Monday, 20 May 2019

Picha : RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MASHINDANO MAALUMU YA 20 YA QUR-AAN AFRIKA UWANJA WA TAIFA DAR

Share:

BABU WA MIAKA 65 AGONGWA VIBOKO NZEGA ,ASUKUMWA JELA MAISHA


Na Lucas Raphael, Tabora 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoni Tabora imemhukumu kifungo cha maisha jela na kumchapa viboko sita mkazi wa mtaa wa National Hausing, Juliasi Katambi (65) baada ya kumnajisi mtoto mwenye umri wa miaka sita mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nyasa Mbili iliyopo Nzega Mjini.

Akitoa hukumu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nzega, Gradness Badha alisema kuwa kutokana na ushahidi usioacha shaka, mahakama hiyo imeridhia kumpa adhabu hiyo Katambi ili kutumikia kifungo hicho baada ya mashahidi watano kutoa ushahidi juu ya tukio hilo la ubakaji.

Hakimu huyo alisema kuwa kutokana na kitendo hicho cha kinyama, mahakama hiyo imetoa hukumu iyo ili iwe fundisho kwake na kwajamii hasa kwa watu wenye kuendekeza vitendo hivyo vya ukatili kwa watoto wa kike na wanawake.

Awali, Wakili wa Serikali Piter Utafu aliieleza makahama hiyo kwamba mnamo Aprili 22, mwaka 2018 majira ya jioni katika maeneo ya Shule ya Msingi Nyasa Mbili iliyopo Nzega Mjini, mwanafunzi huyo alibakwa kwa nguvu na Katambi mwenye umri wa miaka 65 na kumsababishia maumivu makali katika mwili wake.

Wakili huyo alisema kutokana na kitendo hicho na upelelezi kukamilika na mashahidi watano kutoa ushahidi wa kuridhidha mahakamani hapo ni vema mahakama ikatoa adhabu kali kwa Katambi ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye nia na tabia kama hizo.

Mahakama ilitoa nafasi ya utetezi kwa mshitakiwa huyo baada ya kupatikana na hatia ambapo aliomba kupunguziwa adhabu kwa vile ni mara yake ya kwanza kutenda kosa kama hilo na vile vile ana umri mkubwa.

Hata hivyo, Mahakama ya Wilaya ya Nzega haikuridhika na utetezi huo na kumhukumu kutumikia kifungo cha maisha jela na kuchapwa viboko sita.

Share:

SEVILLA FC YA LALIGA KUTUA DAR JUMANNE


Vinara wa soka katika michuano ya Ligi Kuu ya Hispania, LaLiga, timu ya Sevilla FC inatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Simba ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya kwa timu hiyo kucheza nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam, timu hiyo inatarajiwa kuwasili kesho jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Kulingana na taarifa hiyo mechi hiyo itakuwa ni maalum kwa vinara hao wa 'LaLiga ambao wanadhaminiwa na SportPesa' na akaongeza kwamba ziara itahusisha matukio kadhaa ya jamii na michezo ikiwemo kliniki namafunzo mbalimbali.

"Kama ushindani wa kimataifa unakutana na dhamira ya LaLiga kuwa karibu na mashabiki wake. Kwa kweli kwamba mashabiki wetu wa Tanzania wataweza kupata furasa ya kuangalia karibu klabu kubwa kama Sevilla FC inamaanisha kuwa ni fursa kubwa kwa kila mtu," alisema Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kimataifa katika Ligi ya La Liga, Oscar Mayo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas, kampuni yao imeshirikiana na baadhi ya taasisi za soka za kubwa ulimwenguni baada ya kuna kuna haja ya kuleta uzoefu huu mkubwa kwa Tanzania.

"Ili kufurahia kuona moja ya klabu kubwa za mpira wa miguu Ulaya, Sevilla FC. Kwa makubaliano yetu na LaLiga ambayo ni ligi bora duniani, tutaweza kuonyesha vipaji vyetu na kuboresha kiwango cha soka nchini ", alisema Talimba.

Alisema kwamba mechi hiyo ni sehemu ya mradi wa 'LaLiga duniani ambao unalenga kueneza soka la Hispania kimataifa na kueneza pia sera ya 'Marca EspaƱa', kuleta karibu mashabiki wa LaLiga na kukuza klabu nje ya nchi yetu.

Hii itakuwa ni klabu ya pili Ulaya kufanya ziara Afrika Mashariki, baada ya mwaka 2017 Everton FC kucheza na Gor Mahia nchini Kenya, ingawa sio mara ya lkwanza kwa Sevilla kutua katika bara hili kwani mwaka 2015 ilikuwa nchinbi Morocco ambao ilicheza mechi ya kuajindaa na LaLiga dhidi ya timu ya Hassania Union Sport d'Agadir.


Share:

MAFUNZO YA JINSIA KWA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA YAFIKIA YAFUNGWA MWANZA


Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa (Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita) ili kuandika habari za kijinsia kwa weledi yamefikia tamati jijini Mwanza.

Mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia jumamosi Mei 18, 2019 yaliandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na ile ya Vyombo vya Habari nchini Finland VIKES.

Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa alitumia fursa hiyo kuwahimiza waandishi wa habari Tanzania kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, misingi na miiko ya uandishi wa habari huku wakitoa usawa wa vyanzo vyao vya habari kwa kuzingatia jinsia.

"Bado vyanzo vingi vya habari vinawahusisha wanaume huku wanawake wakisahaulika hivyo mafunzo haya yawe chachu ya kuleta mabadiliko kwenye kazi zenu kwa kuibua na kutangaza masuala mbalimbali yanayowahusisha wanawake pia" alisema Gasirigwa.

Naye Maridhia Ngemela kutoka Radio Iqra FM ya jijini Mwanza aliyeshiriki kwenye mafunzo hayo alisema changamoto kubwa katika uandaaji wa habari na makala kwa kuzingatia jinsia ni baadhi ya wanawake kutokuwa tayari kutoa ushirikiano kama ilivyo kwa wanaume hivyo ni vyema elimu ikaendelea kutolewa ili kuondoa hali hiyo.

Hata hivyo mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Alex Mchomvu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza alisema suala la imani, mila na tamaduni mbalimbali linakwamisha usawa wa kijinsia hapa nchini hivyo waandishi wa habari ni vyema wakatumia nyenzo zao kutoa elimu ili kubadili fikra hizo na hivyo kuleta usawa wa kijinsia baina ya wanawake na wanaume.
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa (wa tatu kulia) na Mkufunzi Kenneth Simbaya ambaye ni Mwenyekiti Mtandao wa Waandishi wa Habari za Afya Tanzania (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzio hayo.
Mmoja wa wakufunzi, Alex Mchomvu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza akiwasilisha mada kwenye mafunzi hayo.
Washiriki waki-refesh viungo vya miili yao kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakimsikiliza Mkufunzi, Kenneth Simbaya wakati akiwasilisha mada.
Mkufunzi, Kenneth Simbaya akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washirikiwa wakiwa kwenye majadiliano kupitia makundi.
Mwanahabari mkongwe, Florah Magabe (kushoto) pamoja na mwanahabari chipukizi, Sefroza Joseph (kulia) wote kutoka jijini Mwanza, wakifurahia jambo kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia jambo kwenye mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa umakini jambo kwenye mafunzo hayo

Share:

Lugola Atangaza Kiama Kwa Trafiki wanao wabambikizia makosa Madereva

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewatangazia kiama askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini wanaowabambikia madereva makosa ya picha za mwendokasi (Speed rader) zisizo na uhalisia kwa nia ya kujipatia mapato wakibainika watawajibika kuzilipa wao wenyewe faini hizo na kuondolewa katika kitengo hicho.

Alitoa agizo hilo mjini Morogoro wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu maafikiano kati ya vyama vya watoa huduma za usafirishaji nchini kuhusu kusitisha kusudio la madereva wa mabasi ya abiria kufanya mgomo wakishinikiza kutimiziwa madai yao mbalimbali ikiwamo ya mikataba ya kazi.

Alisema maamuzi hayo yametokana na makubaliano ya pamoja baina viongozi wa vyama hivyo vya usafirishaji pamoja na wizara mtambuka za serikali kwa nia ya kutatua changamoto walizowasilisha katika kikao hicho kuhusu kubambikiwa makosa na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani.

Waziri Lugola, alisema moja ya makosa yanayolalamikiwa na madereva hao ni pamoja tochi zinazopiga picha mabasi na kurushwa kwenye simu za maaskari zinakosa uhalisia wa tukio ikiwamo kutoonekana kwa namba za usajili pamoja na vibao vya kuzuia makatazo mbalimbali na kusababisha utata na mivutano yenye nia ya kujenga mazingira ya rushwa.

Alisema kuanzia sasa askari hao wanapaswa kupiga picha katazo mbalimbali za barabara mbele ya gari ikionyesha mwonekano usio na mashaka, namba ya usajili pamoja na eneo la alama iliyokiukwa na dereva ili kuwapo na ushahidi halali vinginevyo dereva huyo asichukuliwe hatua yoyote.

“Dereva anapokuwa na mashaka na picha iliyopigwa dhidi ya gari lake kama haionyeshi usajili wa namba za gari na eneo la kibao cha zuio asikubali kuadhibiwa na badala yake amweleze huyo askari azitume picha hizo kwa msimamizi wa kikosi cha usalama barabarani na aende huko,” alifafanua Waziri Lugola.

Pia alisema tabia ya baadhi ya askari kukamata mabasi yenye abiria na kuyafikisha kituo cha polisi kwa nia ya kumuadhibu dereva aliyetenda makosa, jambo hilo liachwe mara moja na badala yake dereva aliyetenda kosa anapaswa kukamatwa katika kituo cha mwisho cha safari yake.

“Sheria ya Mamlaka ya Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), inaeleza wazi kila basi linalofanya safari za masafa marefu lazima liwe na madereva wawili, hivyo ukimkamata dereva na kumweka ndani tayari unaenda kinyume na sheria za Sumatra na kulifanya basi kushindwa kuendelea na safari yake,” alisema.

Aidha, aliliagiza Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani kuendelea kuwanyang’anya leseni madereva wanaofanya makosa ya kujirudia pamoja na kukamata magari yanayofanya shughuli za usafirishaji bila kuwa na leseni kwa kushirikiana na Sumatra.


Share:

Mbunge wa Shinyanga mjini na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Stephen Masele Ameshafika Bungeni Tayari Kwa Kuhojiwa

Spika wa Bunge,Job Ndugai ameitaka Kamati ya Kudumu ya Haki,Maadili na Madaraka Bunge kwenda kumuhoji Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Afrika,Stephen Masele.

Agizo hilo amelitoa Leo Mei 20 wakati Wabunge wakichangia mjadala wa Wizara ya Kilimo.

“Nawaomba Kamati ya Maadili mwende sasa maana Mheshimiwa Masele ameishafika,” amesema Spika Ndugai.


Share:

Video Mpyaa Kabisa : BHUDAGALA NG'WANA MALONJA - LING'OMA


Ninakualika kutazama ngoma mpya ya msanii wa Nyimbo za asili Bhudagala Ng'wana Malonja inaitwa Ling'oma imetengenezwa Kalunde Media....Itazame video hii mpya hapa chini
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya May 20

<



Share:

Sunday, 19 May 2019

WAZIRI AWATAKA VIJANA MUHEZA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO VIDOGO


Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mlingano wilayani Muheza Waziri Mohamed ambaye pia ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Tanga.

Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mlingano Jimbo la Muheza wilayani Muheza Waziri Mohamed amewataka vijana wilayani humo kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Magufuli.

Waziri ambaye pia ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Tanga aliyasema hayo wakati aliofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mlingano Jimbo la Muheza aliyoijenga kwa kutumia kiasi cha milioni 7.4

Kwa mujibu wa Waziti alisema ameamua kujenga ofisi hiyo kutokana na kwamba kata hiyo kutokuwa nayo kwa muda mrefu na hivyo kuona haja ya kuhakikisha ujenzi huo unafanyika ili kuwawezesha viongozi kutekeleza wajibu wao wa kukijenga chama hicho.

Aidha alisema pia iwapo vijana watatumia muda wao kufikiria namna ya kujikita kwenye uanzishwaji wa viwanda hivyo utawasaidia kuweza kujiajiri na kuweza kuisaidia jamii kwa kutoa ajira kwa wenzao na hivyo kuchangia pato la mkoa na taifa kwa ujumla.

“Lakini pia vijana wenzangu tuunge mkono juhudi za serikali kwa kushiriki kwenye miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yetu kwa kujitoa na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji maendeleo katika jamii zinazotuzunguka ",alisema.

Muonekano wa Jengo la Ofisi ya CCM kata ya Mlingano wilayani Muheza ambalo limejengwa na Katibu Mwenezi wa Kata ya Mlingano Jimbo la Muheza ambaye pia ni Katibu Hamasa Chipukizi wa UVCCM Mkoa wa Tanga Waziri Mohamed Waziri kwa asilimia 90 ambapo mpaka kukamilika kwake ametumia kiasi cha milioni 7.4.
Share:

MADEREVA WA MALORI YA MAFUTA WAPONGEZA WAKALA WA VIPIMO 'WMA" KUWAFUNGULIA KITUO CHA KUPIMA MAFUTA MISUGUSUGU


Na Emmanuel Mbatilo
Madereva wa Malori ya Mafuta (Trucker) wameishukuru taasisi ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) kwa kuwafungulia kituo cha kupima mafuta kilichopo Misugusugu mkoani Pwani kwa kuwa kimewasaidia kupunguza kero ya kusubiri kupima kwa muda mrefu.

Wamesema uanzishwaji wa kituo hicho umeleta tija kwa sababu kimepunguza sana msongamano wa maroli wakati wa kupima mafuta

Wamesema awali walikuwa wakipima katika kituo cha Ilala ambacho eneo lake ni finyu sana hivyo ilikuwa vigumu sana kupima kwa haraka jambo ambalo lilikuwa likileta kero kwa wasafirishaji wa mafuta.

Kituo hicho kinapima zaidi ya Magali 60 kwa siku kuliko hapo mwanzo katika kituo kilichopo Ilala.

Wamezungumza hayo wakiwa katika harakati za upimaji wa magari yao Misugusugu.

Share:

RIDHIWANI KIKWETE ATOA MISAADA KATA YA UBENA ZOMOZI - CHALINZE

Share:

BASI LA NEW FORCE LAGONGANA NA LORI NA KUUA,KUJERUHI


Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 15 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la New Force lililogongana na lori kati ya eneo la Mafinga na Nyololo mkoani Iringa leo Jumapili Mei 19, 2019.

 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William amesema ajali hiyo imetokea kwenye misitu ya Sao Hill, na dereva wa lori amefariki dunia papo hapo.

Ajali hiyo imehusisha basi la New Force lililokuwa likitoka jijini Dar es Salaam kwenda jijini Mbeya na liligongana na lori hilo lililokuwa limeingia ghafla barabarani likitokea kwenye barabara ya mchepuko.

“Bado tunaendelea kuchambua idadi ya majeruhi lakini hadi sasa aliyefariki dunia katika ajali hiyo ni mtu mmoja ambaye ni dereva wa lori lililohusika kwenye ajali hiyo, idadi ya majeruhi hadi sasa ni 15,” amesema mkuu huyo wa wilaya.

Amesema baadhi ya majeruhi wamepelekwa hospitali ya Mafinga kwa matibabu kutokana na majeraha waliyopata kwenye ajali hiyo.

ANGALIA <<VIDEO>> HAPA
CHANZO - MWANANCHI

Share:

UDOM: CALL FOR APPLICATION FOR ADMISSION INTO POSTGRADUATE PROGRAMMES 2019

CALL FOR APPLICATION FOR ADMISSION INTO POSTGRADUATE PROGRAMMES 2019

Dodoma City is located in the centre of the country (6°10’23’’S; 35°44’31’’E), 455 km west of the former capital, Dar es Salaam; and 441 km south of Arusha City, the cradle of the East African Community. It is also 259 km north of Iringa Municipality through Mtera. The City covers an area of 2,669 km2 of which 625 km2 is urbanised.

Dodoma features a semi-arid climate with relatively warm temperatures throughout the year. Although average maximums are consistent throughout the year, average minimums drop to 13°C in July. The average annual precipitation is 570 mm, most of which occurs during the wet season between November and April, with the remainder of the year comprising dry season.

The recently refurbished Dodoma Airport and the Central Railway Line connecting it over a distance of 465 km with Dar es Salaam serve the city. There are also major highways connecting Dodoma with Dar es Salaam (via Morogoro Region) to the east, Mwanza City (via Singida) to the west, and Arusha (via Kondoa) to the north.

The University is located about 8 km east of the city centre, and is accessible by public transport, which is easily available from the city centre. Given the central location of Dodoma, UDOM is strategically positioned to serve applicants around the country and specifically Government and private sector employees living in Dodoma, who hitherto could not find training opportunities in the area. Such employees can comfortably utilise UDOM to combine work and study for their career advancement. Additionally, the geographical location and Dodoma weather render UDOM a convenient place for international students.

Our Goals
The goal is “To increase the contribution of higher education in Tanzania’s attainment of economic growth, reduction of poverty, and improved social wellbeing of Tanzanians through increased access to higher education, technological innovation, and generation and application of knowledge.”

Our Vision
The vision of the UDOM is “To become a centre of excellence that offers value added training, research and public services”.

Our Mission
The mission of the UDOM is “To provide comprehensive, gender sensitive and quality education to a broad segment of the population through teaching, research, and public services in the fields of education, health and allied sciences, natural sciences, earth sciences, information and communication technologies, business, humanities and social sciences”.

CALL FOR APPLICATION FOR ADMISSION INTO POSTGRADUATE PROGRAMMES 2019

APPLY NOW

The post UDOM: CALL FOR APPLICATION FOR ADMISSION INTO POSTGRADUATE PROGRAMMES 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

SIMBA YAANZA KUNUKIA UBINGWA....YAICHAPA NDANDA FC 2-0

Mabingwa watetezi Simba leo wamebeba pointi tatu mbele ya Ndanda FC na kuanza kunukia ubingwa wa ligi msimu huu kwa ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Uhuru.

Meddie Kagere kipindi cha kwanza amepachika mabao yote mawili ambapo bao la kwanza amefunga dakika ya tatu akimalizia pasi ya John Bocco na bao lake la pili alifunga dakika ya 11 akimalizia pasi ya Clatous Chama.

Ushindi huo umewapa nafasi Simba kujikita kileleni wakiwa na jumla ya pointi 88 na wamebakiwa na michezo mitatu ili kukamilisha mzunguko wa pili.

Kwa nafasi ambayo kwa sasa Simba wamefikia wanahitaji pointi mbili ili kujihakikishia kutetea ubingwa wao msimu huu.

Simba wamepiga jumla ya mashuti 10 ambayo hayakulenga lango huku Ndanda wakipiga jumla ya mashuti sita ambayo hayakulenga lango.

Mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Singida United utakaochezwa uwanja wa Namfua Mei 21.
Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521


Share:

Urusi na Uturuki Kuunda mifumo ya makombora ya S-500

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema kuwa nchi yake na Russia kwa pamoja zitaunda mifumo ya makombora ya S-500 baada ya mpango wake wa awali wa kunununua mfumo wa makombora wa S-400 kutoka Moscow kuzusha mivutano.

Jitihada za Uturuki za kutilia mkazo kununua mfumo wa makombora wa S-400 umezorotesha zaidi uhusiano wa nchi hiyo na Marekani; nchi ambayo imeionya mara kadhaa Ankara kuhusu hatari zinazoikabili vikiwemo vikwazo iwapo itaendelea na mpango wake wa kununua mfumo huo wa makombora kutoka Moscow.

Hata hivyo akizungumza mjini Istanbul, Rais wa Uturuki amesema kuwa na hapa ninamnukuu, "kutakuwepo uundaji wa pamoja wa mfumo wa makombora wa S-500 badala ya ule wa S-400", mwisho wa kunukuu. Ameongeza kuwa makubaliano yamefikiwa, na hapa hakuna swali kwamba Uturuki imeachana na ununuzi wa mfumo wa makombora wa S-400.

Itakumbukwa kuwa, uhusiano kati ya Uturuki na Marekani; nchi mbili ambazo zote ni waitifaki wa Muungano wa Nato umeingia dosari kutokana na masuala kadhaa ikiwemo hatua ya Marekani ya kuwaunga mkono wapiganaji wa Kikurdi wa Syria; wapiganaji ambao Ankara inawataja kuwa magaidi; na pia hatua ya Marekani ya kukataa kumrejesha nchini Uturuki mwanazuoni wa Kiislamu anayetuhumiwa kupanga njama ya mapinduzi dhidi ya Rais Erdogan mwaka 2016.

Wakati huo huo Washington imedai kuwa makubaliano baina ya Ankara na Moscow ya kuunda kwa pamoja mfumo wa makombora wa S-500  ni tishio kwa ulinzi wa Magharibi. 


Share:

Waziri Mwakyembe ampongeza Mbwana Samatta

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, ametoa pongezi kwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta baada ya kuisaidia timu yake ya KRC Genk kuibuka mabingwa wa Ubelgiji.

Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa Samatta amefanya jambo kubwa kwa kuzingatia Ubelgiji ni moja ya mataifa makubwa tena yanayofanya vizuri kwenye mchezo wa soka duniani.

''Samatta amefanikiwa kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania, ni shujaa ambaye mchango wake ni mkubwa na tunajaribu kuona ni vipi Samatta anaweza kuwa Balozi wa vivutio vyetu vya utalii, Sanaa na Michezo'', amesema.

Mbwana Samatta ambeye ni mchezaji wa zamani wa Simba, TP Mazembe na mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2016, mpaka sasa ni kinara wa mabao kwenye ligi kuu ya Ubelgiji akiwa amefunga magoli 20.

Samatta alijiunga na Genk mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ambapo mwaka huo pia alishinda tuzo ya mchezaji bora wa ndani Afrika baada ya kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger