Wednesday, 22 May 2019

Rais Magufuli Atoa Heshima Za Mwisho Kwa Mwili Wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Athumani Hassan Ngwilizi Lugalo Jijini Dar Es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiandika katika kitabu cha maombolezo mara baada ya kuwasili katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 kwaajili ya kuaga mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Athuman Hassan Ngwilizi aliyefariki dunia hospitalini hapo Mei 20,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Athuman Hassan Ngwilizi katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 ,Marehemu alifariki dunia hospitalini hapo Mei 20,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Shekhe Mkuu wa Dsm Alhaji Mussa Salum baada ya kuwasili katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 kwaajili ya kuaga mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Athuman Hassan Ngwilizi aliyefariki dunia hospitalini hapo Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Athuman Hassan Ngwilizi katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 ,Marehemu alifariki dunia hospitalini hapo Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameungana na Viongozi wengine na ndugu kusindikiza kwenye gari mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Athuman Hassan Ngwilizi kutoka katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 kuelekea Mlalo Lushoto Mkoani Tanga kwaajili ya mazishi ,Marehemu alifariki dunia hospitalini hapo Mei 20,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa Mjane wa Marehemu mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Athuman Hassan Ngwilizi katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 ,Marehemu alifariki dunia hospitalini hapo Mei 20, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa Familia ya  Marehemu mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Brigedia Jener ali Athuman Hassan Ngwilizi katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 ,Marehemu alifariki dunia hospitalini hapo Mei 20, 2019.

PICHA NA IKULU


Share:

Picha : WAANDISHI WA HABARI MTANDAONI 'BLOGGERS/ONLINE TV' WAPEWA MAFUNZO YA HAKI ZA KATIBA NA SHERIA ZA HABARI


Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania wamepatiwa mafunzo kuhusu haki za Katiba na sheria  za habari ikiwemo Sheria ya Takwimu 2015, Sheria za Huduma za Vyombo vya Habari 2016 pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 ili kuwajengea uwezo wa kuandika  kwa weledi habari za utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu.


Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza Mei 21,2019 yamefanyika katika Ukumbi wa Morena Hoteli jijini Dodoma, yameandaliwa na 
Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia ya Klabu Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media).

Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) unafadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT ambapo utatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mei 21,2019: Wakili James Marenga akitoa mada kuhusu sheria ya Maudhui Mtandaoni 'The Electronic and Postal Communications (Online Content) Regulations ,2018' wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari mtandaoni 'Bloggers/Online Tv' 23 kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania.

Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa ukumbini.
Wakili James Marenga akiendelea kutoa mada ukumbini.
Wakili James Marenga akitoa mada ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
Meneja Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania, Wakili Daniel Lema akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Mei 22,2019: Wakili James Marenga akitoa mada kuhusu sheria ya huduma ya vyombo vya habari 'The Media Services Act No. 12,2016' wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari mtandaoni 'Bloggers/Online Tv' 23 kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Wshiriki wa mafunzo hayo wakiandika dondoo muhimu wakati Wakili James Marenga akitoa mada ukumbini.
Kushoto ni Albert G. Sengo (GSengo Blog) na Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko wakiwa ukumbini.
Picha ya pamoja Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) 23 kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Picha ya pamoja waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) 23 kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania.

Share:

MWANAHARAKATI MAARUFU WA USHOGA AFARIKI DUNIA

Mwanaharakati wa kupigania haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya Binyavanga Wainaina amefariki dunia. Nduguye James Wainaina amethibitisha kwa BBC.

Mwanaharakati huyo amefariki akiwa na umri wa miaka 48.

Nduguye Binyavanga amsema kuwa familia yake inataka kusherehekea maisha yake , baada ya mwandishi huyo wa Kenya kufariki usiku wa Jumanne alipokuwa akiugua

''Tunasherehekea maisha yake, tunaangazia swala hili kibinaadamu .Turuhusu ule ubinaadamu kung'aa, kwa kuwa watu wanaomboleza'', Nduguye James alizungumza na mwadishi wa BBC Peter Mwangagi.

''Alifariki jana usiku katika hospitali moja alipokuwa akiugua. Lakini hicho ndicho kilicho kwa sasa tunajaribu kukubali habari hiyo'', aliongezea.

James amesema kuwa ijapokuwa habari za kifo cha nduguye tayari zimejaa katika mitandao ya kijamii , familia inajaribu kuwaelezea wale wasiojua.

James alisema kuwa Binyavanga hajakuwa katika afya nzuri katika kipindi cha miaka michache iliopita na hali yake ilikuwa imedorora katika kipindi cha kati ya miezi miwili au mitatu.

Nduguye hatahivyo alikataa kufichua ugonjwa uliosababisha kifo chake.

James anasema kwamba familia yake ilikuwa ikitumai kwamba Binyavanga atapona lakini hilo halikufanyika licha ya juhudu za madaktari.

Wainaina alikuwa mshindi wa tuzo ya Caine na aliorodheshwa na gazeti la Times magazine miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani 2014.

Amefariki siku mbili tu kabla ya mahakama nchini Kenya kutoa uamuzi wa iwapo itafutilia mbali sheria za kikoloni ambazo zinaharamisha haki za wapenzi wa jinsia moja.

Binyavanga Wainaina, alikuwa miongoni mwa Wakenya wa kwanza kujitokeza hadharani na kusema kuwa yeye hushiriki mapenzi ya jinsia moja.

Tangazo hilo lilimfanya Binyavanga kuwa mmoja wa waafrika mashuhuri kujitokeza hadharani.

Alifichua hali hii katika taarifa yake kupitia kwa mtandano wa kijamii wa Twitter iliowiana na siku ya kuzaliwa kwake.

Kifo chake kinajiri wakati ambapo kuna mjadala mkali nchini Kenya na katika baadhi ya mataifa ya Afrika kuhusiana na suala la haki za wapenzi wa jinsia moja.

Uamuzi wa Binyavanga kujitokeza hadharani ulipokelewa kwa hisia mbali mbali nchini Kenya. Kuna wale waliompongeza ingawa baadhi walihisi huenda jamii ikamtenga.

Mwaka 2018 Binyavanga Wainaina ambaye ni mwandishi maarufu wa vitabu aliwashangaza Wakenya wengi alipotangaza atafunga ndoa na raia wa Nigeria.

Alinukuliwa akisema: Nilimuomba mpenzi wangu tufunge ndoa wiki mbili zilizopita. Na alikubali, karibu mara moja. Yeye ni raia wa Nigeria. Tutakuwa tunaishi Afrika Kusini ambapo atakuwa anahudhuria masomo mwaka ujao. Tutaoana huko, mapema mwaka ujao," Bw Wainaina aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.


Aliahidi kwamba kutakuwa na karamu kubwa kwa Wakenya jijini Nairobi

Baadaye, aliongeza kwamba ana uhakika kutakuwa na sherehe kubwa kwa Wanigeria pia.

"Hakuna lililonishangaza zaidi kuliko kupendana na mtu huyu, ambaye ni mpole na mwenye moyo wa ukarimu'', alinukulkiwa akimsifu ,mpenzi wake.

"Najichukulia kuwa mwenye bahati sana kwamba yeye ananipenda na tulipendana majuzi tu, lakini tumefahamiana na tumekuwa tunachumbiana tangu 2012."

Binyavanga ni nani?
Kenneth Binyavanga Wainaina ambaye ana umri wa miaka 48 ni mwandishi wa vitabu na mwanahabari.

Mwaka 2002 alishinda tuzo mashuhuri ya uandishi kuhusu Afrika ya Caine.

Jarida la Time mwaka 2014 lilimuorodhesha Wainaina kuwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani.
Mnamo 1 Desemba, 2016 alitangaza kupitia Twitter Siku ya Ukimwi duniani kwamba alikuwa ana virusi vya Ukimwi.
CHANZO - BBC
Share:

Tundu Lissu Kurejea Nchini Septemba 7

Mbunge Tundu Lissu amesema atarejea nchini Septemba 7, 2019, siku ambayo itatimia miaka miwili tangu aliposhambuliwa kwa risasi jijini Dodoma Septemba 7, 2017, Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji kwa matibabu alishambuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Mara baada ya kushambulia, mwanasiasa huyo  alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na usiku wa siku hiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikopata matibabu hadi Januari 6, 2018 na kuhamishiwa  Ubelgiji kuendelea na matibabu zaidi.

Lissu ambaye kwa sasa anatembea kwa msaada wa gongo moja akizungumza na wapiga kura wake mwishoni mwa wiki kupitia simu ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema anarudi nchini Septemba 7, 2019.

Amesema katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Oktoba, 2019 atakuwepo Tanzania.


Share:

Irani Yakataa Mazungumzo na Marekani

Rais Hassan Rouhani wa Iran amekataa mazungumzo na Marekani, baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa Iran itampigia simu na kuomba kufanya mazungumzo "iwapo na wakati watakapokuwa tayari". 

Iran na Marekani zimeendeleza vita vya maneno katika wiki za karibuni wakati Marekani ikiimarisha vikwazo na kile inachosema ni lengo la kuishinikiza Iran kufanya makubaliano mengine mbali na masharti ya mkataba wake wa nyuklia wa 2015.

Shirika la habari la serikali ya Iran limemnukuu Rouhani akisema kuwa hali ya sasa sio nzuri kwa mazungumzo na chaguo lao kwa sasa ni kuyakataa. 

Trump alisema jana kuwa Iran itakabiliwa vikali kama itajaribu kufanya chochote dhidi ya maslahi ya Marekani katika Mashariki ya Kati. 

Alisema ripoti kuwa Marekani inajaribu kuanzisha mazungumzo na Iran ni za uwongo, lakini akaongeza kuwa Iran itawasiliana nao iwapo, ama lini watakapokuwa tayari. Rouhani amesema Wairan hawatawahi kumpigia magoti mnyanyasaji.


Share:

Marekani yalegeza vikwazo dhidi ya kampuni ya Huawei

Serikali ya Marekani imeondoa kwa muda vikwazo vya kibiashara ilivyoweka wiki iliyopita dhidi ya kampuni ya simu ya China Huawei, hatua inayolenga kupunguza hali ya kuvurugwa wateja wake. 

Hatua hiyo hata hivyo imepuuziliwa mbali na muasisi wa kampuni hiyo anayesema kuwa Huawei ilikuwa imejiandaa kwa hatua ya Marekani. 

Wizara ya Biashara ya Marekani itairuhusu kampuni ya Huawei kununua bidhaa zinazotengenezwa Marekani kwa siku nyingine 90 ili kudumisha mitandao iliyopo na kutoa programu tumishi mpya kwa simu za sasa za Huawei. 

Kampuni hiyo kubwa kabisa duniani ya kutengeneza vifaa vya mawasiliano ya simu bado imezuiwa kununua vifaa kutoka nchini Marekani vya kutengenezea bidhaa mpya bila idhini za leseni ambazo kuna uwezekano kuwa zitakataliwa. 

Serikali ya Marekani ilisema iliweka vikwazo hivyo kwa sababu ya Huawei kujihusisha na shughuli zinazoenda kinyume na usalama wa taifa au maslahi ya sera za kigeni.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 22




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger