Friday, 17 May 2019
HOTUBA YA WAZIRI WA KILIMO, KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA KILIMO KWA MWAKA 2019/2020
1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji, Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Aidha, ninaliomba Bunge lako Tukufu lipitishe Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara na Taasisi zake kwa mwaka wa Fedha 2019/2020.
15. Mheshimiwa Spika, ili kutekeleza vipaumbele hivyo, Shilingi bilioni 204.07 ziliidhinishwa na Bunge lako Tukufu. Kati ya fedha hizo, Fungu 43 – Wizara ya Kilimo iliidhinishiwa Shilingi bilioni 166.26zikiwemo Shilingi bilioni 68.14 za matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 98.12 za matumizi ya maendeleo; Tume ya Taifa ya Umwagiliaji - Fungu 05 iliidhinishiwa Shilingi bilioni 29.77
5.1 Kuongeza Tija katika
65. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara inaomba idhini ya kukusanya maduhuli ya Shilingi 3,472,515,000yatokana
66. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara ya Kilimo inaomba kutumia jumla ya Shilingi 253,856,943,970 ku
67. Mheshimiwa Spika, jumla ya Shilingi 208,044,783,140zinaom
68. Mheshimiwa Spika, jumla ya Shilingi 37,485,090,830zinaomb
Aidha, Shilingi 4,983,628,217 zinaomb
69. Mheshimiwa Spika, jumla ya Shilingi 8,327,070,000 zinaomb
70. Mheshimiwa Spika, Pamoja na hotuba hii, vipo viambatisho vinavyotoa ufafanuzi wa baadhi ya maeneo. Hotuba hii pia inapatikana katika tovuti ya Wizara ya Kilimo, www.kilimo.go.tz. Nina
Video Mpya: Bright - Aibu
Msanii wa muziki Bongo, Bright anakukaribisha kutazama video ya wimbo wake mpya uitwao Aibu. Itazame hapa.
Makampuni Sita Yasaini mkataba wa awali Wa kununua korosho nchini
Serikali imesaini mkataba wa awali na kampuni sita ya kununua korosho kati ya zilizoomba kununua korosho hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Mei 16, 2019 Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema baada ya Kampuni ya Indo Power ya nchini Kenya kushindwa kununua korosho wameendelea kusaini mikataba ya awali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Mei 16, 2019 Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema baada ya Kampuni ya Indo Power ya nchini Kenya kushindwa kununua korosho wameendelea kusaini mikataba ya awali.
“Tumeendelea kusaini mikataba mingine na makampuni mengine, mikataba ambayo tumeisaini ni ya awali.
“Mpaka sasa tumesaini na makampuni sita nisingependa kuyataja kwa majina kwa sababu tunajua hali halisi ya makampuni ya korosho watu wanafuatiliana, wanaharibiana biashara pamoja na majina.
“Lakini kuna kampuni moja tuliikaribisha wiki iliyopita imekuja kukagua maghala ya korosho wamejiridhisha kwamba korosho yetu ni safi na haijaharibika na tumepeleka kwenda kuhakiki TBS na wameenda kufanya uhakiki katika nchi yao na wamejihakikishia kwamba ni nzuri na wanajiandaa kulipa.
“Hawa mabwana wakilipa tunawakabidhi korosho mara moja,”alisema Waziri Kakunda.
Akitoa ripoti ya maagizo aliyoagizwa na Rais Dk. John Magufuli wakati akiapishwa, Novemba 12 mwaka jana ya kusimamia ununuzi wa korosho, Kakunda alisema tangu Novemba 13 mwaka jana hadi Mei 15 mwaka huu zimeweza kukusanywa tani 225,000.
“Kati ya hizo tani 2,200 zinaendelea kubanguliwa na viwanda vya ndani kwa mikataba maalum. Maana yake zinabaki tani 228,000 katika maghala."Alisema
Wagonjwa 1,901 wa Dengue wabainika
Jumla ya wagonjwa 1,901 wamebainika kuwa na virusi vya homa ya Dengue, tangu kuibuka kwa ugonjwa huo nchini, Januari mwaka huu.
Kati ya wagonjwa hao, 1,809 ni wakazi wa jiji la Dar es Salaam, 89 kutoka Tanga mmoja kutoka Singida, mmoja Kilimanjaro na mmoja kutoka mkoani Pwani.
Mganga Mkuu wa Serikali wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Mohammed Kambi, ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya ugonjwa huo nchini
Amesema kwa mujibu wa taarifa ya siku tisa hadi jana, kuna ongezeko la wagonjwa 674 sawa wastani wa wagonjwa 75 kwa kila siku, ikiwa ni tofauti ya wastani wa wagonjwa 32 waliopatikana Aprili mwaka huu.
Amesema wagonjwa wawili waliopatikana katika mikoa ya Kilimanjaro na Pwani wametoka jijini Dar es Salaam.
"Ongezeko hili linatokana na kuongezeka kwa uelewa kuhusu ugonjwa huu kwa wananchi walio wengi wenye dalili na hivyo wanajitokeza kupata huduma za uchunguzi ambazo zimeendelea kupanuka kwenye vituo vyetu katika mkoa wa Dar es Salaam na Tanga," amesema Prof. Kambi.
Ametaja Idadi ya vituo vinavyopima ugonjwa huo imeongezeka hadi kufikia 19 tofauti na vituo saba vilivyokuwapo awali.
Waziri Mbarawa Ateua Wakurugenzi Watatu
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa, Mei 16, 2019 amefanya uteuzi wa Wakurugenzi watendaji watatu wa mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira.
Taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa Wizara hiyo Prof. Kitila Mkumbo imeeleza kuwa walioteuliwa ni Mhandisi Mbike Jones Lyimo ambaye atakuwa Mkurugenzi wa KUWASA mkoani Kigoma.
Mwingine ni Bi. Flaviana Kifizi, ambaye amekuwa mkurugenzi wa SHUWASA mkoa wa Shinyanga.
Wa tatu katika walioteuliwa ni Mhandisi Robert Lupoja ambaye anakuwa mkurugenzi wa MUWASA huko Musoma mkoani Mara.
Serikali Yasema Bado Inaendelea Na Majadiliano Kuhusu Bandari Ya Bagamoyo
MKURUGENZI na Msemaji Mkuu wa, Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali inaendelea na majadiliano kuhusu kuendelea na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani ili kuona kama inaweza kuwa na tija kiuchumi kwa upande wa Tanzania.
Dkt. Abbasi alisema Serikali ina uwezo wa kujenga bandari nyingi na kwa kuwa Tanzania ina ukanda mkubwa wa ufukwe wa bahari na kwamba bado majadiliano yenye tija kwa Taifa yanaendelea kufanywa baina ya Serikali ya Tanzania na wawekezaji wa mradi huo.
“Serikali haijasema kuwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni hatari, tunaendelea na majadiliano ya utekelezaji wa mradi huo, nchi yetu imejaliwa ukanda mkubwa wa ufukwe wa bahari kwa hiyo tuna uwezo wa kujenga Bandari nyingi tu, hii ya Bagamoyo si kweli kuwa imeachwa kuna mambo ya msingi tunayajadili na tusipofikia maamuzi tutaachana nayo” alisema Dkt Abbasi.
Kuhusu suala la uwekezaji wa vitu aliloulizwa kwenye kipindi hicho Dr Abbasi alisema Serikali haitaacha kuwekeza kwenye vitu kwa sababu vitu husaidia maendeleo ya watu, mfano afya, elimu na miundombinu mingine.
“Kwenye sekta ya madini tumekuachia fedha, dawa hospitalini tumeongeza na bei zimepungua, tumekuletea yote hayo lakini bado unasema huna pesa mfukoni, Serikali inafanya yote haya kuhakikisha kuwa uchumi wetu unaleta manufaa mapana kwa Taifa” alisema Dkt. Abbasi.
Kuhusu uhuru wa Habari na kufungia magazeti yasiyofuata sheria za uchapishaji Msemaji huyo wa Serikali alisema kuwa ofisi yake haikurupuki kufungia magazeti, na kusema kuwa ni magazeti mitatu tu yalifungiwa kati ya 266 yaliyosajiliwa nchini na kuwataka wamiliki wa magazeti hayo kufuata sheria.
Kuhusu malamiko ya wafanyabiashara kwenye maeneo mbalimbali nchini ya kufunga biashara hizo kwa kisingizio cha kodi na tozo mbalimbali, Dkt. Abbasi alisema ni muhimu wakaelewa kwamba kwa sasa Serikali inapita katika kipindi cha mabadiliko na hakuna siku serikali haitadai kodi huku akieleza kuwa kodi nyingi zimepunguzwa hususan kwenye sekta za Kilimo, Mifugo na uvuvi.
“Kwanza tukubali tunapita kwenye kipindi cha mabadiliko, hakuna siku serikali haitadai kodi kwa sababu ndio msingi wa maendeleo ya nchi hii, kuna dhana ilijengeka kuwa unaweza kufanya biashara bila kulipa kodi hiyo sasa haipo, lazima tuangalie changamoto ambazo zinakumba sekta mbalimbali mfano sekta ya kilimo, miufgo na uvubvi kulikuwa na kodi zaidi ya 150, serikali imefuta zaidi ya kodi 80 hadi 100” alisema Dkt Abbasi.
Mwisho.
Salum Ramadhan Salum AMEPOTEA Na Anatafutwa na Familia. Ukifanikiwa Kumuona Mahali Popote Toa Taarifa Polisi au Piga Simu Hizi
Mara ya mwisho ameonekana stendi ya Ukonga madafu akipanda gari ya kutoka Gongo la Mboto likielekea buguruni ikiwa ni safari yake ya kurejea nyumbani majira ya saa 2 usiku.
Alikuwa amevaa shati jeupe na Suruali ya kijivu na saa rangi ya dhahabu na sendoz za wazi.
Tafadhali toa taarifa kituo cha polisi kilicho karibu na wewe au naomba unijulishe kwa kupiga ama kuandika sms kwenda nda namba 0713/0766-202748.
Aliyepotea ni shemeji yangu kabisa na mimi ndiye mlezi wake.
Ni kijana mpole na mwenyeji wa Kiwalani BomBom kwa DSM na Mwanza ndio alipozaliwa.
Picha zake ni kama unavyoweza kuona viambatanisho vya ujumbe huu.
Naaomba Ushirikiano wenu kwenye changamoto hii.







