Wednesday, 22 May 2019

Irani Yakataa Mazungumzo na Marekani

Rais Hassan Rouhani wa Iran amekataa mazungumzo na Marekani, baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa Iran itampigia simu na kuomba kufanya mazungumzo "iwapo na wakati watakapokuwa tayari". 

Iran na Marekani zimeendeleza vita vya maneno katika wiki za karibuni wakati Marekani ikiimarisha vikwazo na kile inachosema ni lengo la kuishinikiza Iran kufanya makubaliano mengine mbali na masharti ya mkataba wake wa nyuklia wa 2015.

Shirika la habari la serikali ya Iran limemnukuu Rouhani akisema kuwa hali ya sasa sio nzuri kwa mazungumzo na chaguo lao kwa sasa ni kuyakataa. 

Trump alisema jana kuwa Iran itakabiliwa vikali kama itajaribu kufanya chochote dhidi ya maslahi ya Marekani katika Mashariki ya Kati. 

Alisema ripoti kuwa Marekani inajaribu kuanzisha mazungumzo na Iran ni za uwongo, lakini akaongeza kuwa Iran itawasiliana nao iwapo, ama lini watakapokuwa tayari. Rouhani amesema Wairan hawatawahi kumpigia magoti mnyanyasaji.


Share:

Marekani yalegeza vikwazo dhidi ya kampuni ya Huawei

Serikali ya Marekani imeondoa kwa muda vikwazo vya kibiashara ilivyoweka wiki iliyopita dhidi ya kampuni ya simu ya China Huawei, hatua inayolenga kupunguza hali ya kuvurugwa wateja wake. 

Hatua hiyo hata hivyo imepuuziliwa mbali na muasisi wa kampuni hiyo anayesema kuwa Huawei ilikuwa imejiandaa kwa hatua ya Marekani. 

Wizara ya Biashara ya Marekani itairuhusu kampuni ya Huawei kununua bidhaa zinazotengenezwa Marekani kwa siku nyingine 90 ili kudumisha mitandao iliyopo na kutoa programu tumishi mpya kwa simu za sasa za Huawei. 

Kampuni hiyo kubwa kabisa duniani ya kutengeneza vifaa vya mawasiliano ya simu bado imezuiwa kununua vifaa kutoka nchini Marekani vya kutengenezea bidhaa mpya bila idhini za leseni ambazo kuna uwezekano kuwa zitakataliwa. 

Serikali ya Marekani ilisema iliweka vikwazo hivyo kwa sababu ya Huawei kujihusisha na shughuli zinazoenda kinyume na usalama wa taifa au maslahi ya sera za kigeni.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 22




Share:

Tuesday, 21 May 2019

SIMBA SC YATWAA TENA UBINGWA WA LIGI KUU YA BARA


Simba SC wamefanikiwa kutetea taji lao ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Singida United jioni ya leo Uwanja wa Namfua.

Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Patrick Aussems imefikisha pointi 91 baada ya ushindi wa leo katika mchezo wa 36 ikijihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu, kwani hakuna timu inayoweza tena kuwafikia. 

Hilo linkuwa taji la pili mfululizo la ubingwa wa Ligi Kuu kwa Simba SC na la 19 jumla kihistoria baada ya awali kulibeba katika miaka ya 1972, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004, 2007, 2010, 2012 na 2018.

Watani wao, Yanga SC ndio mabingwa mara nyingi zaidi wa Ligi Kuu, mara 26 wakiwa wamebeba taji hilo miaka ya 1968, 1969, 1970, 1971, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2008, 2009, 2011, 2013, 2015, 2016 na 2017.

Timu nyingine zilizowahi kubeba taji hilo ni Cosmopolitan 1967, Mseto SC ya Morogoro 1975, Pan African 1982, Tukuyu Stars ya Mbeya 1986, Coastal Union ya Tanga 1988, Mtibwa Sugar mara mbili 1999 na 2000 na Azam FC 2014.

Katika mchezo wa leo, mabao ya SImba SC yalifungwa washambuliaji wake tegemeo, Meddie Kagere kutoka Rwanda kipindi cha kwanza na mzawa, John Raphael Bocco kipindi cha pili.

Kagere alifunga bao lake dakika ya tisa tu akitumia makosa ya beki Kennedy Wilson Juma kuzubaa na mpira kufuatia krosi ya beki wa kushoto wa Simba SC, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye pia ni Nahodha Msaidizi wa klabu. 

Nahodha John Bocco akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 60 akimalizia krosi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi aliyenzishwia mpira wa kurushwa na Tshabalala. 

Hata hivyo, bao hilo kidogo lilikuwa la utata, kwani kwani refa Shomary Lawi kutoka Kigoma aliwaruhusu Simba kuanza mpira wakati kipa wa Singida United, Said Saleh Lubawa akiwa nje anaugulia maumivu baada ya kuumia wakati akiokoa.

Wachezaji wa Singida United walibishana na refa kwa dakika mbili kabla ya mchezo kuendelea, huku kipa Lubawa akibebwa mabegani kutolewa nje nafasi yake ikichukuliwa na David Kissu.

Kikosi cha Singida United kilikuwa; Said Lubawa/David Kissu dk66, Frank Mkumbo, Gilbert Mwale, Salum Kipaga, Kennedy Wilson, Rajab Zahir, Boniface Maganga/Mathew Michael dk78, Issa Makamba, Jonathan Daka, Habib Kyombo na Geoffrey Mwashiuya/Assad Juma dk58.

Simba SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Yussuf Mlipili, Erasto Nyoni, James Kotei, Muzamil Yassin, Haruna Niyonzima/Hassan Dilunga dk79, John Bocco, Meddie Kagere/Clatous Chama dk85 na Emmanuel Okwi/Jonas Mkude dk75.
Share:

WAANDISHI WA HABARI RADIO ZA KIJAMII WATEMBELEA OFISI ZA IDARA YA HABARI - MAELEZO DODOMA

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO anayeshughulikia Habari na Picha, Rodney Thadeus (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waaandishi wa Habari za Radio za Kijamii walipotembelea Idara ya Habari –MAELEZO kwa lengo la kujifunza leo Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa utendaji kazi wao. (Picha na Frank Shija)
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO anayeshughulikia Habari na Picha, Rodney Thadeus akizungumza na Waaandishi wa Habari wa Redio za Kijamii walipotembelea kujifunza shughuli za Idara ya Habari leo Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa utendaji kazi wao. Kutoka kulia ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine (SAUT), Dotto Bulendu na Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Abuu Kimario. Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Habari Tanzania (TADIO), Prosper Kwigize akielezea jambo wakati wa ziara ya Waandishi wa Habari wa Radio za Kijamii katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO kwa ajili ya kujifunza shughuli za Idara hiyo leo Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa utendaji kazi wao. Kutoka kulia ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine (SAUT), Dotto Bulendu, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO anayeshughulikia Habari na Picha, Rodney Thadeus na Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Abuu Kimario. Afisa Habari wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bi. Beatrice Lyimo akifafanua kuhusu taratibu za namna ya kupata Vitambulisho vya Waandishi wa Habari “Press Card” wakati ziara ya Waandishi wa Habari wa Radio za Kijamii kwa lengo la kujifunza shughuli za Idara hiyo leo jijini Dodoma. Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Radio ya Kijamii Sibuka FM kilichopo Maswa Mkoani Simiyu, Nicholaus Machunda akionyesha Kitambulisho cha Uandishi wa Habari “Press Card” mara baada ya kukamilisha taratibu na kukabidhi wakati wa ziara ya Waandishi wa Habari wa Radio za Kijamii katika Ofisi ya Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa utendaji kazi wao. Baadhi ya Waandishi wa Habari toka Radio za Kijamii wakifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO anayeshughulikia Habari na Picha, Rodney Thadeus wakati wa ziara yao ya kujifunza namna Idara ya Habari – MAELEZO inavyofanya kazi leo Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa utendaji kazi wao. Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Radio ya Kijamii Pambazuko FM ya Ifakara Morogoro, Amina Mrisho akichangia mada wakati wa ziara ya Waandishi wa Habari wa Radio za Kijamii katika Ofisi ya Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa utendaji kazi wao. Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO anayeshughulikia Habari na Picha, Rodney Thadeus (kushoto) akiagana na Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine (SAUT), Dotto Bulendu mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waaandishi wa Habari za Radio za Kijamii walipotembelea Idara hiyo kwa lengo la kujifunza leo Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa utendaji kazi wao. Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO anayeshughulikia Habari na Picha, Rodney Thadeus (kulia) akiagana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Habari Tanzania (TADIO), Prosper Kwigize mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waaandishi wa Habari za Radio za Kijamii walipotembelea Idara hiyo kwa lengo la kujifunza leo Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa utendaji kazi wao.
Share:

WACHUNGAJI WA KANISA LA KKKT TANZANIA WALA NONDO MAREKANI


Wachungaji watatu kutoka KKKT DMP na mmoja kutoka KKKT
Dayosisi ya Ziwa Victoria Shinyanga wamehitimu katika Chuo Kikuu cha Luther Seminary Minnesota nchini Marekani tarehe 19/05/2019 kama ifuatavyo:- Rev. Dr. Ernest William Kadiva ametunukiwa Phd - Doctor of Ministry, Wengine wametunukiwa Master of Arts degree nao ni Rev. Kishe Dismas Mhando - na Rev. Kaanasia Geofrey Msangi, pia Rev. Martha Ernest Ambarang'u wa Dayosis ya Ziwa Victoria Shinyanga ametunukiwa Masters of Arts degree katika mahafali ya 150 iliyofanyika Central Lutheran Church, Minneapolis na kuhudhuriwa na mamia ya wageni kutoka nchi mbalimbali na kutoka majimbo mbalimbali ya
Marekani. Picha kwa hisani ya Noah William Kadiva akiwa Minnesota, Marekani.
Ndugu, jamaa na marafiki wakifurahia baada ya Rev. Dr. Ernest William Kadiva kutunukiwa Phd - Doctor of Ministry, na wengine waliotunukiwa Master of Arts degree Rev. Kishe Dismas Mhando - na Rev. Kaanasia Geofrey Msangi, pia Rev. Martha Ernest Ambarang'u wa Dayosis ya Ziwa Victoria Shinyanga.
Rev. Dr. Ernest William Kadiva akitunukiwa
Phd - Doctor of Ministry baada ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Luther Seminary Minnesota kwenye sherehe
zilizofanyika Central Lutheran Church, Minneapolis, nchini Marekani
Share:

Waziri Mkuu Aongoza Mazishi Ya Askofu Mmole Mtwara

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania wote wamuenzi marehemu Askofu Mstaafu Gaberiel Mmole (80) wa Jimbo Katoliki Mtwara kwa wema, upole  na utumishi mwema aliouonesha wakati wote wa maisha yake.

Ametoa wito huo leo (Jumanne, Mei 21, 2019) wakati wa mazishi ya Askofu Mmole yaliyofanyika katika Kanisa Katoliki Mtwara na kuhudhuriwa na viongozi, waumini wa Kanisa Katoliki pamoja na wakazi wa mkoa wa Mtwara

Askofu Mmole alizaliwa Januari Mosi, 1939 katika Parokia ya Nangoo, ambapo alibatizwa na kupata kipaimara Oktoba 5, 1952. Mwaka 1971 alipata daraja ya upadre na kuwa Askofu kuanzia mwaka 1988, alifariki Mei 15, 2019 Mkoani Mtwara baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Maeneo aliyoyatumikia tangu apate daraja la padri ni Paroko msaidizi wa Mnero (1972), Pastoral Institute GABA-Uganda (1973), Gombera Namupa seminari (1974 hadi Mei 1988), alitangazwa kuwa askofu wa Jimbo la Mtwara Machi 12, 1988 na alisimikwa kuwa askofu wa Jimbo la Mtwara Mei 25, 1988.

Mwaka 1951 hadi 1954 alipata elimu ya singi katika shule ya msingi Ndanda, 1955 alisoma Nyangao Middle School, 1956 akahamia Lukuledi ambako alihitimu 1958. Alienda chuo cha ualimu Peramiho 1959 hadi 1960, ambapo 1962 alijiunga na seminari ndogo ya Namupa na alihitimu 1964.

1965 hadi 1966 alichukua masomo ya falsafa kwenye seminari kuu ya Peramiho na mwaka 1967 hadi 1971 alichukua masomo ya theolojia katika seminari hiyo hiyo ya Peramiho. 1971 alifanya mitihani ya Baccalaureate inayotoka chuo kikuu cha Kipapa Urbaniana Roma na kupata shahada ya theolojia.

Ibada ya mazishi imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Mhashamu Askofu Damian Dallu ambaye alitumia muda huo kuwaasa Watanzania kuishi katika maadili mema na kuheshimiana.

Waziri Mkuu amesema enzi za uhai wake Askofu Mmole alitoa kipaumbele katika masuala muhimu ya maendeleo ya jamii ikiwemo elimu ambapo alisaidia sana watawa waliomaliza darasa la saba na kuwasaidia wajiunge na shule za sekondari.

“Hata uanzishwaji wa chuo kikuu cha STEMMUCO ambacho ni tawi la SAUT hapa Mtwara ni moja ya jitihada zake alizozifanya katika kuhakikisha anawapa elimu bora vijana na jamii.

Kifo chake ni pigo kubwa kwa Taifa kwa sababu tumepoteza kiongozi wa kiroho aliyesimamia kwa uadilifu ustawi wa jamii ya Kitanzania.”

Kwa upande wake, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Mhashamu Askofu Gervas Nyaisonga wa Jimbo Kuu la Mbeya amesema wamepata simanzi kubwa kufuatia kifo cha Askofu Mmole kwani walitegemea hekima zake katika Baraza la Maaskofu.

Ameongeza kuwa Askofu Mmole alikuwa kielelezo cha dhamira njema na alilitumikia kanisa katika hali yoyote, hivyo yatupasa kumuombea apumzike kwa amani.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwaaliwashukuru viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani Mtwara kutokana kwa ushirikiano mzuri anaopata unaomwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na maelfu ya wananchi, maaskofu wa majimbo mbalimbali nchini, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa, Waziri wa Nchi OR-Utumishi na Utawala Bora Mheshimiwa Huruma George Mkuchika.
 


Share:

Uharibifu wa mazingira waishusha Tanzania hadi nafasi ya 8 vivutio vya dunia

Waziri wa Malisili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangala amesema Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya pili mpaka ya nane katika vivutio vya dunia sababu akizitaja ni uharibifu wa mazingira.

Ameeleza hayo leo Jumanne Mei 21 bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Vunjo James Mbatia (NCCR Mageuzi).

Katika swali lake Mbatia amedai kwamba mwaka 1984 Tanzania ilikuwa inashika nafasi ya pili katika vivutio vinavyochea utalii pamoja na miundombinu.

Mbunge huyo amehoji Je kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya ngapi na miundombinu inayochochea inashika nafasi ya ngapi?

Akijibu swali hilo Kingwangala amesema utafiti unaonesha kwamba Tanzania imeshuka katika vivutio  kutoka  nafasi ya pili mpaka ya nane sababu kubwa ni uharibifu wa mazingira.


Share:

Rais Magufuli Atoa Maagizo Mazito kwa Mashirika Yasiyotoa Gawio kwa Serikali

Rais Magufuli ameyataka mashirika na Taasisi zinazotakiwa kutoa gawio kulingana na sheria kuhakikisha hadi kufikia mwei Julai mwaka huu wawe wameshakamilisha zoezi hilo.

Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 21 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza katika hafla ya kukabidhi gawio kwa serikali kutoka shirika la masiliano Tanzania TTCL ambapo ameagiza mashirika hayo kuchukuliwa sheria iwapo watashindwa kutekeleza agizo hilo.

“Mashirika ambayo hayatoi gawio kila siku ni hasara tu itabidi kutumia sheria na ikishindikana yaondoke maana haiwezekani wao wanaangalia wenzao wakati walipewa mashirika hayo sawa na bure hivyo kabla ya mwezi Julai mashirika yote 253 yanatakiwa yawe yameshafanya hivyo ” amesema.

“Fedha hizi ni ndizo zinazosaidia katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile ujenzi wa barabara, hospitali shule hivyo kwa wale wote wanaotakiwa kutoa gawio kulingana na sheria wanapaswa kufanya hivyo,” amesema.

Aidha ametoa wito kwa watanzania kuendela kuliunga mkono shirika la TTCL kwa kusema kuwa ni la nyumbani lakini pia mapato na faida zitakazopatikana zitatumika kuwasaidia watanzania na kwamba ndio nembo pekee ya kumkumbuka baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.


Share:

Rais Magufuli Aiagiza UCSAF Kuiwezesha Miundombinu Ya Mawasiliano TTCL

Na Paschal Dotto
RAIS Dkt. John Magufuli ameitaka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutoa kipaumbele katika uwekezaji wa miundombinu ya mawasiliano kwa Kampuni ya Mawasiliano Nchini (TTCL) ili liweze kumiliki idadi kubwa ya minara ya mawasiliano ya simu  na kumudu ushindani wa soko la mawasiliano nchini. 

Akizungumza katika hafla ya upokeaji wa Gawio la Serikali la Tsh Bilioni 2.1 kutoka TTCL, leo Jumanne (Mei 21, 2019), Rais Magufuli alisema  njia pekee ya kuiendeleza TTCL ni kwa Viongozi na Watendaji wa Serikali kuwa na moyo wa uzalendo wa kusimamia rasilamali za umma ikiwamo za shirika hilo. 

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema TTCL imekuwa ikitumia kiasi cha Tsh Milioni 700-800 kila mwezi kwa ajili ya kukodisha minara ya mawasiliano, wakati Serikali ina mfuko wa mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unaotoa ruzuku kwa makampuni mbalimbali ya mawasiliano kwa ajili ya kujiwekeza katika miundombinu ikiwemo minara ya mawasiliano maeneo mbalimbali nchini. 

“Hili la TTCL kukopa minara katika makampuni mengine halikubaliki,  Serikali ina mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ambao wanatoa ruzuku kwa makampuni mengine ya simu lazima tulitazame upya, nataka sasa TTCL tuwape mitaji ya kutosha ili kuhakikisha kuwa linaendelea kupanua huduma zake kwa Watanzania wengi zaidi” alisema Rais Magufuli. 

Aidha Rais Magufuli aliitaka Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha inaipatia TTCL kiasi cha Tsh Bilioni 30 kilichobaki kati ya Tsh Bilioni 66 ilizotoa katika mwaka wa fedha 2018/19 kwa ajili ya kupanua mtandao wa huduma zake nchini, kwa kuwa Shirika hilo limeonesha mafanikio makubwa zaidi katika kipindi kifupi tangu serikali ichukue uamuzi wa kununua hisa zake kutoka kampuni ya Airtel mwaka 2016. 

Akifafanua zaidi Rais Magufuli alisema Serikali itandelea kuiwezesha TTCL ili iweze kupanua mtandao wa mawasiliano yake nchini, na kuhakikisha kuwa linatekeleza vyema majukumu yake ikiwemo kusimamia mawasiliano ya Kimkakati nchini kupitia Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa kufuatia kupitishwa kwa Sera ya Taifa ya TEHAMA mwaka 2016. 

Kwa upande wake Mkurugenzi  Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema TTCL imeendelea kupiga hatua kubwa zaidi katika utoaji wa huduma ya mawasiliano nchini ambapo katika mwaka 2018/19, shirika hilo limeweza kupata faida ya Tsh Bilioni 8.3 ambapo kiasi cha Tsh Bilioni 2.1 imetoa gawio kwa Serikali. 

“Katika mwaka 2017/18, tulitoa Tsh Bilioni 1.5, lakini kwa mwaka huu tumetoa Tsh Bilioni 2.1 ikiwa ni ongezeko la Tsh Milioni 600, hii imetokana na kuongezeka kwa makusanyo ya mapato yetu kutoka Bilioni 119 mwaka 2017/18 hadi kufikia Bilioni 167 mwaka 2018/19” alisema Kindamba. 

Kwa  mujibu wa Kindamba alisema TTCL pia imeendelea kusimamia majukumu yake ya msingi ya ikiwemo kuimarisha mfumo wa viwango vya huduma kwa mteja, kujenga uwezo wa teknolojia na miundombinu pamoja na kusimamia mkakati wa mawasiliano kupitia Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa. 

Kindammba anasema katika kuwajengea uwezo vijana katika kujiajiri, TTCL kwa kushirikiana na Ofisi ysa Waziri Mkuu imeweza kuajiri vijana 50 waliomaliza vyuo vikuu mbalimbali nchini ambao baadae wataweza kuajiriwa na makampuni mbalimbali ya mawasiliano nchini kwa ajili ya kuongeza mtandao wa utoaji wa huduma ya mawasiliano nchini. 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omary Nundu aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kutokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa kwani katika kipindi cha miaka mitatu, shirika hilo limeweza kupata mafanikio makubwa kutokana na maono na dhamira ya Rais Dkt. John Magufuli   kwa shirika hilo.


Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521


Share:

MAGUFULI : NILETEWE ORODHA YA VIONGOZI WANAOTUMIA LAINI ZA TTCL....HUWEZI KULIPWA MSHAHARA KAMA HUTUMII


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amehoji juu ya Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL, kuwa na idaidi ya watumiaji wa simu wachache huku watumiaji wa simu wakifikia milioni 40 nchi nzima.


Rais Magufuli amezungumza hayo kwenye shughuli ya upokeaji wa gawio kutoka kwa shirika hilo, shughuli ambayo imefanyika katika ofisi za makao yake makuu jijini Dar es salaam.

"Nakumbuka mwaka jana idadi ya wateja walikuwa milion 1.8 lakini mmeongeza hadi kufikia milioni 2, nawapongeza sana lakini narudia wito wangu kwa Watanzania kuwa rudini nyumbani kumenoga", amesema Rais Magufuli.

"Pamoja na kwamba mmefanya mafanikio makubwa, bado mna safari ndefu ili mufikie kuitwa Shirika la Mawasiliano la Taifa, mnafahamu watu wenye simu nchini wanafikia milioni 40 nyinyi mna watu Mil. 2.2 maanake soko lenu ni chini ya asilimia tano hamna budi kuongeza bidii", ameongeza.

"Naomba niletewe orodha ya viongozi ambao wanatumia laini za TTCL na sio ziwepo tu bila kutumika, huwezi kulipwa mshahara wa serikali na hutumii mtandao huo, sijamaanisha msitumie mitandao mingine"- amesema Rais Magufuli.

Katika hafla hiyo Rais Magufuli amepokea gawio la Shilingi bilioni 2 kutoka shirika hilo.

CHANZO - EATV
Share:

TTCL yatoa gawio la Sh Bilioni 2.1 kwa Serikali

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba amesema mwaka huu wanatoa gawio la Sh2.1 bilioni kwa Serikali kutokana na kukua kwa mapato ukilinganisha na mwaka uliopita.

Ameyasema hayo leo Jumanne ya Mei 21, 2019 katika hafla ya utoaji wa gawio kwa Serikali iliyoenda sambamba na uzinduzi wa awamu ya pili ya huduma ya video conference.

Kindamba amesema katika mwaka uliopita mapato yalikuwa Sh119 bilioni na mwaka huu imefikia Sh167 bilioni.

Akizungumza na wafanyakazi wa TTCL, Magufuli amesema: “Tangu Shirikia la TTCL lianze kuendeshwa na wabia wetu, halikuwahi kutoa gawio hata la shilingi tano kwa miaka 15 na lilikuwa likipata hasara ya Tsh bil.15 kwa mwaka, lakini tangu tulirudishe kwenye mikono ya serikali, shirika hili sasa limeanza kutengeneza faida kubwa.

“Niseme kwa uwazi, TTCL mmekuwa mkipigwa vita sana, vita zingine sio za uwazi ni vita vya chinichini, hata leo kuja hapa kulikuwa na mbinu za kijanja-kijanja kunizuia nisije kupokea gawio, na zimechezwa kwelikweli, hii inathibitisha kuwa nyinyi mnastahili,  lazima tuwasaidie.

“Waziri amesema Mfuko wa Mawasiliano upo chini ya wizara yake, pesa zinachangwa na Watanzania na TTCL ni ya Watanzania, kwa nini inakodi minara ya mashirika mengine na kulipia Sh mil. 700 hadi mil. 800?   Kwa nini usitumie pesa hizo kujenga minara ukawapa TTCL moja kwa moja?

“Mashirika mengine yanalipia kodi, lakini TTCL wanalipa kodi na wanalipa gawio, kwa hiyo faida itayakopatikana itakuwa ni ya serikali, hakuna haja ya kuwaacha TTCL wakateseka, huwezi kumuacha mwanao anateseka na chakula unawapa watu wengine,  lazima tuisaidie TTCL.

“Naomba niletewe orodha ya viongozi ambao wanatumia laini za TTCL na sio ziwepo tu bila kutumika, huwezi kulipwa mshahara wa Serikali na hutumii mtandao huo, asije akawa anaandika meseji tu halafu anaicha, nataka ziwe zinatumika, sijamaanisha msitumie mitandao mingine. Msajili wa Hazina hakikisha ifikapo mwezi Julai, mashirika yote 253 nchini ambayo yamekuwa hayatoi gawio kwa serikali, yawe yametoa gawio la sivyo yafungwe.

“Taasisi zilizojiunga kutumia TTCL, ofisi yangu ya rais haikutajwa, chama changu CCM hakikutajwa, inaonekana hawa hata kwenye ofisi yangu wamo. Kama wananisikia ninataka ndani ya mwezi mmoja tuanze kutumia simu za TTCL na wizara nyingine,” amesema.


Share:

Serikali Kupokea Mashine 60 Za Kusafishia Figo Toka Saudi Arabia

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kupokea mashine 60 za kusafishia figo kutoka Nchini Saudi Arabia ambazo zitafungwa katika maeneo ambayo hayafikiki kirahisi.

Ameyasema hayo Leo Jumanne Mei 21 bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto (CCM).

Katika swali lake, Mwamoto  amedai kwamba mashine za kusafishia figo zipo sehemu chache  hapa nchini na wagonjwa wanapata shida.

Aidha Mbunge huyo amedai kwamba Serikali haioni kwamba umefika muda wa kila Hospitali ya Rufaa  kuwa na Mashine  ya kusafishia figo.

Akijibu swali hilo Ummy amekiri  kuona ongezeko ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambapo amedai kwamba Serikali inatarajiwa kupata mashine 60 kutoka Serikali ya Saudi Arabia na kwamba changamoto ambayo itajitokeza ni ukosefu wa wataalamu lakini wameongea na Serikali ya Saudi Arabia kwa ajili ya kupeleka wataalamu kwaajili ya kujifunza.


Share:

Serikali Yaendelea Kuwa Na Dhamira Ya Kuondoa Kero Kwa Wachimbaji Wadogo Wa Madini.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali imedhamiria kuondoa kero  kwa wachimbaji wadogo  wa Madini hapa nchini  ikiwa ni pamoja na kero za kuondolewa na wachimbaji wakubwa   kwani  asilimia kubwa wachimbaji wadogo  ndio wagunduzi wa kwanza kwenye maeneo ya  Madini   . 

Hayo yamesemwa leo Mei 21,2019 bungeni jijini  Dodoma na Naibu waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum  Rhoda Kunchela aliyehoji serikali iko tayari kutatua kero za wachimbaji wadogo  na vibarua ambao wananyanyasika nchini. 

Katika Majibu yake  Naibu Waziri Stanslaus Nyongo amesema viongozi wanaonyanyasa wenzao serikali ipo tayari kuwafutia leseni zao huku akisema kuwa  serikali imekuwa ikiendelea kutatua migogoro ya Wachimbaji wakubwa na wadogo wanaovamia kwenye maeneo yasiyo ya kwao. 

Aidha ,Mhe.Nyongo amefafanua kuwa hata mchimba kokoto ana wajibu wa kulipia kitambulisho cha Wajasiliamali wadogo ambacho kilitolewa na Rais John Pombe Magufuli kwa ajili ya Maendeleo ya nchi. 

Waziri mwenye dhamana ya Madini, Mhe.Dotto Biteko  ametoa wito kwa watozaji wa kodi za madini zilizoondolewa Bungeni waache Mara moja  kwani imebainika kuna baadhi ya maeneo hapa nchini wanaendelea kutoza. 

Migodi yote nchini inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya madini ya mwaka 2010  na marekebisho yake ya mwaka 2017 na kuzingatia kanuni za uchimbaji,usalama,mazingira na Afya kwa wakazi.

 


Share:

Zitto Aiomba Serikali Kuingilia Kati Dhidi Ya Vijana Wanaojipaka Oil Chafu Na Kubaka Wanawake.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe ameiomba Serikali kuingilia kati dhidi ya baadhi ya vijana  wanaokuwa wakijipaka Oil Chafu na kuvamia wanawake  na kuwabaka   jambo ambalo ni Udhalilishaji wa kijinsia . 

Zitto ametoa ombi hilo leo Mei 21,2019  mbungeni jijini Dodoma wakati  akiwasilisha hoja ya dharura ambapo amesema suala la baadhi ya vijana kujipaka oil chafu na kuvamia wanawake  na kuwabaka limekuwa likijitokeza mara kwa mara jimboni kwake ambapo amebainisha kuwa lengo la kujipaka Oil chafu kwa vijana hao ni kurahisisha kuteleza na  kutojulikana sura zao pindi wanapokamatwa. 

Mhe.Zitto amesema mpaka sasa kuna jumla ya Matukio 43 ya unyanyasaji wa wanawake jimboni kwake tangu Mwaka 2016  na wamekuwa wakipokea vipigo mbalimbali kutoka kwa vijana hao wahuni ,hivyo kuna haja ya serikali kuingilia kati ili kulinda usalama wa wanawake. 

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya     ndani ya Nchi,Kangi Lugola amesema serikali ya Tanzania haiwezi kuvumilia vitendo vya kinyama na udhalilishaji kuendelea katika nchi ya Tanzania hivyo atahakikisha  vitendo hivyo vinadhibitiwa  

Hata hivyo,Waziri Lugola amesema kuna baadhi ya Taasisi zimekuwa zikifanya uchunguzi na kukuza mambo na kujenga hofu kwa wananchi hata kama ni madogo  hali na serikali imeshaanza kuziorodhesha taasisi hizo hali iliyoleta mvutano bungeni kati ya Waziri wa Mambo ya ndani na Zitto Kabwe. 

Mwenyekiti wa Bunge Mhe.Nagma Giga amesema suala la ubakaji sio la kuvumiliwa liwe dogo au kubwa hivyo amemwagiza Waziri wa Mambo ya ndani Kangi Lugola kushughulikia jambo hilo.


 


Share:

Polepole Ateuliwa Kuwa Mjumbe Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger