Thursday, 16 May 2019

CHADEMA WAZUNGUMZIA SINTOFAHAMU INAYOENDELEA BUNGE LA AFRIKA, SPIKA NDUGAI NA MASELE


Makamu wa rais wa Kwanza wa rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akiendelea na shughuli za bunge la Afrika leo Mei 16,2019, juu ni Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang akiendesha kikao cha bunge.

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kumekuwa na taarifa zinazosambaa katika njia mbalimbali za upashanaji habari mitandaoni na baadae kwenye vyombo vya habari tangu asubuhi ya leo kuhusu kile kinachoonekana kuwa ni sintofahamu kubwa inayoendelea katika Bunge la Afrika (PAP) ambako taarifa zimedai kuwa Rais wa PAP, Roger Nkodo Dang anatakiwa kujadiliwa na Bunge hilo kutokana na tuhuma nzito zinazomkabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, unyanyasaji wa kingono, upendeleo na unyanyasaji kwa wafanyakazi wa Ofisi za Makao Makuu ya Bunge hilo, nchini Afrika Kusini.

Taarifa hizo za maneno zilizokuwa zikisambaa zilipewa nguvu na video fupi iliyorekodiwa ikimuonesha Makamu wa Rais wa PAP, Stepehen Maselle (ambaye ni mmoja wa wawakilishi wanne katika PAP) akizungumza wakati akiongoza mojawapo ya vikao vya Bunge hilo vinavyoendelea nchini Afrika Kusini kwa sasa, ambapo amesikika (tafsiri yetu ya Kiswahili) akimlalamikia Rais wa PAP kuwa amemwandikia barua Spika wa Bunge la Tanzania ili amrejeshe Stephen Masele nchini (recalling) ili ikiwa ni namna ya Rais huyo kupambana kuzuia agenda au taarifa ya Kamati Maalum iliyoundwa kuchunguza tuhuma zake isisomwe, kujadiliwa au kufanyiwa kazi na Bunge hilo. Katika video hiyo Mbunge huyo amesikika akisema anayo ruhusa kutoka kwa Waziri Mkuu (Serikalini) hivyo hataondoka nchini Afrika Kusini kama ambavyo Rais huyo wa PAP anataka iwe, katikati ya mapambano yake ya kujisafisha na tuhuma hizo nzito zinazomkabili.

Kabla Watanzania hawajaelewa hasa kinachoendelea, kutokana na mkanganyiko huo ambao umeanza kushika kasi kwenye vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa, Spika wa Bunge Ndugu Job Ndugai ametoa taarifa ya Bunge akithibitisha maneno yaliyokuwa yakisambaa mitandaoni kuwa Bunge limemuagiza Stephen Maselle arejee nyumbani haraka kuja kujibu tuhuma za ukosefu wa maadili zinazomkabili mbele ya Kamati ya Bunge ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge pamoja na Kamati ya Maadili ya Chama chake.

Katikati ya mkanganyiko huu, CHADEMA inapenda kuweka msimamo wake wazi kuwa jina la nchi yetu Tanzania lisitumike vibaya wala kuwekewa taswira hasi na kuendelea kuharibu sura yetu kidiplomasia na katika mahusiano ya kimataifa.

Tunasema hivyo tukiwa na taarifa za uhakika kuwa PAP ililazimika kuunda Kamati Maalum kuchunguza tuhuma hizo nzito zinazomkabili Rais wake, Roger Nkodo Dang, za unyanyasi wa kingono kwa watumishi wa kike walioko Makao Makuu ya PAP (imedaiwa takriban wanawake 10 wamejitokeza mbele ya kamati kuthibitisha walivyonyanyaswa kingono bila ridhaa yao), matumizi mabaya ya madaraka, upendeleo dani ya bunge hilo na unyanyasaji kwa watumishi wa ofisi hiyo hali iliyosababisha kuwepo kwa mgomo wa watumishi kwa takriban wiki nzima.

Taarifa tulizozipata kutoka ndani ya Bunge hilo zimedai kuwa Rais Roger Nkodo Dang anatumia njia mbalimbali kupambana kujisafisha na tuhuma hizo kwa sababu mbali ya kupoteza nafasi yake hiyo kwenye Bunge la PAP, iwapo zikithibitika kuwa ni kweli, pia zitamuondolea kinga za kidiplomasia alizonazo, huku ikijulikana wazi kuwa tuhuma hizo zinazomkabili ni mojawapo ya makosa makubwa ya kijinai yanayochukuliwa kwa uzito mkubwa nchini Afrika Kusini.

Katika mazingira hayo, kitendo cha Bunge kumrejesha nyumbani kwa haraka Makamu wa Rais wa PAP, Stephen Masele ambaye kiutaratibu ndiye aliyetakiwa kuongoza vikao vya Bunge hilo vinapojadili taarifa ya Kamati Maalum kuhusu tuhuma za Rais na kusimamia utekelezaji wa maazimio, inaibua shaka kubwa na kujenga taswira hasi kwa nchi yetu kuwa inatumika au inataka kutumika kumuokoa Rais Roger Nkodo Dang dhidi ya tuhuma hizo au haitaki kuonekana kuwa imesimamia na kuongoza taratibu zinazotakiwa katika suala linalomsibu na pengine kitakachofuatia.

Hivyo basi ili kuiweka nchi yetu katika mahusiano mazuri ya kimataifa na kuendeleza sifa yetu iliyojengwa kwa miaka mingi huko nyuma kuwa Tanzania inasimamia misingi na taratibu na kuondoa kadhia itakayoijengea nchi yetu picha mbaya, si ndani ya nchi pekee mbali kimataifa pia, tunalitaka Bunge (lililomrejesha nyumbani Stephen Masele) na Serikali ya Tanzania ambayo imedaiwa kumwagiza Stephen Masele aendelee kubaki huko hadi amalize majukumu yake, kutoa kauli ya msimamo wetu Tanzania kuhusu tuhuma zinazomkabili Rais wa PAP. Je ni kweli tunaunga mkono unyanyasaji wa kingono? Je tunaunga mkono matumizi mabaya ya madaraka ikiwemo rushwa? Je tunaunga mkono unyanyasaji? Je tunaunga mkono upendeleo katika taasisi hiyo ya kimataifa?

Ni msimamo huo pekee utaweza kuiokoa Tanzania katika jambo hilo ambalo limeanza kuchukua mkondo mbaya kuwa nchi yetu inatumika kulinda tuhuma za uhalifu wa kijinai.
Aidha, kwa sababu Spika wa Bunge ameshalizungumzia na kulitolea taarifa suala hilo hatua iliyomaliza utata wa iwapo taarifa zilizokuwa zikisambaa mitandaoni zilikuwa za kweli, tunalitaka Bunge kuweka wazi tuhuma zinazomkabili Mbunge Stephen Masele zilizosababisha arejeshwe nchini na uwakilishi wake (wa nchi) katika taasisi hiyo ya kimataifa kusitishwa.

Halikadhalika, CHADEMA inaitaka mihimili ya Serikali na Bunge kutoka hadharani na kutoa kauli kuueleza umma juu ya madai kuwa kuna hali ya mgongano wa kauli, misimamo na maamuzi baina ya mihimili hiyo miwili juu ya suala hilo, kiasi ambacho kimeanza kuleta athari katika uwakilishi wa nchi yetu kwenye PAP. Kauli ya mihimili hiyo itawasaidia wawakilishi watatu wa Tanzania waliosalia kwenye PAP kujua misingi ya hoja zao na masuala wanayotakiwa kusimamia katika mtanziko huu uliopo.

Imetolewa leo Alhamis, Mei 16, 2019 na;


Share:

Ujumbe wa Chuchu Hansy kwenye Birthday ya Ray Kigosi

Msanii wa  Bongo Movie, Chuchu Hansy amefunguka kuhusu mzazi mwenzake Vicent Kigosi (Ray), kuwa baada ya kupata mtoto wao aitwaye Jaden, Ray alijiona baba mpaka wa watoto waliokomaa.

 Chuchu amefunguka hilo leo kupitia ukurasa wake wa Instagram wakati akimtakia heri ya siku ya kuzaliwa mzazi mwenzake huyo.

“Happy Birthday baba @jadenthegreatest baba mwenye jeuri zako baada ya kupata mtoto ukajiona baba mpk wa watoto wakubwa waliokomaa😊 Ramadhani iii No matter what Nakutakia Happy Birthday MUNGU azidi kukuweka inshaalah uje mleane na mwanao sina zawadi kubwa zawadi yangu ni @jadenthegreatest na natumai ni zawadi ya milele na yenye historia kwako..Enjoy ur day@raythegreatest @raythegreate“ Ameandika



Share:

Waziri Kakunda: “Kuleni korosho zinaongeza heshima ya ndoa"

Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda, amewashauri Watanzania kula korosho kwa sababu zina virutubisho vya kurudisha heshima ndani ya ndoa.

Kakunda ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Mei 16, kuwaelezea maendeleo ya ununuzi wa korosho, ambapo pamoja na mambo mengine amesema hata watu wa mikoa ya kusini wanazaliana sana kwa sababu wanakula korosho kwa wingi.

“Korosho ni kirutubisho kizuri, ni ajabu Watanzania hawataki kuzitumia, zinaongeza virutubisho, na kuongeza heshima ya ndoa.” amesema Waziri Kakunda.


Share:

Mbunge aliyetuhumiwa kufumaniwa na mumewe abadilisha jina rasmi

Mbunge wa Segerea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bonnah Kaluwa ametoa taarifa ya kubadilisha jina kufuatia kuingia kwenye mvutano wa matumizi ya jina na mume wake Moses Kaluwa ambapo sasa atafahamika kwa jina la Bonnah Kimoli.

Uamuzi wa Mbunge huyo wa Segerea umetangazwa leo Mei 16,2019 Bungeni jijini Dodoma kupitia Spika wa Bunge, Job Ndugai ambapo amesema ameeleza kupata taarifa kutoka kwa mbunge huyo.

“Nimetaarifiwa kuwa Mheshimiwa Bonnah amebadili jina na sasa anatumia jina la Bonnah Ladislaus Kamoli”, amesema Spika Ndugai.

April 28, 2019 kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mbunge huyo wa Segerea  aliandika ujumbe kwamba tuhuma ambazo zilikuwa zikisambaa kwenye mtandao wa kijamii kuwa alifumaniwa na mumewe hazikuwa na ukweli.

"Wahenga wanasema jambo likiongelewa sana bila majibu linaweza kugeuka likawa kweli. Sasa ni hivi mimi Bonnah Ladislaus Kamoli au jina langu lingine Neema, sijawahi kufumaniwa hata siku moja katika maisha yangu". aliandika Bonnah

"Sio kwamba mimi ni muadilifu sana au malaika ila hapakuwepo na mtu wa kunifumania nadhani mtakua mmenielewa na sitaongea tena na kama kuna mtu ana ushahidi alete na kanifumania na nani", alimaliza Bonnah katika maelezo yake.


Share:

Watu 80 wamematwa Nigeria kwa tuhuma za kula wakati wa Ramadhan

Polisi katika Jimbo la Kano, kaskazini mwa Nigeria wamewakamata kwa muda watu 80 waliotuhumiwa kwa kula hadharani badala ya kufunga kuanzia alfajiri hadi jua linapotua kulingana na maagizo ya dini ya Kiislamu katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Polisi wa Sharia, wanaofahamika kama Hisbah, wanasema kuwa watu hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali ya mji wa Kano katika kipindi cha siku kadhaa.

Jimbo la Kano ni moja kati ya majimbo kadhaa ya kaskazini mwa Nigeria ambako Sharia ya Kiislamu ilianzishwa upya tangu mwaka 2000.

Sharia ya Kiislamu inatekelezwa sambamba na sheria ya kawaida kwenye majimbo hayo.

Msemaji wa Hisbah katika jimbo la Kano, Adamu Yahaya ameiambia BBC kuwa wote waliokamatwa walikuwa ni Waislamu na maofisa hawawalengi wasio Waislamu kwa sababu hawafungwi na sheria ya Kiislamu.

Amesema kuwa baadhi ya wale waliokamatwa waliiambia ofisi ya Sharia kuwa walikuwa wanakula kwa sababu hawakuona binafsi mwezi, huku wengine wakisema walikuwa ni wagonjwa, lakini maofisa walisema kuwa madai yao hayakuwa na msingi wowote.

Watu hao 80 walionywa na kuachiliwa huru kwa sababu walikuwa wamefanya kosa hilo kwa ''mara ya kwanza'' alisema Yahaya.

Walionywa kuwa iwapo watakamatwa tena, watapelekwa mahakamani.

Hisbah wamesema kuwa wataendelea kufanya doria katika kipindi chote cha Ramadhani kwa lengo la kuwakamata Waislamu wote ambao hawafungi katika mwezi huu.

Mfungo wa Ramadhani ni lazima kwa kila mtu mzima Mwislamu, lakini baadhi ya watu kama vile wagonjwa  hawatakiwi kufunga.


Share:

Notice To Travelers Planning To Visit Tanzania

The Government of Tanzania wishes to make an official note to travelers planning to visit Tanzania that from 1st June 2019 all plastic carrier bags, regardless of their thickness will be prohibited from being imported, exported, manufactured, sold, stored, supplied and used in Mainland Tanzania.
 
However, plastic or plastic packaging for medical services, industrial products, construction industry, agricultural sector, foodstuff, sanitary and waste management are not prohibited.

Visitors to Tanzania are advised to avoid carrying plastic carrier bags or packing plastic carrier bags or items in plastic carrier bags in the suitcase or hand luggage before embarking on visit to Tanzania. Special desk will be designated at all entry points for surrender of plastics carrier bags that visitors may be bringing into Tanzania.

Plastics carrier items known as “ziploc bags” that are specifically used to carry toiletries will be permitted as they are expected to remain in the permanent possession of visitors and are not expected to be disposed in the country.

The Government does not intend for visitors to Tanzania to find their stay unpleasant as we enforce the ban. However, the Government expects that, in appreciation of the imperative to protect the environment and keep our country clean and beautiful, our visitors will accept minor inconveniences resulting from the plastic bags ban.
 
For further inquiries please contact ps@vpo.go.tz,      www.vpo.go.tz,        Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania,     @vpotanzania,       @VPOTanzania,      +255 685 333 444, +255 743 715 629.                    

Issued by
Government Communication Unit


Share:

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. Simu:   0759208637 au 0620510598


Share:

Kujichua Kwa Muda Mrefu Husababisha Maumbile ya Kiume Kusinyaa na Kupungukiwa Nguvu za Kiume

Wanaume  wengi  waliofanya  mchezo wa  kujichua  kwa  muda  mrefu hupatwa  na  madhara  ya kuwa  na  kusinyaa  na  kudumaa  kwa  maumbile  yao  ya  kiume  ambayo  huenda  pamoja  na  tatizo  a  Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume.

Tendo  la  kujichua  kwa  mwanaume  linapofanyika  kwa  kipindi  kirefu huathiri na  kuharibu mishipa  na  misuli  ya uume  na  hivyo  kusababisha  kujengeka  kwa mafuta na tishu zisizo vutika  kwenye  mishipa  ya  ateri.  Jambo  hili  husababisha  makuu mawili; 1. Huzuia  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  kuongezeka jambo  linalotajwa  na  wanasayansi  kama jambo  muhimu  sana  katika  kukua  kwa  uume. 2. Huzuika  kutirika  kwa  damu  kuingia  kwenye  misuli  ya  uume.

Mambo  hayo  mawili  huathiri  sana  ukuaji  wa  maumbile ya kiume  kwa  sababu  yanapo tokea huathiri uzalishaji  wa  homoni  muhimu  zinazo  husika  na  ukuaji  wa  misuli  ya  uume na matokeo  yake husababisha  uume  wa  mhusika  kudumaa, kusinyaa,kunywea  na  kurudi ndani  kiasi  cha  kuufanya  uonekane  kama uume  wa  mtoto.
 
Hii ndio  sababu  kwanini watu  wengi  walio athirika  na  punyeto  hulalamika  kwamba  maumbile  yao  ya  kiume  hayajaongezeka  tangu  walipo anza  kujihusisha  na  punyeto  wakiwa  na  umri mdogo. 

Maumbile  yao  huonekana  kama  ya  watoto  kwa  sababu hayakupata  nafasi  ya  kupokea  vichochea  vya  kuyafanya  yakue  na  kuongezeka  tangu  walipo  anza  kujihusisha  na  punyeto.

Suluhisho  La  Tatizo La Maumbile  Ya  Kiume  Yaliyo  Sinyaa  Kwa  Sababu  Ya  Punyeto.
Kama  bado  unaendelea  kujihusisha  na punyeto  basi  jitahidi  uache  tabia  hiyo  mara  moja  kwani  inakuharibu. Inaweza  isiwe  rahisi  sana  kuacha  mara  moja  lakini  ukiweka  nia  thabiti  basi  unaweza  kuacha  kabisa  kama  walivyofanikiwa  kuacha  wengine  ambao  walikuwa  wametopea  kwenye  tabia  hiyo  lakini  wakajitahidi  kujilazimisha  na  hatimaye  wakafanikiwa  kuachana  kabisa  na  tabia  hiyo.

==>> Acha kuangalia video chafu za ngono.
Video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayoiona utataka ukaipigie  punyeto hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako.. 


Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.

==>>Epuka kukaa nyumbani peke yako;
Mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine. 


Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata kama vile misuli ya uume kulegea, kushindwa kurudia tendo uwapo na mwenzi wako, kuishiwa nguvu za kiume, maumbile kusinyaa, kurudi ndani na kuwa kama ya mtoto mdogo.

Acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema hivyohivo, kama unaacha acha mara moja ili utunze heshima yako mbele ya mwenzi au mke wako.

Kama utaona  kuna  ugumu  wa  kuacha  tabia  hiyo  na tayari ushaapata madhara ya maumbile kusinyaa na kupungiwa nguvu za kiume, basi  wasiliana nasi kwa ushauri zaidi; Simu  0715741788 au 0754741788


Share:

Serikali Yaanza Kusambaza Gesi Asilia Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam

Serikali  imeanza kutekeleza mradi wa kusambaza gesi asilia katika miji ya Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam ikiwa ni nishati mbadala   kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu Mgalu aliyasema hayo  bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibiti, Ally Ungando (CCM).

Katika swali lake, Ungando  alihoji Serikali inamkakati gani wa kupeleka nishati mbadala katika Jimbo lake ikiwa ni pamoja ni aina  gani ya nishati itakayotumika badala ya kuni na mkaa.

Mbunge huyo alisema  wananchi wanaoishi katika Jimbo la Kibiti hutumia   kuni kwa matumizi ya nyumbani, shuleni, gerezani hivyo husababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kukata miti hovyo .

‘Je serikali inamkakati gani wa kupeleka nishati mbadala? Na je ni aina gani ya nishati itakayotumika badala ya kuni na mkaa?” aliuliza Ungando.

Akijibu, Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu, alisema  Mei 18 mwaka 2018 serikali kupitia Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ilisaini mkataba wa kampuni ya Mihan Gas kwa ajili ya kusambaza vifaa vya kupikia mitungi ya gesi na majiko kwa watumishi wa umma na wananchi wengine   mpango  unaolenga kupunguza matumizi ya mkaa na kuni.

 Mgalu alisema   Sera ya Taifa ya Nishati ya Mwaka 2015 imetoa muongozo wa kuboresha maisha ya wananchi kwa matumizi bora ya nishati kupitia teknolojia ya kisasa badala ya kuni na mkaa.


Share:

Huawei na mashirika yake mengine 70 yawekwa katika orodha nyeusi ya Marekani

Wizara ya Biashara ya Marekani imetangaza kuliweka Shirika la Huawei pamoja na mashirika mengine yapatayo 70 yanayofungamana nalo katika orodha yake nyeusi.

Hatua hiyo iliyotangazwa na wizara hiyo ya Marekani inasema kwamba baada ya hapo shirika hilo litazuiwa kununua vifaa kutoka kwa mashirika ya Kimarekani isipokuwa baada ya kupata idhini ya serikali ya Washington. 

Wizara ya Biashara ya Marekani imedai kwamba, kuna ushahidi unaoifanya Washington kuamini kwamba shughuli za shirika hilo, zinakiuka usalama wa taifa wa nchi hiyo. 

Aidha viongozi wa Marekani wamedai kwamba uamuzi huo utapelekea kuwa magumu mauzo ya baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na Huawei ndani ya Marekani au kulifanya jambo hilo kutowezekana kabisa. 

Jumatano ya jana Rais Donald Trump wa Marekani alitia saini sheria ambayo inapiga marufuku vifaa vya mawasiliano vilivyotengenezwa na mashirika ambayo yanahatarisha usalama wa taifa wa Marekani.
 
Tayari shirika hilo limetoa taarifa ya kulaani hatua hiyo ya Marekani na kuongeza kwamba, uamuzi huo wa Washington unakiuka sheria za kimataifa. 

Serikali ya Trump na kwa visingizio tofauti vikiwemo vitisho vya kiusalama, imekuwa ikishadidisha mashinikizo dhidi ya washirika wake likiwemo Shirika la Huawei ambalo ni shirika kubwa la mawasiliano la China kuuza bidhaa zake ndani ya taifa hilo. 

Hii ni katika hali ambayo Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amedai kwamba shirika hilo la mawasiliano la Huawei linaisaidia serikali ya Beijing kufanya ujasusi.


Share:

Serikali yatoa sababu ya kuvunja mkataba na kampuni ya kununua korosho kutoka Kenya

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda amesema Kampuni ya Indo power ya Kenya iliyokuwa imeingia mkataba wa kununua korosho tani 100,000 ilistahili na ilkuwa halali.

Kakunda ameyasema hayo wakati akihitimisha hotuba yake ya bajeti bungeni jana, Mei 15, ambapo alisisitiza kuwa kampuni hiyo inatambulika nchini Kenya, Afrika Mashariki na dunia nzima.

Alisema kilichosababisha Tanzania kuvunja mkataba huo ni baada ya kampuni hiyo kuchelewa kukamilisha taratibu kadhaa walizokubaliana.


Share:

Ofisi ya CAG Yakaguliwa, Spika Ndugai Anena

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema taarifa ya ukaguzi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imekamilika huku akisema ‘katika ukaguzi hakuna anayejikagua mwenyewe.’

Akitoa taarifa hiyo leo Alhamisi Mei 16, 2019, bungeni, Spika Ndugai amesema kwa mujibu wa sheria ya ukaguzi wa umma, hesabu za ofisi ya CAG hupitiwa na Bunge kwa kuielekeza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kufanya kazi hiyo.

 "Ningependa kuwajulisha juu ya taarifa ya  ukaguzi wa ofisi ya CAG kwa mwaka fedha unaoshia Juni, 2018, hesabu za CAG zinapaswa kukaguliwa walau mara moja kwa mwaka, PAC inajukumu la kukagua ofisi hiyo, kazi imeshafanyika na tumeletewa  taarifa," amesema.

Ameendelea kwa kusema kuwa, "Taarifa ya kukaguliwa ofisi ya CAG, nimeshaipitia kuna mambo, lakini kiutaratibu nimeshaipeleka PAC na wakishamaliza uchambuzi watawasilisha kwangu, niwataarifu kwenye masuala ya ukaguzi hakuna anayebaki kila watu wanawakagua wenzao,".



Share:

Soika Ndugai Atangaza kusitisha uwakilishi wa Mbunge Stephen Masele kwenye Bunge la Afrika (PAP) Kwa Utovu Wa Nidhamu

Spika Job Ndugai ametangaza kusitisha uwakilishi wa Mbunge Stephen Masele kwenye Bunge la Afrika (PAP) ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Bunge hilo kwa tuhuma za utovu wa nidhamu mpaka atakapohojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.

Ndugai ametangaza uamuzi huo leo Alhamisi, Mei 16, 2019 wakati akizungumza bungeni jijini Dodoma.

“Tunao wabunge wanaotuwakilisha kwenye mabunge mbalimbali ya Afrika ikiwemo SADC, Pan African Parliament (PAP), African Caribbean Pacific, Bunge la Afrika Mashariki na Bunge la Maziwa Makuu, wamekuwa wakifanya vizuri katika kutuwakilisha.

“Lakini katika Bunge la Afrika (PAP) kumetokea matatizo makubwa hasa kwa Mheshimiwa Stephen Masele ambayo nisingependa kuyafafanua kwa sababu muda hautoshi, tumelazimika kumtafuta na kumrudisha nyumbani kuanzia Jumatatu lakini ameonyesha kugoma.

“Baada ya kumwandikia barua arudi nyumbani aje kwenye kamati yetu ya maadili, jana wakati akihutubia bunge hilo alisema japo ameitwa na spika, lakini waziri mkuu amemwambia abaki na aendelee na mambo yake, kitu ambacho ni uongo na anatudhalilisha kama nchi.

“Masele ni kiongozi ambaye amekuwa akifanya mambo ya hovyohovyo, ndiyo maana tumemuita atufafanulie huenda yuko sahihi, lakini anafanya mambo ambayo ni hatari kubwa, amejisahau sana, amekuwa akichonganisha mihimili ya Serikali tena ya juu kabisa, hajui hata anatafuta nini.

"Kwa kuwa hataki kuja, nimemwandikia barua Rais wa PAP (Roger Nkodo Dang) ya kusitisha uwakilishi wa Mheshimiwa Masele kwenye bunge la PAP, hadi Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge itakapomalizana naye hapa. Pia, kamati ya maadili ya chama chake (CCM). Kwa hiyo kuanzia sasa siyo mbunge tena wa PAP mpaka tutakapomalizana naye hapa nyumbani,” amesema Ndugai.


Share:

Serikali Kufanya Ukaguzi Na Tathmini Ya Kina Ya Miradi Yote Ya Umwagiliaji Nchini

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo, Dodoma
Serikali iko katika mchakato wa kufanya ukaguzi na tathmini ya kina ya miradi yote ya umwagiliaji nchini ili kufanya uhakiki wa eneo la umwagiliaji kwa lengo la kubaini ubora wa miradi, thamani ya fedha, gharama za mradi na mahitaji halisi ya sasa ya kuboresha, kuendeleza na kuongeza miradi mipya ya umwagiliaji.

Aidha, baada ya tathmini hiyo Serikali itaendelea kutafuta fedha ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha mabwawa na skimu za umwagiliaji nchini ikiwemo mradi wa umwagiliaji katika bonde la Mkomazi zinaendelezwa na kuwanufaisha wananchi wa Mombo na taifa kwa ujumla.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 16 Mei 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Mhe Timotheo Mnzava aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali katika utekelezaji wa mradi wa Umwagiliaji katika Bonde la mto Mkomazi.

Alisema kuwa katika miaka ya 1980 Serikali kupitia washirika wa maendeleo, Wakala wa Ushirikiano wa Kitalaam wa kimataifa wa Serikali ya Ujerumani (Germany Agency for Technical Cooperation Ltd) ulifanya upembuzi yakinifu (Feasibility studies)kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Mkomazi katika tarafa ya Mombo, Halmashauri ya Korogwe. Hata hivyo taarifa za upembuzi yakinifu na usanifu zilibaini kuwa ujenzi wa bwawa hilo ungesababisha kuongezeka kwa maji katika ziwa Manga na kupelekea kuzama kwa Kijiji cha Manga Mikocheni pamoja na mashamba ya wakulima.

Mhe Mgumba alisema kuwa kutokana na changamoto hiyo katika mwaka 2014/2015, wataalam wa ofisi ya kanda ya umwagiliaji ya Kilimanjaro walifanya mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu uliofanywa katika eneo hilo kwa lengo kuepusha uwezekano wa kufurika kwa Ziwa Manga, kuzama kwa Kijiji cha Manga Mikocheni na Mashamba ya wakulima kutokana na ujenzi wa bwawa. Mapitio hayo yalibaini uwezekano wa ujenzi wa bwawa na mradi wa umwagiliaji katika eneo hilo bila kuathiri wakazi wa eneo hilo. Mapitio ya usanifu huo yalibaini kuwa ujenzi wa bwawa pekee utagharimu Shilingi 1,543,736,877.

Aidha, akijibu swali la Mbunge wa Kondoa Mjini Mhe Edwin Mgate Dannda aliyetaka kufahamu ni lini andiko la mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Kijiji cha Mongoroma, Kata ya Serya wenye eneo la ekari 3000 utaanza utekelezaji wake, Mhe Mgumba alisema kuwakatika bajeti ya mwaka 2010/2011 Serikali kupitia Idara ya Umwagiliaji ilituma  Shilingi milioni 300 kwa ajili kuendeleza miradi ya umwagiliaji ya Kisese, Kidoka na Mongoroma Serya katika Halmashauri ya Wilaya ya  Kondoa wakati huo.
 
Alisema Kati ya fedha hizo  Shilingi 143,265,000 zilitumika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu katika mradi wa Mongoroma Serya uliopo katika Kata ya Serya. Kazi zilizofanyika ni pamoja na upimaji wa sura ya ardhi (Topographical Survey), usanifu wa kina (detail design), matayarisho ya gharama za ujenzi, tathmini ya rasilimali maji (Hydrological survey), tathmini ya awali ya mazingira, utafiti wa udongo (Soil analysis) na masuala ya jamii.
 
Aliongeza kuwa Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa bwawa la Mongoroma Serya ulibaini kuwa bwawa hilo lingegharimu Shilingi bilioni 4 kwa wakati huo. Aidha, bwawa hilo lingekuwa na uwezo wa kumwagilia zaidi ya hekta 3,000 na kunufaisha zaidi ya wakulima12,000 kwa ajiili ya kilimo cha umwagiliaji, matumizi ya binadamu, unyweshaji wa mifugo na wanyama pori pamoja na ufugaji wa samaki katika vijiji  vya Mongoroma, Serya na Munguri.
 
Mgumba alisema Serikali iko katika mchakato wa kufanya tathmini ya kina kwa miradi yote ya umwagiliaji nchini ili kubaini thamani ya fedha, ubora wa miradi na mahitaji halisi ya uboreshwaji, uendelezwaji na kuchagua miradi michache kwa utekelezaji wa ujenzi kwa miradi yenye TIJA, matokeo na manufaa makubwa kwa wakulima na Taifa kwa ujumla. Aidha, baada ya tathmini hiyo na kutegemea upatikanaji wa fedha serikali itahakikisha bwawa hilo na skimu zingine zitajengwa.


Share:

Bilioni 14.9 yakusanywa na TRA Njombe

Na Amiri kilagalila-Njombe
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Njombe imefanikiwa kukusanya bilioni 14.9 ya mapato katika mwaka wa fedha 2018/2019 hadi sasa ,licha ya bajeti ya makadilio kuwa bil 17 na kutoa pongezi kwa wilaya ya njombe ambayo imekusanya zaidi ya asilimia 70.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya elimu kwa mlipa kodi mkoani Njombe iliyofanyika mjini Makambako,Afisa mwandamizi wa kodi mkoa wa Njombe Adeliki Alphonce amesema kuwa licha ya kufanikiwa kukusanya kiasi hicho cha fedha lakini bado kuna upungufu wa shilingi bilioni 3.1 ili kukamilisha lengo.

"Mpaka sasa wananchi wenzangu tumeweza kukusanya shilingi bilioni 14.9 katika yale malengo ya bilioni 17 bado tunaupungufu wa bilioni 3.1 kwa hiyo wafanyabiashara tujitoe katika muda uliobaki tuweze kufikisha lengo,tuzitumie hizi mashine za elektroniki na tusione kama TRA wanakuja kutusumbua"alisema Adeliko Alphonce

Aidha katika kuhakikisha mkoa wa Njombe unakuwa kinara kwa ukusanyaji wa mapato mkuu wa wilaya ya Njombe akizindua wiki ya elimu kwa mlipa kodi amezitaka halmashauri kuondoa vikwazo visivyo na tija kwa wawekezaji wa viwanda ili kuwavutia wawekezaji na kukuza uchumi wa kaya , mkoa na taifa kwa ujumla.

"Kama alivyotueleza mh.Rais alipokuwa kwenye mkutano wake wa kwanza katika mkoa wa Njombe kwenye wilaya ya Njombe sehemu inaitwa Lwangu halmashauri ya mji wa Njombe alisema,tunatabia ya kuchelewesha wawekezaji na haya yanafanywa ndani ya halmashauri na mimi nirudie kuwaomba wale wanaohusika na ardhi saidieni ili tuhakikishe kwamba ili tuweze kulipa kodi na kwa ziada na sisi mchango wetu uonekane mkubwa zaidi tupate viwanda"alisema Msafiri 

Licha ya mamlaka hiyo kuonyesha juhudi katika kukusanya mapato lakini Wafanyabiashara mjini Makambako mkoani hapo ulipofanyika uzinduzi, wamesema kuwa hali ya biashara imezidi kuwa mbaya na kusababisha wafanyabiashara wenye mitaji midogo kufunga maduka kutokana na kuwepo kwa mrundikano mkubwa wa tozo ambapo wamedai kuwa wamekuwa wakitozwa tozo zaidi ya kumi katika mlango mmoja wa biashara hatua ambayo inakwamisha maendeleo yao na kuiomba serikali kuweka tozo hizo katika kapu moja.


Share:

Tanzania yapongezwa kwa ukuaji mzuri wa Uchumi




Share:

Kampuni Ya Infinix Na TIGO Yaleta Mapinduzi Ya Selfie Kupitia Infinix S4 Yenye 32mp.


Kampuni ya simu ya Infinix inayozalisha simu zenye teknolojia ya hali ya juu, imezindua simu mpya aina ya Infinix S4 yenye megapixel 32 AI selfie kwajili ya kuwawezesha watanzania kufikia ndoto zao kupitia matumizi ya teknolojia. Na kwa ushirikiano wa TIGO na Infinix, Infinix S4 itapatikana katika maduka ya Infinix na TIGO ikiwa na ofa ya bundle la miezi sita.   

Infinix na Tigo zimeungana katika uzinduzi wa Infinix S4 kuhakikisha wateja na Watanzania kwa ujumla wanaingia katika mapinduzi ya simu zenye selfie bora, ambayo sio tu itainua ujuzi na maarifa ya selfie lakini pia itasaidia kuwasogeza katika ulimwengu wa kidigitali. 
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi Mkurugezi mtendaji wa kampuni ya simu ya Infinix Bwana. Hauson Tu,alisema kwamba, “Uwezeshaji kupitia teknolojia ya simu unategemeana na uhakika wa sifa ya simu kama vile kamera ya nyuma, mwonekano mzuri wa screen ya simu, uwezo wa betri na kasi ya simu yenyewe. Kwa kulizingatia hilo Infinix S4 imeundwa ikiwa na kamera tatu za nyuma 13MP+8MP+2MP with a 6.2’ waterdrop display screen kwaajili ya picha bora. Kamera hizi tatu zenye kufanya kazi tatu tofauti ikiwemo kuhakikisha picha inaonekana kwa kina zaidi, hata kwa umbali wa 120º”. 
 
Bwana Tu, “alisisitiza kuhusu umuhimu wa Betri yenye nguvu inayodumu na chaji zaidi akisema, “Infinix haijawahi kuwaangusha wateja wake katika suala la betri. S4 ina Smart power management system kwaajili ya kuzuia matumizi ya chaji kwa application ambazo hazitumiki kwa muda huo na betri hutumika pale tu ambapo application hiyo itakuwa katika matumizi”. 
 
Na kwa upande wake afisa mahusiano wa kampuni ya Tigo Bwana Tarik Boudiaf alisema “Kasi ya mtandao ni muhimu sana katika kumwezesha Mtanzania, ikiwa ni lengo mojawapo kwa kampuni ya Tigo kuhakikisha wateja na Watanzania kwa ujumla wanahamia katika ulimwengu wa kidigitali kama kampuni tumetoa ofa ya bundle la internet la muda wa miezi sita”. 
 
Kampuni ya simu ya Infinix imekuwa ikiwalenga zaidi vijana na watu wenye ushawishi katika maendeleo ya teknolojia, hii imepelekea uzinduzi wa Infinix S4 kuhudhuriwa na wasanii maaruufu kama Lulu Diva, Mimi Mars, Bi Dozen pamoja na vyombo vya habari maarufu. Infinix S4 kwa sasa inapatikana katika maduka yote ya Infinix na TIGO Nchini kote.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger