Sunday, 19 May 2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya May 19





Share:

Saturday, 18 May 2019

Pakua App ya Malunde 1 blog ili Upokee Habari Moja kwa Moja kwenye Simu Yako

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:

Picha : TAASISI YA MISA TANZANIA YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA KUHUSU HABARI ZA JINSIA


Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na ile ya VIKES ya nchini Finland, imeandaa mafunzo ya kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kuwajengea uwezo wa kuripoti habari za kijinsia kwa weledi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika jijini Mwanza kuanzia leo jumamosi Mei 18, 2019 yakiwashirikisha waandishi wa habari 25 kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Geita, Shinyanga pamoja na Simiyu.

Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa amesema mafunzo hayo pia yamelenga kuwajengea uwezo waandishi wa habati katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kuibua na kuripoti habari mbalimbali za kijinsia hususani zinazowagusa wanawake kwani wamekuwa hawapewi kipaumbele na vyombo vya habari.

"Tunahitaji kubadili fikra katika kuripoti habari za kijinsia, bado wanaume wanapewa kipaumbele huku wanawake wakisahaulika hivyo mafunzo haya yatusaidie kutoka tuliko na kuanza kuibua mambo mazuri yanayofanywa na wanawake na kuyaripoti kupitia vyombo vyetu vya habari", amesisitiza Gasirigwa.

Akiwasilisha mada ya jinsia kwenye mafunzo hayo, Alex Mchomvu kutoka Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza amesema baadhi ya mila na desturi zimekuwa zikiathiri masuala mbalimbali ya usawa wa kijinsia hivyo waandishi wa habari wanapaswa kutumia vyombo vya habari kubadili hali hiyo ili kuleta usawa kwenye masuala ya kijinsia.

Naye Kenneth Simbaya, Mwenyekiti Mtandao wa Waandishi wa Habari za Afya Tanzania (Africa Media Network on Health Accountability Tanzania Chapter), akiwasilisha mada kuhusu misingi ya uandishi wa habari amehimiza waandishi wa habari kuiishi misingi hiyo ikiwemo ukweli na usahihi bila kupendelea kwani wamepewa dhamana kubwa katika jamii.

“Kuna wasiwasi mkubwa kwa sasa juu ya utendaji wa wanahabari ambapo ukweli ni kwamba jamii haituamini tena. Lakini imani au kuaminika ni jambo la muhimu katika kazi yetu kama wanahabari” amesema Simbaya na kuongeza;

“Ili kurudisha imani hiyo ni lazima waandishi wa habari na vyombo vya habari kuiishi misingi au miiko ya wanahabari ambayo ni ukweli na usahihi, uhuru (kutokuwa tegemezi), kuzingatia usawa (fairness and impartiality), utu (humanity) na uwajibikaji (Accountability)” amesisitiza Simbaya.

Washiriki wameishukru taasisi ya MISA Tanzania kwa kuandaa mafunzo hayo wakisema yatawasaidia katika utendaji wao wa kazi ikiwemo kuandaa habari na makala mbalimbali kuhusu usawa wa kijinsia kwa kutoa nafasi sawa baina ya wanawake na wanaume tofauti na ilivyo sasa ambapo asilimia kubwa ya vyanzo vyao ni wanaume wakati kuna wanawake wengi wanafanya mambo makubwa lakini habari zao hazipati nafasi.
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akitoa ufafanuzi kwa washiriki kuhusiana na mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuripoti habari za kijinsia kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakimsikiliza Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa.
Mmoja wa wakufunzi, Alex Mchomvu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Kampasi Kuu ya Mwanza akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Mmoja wa wakufunzi, Kenneth Simbaya ambaye pia ni Mwenyekiti Mtandao wa Waandishi wa Habari za Afya Tanzania (Africa Media Network on Health Accountability Tanzania Chapter) akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Mmoja wa washiriki, Erica Elias kutoka mkoani Shinyanga akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Wakufunzi wa mafunzo hayo, Alex Mchomvu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Kampasi Kuu ya Mwanza (kushoto) pamoja na Kenneth Simbaya (kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti Mtandao wa Waandishi wa Habari za Afya Tanzania (Africa Media Network on Health Accountability Tanzania Chapter).
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa (katikati), akiteta jambo na wakufunzi wa mafunzo hayo ambao ni Alex Mchomvu (kushoto) pamoja na Kenneth Simbaya (kulia).
Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kuripoti habari za kijinsia.
Mshiriki Erica Elias akiwasilisha mada kwa niaba ya wanakundi wenzake.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akiwasilisha mada kwa niaba ya washiriki wenzake.
Mshiriki Beatrice Rabach kutoka jijini Mwanza pamoja na wenzake wakiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Share:

Wadau Waombwa Kujitokeza Kusaidia Maandalizi Ya Mashindano Ya Soka Kwa Wenye Ulemavu Afrika Mashariki

NA : Mwandishi Wetu
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu imewataka wapenzi na wadau wa soka nchini kushiriki  maandalizi ya mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa watu wenye ulemavu Afrika Mashariki (CECAAF) yanayotarajiwa kufanyika nchini Mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

Akizungumza  na waandishi wa habari   Mei 16, 2019 Jijini Dodoma,katika mkutano uliolenga kuitambulisha kamati ya wabunge watano waliojitolea kuhamasisha Watanzania,kushiriki kwa hali na mali katika mashindano hayo,  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha nchi za Tanzania Bara, Zanzibar, Uganda, Kenya na Rwanda.

“Mashindano haya yatakayokuwa ya kwanza kufanyika katika ukanda huu wa Afrika yameanzishwa kwa mujibu wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa haki za Walemavu wa mwaka 2006, unaotaka haki ya Walemavu kushiriki katika mambo kadhaa ikiwemo michezo”

Akifafanua zaidi, Dkt. Mwakyembe amesema kuwa lengo la kuhamasisha umma wa watanzania ni kuunga mkono mashindano hayo kwa hali na mali.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi  ya Waziri mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe. Stella Ikupa amesema kuwa mashindano hayo yatasaidia kuibua vipaji vya watu wenye ulemavu na hivyo kushiriki katika kukuza sekta ya michezo.

Pia ameiomba jamii kwa upana kujitokeza kuchangia na kushiriki mashindano hayo kwa kuzingatia kuwa watu wenye ulemavu wana nia ya kushiriki vyema katika mashindano hayo.

Naye mbunge wa Sengerema mhe. William Ngeleja,ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya michezo ya Bunge, akizungumza kwa niaba ya Spika wa Bunge, amesema  kuwa watashiriki kikamilifu katika kuhakikisha kuwa mashindano hayo yanafanikiwa kwa kuzingatia malengo yake.

Mheshimiwa Ngeleja,aliongeza kusema kuwa watashiriki kwa vitendo kwa kuzingatia  kuwa Bunge ni wasimamizi  wa  sheria za sekta ya michezo ,mikataba ya kimataifa, sheria na kanuni  katika sekta hii.

Wizara ya Habari kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, inawaomba wananchi kuipa Kamati hii ya wabunge ushirikiano wakutosha katika maandalizi ya michuano hiyo ambayo inahitaji fedha ya kutosha na vifaa.

Wabunge wanaounda kamati hiyo ni Mheshimiwa William Ngeleja,Mheshimiwa Venance Mwamoto,Mheshimiwa Margareth Sitta, Mheshimiwa Amina Mollel na Mheshimiwa Riziki Said Lulida.


Share:

Ujenzi Wa Bwawa La Mbangala Watakiwa Kukamilika, Wafugaji Kunufaika

Na. Edward Kondela
KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel ameutaka uongozi wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) uliopo chini ya Wizara ya Maji, kukamilisha ujenzi wa Bwawa la Mbangala lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songwe iliyopo Mkoani Songwe ili kutatua kero za wananchi kukosa maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo na pia kuondoa migogoro kati ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

Prof. Gabriel amebainisha hayo alipotembelea eneo hilo kushuhudia ujenzi wa bwawa ambapo amesema anaridhishwa na ubora na viwango vya ujenzi japo amesisitiza kwamba DDCA waongeze kasi ya kazi hiyo ili iishe mapema iwezekanavyo ili kukidhi mahitaji ya wafugaji kama ilivyokusudiwa. Sambamba na hilo amehimiza uiongozi wa juu wa DDCA kuzingatia maelekezo na ushuri wa kitendaji ambao amewapatria na wawasilishe ripoti ya utekelezaji katika muda walioyoelekezwa.  

Katibu mkuu huyo amesema kulingana na ibara ya 25 ya ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 inaelekeza kuna haja ya kuongeza malambo, mabwawa na visima virefu katika maeneo yanayohitaji maji na malisho.

“Lengo la wizara ni kuhakikisha tunaondokana na kadhia ya maeneo ya malisho na maji kwa mifugo katika maeneo yote nchini ili kuhakikisha sekta ya mifugo inaimarika.” Alifafanua Prof. Gabriel

Kuhusu migogoro kati ya wafugaji na watumaji wengine wa ardhi Katibu Mkuu huyo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha migogoro inaondoka katika maeneo mbalimbali nchini kwa kushirikiana na viongozi wa mikoa.

Kwa upande wake Msaidizi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Bw. Evance Kulanga amesema Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ina idadi kubwa ya ng’ombe wapatao 680,000 ikiwa ni idadi kubwa ya ng’ombe kuliko wilaya zote zilizopo Mkoani Songwe, hivyo kutoa rai kwa wananchi kulitunza bwawa hilo mara litakapokamilika.

Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Mbangala linapojengwa bwawa la kunyweshea mifugo Bw. Revocatus Nkonoki amesema bwawa litanufaisha wafugaji  kwa kuwa kata hiyo ina ng’ombe Elfu Nne na wafugaji katika kata hiyo wamekuwa wakiuliza mara kwa mara juu ya kukamilika kwa bwawa hilo ili waweze kupata maji kwa ajili ya mifugo yao.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ujenzi wa Mabwawa katika Idara ya Mabwawa katika Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) uliopo chini ya Wizara ya Maji Mhandisi Sadara Sadick amesema atayafikisha maagizo yote yaliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulika Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel ili waweze kukamilisha ujenzi wa bwawa mwaka huu.

Bw. Sadick amesema watafika katika ofisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi Tarehe 24 mwezi huu kama walivyoelekezwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel ili waweze kujadiliana na wizara juu ya utekelezaji wa haraka wa mradi huo.

Ujenzi wa bwawa la maji la Mbangala kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo umeanza kutekelezwa rasmi mwezi Novemba Mwaka 2018 ambapo mradi huo hadi kukamilika kwake utagharimu Shiling Bilioni Moja.

Imetolewa: Kitengo cha Mawasiliano Serikalin                   Wizara ya Mifugo na Uvuvi


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya May 18



















Share:

Friday, 17 May 2019

MGODI WA NYAMONGO WAPIGWA FAINI YA BILIONI 5.6


Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), imeupiga faini ya shilini bilioni 5.6 mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime, kwa kushindwa kudhibiti bwawa la maji yenye sumu na hivyo kuhatarisha afya za wakazi wanaozunguka mgodi huo.

Maamuzi hayo yalitolewa jana baada ya Waziri wa Madini, Doto Biteko pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba kufanya ziara mgodini hapo, wakiambatana na Watendaji mbalimbali.

Faini hiyo ilitangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka baada ya ripoti ya Kamati Huru iliyoundwa kwa ushirikiano wa Wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Madini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) pamoja na Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam kubaini mgodi huo umekuwa ukitiririsha maji yenye sumu kwa zaidi ya miaka 10 huku ukitoa taarifa zenye udanganyifu kuhusiana na maji hayo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba (kushoto), pamoja na Waziri wa Madini Doto Biteko (katikati) wakisikiliza ufafanuzi kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa Kamati Huru iliyoundwa kuchunguza malalamiko ya utirishaji wa maji yenye sumu kutoka mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime.
Sehemu ya eneo linalokusanya maji yenye sumu kwa ajili ya kuyasukuma kwa mashine kuyarudisha kwenye bwawa la kuhifadhia maji yenye sumu katika mgodi wa Acacia North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba pamoja na Waziri wa Madini Doto Biteko wakiwa wameambataba na viongozi mbalimbali kukagua mazingira mbalimbali yanayozunguka mgodi wa Acacia North Mara.
Viongozi hao wakijionea mtaro uliochimbwa na mgodi wa Acacia North Mara kwa ajili ya kunasa maji yenye sumu yanayotiririka kutoka kwenye bwawa la kuhifadhia maji/ tope sumu.
Sehemu ya maji yenye sumu yanayotiririka kutoka kwenye bwawa la maji yenye sumu kutoka mgodi wa Acacia North Mara wilayani Tarime.
Sehemu ya dimbwi la maji yenye sumu yanayotiririka kutoka kwenye bwawa (TFS) la kuhifadhia maji hayo.
Baadhi ya askari wanaoimarisha ulinzi katika mgodi wa Acacia North Mara wilayani Tarime.
Tazama Video hapa chini


Share:

Wimbo Mpya : BHUDAGALA - BHUSAMI....Ngoma Kali Balaa...


Msanii nguli wa nyimbo za asili Bhudagala Mwanamalonja ameachia ngoma mpya inaitwa Bhusami,isikilize hapa mtu wangu
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger