Friday, 3 May 2019
Ujerumani Yaipatia Tanzania Msaada wa Sh. Bilioni 330 Za Mradi Mkubwa Wa Maji Mkoani Simiyu
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
SERIKALI ya Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo (KfW), imeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 127.7, sawa na sh. bilioni 330, kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria katika mkoa wa Simiyu.
Makubaliano ya msaada huo kupitia mikataba miwili yamesainiwa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James kwa niaba ya Serikali na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani, (KfW) anayeshughulikia nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya, Dkt. Klaus Mueller.
Katika mkataba wa kwanza, kiasi cha Euro 102.7, sawa na shilingi bilioni 265 kimetolewa na Mfuko wa Kimataifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi (Green Climate Fund) na mkataba wa pili unahusisha Euro milioni 25, sawa na sh. bilioni 65 ambazo zimetokelewa na Benki ya Maendeleo ya UJerumani (KfW).
Mbali na mradi wa maji wa Simiyu ambao chanzo chake cha maji ni kutoka Ziwa Victoria, miradi mingine itakayonufaika na msaada huo ni kilimo endelevu cha umwagiliaji, usafi wa mazingira, maji na malisho ya mifugo na kuzijengea uwezo taasisi zitakazotekeleza mradi huo hasa mamlaka za maji katika Wilaya tano za Bariadi, Itilima, Meatu, Busega na Maswa zitakazonufaika na mradi huo.
"Kutokana na umuhimu wa mradi huo wa maji, Serikali kwa upande wake itachangia Euro milioni 40.7 sawa na sh. bilioni 104 na wananchi watakao nufaika na mradi huo watachangia Euro milioni 1.5 sawa na sh. bilioni 3.8 na kufanya gharama za mradi mzima kufikia zaidi ya Euro milioni 171 sawa na zaidi ya sh. bilioni 446" alisema Bw. Doto James
Aliishukuru Serikali ya Ujerumani kupitia Mfuko wake wa Kimataifa wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi (GCF) na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) kwa kutoa kiasi hicho kikubwa cha fedha kitakachotumika kutekeleza mradi huo utakachukua miaka mitano hadi kukamilika kwake.
"Katika kipindi cha miaka mitatu Serikali ya Ujerumani imeipatia Tanzania zaidi ya Euro 202.8 sawa na shilingi bilioni 518.5 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za afya, nishati, uhifadhi wa maliasili, udhibiti wa fedha za umma na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi" alisisitiza Bw. James
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya KfW amesema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Mfuko wa Kimataifa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kutoa kiasi kikubwa cha fedha cha Euro milioni 102.7 kwa mkupuo katika nchi za kiafrika tangu mfuko huo uanzishwe.
"Tunaamini kuwa zaidi ya watu 500,000 watanufaika na mradi huu wa maji kutoka Ziwa Victoria unaohusiana na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa kutuhifadhi vyanzo vya maji, usafi wa mazingira, kuendesha kilimo bora chenye kuhifadhi mazingira" aliongeza Dkt. Mueller.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo, amempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli na uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuipatia Wizara yake zaidi ya shilingi trilioni 3 katika kipindi kifupi cha miaka mili kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maji inayoendelea kujengwa nchini kote.
Alitaja sababu za mkoa wa Simiyu kunufaika na msaada huo kuwa ni mkoa unaokabiliwa na hali mbaya ya hewa ukiwemo ukame na kwamba mradi huo utawawezesha wananchi kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kwamba katika ukanda huo wa Ziwa kutakuwa na miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 1.2 itakayokuwa inatekelezwa.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Mahamoud Mgimwa amesema Bunge litahakikisha linausimamia mradi huo utekelezwe kwa wakati kwa sababu Serikali imedhamiria kwa dhati kuona kwamba wananchi wanapata maji safi na salama kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2025.
Mwisho.
Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.
Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).
Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.
Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;
Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.
Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521
Wimbo Mpya wa Diamond Platnumz ft. Fally Ipupa - Inama
Video Mpya: Best Naso - Ngongingo
Msanii wa muziki Bongo, Best Naso anakukaribisha kutazama video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Ngongingo. Itazame hapa.
Familia yatoa Ratiba Kamili Mazishi Ya Dk Mengi
Kufutia kifo cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dr. Reginald Mengi kilichotokea Mei 2 huko Dubai, familia kupitia kwa mwanasheria wake Michael Ngalo, imeweka wazi ratiba ya msiba.
Akiongea leo Mei 3, 2019 nyumbani kwa Dr. Mengi, Ngalo amesema mwili utawasili nchini Jumatatu ya Mei 6, 2019 na kupelekwa katika hospitali ya Lugalo kwaajili ya kuhifadhiwa.
Aidha Ngalo ameongeza kuwa Jumanne ya Mei 7, 2019, mwili utapelekwa katika ukumbi wa Karimjee, kwaajili ya watu wote kuuga na kisha utarejeshwa nyumbani kwake.
Siku ya Jumatano mwili utasafirishwa kupelekwa Moshi Machame ambako Ibada ya mazishi itafanyika siku ya Alhamis katika kanisa la Kisereni (KKKT).
Akiongea leo Mei 3, 2019 nyumbani kwa Dr. Mengi, Ngalo amesema mwili utawasili nchini Jumatatu ya Mei 6, 2019 na kupelekwa katika hospitali ya Lugalo kwaajili ya kuhifadhiwa.
Aidha Ngalo ameongeza kuwa Jumanne ya Mei 7, 2019, mwili utapelekwa katika ukumbi wa Karimjee, kwaajili ya watu wote kuuga na kisha utarejeshwa nyumbani kwake.
Siku ya Jumatano mwili utasafirishwa kupelekwa Moshi Machame ambako Ibada ya mazishi itafanyika siku ya Alhamis katika kanisa la Kisereni (KKKT).
Serikali Yasema Polisi hawatowi fedha kununua chakula cha mahabusu
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamadi Masauni amesema hakuna utaratibu wa askari polisi kutoa fedha zao mfukoni kwa ajili ya chakula cha mahabusu.
Kauli hiyo aliitoa jana bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Masasi, Rashid Chuachua (CCM).
Katika swali lake Mbunge huyo alitaka kujua serikali ni lini itarekebisha utaratibu uliopo ambapo askari wanalazimika kutoa pesa zao mfukoni ili kuwapa chakuka mahabusu.
Masauni alisema utaratibu uliopo ni kwa serikali kupitia Jeshi la Polisi ina wajaibu wa kuwapatia chakula mahabusu waliopo selo
“Ndugu wa Mahabusu pia wanaruhusiwa kupeleka chakula kwa mahabusu wao ambao wapo korokoroni,” alisema Masauni .
Alisema serikali inatambua uhaba wa vitendea kazi kwa Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja uchache wa magari na nyumba za askari.
Alisema kwa sasa Wilaya ya Masasi ina nyumba za makazi ya askari zipatazo 15 ambazo zinaishi familia 30.
Alisema ni kweli askari wengine 154 bado wanaishi uraiani lakini hata hivyo serikali itaendelea kujenga nyumba za makazi ya askari kwa awamu kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.
Mbunge Atishia Kufanya Fujo Jimboni Kwake Kisa Maji
Mbunge wa Ulyankulu, John Kadutu (CCM) ametishia kufanya fujo jimboni kwake kama Serikali haitawaondolea kero ya maji.
Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji jana bungeni jijini Dodoma, Kadutu amesema jimbo lake kwa muda mrefu limetengwa na halipewi kipaumbele huku wananchi wake wakitaabika kwa ukosefu wa maji.
Kadutu ambaye amezungumza kwa hisia, amesema yeye na wananchi wanakwenda kuziba Mto Malagalasi kwa sababu mradi wa Mto huo badala ya kuhudumia pia wananchi wa Ulyankulu, umeelekezwa Kaliua na Urambo mkoani Tabora.
“Mheshimiwa Waziri na wataalam mlioko hapa nyuma yangu hebu fanyeni mnavyoweza, je tutatengwa hadi lini?, sisi sio wakimbizi kama hamtaki kutupa tawala za mikoa tupeni maji, wataalam msikie tutaleta vagi hata wao hawatakanyaga huko,” amesema.
Musukuma ataka Wizara ya Maji iongozwe na mtu mwenye elimu ya darasa la saba
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu Musukuma (CCM), ameitaka Wizara ya Maji, iongozwe na mtu mwenye elimu ya darasa la saba kama yeye kwani maprofesa wameshindwa kazi.
Musukuma ameyasema hayo bungeni leo wakati akichangia mjadala wa wizara hiyo, ambapo aliwataja mawaziri waliowahi kuwa mawaziri wa wizara hiyo ambao ni maprofesa.
“Mheshimiwa Spika, tuliwahi kuwa na maprofesa, Mwandosya, Magembe, sasa Mbarawa na Katibu Mkuu Kitila Mkumbo, sasa tujaribu na darasa la saba muone, mimi nitaziba mitaro yote na mtashangaa,” amesema.
Bunge lamlilia Dr. Mengi... Tazama hapa Dakika mbili za Spika Ndugai alivyoelezea mchango wake
Spika wa Bunge Job Ndugai ametoa taarifa ya Bunge ndani ya ukumbi wa Bunge kuhusu kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa IPP Media Dr. Reginald Mengi kilichotokea Dubai usiku wa kuamkia Mei 2, 2019 ambapo amewaeleza Wabunge kuhusu mchango aliokuwa nao marehemu katika Bunge na taifa kwa ujumla.
"Katika kuomboleza kifo sisi Bunge tunaungana na Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, familia ya marehemu na Watanzania wote tukimshukuru Mwenyenzi Mungu na kumshukuru Mhe. Mengi kwa mchango wake mkubwa usiopimika kwetu Watanzania," amesema Spika.
==>>Tazama hapo chini
VIDEO: Wanaume wanaopigwa na wake zao watakiwa kupeleka malalamiko ya Polisi
Wanaume wanaopigwa, kunyanyaswa kingono na wake zao na ukatili mwingine wametakiwa kuripoti matukio hayo katika madawati ya jinsia yaliyopo vituo vya Polisi nchini.
Wito huo umetolewa na bungeni leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Iringa, Rita Kabati (CCM).
Katika swali lake Kabati aliuliza: Kwakuwa vitendo vya wanaume kupigwa , kunyanyaswa na wake zao vimeongezeka ni lini serikali italeta sheria ili kuwalinda wanaume hao?
Katika majibu yake, Dk. Ndugulile amesema sheria ya ukatili wa kijinsia haibagui nani amefanyiwa ukatili huo kati ya wanaume na wanawake, hivyo wanaume wanaopigwa na kufanyiwa vitendo vyovyote vya ukatili waripoti madawati ya jinsia yaliyopo vituo vya polisi.
==>>Tazama hapo chini
==>>Tazama hapo chini
Omar al Bashir Kuhojiwa Kuhusu utakatishaji fedha na kufadhili ugaidi"
Mwendesha mashitaka mkuu nchini Sudan ameamuru kuhojiwa kwa Rais aliyeondolewa madarakani Omar al Bashir kuhusu madai ya "utakatishaji fedha na kufadhili ugaidi"
Chini ya Utawala wa Bashir, Sudan iliwekwa kwenye orodha ya Marekani ya mataifa yanayofadhili ugaidi kutokana na mahusiano yake na kundi la itikadi kali.
Muasisi wa al-Qaeda Osama bin Laden, aliyehusika na mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 mijini New York na Washington mwaka wa 2001, aliishi Sudan kati ya mwaka wa 1992 na 1996.
Jenerali Abdel-Fattah Burhan, mkuu wa baraza la kijeshi, alisema mwezi uliopita kuwa zaidi ya dola milioni 113 pesa taslimu zilipatikana katika makazi ya al-Bashir.
Amri hiyo ya kaimu mwendesha mashitaka mkuu Al Waleed Sayyed Ahmed imetolewa wakati mamia kwa maelfu ya waandamanaji wakiendelea kupiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi kulitiaka likabidhi madaraka kwa raia.
Al-Bashir aliondolewa madarakani na kukamatwa na jeshi la Sudan mnamo Aprili 11 baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya kuupinga utawala wake wa miaka 30. Jeshi na viongozi wa upinzani sasa wanafanya mchakato wa kuunda serikali ya mpito.
Rais Magufuli Akerwa na Majungu Mbaralali.....Afunguka Mbunge Anavyohujumiwa Ikiwemo Kuwekewa Bunduki
Rais John Magufuli, amefichua njama anazofanyiwa Mbunge wa Mbarali, Haroub Mohamed (CCM), zikiwamo kuwekewa bunduki kwenye shamba lake kwa lengo la kumchafua.
Vilevile, amesema mbunge huyo ameundiwa kundi la watu ambao wanalipwa pesa na watu wenye nia ovu dhidi yake.
Rais Magufuli alifichua njama hizo jana katika mkutano wa hadhara alioufanya katika Viwanja vya Rujewa wilayani Mbarali ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Mbeya.
“Changamoto nyingine iliyopo Mbarali ni majungu, mtaichelewesha kwenda mbele, ninajua wapo watu ambao wamelipwa hela, wamepangwa kuja kumzomea mbunge, haya hayatawasaidia, ukiwa unataka ubunge, usububiri wakati, subiri uje umshinde kwenye kula, lakini haya majungu yanawachelewesha," alisema.
Rais Magufuli aliongeza: "Majungu hayajengi, ninawaambia ndugu zangu kwa dhati kabisa, mnapochagua watu hamchagui malaika, huyu ni mbunge wa kuwatumikia watu, mmepanga kumchafua, hatachafuka.
"Mmefanya mengi ya ajabu, mkaenda kwenye shamba lake mkaenda kufukia silaha ambazo wala siyo zake kwa umiliki, msifikiri hatujui, acheni mambo ya namna hiyo na bahati nzuri wanaofanya hayo wanajulikana, kama hizo ndizo mbinu za kupata ubunge hupati, mimi ndiyo mwenyekiti."
Rais Magufuli pia aliaziga apewe majina ya watu waliopewa hekta 5,900 ambazo serikali iliagiza zirudishwe kwa wananchi kutoka kwa wawekezaji.
"Ninachotaka hizo hekta nipate orodha ya watu waliopewa, mnipangie orodha, kwamba huyu ni fulani amepewa hekta kadhaa, ili hekta hizi 5,900 zijulikane wamepewa kina nani, inawezekana zikawa hewa.
"Haiwezekani wananchi wote wa Mbarali mimi nimetoa ardhi halafu wao walalamike kwamba hawajapata ardhi wakati mimi nimetoa, isije ikawa zimerudi tena kwa wawekezaji au wamekuja wengine wapya kisirisiri.
"Lengo la yale mashamba yalikuwa si kupewa wawekezaji tena, lengo lilikuwa ni kupewa wananchi kwa ajili ya kulima," Rais Mgufuli alisema.
Kiongozi huyo wa nchi pia aliagiza kutafutwa madalali ambao wamekuwa wakiwawakodishia wananachi mashamba kwa kiwango kikubwa cha fedha ili kulima.
“Mwekezaji wa shamba namba 70 na 78 alipewa kihalali kwa mujibu wa sheria, na alipokuwa na shamba lake amekuwa akilima lakini katika maeneo mengine amekuwa akiwapa watu kwa kuwakodisha, lakini kwa bahati mbaya kuna madalali hapa katikati wamekuwa wakiuza kwa kukodisha kwa Sh. 600,000 mpaka Sh. 700,000, ninaomba watafutwe," aliagiza.
Kabla ya kuhutubia katika viwanja vya Rujewa, Rais Magufuli alisimama mara kwa mara njiani kwa ajili ya kusikiliza kero na kuzungumza na wananchi, akitoa onyo kwa watumishi wasio waamifu ambao wamekuwa wakipewa kusimamia miradi ya serikali na kuiba pesa za serikali.
Rais Magufuli pia alitoa wito kwa watendaji wa serikali kuhaki
Taasisi za dini zinazoanzisha hospitali Zatakiwa kuweka gharama nafuu kwa wananchi
Rais John Magufuli amezitaka taasisi za dini zinazoanzisha hospitali kuweka gharama nafuu kwa wananchi ili waweze kumudu kupata huduma za matibabu,kutobagua dini, madhehebu wala kabila.
Rais ameyasema hayo jana wakati akifungua hospitali ya Uwata (Umoja wa Uamsho wa Wakristo Tanzania) iliyopo jijini Mbeya yenye uwezo wa kulaza hadi wagonjwa 134 kwa siku.
“Pia endapo mgonjwa asiye na uwezo wa kumudu gharama za matibabu amefika katika hospitali hizo hawatakiwi kumfukuzwa kwa sababu inawezekana ni malaika amefika kuwajaribu katika utoaji huduma,” alisema kwa utani.
Rais Magufuli alisema Serikali imekuwa ikijitahidi kuchangia uendeshaji wa hospitali binafsi ili kuhakikisha huduma zinazotolewa gharama yake inakuwa nafuu na kila mtu anaweza kumudu.
“Sisi Watanzania siyo wote wenye uwezo wa kulipa gharama kubwa, upo mchango wa Serikali ikiwamo katika ulipaji wa mishahara, hata mashuka niliyoyakuta mle hata vifaa vingine inawezekana vimetolewa na Serikali kwahiyo Uwata inakuwa msimamizi ikishirikiana na Serikali hivyo gharama isije ikawa kubwa sana ikawaumiza wananchi hawa.
“Hospitali hizi zinahesabika kama zinatoa huduma kwa watu, kuwa ni mahali ambapo watu wanapakimbilia kwenda kutibiwa na kupata uponyaji, ninyi mnasimama badala ya Mungu, ninyi mnasimama badala ya Yesu ambaye alikuwa akiwaponya wanasimama na kurudi nyumbani bila kudai hela,” alisema.
Aidha, Rais Magufuli ameahidi kujenga barabara ya lami kutoka Mabanzini hadi katika eneo la hospitali hiyo yenye urefu wa mita 700.
TFF yatuma salamu za rambirambi Kifo Cha Mzee Reginald Mengi
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za Kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Mlezi wa Timu ya Taifa ya Vijana U17 “Serengeti Boys” Dkt.Reginald Mengi aliyefariki usiku wa kuamkia jana huko Umoja wa Falme za Kiarabu.
Rais wa TFF Ndugu Karia ametoa pole kwa Familia ya Dkt.Mengi,Makampuni ya IPP,Ndugu,Jamaa,Marafiki na Familia ya Mpira wa Miguu kwa msiba huo.
Amesema Dkt.Reginald Mengi amekua na mchango mkubwa katika Mpira wa Miguu mchango ambao bado ulikua unahitajika.
“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za Msiba wa Mlezi wetu wa Serengeti Boys Dkt.Reginald Mengi sote ni mashahidi kwa namna alivyojitolea katika Mpira wa Miguu kuanzia ngazi ya Klabu mpaka Timu za Taifa hakika mchango wake bado ulikua unahitajika,Kwa niaba ya TFF natoa pole kwa Familia yake,Makampuni ya IPP,Ndugu,Jamaa,marafiki na WanaFamilia ya Mpira wa Miguu” amesema Rais wa TFF Ndugu Karia.
Kabla mauti hayajamkuta Dkt.Mengi alikua ndio mlezi wa Timu ya Taifa ya Vijana U17 “Serengeti Boys” ambapo mara ya mwisho alikua na Timu hiyo wakati ikishiriki kwenye Fainali za Afrika za Vijana U17(AFCON) zilizofanyika Tanzania na kumalizika Aprili 28,2019 Uwanja wa Taifa.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Dkt.Reginald Mengi mahala pema peponi,Amina
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Azindua Soko la Madini Chunya
Na Greyson Mwase, Chunya
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amezindua Soko la Madini Chunya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Wilaya ya Chunya kuhakikisha imekamilisha na kuzindua soko la madini ndani ya kipindi cha siku saba. Rais Magufuli alitoa agizo hilo tarehe 27 Aprili, 2019 wilayani Chunya katika mkutano wake na wachimbaji na wachenjuaji wa madini.
Uzinduzi huo ulishirikisha Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Madini, Issa Nchasi, Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Anthony Tarimo na Kamishna Msaidizi- Uendelezaji wa Migodi kutoka Wizara ya Madini, Ali Ali.
Wengine walioshiriki katika uzinduzi huo ni pamoja na Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, Dk. Venance Mwase, wawakilishi wa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini, viongozi wa dini pamoja na vyombo vya habari.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Profesa Msanjila alisema kuwa, tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha Sekta ya Madini inakua, inanufaisha watanzania pamoja na kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa.
Akielezea mafanikio ya Serikali kupitia Wizara ya Madini kwenye usimamizi wa rasilimali za madini, Profesa Msanjila alisema kuwa, ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wananufahika na rasilimali za madini, Serikali ilitunga Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili Namba 5 ya Mwaka 2017; Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi Namba 6 ya mwaka 2017 pamoja na kufanya marekebisho ya Sheria ya Madini Sura ya 123.
Aliendelea kueleza kuwa Serikali pia imefuta baadhi ya tozo ambazo zilikuwa kero kwa wafanyabiashara wa madini hususan wachimbaji wadogo na kufafanua kuwa tozo hizo kuwa ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) asilimia 18 na kodi ya zuio ya asilimia tano kwa wachimbaji wadogo.
Alisema kuwa, kuwekwa kwa mazingira mazuri ya kibiashara kwenye sekta ya madini pamoja na kufuta kodi na tozo mbalimbali zinazofikia asilimia 23 kutaondoa utoroshwaji wa madini na kusaidia wachimbaji wadogo kutambuliwa kupitia uanzishwaji wa masoko ya madini.
Alieleza manufaa mengine kuwa ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za wachimbaji wadogo na kuongeza wigo wa mapato ya nchi.
Katika hatua nyingine, Profesa Msanjila aliwataka wachimbaji wote wadogo na wafanyabiashara wa madini kuendelea kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali katika kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali.
Akielezea manufaa ya soko jipya la madini Chunya, Profesa Msanjila alisema soko litaziba mianya ambayo imekuwa chanzo cha utoroshwaji wa madini, ukwepaji kodi na hivyo kusababisha biashara nzima ya madini kufanyika kiholela katika maeneo mengi ya nchi.
Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa Soko la Madini Chunya kutawezesha na kurahisisha biashara nzima ya madini na kuwa kiungo muhimu cha kuwakutanisha wachimbaji na wafanyabiashara kwa lengo la kuuza na kununua madini.
Profesa Msanjila aliendelea kufafanua manufaa mengine ya soko kuwa ni pamoja na kuwa suluhisho la tatizo la kupunjwa na kudhulumiwa na kuondoa vitendo vya dhuluma ambavyo vimekuwa vikiwahusisha wafanyabiashara wa madini wasiokuwa waaminifu kwa baadhi ya wachimbaji wadogo.
“Soko hili litaondoa uwezekano wa wanunuzi wa madini kuibiwa na wajanja wachache wanaojifanya kuwa na madini wakati hawana, nawasihi wanunuzi wa madini kulitumia soko kikamilifu ili kuepuka udanganyifu na matapeli tu” alisema Profesa Msanjila.
Katika hatua nyingine Profesa Msanjila aliupongeza uongozi wa Wilaya ya Chunya, wafanyabiashara wa madini kwa kuhakikisha Soko la Madini Chunya limezinduliwa ndani ya muda uliopangwa.
Wakati huo huo akizungumzia hali ya uanzishwaji wa masoko ya madini nchini, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula alisema kuwa, hadi kufikia sasa masoko matano ya madini yameshafunguliwa katika mikoa ya Geita, Singida, Kahama, Arusha – Namanga na Chunya.
Aliongeza kuwa masoko mengine ya madini yanatarajiwa kufunguliwa kabla ya tarehe 05 Mei, 2019 ikiwa ni pamoja na Soko la Madini ya Dhahabu na Vito vya Thamani Ruvuma, Soko la Madini Shinyanga, Soko la Madini Dodoma na Soko la Madini Mbeya.
Profesa Kikula alitaja masoko mengine ambayo yanatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni kuwa ni pamoja na Soko la Madini ya Bati (tin) na Soko la Madini ya Dhahabu Handeni.
Alisisitiza kuwa mikoa mingine ipo katika hatua za mwisho kukamilisha vigezo mbalimbali vikiwemo vya kiusalama na miundombinu.












