Tuesday, 15 January 2019

POLISI SONGWE: DEREVA HAKUPIGWA NA TRAFIC WATATU..WALIKUWA WANAMDHIBITI.

Na, Mwandishi wetu. Jeshi la Polisi mkoani Songwe limeeleza sababu ya Askari wa usalama barabarani kusuguana na dereva, kuwa alitumia lugha ya matusi na kutotii amri ya kumtaka atoe ushirikiano kwa wanausalama hao ambao walikuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana na maofisa toka Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra). Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Songwe, Yusuph Sarungi amewaambia waandishi wa habari jana Jumatatu Januari 14, 2019 kuwa tukio hilo lilitokea siku ya Jumamosi Januari 12, 2019 saa 2:30 asubuhi katika eneo la Transforma, halmashauri ya mji wa Tunduma wilayani…

Source

Share:

TETESI ZA SOKA ULAYA JAN 15,2019

Chelsea itaomba £100 kwa Eden Hazard kujiunga na Real Madrid,
Chelsea itaomba £100m iwapo mchezaji raia wa Ubelgiji Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 28, ataiambia klabu kwamba anataka kujiunga na Real Madrid. (Telegraph)

Meneja wa Arsenal Unai Emery anaridhia kumruhusu mchezaji wa Ujerumani Mesut Ozil, mwenye umri wa miaka 30, kuondoka katika klabu hiyo ili kuweza kuwasajili wachezaji wawili wapya. Kwa sasa Ozil ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi Arsenal katika mkataba wenye thamani ya £350,000 kwa wiki. (Mail)

Mshambuliaji wa West Ham raia wa Austria Marko Arnautovic, mwenye umri wa miaka 29, atakamilisha uhamisho wa thamani ya £35m kwenda katika timu ya ligi kuu ya China Shanghai SIPG kabla ya mwisho wa wiki. (Sun)

Hammers itamlenga mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson, mwenye umri wa miaka 26, iwapo watamruhusu Arnautovic kuondoka mwezi huu. (Sky Sports)

Sevilla imevunjika moyo kumsajili mshambuliaji wa Chelsea raia wa Uhispania Alvaro Morata, mwenye umri wa miaka 26, kutokana na gharama yake kubwa, na baada ya kukataliwa pendekezo lao la thamani ya £40m. (Evening Standard)

Morata yu tayari kupokea kato la mapato ili kujiunga na Atletico Madrid, itakayohitaji kumuuza mchezaji mwingine ili kuweza kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid. (Marca)Alvaro Morata alijitosa katika soka ya kimataifa mnamo 2014

Wachezaji wa Manchester United wanaendelea kushinikiza meneja wa mpito Ole Gunnar Solskjaer apewe mkataba wa kudumu mwishoni mwa msimu. (Telegraph)

Solskjaer anataka kumuondoa Marouane Fellaini na huenda akamruhusu mchezaji huyo wa kiungo cha kati mwenye miaka 31 raia wa Ubelgiji aondoke kwa mkopo mwezi huu Januari. (Talksport)

Kocha huyo raia wa Norway ameshauriana na meneja wa zamani Sir Alex Ferguson kuhusu uteuzi wa timu tangu apokee mikoba kutoka kwa meneja aliyefutwa kazi Jose Mourinho. (Manchester Evening News)

Chelsea wamekubali makubaliano binafsi na mchezaji wa kiungo cha kati raia wa Argentina Leandro Paredes, aliye na miaka 24, na wamewasilisha ombi la thamani ya £27m kwa Zenit St Petersburg. (Mirror)
Share:

MBUNGE WA CHADEMA AMPIGIA NGOMA NDOGO YA URAIS TUNDU LISSU.

Na Bakari Chijumba, Mtwara. Wakati Mbunge wa Singinda Mashariki, Tundu Lissu akitua nchini Uingereza kwa ajili ya ziara yake bara la Ulaya hiyo jana, Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Jesca Kishoa amesema zawadi pekee ambayo Watanzania wanaweza kumpa Lissu ni kumuunga mkono katika ndoto zake za kugombea urais mwaka 2020. Kishoa ametoa kauli hiyo jana Januari 14, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali kuhusu afya na maendeleo ya Lissu. “Zawadi pekee ambayo watanzania wanaweza kumpa Tundu Lissu ni kumuunga mkono katika ndoto zake…

Source

Share:

MWEKEZAJI KUTOKA KOREA KUSINI AMEAHIDI KUJENGA KITUO CHA AFYA KATIKA KIJIJI CHA KAZINGATI WILAYANI NGARA.

Ngara. Na mwandishi wetu Mwekezaji huyo Kim Won Dae ametoa ahadi hiyo jana alipokuwa akitembelea eneo atakalowekeza kilimo cha kahawa na mpunga na kujenga kiwanda cha kukoboa na kusaga zao hilo kisha kujenga kiwanda cha mbolea. Akizungumza kwa niaba ya mwekezaji huyo mwekezaji mzawa kutoka kampuni ya Amri Karim kutoka Amiry Karim Co.Tanzania Ltd amesema kituo hicho kitajengwa kwa thamani ya Sh250 milioni za Kitanzani “Malengo ya mwekezaji ni kutoa huduma kwa wakazi wa kazingati na maeneo jirani lakini pia itasaidia kuwapatia matibabu wafanyakazi watakaokuwa katika miradi itakayoanzishwa” Amesema Karim…

Source

Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO JANUARI 15,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 15, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

NACTE: March-Application Window 2019 Now Open

NACTE: March-Application Window 2019

The National Council for Technical Education (NACTE) is a corporate body established by the National Council for Technical Education Act, 1997 (Act No. 9 of 1997). The Act provides a legal framework for the Council to coordinate provision of technical education and training and establish an efficient national qualifications system that will ensure that products from technical institutions are of high quality and respond to changing needs as well as technological innovations in the world.

NACTE: March-Application Window 2019

The post NACTE: March-Application Window 2019 Now Open appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

NACTE how to apply for diploma or certificate programs via NACTE or any Training Institution for 2018/19 acamic year

If you are form four or Form six leaver and you are interested in studying diploma or certificate programs in a public or private collage, you must complete the Online Application on NACTE Admission Verification System or apply directly to the Training Institution in . 
The NACTE 2018–19 Online application system is now open. You should fill out the online application forms as soon as possible on the official NACTE site OR institution site,

READ ALSO :NACTE : list of institutions allowed to admit new students for Health and Allied Sciences programmes

It’ll be easier to complete your application process if you are aware of some important issues and gather what you need ahead of time. Below is everything you need to do before attempting to apply and how to apply for Certificate and Diploma programs.

Carefully Read the NACTE admission guidebook for the Category/Profession you wish to apply.

The Admission Guidebook (Guidebook) is meant to provide the applicants with basic information on matters related to the entire process of admissions through the Central Admission System. The Guidebook indicates the programmes offered in each institution as approved by NACTE. 
In addition, it indicates the minimum entry requirements, institutional capacity, fee structure for each programme
Applicants are therefore, strongly advised to read the Admissions Guidebook before they start lodging their applications in order to know exactly requirement of programmes they wish to apply, it is highly recommended to carefully read admission guidebook

DOWNLOAD: NACTE 2017/18 admission guidebooks Compiled Full PDF Download 

All the admission guide books for Health and allied sciences (including community health, health records etc) programmes, Teacher education programmes, Administration, Business, Law, Planning, Social Work, Community Development, Tourism and related Programmes, Agriculture, Livestock, Engineering, ICT, Computer Science and other related Sciences Programmes are available here download it here

READ ALSO :NACTE :PUBLIC NOTICE FOR MARCH/APRIL INTAKE, 2018 ADMISSION CYCLE FOR ACADEMIC YEAR 2017/2018 FOR HEALTH AND ALLIED SCIENCES PROGRAMMES

Prepare your Application fee (Nonrefundable):

It is important to pay Application fee first in order to get M-pesa confirmation code, the application fees for this academic year are as in following categories: –
For Certificate/Diploma and Higher Diploma in Health and Allied Sciences (Including Community Health, Health Records etc): – TShs 10,000/= Per Institution Which shall be paid through M-PESA
All applicants are advised to keep in safe place their confirmation number from Vodacom M-PESA payment for future reference (For Online or NOAVAS applicants)

Prepare the following things Before initializing the application process

It is important to gather the following particulars before initializing the application process,
  • Valid Phone Number, Valid and Working Email Address, for receiving your login password and other important updates
  • Payment M-pesa Confirmation Code (For NOVAS applicants)
  • Your form four /form six index number

Start your registration:

Soon After paying application fee you will be able to apply for any category you want, you can start your application process by making a self-registration through NOAVS. Where you will be required enter your initial qualification details. Follow the below link to proceed;
  • If this is your first time click here to start your application.
  • If you are already registered please click here
You can also send your application directly to the training institution, Here is a full list of institutions allowed to admit new students for Health and Allied Sciences programmes

Qualifications Overview

You must be holder of Ordinary Certificate of Secondary Education (CSEE) or its equivalent recognized by NECTA, or National Vocational Award (NVA) 3 from VETA or its equivalent recognized by VETA or General Certificate of Engineering(GCE) from NECTA or Certificate of Education Under Mpango wa MUKA.
For other privante Training Institutions you are advised to visit their websites for more info on how to apply or you can check the list of institutions allowed to admit new students for Health and Allied Sciences programmes for more details

IMPORTANT

Remember that you are advised to read carefully the admission requirements of each programme you anticipate to apply in the guidebook before initializing the application process in order to avoid problems that may arise due to failure to follow appropriate instructions.
Please don’t forget to share this great article with your colleagues, if you have any doubt or opinion just let us know by commenting on the box below

© bango magazine

PLEASE DONT MISS THIS

The post NACTE how to apply for diploma or certificate programs via NACTE or any Training Institution for 2018/19 acamic year appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

NACTE public notice about admission requirement for various courses

Share:

Monday, 14 January 2019

TRUMP KUIANGAMIZA UTURUKI

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia ‘kuiangamiza Uturuki kiuchumi’ iwapo taifa hilo litawashambuliwa vikosi vya wakurdi nchini Syria baada ya wanajeshi wa Marekani kuondoka Syria. Katika ujumbe wake alioutuma kwenye mtandaoi wa kijamii Twitter, Trump amesema hakutaka Wakurdi kwa upande wao nao pia waichokoza Uturuki. Vikosi vya Marekani vimepambana kwa ushirikiano na wanamgambo wa Kikurdi kaskazini mwa Syria dhidi ya kundi la Islamic State (IS). Rais Recep Tayyip Erdogan amezungumza kwa hasira kuhusu Marekani kuliunga mkono kundi hilo, na kuapa kuliangamiza. Kauli ya Trump Jumapili inafuata shutumza zaidi dhidi ya…

Source

Share:

Picha:KANISA LA P.A.G.T LATOA MSAADA KWA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KISHAPU

Na  Malaki Philipo- Malunde 1 blog
Kanisa la Pentekoste Assemblise of God Tanzania (P.A.G.T) limetoa msaada wa nguo na vifaa vya shule kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kata ya mwadui lohumbo Wilayani Kishapu. 

Msaada huo umekabidhiwa wakati wa ibada maalumu ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu iliyofanyika jumapili Januari 13,2019 . 

Akikabidhi msaada huo Askofu wa kanisa la P.A.G.T Nyenze Mchungaji Robert Joseph ameiomba jamii pamoja na taasisi zisizo za kiserikali kuunga mkono juhudi za serikali kutoa misaada mbalimbali kwenye jamii, pia utoaji ni agizo la mungu linaloashiria upendo kwa wahitaji. 

“sababu Mungu anatupenda wote hivyo yatupasa kuwasaidia wahitaji na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuwasaidia wanyonge,” alisema Joseph. 

Akizungumza kwenye ibada hiyo kaimu afisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Kishapu Ndola Masunga ambaye amemuwakilisha mkuu wa wilaya kishapu Nyabaganga Talaba amewapongeza walezi ambao wamechukua jukumu la ulezi bila manyanyaso kwa watoto . 

“Tunashuhudia kwenye ofisi zetu za maendeleo ya jamii vihoja vingi vya kuwanyanyasa watoto wanaoishi mazingira magumu,niwapongeze walezi waliochukua jukumu la kuwalea watoto bila ya kuwanyanyasa na kuwapatia mahitaji muhimu,” alisema Ndola. 

Kanisa hilo limetoa msaada wa nguo na vifaa vya shule kwa wanafunzi wanaoishi mazingira magumu lengo ikiwa ni kuwasaidia wazazi na walezi , diwani wa kata ya Masengwa Nicodemas Simon amesema msaada huo ni chachu ya kufanya vizuri kimasomo kwa wanafunzi hao.
 Askofu wa kanisa la P.A.G.T Nyenze Mchungaji Robert Joseph ameiomba jamii pamoja na taasisi zisizo za kiserikali kuunga mkono juhudi za serikali kutoa misaada mbalimbali kwenye jamii yenye wahitaji.. Picha zote na Steve Kanyefu-Malunde 1 blog
 Kaimu Afisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Kishapu Ndola Masunga ambaye amemuwakilisha mkuu wa wilaya kishapu Nyabaganga Talaba  amewapongeza walezi ambao wamechukua jukumu la ulezi bila manyanyaso kwa watoto . 
Diwani wa Kata ya Masengwa Nicodemas Simon akisisitiza juu ya umuhimu wa  msaada huo huku akisema kuwa msaada  ni chachu ya kufanya vizuri kimasomo kwa wanafunzi hao.
      Baadhi ya watoto waliopatiwa msaada wakiwa kanisani  .

Mgeni rasmi kaimu afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Kishapu Ndola Masunga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba Akikabidhi msaada kwa watoto hao. 

Zoezi la kukabidhi msaada huo likiendelea
 Baadhi ya Wazazi/walezi wa watoto hao wakifuiatilia kwa umakini zoezi la utolewaji msaada kwa watoto hao


Share:

DE GEA KWA KIWANGO HICHO BADO SAANA-SOLSKJAER

David de Gea huenda akajijengea hadhi ya kuwa mlinda lango bora zaidi kuwahi kuichezea klabu ya Manchester United hasa baada ya ustadi wake Jumapili, kwa mujibu wa kaimu meneja wao Ole Gunnar Solskjaer. Mhispania huyo mwenye miaka, 28, aliokoa mipira 11 na kuwawezesha United kuwalaza Tottenham 1-0 katika mechi iliyochezewa uwnaja wa Wembley. Katika miaka 11 aliyokuwa Old Trafford akiwa mshambuliaji, Solskjaer alicheza na magolikipa stadi kama vile Edwin van der Sar na Peter Schmeichel. “Tumekuwa na magolikipa wazuri sana katika klabu hii na nafikiri kwa sasa anawatishia wote wawili…

Source

Share:

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA UPINZANI TANZANIA

Mahakama nchini Tanzania imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na vyama vya upinzani nchini humo kupinga Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018. Shauri hilo, lilifunguliwa na muungano wa vyama 10 vya upinzani wakidai unakiuka haki za Kikatiba za kisiasa kwa kuzifanya shughuli mbalimbali za kisiasa kuwa jinai. Wanasiasa hao wanadai muswada huo unampa mamlaka makubwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuingilia mambo ya ndani ya vyama hivyo ikiwemo uchaguzi wa viongozi na kusimamisha uanachama kwa wanachama wa vyama hivyo. Pia walikuwa wanapinga kifungu cha…

Source

Share:

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 15.01.2019: WILSON, AKE, LLORENTE, NEVES, ARNAUTOVIC, BABEL

Bournemouth iko radhi kumuuza mshambuliaji wa England Callum Wilson kwa Chelsea kwa pauni £75m – mara 25 zaidi ya kiwango walicholipa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mnamo 2014. (Star) Wolves watapambana na Chelsea katika kuwania kumsajili Wilson, ambaye amefunga mabao 10 kufikia sasa msimu huu.(Birmingham Mail) Chelsea pia inataka kumsajili upya beki wa kati wa Bournemouth Nathan Ake, miaka miwili tu baada ya kumuuza Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa Cherries. (Sun) Mshambuliaji wa Tottenham na timu ya taifa ya Uhipania Fernando Llorente, mwenye umri…

Source

Share:

DC KIZIGO AWAKARIBISHA WWF NAMTUMBO..ASEMA ELIMU YA UHIFADHI INAHITAJIKA KWA WANANCHI.

Na Bakari Chijumba, Mtwara Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,Sophia Kizigo amelipongeza Shirika la kimataifa la utunzaji wa mazingira (WWF), kwa elimu ya uhifadhi wanayoendelea kuitoa huku akiwaomba kujikita zaidi kutoa elimu vijijini hasa kwa kuwatumia watendaji wa vijiji ambao watasambaza taarifa kwa haraka. Bi.Kizigo, ametoa kauli hiyo wakati Wafanyakazi wa WWF, walipotembelea ofisi yake kujadili miradi ya pamoja wanayoweza kufanya na wilaya ya Namtumbo katika mwaka huu wa 2019 ili kuboresha uhifadhi. “Mnaweza kuandaa semina ya watendaji wote wa vijiji, mukawapa elimu ya kutosha wakasambaza kwa wanavijiji, mie…

Source

Share:

MRADI WA MAJI WAMLAZA NDANI MHANDISI WA MAJI.

Na Allawi Kaboyo-Kagera. Naibu waziri wa maji Jumaa Aweso amemuagiza kamanda wa polisi wilaya ya Muleba kumkamata mhadisi wa maji wilayani humo Boniface Lukoho na kuagiza kutafutwa kwa mkandarasi M/S SAGUCK ENGINEERING baada ya kukagua mradi wa maji Katoke ulioanza kujengwa novemba 2013 na kutakiwa kukamilika mei 2014, wenye thamani ya shilingi milioni 467 na zaidi ya shilingi milioni 400 zikiwa zimeshalipwa huku mradi huo ukiwa hautoi maji. Naibu waziri Jumaa Aweso akiwa katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Kagera, amefika wilayani Muleba katika mradi wa maji Katoke na kuwakuta…

Source

Share:

VYAMA VYA SIASA VYAALIKWA KUTOA MAONI MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA.

Na,Mwandishi wetu. Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria inatarajia kukutana na wawakilishi wa vyama vya siasa Januari 19 na 20, 2019 kuwasikiliza na kupokea maoni yao kuhusu muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018. Kamati hiyo itapokea maoni yao baada ya kumaliza vikao vyake na wadau wengine vitakavyofanyika Januari 17 na 18, 2019 mjini Dodoma kuhusu muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2018 na kufuatiwa na mkutano wake na wawakilishi wa kila chama cha siasa chenye usajili wa…

Source

Share:

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMPA MIMBA DADA YAKE



Picha haihusiani na habari hapa chini

Gabriel Nyantori (25) amefikishwa mbele ya mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti mkoani Mara akituhumiwa kwa makosa ya kuzini na dada yake na kumpa mimba.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile, mwendesha mashitaka, Faru Mayengela leo Jumatatu Januari 14, 2019 amesema mshitakiwa anakabiliwa na makosa mawili.

Amesema kosa la kwanza ni kuzini na dada yake mwenye umri wa miaka (16) mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Kibeyo na kosa la pili ni kumpa mimba dada yake, makosa ambayo aliyatenda Aprili 30, 2018 nyumbani kwao, Kibeyo.


Na Anthony Mayunga, Mwananchi
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger