Sunday, 6 January 2019

MGOGORO WA UUZAJI VIWANJA VYA KKKT WAMFIKISHA LUKUVI NJOMBE

Na Maiko Luoga Njombe. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.Willium Lukuvi Amewataka Watumishi wa Wizara hiyo Nchini kuwafikia Wananchi Katika Maeneo yao Ili kutatua Kero zinazowakabili Ikiwemo Kumaliza Migogoro ya Ardhi Inayowakabili Wananchi Kote nchini. Waziri Lukuvi Ametoa Agizo hilo Mapema Hii leo katika Ukumbi wa Turbo Njombe Mjini wakati Akizungumza na Mamia ya Wananchi waliojitokeza katika Ukumbi huo na Kuwasilisha Kero zao Kupitia Program ya Funguka kwa Waziri Ambapo Baada ya Kuona Kero nyingi za Wananchi wa Njombe zaidi ya 300 Ndipo Mh. Lukuvi Aliamua kutoa…

Source

Share:

DKT. BASHIRU AWAONYA VIONGOZI WALIOANZA KUTAFUTA UBUNGE KABLA YA WAKATI.

  Na Stella Kalinga, Simiyu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpinduzi (CCM) Taifa Dkt. Bashiru Ally amewaonya baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, na Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma, ambao wameanza kukaa vikao kwa ajili ya kutafuta majimbo kabla ya wakati wa Chama hicho kutangaza mchakato wa kutafuta wagombea wapya wa ubunge na udiwani.   Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali katika wilaya…

Source

Share:

MABULA AMFAGILIA MHE. MAGUFULI KWA KASI YA UTENDAJI WA TARURA KWENYE MIRADI 10 INAYOGHARIMU BI. 5.8

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula amempongeza Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa uanzishwaji wa Wakala wa barabara Mjini na Vijijini TARURA ambacho kimekuwa chapa halisi ya ukombozi kwenye sekta ya miundombinu ya barabara Wilayani Nyamagana kwa kutekeleza miradi 10 yenye thamani ya shilingi 5,822,854,934.00 kwa kasi na kiwango katika mwaka wa fedha 2018 hadi 2019. Mhe. Mabula akiwa ameambatana na Mjumbe kamati ya siasa CCM wilaya ya Nyamagana ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya Mhe. Witness Makale walilakiwa na mwenyeji wao Meneja TARURA wilaya ya Nyamagana Mhandisi…

Source

Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO JANUARI 06,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 5, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.  

Source

Share:

Saturday, 5 January 2019

MATINGA: UTAFITI KUONGEZA TIJA NA UZALISHAJI WA MADINI KWA WACHIMBAJI WADOGO

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga amewataka wachimbaji wadogo kuachana na kutafuta na kuchimba madini kimazoea badala yake wafuate njia ya kisayansi katika kutafuta, kuchimba na kuchenjua madini katika maeneo yao ili kuongeza tija, pato lao na Taifa kwa ujumla. Aliyasema hayo Disemba 4 wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wachimbaji wadogo eneo la D reef na Kapanda Mkaoni Katavi, na kuongeza kuwa, masuala ya madini ni ya kisayansi na hivyo kuwataka wachimbaji wadogo kuondoa dhana mbaya iliyojengeka kwa…

Source

Share:

WAKO WAPI YANGA WALE WA KUTOFUNGWA?,WANALAMBALAMBA WAWALAMBISHA MAGOLI 3.

  NA KAROLI VINSENT. MAJANGA kwa mabingwa wa kihistoria timu ya Soka ya Yanga baada ya kuchapangwa bila huruma ni timu ya wanalambalamba ya Azam Fc kwa mabao 3 kwa nunge kwenye michuano ya mapinduzi Cup inayoendelea visiwani Zanzibar. Yanga ambao kwa sasa wanarekodi ya kipekee kwenye ligi kuu soka ya Tanzania Bara baada kucheza mechi 18 bila kufungwa huku mchezo wao wa mwisho wakibakisha na wanalambalamba hao wamalize mzunguko wa kwanza wa ligu kuu. Muuaji mkubwa kwenye mtanange huo wa kusisimua alikuwa Obrey Chirwa alifunga mabao mawili dakika ya…

Source

Share:

‘KUFURU NDOA YA DIAMOND NA TANASHA’

Mwanamuziki Diamond Platnumz na mwanadada Tanasha kutoka pande za Kenya wapo katika mahaba mazito kiasi kwamba wamekuwa wakifuatana kama kumbi kumbi kila mahali.Hali hiyo inaelezwa kwamba ni kutokana na kunogewa na utamu wa penzi lao ambalo bado ni change lakini likiwa na malemgo makubwa katika maisha yao ya baadae Diamond ambaye ni baba wa watoto watatu Tiffa na Nilan ambao kawapata akiwa na Zari na Mwingine Dylan ambaye kazaa na mwanamitindo ambaye pia ni mwanamuziki Hamisa Mobetto inaonekana kukolea vilivyo kwa binti huyo mkenya ambaye pia ana uraia wa Italia.…

Source

Share:

MAKONDA AWAPA MIKAKATI YA KUKUSANYA MAPATO WAKURUGENZI.

  Na, HERI SHAABAN. MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameeleza Mikakati ya ukusanyaji Mapato kwa Wakurugenzi wa Mkoa huo. Agizo hilo Makonda alilitoa Dar es Salam leo wakati wa kikao cha Mkakati wa Mpango wa ukusanyaji mapato baina yake na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wote wa Mkoa Dar es Salam. Aliwataka Wakurugenzi kubuni mbinu za ukusanyaji wa vyanzo vya mapato ili kuongeza idadi ya walipa kodi ambapo alisema kwa Mwaka huu jiji hilo limedhamiria kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato na kuendelea kuwa kinala. “Vyanzo vipo vingi…

Source

Share:

MAWAZIRI WAWILI NA MKUU WA MKOA WATAKIWA KURIPOTI KWA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka viongozi waandamizi wa mkoa wa Iringa akiwemo mkuu wa mkoa huo, Ally Hapi kuripoti ofisini kwake Dodoma saa 5 asubuhi Jumatatu 7, 2019.

Wengine wanaopaswa kuwapo katika kikao hicho ni, Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani na Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo pamoja na wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri za mkoa huo.

Majaliwa alitoa agizo hilo jana Ijumaa wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyoni wilayani Mbinga mkoani Ruvuma akisema inashangaza kuona Serikali inafanya jitihada za kusambaza umeme halafu watendaji wa Serikali wanaweka vikwazo.

“Nataka waje waniambie kwa nini wanazuia nguzo, wananchi wanasubiri wao wamezuia nguzo wanasubiri posho wanaidai Serikali na wao Serikali sasa tutakutana ofisini.”

“Yaani sisi tunaahidi umeme uwake kila nyumba ya Mtanzania mpaka yule mnyonge halafu kuna mtu anazuia nguzo na miti hii tumeipanda wenyewe,” amesema.

Na Elizabeth Edward, Mwananchi 
Share:

AZAM FC WAIADHIBU YANGA BILA HURUMA...CHIRWA BALAA!!


Dakika 90 za mchezo wa kombe la Mapinduzi kati ya Yanga na Azam FC katika Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar zimemalizia kwa Azam FC kuiadhibu Yanga mabao 3 - 0 

Waliofunga magoli

Obrey Chirwa dakika ya 33 

Ennock Atta dakika ya 44

Obrey Chirwa dakika ya 60
Share:

VIKAO VYA KAMATI YA 14 ZA KUDUMU ZA BUNGE VITAANZA JANUARI 14 HADI 27,2019.

DODOMA. Vikao vya Kamati ya 14 za kudumu za Bunge vitaanza Januri 14 hadi 27 mwaka huu Jijini Dodoma. Aidha, kamati ya masuala ya UKIMWI, kamati za hesabu za Serikali (PAC), kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ma Kamati za Bajeti zitaanza vikao vyake Januari 7.

Source

Share:

PICHA YA MKE WA WAZIRI KIGWANGALLA YAZUA GUMZO MTANDAONI..WABONGO WADAI ANATANGAZA UTALII WA MKEWE



Picha ya Dk. Bayoum, mke wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla, ambayo ameiweka mtandaoni akiwa kwenye hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha, imezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii watu wakimponda kwa kufanya hivyo. 

Kigwangalla alituma picha hiyo ya mke wake kwenye ukurasa wake wa Instagram iliyokuwa na ujumbe unaosema kuwa Ngorongoro siku zote huwa hapachoshi kutembelewa na ndiyo sababu huwa yeye Waziri hakosi kutembelea mbuga hiyo kila mwaka.

Dk. Kigwangalla aliendelea kuandika kuwa maeneo hayo yanavutia na kumfanya mtu anayetembelea mbuga hiyo kuwa wa tofauti na kuwahimiza Watanzania wajenge utamaduni wa kwenda huko.

Picha hiyo ilimwonyesha kwa nyuma mke wake aliyekuwa amevaa fulana nyeusi na suruali yenye mabaka meusi na meupe akiangalia mandhari ya mbuga hiyo.

Wachangiaji kwenye ukurasa wake wa Instagram walianza kutiririka na hoja wakimponda kuwa alikuwa akitangaza maumbile ya mke wake badala ya kutangaza utalii ambao hauonekani kwenye picha aliyoituma.

Picha hiyo ilimwonyesha mke wake akiwa anaangalia madhari ya hifadhi ya Ngorongoro iliyokuwa ikionekana mawingu na sehemu kidogo ya maji na miti.

Clara Masanja ni mmoja wa watu waliomwomba Dk. Kigwangalla kufuta picha hiyo kwa sababu alizodai kuwa inamdhalilisha mke wake na wala haitangazi utalii.

“Kaka yangu Kigwangalla tunatoka wote Puge (Puge Madukani) mimi ni ukoo wa Wapandanzuki (Nzuki), Dk. Nzuki ni mtoto wa baba yangu mkubwa) babu mkubwa kwa babu mdogo). Nakushauri hii posti yako itoe haiko vizuri kabisa kaka yangu,” alisema Clara katika ukurasa huo wa facebook.

Pia alieleza kuwa Kigangwalla ni taswira kubwa katika jamii na watu wanategemea kujifunza mengi kutoka kwake, hivyo picha kama hizo zinaweza kumharibia sifa.

Mchangiaji mwingine, aliandika kuwa: “Mheshimiwa hapo hakuna anayesikiliza maneno yako ya utalii bali kila mtu yupo bize kuangalia maumbile ya mke wako. Wewe ni kioo cha jamii. Tunajifunza nini kutoka kwako kama kiongozi wa juu kabisa mwenye dhamana?” aliongeza.

“Hapo Mkuu unatangaza vitu zaidi ya viwili. Tafakari wakati mwingine watafute wenye kazi zao na si mke wako kwa upande mmoja,” alisema Donnell Pellagio.

Hata hivyo, Dk. Kigwangalla aliamua kufuta picha na maelezo aliyokuwa ameweka kwenye ukurasa wake huo wa Instagram na Facebook baada ya kuona imesambaa na kuzua mjadala.

Share:

Usisumbuke : NJIA RAHISI KABISA YA KUANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2018 NA DARASA LA NNE KAMA UNATUMIA SIMU YA MKONONI HII HAPA



Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa ya Kidato cha Pili (FTNA) 2018 Na Darasa la nne (SFNA) 2018 yametangazwa.
Watumiaji wengi wa simu za mkononi hata wale wanaotumia computer/laptop wamejikuta wakishindwa kuona matokeo kutokana na jinsi yalivyopangiliwa.

Malunde1 blog tupo kwa ajili ya kukuhudumia.

Kama unatumia simu
1.Fungua link ya matokeo 

2.Angalia juu kulia kwenye simu yako,utaona vidoti vitatu 

3.Bonyeza penye vidoti utaona sehemu imeandikwa Find in page

4.Bonyeza palipoandikwa Find in page utaona  sehemu ya kuandikia...kisha andika jina la Shule unayotaka...kiulaini kabisa utaona unachokitaka.

 Kama unatumia Computer/Laptop

1.Fungua link ya matokeo 

2. Shikilia palipoandikwa CTRL na F

3.Utaona kibox ambapo utaandika jina la shule unayotaka

 Angalia matokeo hapa chini 
Share:

MAITI YAFUKULIWA, NUSU YA MWILI YAWEKWA KWENYE MFUKO 'KIROBA'


Mwili wa mkazi wa kitongoji cha Mbomai wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro, Florid Lazari umefukuliwa na polisi na kukutwa nusu yake ukiwa umewekwa kwenye mfuko maarufu kama kiroba.

Tukio hilo limekuja siku chache baada ya mwili mwingine kufukuliwa katika kijiji cha Mpinji, kata ya Mamba wilayani Same mkoani humo na kubainika kuwa ni wa mwalimu Alison Mcharo aliyetoweka mwaka 2006.

Jeshi la Polisi linamshikilia mkewe, Nasemba Alison (80) na mwanaye Orgenes Alison (45) kwa mahojiano na taarifa za awali za polisi zinadai mkewe alikiri kuhusika na mauaji ya Alison.

Hata hivyo, juzi tukio hilo likiwa bado vichwani mwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro, polisi wilayani Rombo walifukua mwili mwiingine na kutambuliwa kuwa ni wa Lazari aliyetoweka usiku wa Desemba 16, 2018.

Taarifa zinasema usiku huo, watu wasiojulikana walifika nyumbani kwake na kumuita atoke nje na alipotoka hakurudi na hakuonekana hadi taarifa zilipotolewa polisi.

Diwani wa Tarakea Motamburu, Michael Beda alisema mwili huo uligunduliwa umezikwa katika msitu wa Serikali wa Nusu Maili unaopakana na msitu wa Mlima Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa diwani huyo, mwili huo ulipofukuliwa ulibainika kuwa umewekwa kwenye kiroba kuanzia kichwani hadi kiunoni, huku kichwa kikiwa na jeraha la kupigwa na kitu kizito.

Akifafanua zaidi, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agnes Hokororo alisema taarifa za kutoweka kwa mtu huyo zilitolewa Desemba 17, 2018 na jitihada za kumtafuta hazikuzaa matunda hadi juzi mwili wake ulipofukuliwa.

“Tarehe 1.01.2019 ndio zikapokelewa taarifa kuwa hapo msituni kunaonekana kama kuna kitu kimefukiwa, kwa hiyo kukawa na hisia huenda ni mwili wa huyo mtu aliyepotea,” alisema.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, polisi walifika eneo hilo na kulizungushia uzio na kisha taratibu za kuomba kibali cha mahakama zilifanyika na kibali cha kufukua kikapatikana hiyo juzi.

“Kwa hiyo lile eneo lilipofukuliwa ndio ukakutwa huo mwili japo ulikuwa umeharibika sana. Ndugu waliutambua na waliuchukua siku ileile kwenda kuuzika upya nyumbani kwake.”

Alisema, “Sasa kuhusu nani ni mhusika wa mauaji yale, ilikuwaje na kwa nini afanye unyama wote ule hilo nawaachia polisi kwa sababu wao ndio mamlaka ya uchunguzi wa matukio hayo.”

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Hamis Issah jana alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa watu kadhaa wanashikiliwa na jeshi hilo wakiwamo baadhi ya ndugu wa marehemu.

Na Daniel Mjema na Florah Temba mwananchi
Share:

ALIKIBA ATUHUMIWA KWA WIZI WA KAZI ZA WASANII...DOMOKAYA AMCHANA



Alikiba.
Msanii mkonge wa muziki wa Bongo Fleva, Domo Kaya amesema kuwa wasanii wapya kwenye muziki huo wanatakiwa kuwa wabunifu, baada ya msanii Alikiba kutumia kidokezo 'Yebaba' ambacho alikuwa alikitumia yeye mwanzo.

Domo Kaya amefunguka hayo kupitia FRIDAY NIGHT LIVE ya EATV, ambapo amesema kuwa Alikiba kutumia neno hilo sio vibaya lakini alitakiwa kuomba ruhusa kwanza kwake.

"Nawasihi wadogo zetu kuwa wabunifu, na kuacha ujanja ujanja maana kutumia kitu hukatazwi lakini uombe kwa muhusika akupe baraka zake", amesema Domo Kaya.
Msanii Domo Kaya.

Hivi karibuni msanii Alikiba ameonesha kutumia msemo huo 'yebaba' katika wimbo wake mpya wa 'Kadogo' aliouachia mwishoni mwa mwaka uliopita na kuupa umaarufu mkubwa kwa mashabiki wake badala ya ule ambao ulizoeleka wa 'Yooo', ambao alikuwa akiutumia hapo kabla.

Chanzo - EATV
Share:

Gospel Song : DAMIAN SOUL ft BARNABA - ASANTE

Msanii wa muziki Bongo, Damian Soul kwa kushirikiana na Barnaba wanakukaribisha kutasikiliza wimbo wao uitwao Asante. Usikilize hapa.
Advertisement
Share:

Video Mpya : DULLY SYKES - SAMBA

Video Mpya ya Dully Sykes - Samba

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger