake ikamuongoza kukata rufaa na ndio sababu ya kuwasiliana na mwenyekiti wa CCM na Waziri Mkuu ambaye ni mwenyekiti wa wabunge wa CCM.

Akizungumza kwa kujiamini, Masele alisema, “Niliwaandikia ujumbe na kuwatumia barua hii nikiomba ushauri. Barua hii ilitaka kutumika kunichinja, kukata kichwa changu nisiwe Makamu wa Rais na mjumbe wa PAP, kama ni mbunge wa Bunge hili ungefanya nini.”

Alisema Spika kwa nafasi yake angeweza kumpigia simu na kumuuliza kipi kimetokea lakini aliamua kumhukumu bila hata kamati ya maadili kumsikiliza na “ninasikitika kwamba sikuchonganisha muhimili, nisingeweza kupeleka jambo hili kwa waziri au katibu wa wabunge wa CCM.”

Alisema video iliyoonekana, ilikuwa sehemu ya sekunde tu ikimwonyesha akisema kwamba anaungwa mkono na Serikali na barua ya Spika haitambui.

“Spika nimekubali mimi ni kijana, nimebeba dhamana, ninakuomba radhi. Ieleweke sikufanya kwa makusudi kukuvunjia heshima, kukudharau, nilipokea wito wako saa 11 jioni na kunitaka kesho yake nifike Dodoma saa nne asubuhi. Nimekwenda Afrika Kusini bila kupewa posho, nauli, tiketi na ningepata wapi watu wa kulipa bili hotelini?” alisema

Masele aliyewahi kuwa naibu waziri wa nishati na madini na Ofisi ya Makamu wa Rais katika utawala uliopita alisema, “na wakati huo Rais PAP alikuwa na hatia za udhalilishaji wa kijinsia, natambua Rais wa PAP anafanya mawasiliano na wewe (spika) ili mimi nisirudi PAP, najua na ninatambua.”

“Naamini umefanya ushauri wa kutosha, nimekubali makosa, kwa heshima ya Bunge langu, nakuja mbele yako kuomba radhi kwa usumbufu ulioupata, nashukuru kwa nafasi hii, Bunge na Watanzania kujua ukweli,” alisema.

Masele alimaliza kwa kusema amekuwa mbunge miaka tisa na hajawahi kuitwa katika kamati yoyote ya nidhamu, sijawahi kufanya kosa lolote, najitambua, najiheshimu huku akisema kwa kutumia kanuni ya 68(1) kanuni inayovunjwa ya 63(1) kwa mwenyekiti wa kamati kuleta taarifa yenye upungufu, alitoa hoja ya kukataa ripoti yake.

Chanzo - Mwananchi

                    SOMA ZAIDI <<HAPA>>
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa May 24




Share:

Thursday, 23 May 2019

BINTI AUNGUZWA MAJI YA MOTO BUKOBA


Mwanafunzi aliyeunguzwa maji ya moto

Binti wa darasa la saba, shule ya msingi Kashenge katika Manispaa ya Bukoba, amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera akiuguza majeraha anayodai kuyapata baada ya kuunguzwa kwa maji ya moto na mama yake wa kambo.

Akizungumza kwa shida akiwa wodini, binti huyo mwenye umri wa miaka 16, amesema kuwa alimwagiwa maji ya moto na mama huyo kwa sababu alipika viazi bila kuambiwa.

Afisa Muuguzi Msaidizi wa wodi namba kumi upande wa upasuaji, Edith Ezekiel amesema kuwa walimpokea binti huyo jana akiwa ameunguzwa mkono wa kulia, titi na sehemu za bega, na kuwa hali yake kwa sasa sio mbaya na anaendelea na matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa atatoa taarifa rasmi kesho kuzungumzia tukio hilo ambalo tayari limeripotiwa polisi na kufunguliwa jalada la kujeruhi namba RB/2466/19.
Share:

Sikiliza : MABISHANO MAKALI KATI YA MASELE NA NDUGAI LEO BUNGENI...AANIKA UKWELI KWA WATANZANIA


Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele leo tarehe 23 Mei 2019 ambaye ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), ameshutumu mawasiliano ya Spika Ndugai na Roger Nkodo Dang, Rais wa Bunge la Afrika (PAP) kwamba, yalikuwa na malengo hasi kwake na nafasi yake ya umakamu wa rais wa PAP.


Share:

MABAO YA BOCCO, KAGERE YAMPAGAWISHA MO DEWJI SEVILLA WAKIICHAPA SIMBA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji 'Mo Dewji' ameshindwa kujizuia kwa kushangilia kwa nguvu wakati vijana wake wakichapwa mabao 4-5 na Sevilla kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mo Dewji alishindwa kujizuia ni baada ya kufungwa bao la tatu na John Bocco aliyepokea pasi kutoka kwa Meddie Kagere.

Mo Dewji aliyekuwa ameketi karibu na Mkurungezi wa Utawala na Udhibiti wa Sportpesa, Abbas Tarimba alianza kushangilia kwa nguvu huku akirukaruka baada ya Simba kupata bao la tatu.

Mo Dewji alikuwa amesimama huku akirukaruka na kumpa mkono wa pongezi Tarimba.

Baada hapo Mo Dewji alikaa chini huku akionekana bado kuwa na furaha akiwapa mkono wa pongezi waliokuwa karibu yake.

Mo Dewji hakushangilia bao hilo peke yake kwa upande wa viongozi waliokuwa jukwaa Kuu ni Mtendaji Mkuu wa Simba, Magori, Mwenyekiti Swedy Mkwabi.

Na Thobias Sebastian
Share:

RAIS APIGA MARUFUKU PICHA ZAKE KUWEKWA OFISINI..ADAI URAIS SIYO UMAARUFU


Rais wa Ukraine, Volodymyr Oleksandrovych Zelensky.

Rais mpya wa Ukraine, Volodymyr Oleksandrovych Zelensky amepiga marufuku picha yake kuwekwa kwenye ofisi za umma kwa kile alichodai kuwa Urais sio umaarufu.

Rais Zelensky amesema kuwa badala ya kuwekwa picha zake ukutani, kila mmoja aweke picha za watoto wake ili awe anaitazama kila anapofanya maamuzi.

"Ni marufuku kuning'iniza picha zangu kwenye Ofisi zote za Umma, u-Rais si umaarufu ama kuwekwa ukutani, badala yake kila mmoja wenu aweke picha za watoto wake awe anazitazama kila anapofanya maamuzi ya nchi hii", amesema Zelensky, Rais mpya wa Ukraine.

Volodymyr Oleksandrovych Zelensky, Rais mpya wa Ukraine alishinda katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika April 21. Kabla ya kuamua kugombea urais, Zelensky alikuwa msanii maarufu wa vichekesho nchini humo.
Share:

Utauzi Mpya Uliofanywa na Rais Magufuli Leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Onorius John Njole kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria (Chief Parliamentary Draftsman – CPD).

Uteuzi wa Njole umeanza leo May 23, 2019.

Kabla ya uteuzi huo, Njole alikuwa Mkurugenzi wa Sheria na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).

Njole anachukua nafasi ya Sara K. Barahomoka ambaye anastaafu.



Share:

TAMASHA LA LAKWETU CONCERT 2019 KUTIKISA MWANZA

Lile tamasha kubwa la Muziki wa Injili Mkoani Mwanza Liitwalo Lakwetu Concert linatarajia kufanyika kwa Kishindo Jijini humo tarehe 9 Juni Mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Meneja wa Famara Promotion waandaji wa Lakwetu Concert Bi Catherine Mniko alisema kuwa tamasha la Mwaka huu litakuwa kubwa kutokana Maandalizi yaliyofanywa na Kamati ya uratibu.

Catherine alisema Kamati imejiandaa vya kutosha kuratibu kila kitu na wanaamini tamasha la mwaka huu litakuwa kubwa tofauti ya miaka miwili iliyopita toka lianzishwe Jijini Mwanza.

"Toka Lakwetu Concert lianzishwe tumeona ukuaji mkubwa wa tamasha, watu wameanza kutuelewa na kulipenda tamasha letu" alisema Bi Catherine.

"Mwaka huu tumeanza Maandalizi mapema Sana toka mwezi wa pili na hadi kilele chake tunaamini kusudi letu litakuwa limefikia hatua nzurii zaidi" 

"Tumepita kwenye makanisa Saba Jijini Mwanza kwa kuandaa matamasha ya kuimba  kwa kuzileta kwaya mbalimbali kutoka madhehebu yote, waimbaji wa bendi na waimbaji binafsi kwa ajili ya kumsifu Mungu pamoja na kujiandaa na kilele Cha tamasha letu la Grand Finale"

Bi Catherine alisema tamasha la finali la Lakwetu Concert litakuwa na Mambo Mbalimbali mazuri Sana kupita miaka miwili iliopita .

Alisema tamasha hilo litafanyika Katika Uwanja wa CCM Kirumba tarehe 9 Juni Mwaka huu kwa vikutanisha Vikundi zaidi ya arobaini kutoka Mikoa mbalimbali Nchini.

Pia watakuwepo washiriki wa Shindano la Rock City Gospel Search 2019 siku hiyo na watazamaji watapata nafasi ya kuwaona ili wawafahamu na kuviona vipaji walivyonavyo.

Tamasha la Lakwetu Concert ni Kongamano kubwa la Kuimba na kusifu lililobuniwa makusudi kuwaleta waimbaji wa Muziki wa Injili pamoja ili kumsifu Mungu kwa Nyimbo na tenzi, linalozunguka Mikoa mbalimbali Nchini.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger