Thursday, 23 May 2019

Picha : MAFUNZO YA SHERIA KWA BLOGGERS YAFUNGWA

Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Vyombo Vya Habari Mbadala (Alternative Media), wakinasa matukio jana jijini Dodoma wakati Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi hao kuhusu sheria mbalimbali za habari ili kutekeleza kwa weledi mradi wa Utetezi na Ushawishi kwa kutumia Takwimu (Data Driven Advocacy-DDA), unaosimamiwa na UTPC kupitia Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa taasisi ya Freedom House.
Picha na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs -UTPC), umekamilisha taratibu za kulichukua Shirikisho la Klabu za Waandishi wa Habari katika nchi za Afrika na Karibiani (African and Caribbean Press Club-ACP) ambapo makao makuu yake yatakuwa jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan aliyasema hayo jana wakati akifunga mafunzo ya sheria mbalimbali za habari kwa waandishi wa habari wa Vyombo vya Habari Mbadala (Alternative Media) yaliyofanyika Morena Hoteli jijini Dodoma kwa siku mbili kuanzia Mei 21, 2019 hadi Mei 22,2019.

“Waambieni watanzania jambo hilo, waambieni watu wasioijua UTPC jambo hilo, waambieni watu wenye mashaka na UTPC jambo hilo, kwamba sasa tunaisimamia “Federation” (shirikisho) ya nchi zaidi ya 160” alisema Karsan akisisitiza kwamba hilo si jambo dogo bali ni hatua kubwa.

Aidha Karsan alitumia nafasi hiyo kushukru uwepo wa mradi wa DDA ambapo alisisitiza washiriki wake kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha matarajio yanafikiwa na kuondokana na changamoto ya kutotimiza makubaliano jambo ambalo limekuwa likisababisha taasisi nyingi ikiwemo za waandishi wa habari kuvunjika.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari (APC), Claude Gwandu alisisitiza kwamba klabu hiyo itahakikisha mradi huo unafanikiwa na kwamba haitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayetaka kukwamisha mradi huo lengo likiwa ni kuleta mabadiliko katika jamii na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kupitia mradi wa utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu (DDA), Midraji Ibrahim alisema mafunzo hayo yatawasaidia kupiga hatua katika majukumu yao ikiwa kila mmoja atafanyia kazi yale aliyojifunza huku akiishukru taasisi ya Freedom House kwa ushirikiano wake.

Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) unafadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka jana 2018 ambapo kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) unasimamiwa na UTPC kupitia APC.

Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan akizungumza kwenye kwenye kilele cha mafunzo ya siku mbili kuanzia Mei 21-22, 2019 kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Altenative Media) yaliyofanyika jijini Dodoma.Picha na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan akiwahimiza waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha mategemeo ya mradi huo wa utetezi na ushawishi kwa kutumia takwimu yanatimia.
Wakili James Marenga ambaye alikuwa Mkufunzi wa Mafunzo hayo akitoa salamu zake .
Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko akitoa ufafanuzi kwenye kilele cha mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kupitia mradi wa utetezi na ushawishi kwa kutumia takwimu (DDA), Midraji Ibrahim akitoa salamu zake kwenye kilele cha mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Arusha Press Club, Claude Gwandu akitoa salamu zake kwenye hitimisho la mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada kutoka kwa Wakili James Marenga.
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi May 23




Share:

Wednesday, 22 May 2019

Picha : AGAPE YAKUTANA NA VIONGOZI WA JAMII KUWAPA NONDO ZA KUENDELEZA VITA DHIDI YA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

Shirika lisilo la kiserikali la mkoani Shinyanga AGAPE ACP, limeendesha kikao kwa viongozi wa jamii 30 wakiwemo wenyeviti wa vitongoji 30,viongozi wa kidini na kimila, wazee maarufu na waelimishaji rika kwenye  kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuendeleza mapambano ukatili dhidi ya wanawake na watoto.



Kikao hicho kimefanyika leo Mei 22, 2019 katika shule ya msingi Singita kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa Afisa mtendaji wa kata hiyo Emmanuel Maduhu, ambapo amewataka viongozi hao kuwa mstari wa mbele kupambana na matukio ya ukatili ndani ya jamii, ikiwamo kutokomeza mimba
na ndoa za utotoni.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape mkoani Shinyanga Lucy Maganga, amesema mradi huo unaelekea ukingoni ambapo ulianza (2017) na kutarajiwa kuisha Julai 2019, ambapo walianza kwa kuwajengea uwezo viongozi hao namna ya kuendelea kupambana kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Amesema wameamua kuendesha kikao hicho kwa viongozi hao ambao ndiyo wapo karibu na wananchi zaidi muda wote, kwa kuwapatia elimu namna ya kutokomeza matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto, licha ya mradi wao huo kukoma ambapo elimu itakuwa ikizidi kutolewa ndani ya jamii na hatimaye kuishi salama.

“Mradi wetu huu umekaribia kuisha kutekelezwa katika kata hii ya Usanda,ambao ulikuwa wa miaka miwili na utakoma Julai 2019, hivyo kutokana na mafanikio yaliyopatikana ikiwemo kupunguza matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto zikiwamo mimba na ndoa za utotoni, tukaona pia tuwajengee uwezo viongozi hawa ambao wataendeleza gurudumu la kutokomeza kabisa matukio haya,”amesema Maganga.

“Kikao chetu hiki cha leo kimeshirikisha wenyeviti wa vitongoji 30 wa kata ya Usanda, waelimishaji rika, wazee maarufu, wazee wa kimila, ambapo wamepewa elimu namna
ya kupambana kutokomeza matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto zikiwamo mimba na ndoa za utotoni ili kuendeleza kupinga ukatili ndani ya jamii,” ameongeza.

Naye mgeni rasmi mtendaji huyo wa kata ya Usanda Emmanuel Maduhu, amewataka wenyeviti wa
vitongoji kwenye kata hiyo elimu ambayo wamepewa wakaitumie vizuri katika kutokomeza matukio hayo ya ukatili kwa wanawake na watoto, na kuzuia ndoa za utotoni kwa kufanya uchunguzi kama binti anayeolewa si chini ya umri
wa miaka 18.

Amesema wenyeviti wa vitongoji ndiyo wanaishi karibu zaidi na wananchi na wanawafahamu kila mmoja na kaya yake, hivyo wanamchango mkubwa katika kupunguza ama kumaliza kabisa matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto likiwamo na suala la mimba na ndoa za utotoni, kwa kusimamia hata sheria za kimila kwa kuwatenga wale ambao
bado wanaendekeza vitendo hivyo.

Kwa upande wake Ofisa elimu wa kata ya Usanda Sospeter Kasonta, amelipongeza Shirika hilo la Agape ambalo limekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya elimu na afya, kwa kuibadilisha jamii kupenda kusomesha watoto wao pamoja na wanafunzi wenyewe kujitambua, ambapo ufaulu wa wanafunzi umeongezeka hasa wa kike tofauti na
kipindi cha nyuma.

Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho akiwemo Daudi Shija kutoka kitongoji cha Uswahilini  amesema mafunzo hayo watayatumia vizuri na kuleta matokeo chanya ndani ya jamii, ili kupunguza matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mratibu wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga akizungumza katika kikao hicho ambapo amewataka wenyeviti wa vitongoji kata ya Usanda na waelimishaji rika, kuwa elimu ambayo wameipata ya kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto wakaitumie vizuri kuisambaza kwa wananchi ili kuibadilisha na kuachana na vitendo hivyo vya ukatili likiwamo na suala la kuozesha watoto wa kike ndo za utotoni. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
 Mratibu wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga,amewataka wenyeviti wa vitongoji Kata hiyo ya Usanda na waelimishaji Rika, pia wakatoe elimu kwa jamii namna ya kuvunja ukimya na kuzungumza na watoto wao hasa wa kike kuacha mapenzi wakiwa katika umri mdogo pamoja na kuwa elezea madhara yake.
 Mtendaji wa Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Emmanuel Maduhu, akiwataka wenyeviti wa vitongoji kwenye Kata hiyo, kuitumie kikamilifu elimu ambayo wameipata kutoka Shirika hilo la Agape kutokomeza kabisa matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto likiwamo na suala la mimba na ndoa za utotoni, na ikibidi hata watumie sheria za kimili kwa kuwatenga wale ambao ni wagumu kubadilika.


 Wenyeviti wa vitongoji, waelimishaji rika, wazee maarufu na wa kimila wakisikiliza elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye kata hiyo ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

 Wazee maarufu na wa kimila katika kata ya Usanda wakiwa kwenye kikao cha shirika la Agape cha kuwajengea uwezo namna ya kupambana kutokomeza matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na tatizo la mimba na ndoa za utotoni.
 Afisa elimu wa kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sospeter Kasonta, akilipongeza Shrika la Agape kwa kazi nzuri ambayo limeifanya kwenye kata hiyo, ambapo wameleta mabadiliko makubwa sana kwenye sekta ya elimu kwa kuongeza ufaulu hasa kwa wanafunzi wa kike.
 Afisa elimu wa Kata ya Usanda halmshauri ya wilaya ya Shinyanga Sospeter Kasonta, akiwataka wenyeviti wa vitongoji kwenye kata hiyo wakayaendeleze yale ambayo yalianzishwa na Shirika hilo la Agape, ikiwemo kutokomeza utoro wa reja reja kwa wanafunzi kwa kuwafuatilia hadi kwenye kaya zao wale wanafunzi ambao wanaonekana mitaani na kutokwenda shule.
 Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Elizabeth Mweyo, akitoa elimu ya ukatili kwa wenyeviti hao wa vitongoji na madhara yake, na kuwataka wakaitumie vizuri ndani ya jamii katika kuleta matokeo chanya na hatimaye kutokomeza vitendo hivyo hasa kwa wanawake na watoto ambao waathirika wakubwa.

 Wenyeviti wa vitongoji, waelimishaji Rika, wazee maarufu na wakimila  wakiendelea kusikiliza elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye kata ya Usanda
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
 Elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto  ikiendelea kusikilizwa.
  Elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto  ikiendelea kusikilizwa.
  Elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto ikiendelea kusikilizwa.
 Wenyeviti wa vitongoji, waelimishaji rika, wazee maarufu na wa kimila  wakiendelea kusikiliza elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na  kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye kata hiyo ya Usanda  halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
 Elimu ya ukatili ikiendelea kusikilizwa.
 Washiriki wa kikao hicho cha kupinga ukatili kwa wanawake na watoto kwenye kata ya Usanda wakichukua kumbukumbu za kwenda kuzitumia katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya kutomoeza ukatili huo likiwamo na suala la mimba na ndoa za utotoni.
 Wenyeviti wa vitongoji, waelimishaji Rika, wazee maarufu na wa kimila  wakiendelea kusikiliza elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
 Mwenyekiti wa Kitongoji cha Uswahilini kata ya Usanda Daudi Shija, akielezea namna Shirika hilo la Agape lilivyosaidia kuibadilisha jamii katika kupunguza masuala ya ukatili kwa wanawake na watoto na kuahidi kuendeleza gurudumu hilo ikiwa elimu ambayo amepatiwa itamsaidia sana kuendeleza mapambano hayo ya kupinga ukatili.
 Mwenyekiti wa Kitongoji cha Butwale Paulo John, akielezea namna Shirika hilo la Agape lilivyosaidia kupunguza matukio ya ukatili ndani ya jamii likiwamo na suala la utekelezaji wa watoto ambapo sasa hivi wazazi wanaishi na watoto wao pamoja na kuwapeleka shule, wakiwamo na watoto walemavu ambao walifichwa lakini kwa sasa wapo shule.
 Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwagala kata ya Usanda Ramadhani Kulwa,akielezea namna walivyo saidiwa na shirika hilo la Agape kupatiwa elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto ambapo wao kama viongozi walishapiga marufuku watoto wa kike kwenda kucheza shoo kwenye harusi, ili kuwaepusha na vishawishi vya kutongozwa na kuambulia ujauzito.
 Mwenyekiti wa kitongoji cha Manyada kata ya Usanda John Masanja naye akitoa ushuhuda namna shirika hilo la Agape lilivyosaidia kupunguza matukio ya ukatili, ambapo na wao wamekuwa wakifuata nyayo hizo na kufanikiwa kutatua baadhi ya matukio hayo ya ukatili ndani ya jamii.
Awali katikakati ya kikao washiriki wakinyoosha mikono ya utayari wa kuendeleza mapambano ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ndani ya jamii.
Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Share:

The key requirements for carrying on the jkt camps – For jkt Selected students 2019

vifaa vya kwenda navyo jkt mujibu wa sheria – National Services JKT 2019 , vitu vya kwenda navyo jkt 2019, post za jkt 2019, mujibu wa sheria 2019, JKT 2019, JKT selection 2019 . jkt 2019, , jkt mafinga 2019 , kidato cha sita jkt 2019, mahitaji muhimu jkt 2019, The list of Form Six leavers joining the  – jkt selection 2019, waliochaguliwa jkt form six 2019, jkt form six 2019 , form 6 jkt 2019, – Check majina ya waliochaguliwa jkt 2019. JKT selection 2019 intake – www.jkt.go.tz 2019

Below are the comprehensive jkt checklist, covering all the things that any Form six student could possibly need during JKT national service training course….

Take a good look at the whole checklist on the pdf document below

SEE ALSO

The post The key requirements for carrying on the jkt camps – For jkt Selected students 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Mo Dewji Aipongeza Yanga...Amwaga Bodaboda Kwa Wachezaji Na Kutangaza Hatma Ya Kocha.

Na Bakari Chijumba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Timu ya SimbaSC , Mo Dewji amesema baada ya Kocha Mkuu wa Klabu hiyo,Patrick Aussems kutimiza malengo yaliyowekwa na Klabu,tayari bodi imepanga kukaa naye na kumuongezea mkataba mpya ili aendelee kuifundisha Simba SC.

Kuhusu ahadi ya Milioni 5 kwa kila mchezaji baada ya ubingwa, Mo Dewji amesema hakutoa ahadi hiyo bali alisema atatoa zawadi ya Pikipiki(Boxer) kwa kila mchezaji na tayari amewapa ili kuinua vipato vyao,MO amesema wakiweka watu wa kuziendesha zitawaingizia kipato.

Dewji amesema ameshaongea na viongozi wa klabu ya DC United ya Marekani na kuwaomba wakafanye maandalizi ya msimu ujao huko pia wacheze nao na timu nyingine za LMS au kwenda nchini Ureno ili wakacheze na timu za huko.

Katika hatua nyingine MO ameipongeza Klabu ya Yanga kwa kuongeza ushindani kwenye Ligi.

"Naipongeza Yanga SC kwa kuleta ushindani mkubwa kwenye Ligi yetu na nichukue fursa hii kuwapongeza viongozi wapya wa Yanga SC na niwaombee wajipange ili waweze kufanikiwa, najua msimu ujao utakuwa mgumu sana"amesema Mo na kuongeza;

''Kwenye usajili tupo makini sana,leo tunapata ripoti ya kocha juu ya wachezaji wa nyumbani anaowataka,pia katika wachezaji 10 wa kigeni mpaka leo usiku kocha atatuambia anabaki na nani na nani waondoke..Simba itakuwa kwenye soko la kushindana na timu kama Mazembe na Al Ahly"

''Katika kusajili, kuna wachezaji wengine tutawatoa kwa mkopo lengo ni kutengeneza timu yenye ushindani zaidi na tutajitahidi usajili wetu uende sawa na vilabu vikubwa Afrika ili tukafanye vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa''


Share:

Waziri Mpina Atoa Onyo kwa Watumishi Wanaokamata Mifugo na zkuishikilia Hadi Kufa ikiwa Mikononi mwao

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Mpina  amesema serikali itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria  watu wanaofanya ukatili kwa wanyama ambapo amesema ifikapo tarehe 1.Julai ,2019  watendaji wanaoshikilia mifugo hadi kufa ikiwa mikononi mwao  watashughulikiwa. 

Mhe.Mpina amesema hayo leo Mei 22,2019 Bungeni jijini Dodoma  ambapo amesema  mifugo ni rasilimali za nchi kama rasilimali nyingine na wizara yake haitavumilia kuona mtendaji wa Serikali akishikilia mifugo mpaka ina kufa kwa kigezo cha kufuata sheria kwani hata mifugo nayo ina sheria zake. 

Awali ,Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega wakati akijibu swali la mbunge wa Wa Morogoro Kusini  Prosper Mbena aliyehoji  juu ya ukatili wa wanyama kushamiri nchini ,chama cha kuzuia ukatili wa wanyama Tanzania ,TSPCA  kina shirikiana kwa kiasi gani na Serikali ili kuzuia ukatili ,Mhe.Ulega amezitaja sheria za wanyama pindi wanapokamatwa ikiwa ni pamoja na kupatiwa malisho,maji na chanjo. 

Kuhusu uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata na kusindika nyama katika maeneo yaliyo karibu na wafugaji ili kupunguza ukatili wa wanyama pindi wanaporundikwa kwenye magari wakati wanaposafirishwa Kwenda Dar Es Salaam  kwa ajili ya kuchinjwa,Mbunge wa Msalala  Ezekiel Maige  amehoji lini serikali itaanzisha viwanda  katika maeneo mbalimbali ya wafugaji nchini ikiwa ni pamoja na Shinyanga. 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema mchakato wa kufufua viwanda vya kuchakata na kusindika  nyama nchini upo palepale  na kinachotakiwa ni kupata mwekezaji aliyejipanga vizuri.

Hata hivyo,Serikali inashirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali  kama TSPCA  katika kudhibiti vitendo vya kikatili kwa wanyama  kwa kuzingatia sera ya mifugo  ya mwaka 2006  na sheria ya Ustawi wa wanyama ya mwaka 2008 kwa kuelimisha jamii. 

Mwaka 2018 jumla  ya Makosa  3,542 kwa kosa la ukatili wa wanyama yaliripotiwa  ambapo ni  ng’ombe  847 ,mbuzi na kondoo 1,578,nguruwe 88,kuku 539 na punda 490. .
 


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger