Thursday, 4 April 2019

Waziri Mkuu: Ekari 127,859 Zimetengwa Kwa Ajili Ya Viwanda

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesemma ili kutimiza azma ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 kupitia sekta ya viwanda, jumla ya ekari 127,859 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya viwanda.

Vilevile, Waziri Mkuu amesema Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka za upangaji za Halmashauri za Wilaya za Kibaha na Kilosa, imetenga hekta 2,710 za ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vikubwa na vidogo.

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Aprili 4, 2019) wakati akiwasilisha hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2019/2020.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeziagiza Mamlaka za Upangaji zizingatie utengaji wa asilimia 10 ya kila eneo la Mpango Kabambe wa Mji kwa ajili ya uwekezaji wa biashara na viwanda.

Amesema katika mwaka 2018/2019, Serikali imeandaa Mwongozo wa Tathmini ya Mazingira Kimkakati ambao utawezesha mpango wa uchumi na viwanda kufanyiwa Tathmini ya Mazingira Kimkakati.

“Katika maboresho ya kanuni yaliyofanyika, yanampa Waziri mwenye dhamana ya mazingira mamlaka ya kutoa vibali vya muda kwa ajili ya miradi ya uwekezaji kwenye sekta ya viwanda na hivyo kuboresha taratibu za uwekezaji wa viwanda nchini.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema katika mwaka 2019/2020, Serikali itaendelea kuhuisha, kuboresha na kutekeleza sera, sheria, taratibu na mikakati ya maendeleo ya viwanda, biashara na masoko.

Amesema maboresho hayo yatahusu uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu na madini; kuimarisha na kusimamia mfumo wa biashara ya ndani na kutumia kikamilifu fursa za masoko.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali itaendelea kujenga uwezo wa taasisi za utafiti zinazohusika na maendeleo ya viwanda na kuhamasisha uanzishaji na maendeleo ya viwanda vidogo sana, vidogo na vya kati.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema sekta ya madini ina mchango  mkubwa katika kukuza uchumi, hivyo Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika kulinda rasilimali hizo kwa manufaa ya Watanzania.

“Katika hilo tuna kila sababu ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli, kwa kuelekeza mamlaka za Serikali kutunga Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusu Umiliki wa Maliasili Na. 5 ya mwaka 2017. Sheria ya mapitio na majadiliano kuhusu masharti hasi katika mikataba ya maliasili za nchi na. 6 ya mwaka 2017 pamoja na kufanya marekebisho ya sheria ya madini sura 123.”

Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kutoa kipaumbele kwa wachimbaji wadogo kwa kuwapatia maeneo na kuwakopesha zana za uchimbaji; kuwapatia utaalamu na matumizi ya teknolojia katika uchimbaji na uchenjuaji wa madini.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali inashughulikia kero zinazowakabili wachimbaji wadogo ili waweze kuendesha shughuli zao za uchimbaji mdogo na kunufaika na rasilimali ya madini.

Amesema katika mwaka 2019/2020, Serikali itaendelea kukuza soko la ndani la madini kwa kuvutia wawekezaji na kuhamasisha shughuli za uongezaji wa thamani madini nchini.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Rais Magufuli: Bila Mkapa Nisingekuwa Waziri, na Urais Yawezekana Msingeniona

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema hatajali maneno ya watu ambao watasema kuwa yeye anajenga miundombinu kwenye Mkoa anaotoka Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa, kwa kuwa anajua alipomtoa.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Mtwara kwenye uznduzi wa Kituo cha Afya Mbonde kilichopo Masasi ambapo

“Watu watasema ninamjengea Mkapa, ndio ni kweli ninamjengea Mkapa kwasababu bila yeye nisingekuwa waziri na inawezekana hata urais nisingepata kwahiyo kumjengea kabarabara tu nishindwe

“Ninafahamu Mkapa alinitoa wapi, yako maeneo ya barabara hii kilomita 40 mimi nimeyajua kuliko watu wa Mkoa huu kwasababu Mkapa alikuwa ananituma kwenda kufanya kazi.

"Tulipomaliza ujenzi wa daraja la Mkapa tulimwambia tunalipa jina lake akakataa lakini siku anaenda kulizindua alikuta tumeandika jina lake sasa hivi ana miaka karibu 80 haiwezekani kila anapokwenda mahali walipozikwa wazazi wake tushindwe kutengeneza barabara"

Kuhusiana na Waziri wa awamu ya tatu kupewa kiwanda cha korosho lakini hakiendelezi Rais Magufuli amesema; "kuna kiwanda naambiwa ni cha Waziri wa awamu ya tatu mumnyang'anye, akikataa shikeni pelekeni mahakamani hata kama alikuwa Waziri, tukibembelezana hatutafika ndugu zangu, tubembelezane mimi nikishamaliza muda wangu."

"Nitoe wito kwa waliouziwa viwanda vya kubangua Korosho na Serikali, ni lazima waanze kubangua Korosho na wazinunue, wakishindwa wavirudidhe viwanda, mfano yule wa Newala kiwanda hakifanyi kazi kabisa Waziri wa Kilimo mnyanganye hata kama ni leo." amemalizia Rais Magufuli


Share:

Picha : FISI AVAMIA NYUMBANI KWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI KISHAPU,AUA MBUZI NA KONDOO 16

Katika hali isiyokuwa ya kawaida fisi amevamia nyumbani kwa Diwani wa kata ya Lagana ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga,Boniface Butondo kisha kuua mbuzi na kondoo 16. 

Kwa Mujibu wa Butondo tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Aprili 4,2019 majira ya 10 alfajiri katika kijiji cha Lagana ambapo fisi huyo ameshambulia watoto wa mbuzi na kondoo katika nyumba ya mifugo hao wapatao 16. 

“Ilikuwa majira ya saa 10 alfajiri ndipo fisi huyo alipoingia katika nyumba hiyo na baada ya kusikia makelele ya mbuzi na kondoo hao wadogo wanafamilia wakaamua na kuita majirani wazingira nyumba kwa marungu, mikuki,mawe na pia kufanya kazi ya kufumua paa juu ,wakafanikiwa kumuua majira ya saa 1 na tayari alikuwa ameshakula watatu na kuua wengine 13 na kubakiza wanne ”,ameeleza Butondo. 

“Mimi ni mfugaji wa mbuzi na kondoo,hao watoto wa mbuzi na kondoo nimejengea nyumba yao,mbuzi na kondoo wakubwa nao banda lao,kwa kweli tukio hili limenisikitisha sana na limetokea wakati mimi sipo nyumbani”,ameongeza Butondo.

Na Kadama Malunde - Malunde1 Blog
Share:

Spika Ndugai: Bunge Halitafanya Kazi na CAG Professa Mussa Assad na Si Ofisi yake

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kwamba, Bunge limekataa kufanya kazi na mtu ambaye ni Profesa Mussa Assad, na siyo ofisi ya CAG, kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyonukuu.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo mchana Alhamisi Aprili 4, 2019 baada ya kuwatambulisha wageni walioalikwa bungeni.
 
"Bunge hili limekataa kufanya kazi na mtu anayeitwa Prof. Mussa Juma Assad, halijakataa kufanya kazi na Ofisi ya CAG, sisi kama Bunge hatujawahi kukataa kufanya kazi na taasisi yoyote" Amesema Spika Job Ndugai

Juzi, Aprili 2, 2019 Bunge lilipitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad kwa sababu ya kauli yake aliyoitoa wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuwa Bunge ni dhaifu.


Share:

Breaking : ASKARI POLISI AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI KAHAMA


Habari zilizotufika hivi punde zinasema Askari Polisi (pichani) jina halijafahamika wa kituo cha Polisi Mjini Kahama mkoa wa Shinyanga amejipiga risasi kichwani na kufariki dunia papo hapo asubuhi wakati akiwa kwenye lindo katika  benki ya Access mjini Kahama.



Haijajulikana mara moja sababu za askari polisi huyo kuchukua maamuzi hayo.

Taarifa Rasmi kuhusu tukio hili tutakuletea hivi punde...
Share:

Godbless Lema Afunguka Baada ya Kupewa Adhabu ya Kutohudhuria Mikutano Mitatu ya Bunge

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema adhabu aliyopewa na Bunge ya kutohudhuria mikutano mitatu ni kitu kinachompa nguvu kwenye mapambano dhidi ya kudai haki na kamwe hatanyamaza hata kama adhabu yake itakuwa ni mauti

Katika ujumbe ambao ameuandika katika akaunti yake ya Twittwer, Lema amesena, “Nimesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge mpaka Januari 2020. Moyo wangu una amani sana, kwani mahusiano yangu na HAKI yanaendelea kuimarika zaidi.Nawatakia Wabunge wenzangu kazi njema katika wajibu huu, sitanyamaza hata kama adhabu itakuwa ni mauti.”

“Msiogope. Mungu aliyetupa macho sio kipofu kwamba haoni, Mungu aliyetupa masikio sio kiziwi kwamba hasikii.Yeye ni Mungu asiyekuwa na msongo wa mawazo kama sisi. Siku imekaribia sana kwa kila mtu kulipa kwa kadri alivyopanda.” Ameandika Godbless Lema


Share:

Godbless Lema Asimamishwa Kuhuduria Mikutano Mitatu Ya Bunge....Wabunge wa Upinzani Wasusa na Kutoka Nje

Bunge limepitisha Azimio la kumzuia  Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge kwa kosa la kulidhalilisha Bunge kwa kusema “Bunge ni dhaifu” na alipoitwa kwenye kamati ya Bunge ya kinga haki na madaraka ya Bunge hakuonyesha kujutia kufanya kosa hilo

Akiwasilisha hoja hiyo Bungeni leo April 4, 2019  mwenyekiti wa kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka  amesema kuwa Mbunge huyo alipopewa nafasi ya kujitetea kwenye kamati alisema ahukumiwe tu kwani alichozungumza ni kweli.

Wakati azimio hilo linapitishwa wabunge wa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA  wamesusia kikao hicho cha bunge  na kutoka nje.



Share:

Askari Magereza Anaswa Na Pembe Za Ndovu Jijini Dodoma

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Jeshi La Polisi  Mkoa Wa Dodoma Linawashikilia Watu Watatu  Kwa Tuhuma Za Makosa Mbalimbali  Yakiwemo Kupatikana Na Nyara Za Serikali,kughushi Na Kujipatia Mali Kwa Njia Ya Udanganyifu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana  April 3 ,kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma  SACP.Gilles  Muroto alisema tukio la kwanza ni kupatikana na nyara za serikali  ambapo amebainisha mnamo tarehe 1 April, 2019  mtaa wa Kilimani wilaya na Jiji la Dodoma  alikamatwa  A.8070  SSGT Comas Joseph Ndasi  askari magereza wa gereza la Msalato [51] akiwa na pembe za ndovu  vipande 6 sawa na tembo 3  vye uzito wa kg 13 thamani ya Tsh.103,5000,000 alivyoficha kwenye mfuko  akiwa anamsubiri mteja kwa ajili ya kufanya mauzo.

Kamanda Muroto ametaja tukio la pili ni la Mohammed  Ahmed Hamis  ambaye amekamatwa kwa kosa la kujipatia  mali kwa njia ya udanganyifu  ambapo alijipatia magari mawili ,Toyota Land cruiser  V-8   Lenye namba za usajili T.366 BRX  rangi Nyeusi na gari No.T.581 DKS Toyota aina ya Noah .

Kamanda Muroto amefafanua tukio lilitokea Mikocheni  jijini Dar Es Salaam  mwaka 2017  ambapo mtuhumiwa alijitambulisha kwa mwenye magari  kuwa afisa  usalama  anahitaji magari kwa ajili ya kazi maalum  ambapo aliandika mkataba wa kukodi magari hayo  na alipoyapata alitoweka nayo  na hakurejesha  hadi alipokamatwa   April 2 jijini Dodoma .
 
Mtuhumiwa aliyatumia magari hayo pia kujipatia pesa kwa watu mbalimbali kwa kuyawekea dhamana  kukopa pesa  kisha kulitelekeza gari  na jeshi la polisi litampeleka  Dar es Salaam  alikoshitakiwa na atafikishwa mahakamani.
 
Na tukio la tatu ni la kujifanya Afisa wa serikali ambapo mnamo tarehe 26 Machi,2019 alikamatwa  Ambokile Hezron  Mwampulo [32]  akijifanya afisa usalama wa Taifa  akidanganya watu na kukusanya fedha  akiwaahidi kuwapatia ajira  katika idara ya usalama wa Taifa  na taasisi nyingine za serikali .
 
Kabla ya kukamatwa  alijipatia fedha kiasi cha Tsh.950,000 kutoka kwa watu wawili ambapo Tsh.550,000 kwa mtu mmoja na Tsh.400,000 kwa mtu wa pili.

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa alifanyiwa upekuzi  Nyumbani kwake Ndachi jijini Dodoma  ambapo alikamatwa na nakala 15  za vyeti vya watu mbalimbali ,barua 3 za maombi ya ajira  za watu tofauti  na nakala ya leseni moja  na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
 
Hata hivyo jeshi la polisi limetahadharisha watu kujihadhari  na matapeli  wanaotumia vibaya majina ya taasisi  za serikali na kuwaibia na serikali ina utaratibu wake wa kuajiri watu  .


Share:

Rais Magufuli kuanza ziara ya siku tano mkoani Ruvuma




Share:

Serikali Kuwachukulia Hatua Wanaowanyanyasa Watoto

Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Serikali imesema haitasita kuwachukulia hatua watu wanaowanyanyasa watoto kwa kukiuka Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.

Hayo yamesemwa jana,  Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Kandege alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Mgebi Jadi Kadika juu ya mikakati ya Serikali ya kuondoa tatizo la kuwakosesha watoto haki za msingi na malezi bora kwa kuwatumia katika kutoa huduma ya kubeba mizigo na kupewa ujira mdogo.

“Huduma za ulinzi wa mtoto zinatekelezwa kupitia Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009. Katika kusimamia utekelezaji wa Sheria hiyo, Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ulioanza kutekelezwa kuanzia mwaka wa Fedha 2017/18 hadi 2021/22,” alisema Kandege.

Ameendelea kusema, tathmini imebaini kuwa watoto wengi wanaojihusisha na kazi za kubeba mizigo masokoni ni matokeo ya umaskini uliokithiri kwa baadhi ya Kaya, kuondokewa na wazazi wao kwa maambukizi ya UKIMWI, migogoro ya ndoa na ukatili dhidi ya watoto.

Alisema, mkakati unaotekelezwa na Serikali ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu haki za msingi za mtoto kupata elimu na malezi bora. Aidha, utoaji wa elimu msingi bila malipo umetoa fursa kwa watoto wengi wenye umri wa kwenda shule kuandikishwa kuanza elimu ya awali kupitia mfumo rasmi na mfumo usio rasmi.

Aidha ametoa wito kwa wazazi kutimiza wajibu wao wa kuwalea, kuwatunza na kuwalinda watoto ambao ni Taifa la kesho kwa kutowatumikisha katika kazi ambazo haziendani na umri wao.


Share:

Rais Magufuli Aahidi Kuiunganisha Kanda Ya Kusini Kiuchumi

Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Rais Dkt John Pombe Magufuli  amewahakikishia wananchi wa Nanyamba, Tandahimba, na Newala Mkoani Mtwara kuwa Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya uhakika ili kuunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi na wananchi wa Mkoa huo kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ili kuweza kujiletea maendeleo yao.

Akizungumza katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo, Rais Magufuli amesema Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba-Nanyamba yenye urefu wa kilometa 50 itakayogharimu kiasi cha Tsh.bilioni 86 na kumwagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe kutangaza zabuni ya ujenzi wa kilometa zingine na kufikia kilometa 100 na hivyo kuunganisha kwa urahisi nyanda za kiuchumi katika mikoa ya kusini.

“Barabara hii itakuwa ni kiunganishi cha uchumi mikoa ya kusini, hatuwezi kushindwa kujenga kilometa 100, lengo letu kuu ni kuiunganisha Bandari yetu ya Mtwara na mizigo inayotoa Malawi,” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema kuwa katika kuwainua wakulima wa Mkoa wa Mtwara, ambapo Serikali imetekeleza ununuzi wa korosho kutoka kwa wananchi wenye korosho zaidi ya kilo 1500, na Tsh Bilioni 50 tayari zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa wakulima hao, na kwa upande wa wakulima wa korosho wenye kilo chini ya 1500 wamelipwa kiasi cha Tsh Bilioni 578.

Rais Magufuli amewahiza wafanyabiashara walanguzi wa zao la korosho ‘Kagomba’ kuacha kuwadhulumu wakulima wadogo kwa kuwapa bei ambayo hailidhishi huku wakijua wametumia gharama kubwa katika kuendeleza zao hilo, na kusema serikali ya Awamu ya tano haitarudi nyuma kuwatetea wakulima hao.

“Utakuta mtu amelima korosho zake, amenunua madawa, ametumia gharama kuzivuna unakuja kumpa bei ya 1500, kwa Serikali ya Awamu ya Tano hili halikubaliki”, alisema Rais Magufuli.

Akiongelea miradi mingine inayotekelezwa serikali ya Awamu ya Tano kuwa  ni pamoja na upanuzi wa bandari ya Mtwara, , upanuzi wa uwanja wa Ndege na ukarabari wa mradi wa maji wa makonde ambao utagharimu kiasi cha Tsh.bilioni 160 zikiwa ni fedha za mikopo kutoka Serikali ya India unaowezesha ujenzi wa miradi ya maji katika miji 28 nchini..


Share:

Makamu Wa Rais Kufungua Kongamano La Pili La Maadhimisho Ya Kumbukumbu Ya Hayati Sheikh Abeid Amani Karume Leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi tarehe 4, Aprili 2019 atakuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Pili la Maadhimisho ya kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume. 
 
Mada kuu ya Kongamano hili ni “Uhai wa Fikra za Falsafa za Abeid Amani Karume katika Zanzibar ya leo”.
 
Kongamano hilo limeandaliwa na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na litafanyika kwenye Kampasi ya Zanzibar Bubu ambapo baada ya Makamu wa Rais kufungua Kongamano hilo atatunuku zawadi kwa washindi wa Insha.
 
Aidha baada ya ufunguzi kutaendeshwa mada mbali mbali zitakazotolewa na Mhe.Dkt. Saada Mkuya Salum na Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud

Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais
Zanzibar


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamis April 4




Share:

Wednesday, 3 April 2019

Ngoma Mpyaa!! SENGI MILEMBE - BUSUGWA

Ninayo hapa ngoma mpya ya Msanii Sengi Milembe inaitwa Busugwa...Ngoma kali itazame hapa mtu wangu
Share:

Video Mpya : SENGI MILEMBE - KUBYALA


Msanii wa Nyimbo za asili Sengi Milembe anakukaribisha kutazama video ya wimbo wake mpya unaitwa Kubyala...Utazame hapa chini
Share:

Video Mpya : NYANDA MADIRISHA OBHADO - PILIKA PILIKA


Tazama video mpya ya Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' inaitwa Pilika Pilika...
Share:

Video Mpya : NYANDA MADIRISHA OBHADO 'MALIGANYA' - MCHAKA MCHAKA

Ninayo video mpya kabisa ya Msanii Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' inaitwa Mchakamchaka..Itazame hapa chini
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger