Wednesday, 16 January 2019

WAZIRI MKUU UINGEREZA KUKABILIWA NA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NAYE

Wabunge wa Uingereza Jumanne waliyakataa pakubwa makubaliano ya Waziri Mkuu Theresa May na Umoja wa Ulaya kuhusu Uingereza kujiondoa kutoka kwenye Umoja huo, jambo lililouvuruga mchakato wa Brexit.

Hatua hiyo imepelekea kura isiyokuwa na imani kuwasilishwa, hatua ambayo inaweza kuiangusha serikali ya May. Wabunge walioyapinga makubaliano hayo ni 432 huku walioyaunga mkono wakiwa 202 pekee.

 Kushindwa kwa Waziri Mkuu huyo kulitarajiwa na wengi ingawa kiasi cha kura alizoshindwa nazo ni jambo ambalo limeuharibu uongozi wake unaosuwasuwa.

Kushindwa huku ni kwa kihistoria kwa kuwa ndiyo mara ya kwanza kwa serikali kushindwa kwa kiasi kikubwa cha kura katika bunge la Uingereza na kunafuatia msukosuko wa kisiasa wa zaidi ya miaka miwili ambapo May alijiwekea hadhi ya kisiasa kwa kuhakikisha amepata makubaliano ya Brexit. 

Jeremy Corbyn aliwasilisha mswada wa kutokuwa na imani na serikali ya May

Muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na spika John Bercow Waziri Mkuu May, alizungumza.

Chanzo:Dw
Share:

MAGAIDI WALIOSHAMBULIA NAIROBI WAUAWA

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema  oparesheni ya kukabiliana na washukiwa wa ugaidi waliovamia hoteli ya Dusit2 mjini Nairobi imekamilika na kwamba washambuliaji wote wameangamizwa.

Watu waliyokuwa wamejihami kwa silaha siku ya Jumanne walivamia jengo la hoteli ya kifahari ya Dusir2 katika eneo la Westlands katika jiji kuu la Nairobi nchini Kenya na kuwaua watu 14.

Awali maafisa walitangaza kuwa oparesheni hiyo ilikamilika saa kadhaa baada ya shambulio hilo lakini mlilio ya risasi na milipuko ilisikika mapema alfajiri ya leo (Jumatano)


Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabab, limedai kuhusika na shambulio.

Haijabainika ni washambuliaji wangapi walihusika na shambulio hilo.

Akihutubia taifa kwa moja kwa moja kupitia televisheni kutoka Ikulu, rais Kenyatta amesema kuwa watu 14 waliuawa katika shambulio hilo na wengine 700 kuokolewa kutoka jengo hilo.

Shirika la msalaba mwekundu hata hivyo limeripoti kuwa waliyofariki katika mkasa huo ni watu 24.

Raia wa Marekani ni miongoni mwa waliyofariki, imesema wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Raia mmoja wa Uingereza pia anahofiwa kufariki dunia.

Chanzo:Bbc
Share:

DC NJOMBE AAGIZA KUSHUSHWA VYEO AFISA ELIMU,MRATIBU ELIMU KATA YA RAMADHANI

Na Amiri kilagalila Mkuu wa Wilaya ya NJOMBE RUTH MSAFIRI ameagiza kushushwa vyeo afisa elimu kata ya Ramadhani ESTER MJUJULU, Mratibu Elimu wa kata hiyo HURUMA MGEYEKWA pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari MAHEVE, VALENO KITALIKA kwa Tuhuma za kuwatoza wazazi michango ya madawati kiasi cha shilingi Elfu Thelathini. Hayo yameibuka wakati Mkuu wa wilaya ya Njombe alipokuwa akikagua ujenzi wa madarasa yanayojengwa kwa ajili ya kidato cha kwanza Katika Shule hiyo ambapo amesema kitendo hicho ni kinyume na maelekezo ya Rais JOHN MAGUFULI ya kukataza watendaji kuchangisha michango…

Source

Share:

MAKAMANDA WA POLISI MIKOA MITATU WATENGULIWA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametengua uteuzi wa makamanda wa polisi wa mikoa mitatu; Salum Hamduni (Ilala), Emmanuel Lukula (Temeke) na Ramadhani Ng’azi (Arusha). Ametangaza uamuzi huo leo Jumatano Januari 16, 2019, katika mkutano na waandishi wa habari akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya kushauriana na vyombo anavyoviongoza. Amesema sababu za kutengua uteuzi wa kamanda wa Ilala na Temeke ni kushindwa kusimamia mianya ya rushwa na utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa. Pia, amemuagiza katibu mkuu wa wizara yake kuunda kamati ambayo itapewa miezi mitatu kuchunguza vitendo…

Source

Share:

MAKAMBA AITA NEMC KUIGA UTENDAJI WA TFS

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira ) Mhe. January Makamba ameitaka bodi ya NEMC kuiga utendaji kazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Makamba aliyasema hayo wakati akimkabidhi rasmi vitendea kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo mara baada ya kuzindua Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere mapema siku ya jana Prof. Silayo ni miongoni mwa wajumbe nane walioteuliwa kuunda bodi…

Source

Share:

UMOJA WA AFRIKA NA MAREKANI WALAANI SHAMBULIZI LA NAIROBI

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat amelaani vikali shambulio la Hoteli ya kifahari ya DusitD2 jijini Nairobi.


Katika taarifa yake, Faki amevisifu vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwa kuchukua hatua za uokozi wa raia na kupambana na wahalifu mapema iwezekanavyo. Pia amesema tukio hilo linaonesha umuhimu wa kupitia upya mipango ya kuongeza nguvu ya kupambana na vikundi vya kigaidi barani Afrika.

Mwenyekiti wa Kamisheni anathibitisha utayari wa AU kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na Nchi Wanachama katika kupambana na visa vya ugaidi pamoja na harakati za kutuliza hali nchini Somalia na mapambano dhidi ya kundi al-Shabaab kupitia vikosi vyake vya AMISOM.

Balozi wa Marekani anayemaliza muda wake nchini Kenya Bw Robert Godec ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa Marekani inashutumu vikali shambulio hilo.


Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa raia wake mmoja ni kati ya watu waliopoteza maisha kwenya mkasa huo.

Chanzo:Bbc
Share:

KANGI LUGOLA ATUMBUA MAKAMANDA WA POLISI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametengua uteuzi wa makamanda wa polisi wa mikoa mitatu; Salum Hamduni (Ilala), Emmanuel Lukula (Temeke) na Ramadhani Ng'azi (Arusha).

Ametangaza uamuzi wake huo leo Jumatano Januari 16, 2019, katika mkutano na waandishi wa habari akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya kushauriana na vyombo anavyoviongoza.

Amesema sababu za kutengua uteuzi wa kamanda wa Ilala na Temeke ni kushindwa kusimamia mianya ya rushwa na utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa.

Pia, amemuagiza katibu mkuu wa wizara yake kuunda kamati ambayo itapewa miezi mitatu kuchunguza vitendo vya rushwa akitaka mkazo uwekwe zaidi kwa askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani.

Waziri huyo amemtaka Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslimukujitafakari na kujipima kama anatosha katika nafasi hiyo.


Na Sharon Sauwa, Mwananchi
Share:

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMATANO 16.01.2019

Manchester United wamekubali kumuuza kiungo wao wa kati, mbelgiji Marouane Fellaini, 31, kwa kima cha euro milioni 15 mwezi huu.

Tayari vilabu vya AC Milan, Porto na Guangzhou Evergrande ya Uchina vimeonesha nia ya kutaka kumsajili. (Mirror)

Chelsea wanatarajiwa kuendelea mbeli na mpango wao wa kumsajili mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, ambaye yuko kwa mkopo AC Milan, kufikia mwisho wa wiki hii. (Telegraph)

Meneja wa AC Milan Gennaro Gattuso amesema kuwa Higuain hajamwambia kuwa anataka kuondoka klabu hiyo. (Evening Standard)

Christian Eriksen, 26,huenda akatia saini mkataba mpya na Tottenham, wakati ambapo Real Madrid pia inapigiwa upatu kumsajili kiungo huyo wa kati raia wa Denmark. (AS)

Chanzo:Bbc
Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO JANUARI 16,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 16, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

MILIPUKO NA MILIO YA RISASI YASIKIKA JIJINI NAIROBI, MAGARI YACHOMWA MOTO,WENGI WAJERUHIWA.

Na,Jovine Sosthenes. Taharuki iliibuka jana mjini Nairobi kufuatia shambulio la milipuko na risasi inayosadikiwa kufanywa na magaidi katika eneo la 14 Riverside Drive, katika Hoteli ya Dusit D2 jijini Nairobi, Kenya na kusababisha vifo vya watu watano na kujeruhi wengine tisa. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya, Shambulio hilo linadaiwa kutokea Januari 15,2019. Mda, saa 9 alasiri na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa huku magari manne yakichomwa moto na milio ya risasi ikidaiwa kusikika kutoka eneo la tukio. Bado wahusika wa shambulio hilo hawajajulikana lakini askari wa Kitengo cha…

Source

Share:

Tuesday, 15 January 2019

KAMPUNI YA GURU,MANISPAA YA ILALA WAANDAA TAMASHA KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA

Na Heri Shaban,Dar es salaam. Kampuni ya Guru Planet Kwa kushirikiana na manispaa ya Ilala wanatarajia kufanya tamasha la wajasiriamali January 29 Mwaka huu. Tamasha hilo linatarajia kufanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja wilayani Ilala jijini Dar es Salam ambapo wajasiliamali watapata fursa mbalimbali. Akizungumza Dar es Salam leo mkurugenzi wa kampuni ya Guru Planet Nickson Martin alisema tamasha hilo wameshirikiana na Idara ya maendeleo ya jamii manispaa Ilala dhumuni la tamasha hilo kuwapa fursa Wajasiriamali waweze kutangaza biashara zao na kubadilishana uzoefu. “Katika tamasha hili litakuwa siku tatu mgeni…

Source

Share:

TZS 94.01 BILLIONS ZAKUSANYWA NA HESLB KATI YA JULAI– DESEMBA, 2018

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imekusanya jumla ya TZS 94.01 bilioni kutoka kwa wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu katika kipindi cha Julai – Desemba, 2018 na kuvuka lengo lake la kukusanya TZS 71.4 bilioni katika kipindi hicho. Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema leo jijini Dar es salaam kuwa makusanyo hayo yametoka kwa jumla ya wanufaika zaidi 198,659 ambao wamejiari au kuajiriwa katika sekta binafsi na umma. Wanufaika waliobainika na kuanza kulipa kati ya Julai – Disemba 2018 “Katika kipindi hicho cha…

Source

Share:

MKUU WA WILAYA AWAFUKUZA UKUMBINI MKURUGENZI , MWENYEKITI WA HALMASHAURI


Uamuzi wa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kuwaondoa ukumbini mkurugenzi na mwenyekiti wa halmashauri ya Hai waliokuwa wakiongoza kikao cha kamati ya fedha umezua taharuki kwa viongozi hao.

Mkurugenzi huyo, Yohana Sintoo na mwenyekiti, Helga Mchomvu na wajumbe wengine waliondolewa katika ukumbi huo huku mkuu huyo wa wilaya akiingia na watu wengine kwa ajili ya kutumia ukumbi huo.

Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi leo jioni Jumanne Januari 15, 2019, Sabaya amesema aliwaondoa akiwataka kutumia ukumbi mwingine.

Amesema kikao hicho kilikuwa na wajumbe 10, aliwataka kuhamia ukumbi mdogo ili yeye ahudumie zaidi ya wamachinga 200 walioomba ukumbi huo mkubwa mapema.

Akisimulia tukio hilo leo, Mchomvu amesema kitendo hicho hakipaswi kufanywa na kiongozi huyo wa Serikali.

“Tulikuwa na kikao cha kamati ya fedha katika ukumbi wa Halmashauri. Tumeanza tangu saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana. Aliingia mkuu wa wilaya na kututaka kutoka nje ya ukumbi na kuamuru waliokuwa naye nje ya ukumbi huo, kuingia ndani,” amesema.
Na Janeth Joseph, Mwananchi
Share:

YANGA WAIBUTUA MWADUI 3-1

Nahodha wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu anaanza na rekodi yake leo katika mchezo wake wa kwanza akiwa amevaa kitambaa cha unahodha baada ya kufunga bao la kwanza katika mchezo wao wa ligi dhidi ya Mwadui Uwanja wa Taifa.

Ajibu amefanikiwa kuandika bao hilo baada ya kupiga faulo akiwa nje ya 18 dakika ya 12 ikamshinda mlinda mlango na kuzama moja kwa moja langoni.

Dakika ya 18 Yanga walipata penati baada ya Tambwe kuchezewa rafu eneo la hatari ila Penalti hiyo ilipigwa na Ajibu iliokolewa na mlinda mlango wa Mwadui Anold Masawe.

Dakika 39 Ajibu alimpa pasi ya bao Amiss Tambwe akamalizia kwa kichwa na kipindi cha pili dakika ya 57 Fei Toto anafunga bao la tatu akimalizia pasi ya Ajibu.

Dakika ya 82 Mwadu wanapata bao la kufutia machozi kupitia kwa Salum Aiyee akimalizia pasi ya Ditram Nchimbi.
Share:

RAIS MAGUFULI ASITISHA ZOEZI LA KUONDOA VIJIJI NDANI YA MAENEO YA HIFADHI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kusitishwa mara moja kwa zoezi la kuviondoa vijiji na vitongoji vinavyodaiwa kuwepo katika maeneo ya hifadhi na amewataka viongozi wa wizara zote zinazohusika kukutana ili kubainisha na kuanza mchakato wa kurasimisha maeneo ya vijiji na vitongoji hivyo. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 15 Januari, 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamis Kigwangallah, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.…

Source

Share:

MAGAIDI WASHAMBULIA HOTELI YA KIFAHARI KENYA



Milipuko na milio ya risasi yasikika katika eneo la 14 Riverside, Nairobi
Milipuko miwili mikubwa ya risasi ilisikika na baadaye ufyatuaji wa risasi.
Share:

UKOSEFU WA DAMU HOSPITAL YA NYERERE DDH BADO NI KITENDAWILI.

Na,Mwandishi Wetu. Hospitali Teule ya Nyerere wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara inakabiliwa na uhaba wa damu kutokana na kasi ndogo ya uchangiaji na ongezeko la matumizi kwa wajawazito na watoto wachanga. Mratibu wa kitengo cha Damu Salama Mwita Kisaka alisema kwa mwezi wanatumia ziadi ya Unit 100 za damu,matumizi ambayo hayawiani na kasi ya kuchangia hali ambayo inawalazimu wanaohitaji kuleta ndugu zao. Akitoa ufafanuzi mbele ya kikundi cha Ujamaa na Ujilani Mwema Serengeti (Kichaumwese)kinachoundwa na vyama vyote vya siasa waliochangia unit 10 za damu ,alisema vikundi mbalimbali ikiwemo Vikoba…

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger