Monday, 21 January 2019

MHE.ULEGA : SERIKALI IMEWEKA MIKAKATI KUBORESHA SEKTA YA MIFUGO



Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega,akizungumza na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Singida kabla ya kuanza ziara ya uhamasishaji wa kuogesha ng'ombe katika kijiji cha Mgori.
Bw.Rashid Mandoa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Singida akitoa taarifa kwa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega.
Bw.Elia Digha,Mwenyekiti wa halmashauri ya Singida akitoa ujumbe kwa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega (hayupo pichani)kuhusu kuweka mikakati katika sekta ya mifugo nchini.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akikagua ng'ombe katika kijiji cha Mgori kilichopo Singida vijijini alipokuwa ameenda kuzindua zoezi la uhamasishaji wa kuogesha mifugo.
Baadhi ya ng'ombe wakisubiri kuogeshwa dawa katika josho la Mgori katika hamshauri ya wilaya ya Singida vijini ambapo Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega alizindua zoezi la uhamasishaji wa kuogesha mifugo.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega,akichanganya dawa za kudhibiti magonjwa ya mifugo katika kijiji cha Mgori kwa ajili ya kuhamasisha kuogesha ng'ombe katika majosho yalipo nchini ambapo Serikali imeamua kutoa dawa bure kwa wafugaji.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akisaidiana na baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo katika josho lenye dawa ambazo zimetolewa bure na Serikali zoezi hilo la uzinduzi katika mkoa wa Singida lilifanyika katika kijiji cha Mgori kilichopo halmshauri ya wilaya ya Singida vijijini.Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

........................

Na.Alex Sonna,Singida

Serikali imeandaa mkakati wa kuboresha sekta ya mifugo pamoja na kudhibiti magonjwa ya mifugo huku ikiwahimiza wafugaji kuzingatia matumizi ya majosho yenye dawa.

Akizungumza na wafugaji Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega wakati wa zoezi la uhamasishaji wa uogeshaji wa ngo’mbe kanda ya kati mkoani Singida, katika kijiji cha Mgori kilichopo halmshauri ya wilaya ya Singida vijijini.

Katika uhamasishaji huo waziri Ulega aliwataka wafugaji kufanya zoezi la uogeshaji wa mifugo uliyoanzishwa uwe wenye tija na endelevu, kwa vile hivi sasa hakuna sababu za kushindwa kuogesha mifugo yao katika majosho yenye dawa ya kudhibiditi kupe.

Aidha amesema kuwa kwa sasa serikali katika zoezi hili, imetoa dawa bure kwa halmashauri zote nchini, na kukarabati majosho yote yaliyokuwa hayafanyi kazi, ili wafungaji waweze kuogesha mifugo yao , kukinga ugonjwa hatari unaoenezwa na kupe, ambao unaoongozwa katika vifo vya ng’ombe hapa nchini.

"Mwanzo shughuli hizo zilikuwa zikifanywa kwa ,kutofuata taratibu nzuri za makusanyo yalikuwa yakitoka kwa wafugaji walipokuwa wakipata huduma za kuongesha mifugo yao, hazikuwa na taarifa ya mapato na matumizi na hivyo kushindwa kuwa na utaratibu endelevu wa shughuli hiyo, majosho mengi yalisimama kufanya kazi"amesema Ulega

Katika kampeni hii ya uhamamishaji wa uongeshaji wa mifugo tozo imepunguwa ambapo hivi sasa kila ng’ombe ana ogeshwa katika majosho ni shilingi 50 tu, huko nyuma uogeshaji ulikuwa unatozwa wastani wa shilingi mia 2 kwa kila ngo’mbe na kwa mbuzi ilikuwa shilingi 10.

“Nyie wafugaji msikalie rasialimali hii ya mifugo mliokuwa mnayo, kwani ni uchumi mkubwa sana mliyokuwa nayo kwenu na pia kwa Taifa ili kuongeza mapato, yanayotokana na mifugo yenu”amesisitiza Ulega.

Aidha alifafanua kuwa ufungaji kwa kufuata taratibu za ufugaji wa kisasa na kibiashara kwa kuvuna mifugo inapozidi katika eneo uliyokuwa nayo, itakusaidia kupata kipato katika kuboresha maisha yako na ya familia.

Uhamasishaji huu unafuatia uzinduzi wa kampeni ya uogeshaji wa mifugo,iliyofanywa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina katikati ya mwezi jana katika kijiji cha Buzirayombo halmashauri ya chato.

Share:

BODI YA WAKURUGENZI DAWASA YAWATAKA WAFANYAKAZI DAWASA WAWE WAADILIFU

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi wakipewa maelezo juu ya mfumo wa usambazaji wa maji kutoka katika tanki la Makongo jijini Dar es Salaam. Bodi hiyo inafanya ziara ya siku tatu ili kuweza kujifunza na kujionea jinsi mifumo ya usambazaji wa maji kwa jiji la Dar es Salaam na Pwani. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

 Mashine zilizofungwa katika tanki la makongo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi wakionyeshwa mtambo wa kuendeshea maji. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Wakiangalia mfumo wa Tenki la SalaSala jijini Dar es Salaam ikiwa ni ziara yao ya kujifunza masual mbali mbali ya maji.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi  wakiwa wamewasili kituo cha mtambo wa Ruvu chini- eneo la Bagamoyo - Pwani. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi wakiongea na wafanyakazi wa DAWASA kituo cha mtambo wa Ruvu chini- eneo la Bagamoyo - Pwani. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi wakiongea wakiangalia zoezi la kutandika mabomba ili kuwagawia maji wakazi wa Goba -Kizudi jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange jinsi maji yanavyovunwa katika Mtambo wa Ruvu Chini - eneo la Bagamoyo - Pwani.
Wakikagua eneo la mto Ruvu chini...

Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) pampu za kuvuta maji.
Meneja wa DAWASA ofisi ya Bagamoyo, Alexander Ng'wandu akitoa maelezo machache mbele ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange mara baada ya kutembelea ofisi hizo zilizopo mjini Bagamoyo - Pwani.
Meneja wa DAWASA ofisi ya Bagamoyo, Alexander Ng'wandu akitoa maelezo machache mbele ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis mara baada ya kutembelea tenki  la maji la Bagamoyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi wakiongea na wanahabari mara baada ya kumaliza kutembelea kituo cha mtambo wa Ruvu chini- eneo la Bagamoyo - Pwani.

JENERALI MWAMUNYANGE ATEMBELEA MTAMBO WA RUVU CHINI

NaCathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imewataka wafanyakazi wa DAWASA kuendelea kuwa waadilifu katika kazi zao ili kuweza kuwapa huduma bora wananchi wa Dar es Salaam na Pwani.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi mara baada ya kutembelea mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini na kuongea na wafanyakazi wa DAWASA wa kituo hicho.

Jenerali Mstaafu Mwamunyange amefurahishwa na utunzaji wa mazingira katika eneo la mto Ruvu ikiwa ndio chanzo kikubwa kinachozalisha maji kwa asilimia 88 katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Akiwa katika ziara yake ya siku ya pili, Jenerali mstaafu Mwamunyange ametembelea mtambo huo ikiwa ni mara ya kwanza toka achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo.

"Nimejifunza mambo mengi hata wenzangu wamekili kuna mambo mengi tulikuwa hatuyafahamu hakika sasa tutakuwa watendaji wazuri kwa kutambua kile tunachokisimamia," Amesema Jenerali Mstaafu Mwamunyange.

Amesema jitihada kubwa za serikali zinafanyika kuhakikisha wananchi wote wanapata maji hususani kwenye maeneo yaliyokuwa hayana maji kwa kipindi chote kikubwa wananchi wawe wavumilivu kwakuwa DAWASA wanafanya kazi kuwapelekea maji.

Baada ya kuwasili katika mtambo huo walipata fursa ya kuzungumza na wafanyakazi wa mtambo huo na kuwataka wafanye kazi kwa juhudi kubwa ili kutimiza adhma ya serikali ya kufikia asilimia 95 ya wananchi wote ifikapo 2020.

Amesema, anafahamu kuna changamoto mbalimbali za wafanyakazi ila amewaahidi atazifanyia kazi atakapokutana na Sekretarieti ya DAWASA.

Mbali na kutembelea mtambo wa Ruvu Chini, Bodi hiyo ilitembelea Tenki la maji la Changanyikeni, Busta pampu zilizofungwa Makongo kwa ajili kusukuma maji na maunganisho mapya Salasala.

Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi itaendelea kwenye maeneo mengine tofauti kwa ajili ya kujifunza na kuona namna DAWASA wanavyotoa huduma ya maji kwa wananchi wa Dar esSalaam na Pwani.
Share:

YANGA NA SIMBA KUPOZA MACHUNGU YA VIPIGO PAMOJA LEO


Wachezaji wa Simba kushoto na Yanga kulia.

Klabu za soka za Yanga na Simba zote zimerejea Dar es salaam usiku wa kuamkia leo, Januari 21, 2019, zikitokea kwenye mechi zake za uganini ambapo zote ziliambulia kichapo.

Timu hizo mbili zote zimeunganisha kwenye maandalizi ya michuano ya SportsPesa ambapo kila timu imeingia kambini kuanza mazoezi tayari kwa michuano hiyo inayoanza kesho.

''Kikosi kimerejea salama jijini Dar es salaam jana usiku na kuingia kambini moja kwa moja tayari kwa maandalizi ya michuano hiyo ambapo mchezo wa kwanza kwetu utakuwa kesho Jumanne dhidi ya Kariobangi Sharks'', imeeleza taarifa ya Yanga.

Kwa upande wake msemaji wa Simba Haji Manara amesema baada ya timu kurejea salama nyumbani, leo inaanza mazoezi kwa ajili ya michuano hiyo, ambapo inatarajia kucheza na AFC Leopards ya Kenya katika mchezo wake wa kwanza kesho Jumanne.

Simba ilikuwa nchini DR Congo ambapo ilifungwa mabao 5-0 na AS Vita Club kwenye mechi ya kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga ikifungwa bao 1-0 na Stand United kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
Share:

CAG ALIVYOTUA DODOMA KUHOJIWA NA KAMATI YA BUNGE KAULI YAKE YA 'UDHAIFU WA BUNGE'


 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad leo asubuhi Januari 21, 2019 amefika mbele ya kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu kauli yake ya “udhaifu wa Bunge.”

CAG Assad aliyeteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, Desemba Mosi mwaka 2014 ameitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa wakati alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa (UN) akiwa New York, Marekani alikokuwa akihudhuria mkutano.

Alitumia neno “udhaifu” wa Bunge alipokuwa akieleza sababu za kutofanyiwa kazi kwa ripoti zake ambazo zimekuwa zikibainisha ufisadi.

Mara baada ya kuingia katika ukumbi yanapofanyika mahojiano hayo saa 5:01 asubuhi, CAG aliyekuwa amebeba begi dogo jeusi, aliwasha kompyuta yake mpakato na kisha kuwasalimu wajumbe wa kamati hiyo.

Alifika katika viwanja vya Bunge saa 4:49 asubuhi akiwa peke yake bila wasaidizi, akateremka katika gari jeupe na kupita katika mashine za ukaguzi.

Katika mashine hizo Profesa Assad alivua viatu, koti, saa, miwani na kisha kuvaa tena vitu hivyo baada ya ukaguzi.

Huku ulinzi ukiwa umeimarishwa, baada ya ukaguzi Profesa Assad alikwenda kuketi eneo la mapumziko na msaidizi wa Spika, Said Yakubu alimpelekea kitabu cha kusaini.
Share:

MTUMISHI WA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI APOTEA



Share:

TAKUKURU YAZIANIKA IDARA ZINAZOONGOZA KWA RUSHWA SHINYANGA

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Shinyanga imetoa taarifa ya utendajikazi wake kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2018,katika kuchunguza,kuelimisha umma na kufanya utafiti,kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na.11 ya mwaka 2017. 

Taarifa hiyo imeonyesha kupokea taarifa 90 ambapo idara ya polisi(10), elimu(12), mahakama(11), serikali za mitaa(10), ardhi(10), afya(7) na huduma za kifedha(7) zikitajwa kulalamikiwa kwa vitendo vya rushwa. 

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Francis Luena alisema ofisi hiyo imetembelea miradi 9 yenye thamani ya shilingi bilioni 5.424 na kubaini baadhi ya miradi kuwa na dosari. 

“Miradi yenye dosari ni pamoja na mradi wa machinjio na banda la kuanikia ngozi wilaya ya kishapu ambao thamani yake ni shilingi milioni 12, fedha zinazochunguzwa ni shilingi milioni 4.3, pamoja na mradi ujenzi wa kituo cha mabasi baada ya kuufuatilia iligundulika shilingi milioni moja matumizi yake yalikuwa hayaeleweki,” alisema Luena. 

Kaimu Mkuu huyo alisema kesi zinazoendelea mahakamani ni 19 na kwamba taasisi hiyo imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa watumishi mbalimbali, kufanya uchunguzi wa vitendo vya rushwa na kwafikisha mahakamani wahusika. 

Na Malaki Philipo – Malunde1 blog
Share:

ODINGA AMKUMBUKA BABA YAKE MZAZI ASEMA ALIKUWA JASIRI

Kiongozi wa ODM Raila Odinga Jumapili, Januari 20 
aliadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 ya kifo cha baba yake mzazi Jaramogi Oginga Odinga 


Oginga alikuwa mwanasiasa maarufu sana katika kupigania uhuru wa Kenya, na aliaga dunia Januari 20 1994. 


Kupitia mtandao wa kijamii, Raila alimtaja baba yake kuwa mtu jasiri, aliyejali wengine na aliyefanikisha kupatikana uhuru wa nchi ya Kenya. 

"Miaka 25 tangu ulipotuacha. Lakini vitendo vyako vya kijasiri na kujitolea bado vinaendelea kutupa motisha Kenya na mamilioni barani Afrika.Leo tunakukumbuka Jaramogi," ulisoma ujumbe huo. 

Baba ya Raila atakumbukwa sana kwa kuwa makamu wa kwanza wa rais baada ya Kenya kupata uhuru na alikuwa ofisini kati ya 1964 na 1966. 

Kinachoshangaza ni kwamba, baba na mwana wana vitu vingi vinavyolingana katika siasa zao. Itakumbukwa Raila alikiongoza kikosi cha kupinga katiba iliyokuwa imependekezwa na alama yao ilikuwa ‘No’ na nembo ya chungwa. 

Alipokuwa makamu wa rais, Jaramogi alipinga vitu kadhaa alivyotaka Jomo Kenyatta, aliyekuwa akiegemea sana mataifa ya Magharibi. 

Yeye ndiye aliyeanzisha kauli maarufu ya "Bado Uhuru” (Not Yet Uhuru) ambacho pia ni kichwa cha kitabu kuhusu maisha yake. 

Raila, wakati akiwa waziri wa barabara na baada ya kuongoza kampeni za kura ya maamuzi na kushinda, alianzisha chama cha Orange Democratic Movement (ODM), alivyofanya baba yake akianzisha chama cha Kenya People's Union (KPU) alipokuwa haelewani na Jomo Kenyatta.


Share:

RAPPER OCTOPIZZO AINGIA KWENYE TUHUMA NZITO ZA MAUAJI YA MWANAFUNZI

Msanii wa Hip Hop nchini Kenya, Octopizzo Jana Jumapili 20, 2019 ametuhumiwa kwa mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha 
Strathmore kilichopo jijini Nairobi.Octopizzo

Familia ya mwanafunzi huyo, imesema kuwa kijana wao alijeruhiwa katika nyumba ya Octopizzo kabla ya kujirusha kwenye ghorofa siku ya Jumamosi iliyopita.

Mwanafunzi huyo aitwaye, Kenneth Abom (19) inaelezwa kuwa kabla ya kuaga dunia alishambuliwa kwa panga na watu wasiojulikana na baadae alijirusha kutoka kwenye ghorofa baada ya kufanyiwa matibabu.

Tayari rapper Octopizzo, amekanusha taarifa hizo, ambapo amekiambia kituo cha NTV Kenya kuwa kijana huyo alipitia nyumbani kwake akiwa tayari amejeruhiwa na vitu vyenye ncha kali kichwani.

Octopizzo amesema Alhamisi iliyopita kijana huyo, alikatiza kwenye nyumba yake akiwa na majeraha hayo na kumshauri aende hospitali.

Baadae Octopizzo akaja kusikia, kijana huyo amejirusha kutoka ghorofani baada ya kupatiwa matibabu.
Share:

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM -UDSM CHAPATA MAPROFESA WAPYA


Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), limewathibitisha maprofesa wawili wasaidizi kuwa maprofesa kamili.


Pia baraza hilo limewathibitisha wahadhiri watano kuwa maprofesa wasaidizi, wahadhiri 13 kuwa wahadhiri waandamizi ikiwa ni pamoja na wahadhiri wasaidizi tisa kuwa wahadhiri kwa kutumia vigezo mbalimbali vya kitaaluma vinavyotakiwa.

Naibu Makamu Mkuu wa chuo anayeshughulikia masuala ya taaluma, Profesa Bonaventure Rutinwa amesema hayo katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari.

Rutinwa alisema baraza hilo la chuo hicho limewathibitisha Wineaster Anderson na Imani Sanga kuwa maprofesa chuoni hapo kutokana na kuandika machapisho mbalimbali ya kitaaluma ambayo yamewapatia alama inayohitajika.

Pia kwa kutumia vigezo mbalimbali vya kitaaluma, Yusup Koleleni, Gastor Mapunda, Esther Ishengoma, Dev Jani na Ulingeta Mbamba wamekuwa maprofesa wasaidizi kutoka wahadhiri waandamizi.

Kwa mujibu wa Profesa Rutinwa, Elinaza Mjema, Evarist Magoti, Noel Lwoga, Grace Kinunda, Richard Sambaiga, Nandera Mhando, Edith Lyimo, Ernesta Mosha na Mussa Hans wamekuwa wahadhiri waandamizi.

Vilevile Juma Masele, Deusdedit Rwehumbiza, Kelefa Mwantimwa na Chacha Nyamkinda nao wamekuwa wahadhiri waandamizi.

Waliopandishwa kwa vigezo vya kitaaluma kuwa wahadhiri ni Makarius Itambu, Alfred Mulinda, Rodreck Henry, Leonia John, Michael Mashauri, Titus Ngeme, Gerald Tinali, Patrick Singogo na Cosmas Masanja.

Ametoa angalizo kuwa kupanda madaraja hayo kunaongeza idadi ya watumishi wabobevu chuoni hapo.
Share:

MAJIBIZANO YA NDUGAI NA LISSU YAKOLEA.."SPIKA HAJUI CHOCHOTE,HAJUI NIMEPONA AU SIJAPONA"

Majibizano kati ya Tundu Lissu na Spika Job Ndugai yamezidi kukua baada ya mbunge huyo wa Singida Mashariki (Chadema), kuhoji maswali lukuki kuhusu taarifa za matatizo yake akijibu hoja kwamba hana kibali cha kuwa nje ya nchi.

Juzi, Lissu alitoa waraka alioupa jina la “Baada ya Risasi Kushindwa, Sasa Wanataka Kunivua Ubunge”, ukieleza tuhuma zake dhidi ya Serikali kuwa kuna mpango wa kumvua uwakilishi wake wa Singida Mashariki.

Lakini Spika Ndugai aliiambia Mwananchi juzi madai hayo ya Lissu ni “uzushi”, akieleza kuwa Lissu anapaswa kutambua “hana ruhusa ya Spika ya kuwa huko anakozurura”.

“Yeye ametoka kuugua aache uzushi, arudi nyumbani. Tunamsubiri nyumbani,” alisema Spika Ndugai juzi.

“Kitu muhimu ni kwamba ajue hana ruhusa ya Spika ya kuwa huko anakozurura. Sasa achunge kidogo, maana Spika ana nguvu zake, asimpe sababu.”

Ndugai alisema hawezi kumpangia Lissu mambo ya kusema ila ofisi yake haina taarifa.

Hata hivyo, Lissu, ambaye ni mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, alikuwa na maswali mengi wakati alipozungumza na Mwananchi jana kuhusu majibu hayo ya Ndugai.

“Spika anajuaje kwamba nimepona? Anajua masharti niliyopewa na daktari ni yapi? Anajua nimetokaje hospitalini?” alihoji Lissu, ambaye alipelekwa Ubelgiji kumalizia matibabu ya majeraha aliyopata mwaka juzi baada ya kushambuliwa kwa risasi takriban 30 na watu wasiojulikana akiwa nje ya makazi yake, Area D mjini Dodoma.

“Spika hajui. Hajui kwa sababu yeye, tume ya utumishi wa Bunge au maofisa wa Bunge hawajaja kuniona tangu Septemba 7 mwaka juzi niliposhambuliwa.

“Spika Ndugai hajui chochote, hajui nimepona au sijapona. Hajui kwa sababu hajataka kujua, hajataka kunipigia simu kuniuliza kama ambavyo wengine wananipigia simu. Hajataka kuwasiliana na familia yangu, hajui kwa sababu ametaka kubaki asiyejua,” alisema Lissu.

Lissu, mmoja wa watu walioibukia kuwa wakosoaji wakubwa wa Serikali, alisema Spika amesikia tu kuwa yuko Uingereza lakini hajui yuko wapi.

“Ukimuuliza leo Lissu yupo wapi sidhani kama atakuwa na jibu. Hawezi kuwa na jibu kwa sababu yeye na watu wake hawataki kumjulia hali Lissu,” alisema.

Mwanasheria huyo alisema Spika aliwahi kusema kuwa angemtembelea wakati akiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya au sehemu yoyote ile, lakini mpaka jana hakuwa ametimiza ahadi hiyo.

Lissu pia alizungumzia hoja ya Ndugai kuwa hana kibali cha ofisi ya Spika.

“Hicho kibali kinatolewa katika mazingira gani? Nilishambuliwa mchana kabisa Dodoma na kusafirishwa nikiwa sijitambui. Sasa ni muda gani nilipaswa kuomba kibali?” alihoji.

Alisema suala hilo la kusafirishwa kwenda Nairobi kwa matibabu liliamuliwa katika kikao kilichofanyika Dodoma kilichomuhusisha Ndugai, Dk Tulia Ackson (Naibu Spika), Dk Thomas Kashililah (katibu wa Bunge wa wakati huo, Freeman Mbowe (Mwenyekiti Chadema), Ummy Mwalimu (Waziri wa Afya) na Dk Mwigulu Nchemba (aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani).

“Mimi nikiwa sijitambui, napigania roho yangu,” alisema Lissu ambaye alisema taarifa za kikao hicho alipewa baadaye.

“Katika kikao kile iliamuliwa mimi nipelekwe Hospitali ya Nairobi na nikasindikizwa na daktari wa Dodoma na ndege ikaruhusiwa kuruka saa 6:00 usiku. Sasa hicho kibali ninachoambiwa na Spika Ndugai ni kipi?

“Yeye alikuwepo, aliniona, hicho kibali anachokisema ni kipi? Mtu aliyejeruhiwa vile anaweza kuomba kibali? Au kuniona Uingereza ndio nimepona?”

“Hawajaja kuniona ndio maana wanasema nimepona. Wangekuja kuniona wangejua hicho wanachokisema kina ukweli kiasi gani. Wangejua nimepona au bado, sasa wanabaki kusema nimepona bila kuja kuniona?”

Via Mwananchi
Share:

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU JAN 21, 2019

Mchezaji wa West Ham Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 30, ameibuka na kuwashangaza wengi kwa kupigiwa upatu kuichukua nafasi ya mshambulizi wa Tottenham kutokana na kujeruhiwa kwa wachezaji wa timu hiyo.' (Sun)

Eden Hazard hatojiunga na Real Madrid mwezi huu lakini mchezaji huyo wa miaka 28 anataka kukataa maombi mengine yoyote na ahamie katika klabu hiyo bingwa wa Uhispania mwishoni mwa msimu. (Marca, kupitia Mirror)

Chelsea inatarajiwa kukamilisha usajili kwa mkopo wa mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, mwenye umri wa miaka 31, huku naye mlinzi Emerson Palmieri, mwenye miaka 24, huenda akavuka upande wa pili kwa thamani ya £15m. (Star)Ganzalo Higuan anatarajiwa kuwasili London kesho Jumanne kukamilisha uhamisho wake kutoka Juventus kwenda Chelsea

Higuain anatarajiwa kuwasili London kesho Jumanne kukamilisha uhamisho wake kutoka Juventus kwenda Chelsea.(Express)

Kocha wa Milan Gennaro Gattuso, aliyetarajia kuwa na Higuain kwa mkopo msimu huu, anasema anakubali uamuzi wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina kuondoka. (Marca)

Juventus inakaribia kufikia makubaliano ya uhamisho kwa mkopo kwa mlinzi wa Manchester United Matteo Darmian, mwenye umri wa miaka 29. (Guardian)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa timu ya taifa ya Colombia James Rodriguez, mwenye umri wa miaka 27, anatarajiwa kukataa nafasi ya uhamisho kwenda Arsenal na atasalia kwa mkopo Bayern Munich hadi 'angalau'mwisho wa msimu. (ESPN)
Chanzo : Bbc
Share:

Usikubali Kupitwa na Habari : Pakua Upya App ya Malunde 1 blog ...Imeboreshwa Kukupa Raha zaidi

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Share:

MANARA ATOA SABABU ZA KUTOJIBU SALAMU ZA WANAJANGWANI

Simba imereja nyumbani ikiwa na kumbukumbu mbaya kichwani, ikipoteza mchezo huo kwa mabao 5-0.
Afisa Habari wa Simba, Haji Manara ambaye amekuwa akiandamwa na mashabiki wa Yanga kutokana na tambo zake, amejitokeza na kueleza sababu ambayo imepelekea ukimya wake baada ya mchezo huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amesema kuwa sababu iliyomfanya kushindwa kujibu ujumbe wa watani wake ni tatizo la mtandao nchini DR Congo.

"Alhamdulillah tumerejea salama nyumbani na leo tunaanza mazoezi kwa ajili ya tournament ya @SportPesaCup!!
Nitumie pia fursa hii kuwashukuru nyote mlionitakia kheri na baraka ktk siku yangu ya kuzaliwa (kumbukizi) juzi Ijumaa, ila niwaombe radhi kwa kutokujibu salaam zenu,na sababu kubwa Congo nzima haina internet kwa sasa ila maeneo machache tena kwa wakati mfupi sana!!
Niseme tu Asanteni Sana na nimefarijika mno,na hasa zile salaam zilizotoka kwa Watani zangu 
Mungu atubariki sote Insha'Allah" ameandika Manara


Kufuatia matokeo hayo, sasa Simba inakamata nafasi ya tatu katika kundi lake la D, ikiwa na alama 3 na magoli 3. Kundi hilo linaongozwa na Al Ahly iliyo na alama 4, AS Vita iliyo nafasi ya pili kwa alama 3 na JS Saoura inayoburuza mkia kwa alama moja pekee.

Baada ya kurejea nchini, Simba itaingia moja kwa moja kambini tayari kwa maandalizi ya mashindano ya Sport Pesa Seper Cup yanayotarajia kuanza kesho katika uwanja wa taifa, kwa mujibu wa taarifa rasmi ya klabu hiyo.

Simba inatarajia kukutana na AFC Leopards ya Kenya katika mchezo wa awali na imesema kuwa itayatumia mashindano hayo kwaajili ya kujiandaa na michuano inayoendelea ya Klabu Bingwa Afrika.
Share:

YAMEBAKI MASAA, HATMA YA SAKATA LA CAG NA SPIKA

Hatimaye lile sakata lililoibuliwa na Spika Job Ndugai la kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kufika mbele ya Kamati ya Bunge kuelezea kauli yake kuhusu, 'Udhaifu wa Bunge', leo ndio maamuzi rasmi ya sakata hilo.
Katika mkutano wake na wanahabari, Spika Ndugai alimtaka CAG Prof. Mussa Assad kufika mbele ya kamati ya maadili leo Januari 21, jijini Dodoma na kufafanua juu ya kauli yake ya 'Udhaifu wa Bunge', jambo ambalo Spika alidai ni kulidhalilisha Bunge.

CAG alitumia neno “udhaifu” wa Bunge alipokuwa akieleza sababu za kutofanyiwa kazi kwa ripoti zake ambazo zimekuwa zikibainisha ufisadi.

Wakati hayo yakiendelea, Ndugai amesitisha kufanya kazi na ofisi ya CAG na kuwatawanya wajumbe wa kamati mbili; ya Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na kuongeza nguvu kwenye kamati nyingine wakati huu ambao zitakuwa hazina majukumu.

PAC na LAAC zinazoongozwa na wenyeviti kutoka vyama vya upinzani, ndizo zimekuwa zikifanyia kazi ripoti za CAG na ratiba ya awali ya Bunge ilionyesha kamati hizo zingetakiwa zikijadili ripoti ya sasa.

Hata hivyo, Januari 17, Profesa Assad aliita waandishi wa habari na kueleza nia yake ya kwenda mbele ya Kamati ya Maadili, akieleza kusikitishwa na jinsi kauli yake ilivyozua mjadala na kutia doa uhusiano baina ya ofisi yake na Bunge.

Mbali na kukubali wito huo CAG, amesema kauli yake haikulenga kulidhalilisha Bunge na kwamba neno udhaifu ni la kawaida hasa kwenye kada hiyo ya ukaguzi na amekuwa akilitumia hata katika ripoti zake.

CAG Assad aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, Desemba Mosi mwaka 2014 ameitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa wakati alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa (UN) akiwa New York, Marekani alikokuwa akihudhuria mkutano.
Chanzo: Eatv
Share:

KAULI YA LISSU KUVULIWA UBUNGE, CHADEMA WASHANGAZWA NA SPIKA

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeamua kuingilia kati kufuatia kauli ya Spika wa Bunge wa Job Ndugai kusema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu lissu anaweza kuondolewa Ubunge wake kufuatia kiongozi huyo kufanya ziara nchini Uingereza bila kibali cha Spika.

Akizungumzia kauli hiyo ya Spika Ndugai, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi na Mambo ya Nje wa CHADEMA John Mrema amesema kauli ya Spika haina tija kwa kuwa Tundu Lissu bado hajapewa ruhusa na Daktari wake kurejea nchini kwa madai kuwa amepona kabisa.

Mrema amesema, "Spika si Daktari mpaka aseme kuwa Lissu amepona na hajawahi kumtembelea kwa kipindi chote tokea apelekwe hospitali. Tunakumbuka aliyewahi kuwa waziri wakati wa serikali ya awamu ya nne, Prof. Mwandosya aliugua kwa zaidi ya mwaka, lakini hatukusikia kauli za aina hii."
 
Akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari jana, Spika Ndugai alimtaka Mbunge Tundu Lissu huyo kurejea nchini ili kuendelea na shughuli za Bunge kwa kuwa hana kibali cha kuwa nje ya nchi.

Spika Ndugai aliongeza Lissu hana ruhusa ya kuwa nje ya Bunge, hivyo anatakiwa kurejea nchini kuendelea na shughuli za ubunge.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger