Tuesday, 30 April 2019

WAKALA WA SERIKALI MTANDAO WAJA NA MFUMO WA KUONGEZA UFANISI SERIKALINI


Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuwa Wakala wa Serikali Mtandao umetengeneza mfumo wa matumizi ya Tehama katika kuboresha utendaji kazi Serikalini.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa usikivu Taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari, leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuwa Wakala wa Serikali Mtandao umetengeneza mfumo wa matumizi ya Tehama katika kuboresha utendaji kazi Serikalini.
Sehemu ya wafanyakazi wa Wakala wa Serikali Mtandao wakifuatilia taarifa ambayo ilikuwa inatolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari, leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari

Picha na Alex Sonna-Fullshangwe blog

WAKALA wa Serikali Mtandao umetengeneza Mfumo Shirikishi wa Kusimamia Shughuli na Rasilimali za Taasisi (ERMS) utakaowezesha kusimamia, kufuatilia, kukagua na tathmini ya utekelezaji wa shughuli zote za umma kwa ufanisi.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari,wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dodoma amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa matumizi ya tehama katika kuboresha utendajikazi serikalini.

Dk.Bakari amesema kuwa wameamua kutumia utaalamu wetu wa kidigitali kutengeneza mfumo wa ERMS ambao ni dirisha moja linalounganisha shughuli zote za ndani ya taasisi kuongeza ufanisi katika utendajikazi na utoaji huduma bora kwa umma.

Aidha amesema kuwa kuwa mfumo huo utakuwa na moduli 18 zinazounganisha shughuli mbalimbali za utendajikazi zinazotegemeana kuwezesha kubadilisha taarifa miongoni mwa idara na kusimamia rasilimali watu, fedha na vitendea kazi.

Dk.Bakari amesisitiza kuwa mfumo huo unawezesha ushughulikiaji wa miamala kutoka idara moja hadi nyingine zikiwemo ankara za bidhaa na huduma, mapato na matumizi, ufuatiliaji na utekelezaji wa shughuli kulingana na mipango na bajeti.

"Pia utawezesha usimamizi wa majukumu ya watumishi, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi, utekelezaji wa shughuli za manunuzi na utayarishaji wa taarifa mbalimbali za utendaji'',amesema Dk.Bakari

Hata hivyo amesema kuwa mfumo huu utawawezesha maofisa masuuli na watumiaji wengine wa mfumo kupata taarifa mbalimbali kulingana na mahitaji yao.

Dk. Bakari amesema kuwa mfumo huo wa ERMS unaweza kuunganishwa na kubadilishana taarifa na mifumo mingine mikuu ya serikali ikiwemo Mfumo Mkuu wa Uhasibu, Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Rasilimaliwatu (HCMIS), Mfumo wa Malipo ya Serikali Kieletroniki (GePG), Mfumo wa Barua pepe Serikalini (GMS) na Mfumo wa Ofisi Mtandao.

Pia amesisitiza kuwa moduli za mfumo huo zinaweza kuongezwa au kupunguzwa bila kuathiri utendaji kazi wa moduli nyingine au mfumo kwa ujumla.

Amezitaja baadhi ya mifumo mingine ambayo wakala umeitengeneza katika utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao ambao ni tovuti kuu ya serikali, tovuti kuu ya ajira, mfumo wa barua pepe serikalini ambao unatumiwa na taasisi za umma 402 zikiwemo ofisi za ubalozi nje ya nchi kwa ajili ya kubadilishana taarifa serikalini.

Aidha Dk. Bakari amezitaka taasisi za umma kuendelea kutumia tehama katika kuboresha utendaji kazi serikani na utoaji huduma kwa umma kwa kuzingatia miongozo na viwango vya serikani mtandao.
Share:

ALMASI KUBWA KULIKO ZOTE YAPATIKANA SHINYANGA....HAIJAWAHI KUTOKEA

Almasi yenye ukubwa wa karati 521 imepatikana katika mgodi wa Mwadui Mkoani Shinyanga tangu mgodi huo uanze uzalishaji miaka 87 iliyopita.

Akitoa taarifa hiyo Ofisini kwake mbele ya waandishi wa Habari leo tarehe 30 Aprili, 2019, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amesema almasi hiyo itauzwa ndani ya nchi ili kodi itakayopatikana ibaki katika mkoa wa Shinyanga na nchini.

"Ni almasi kubwa ambayo haijawahi kupatikana kwenye Mkoa wetu hususani katika Mgodi wa Mwadui ambao ni wa zamani sana, ni fahari kubwa kwa Mkoa wetu" amesema Mhe. Telack.

Mhe. Telack ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara wote wa Almasi kuja kununua katika mkoa wa Shinyanga ambapo tayari soko la madini katika Wilaya ya Kahama linaendelea vizuri wakati soko jingine la madini litafunguliwa katika Wilaya ya Shinyanga hapo tarehe 3 Mei, 2019.

Aidha, ametoa wito kwa wafanyabiashara wote ndani ya Mkoa kuendelea kutumia masoko yaliyoandaliwa kwa ajili ya uuzaji wa madini, waache kununua katika maeneo yasiyo rasmi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akionesha almasi hiyo. Almasi hii ndiyo yenye uzito mkubwa kupatikana katika mgodi wa Mwadui uliopo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga tangu mgodi hio uanzishwe miaka zaidi ya 80 iliyopita. Almasi hii yenye ukubwa wa karato 521 itauzwa ndani ya masoko ya madini ndani ya Mkoa wa Shinyanga.
Share:

Waziri Mkuu Ahimiza Wakazi Dodoma Wachangie Damu ...Asisitiza Wanaume Wapime Vvu Ili Wajue Hadhi Zao, Wasitegemee Wake Zao

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Dodoma wajitokeze kwa wingi kuchangia damu ili iweze kutumika kuokoa maisha ya wengine.

Ametoa kauli hiyo hilo leo (Jumanne, Aprili 30, 2019) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Dodoma waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya miaka 10 ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mwl. Nyerere, jijini Dodoma.

Amesema Serikali inaendelea na kampeni ya kuhakikisha vituo vya afya na hospitali vinakuwa na akiba ya kutosha ya damu kwa ajili ya wagonjwa wenye kuhitaji damu.

“Tunawasihi Watanzania waende kuchangia damu ili benki ya damu iwe na akiba ya kutosha endapo mtu ataenda pale kufanyiwa upasuaji na akapoteza damu nyingi, au awe amepata ajali au ameenda kujifungua, apate damu kwa haraka kutoka kwenye benki yetu,” amesisitiza.

Akitumia wingi wa watu kwenye hafla hiyo, Waziri Mkuu amesema: “Leo hii hapa Dodoma kuna hospitali kubwa ya Benjamin Mkapa kule UDOM, tuna vituo vya afya kama kile cha Makole vyote vinahitaji kutoa huduma hii lakini haitoshi. Tuliagiza kila penye mkusanyiko wa watu wengi, lazima kujengwe banda la kupima afya na kuchangia damu.”

Akizungumziai kuhusu upimaji wa virusi vya UKIMWI (VVU), Waziri Mkuu amesema kampeni inafanyika lakini kasoro iliyopo ni kwamba wanaojitokeza kwa wingi kupima afya zao ni wanawake na wanaume hawapimi. “Takwimu zilizopo zinaonyesha hivyo,” amesema.

“Mimi ndiye balozi wenu akinababa kwenye kampebi ya kitaita ya upimaji VVU. Nataka niwahimize twende leo tukapime, tusitegemee matokeo ya vipimo vya mke. Wengi mnasubiri matokeo ya mke, akisharudi kutoka kupima na kusema niko safi, basi na wewe unaanza kufurahi unasema niko safi, hapana!”

“Wanaume msijidanganye, nenda ukapime wewe mwenyewe ujijue afya yako na mkeo naye apime ajijue ili nyumba nzima iwe na uhakika kwamba mko salama. Kwa hiyo wanaume tukitoka hapa, twende tukapime,” alisema.

Mapema, Mkuu wa Kitengo cha Damu Salama Mkoa wa Dodoma, Dk. Leah Kitundya alimweleza Waziri Mkuu kwamba Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ina upungufu wa damu kwa sababu kuna matukio mengi yanayosababisha upungufu wa damu,

“Tukisema kuwa tunakusanya chupa za kutosha, tunahitaji tuwe na chupa 1,000 hadi 1,500 za damu lakini katika hali ya kawaida huwa tunakusanya chupa za damu 850 hadi 950 tu,” alisema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Nyumba imeshuka bei: Mapinga (Baobab sec

Nyumba imeshuka bei: Mapinga (Baobab sec)
Nyumba hii imeshuka bei kutoka mil 55 mpaka mil 45, kwa mwenye uhitaji awahi kuona na kununua. Nyumba ni kubwa sana, imejengwa kwa kiwango, ina vyumba 4, sebure, dining na kitchen. Nyumba hii ina kiwanja kikubwa chenye sqm 2200, ( 35/63 mita) na kimepimwa.

Pia kipo kiwanja cha sqm 2000 bei yake mil 24 kinachopakana na hiyo nyumba, kwa mwenye uhitaji anaweza kuunganisha vyote akapata nyumba pamoja na eka nzima (sqm 4200).

Hakuna dalali, mpigie mhusika kwa namba 0758603077


Share:

IGP Sirro Asema Jeshi la Polisi Limejipanga Vizuri Kuelekea Uchaguzi wa serikali za mitaa

Na Amiri kilagalila-Njombe
Jeshi la polisi Nchini limesema limejipanga vizuri kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe,mkuu wa jeshi la polisi Nchini IGP Simon Siro wakati akiwa katika ukaguzi wa kawaida, kukagua jeshi hilo pamoja vifaa mbali mbali kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa,amesema kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu huku akiahidi kupambana na wachache watakao jaribu kuvuruga amani.

“Kwa uchaguzi huu wa serikali za mitaa tumejipanga vizuri sana kwa hiyo mtu asiwe na hofu lakini wale wachache watakaotaka kuleta vurugu huyo ni wa kwetu na wale waungwana tutakwenda nao vizuri kuhakikisha uchaguzi unakwenda vizuri mpaka ule wa 2020”alisema Siro

Aidha kamanda Siro amesema wakati wa uchaguzi kukiwa na amani huchaguliwa kiongozi mzuri  huku kukiwa na vurugu hupatikana kiongozi wa hovyo, hivyo jeshi hilo na watanzania tunahitaji kiongozi mzuri ili kutufikisha mbele kimaendeleo.


Share:

Rais Magufuli Aelezea masikitiko yake kufuatia timu za soka za taifa Kufungwa na Mataifa Mengine

Rais   Magufuli ameeleza masikitiko yake kufuatia timu za soka za taifa ambazo ni timu ya wakubwa (Taifa Stars) na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys,  kufungwa na timu za mataifa mengine katika michuano mbalimbali ambayo imechezwa hivi karibuni.

Magufuli amesema hayo leo Aprili 30, 2019 wakati wakiwahutubia wananchi wa Kyela mkoani Mbeya ikiwa ni siku chache baada ya Serengeti Boys kuondolewa kwenye michuano ya Afcon U17, iliyokuwa ikichezwa hapa nchini na kusema  kitendo cha kufungwa kwa timu hizo kimekuwa kikimnyima raha huku akimtaka waziri wa micghezo, Dkt Harrison Mwakyembe kubeba aibu hiyo ya kufungwa kila mara.

“Kukatika kwa umeme kunaumiza sana, unakuta unaangalia mpira umeme unakatika halafu goli linaingia, na Waziri wa Michezo anatoka huku Mbeya, ingawaje kwenye timu ya vijana ameniangusha sana. Katika vitu ambavyo huwa vinaniudhi ni kufungwa timu zangu, huwa inaniuma mno, yani watu milioni 55, mnafungwa na timu ya nchi yenye watu milioni 33, hii ni aibu kubwa mno.

“Natamani siku moja niwe waziri wa michezo halafu niwaonyeshe mimi ni nani, kwanza kikosi nitakipanga mimi mwenyewe halafu tuone kama tutafungwafungwa tena, timu ya wakubwa nayo hivi karibuni itaanza mashindano, sijui nayo mechi ya kwanza tu itafungwa! Labda kufungwa nao ndiyo mchezo mzuri,” amesema Magufuli.


Share:

Waziri Mkuu: Serikali Imetoa Sh. Bilioni 118 Kuimarisha Mawasiliano

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema tangu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote uanzishwe, Serikali imechangia shilingi bilioni 118 ili kuimarisha huduma za mawasiliano ambapo wakazi zaidi ya milioni tano kwenye kata 703 zenye vijiji 2,501 wameweza kufikiwa.

Ametoa kauli hiyo hilo leo (Jumanne, Aprili 30, 2019) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Dodoma waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya miaka 10 ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mwl. Nyerere, jijini Dodoma.

“Ninayo furaha kubwa moyoni mwangu, ninaposhuhudia mfuko huu ukitimiza miaka 10 huku sehemu kubwa ya nchi yetu ikiwa na mawasiliano ya uhakika. Napenda niwakikishie kwamba Serikali itaendelea kupeleka mawasiliano kwenye sehemu zilizobakia hapa nchini ili wananchi wote waweze kunufaika na uwepo wa mawasiliano,” amesema.

Amesema Serikali inatambua mchango wa watoa huduma za mawasiliano katika kufikisha huduma hiyo sehemu mbalimbali, kwani kwa sasa kuna baadhi ya minara imejengwa kwa ushirikiano baina ya kampuni za simu. “Nitoe rai kwa wananchi wahakikisha mnailinda minara ya mawasiliano, na tena mhakikishe popote ilipo inalindwa kwa mguvu zote ili tusirudishe nyuma juhudi za maendeleo,” amesisitiza.

Waziri Mkuu ameipongeza Bodi na menejimenti ya mfuko huo kwa kupeleka vifaa vya TEHAMA katika shule zaidi ya 500 nchini pamoja na kutoa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu 800.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhira hiyo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye alisema mfuko huo umejenga vituo 10 vya TEHAMA huko Zanzibar (Pemba na Unguja) ili viwe ni vituo vya mafunzo ya TEHAMA.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Peter Ulanga alisema mpaka sasa takribani asilimia 94 ya Watanzania wanapata huduma za mawasiliano mijini na vijijini.

“Kama unavyotambua kwa ukubwa wa nchi yetu, bado kuna maeneo yenye changamoto za mawasiliano. Mfuko umekwishaainisha jumla ya kata 234 ambazo zabuni yake inatarajiwa kutangazwa Mei 2019,” amesema.

Alisema Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote pamoja na kupeleka huduma za mawasiliano vijijini umeweza kuanzisha matumizi ya TEHAMA katika shule za msingi na sekondari nchini ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake kama yalivyoainishwa katika sheria iliyoanzisha mfuko huo.

“Katika kipindi cha miaka 10, Mfuko umeweza kupeleka vifaa vya TEHAMA katika shule za Serikali. Kupitia mradi wake wa kuunganisha shule na mtandao wa Internet, mfuko huo umepeleka vifaa hivyo kwenye shule za serikali 503, ambapo kila shule ilipata kompyuta tano. Aidha, printa zaidi ya 150 zimeweza kutolewa katika shule za umma za msingi na sekondari, alisema Mhandisi Ulanga.

Alisema kupitia mradi wa kuunganisha shule za umma na mtandao wa internet, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano na kampuni ya Satelaiti ya Avanti Communications, imeweza kuunganisha shule 301 na mtandao wa internet.

Aidha, Mhandisi Ulanga alisema Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kwa kushirikiana na TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia umeweza kutoa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu 583 katika mwaka wa fedha 2017/2018 wa shule za umma kwa ajili ya kuufanya mradi wa kupeleka vifaa vya tehama uwe endelevu.

“Lengo hasa la mafunzo haya ni kutoa elimu ya kutatua matatizo ya awali katika vifaa mbalimbali vya TEHAMA, ili kupunguza gharama za uendeshaji kwa vifaa vinavyopelekwa shuleni na kuboresha namna ya kuandaa na kufundisha masomo mbalimbali. Mwaka huu wa fedha 2018/2019 tumetoa mafunzo kwa idadi hiyo hiyo ya walimu,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kuwashukuru TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa kufanikisha mafunzo hayo.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

IGP Sirro Atua Mkoani Njombe na Kutoa Maelekezo Mazito Kuhusu Matukio ya Ubakaji na Mauaji

Na Amiri kilagalila-Njombe
Jeshi la polisi Nchini limeahidi kushughulika na vitendo vya mauaji vinavyoendelea kutokea mkoani Njombe kwa njia yoyote.

Kamanda wa polisi Nchini IGP Simon Siro akiwa mkoani Njombe kwa ukaguzi wa kawaida, amesema kuwa amezielekeza timu za upelelezi kuhakikisha yeyote atakayehusika na mauaji anapatikana na kushughulikiwa.

“Hali ya uhalifu ipo chini lakini tunashida bado ya mauaji na nimetoa maelekezo kwamba lazima haya tuyamalize mkoa wa Njombe,wale wanaofanya kwa ulevi,kwa ugomvi na kwa ushirikina waache kwasababu wataishia magerezani

"Nimeelekeza timu zetu maalumu za upelelezi kuhakikisha kuwa yule anayefanya mauaji anapatikana, kuna tukio hapa juzi kwasababu ya ushirikina  mzee amekamatwa amepasuliwa pasuliwa ni mambo ya kishamba, haiwezekani mkoa mmoja kila siku Njombe mauaji watu hawataki kuacha ”alisema Siro

Katika hatua nyingine kamanda Siro ameliagiza jeshi la polisi mkoa wa Njombe kutoa elimu kuanzia mashuleni mpaka vyuoni juu ya madhara ya ubakaji kutokana na changamoto hiyo kuonekana kuwa kubwa mkoani Njombe.

“Lakini pia nimeona tunashida ya kubaka na makosa haya ya kubaka ni mengi nimeelekeza waende kutoa elimu kuanzia mashuleni kueleza madhara ya kubaka,lakini mbaya zaidi imeonekana kesi ikienda mahakamani makosa mengi ya kubaka yanashirikisha ndugu ,nimesema biashara ya ndugu haipo ukifanya kosa la jinai

"Kwa hiyo unapobaka ujue inakushtaki jamhuri haya mambo ya kizamani tuyaache wanawake mbona ni wengi sana swala kufuata tu sheria”alisema kamanda

Hata hivyo kamanda Siro amesema ili kuimarisha utendaji kazi wa jeshi hilo serikali imetoa fedha takribani bilioni 900 ambazo zimeanza kutumika katika ujenzi wa makazi ya askari hivyo ujenzi unaendelea kwa awamu ili kukamilisha maeneo yote nchini.


Share:

Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba Aukosoa Mfumo wa Elimu Tanzania

Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba (CCM),  amesema elimu ya Tanzania ni kama kifungo cha maisha.

Akichangia mjadala wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, bungeni leo Aprili 30,  Kishimba amesema muda wa kusoma shule Tanzania ni mrefu na unachangia vijana kuzeeka kabla ya kuanza kufanya kazi.

Amesema ni vyema mwaka mmoja mwanafunzi asome madarasa matatu ili kuokoa muda wa kuchukua miaka mingi kabla ya kumaliza shule.

Kishimba ameishauri Serikali iunde tume ya kukusanya maoni kuhusu elimu kwa sababu hali ni mbaya, kila mwaka vyuo vinatoa wahitimu lakini wapo mtaani kila kona na hawana faida yoyote.

“ Nashauri serikali iunde tume wananchi watoe  maoni ni elimu ipi tuwe nayo.

“ Hivi ni utafiti gani unaosema ubongo wa binadamu kila mwaka usome darasa moja”? tufanye mabadiliko makubwa kwenye sera hii, wenzetu Afrika Kusini nao wanateseka na mfumo kama huu,” amesema Kishimba.


Share:

Rais Magufuli Akataa Ombi la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kuhusu Vyama vya Upinzani

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Albert Chalamila amesema,haoni sababu ya kuwa na mfumo wa vyama vingi nchini badala yake kuwe na chama kimoja tu kitakachoitwa 'Magufuli Ruling Party'. 

Chalamila ameyasema hayo leo Jumanne, Aprili 30, 2019, wakati akitoa salamu za mkoa wake kwa Rais Magufuli kwenye mkutano wake na wananchi wa Wilaya ya Kyela.

“Mheshimiwa Rais umefanya mengi sana mema kwa nchi yetu, umetoa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo, hapa Kyela umetupatia vitambulisho 10,000, wananchi 8,850 wameshagawiwa vitambulisho hivyo kwa gharama ya shilingi 20,000 kwa kila kitambulisho.

“Katika suala la elimu bure, katika mkoa wa Mbeya unawalipia wanafunzi wa shule za msingi zaidi ya 400,000 na wa sekondari zaidi ya 86,000.  


"Tunakushukuru sana mheshimiwa Rais. Katika mazuri haya unayoyafanya, sioni kama kuna haja ya kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa, badala yake kuwe na chama kimoja tu kinachoitwa ‘Magufuli Ruling Party’, amesema Chalamila.

Hata hivyo Rais Magufuli ameyakataa maoni hayo na kusema anatamani kuwe na vyama vingi, lakini CCM ishinde wakati wote.



Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521


Share:

Makatibu Wakuu Tanzania Na Uganda Wakutana Kujadili Changamoto

Na Munir Shemweta, WANMM BUKOBA
Makatibu Wakuu wa Tanzania na Uganda wanakutana mjini Bukoba mkoani Kagera katika mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi hizo ikiwemo Uimarishaji Mpaka wa Kimataifa pamoja na Matumizi endelevu ya rasilimali za Bonde la mto Kagera..

Mkutano huo wa siku mbili umeanza tarehe 29 April 2019 mjini Bukoba na kuwakutanisha Makatibu Wakuu wa nchi hizo mbili kutoka Wizara za Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mifugo, Wizara ya Maji pamoja na Wizara ya Nishati.

Kabla ya mkutano huo, Wataalamu wa sekta shiriki kutoka Tanzania na Uganda walikutana na kujadiliana kuhusiana na changamoto zinazozikabili nchi hizo mbili kwa nia ya kuwasilisha mapendekezo yaliyofikiwa kwa Makatibu Wakuu wa nchi hizo.

Baadhi ya Changamoto zinazojadiliwa  kwenye mkutano huo, ni pamoja na Uimarishaji na Uthamini wa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Uganda, Mpango kabambe wa utunzaji mto Kagera na Matumizi endelevu ya rasilimali kati ya Tanzania na Uganda katika Bonde la Mto Kagera.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe alisema mkutano huo ni mfululizo wa mikutano kati ya nchi hizo mbili wenye lengo la kutatua changamoto zinazozikabili nchi hizo kwa nia ya kuleta maendeleo.

Alisema, pamoja na kuwepo changamoto kadhaa lakini Tanzania na Uganda zinaendelea kufurahia mahusiano mazuri yaliyopo kwa kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali yenye lengo la kuleta manufaa kwa nchi na watu wake.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Profesa Faustin Kamuzora aliuzungumzia mkutano huo kama njia ya kuzifanya nchi husika kufanya kazi pamoja na kuzidisha ushirikiano wenye nia ya kuleta maendeleo na kusisitiza kuwa, utekelezaji wa makubaliano yatakayofikiwa unapaswa kufanywa kwa wakati.


Share:

Taarifa Kuhusu Tuzo za Mo Simba 2019

Tuzo za Mo Simba zilizoasisiwa na Mohammed Dewji mwaka 2018 zinatarajiwa kutolewa kwa awamu ya pili baada ya kumalizika kwa msimu wa 2018/2019.

Tuzo za mwaka huu zitahusisha wachezaji na mashabiki wa klabu ya Simba ambao juhudi zao zimewezesha klabu kufikia mafanikio ambayo imeyapata kwa msimu wa 2018/2019.

Kwa mwaka huu kutakuwa na vipengele 11, ambavyo ni Mchezaji Bora wa Mwaka, Goli Bora la Mwaka, Golikipa Bora wa Mwaka, Beki Bora wa Mwaka, Kiungo Bora wa Mwaka na Mshambuliaji Bora wa Mwaka.

Tuzo zingine ni Mchezaji Bora Mwanamke wa Mwaka, Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka, Shabiki Bora wa Mwaka, Tuzo ya Heshima na Mhamasishaji Bora wa Mwaka katika Mitandao ya Kijamii.

Washindi wa tuzo hizo watatokana na kura ambazo zitapigwa na mashabiki kupitia mitandao ya kijamii, tovuti rasmi ya tuzo ambayo tutaitangaza hivi karibuni na kamati maalumu ambayo itahusisha wadau mbalimbali wa mpira wa miguu nchini.

Akizungumza kuhusu tuzo za mwaka huu, Dewji amesema tuzo hizo zitatolewa kama sehemu ya kutambua mchango wa baadhi ya watu ambao juhudi zao kubwa zimesaidia Simba kufika hapa ilipo sasa.

Amesema tuzo za mwaka huu zitakuwa na hadhi kubwa tofauti na mwaka uliopita kwani yamefanyika maandalizi makubwa ambayo yatawezesha hafla ya utoaji wa tuzo kwa mwaka huu kuwa ya kisasa zaidi na yenye kuvutia kwa watakaohudhuria na ambao wataangalia kupitia runinga.

“Tumepata mafanikio makubwa kwa msimu huu ikiwepo kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hili ni jambo kubwa kwetu na Taifa kwa ujumla na kama tulivyofanya mwaka jana na mwaka huu tena tunafanya kuwapa tuzo wote waliofanikisha Simba kufanikiwa,

“Najua kila shabiki wa Simba ana mchango wake kufanikisha sisi kufika hapa kwa maana hata kuja tu uwanjani kushangilia timu hilo ni jambo kubwa sana, lakini kwa kawaida tuzo inatolewa kwa watu wachache kati ya wengi hivyo tutachagua wachache kati yetu na kuwapa tuzo, na sisi mashabiki wenyewe ndio tutachagua,” amesema Dewji.

Tarehe ya kufanyika kwa tuzo na sehemu ambayo hafla itafanyika tutatoa taarifa hivi karibuni baada ya kutangaza vipengele na mchakato wa kupiga kura kuanza.

            Imetolewa na;
     Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Mo Simba 2019
            30/04/2019


Share:

Kujichua Kwa Muda Mrefu Husababisha Maumbile ya Kiume Kusinyaa na Kupungukiwa Nguvu za Kiume

Wanaume  wengi  waliofanya  mchezo wa  kujichua  kwa  muda  mrefu hupatwa  na  madhara  ya kuwa  na  kusinyaa  na  kudumaa  kwa  maumbile  yao  ya  kiume  ambayo  huenda  pamoja  na  tatizo  a  Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume.

Tendo  la  kujichua  kwa  mwanaume  linapofanyika  kwa  kipindi  kirefu huathiri na  kuharibu mishipa  na  misuli  ya uume  na  hivyo  kusababisha  kujengeka  kwa mafuta na tishu zisizo vutika  kwenye  mishipa  ya  ateri.  Jambo  hili  husababisha  makuu mawili; 1. Huzuia  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  kuongezeka jambo  linalotajwa  na  wanasayansi  kama jambo  muhimu  sana  katika  kukua  kwa  uume. 2. Huzuika  kutirika  kwa  damu  kuingia  kwenye  misuli  ya  uume.

Mambo  hayo  mawili  huathiri  sana  ukuaji  wa  maumbile ya kiume  kwa  sababu  yanapo tokea huathiri uzalishaji  wa  homoni  muhimu  zinazo  husika  na  ukuaji  wa  misuli  ya  uume na matokeo  yake husababisha  uume  wa  mhusika  kudumaa, kusinyaa,kunywea  na  kurudi ndani  kiasi  cha  kuufanya  uonekane  kama uume  wa  mtoto.
 
Hii ndio  sababu  kwanini watu  wengi  walio athirika  na  punyeto  hulalamika  kwamba  maumbile  yao  ya  kiume  hayajaongezeka  tangu  walipo anza  kujihusisha  na  punyeto  wakiwa  na  umri mdogo. 

Maumbile  yao  huonekana  kama  ya  watoto  kwa  sababu hayakupata  nafasi  ya  kupokea  vichochea  vya  kuyafanya  yakue  na  kuongezeka  tangu  walipo  anza  kujihusisha  na  punyeto.

Suluhisho  La  Tatizo La Maumbile  Ya  Kiume  Yaliyo  Sinyaa  Kwa  Sababu  Ya  Punyeto.
Kama  bado  unaendelea  kujihusisha  na punyeto  basi  jitahidi  uache  tabia  hiyo  mara  moja  kwani  inakuharibu. Inaweza  isiwe  rahisi  sana  kuacha  mara  moja  lakini  ukiweka  nia  thabiti  basi  unaweza  kuacha  kabisa  kama  walivyofanikiwa  kuacha  wengine  ambao  walikuwa  wametopea  kwenye  tabia  hiyo  lakini  wakajitahidi  kujilazimisha  na  hatimaye  wakafanikiwa  kuachana  kabisa  na  tabia  hiyo.

==>> Acha kuangalia video chafu za ngono.
Video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayoiona utataka ukaipigie  punyeto hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako.. 


Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.

==>>Epuka kukaa nyumbani peke yako;
Mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine. 


Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata kama vile misuli ya uume kulegea, kushindwa kurudia tendo uwapo na mwenzi wako, kuishiwa nguvu za kiume, maumbile kusinyaa, kurudi ndani na kuwa kama ya mtoto mdogo.

Acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema hivyohivo, kama unaacha acha mara moja ili utunze heshima yako mbele ya mwenzi au mke wako.

Kama utaona  kuna  ugumu  wa  kuacha  tabia  hiyo  na tayari ushaapata madhara ya maumbile kusinyaa na kupungiwa nguvu za kiume, basi  wasiliana nasi kwa ushauri zaidi; Simu  0716-263605


Share:

Mikononi mwa polisi kwa kukutwa na nyaraka za serikali

Na Amiri kilagalila-Njombe
Kijana aliyefahamika kwa jina la Ford Abel mwakatundu  (28) mkazi wa makambako mkoani Njombe anashikiliwa na polisi kwa makosa ya kukutwa na nyaraka za serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Salum Hamduni,amesema kijana huyo anashikiliwa kwa makosa hayo kinyume na taratibu za kisheria.

"Mnamo April 22 majira ya saa 12:30 huko Makambako alikamatwa Ford Abel mwakatundu kyusa mwenye umri huo mkazi wa mwembetogwa Makambako kwa kosa la kughushi nyaraka mbali mbali za serikali ikiwemo leseni za kuendesha magari,Tin number, Bima za magari pamoja na nyaraka za sumatra zanazohusiana na Rout za mabasi na magari madogo ya biashara" alisema Hamduni

Ameongeza kuwa nyaraka hizo alikuwa akighushi na kuziuza kwa watu mbali mbali kwa kiasi cha Tsh 100,000/= kwa lengo la kujipatia kipato.

Kamanda amesema upelelezi unaendele na atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.

Meneja wa TRA  mkoa wa Njombe Musib shaaban ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia za kutumia njia za mikato kutafuta kipato kwa kuwa njia hizo zimekuwa zikikwamisha juhudi za serikali.


Share:

Watano Mbaroni kwa kumuua Mwanamke na Kumchana Sehemu za Siri

Na Amiri kilagalila-Njombe
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe linawashikilia watuhumiwa watano kwa kuhusishwa na tukio la mauaji ya mwanamke aliyefahamika kwa jina la Edina Ng'uku (50)

Akizungumza na waandishi wa habari,kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Salum Hamduni amesema : Mnamo April 6 majira ya saa 11:30 kijiji cha Ikwete kata ya Lyamkena mjini Makambako mkoani Njombe lililipotiwa tukio la kuuawa kwa Edina Ng'uku (50) Mbena,mkristo na mkulima baada ya kushambuliwa kwa kupigwa na kitu kizito na butu sehemu mbali mbali za mwili wake, na amechanwa na kitu chenye ncha kali sehemu zake za siri kisha kuchomwa na bua bichi la zao la alizeti "alisema kamanda Hamduni

Kamanda ameongeza kuwa mama huyo alichomwa na bua sehemu zake za siri na kutokea begani.

Amesema kuwa baada watu hao wasiofahamika baada ya kutenda kosa hilo walitoweka eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana.

" Aidha katika eneo la tukio mwili umekutwa ukiwa umelala upande wa kushoto ndani ya shamba lililopandwa mazao ya mahindi na alizeti ambalo linamilikiwa na Eda Nziva huku ukiwa na majeraha sehemu za kifuani upande wa kushoto karibu na ziwa lake pia ukiwa na mchubuko kwenye magoti iliyotokana na kuburuzwa chini umbali wa mita 5.5 na vilevile vimekutwa vipande viwili vya vitenge eneo tofauti,aidha mwili  wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi"alisema kamanda


Share:

Polisi Njombe yaua majambazi wawili, mmoja atoroka

Na Amiri kilagalila-Njombe
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe limefanikiwa kuwaua majambazi wawili kati ya watatu waliokuwa wakijaribu kupora mali kwa kutumia Jambia,kisu na Panga.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ACP Salum Hamduni,amesema tukio hilo limetokea kijiji cha Lupembe wilayani Njombe  April 28 majira ya saa 01:40 usiku ambapo watu wasiofahamika walivamia nyumba ya Esau Muhavile kwa kuvunja geti na mlango kwa kutumia Spring ya gari na kuingia ndani kwa nia ya kupora mali.

"Awali majira ya saa 01:30 usiku mlinzi aitwae Linus Matimbwi akiwa Lindoni alisikia vishindo vya watu kuzunguka nyumba hiyo na kumgongea Baraka mayemba mfanyakazi wa Esau na kumweleza kuwa huku nje hali si shwari ndipo Baraka akaamua kumpigia simu mkuu wa kituo kidogo cha polisi Lupembe kwa msaada"alisema kamanda.

Amesema kuwa Polisi waliwahi kufika katika eneo la tukio na kugundua kuwa majambazi hao wapo ndani na kupiga Risasi hewani kuwataarifu kuwa wapo chini ya ulinzi lakini hawakutii amri na matokeo yake jambazi mmoja wapo alirusha jambia na kumjeruhi mkuu wa kituo begani kitendo kilichopelekea Polisi kumpiga Risasi kifuani jambazi Newton Mbanga aliyerusha jambia huku Leonard Alphonce akipigwa risasi kichwani na kusababisha vifo vyao.

"Mbinu iliyotumika na majambazi hao ni kuvunja mlango kwa kutumia spring ya gari na kuingia ndani kwa nia ya kupora mali/pesa na watuhumiwa ambao ni majambazi wawili kati yao walifariki dunia na mmoja alifanikiwa kutoroka,na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo" aliongeza kusema kamanda.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger