Na Shabani Rapwi. Afisa Habari wa klabu ya Simba SC, Haji Manara ametangaza kuachana na klabu hiyo, baada ya kuwepo kwa tetesi ya kutemwa katika nafasi hiyo. Leo February 10, 2019 kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amesema kuwa anafahamu kuwa mashabiki wengi wa Yanga hawapendi kumwona akiwepo Simba na siku atakayoondoka watafanya sherehe. “Kuna watu wa Yanga hamu yao nife kabisa, nawaumiza sana na siku mtakaposikia sipo kikazi Simba, mtafanya sherehe. Ila nikuhakikishie kuwa Mungu akinipa uhai nitaacha kazi Januari 2021 tena kwa hiari” alisema Manara.
Sunday, 10 February 2019
YANGA YAAMKA, YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 NA KUJIIMARISHA KILELENI LIGI KUU
Timu ya Yanga imezinduka baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Ushindi huo wa kwanza ndani ya mechi nne za Ligi Kuu ikitoka kufungwa 1-0 na Stand United Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na sare mfululizo, 1-1 na Coastal Union hapo hapo Mkwakwani na 0-0 na Singida United Uwanja wa Namfua, Singida unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 58 baada ya kucheza mechi 23.
Na hiyo inamaanisha Yanga SC sasa inaongoza Ligi Kuu kwa pointi 10 zaidi ya Azam FC wanaofuatia katika nafasi ya pili, ingawa wana mechi mbili mkononi, wakati mabingwa watetezi, Simba SC ni wa tatu kwa pointi zao 36 za mechi 15.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Heri Sasii aliyesaidiwa na Soud Lila na Shaffid Mohammed, bao pekee la Yanga SC limefungwa na kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah, maarufu kwa jina la utani Fei Toto dakika ya 26 kwa shuti la mguu wa kulia akimalizia krosi ya beki Gardiel Michael kutoka kushoto
Yanga SC walioonekana kuathiriwa na uchovu wa kucheza mechi tatu ndani ya wiki moja mikoa miwili tofauti, leo walionekana kucheza kwa maarifa mno, muda mwingi wakiwa kwenye eneo lao na hawakutaka kutumia nguvu katika kuwania mipira dhidi ya wachezaji wa JKT Tanzania.
Hali hiyo iliwafanya waelemewe na kuzidiwa umiliki wa mpira, ingawa safu ya ulinzi ikiongozwa na kipa chipukizi Ramadhani Awam Kabwili ilitekeleza majukumu yake vizuri kwa kuokoa.
Kocha Mwinyi Zahera kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alimuingiza kiungo Mohammed Issa ‘Banka’ kumalizia dakika 30 za mwisho za mchezo, lakini alionekana kuathiriwa na kuwa nje muda mrefu akitumikia adhabu yake ya kufungiwa miezi 14 kwa kosa la kuvuta bangi.
Kwa mara nyingine leo, Nahodha Ibrahim Ajibu alishindwa kumaliza mechi baada ya kutolewa dakika 25 za mwisho akimpisha Deus Kaseke.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, KMC imelazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Alliance FC ya Mwanza Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. Abdul Hillary alianza kuifungia KMC dakika ya 50, kabla ya Israel Patrick kuisawazishia Alliance dakika ya 64.
Kikosi cha JKT Tanzania kilikuwa; Patrick Muntary, Anuary Kilemile, Dickson Chota/Ally Bilal dk59, Frank Nchimbi, Mohammed Fakhi, Geeorge Mande, Hassan Matelema, Mwinyi Kazimoto, Samuel Kamuntu/Said Luyaya dk75, Ally Ahmed ‘Shiboli’/Najim Magulu dk89 na Edward Songo.
Yanga SC; Ramadhani Kabwili, Paulo Godfrey, Gardiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Feisal Salum, Mrisho Ngassa/Mohammed Issa ‘Banka’ dk59, Papy Kabamba Tshishimbi, Amissi Tambwe, Pius Buswita/Kelvin Yondan dk75 na Ibrahim Ajibu/Deus Kaseke dk67.
Via>>binzubeiry
MBUNGE WA CHADEMA APATA AJALI

Gari la Mbunge lililopata ajali
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimethibitisha Mbunge wake wa viti maalum kutokea Zanzibar, Zainab Mussa Bakari kupata ajali katika eneo la Dumila mkoani Morogoro alipokuwa akitokea Jijini Dodoma kuja Dar es salaam kufuatia kuahirishwa kwa vikao vya Bunge.
Taarifa ya ajali hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene akisema kuwa Mbunge huyo anatarajiwa kuhamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
"Mbunge wa CHADEMA (VM) Zanzibar, Bi. Zainab Mussa Bakari amepata ajali eneo la Dumila akitoka Dodoma leo, abiria wote 3 na dereva wamejeruhiwa."
"Baada ya kutibiwa kwa dharura Morogoro, sasa wanapelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili1 kwa uchunguzi na matibabu zaidi" ameongeza Makene
Mapema jana, mmoja wa viongozi wa juu wa chama hicho, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye alihamishiwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kuzidiwa alipokuwa kwenye majukumu ya kikazi mkoani Tanga.
ULEVI WAMPONZA MUUGUZI ARUSHA,ASIMAMISHWA KAZI MWAKA MMOJA
Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha Martin Chama amesimamishwa kazi ya kutoa huduma za uuguzi na ukunga kwa mwaka mmoja na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania. Uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha baraza hilo cha 196 baada ya kumtia hatiani kwa makosa mawili kati ya manne yaliyowasilishwa katika baraza hilo Septemba mwaka jana na aameanza kuitumikia adhabu hiyo tangu Februari 7, 2019. Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa ameyataja makosa hayo kuwa ni kufika kazini akiwa amelewa na kutaka kuhatarisha usalama wa wagonjwa na ndugu zao…
CHADEMA YATHIBITISHA AJALI YA MBUNGE WAKE
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimethibitisha Mbunge wake wa viti maalum kutokea Zanzibar, Zainab Mussa Bakari kupata ajali katika eneo la Dumila mkoani Morogoro alipokuwa akitokea Jijini Dodoma kuja Dar es salaam kufuatia kuahirishwa kwa vikao vya Bunge. Taarifa ya ajali hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene akisema kuwa Mbunge huyo anatarajiwa kuhamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi. “Mbunge wa CHADEMA (VM) Zanzibar, Bi. Zainab Mussa Bakari amepata ajali eneo la Dumila akitoka Dodoma leo, abiria wote…
Picha : NDEGE ZAGONGANA UWANJANI

Kimetokea kioja ndege mbili za kampuni ya Kenya Airways zilipogongana katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini Kenya jioni ya Ijumaa, Februari 9,2019.
Imebainika kuwa ndege hizo mbili za mizigo ziligongana zilipokuwa gereji katika shughuli ya kufanyiwa ukarabati.
Walioshuhudia kisa hicho wanadai kuwa ndege yenye usajili 5Y- KYR iliruka ikiwa ardhini, wahudumu walipokuwa wakiizuia dhidi ya kugonga ukuta, iligonga ndege nyingine yenye usajili 5Y-FFF iliyokuwa imeegeshwa.
Hakuna aliyeriporiwa kujeruhiwa katika kisa hicho.
Hii ndiyo mara ya kwanza ambapo kisa aina hiyo kuripotiwa kufanyika kati ya ndege za kampuni hiyo maarufu





MBOWE ATUMA SALAMU ZA POLE KWA SUMAYE,AMTAKIA UPONAJI WA HARAKA
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe licha ya kuwa gerezani amemtumia salamu za pole Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ambaye alipatwa maradhi ya ghafla alipokuwa mkoani Tanga.Taarifa ya salamu hizo zimetolewa na chama chake ambapo amesema, "Mwenyekiti Freeman Mbowe ambaye bado yuko mahabusu Gereza la Segerea na Mbunge Esther Matiko, wamemtumia salaam za pole na kumtakia uponaji wa haraka Sumaye ili arejee katika siha njema"
Aidha taarifa ya chama hicho imeeleza kuwa Sumaye anaendelea vizuri na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari wa Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) alikohamishiwa baada ya kupokelewa Hospitali ya Taifa Muhimbili akitokea Hospitali ya Mkoa wa Tanga.
Aidha Katibu Mkuu wa Chama, Dkt. Vincent Mashinji, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Patrick Ole Sosopi pamoja na viongozi wengine wa Chama ngazi na maeneo mbalimbali ya nchi, wamefika hospitalini hapo kumjulia hali.
Mzee Sumaye alipatwa na shida ya afya mapema juzi akiwa mkoani Tanga ambako alikuwa anaendelea na ratiba ya shughuli mbalimbali za Chama mkoani humo.
Kabla ya kuwasilishwa Muhimbili Sumaye alilazwa Hospitali ya Bombo kabla ya kuletwa Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya yake.
MANARA AWAPA DONGO WANA YANGA "NITAACHA KAZI SIMBA JANUARI 2021 TENA KWA HIARI"

Haji Manara
Baada ya kusambaa kwa tetesi nyingi kuwa Afisa Habari wa Simba, Haji Manara yuko mbioni kutemwa katika nafasi yake, mwenyewe ameibuka na kueleza kinagaubaga kuhusiana na taarifa hizo.
Tetesi hizo zilisambaa mara baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simba Sports Club, Mohamed Dewji 'Mo' kuitisha mkutano na wanahabari, Ijumaa Februari 8 kuhusiana na masuala mbalimbali ya klabu hiyo pamoja na maandalizi ya mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amesema kuwa anafahamu kuwa mashabiki wengi hasa wa Yanga wanapenda asiendelee kuwepo Simba na siku wakisikia ameondoka watamfanyia sherehe kutokana na jinsi anavyowatesa.
"Kuna watu wa Yanga hamu yao nife kabisa!!, nawaumiza sana na siku mtakaposikia sipo kikazi Simba, mtafanya sherehe. Ila nikuhakikishie kuwa Mungu akinipa uhai nitaacha kazi Januari 2021 tena kwa hiari", amesema Manara alipokuwa akijibu 'comment' ya moja ya mfuasi wake.
Pia tetesi za Simba kuachana na Manara zimezidi kutiwa chumvi hasa pale Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi alipotangaza ujio wa nafasi za kazi katika idara mbalimbali hivi karibuni, ambapo watu wenye taaluma hizo watatuma maombi.
MUUGUZI ASIMAMISHWA KAZI KWA KULEWA KAZINI HOSPITALI YA MOUNT MERU
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, katika kikao chake cha 196 limemsimamisha Muuguzi Martin Chama kutoa huduma za Uuguzi na Ukunga kwa muda wa mwaka mmoja tangu tarehe 7.02.2019 baada ya kumtia hatiani na makosa mawili kati ya manne yaliyowasilishwa katika Baraza la Uuguzi na Ukunga mwezi Septemba 2018.
Makosa hayo ni pamoja na kufika kazini akiwa amelewa na kutaka kuhatarisha usalama wa wagonjwa na ndugu zao kwa kushindwa kutoa huduma kwa umakini na weledi.
Awali ofisi ya Msajili wa baraza la Uuguzi na Ukunga lilipokea tuhuma kutoka Hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mount Meru Arusha kupitia kwa Muuguzi mkuu wa mkoa ambaye pia ni msimamizi wa maadili wa mkoa wa Arusha kwa mujibu wa sheria N0 1ya mwaka 2010.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo muuguzi huyu alifika kazini tarehe 26.09.2018 zamu ya usiku majira ya saa tatu husiku akiwa amelewa na alianza kuwasumbua ndugu waliokuwa wakiwaangalia wagonjwa wao kutaka kuendelea kutoa huduma kwa wagonjwa ili hali akiwa amelewa sana hali ambayo ingesababisha kuhatarisha maisha ya wagonjwa kwa kuwa hakuwa na umakini.
Tuhuma hizi ziliwasilishwa na walalamikaji wawili waliokuwa wakiuguza wagonjwa wao.
Ofisi ya Msajili ilituma Afisa kutoka baraza la Uuguzi na Ukunga ambaye aliungana na timu ya Mkoani Arusha ikiongozwa na Muuguzi mkuu wa Mkoa wa Arusha.Timu hii ilifanya uchunguzi wa awali na kubaini mapungufu yaliyofanywa na muuguzi huyu ambayo ni kinyume na maadili ya Uuguzi na Ukunga.
Taarifa hiyo ilipelekwa katika kikao cha dharura cha bodi cha 195 ambacho pamoja na mambo mengine ilijadili taarifa hii na kuamua shauri hili lisikilizwe kataka kikao cha bodi cha 196 ambayo itahusisha mtuhumiwa na mashahidi ambao ni walalamikaji na watumishi waliokuwepo siku ya tukio.
Shauri hili limesikilizwa tarehe 07.02.2019 ambapo Ushahidi uliotolewa umemtia hatiani bwana Martini kwa kulewa na kushindwa kutoa huduma kwa wagonjwa kwa weledi na kutaka kuhatarisha Maisha ya wagonjwa na ndugu zao.baraza liliadhimia kwa kauli moja kumsimamisha kutoa huduma hizi kwa muda wa mwaka mmoja.
Baraza la Uuguzi na Ukunga ni Mamlaka iliyoanzishwa kisheria na kufanya kazi chini ya Sheria inayoitwa The Nursing and Midwifery Act, of 2010.Baraza lilianzishwa kwa ajili ya kulinda umma kutokana na huduma zinazotolewa na wauguzi na wakunga nchini na linafanya kazi kwa kusimamia ubora katika mafunzo na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinazingatia viwango vilivyowekwa.
Imetolewa na
Agnes Mtawa
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga
09.02.2019
WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO YATOA TAMKO MAUAJI YA WATOTO NJOMBE
Na Amiri kilagalila Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto imewashukuru waganga wa tiba asili na tiba mbadala kwa ushirikiano katika afya za binaadamu na maendeleo ya jamii kwa ujumla huku serikali ikiendelea kutambua umuhimu wa fani hiyo muhimu na kuwataka waganga wa tiba asili kuendelea kutoa ushirikianao katika zoezi la uhakiki ili waweze kufanya kazi kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na wizara ya afya. Akizungumza na waganga wa tiba asili na tiba mbadala katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe kwa niaba ya katibu mkuu wa…
MTOTO ALIYEKATWA KOROMEO NJOMBE AFARIKI DUNIA
Njombe. Meshack Myonga (4), aliyenusurika kuuawa baada ya kutekwa na kukatwa koromeo wilayani Njombe amefariki dunia mchana Jumamosi Februari 9, 2019 katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Desemba 23, 2018 mtoto huyo alitekwa na mtu asiyejulikana akiwa nyumbani kwa wazazi wake mtaa wa Mji Mwema wilayani Njombe, kisha kupelekwa msituni na kukatwa koromeo kabla ya kuokolewa na kijana mmoja. Baada ya kuokolewa alipelekwa Hospitali ya Mkoa ya Kibena-Njombe na baadaye kuhamishiwa hospitali ya rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi. mama mzazi wa mtoto huyo, Rabia Mlelwa amesema, “Leo tumekwenda Hospitali…
HAYA NDIYO MAGONJWA MANNE MAPYA YA ZINAA YANAWATOA JASHO WATAALAMU

Magonjwa mapya huibuka kila uchao, na magonjwa yaambukizwayo kwa ngono nayo ni miongoni mwao.
Hawa ni bakteria wanne ambao husababisha magonjwa makali ya zinaa ambayo yanaweza kuleta tishio la afya ya jamii.
1. Neisseria meningitides

Neisseria meningitidis, pia hufahamika kama meningococcus husababisha uvimbe hatari wa tando za uti wa mgongo na ubongo.
Lakini, bakteria huyo sasa anapata umaarufu zaidi kwa kusababisha maambukizi kwenye maungo ya uzazi.
Utafiti mmoja uliofanywa miaka ya 1970 ulibainisha ni kwa namna gani dume moja la sokwe alihamisha bakteria hao hatari kutoka mdomoni na puani kwenda kwenye uume wake baada ya kujilamba sehemu zake nyeti.
"Mnyama huyu (sokwe) mara kwa mara hujilamba uume wake," waandishi wa utafiti huo walibaini.
Takribani asilimia 10 ya watu wazima wana bakteria aina ya Neisseria katika makoo na pua zao. Tafiti zinabainisha kuwa wanaweza kuhamisha bakteria hao kupitia mabusu makali yahusishayo ndimi, ama kunyonya sehemu za siri za watu ambao hawana bakteria hao.
Watafiti hata hivyo hawana hakika ni kwa nini bakteria hao wamesambaa kwa kasi na kuzuz ugonjwa hatari kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja barani Ulaya, nchini Marekani na Canada.
Hata hivyo, utafiti mmoja juu ya uwasho mkali wa mrija wa kupitisha mkojo toka kweye kibofu unaosababishwa na bakteria huyo ulibainisha kuwa wanaume waliopata maambukizi hayo kupitia ngono ihusishayo mdomo.
Wanasayansi wanaamini kuwa, maambukizi makali ya bakteria huyo yaliyokumba kwa nguvu miji kadhaa ya Marekani mwaka 2015 yalichochewa na vinasaba vya karibu vya bakteria wa familia mojaNeisseria gonorrhoeae, ambaye husababisha ugonjwa mwengine wa zinaa wa kisonono.
Ukaribu wa bakteria ha ulisababisha kusambaa kwa haraka kwa maambukizi hayo hatari.
Kuna aina tano ya bakteria hatari wa Neisseria meningitidis duniani, lakini kwa bahati nzuri kuna chanjo za aina mbili ambazo zinapatikana na zinakinga dhidi ya aina zote za bakteria hao.
2. Mycoplasma genitalium
Mycoplasma genitalium ni hatari sana kwa mfumo wa uzazi kwa wanawake
Mycoplasma genitalium ni hatari sana kwa mfumo wa uzazi kwa wanawakeMycoplasma genitalium, moja ya bakteria wadogo zaidi wanaofahamika, wanapata umaarufu mkubwa zaidi ya maumbo yao kwa kusabisha maambukizi hatari ya ugonjwa wa zinaa.
Bakteria huyo aligunduliwa miaka ya 1980, na leo hii anaambukiza asilimia moja mpaka mbili ya watu hususani vijana.
Maambukizi ya Mycoplasma genitalium ambayo kwa kawaida hayana dalili, wakati mwengine hufanana na dalili za kisonono na kaswende kwa kuwashwa mfululizo kwa mrija wa mkojo kwa wanaume na mlango wa kizazi kwa wanawake.
Kutokana na kuweza kusamabisha maumivu makali ya nyonga kwa wanawake, bakteria huyo anahusishwa pia ugumba, kuharibika kwa mimba, kuzaliwa watoto njiti na hata kufariki watoto tumboni kwa mama.
Ijapokuwa kondomu inaweza kuzuia maambukizi yake, watafiti wanatoa tahadhari juu ya usugu wa bakteria huyo kutibika na dawa za antibaotiki za azithromycin na doxycycline.
3. Shigella flexneri
Shigella flexneri hupelekea maumivu makali ya tumbo, na kuhara damu ambapo hustawisha kusambaa kwa bakteria hao.
Shigella flexneri hupelekea maumivu makali ya tumbo, na kuhara damu ambapo hustawisha kusambaa kwa bakteria hao.Shigellosis husababishwa kwa kugusa moja kwa moja au kwa njia moja au nyengine kinyesi cha binadamu.
Maambukizi ya bakteria ho hupelekea maumivu makali ya tumbo, na kuhara damu ambapo hustawisha kusambaa kwa bakteria hao.
Ijapokuwa ugonjwa huo umekuwa ukionekana zaidi kwa watoto na wasafiri kwenye nchi zenye uchumi mdogo na wa kati, watafiti walianza kupokea kesi za ugonjwa huo kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja toka miaka ya 1970.
Ugonjwa huo, wanasayansi wanaamini, umechukuwa njia mpya ya maamukizi kwa kutumia ngono ya kinyume na maumbile na ngono inayohusanisha midomo na kusabisha maambukizi kadhaa ya gonjwa hilo la zinaa kwa miongo minne sasa.
4. Lymphogranuloma venereum (LGV)
Magonjwa mengi ya zinaa yanaweza kuepukwa kwa kutumia kondomu
Magonjwa mengi ya zinaa yanaweza kuepukwa kwa kutumia kondomuLGV mwanzo hutokea kama kipele ama lengelenge na kisha kushambuli mfumo wa kinga ya mwili na hivyo kupelekea uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Ugonjwa huu pia husababisha maambukizi katika njia ya haja kubwa na pia kusababisha maumivu makali ya tumbo.
Katika miaka 10 iliyopita, kumekuwa na maambukizi makubwa ya LGV barani Ulaya na Amerika ya Kaskazini hususani kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Kutumia kondomu kunaweza kupunguza uwezekano wa maambukizi, na kutibu ugonjwa huu kunahitaji walau matibabu ya wiki tatu na kunywa antibaotiki kama doxycycline.
Chanzo- BBC
DKT. GWAJIMA AZITAKA TIMU ZA AFYA MIKOANI KUJITATHIMINI KIUTENDAJI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, anayeshughulikia afya, Dkt. Dorothy Gwajima, ameziagiza timu za Afya za Mikoa (Regional Health Management Team- RHMT) yote nchini, kujitathmini hali yao ya utendajikazi na kuona kama wanatija inayokubalika kwa taifa. Gwajima ameitoa kauli hiyo, alipokuwa akizungumza na timu ya Afya ya Mkoa wa Dodoma inayo ongozwa na James Kiologwe, Mganga Mkuu wa Mkoa huo wakati alipofanya ziara yake ya kwanza toka ateuliwe kushika wadhifa huo Januari 08,2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John…
MAPACHA WANAOFANANA WATANGAZA NDOA NA MWANAUME MMOJA
Mapacha Anna na Lucy
Mapacha wanaofahamika kufanana ulimwenguni mzima wamefichua kwamba wanapanga kuolewa kwa mpenzi mmoja hivi karibuni.
Anna na Lucy DeCinque wenye umri wa mia 33 kutoka Perth nchini Australia walisema wao hulala kwenye kitanda kimoja na mpenzi wao na hata hushiriki tendo la ndoa kwa pamoja.
Mapacha wanaofanana ambao wako na mpenzi mmoja, wanalala kwenye kitanda kimoja.
Wakizungumza kwenye mahojiano na runinga moja nchini Australia, mapacha hao walisema hawana wivu kati yao na wao kuonyeshwa mapenzi ya dhati na mpenzi wao.
Kulingana na mapacha hao ambao wanaishi pamoja na mama yao, walisema wanapanga harusi hivi karibuni licha ya serikali ya Australia kutokubali ndoa za mitala.
Anna na Lucy DeCinque wenye umri wa mia 33 kutoka Perth nchini Australia walisema wao hulala kwenye kitanda kimoja na mpenzi wao na hata hushiriki ngono kwa pamoja.
" Hakuna wivu kati yetu, mpenzi wetu akimbusu mmoja wetu, atambusu tena mwingine, mpenzi wetu hufurahia mtindo wetu wa kimavazi na hutusifia kila mara, tunampenda sana sisi wote," Mapacha hao walisema.
Mapacha hao pia walisema wanapanga kupata mimba pamoja na kuzaa watoto wao wakati mmoja.
MTOTO ALIYEKATWA KOROMEO NJOMBE AFARIKI DUNIA
. Meshack Myonga (4), aliyenusurika kuuawa baada ya kutekwa na kukatwa koromeo wilayani Njombe amefariki dunia leo mchana Jumamosi Februari 9, 2019 katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Desemba 23, 2018 mtoto huyo alitekwa na mtu asiyejulikana akiwa nyumbani kwa wazazi wake mtaa wa Mji Mwema wilayani Njombe, kisha kupelekwa msituni na kukatwa koromeo kabla ya kuokolewa na kijana mmoja.
Baada ya kuokolewa alipelekwa Hospitali ya Mkoa ya Kibena-Njombe na baadaye kuhamishiwa hospitali ya rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi.
Na Godfrey Kahango, Mwananchi
HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO FEBRUARI 10,2019.
Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Februari 10, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.
Saturday, 9 February 2019
30 WASHIKILIWA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE,KESI KUFIKISHWA MAHAKAMANI JUMATATU
Jeshi la Polisi Makao Makuu Kitengo Maalum cha Kupambana na uhalifu kikiongozwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas, kimeshirikina na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe kuendesha Operesheni Maalum ya kukabiliana na matukio ya mauaji ya watoto wadogo ambayo yamejitokeza mkoani humo, mpaka sasa watuhumiwa 30 wamekamatwa waliojihusisha na matukio hayo, Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas, amesema watuhumiwa hao ifikapo Jumatatu watakuwa wamefikishwa Mahakamani kukabiliana na tuhuma za mauaji ya watoto, Aidha Naibu Kamishna Sabas, amewataka…



