Saturday, 19 January 2019

KASEJA KUMPIKU MANULA STARS

Mlinda mlango mkongwe nchini Juma Kaseja, amekuwa kwenye kiwango bora siku za hivi karibuni, akiiongoza KMC kukaa katika nafasi ya 3 kwenye ligi kuu soka Tanzania bara, baada ya kutoruhusu kufungwa bao katika mechi 3 mfululizo.

Ubora wa Kaseja ulionekana alipoiongoza timu yake kushinda mabao 2-0 dhidi ya African Lyon kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya JKT Tanzania na kumaliza mechi tatu mfululizo bila kufungwa waliposhinda 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

Katika mchezo wa 4 Kaseja aliruhusu mabao 2 huku timu yake ikishinda mabao 5-2 dhidi ya Coastal Union ya Tanga. Hivyo mkongwe huyo aliyewahi kuzichezea Simba na Yanga kukamilisha dakika 360 za kucheza lakini akiwa ameruhusu mabao 2 pekee.

KMC sasa ipo juu ya Simba ikiwa na alama 34 katika nafasi ya 3 na Simba wakiwa na alama 33 katika nafasi ya 4. KMC wamecheza mechi 22 huku Simba wakiwa wamecheza mechi 14.

Kaseja mwenyewe amewahi kuweka wazi  kuwa bado ana mpango wa kuichezea timu ya taifa na kwa kiwango chake cha sasa huenda ikawa ni miongoni mwa machaguo ya Emmanuel Amunike.

Endapo Kaseja ataitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars, atakumbana na upinzani mkali kutoka kwa mlinda mlango namba moja wa Simba na Stars Aishi Manula ambaye naye anafanya vizuri na klabu yake.

Share:

Rais Magufuli: Changamoto Zilizopo Sasa Zisipotatuliwa, Sidhani Kama Ajaye Atazitatua

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema hana uhakika endapo mrithi wake ataweza kutekeleza mambo anayoyafanya katika uongozi huu wa awamu ya tano.

Magufuli ameyasema hayo jana  Ijumaa Januari 18, 2019 katika hafla ya makabidhiano ya mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Alisema katika safari ya kutatua changamoto anakutana na magumu mengi na ndiyo maana amekuwa akihitaji nguvu za Mungu kutekeleza majukumu yake.

“Viongozi wa dini endeleeni kuliweka Taifa hili kwenye mikono ya Mungu. Hii ni vita kama ilivyo nyingine na vita ya uchumi inahitaji maombi sana, bila maombi kazi hii haiwezi kufanyika,” alisema.

“Hao wanaokaa gizani hauwezi kujua ana kisu, ana panga au ameweka nyoka mfukoni lakini huko gizani huwa wanatolewa kwa maombi, yatawapumbaza huko gizani wasitake kufanya walichokusudia.”

Alisema kufanya hivyo kutawafanya viongozi wa nchi kusimamia misingi ya uadilifu na upendo wa kweli katika kulitumikia Taifa tajiri, lenye changamoto nyingi zinazohitaji kutatuliwa.


from MPEKUZI http://bit.ly/2R0Ug7A
via Malunde
Share:

Zitto Kabwe Adai Kutishiwa Kuuawa Dodoma .....Amwandikia Barua Spika wa Bunge




from MPEKUZI http://bit.ly/2VWjGHc
via Malunde
Share:

Kigwangalla Aivunja Bodi ya Utalii (TTB)

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amevunja bodi ya wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuanzia jana Ijumaa na kutoa miezi mitatu kwa menejimenti kujirekebisha kinyume na hapo ataifumua.

Waziri huyo ametangaza kuunda bodi mpya ya wakurugenzi ambayo itakuwa na wajumbe vijana watakaokwenda na kasi katika kazi hiyo ya kutangaza vivutio.

Dk Kigwangalla amefikia uamuzi huo kwa kile alichoeleza kuwa TTB imeshindwa kutekeleza maelekezo yake yenye lengo la kutangaza vivutio vya utalii.

Akitoa uamuzi huo jana Ijumaa Januari 18, 2019 mbele ya waandishi wa habari Dk Kigwangalla ameeleza kutotangazwa kwa vivutio vya utalii kunaifanya Serikali inyooshewe kidole na kuonekana haifanyi kazi.

Amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja ametoa maelekezo zaidi ya 15 lakini hayajafanyiwa kazi jambo linalosababisha yeye kutukanwa.

“Serikali ikitukanwa kwenye sekta ya maliasili na utalii maana yake natukanwa mimi naonekana sitoshi kwenye nafasi hii, “ amesema Dk Kigwangalla.

Miongoni mwa maelekezo ambayo hayajafanyiwa kaiz ni pamoja na TTB kutoweka mabango ya kutangaza utalii katika miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)

Jingine ni kushindwa kuwatumia watu maarufu na wasanii kutangaza vivutio vya utalii, kushindwa kutangaza vivutio kwenye michezo, kutotengenezwa kwa video na filamu fupi zinazojumuisha vivutio na nyingine nyingi.


from MPEKUZI http://bit.ly/2RVOg4C
via Malunde
Share:

Alichokisema Zitto Kabwe Baada ya Spika Ndugai Kusema Anamuumiza Sana Kichwa

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe amesema kuwa si kweli kwamba yeye ndiye Mbunge anayemsumbua zaidi Spika Job Ndugai kama alivyodai kwani amekuwa akifuata taratibu na kanuni bila kuvunja sheria.

Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo ametoa kauli hiyo  baada ya kuulizwa kuhusu maoni yake kufuatia kauli ya Spika aliyoitoa jana akidai kuwa Zitto ni mbunge anayempa tabu kutokana na kauli zake.

"Sijui kwanini Spika amesema vile kwani mimi simpi tabu, nasimamia haki na Spika afuate kanuni tu”, amesema Zitto.
 
Januari 17 katika mkutano wake na wanahabari, Spika Ndugai amesema amekuwa akishindwa kumfukuza bungeni mbunge huyo wa Kigoma Mjini kwa kuwa ndiye pekee anayekiwakilisha chama cha ACT- Wazalendo.

"Ni kweli Zitto Kabwe ananisumbua sana lakini, ukisema umtoe Bungeni unawaza mtu mwenyewe yuko peke yake ukimsimamisha atawakilishwa na nani?. Unamuacha tu lakini wale wengine nafukuza tu maana wako wengi akikosekana kwenye mjadala atawakilishwa na wenzake, hebu nisaidieni Zitto nimfanyeje?, alihoji Spika Ndugai.


from MPEKUZI http://bit.ly/2FBmDYH
via Malunde
Share:

TEKNOLOJIA MPYA KUWASAIDIA VIZIWI KUENDESHA TAXI

Mji mkuu wa Korea Kusini umepata madereva wa kwanza wa teksi viziwi wiki hii, kwa msaada wa teknolojia ambayo imezinduliwa ya kupunguza unyanyapaa wa kuwaajiri watu walio na ulemavu huo.

Kulingana na mtandao wa habari wa Korean Times, dereva wawili viziwi walianza kusafirisha abiria kwenye mji mkuu wiki hii wakisaidiwa na teknolojia iliyoundwa na kampuni mpya ya Coactus.

Akielezea jinsi teknolojia hiyo inafanya kazia mtandao wa Yonhap unasema kuwa vifaa hivyo vimewekwa viti vva mbele na nyuma vya teksi na vimeunganishwa na kampuni kampuni za teksi za Goyohan au silent Taxi.

Teknolojia hiyo inawezesha mawasiliano ya sauti na ujumbe ulioandikwa kuwasaidia abiria kuelezea maeneo wanataka kwenda na mifumo ambayo wangependa kutumia kulipa.

Iliundwa na kundi la wanafunzi mjini humo na kuongozwa na mwanafunzi aliyefuzu na taalumaa ya uandisi Song Min-pyo.Haki miliki ya pichaGOYOHAN TAXIImage captionMkurugenzi mkuu Song Min-pyo

"Tulitaka kuwapa watu viziwi ajira zaidi," Bw Song aliliambia gazeti la Korea Times.

"Tulijua kuwa wakorea watatoka nje ya gari ikiwa dereva ataanza kuwasiliana akitumia simu na kalamu kwa hivyo tukaunda teknolojia hii.'

Yonhap anasema kuwa Coactus itapunguza unyanyapaa unaowakumba madereva visiwi nchini Korea Kusini.

Watu 255,000 wana matatizo ya kusikia nchini Korea Kusini kwa mujibu wa wizara ya afya.
Chanzo : Bbc
Share:

Wanne Watiwa Mbaroni Jijini Arusha kwa Kutengeneza Fedha Bandia

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limewakamata watuhumiwa sita kwa makosa mbalimbali.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ramadhani Ng'anzi amesema jana Ijumaa Januari 18, 2019 kuwa watuhumiwa wanne ambao hakuwataja majina yao kwa sababu za kipelelezi wanajihusisha na utengenezaji wa fedha bandia.

Amesema mtuhumiwa wa kwanza alikutwa na noti bandia za dola za Marekani  zenye thamani ya dola 500 (zaidi ya Sh 1.1 milioni).

"Huyu mtuhumiwa wa kwanza aliwapeleka askari wetu nyumbani kwake eneo la Daraja Mbili ambako zilikutwa fedha bandia za mataifa mbalimbali," alisema Ng'anzi

Fedha hizo ni dola za Marekani, fedha za Umoja wa Ulaya (Euro), Kenya, Malawi, Zambia, Rwanda na Sudan.

Alisema watuhumiwa wanashikiliwa kwa ajili ya mahojiano na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, Ng'anzi amesema kuwa watuhumiwa wengine wawili ambao ni Kennedy Mbilinyi na Richard Loishiye wamekamatwa kwa kuiba gari aina Harrier lenye namba za usaili T 241 DKC na kujaribu kulivusha mpaka wa Namanga kuelekea nchi jirani ya Kenya.


from MPEKUZI http://bit.ly/2FJALhU
via Malunde
Share:

Sekta ya Afya Nchini Yaendelea Kukua Kwa Kasi

Na WAMJW – DOM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Sekta ya Afya nchini yaendelea kukua kwa kasi, kutokana na Serikali kuendelea kuboresha Huduma kwa Wananchi zikiwemo upatikanaji wa Dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi, huduma za chanjo, huduma za afya ya uzazi na mtoto na Huduma za Dharura.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akitoa tamko mbele ya Waandishi wa Habari na baadhi ya viongozi wa Wizara, kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018, katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema kuwa Katika mwaka 2018, jumla ya wajawazito 2,086, 930 walihudhuria na kuandikishwa Kliniki, ikilinganishwa na wajawazito 2,009,879 Mwaka 2017, huku mwongozo wa utoaji huduma za afya ya uzazi na mtoto unaelekeza wajawazito kuanza huduma mapema kabla ya majuma 12 ya ujauzito na kuhudhuria kliniki angalau mara nne katika kipindi cha ujauzito.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa, Katika kipindi cha mwaka 2018 jumla ya watoto 1,568,832 walizaliwa ikilinganishwa na Watoto 1,498,488 mwaka 2017, huku wakipatiwa huduma mbalimbali za chanjo ili kuzuia magonjwa yanayowaathiri Watoto ikiwemo ugonjwa Kupooza, Kuharisha, Pepopunda, Pneumonia, homa ya ini na Surua.

“Katika kipindi cha mwaka 2018 hali ya chanjo kwa Watoto nchini imeendelea kuwa katika kiwango cha juu zaidi ya asilimia 85 ya kiwango kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani kama inavyoonyeshaa katik hapa chini” Alisema Waziri Ummy.

Hata hivyo nWaziri Ummy amesema mwaka 2018 kumetokea jumla ya vifo 20,087 ikilinganishwa na vifo 19,693 mwaka 2017, huku Katika kipindi cha miaka yote miwili 2017 na 2018, homa ya mapafu imeongoza kwa kusababisha vifo, ambapo kwa mwaka 2017, imechangia asilimia 18.2 ya vifo vyote na mwaka 2018 imechangia kwa asilimia 12.9 ya vifo vyote.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa Mwaka 2018, ugonjwa usio wa kuambukiza (shinikizo la damu) umejitokeza katika magonjwa 10 yanayoongoza kwa kusababisha vifo ambapo umechangia vifo kwa asilimia 1.9 ya vifo vyote.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa Hali ya upatikanaji wa Dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini imeendelea kuimarika, hii ni kutokana na Serikali kuongeza bajeti ya dawa kutoka Shilingi Milioni 31 mwaka 2015/16 hadi kufikia Shilingi milioni 251 mwaka 2016/17 na Shilingi 270 mwaka 2018/19.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa hali ya upatikanaji wa Damu Salama ambapo katika kipindi cha mwaka 2018, huku jumla ya chupa za damu salama 307,835 sawa na asilimia 85.5 ya lengo zilikusanywa ikilinganishwa na chupa 233,933 mwaka 2017, huku akiwahasa Wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kuendelea kuokoa maisha ya wahitaji.

“Chupa zote 307,835 zilizokusanywa zilipimwa makundi ya damu pamoja na magonjwa makuu manne ambayo ni Ukimwi (HIV,) Homa ya Ini B na C (HBV, HCV) na Kaswende (Syphilis). Jumla ya chupa 262,283 sawa na asilimia 85.3 zilikuwa salama na kusambazwa katika hospitali kwa ajili ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.” Alisema Waziri Ummy.

Hata hivyo Waziri Ummy amesema kuwa, katika mwaka 2018 jumla watu 47,967 waligundulika kuwa na vijidudu vya Kifua kikuu ikilinganishwa na wagonjwa 44,714 waliogunduliwa mwaka 2017., huku akisisitiza kuwa tatizo la ugonjwa wa Kifua Kikuu limeendelea kuwepo takribani mikoa yote nchini.

kwa upande mwingine, Waziri Ummya amesema kuwa, hadi kufikia Desemba 2018, jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya vilifikia 7,768 kutoka vituo 7,435 mwaka 2017 sawa na ongezeko la vituo 333 kwa mwaka, amedai kuwa Serikali ilikuwa inamiliki asilimia 71 ya vituo vya kutolea huduma; Mashirika ya dini asilimia 12, Taasisi za Serikali asilimia 3 na vituo binafisi asilimia 15.

Sambamba na hilo, waziri Ummy amesema kuwa, hadi kufikia Desemba mwaka 2018, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulikuwa na jumla ya wanachama 899,654 na ikihudumia jumla ya wanufaika 4,219,192 sawa na asilimia 8 ya Watanzania wote.


from MPEKUZI http://bit.ly/2ROM4vV
via Malunde
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya January 19




from MPEKUZI http://bit.ly/2MjZ4Et
via Malunde
Share:

Kilosa Wataka Mabwawa Kupunguza Athari Za Mafuriko

Wilaya ya Kilosa imekuwa ikiathiriwa na mafuriko ya mara kwa mara kutokana na  mvua nyingi zinazonyesha nchini na kusababisha kujaa kwa maji katika mito mikubwa inayopita katika wilaya hiyo ambayo ni mto Mkondoa na Mkundi. Kutokana na hali hiyo Kamati ya Wilaya ya Usimamizi ya Maafa Kilosa imeliomba Baraza la Taifa la Usimamizi wa Maafa kuzielekeza wizara za kisekta kukamilisha mpango wa kufufua na kujenga mabwawa wilayani humo, ili kupunguza kasi ya maji yanayo jaa katika mito hiyo.

Akiongea wilayani Kilosa wakati wa kufuatilia hatua za urejeshaji hali kutokana na athari za maafa ya mafuriko yaliyotokana na mvua zilizonyesha, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe ameeleza kuwa wamelipokea ombi hilo ambalo ni muhimu kutekelezwa kwa ajili ya kupunguza athari za maafa wilayani humo.

“Mvua zinaponyesha na tukawa na utaratibu mzuri wa kuyavuna maji hayo, matokeo ya mvua hizo huwa zinachochea shughuli za maendeleo hasa kilimo, lakini bila kuyavuna maji yanaweza kusababisha maafa kama  mafuriko. Kwa kulitambua hili, tutaratibu wizara husika kuhakikisha mabwawa yanafufuliwa ili kuhifadhi maji na kupunguza maji mengi yanayoingia mto Mkondoa” Alisisitiza Kanali, Matamwe.

Kanali Matamwe amewataka wananchi wa kilosa kutoendeleza shughuli za kibinadamu kando ya mto huo kutokana na kuwa serikali imetumia gharama kubwa za kujenga tuta la mto Mkondoa kwa lengo la kupunguza athari za maafa yaliyokuwa yanatokea baada ya mto huo kujaa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Wilaya ya Maafa Bw. Asajile Mwambambale, amefafanua kuwa ipo haja ya kuharakisha ujenzi wa bwawa  la Kidete ili kuweza kupunguza kasi ya maji ma wingi wa maji yanayo ingia mto Mkondoa, ambapo athari zake za mafuriko huathiri watu, mali na miundombinu ya Kilosa.

“Pamoja na kuwa tungependa utafiti wa kina ufanyike kuanzia kwenye chanzo cha mto Mkondoa  ili kuweza kuelewa tabia ya mto huu, niliombe Baraza la Taifa la Usimamizi wa maafa, litusaidie kuzielekeza hizi wizara za kisekta, ikiwemo wizara ya maji, zikamilishe mipango ya kufufua  na kujenga mabwawa ambayo yatasaidia kuhifadhi maji na kupunguza wingi wa maji yanaoyoingia katika mto Mkondoa” alisema Mwambambale.

Mwambambale amefafanua kuwa wilaya ya kilosa imeendelea kutekeleza mpango wa Kujiandaa na Kukabiliana na mafuriko kwa kutoa mchanga kwenye mto Mkondoana Mkundi, ili kuongeza kina cha mito hiyo. Pia zoezi la Upandaji wa miti na matete kando ya  mto Mkondoa limefanyika. Aidha Kamati za maafa za kata na vijiji pamoja na timu za uokoaji na kutoa misaada kwa waathirika wakati wa maafa zimejengewa uwezo.

Wilaya ya Kilosa ni miongoni mwa wilaya 7 za mkoa wa Morogoro ambayo imekuwa ikiathiriwa na mafuriko ya mara kwa mara kutokana na mvua zinazonyesha mikoa ya jirani ya Dodoma na Manyara hususani Wilaya za Mpwapwa, Kongwa na Kiteto, maji ya mvua hizo hupita wilayani Kilosa kupitia mto Mkondoa na Mkundi.


from MPEKUZI http://bit.ly/2S0zB8a
via Malunde
Share:

NewVideo : MR. BLUE FT NANDY-BLUE

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ,Kherry Sameer Rajab a.k.a Mr. Blue ameachia wimbo wake wa kwanza kwa  mwaka 2019  aliomshirikisha Nandy  wimbo huo unaitwa "BLUE"

Utazame hapa chini
Share:

Friday, 18 January 2019

WATENDAJI KATA NJOMBE WAKALIA KUTI KAVU, DC APIGILIA MSUMALI MZAZI ALIYECHANGISHWA DAWATI AKALICHUKUE

Na Amiri kilagalila Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri ameapa kupambana na kiongozi yeyote atakayediriki kumchangisha mzazi fedha ya dawati kama walivyochangishwa baadhi ya wazazi katika shule ya secondari Maheve pamoja na shule ya Secondari Mabatini zilizopo katika halmashauri ya mji wa Njombe. Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo ofisini kwake mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa utaratibu wa kufuata waraka wa elimu bure uko pale pale, hivyo swala la kumchangisha mzazi dawati ni kinyume na maagizo ya serikali na endapo kutakuwa na ulazima wa kuchangisha mchango…

Source

Share:

Waziri Mkuu Majaliwa Akagua Eneo Itakapojengwa Hospitali Ya Uhuru Katika Kijiji Cha Maduma Wilayani Chamwino

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua eneo la ujenzi wa hospitali ya Uhuru lenye ukubwa wa ekari 109 lililoko katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

 Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Maduma wilayani humo leo mchana (Ijumaa, Januari 18, 2019), Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Serikali ya kijiji hicho wa kutenga maeneo ya maendeleo ni wa kupigiwa mfano na vijiji vya maeneo mengine.

 “Uamuzi wenu wa kutenga maeneo ya miradi ya maendeleo umekuwa na tija, ndiyo maana Mheshimiwa Rais Magufuli aliposema ijengwe hospitali, hamkupata shida sababu eneo tayari lilikuwepo. Ninawapongeza wazee waliojitolea maeneo yao ili kuongeza kwenye eneo la hospitali,” amesema.

 Wazee waliotoa maeneo yao ni Mzee Meshack Njamasi (ekari 5.50), Mzee Jobu Malogo (ekari 3.50) na Bw. Nehemia Mwikwi (ekari 4.50). Ekari 95.5 zilizobakia, zimetolewa na Seriakli ya kijiji hicho.

 Waziri Mkuu aliwataka wakazi wa wilaya ya Chamwino wasibweteke bali wajipange na kila mmoja ajipange kufanya kazi kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa akihimiza. “Ujenzi wa mji wa Serikali unaoendelea hivi sasa ni fursa kwenu. Na ujio wa hospitali hii ni fursa nyingine kwa wana-Chamwino hasa kwa vile ujenzi wake utatumia mfumo wa force account ambao unatoa fursa kwa wanajamii kushiriki kazi za miradi ya eneo husika,” amesema.

 Waziri Mkuu amesema ujenzi wa hospitali hiyo yenye hadhi ya wilaya ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayoelekeza wananchi wapatiwe huduma za matibabu huko huko waliko. “Hadi sasa tumeshajenga vituo vya afya 350 ili kusogeza huduma kwa wananchi na jumla ya hospitali za wilaya 67, zinajengwa nchi nzima kwa mwaka huu,” amesema.

 Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wakazi wa vijiji jirani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Bw. Selemani Jafo alisema eneo la ujenzi wa hospitali hiyo liko umbali wa kilometa mbili kutoka barabara kuu ya Dar es Salaaam-Dodoma na kilometa tatu kutoka Ikulu ya Chamwino.

Naye, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine aliwataka wakazi hao wachangamkie fursa hiyo kwa kusomba mawe, mchango, maji na kwamba Kamati za usimamizi wa ujenzi zitapaswa kusimamiwa na wanakijiji.

 Aliwataka wakazi hao wasiishie kwenye lengo la kuwa na hospitali ya wilaya, bali walenge kujenga hospitali yenye hadhi ya mkoa kwa kadri bajeti itakavyoruhusu.

 Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Bilinith Mahenge alisema ujenzi wa hospitali hiyo ni wa hadhi ya wilaya ikiwa na nyongeza ya huduma za wagonjwa wa dharura na wagonjwa mahututi (Emergency Department and Critical Care Unit).

 Alimshukru Rais Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa hospitali hiyo sh. milioni 995.18 ambazo zilipaswa kutumika kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru, Desemba 9, mwaka jana. “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutuongezea kiasi kingine cha fedha cha sh. bilioni 2.35 na kutufanya sasa tuwe na sh. bilioni 3.22 za ujenzi huo,” alisema.


from MPEKUZI http://bit.ly/2Hk9MMo
via Malunde
Share:

Spika Ndugai amhakikishia Rais Magufuli kuwa Bunge si dhaifu

 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa Bunge lake si dhaifu kama alivyosema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu na Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.

Spika Ndugai ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 18, 2019 katika hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) iliyofanyika katika ofisi za Mamlaka ya Udhibiti wan Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo baada ya kuombwa na Rais Magufuli, Spika Ndugai amesema utekelezaji wa mradi huo ulitegemea sana maoni ya wabunge kabla ya kupitisha fedha hivyo ni ishara kuwa Bunge si dhaifu kwa sababu wamefanikisha suala hilo.

“Wakati bajeti hiyo inapitishwa kulikuwa na mjadala mkali kwa sababu wabunge walikuwa wanahitaji kujua kwa nini kodi inayotokana na matumzi ya simu ni ndogo kuliko idadi ya watumiaji wa simu.”

“Ilibidi tutengeneze sheria, hatukufaulu lakini ulipoingia madarakani ukasema jambo hili lirudishwe bungeni lifanyiwe kazi, ukasaini na hiki ndicho kilichotokea,” amesema Spika Ndugai

Amesema jambo hilo si dogo kwa wasiolewa na badala yake watu wanapenda giza hivyo mtambo huo ni tochi utakaoweza kumulika kuangalia sehemu ambayo haionekani vizuri na wasiopenda mwanga ni watu wenye pesa.


from MPEKUZI http://bit.ly/2T6xg9m
via Malunde
Share:

Waziri Mkuu Atoa Maagizo 14 Kuharakisha Ujenzi Wa Mji Wa Serikali

*Awataka Makatibu Wakuu wasimamie upandaji miti, maua
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa mji wa Serikali na kutoa maagizo 14 ambayo yataharakisha kukamilika kwa kazi hiyo.

 Ametoa maagizo hayo jana (Alhamisi, Januari 16, 2019) mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi za wizara zote pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika eneo la Ihumwa lililoko km. 17 kutoka jijini Dodoma.

 Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa tenki la maji lenye ujazo wa lita milioni moja, Waziri Mkuu alisema pamoja na spidi anayoihimiza, bado wakandarasi wanapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia ubora unaotakiwa (quality).

 “Kazi ya ujenzi ikamilike tarehe 31 Januari 2019 kwa kasi na viwango vyenye ubora; mifumo ya ICT, umeme na maji izingatiwe wakati wa ujenzi na zile sites zenye upungufu wa nguvu kazi, vijana waongezwe na kazi ifanyike mchana na usiku,” alisema.

 Aliwataka waratibu wa zoezi la Serikali kuhamia Dodoma wakiwemo Wizara husika na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wahakikishe kuwa wakandarasi ambao hawajalipwa hususan vikosi vya ujenzi wanaojenga jengo la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wanalipwa.

 Waziri Mkuu aliwataka Makatibu Wakuu wote wasimamie upandaji miti, maua (hata landscaping) kwenye maeneo waliyopewa hasa katika kipindi hiki cha mvua ili mandhari za ofisi zianze kuvutia.

 “Wizara zifanye usafi ndani na nje wakati ujenzi ukiendelea. Wizara kwa kushirikiana na TFS (Wakala wa Misitu) waendelee na zoezi la upandaji miti na wataalam wa bustani wahusishwe mapema wakati huu wa ujenzi. Lakini ninawaagiza Makatibu Wakuu wasimamie kwa karibu suala hili kwa sababu eneo kubwa liko chini ya ofisi zao, hawa wakandarasi wakimaliza ujenzi watabomoa mabati na kusafisha eneo la ujenzi tu,” alisema

 Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameagiza Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wahakikishe wanafungua ofisi ya muda katika Mji wa Serikali ili kurahisisha usimamizi wa miundombinu inayowahusu.

 Ametumia fursa hiyo kuwataka Wakala wa Majengo nchini (TBA) wawasilishe taarifa ya maendeleo ya ujenzi kwa kila Wizara kwa kila hatua inayoendelea.

 Alisema ununuzi wa vifaa vya ujenzi kwenye wizara mbalimbali hususan wakati wa ukamilishaji ujenzi, havina budi kununuliwa mapema na vile vinavyounganishwa kama vile chuma za kenchi vifanyike kwenye eneo la ujenzi (sites) ili vikaguliwe na TBA.

 Kuhusu majengo ya ofisi ambayo kasi yake inasuasua kama vile TAMISEMI, Madini na baadhi ya sites za Mzinga Holdings, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka Mawaziri na Makatibu Wakuu wachukue hatua stahiki kusimamia ujenzi na kushauri ipasavyo.

 Amesema wakandarasi kama Mzinga, SUMA JKT na NHC waangalie namna ya kuwapa ajira za kudumu hususan zinazohusiana na ujenzi mafundi wanaoshiriki shughuli za ujenzi Ihumwa.

 Pia aliwataka Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kushirikiana na Wizara husika wahakikishe barabara za mji wa Serikali zinatengenezwa angalau kwa kiwango cha changarawe ili zipitike kwa urahisi katika kipindi cha mpito wakati taratibu za kudumu za kuweka lami zikiendelea.

 Ili kuokoa muda, Waziri Mkuu aliwataka wakandarasi wahakikishe kazi zisizo za masharti kama vile kusuka nondo zitekelezwe kwa pamoja wakati wa shughuli za ujenzi wa ujumla zikiendelea.

 Akihitimisha, Waziri Mkuu alisema Ofisi ya Waziri Mkuu ipatiwe taarifa ya idadi ya ajira iliyotengenezwa kutokana na ujenzi wa mji wa Serikali hususan za wale ambao hawana ajira za kudumu kwa wakandarasi wanaotekeleza ujenzi huo.

 Waziri Mkuu ameahidi kurudi Ihumwa Januari 31, mwaka huu ili akapokee funguo za ofisi za wizara zote.

 Mapema, akitoa taarifa ya ujenzi huo, Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma, Bw. Meshack Bandawe alisema ujenzi wa tenki la maji lenye ujazo wa lita milioni umegharimu sh. bilioni 3.6 na uko kwenye hatua za mwisho.

 “Jiji la Dodoma lina ziada ya maji ya lita za ujazo milioni 13.5, na kwa upande wa umeme, kuna ziada ya megawati 20 kwa sababu uwezo wa kuzalisha umeme ni megawati 48 na zinazotumika hadi sasa ni megawati 28 tu,” alisema.


from MPEKUZI http://bit.ly/2RyMebf
via Malunde
Share:

WAJASIRIAMALI NJOMBE WAPEWA DARASA KUFIKIA MAFANIKIO.

Na, Amiri kilagalila Wajasiriamali Mkoani Njombe wametakiwa kuzingatia kanuni za Kibiashara ikiwemo kulinda Mitaji yao ili kuhakikisha Mitaji inabaki salama bila kufilisika kutokana na Wajasiliamari wengi kufanya kazi Bila kuzingatia kanuni za Kibiashara na Mwisho hujikuta wamefilisika. Rai hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la General Bussness Company Limited Alexander Malya jana januari 17 alipokuwa akitoa Mafunzo ya Ujasiriamali katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe kwa baadhi ya wakazi Mjini Njombe ambapo amesema kuwa wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa wakishindwa kukua kutokana na Kutofuata kanuni za Kibiashara. Pamoja…

Source

Share:

Waziri Mkuu Aitaka Bodi Ya Pamba Ifanye Kazi Karibu Na Wakuu Wa Mikoa

*Ataka viongozi wote wasimamie kilimo hicho
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Bodi ya Pamba ifanye kazi kwa karibu na Wakuu wa Mikoa ili kuhakikisha msimu huu zao hilo linafikia malengo ya uzalishaji.

 Ametoa agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Januari 18, 2019) wakati akizungumza na Wakuu wa mikoa nane ya Mara, Mwanza, Simiyu, Geita, Kagera, Shinyanga, Singida na Tabora inayolima pamba pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga.

 Waziri Mkuu ameendesha kikao hicho kwa njia ya video (video conference) kutokea ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma ili aweze kupata picha halisi ya kilimo cha pamba na hatua zilizofikiwa hadi sasa katika msimu huu wa kilimo.

 “Lego letu mwaka huu 2019 ni kuzalisha tani zisizopungua 600,000. Wote mmeeleza kuwa wakulima wako kazini, pamba inalimwa, mnachosubiria ni dawa za kuuza wadudu waharibifu, na Bodi imeeleza kuhusu upatikanaji wa dawa hizo.”

 Waziri Mkuu pia amesema viongozi wote wanapaswa kuwa karibu na wakulima ili waweze kubaini shida zao na kuzitatua kwa haraka. “Viongozi wote huko tuliko, zaidi ya asilimia 75 ya wa wananchi wetu ni wakulima. Kwa hiyo basi, tunapaswa tutenge asilimia zaidi ya 50 ya muda wa wetu kwenye mpango kazi ili tuweze kusimamia kilimo,” amesema.

 “Wakuu wa mikoa peke yenu hamuwezi kufika kila mahali. Ni lazima maafisa ugani, maafisa kilimo na maafisa ushirika kwenye Halmashauri zetu waende kwa wakulima. Nikisema viongozi siyo Wakuu wa Mikoa na Wilaya peke yao, Wizara nayo ina jukumu la kusimamia, viongozi wa AMCOS, vyama vikuu vya ushirika wote wawajibike kushirikiana na Serikali, waangilie ni nini tufanye ili kumkomboa mkulima.”

“Warajis wasaidizi, Ma-Ras wasaidizi wanaohusika na kilimo ni lazima washirikane kuhakikisha wakulima wetu wanajikwamua kutoka hapo walipo,” amesisitiza.

 Mapema, akitoa taarifa ya maandilizi ya kilimo cha pamba kwa msimu huu, Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba alisema hadi sasa wamekwishasambaza tani 27,000 za mbegu ambao ni zaidi ya asilimia 37 ikilinganishwa na usambazaji wa mbegu wa msimu uliopita.

 “Hadi sasa mikoa yote imepata mbegu na zimeshapandwa na hali ya uotaji ni asilimia 100 kwani hatujapata malalamiko yoyote,” alisema.

 Kuhusu dawa za viuadudu, Mkurugenzi huyo alisema wameshanunua chupa milioni sasa na vinyunyizi 23,000.

 Wakichangia mjadala kwenye kikao hicho, kwa nyakati tofauti, Wakuu hao wa mikoa waliunga mkono dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya kufufua ushirika kama njia pekee ya kumkomboa mkulima.

 Walisema kuna haja ya kutafuta njia mbadala ya kuwatoa wakulima wa pamba kwenye utegemezi wa mikopo ili waweze kupata mbegu na pembejeo na badala yake wapewe elimu ya kujiwekea akiba tangu wanapovuna na lkuuza mazao yao.


from MPEKUZI http://bit.ly/2DgUsMk
via Malunde
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger