Sunday, 6 January 2019

UKIMSHIKA HAPA AUNT EZEKIEL USHAMMALIZA

SUPASTAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel, amesema kama unataka kumjua upande wake wa pili wa shilingi, jaribu kuyafuatilia mapenzi yake na mzazi mwenzake, Moses Iyobo ambaye ni dansa wa kutegemewa katika Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), utakiona cha mtemakuni. “Hivi kwa nini uhangaike kuyajua maisha yangu na mpenzi wangu? Leo tumegombana au tumepatana au tunaelekea kuachana, inakuhusu nini wewe? Maana hata tulivyoanza uhusiano watu walishtukizia tuko kwenye uhusiano hivyo hata kama tukiachana wataona hivyohivyo,” alisema wakati akizungumza na Ijumaa hivi karibuni. Aliongeza: “Nimekuwa nikisikia minon’gono mingi kuhusu kuachana…

Source

Share:

ALIKIBA KWENYE TUHUMA NZITO ZA WIZI

Msanii mkonge wa muziki wa Bongo Fleva, Domo Kaya amesema kuwa wasanii wapya kwenye muziki huo wanatakiwa kuwa wabunifu, baada ya msanii Alikiba kutumia kidokezo ‘Yebaba’ ambacho alikuwa alikitumia yeye mwanzo. Domo Kaya amefunguka hayo kupitia FRIDAY NIGHT LIVE ya EATV, ambapo amesema kuwa Alikiba kutumia neno hilo sio vibaya lakini alitakiwa kuomba ruhusa kwanza kwake. “Nawasihi wadogo zetu kuwa wabunifu, na kuacha ujanja ujanja maana kutumia kitu hukatazwi lakini uombe kwa muhusika akupe baraka zake”, amesema Domo Kaya. Hivi karibuni msanii Alikiba ameonesha kutumia msemo huo ‘yebaba’ katika wimbo…

Source

Share:

MWANAMKE AKIKUJIBU HIVI,KIMBIA HARAKA

Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu. KWA MFANO: 1. Ukimtumia sms ”Mambo mpenzi wangu?” akikujibu ”mambo mabaya”, usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ”sina hela dear” 2. Ukimtumia sms ”Maisha yanasemaje kipenzi changu” akikujibu ”maisha magumu hubby wangu we acha tu” usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ”nimefulia mwenzio kama nini sijui” 3. Ukimtumia sms ”Mbona…

Source

Share:

DIWANI WA CCM AVAMIWA KWA SHOKA NA NONDO KAHAMA


Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao

Diwani wa kata ya Sabasabini halmashauri ya wilaya ya Ushetu wilayani Kahama Emmanuel Makashi (49) kupitia Chama Cha Mapinduzi amenusurika kifo baada ya watu wasiofahamika kuvunja nyumba yake kwa shoka na nondo na kumjeruhi kichwani na mkononi na kufanikiwa kupora shilingi milioni 5.


Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Januari 3,2019 majira ya saa saba kamili usiku katika kijiji cha Ifunde, kata ya Mpunze, tarafa ya Dakama, wilaya ya Kipolisi Ushetu na mkoa wa Shinyanga.

Kamanda Abwao amesema watu watatu wasiofahamika walivunja nyumba ya Emmanuel Makashi diwani wa kata ya Sabasabini kwa kutumia shoka na nondo kisha kuiba pesa zinazokadiriwa kuwa ni Tshs 5,000,000/=.

"Katika kupambana na wahalifu hao,diwani huyo alipata michubuko kichwani na mikononi na kutibiwa katika hospitali ya Halmashauri Mji wa Kahama na hali yake inaendelea vizuri",ameeleza. 

Amesema chanzo cha tukio hilo ni kuwania mali.

“Aidha, mmoja kati ya wahalifu hao aitwaye Yohana Masanja (19) mkazi wa kijiji cha Lowa alikamatwa na kuuawa kwa kuchomwa moto na wananchi waliojichukulia sheria mkononi, Juhudi za kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa wengine waliohusika na tukio zinaendelea”,amesema  Kamanda Abwao.

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog

Share:

DKT. BASHIRU ASHAURI WAKUU WA MIKOA KUJIFUNZA SIMIYU

  Na Stella Kalinga, Simiyu Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewashauri Wakuu wa Mikoa hapa nchini kwenda(kuja) kujifunza namna ya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kati ya Chama na Serikali sambamba na ubunifu na uchapakazi wa viongozi wa mkoa huo.   Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali, Mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.   Dkt. Bashiru amewapongeza Viongozi wa Serikali wakingozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,…

Source

Share:

DKT. BASHIRU ASHAURI WAKUU WA MIKOA KUJIFUNZA SIMIYU

  Na Stella Kalinga, Simiyu Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewashauri Wakuu wa Mikoa hapa nchini kwenda(kuja) kujifunza namna ya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kati ya Chama na Serikali sambamba na ubunifu na uchapakazi wa viongozi wa mkoa huo.   Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali, Mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.   Dkt. Bashiru amewapongeza Viongozi wa Serikali wakingozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,…

Source

Share:

Video Mpya ya asili 2019 : NCHAINA MADIRISHA - MASAMVA


Msanii wa nyimbo za asili Ng'wana Nchaina 'Nchaina Madirisha' kutoka Kahama mkoani Shinyanga anatualika kutazama video yake mpya kabisa mwaka 2019 inaitwa Masamva...

Tazama video hii hapa chini
Share:

MGOGORO WA UUZAJI VIWANJA VYA KKKT WAMFIKISHA LUKUVI NJOMBE

Na Maiko Luoga Njombe. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.Willium Lukuvi Amewataka Watumishi wa Wizara hiyo Nchini kuwafikia Wananchi Katika Maeneo yao Ili kutatua Kero zinazowakabili Ikiwemo Kumaliza Migogoro ya Ardhi Inayowakabili Wananchi Kote nchini. Waziri Lukuvi Ametoa Agizo hilo Mapema Hii leo katika Ukumbi wa Turbo Njombe Mjini wakati Akizungumza na Mamia ya Wananchi waliojitokeza katika Ukumbi huo na Kuwasilisha Kero zao Kupitia Program ya Funguka kwa Waziri Ambapo Baada ya Kuona Kero nyingi za Wananchi wa Njombe zaidi ya 300 Ndipo Mh. Lukuvi Aliamua kutoa…

Source

Share:

DKT. BASHIRU AWAONYA VIONGOZI WALIOANZA KUTAFUTA UBUNGE KABLA YA WAKATI.

  Na Stella Kalinga, Simiyu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpinduzi (CCM) Taifa Dkt. Bashiru Ally amewaonya baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, na Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma, ambao wameanza kukaa vikao kwa ajili ya kutafuta majimbo kabla ya wakati wa Chama hicho kutangaza mchakato wa kutafuta wagombea wapya wa ubunge na udiwani.   Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali katika wilaya…

Source

Share:

MABULA AMFAGILIA MHE. MAGUFULI KWA KASI YA UTENDAJI WA TARURA KWENYE MIRADI 10 INAYOGHARIMU BI. 5.8

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula amempongeza Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa uanzishwaji wa Wakala wa barabara Mjini na Vijijini TARURA ambacho kimekuwa chapa halisi ya ukombozi kwenye sekta ya miundombinu ya barabara Wilayani Nyamagana kwa kutekeleza miradi 10 yenye thamani ya shilingi 5,822,854,934.00 kwa kasi na kiwango katika mwaka wa fedha 2018 hadi 2019. Mhe. Mabula akiwa ameambatana na Mjumbe kamati ya siasa CCM wilaya ya Nyamagana ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya Mhe. Witness Makale walilakiwa na mwenyeji wao Meneja TARURA wilaya ya Nyamagana Mhandisi…

Source

Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO JANUARI 06,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 5, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.  

Source

Share:

Saturday, 5 January 2019

MATINGA: UTAFITI KUONGEZA TIJA NA UZALISHAJI WA MADINI KWA WACHIMBAJI WADOGO

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga amewataka wachimbaji wadogo kuachana na kutafuta na kuchimba madini kimazoea badala yake wafuate njia ya kisayansi katika kutafuta, kuchimba na kuchenjua madini katika maeneo yao ili kuongeza tija, pato lao na Taifa kwa ujumla. Aliyasema hayo Disemba 4 wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wachimbaji wadogo eneo la D reef na Kapanda Mkaoni Katavi, na kuongeza kuwa, masuala ya madini ni ya kisayansi na hivyo kuwataka wachimbaji wadogo kuondoa dhana mbaya iliyojengeka kwa…

Source

Share:

WAKO WAPI YANGA WALE WA KUTOFUNGWA?,WANALAMBALAMBA WAWALAMBISHA MAGOLI 3.

  NA KAROLI VINSENT. MAJANGA kwa mabingwa wa kihistoria timu ya Soka ya Yanga baada ya kuchapangwa bila huruma ni timu ya wanalambalamba ya Azam Fc kwa mabao 3 kwa nunge kwenye michuano ya mapinduzi Cup inayoendelea visiwani Zanzibar. Yanga ambao kwa sasa wanarekodi ya kipekee kwenye ligi kuu soka ya Tanzania Bara baada kucheza mechi 18 bila kufungwa huku mchezo wao wa mwisho wakibakisha na wanalambalamba hao wamalize mzunguko wa kwanza wa ligu kuu. Muuaji mkubwa kwenye mtanange huo wa kusisimua alikuwa Obrey Chirwa alifunga mabao mawili dakika ya…

Source

Share:

‘KUFURU NDOA YA DIAMOND NA TANASHA’

Mwanamuziki Diamond Platnumz na mwanadada Tanasha kutoka pande za Kenya wapo katika mahaba mazito kiasi kwamba wamekuwa wakifuatana kama kumbi kumbi kila mahali.Hali hiyo inaelezwa kwamba ni kutokana na kunogewa na utamu wa penzi lao ambalo bado ni change lakini likiwa na malemgo makubwa katika maisha yao ya baadae Diamond ambaye ni baba wa watoto watatu Tiffa na Nilan ambao kawapata akiwa na Zari na Mwingine Dylan ambaye kazaa na mwanamitindo ambaye pia ni mwanamuziki Hamisa Mobetto inaonekana kukolea vilivyo kwa binti huyo mkenya ambaye pia ana uraia wa Italia.…

Source

Share:

MAKONDA AWAPA MIKAKATI YA KUKUSANYA MAPATO WAKURUGENZI.

  Na, HERI SHAABAN. MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameeleza Mikakati ya ukusanyaji Mapato kwa Wakurugenzi wa Mkoa huo. Agizo hilo Makonda alilitoa Dar es Salam leo wakati wa kikao cha Mkakati wa Mpango wa ukusanyaji mapato baina yake na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wote wa Mkoa Dar es Salam. Aliwataka Wakurugenzi kubuni mbinu za ukusanyaji wa vyanzo vya mapato ili kuongeza idadi ya walipa kodi ambapo alisema kwa Mwaka huu jiji hilo limedhamiria kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato na kuendelea kuwa kinala. “Vyanzo vipo vingi…

Source

Share:

MAWAZIRI WAWILI NA MKUU WA MKOA WATAKIWA KURIPOTI KWA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka viongozi waandamizi wa mkoa wa Iringa akiwemo mkuu wa mkoa huo, Ally Hapi kuripoti ofisini kwake Dodoma saa 5 asubuhi Jumatatu 7, 2019.

Wengine wanaopaswa kuwapo katika kikao hicho ni, Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani na Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo pamoja na wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri za mkoa huo.

Majaliwa alitoa agizo hilo jana Ijumaa wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyoni wilayani Mbinga mkoani Ruvuma akisema inashangaza kuona Serikali inafanya jitihada za kusambaza umeme halafu watendaji wa Serikali wanaweka vikwazo.

“Nataka waje waniambie kwa nini wanazuia nguzo, wananchi wanasubiri wao wamezuia nguzo wanasubiri posho wanaidai Serikali na wao Serikali sasa tutakutana ofisini.”

“Yaani sisi tunaahidi umeme uwake kila nyumba ya Mtanzania mpaka yule mnyonge halafu kuna mtu anazuia nguzo na miti hii tumeipanda wenyewe,” amesema.

Na Elizabeth Edward, Mwananchi 
Share:

AZAM FC WAIADHIBU YANGA BILA HURUMA...CHIRWA BALAA!!


Dakika 90 za mchezo wa kombe la Mapinduzi kati ya Yanga na Azam FC katika Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar zimemalizia kwa Azam FC kuiadhibu Yanga mabao 3 - 0 

Waliofunga magoli

Obrey Chirwa dakika ya 33 

Ennock Atta dakika ya 44

Obrey Chirwa dakika ya 60
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger