Monday, 20 May 2019

Picha : BLOGGERS WAKUTANA DODOMA KUJADILI MPANGO KAZI WA MRADI WA UTETEZI NA USHAWISHI WA HAKI ZA BINADAMU


Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umewasilisha mpango kazi wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA), unaotekelezwa na waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) hapa nchini kupitia Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC).

Mpango kazi huo umewasilishwa leo Mei 20, 2019 jijini Dodoma kupitia kikao kazi kilichowajumuisha waandishi wa habari wa mitandaoni 23 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.

Akiwasilisha mpango kazi huo, Victor Maleko ambaye ni Afisa Programu kutoka UTPC amesema pamoja na mambo mengine, umelenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mitandaoni kuzifahamu sheria mbalimbali za habari ikiwemo Sheria ya Takwimu 2015, Sheria za Huduma za Vyombo vya Habari 2016 pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 ili kuripoti kwa weledi habari za utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC), Claude Gwandu amewataka washiriki wa mradi huo kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha unafikia malengo yaliyokusudiwa na kwamba chama hicho hakitakuwa tayari kuona mradi unakwamba kutokana na baadhi ya washiriki kutowajibika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa waandishi wa habari wa mitandaoni (Bloggers/ Online TV), Midraji Ibrahim amesema ili mitandao ya kijamii iendelee kuwa na manufaa katika jamii, lazima waandishi wa mitandao hiyo waweke habari zenye maudhui bora ikiwemo utetezi na uchechemuzi wa haki za binadamu kupitia takwimu sahihi.

Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) unafadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT ambapo ulianza mwaka jana 2018 ukitarajiwa kufikia tamati mwaka 2022.
Kikao kazi hicho kimewajumuisha Kadama Malunde (Malunde 1 Blog), William Bundala (Kijukuu Blog), Merina Makasi (Ngasa TV), Mohamed Zengwa (Global TV), Eliya Mbonea (Mtanzania Digital), Midraji Ibrahim (Sub Editor Mwananchi Digital), Mika Ndaba (Ayo TV), James Range (Sub Editor/ Programme Manager Global TV), Frankius Cleophace (Cleo24 News and Dar Mpya), Asha Shabani (Asha Shabani TV), George Binagi (Binagi Media Group), Albert G. Sengo (GSengo Blog).

Wengine ni Francis Godwin (Dar Mpya Blog/ Matukio Daima Blog), Abubakar Kisandu (Kisandu Zenji Blog), Rashid Said Rukungu (Rukungutz Blog CG Online Tv), Edither Karo (Correspondent (Michuzi Blog and Malunde Blog), Joseph Mwaisango (Mbeya Yetu Online TV), Bakari Chilumba (Correspondent Dar Mpya Blog, Millard Ayo, Mpekuzi na Muungwana), Abdulaziz Ahmed (Lindi Yetu Blog na Lindi yetu Online TV), Gabriel Kilamlya (Dar 24 Blog), Ibrahim Said Limala (Correspondent Global TV online), Clavery Christian (Muungwana Blog) pamoja na Hamza Mashore (Ruvuma TV).
Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko akifafanua jambo kwenye kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dodoma. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko akiwasilisha mpango kazi wa utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (Data Drive Advocacy- DDA) kupitia kundi namba tatu linalowajumuisha waandishi wa habari wa mitandaoni (Bloggers).
Mwenyekiti wa Arusha Press Club (APC), Claude Gwandu akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakimsikiliza Mwenyekiti wa Arusha Pres Club (APC), Claude Gwandu kwenye kikao kazi hicho.
Meneja Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania, Wakili Daniel Lema akifafanua jambo kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakimsikiliza Meneja Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania, Wakili Daniel Lema.
Mwenyekiti wa kundi namba tatu linalowajumuisha waandishi wa habari wa mitandaoni (Bloggers/ Online TV), Midraji Ibrahim (aliyesimama), akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wa kikao kazi hicho wakifuatilia mada.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi hicho.
Washiriki wa kikao kazi hicho.
Kikao kazi hicho kimewajumuisha washiriki 23 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Washiriki wakifuatilia mada kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakifuatilia kikao kazi hicho.
Washiriki wakifuatilia mpango kazi wa utekelezaji Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia kundi namba tatu linalowajumuisha waandishi wa habari wa mitandaoni (Bloggers/ Online TV) nchini Tanzania.
Washiriki wa kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dodoma.
Maafisa Programu wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania wakiwa kwenye kikao kazi hicho.


Picha na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Share:

Mdude CHADEMA ataja sababu ya Yeye Kutekwa na Wasiojulikana

Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mdude Nyagali amesema licha ya kupotea hivi karibuni kwa kile alichokidai kuwa ni kutokana na misimamo yake, alifikia hatua ya kukata tamaa ya kuishi.

Mdude ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo ameeleza namna tukio hilo lilivyotokea.
 
"Mimi nilikata tamaa ya kuendelea kuishi na nilishaomba sala ili Mungu aipokee roho yangu, mwacheni Mungu aitwe Mungu, Mungu ni fundi", amesema Mdude.

Aidha Mdude amesema kuwa, "moja ya vitu ambavyo vinashangaza, sikuguswa maeneo mengine zaidi ya kupigwa kichwani lakini cha kushangaza zaidi, baada ya kupata fahamu nikakutwa nina majeraha mikononi na kwa mujibu wa wataalamu ni majeraha yalitokana na kufungwa pingu".

"Vitu vinavyothibitisha kuwa tukio langu la kutekwa ni la kisiasa, ni tweets zangu za mara ya mwisho kuhusu yule wakili aliyepotea", ameongeza Mdude.

Katika mkutano huo na wanahabari Mdude alimwaga machozi wakati akizungumzia namna alivyojikuta yupo porini baada ya waliomteka kumtupa.

“Nilijiuliza kosa langu ni lipi katika nchi hii na kama nina kosa mahakama si zipo kwa nini nifanyiwe hivi,” amesema Mdude huku akilia.

Mapema wiki mbili zilizopita zilienea taarifa juu ya kupotea kwa mwanachama huyo wa CHADEMA, lakini baadaye alipatikana wilayani Mbozi mkoani Mbeya akiwa hajitambui.


Share:

Selasini Amshauri Spika Job Ndugai kuunda kamati ya wabunge ikague maghala ya kuhifadhi korosho ili kubaini nzima na zilizooza.

Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini amemshauri Spika Job Ndugai  kuunda kamati ya wabunge wachache ikague maghala ya kuhifadhi korosho ili kubaini nzima na zilizooza.

Kaimu Mnadhimu huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Mei 20, 2019 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo mwaka 2019/2020.

Huku akimsifu Ndugai kwa kuunda kamati zilizochunguza masuala mbalimbali ikiwemo ya madini ya Tanzanite, Selasini amesema, “Nimeitazama picha ya Rais akiwa ameshika paji la uso anaonyesha kutafakari sana.

“Inaonekana Rais ana mawazo mengi. Kazi ya Bunge hili ni kuishauri Serikali. Kazi ya Bunge hili ni kuisimamia Serikali tunafanya makosa makubwa sana kufanya siasa ndani ya Bunge hili.”

Huku akieleza kuwa yeye ni msafirishaji wa korosho, amesema zao hilo huoza kama  vitunguu

“Nimetangulia kukusifu Spika kama kuna ubishi wa korosho zimeoza ama hazijaoza tengeneza kamati ya watu wachache waende wakague kwenye maghala. Nataka nikwambie kuwa korosho imeoza kwa asilimia 30. Weka watu wakakague maana tukiendelea kuzubaa hata zilizopo zitaoza tutapata hasara zaidi.”


Share:

Mnyika Ataka Baraza la Mawaziri Livunjwe

Mbunge wa Kibamba John Mnyika (Chadema) ,amemwomba Rais Dk.John Magufuli alivunje Baraza la Mawaziri kwa kumshauri vibaya katika suala la Korosho.

Kauli hiyo ameitoa leo bungeni Mei 20 wakati akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, kwa mwaka wa fedha 2018-2019.

Mnyika amesema Baraza la Mawaziri linatakiwa kuwajibishwa kwa kumshauri vibaya Rais Dk.John Magufuli katika suala la Korosho kwani kwa sasa Korosho inaoza kutokana na kukosekana kwa wanunuzi.


Share:

Ufafanuzi Kuhusu Kuwepo Kwa Dawa Za Vidonge Zinazodhaniwa Kutibu Homa Ya Dengue




Share:

Wizara Ya Ardhi Yaandaa Mpango Wa Kuendeleza Maeneo Ya Ukanda Wa reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR)

Na Grace Semfuko,MAELEZO
Wizara ya ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi  inaandaa mpango maalum wa uendekezaji wa Ukanda wa reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR) inayotoka Dar Es Salaam hadi Kigoma unaolenga kuwawezesha wakazi waishio kando ya Reli hiyo kunufaika kiuchumi kupitia ardhi zao kwa kufanya biashara zitakazopangwa kwenye maeneo hayo na ambazo wananchi wataamua kuzifanya.

Lengo la mpango huo  ni kutoa mwongozo wa namna matumizi ya ardhi yatakavyofanyika katika ukanda mzima wa SGR ambao utasaidia kuondoa matumizi yasiyokusudiwa na pia  utasaidia kuondoa migogoro ya adhi na kuibua fursa ambazo bado hazijajulikana na Wakazi wa maeneo hayo.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi wakati akizungumza na wakazi wa Vijiji vya Kwala na Soga vilivyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani kuhusu mpango bora wa matumizi ya ardhi kwenye ukanda wa Reli ya Kisasa ya SGR.

“Kila mahali kutakuwa na fursa za kiuchumi zinazopatikana mahali husika, haimaanishi tunaipanga ile ardhi ili ichukuliwe na serikali, hapana!  wananchi wenyewe watayatumia maeneo yao kwa mpango maalum,  tunataka wananchi wanufaike na ardhi yao” alisema Waziri Lukuvi.

Waziri Lukuvi aliwatoa hofu wakazi wa Maeneo yote ya SGR kuwa Serikali haina mpango na kuchukua ardhi zao na kuwataka pia kutouza ardhi hizo kwani tayari Serikali imeshazipandisha hadhi na thamani.

“Serikali inapanga matumizi bora ya ardhi yote katika Wilaya zote ambapo SGR inapita, tunataka kuwa na ukanda wa maendeleo ya kiuchumi , yaani mtu akifika hapa anajua kitu gani anakipata wapi, ukanda huu unaopitiwa na SGR sasa utapangwa rasmi, hatuwezi kuwa na reli ya kisasa yenye gharama kubwa kama hii lakini uendelezaji wa ardhi ni mbovu,mtu hataruhusiwa kufanya shughuli isiyoruhusiwa, hapa lazima ardhi ipangwe vizuri na tuwe na mpango mzuri  wa kiuchumi” alisema Lukuvi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji wa Wizara ya Ardhi Immaculata Senje alisema pamoja na kuinua pato la wakazi waishio kando ya reli hiyo mpango huo pia unalenga kulinda mazingira na kupendezesha maeneo hayo na wameshaanza maandalizi ya awali ya kukusanya taarifa za mpango huo.

 “Utakuwa ni mpango shirikishi kuanzia ngazi za vijiji hadi Taifa, mpaka sasa timu ya wataalamu imeundwa na imeshaanza maandalizi ya awali kwa kukusanya taarifa muhimu ambazo zitasaidia kuutekeleza mpango huu, tutafanya kazi na wote, lengo la mpango huu ni kutoa mwongozio wa namna matumizi ya ardhi yatakavyofanyika katika ukanda mzima” alisema Senje


Share:

CCM Watuma Salamu za Rambirambi Kifo cha Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi




Share:

Mbunge wa Kahama Ataka Kilimo Cha Bangi Kiruhusiwe Tanzania

Mbunge wa Kahama Mjini (CCM),   Jumanne Kishimba ameishauri Serikali ya Tanzania kuruhusu kilimo cha  bangi nchini kwa ajili ya utengenezaji wa dawa za binadamu.

Amesema hayo leo Jumatatu Mei 20,  2019 bungeni jijini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo mwaka 2019/2020.

Amesema nchi nne barani Afrika zimeruhusu kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa za binadamu.

“Amebainisha dawa nyingi za maumivu ya saratani asilimia 80 zinatokana na bangi, “Nashangaa wataalam wetu wa Mamlaka ya Chakula la Dawa (TFDA) wangekuwa wameshachukua sampuli na wangewajulisha kuwa dawa zilizo na bangi ndani yake.”

“Wangemuuliza  msambazaji hiyo bangi anaitoa wapi? Spika sisi wenyewe tunayo bangi hiyo tunaona kila siku inakatwa ukweli nyingi sio kwa ajili ya kuvuta. Bangi hiyo imekuwa ikienda katika dawa za binadamu.”

Amesema ana ushahidi Lesotho na Zimbabwe kuruhusu ulimaji wa bangi na kuna viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu kwa kutumia bangi.

Amesema gunia  moja la bangi nchini ni kati ya Sh4milioni hadi Sh4.5milioni na kwamba Lesotho na Zimbabwe gunia moja ni Sh20milioni.

“Bangi yote ya Tanzania inakwenda katika dawa za binadamu ambazo tunaletewa kutumia. Kuna ubaya gani ikaanza kutoa vibali kwenye maeneo mbalimbali na kuhalalisha watu waanze kulima bangi hiyo na kupata faida.” amesema.

Amesema haungi mkono kauli ya mbunge wa Geita (CCM),  Joseph Msukuma ambaye amekuwa akitaka bangi kuhalalishwa kwa ajili ya kuvuta.

Akichombeza Spika Ndugai aliwataka Wabunge kuchangia kama ambavyo amechangia Mbunge huyo kwa kujikita katika eneo moja

“Niwape siri muongee kama Kishimba unakuja na kitu chako fulani.unajikita sehemu moja.Hii hoja ni nzuri sana Naamini Jenista (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Ajira,Kazi,na watu wenye ulemavu) ameipigia mstari,”amesema Spika Ndugai.



Share:

Wizara Ya Kilimo Yaunda Tume Maalumu Kushughulikia Udhaifu Uliopo Katika Miradi Ya Umwagiliaji

Wizara  ya Kilimo imesema imeona udhaifu mkubwa katika miradi ya umwagiliaji hivyo imeunda timu maalum kulishughulikia hilo.

Hayo yameelezwa leo Mei 20 Bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo,Omari Mgumba wakati ahitimisha mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, kwa mwaka wa fedha 2018-2019.

Mgumba amesema ripoti ya CAG imeonesha kuna udhaifu mkubwa katika miradi ya umwagiliaji nchini hivyo Wizara ya Kilimo imeunda timu maalum kwenda kuthibitisha hayo.


Share:

Nape Ageuka Mbogo Kwa Waliohujumu Zao la Korosho

Mbunge wa Mtama,Nape Nnauye (CCM) ametaka wote waliohusika na kuhujumu Korosho wachukuliwe hatua na wasipochukuliwa ataleta kusudio jinsi walivyofanya mmoja mmoja.

Kauli hiyo ameitoa leo,Mei 20 bungeni,wakati akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, kwa mwaka wa fedha 2018-2019.

Nape amesema waliofanya mambo ya hovyo katika kuhujumu Korosho,Serikali inatakiwa iwachukulie hatua kali na isipofanya hivyo atakuja na kusudio jinsi walivyofanya mmoja mmoja

“Watu waliofanya hovyo wanajulikana na kama wasipochukua hatua wenyewe, wasipofanya tutaleta kusudio jinsi walivyofanya mmoja mmoja na jinsi ambavyo wanatakiwa kuchukua hatua kwa sababu waliyoyafanya ni kuhujumu,Korosho,wananchi lakini pia ni kuhujumu uchumi wa Nchi.

Nape amesema Rais alikuwa na nia njema lakini walioenda kuitekeleza wameenda kuiua sekta ya Korosho.

“Hivi tunavyoongea Mheshimiwa Spika bahati mbaya zoezi lilikuwa na dhulma,lilikuwa na rushwa lilikumbwa na ubabaishaji mwingi na uongo mwingi sana.

“Hivi tunavyoongea Jimbo la Mtama peke yake kwenye vyama vya msingi 11 wakulima ambao wana korosho chini ya tani 1500 ambao wamehakikiwa mashamba yao zaidi ya 1281 kwa miezi nane tangu Korosho yao ichukuliwe hawajapa hata senti tano.

“Lakini Korosho yao imechukuliwa hawana fedha za kutengeneza mashamba yao.

Nape alisema mapendekezo yake ni iletwe sheria ya Korosho yote ili ipitiwe upya.

“Kile kipengele tulichokinyofoa kimetuletea shida sana sasa leteni sheria yote tuipitie.

“Napendekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aende kukagua atuletee ripoti hapa ndani namna zoezi lilovyoenda ili tuchukue hatua ya kuziba mapengo.

“Kama nilivyosema Rais wengi wamemdanganya sasa ni vizuri wawajibike na Mheshimiwa Spika ni vizuri tukawa ‘Specific’ si sahihi kuiingiza Serikali katika mambo yaliyofanyika hovyo.

“Leo tukiulizana Korosho yetu ipo wapi haiwezi kukaa zaidi ya miezi sita hapa nchini ikabaki salama mngetuambia kuna korosho sahihi, huu ni uongo na tukiendelea kuusema huu uongo na bado tunaendelea kubaki hatutabaki salama,amesema Nape.


Share:

Wimbo Mpya: Dudu Baya - Dude

Wimbo Mpya: Dudu Baya - Dude


Share:

RAIS WA IFAD AKUTANA NA RAIS MAGUFULI IKULU

Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) umetenga shilingi Bilioni 127.3 kwa ajili ya kufadhili miradi ya kilimo nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia mwaka 2020.

Rais wa IFAD, Gilbert Fossoun Houngbo amesema hayo leo Ikulu Jijini DSM alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Pamoja na kutenga fedha hizo, Houngbo ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Togo amempongeza Rais Magufuli na Serikali anayoiongoza kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kukuza uchumi ikiwemo utekelezaji mzuri wa miradi inayofadhiliwa na IFAD, kutilia mkazo umuhimu wa uwekezaji usiokuwa tegemezi, unaolinda utu, unaozalisha kipato kwa wananchi na unaojenga misingi endelevu ya kujitegemea.

Amebainisha kuwa baada ya kutenga fedha hizo, IFAD inasubiri upande wa Tanzania kuainisha maeneo mahususi ya miradi ya kilimo ambako fedha zitaelekezwa na ameeleza kuwa ana matumaini miradi hiyo itafanikiwa kwa kuzingatia kuwa Tanzania ni nchi yenye amani na namna Serikali ilivyo na dhamira ya maendeleo.

Rais Magufuli ameishukuru IFAD kwa ushirikiano wake mzuri na Tanzania na amemhakikishia Mhe. Houngbo kuwa ushirikiano na uhusiano huo ulioanza mwaka 1978 utadumishwa kwa maslahi ya Watanzania.

Rais Magufuli amesema fedha zilizotengwa katika mpango huo wa miaka 3 zitaelekezwa katika maeneo yenye maslahi mapana ya sekta ya kilimo ikiwemo kuwezesha matumizi ya zana bora za kilimo katika uzalishaji, kuzalisha mbegu bora za mazao, kutatua changamoto ya masoko ya mazao, kuboresha ufugaji na ameipongeza IFAD kwa kutoa fedha pasipo kuweka masharti ya maeneo zinakopaswa kuelekezwa.

Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Kilimo kuharakisha mchakato wa kuainisha maeneo yatakayopokea fedha hizo ili utekelezaji wa mpango huo uanze.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Sweden, Peter Eriksson.

Baada ya mazungumzo hayo, Peter Eriksson amempongeza Rais Magufuli na Serikali yake kwa mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya rushwa na ameeleza dhamira ya Sweden kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Anders Sjöberg na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Prof. Palamagamba Kabudi.


Share:

Picha: Mbunge Masele mbele ya Kamati ya Bunge

Mbunge wa Shinyanga mjini na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Stephen Masele akiwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge jijini Dodoma kujibu tuhuma za utovu wa nidhamu zinazomkabili



Share:

Naibu Waziri: Askari Polisi anamamlaka ya Kusimamisha, kukagua na kukamata chombo barabarani

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,imesema Sheria ya Usalama Barabarani sura ya 168 iliyorejewa 2002 inampa Mamlaka askari polisi kusimamisha chombo chochote barabarani na kukikagua na hatimaye kukizuia na kukikamata.

Hayo yameelezwa Leo Mei 20 Bungeni na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,Hamadi Masauni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,Rehema Juma Migilla (CUF).

Katika swali lake,Migilla alitaka kujua ni kwanini askari polisi wanapowakamata huchukua baadhi ya vifaa.


Share:

Google yaizuia Huawei kutumia programu za android

Uhasama wa Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya makampuni makubwa ya mawasiliano kutoka China umeanza kuiweka kampuni ya simu za mkononi ya Huawei katika matatizo makubwa. 

Kampuni ya Kimarekani ya Google imetangaza kuizuia Huawei kutumia toleo jipya la programu ya kuendesha simu za mkononi ya Android, hiyo ikiwa na maana kuwa kampuni hiyo ya Kichina haitapata tena ruhusa ya kutumia programu hiyo muhimu katika simu zake mpya. 

Marekani inashuku kuwa Huawei huweka katika vifaa inavyovitengeneza, programu za siri za kijasusi zinazoweza kuhatarisha usalama wake wa taifa. 

Huawei inazikanusha shutuma hizo. Katika tangazo lake la hivi punde, Huawei imesema itaendelea kutoa huduma za kiusalama kwa watumiaji wa simu zake ambazo tayari zimekwishanunuliwa, na zile ambazo bado ziko madukani.


Share:

Marekani Yatishia Kuiangamiza Iran

Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kuizuia Iran kuwa na silaha za nyuklia saa chache baada ya kutishia kuiangamiza kufuatia matamshi ya kikosi cha walinzi wa Mapinduzi cha nchini Iran kwamba hawahofii vita.

Aidha Saudi Arabia imeionya Iran kuwa itajibu hatua za uchokozi kwa nguvu zote na kuiambia ni jukumu lake kuhakikisha inazuia vita.

Rais Trump alipozungumza na kituo cha televisheni cha Marekani cha Fox News amesema  hapendelei mvutano, lakini hatukubali kuiruhusu Iran kuwa na silaha za nyuklia na kusisitiza hilo halitaweza kutokea.

Rais Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter jana Jumapili kwamba, kama Iran inataka vita, huo utakuwa mwisho rasmi wa taifa hilo. Aliongeza kuionya Iran kutoitishia tena Marekani. Hatua hiyo imezidi kuongeza hofu kuhusu kuibuka kwa mzozo kati ya mataifa hayo, wakati hali ya wasiwasi ikizidi kuongezeka.
 
Salami hapo awali alinukuliwa akisema ni rahisi kuwashinda wanajeshi wa Marekani kwa sababu wanahofia kifo, tofauti na wanajeshi wa kikosi cha walinzi wa Mapinduzi wanaoamini katika kufia imani kulingana na dini ya Kiislamu.

Hata hivyo mvutano kati ya Marekani na Iran umezidi kuongezeka tangu Tehran ilipotangaza kwa kiasi itajiondoa kwenye mkataba wa silaha za nyuklia, ambao ilikubaliana na mataifa yenye nguvu duniani mwaka 2015, ambao hata hivyo Marekani ilijiengua mwaka jana.

Wiki iliyopita kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alisisitiza kwamba Iran haitaki vita na Marekani, ingawa anakataa mazungumzo na Trump na kusema Iran imechagua  kuwa mpinzani.

Kwa upande mwingine waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Adel al-Jubeir imeionya Iran kwamba imejiandaa vyema kujibu kwa nguvu zote uchokozi dhidi yake, na ni jukumu la Iran kuvizuia vita. 

Vita hivi vya maneno vimeongezeka kufuatia mashambulizi ya wiki iliyopita kwenye mabomba ya mafuta na mashambulizi ya jana ya roketi kwenye eneo lenye ulinzi mkali, ambako kunapatikana majengo ya ofisi za serikali na balozi za mataifa ya kigeni.

Saudi Arabia ambayo hata hivyo nayo inasisitiza haiko tayari kwa vita, imeituhumu Iran kwa kuagiza mashambulizi hayo kwenye mabomba ya mafuta yaliyofanywa na waasi wa Houthi wa Yemen. Hata hivyo, Iran imekana madai hayo.

Lakini ili kutuliza hali ya mambo, Saudi Arabia imeitisha mazungumzo ya dharura ya kikanda kujadiliana kuhusu kuongezeka kwa wasiwasi katika eneo hilo la Ghuba.

Kulingana na shirika rasmi la habari nchini humo la SPA, Mfalme Salman amewaalika viongozi wa mataifa ya Ghuba na Muungano wa mataifa ya Kiarabu kwenye mkutano huo wa dharura wa kilele wa siku mbili utakaofanyika mjini Mecca Mei 30 kujadilia uchokozi wa hivi karibuni na matokeo yake.

SPA limesema mkutano huo utakuwa ni fursa muhimu kwa mataifa ya ukanda huo kukubaliana kuhusu matarajio yao katika kuimarisha amani na utulivu wa kikanda.

-DW


Share:

Wafuatao Sio Watumishi wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger