WAKATI timu ya Yanga ikiwa haijafungwa hata mchezo mmoja katia mechi za ligi kuu soka Tanzania Bara,Kocha mkuu wa Mabingwa wa Ligi kuu hiyo Timu ya Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amesema nao wao watahakikisha katika mechi zao 24 za Ligi Kuu Bara zilizobaki, hawatafungwa kwenye uwanja wao wa nyumbani kwa lengo la kuipiku Yanga na kutetea ubingwa wao. Kocha huyo ambaye anasifika kwa “Fomesheni’ ya alisema kuwa licha ya wapinzani wao Yanga kuwa juu katika msimamo wa ligi hiyo siyo kigezo cha wao kushindwa kutetea ubingwa wao. Yanga inaongoza msimamo…
Thursday, 3 January 2019
VYAMA 10 VYA UPINZANI NCHINI KUIBURUZA SERIKALI YA JPM MAHAKAMANI,NI KUPINGA MSWAADA HATARI
NI VITA mpya sasa unaweza ukasema ni mara baada ya Vyama 10 vya upinzani nchini kupitia muungano wao vimepanga kwenda fungua kesi Mahakamani Kuu ya Tanzania kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa na Bunge kwa ajili ya kuupitishwa kuwa sheria. Kesi hiyo ya kupinga mswaada huo ambao unatajwa ni hatari zaidi imefunguliwa Desemba 20,2018 ikitarajiwa kuanza kusikilizwa kesho Ijumaa Januari 4,2019 huku mlalamikiwa akiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Akisoma tamko la umoja huo leo Alhamisi Januari 03, 2019, Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe akiongea kwa…
UMOJA WA VYAMA 10 VYA UPINZANI NCHINI TANZANIA VIMEFUNGUA KESI MAHAKAMA KUU TANZANIA.
Na. Jovine Sosthenes. Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu CUF bara, Joram Bashange pamoja na viongozi wengine wa vyama mbalimbali vya siasa vya upinzani leo Januari 3 wamethibitisha kufungua kesi katika Mahakama kuu ya Tanzania kwa ajili ya kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa Bungeni kwa minajiri ya kuupitisha kuwa sheria. Kesi hiyo imefunguliwa Desemba 20,2018 ikitarajiwa kuanza kusikilizwa kesho Ijumaa Januari 4,2019 huku mlalamikiwa akiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Akisoma tamko la umoja…
HARMONIZE ATOA MSAADA KWA WALEMAVU
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya WCB iliyochini ya Diamond Platnumz, Harmonize alimaarufu Kondeboy ameamua kutoa msaada kwa walemavu jijini Dar Es Salaam maeneo ya Kariakoo.
Msanii huyo ameamua kurudisha shukrani hizo kwa mashabiki zake ambao wana matatizo mbalimbali hasa walemavu wa miguu na katika kipindi hiki ambapo tumeingia mwaka mwingine.
Mbali na kutoa msaada huo msanii huyo ameandika ujumbe mrefu sana kweny ukurasa wake wa Instagram akitoa shukrani zake kwa wale wote walioweza kwa namna moja ama nyingine kuusapot muziki wake. na Ujumbe mwenyewe ndio huu hapa:-
“HERI YA MWAKA MPYA….!!! NDUGU ZANGU …!!! NINGEPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA WAANDISHI WA HABARI PAMOJA NA MEDIA ZOTE AMBAZO ZIMEKUWA SAMBAMBA NAMI BILA KUWASAHAU DJ’S WOTE DUNIANI KWA KUUNGANA NAMI NA KUNI SUPPORT KUSOPPORT MUZIKI WANGU AMA KWA HAKIKA BILA NYINYI BASI PASINGEKUWA NA HARMONIZE HATA MUZIKI WENYEWE HUWENDA USINGEKUWEPO MWAKA 2018 UMEKUWA MWAKA WENYE KUONYESHA MWANGA AMA NURU YA MUZIKI KWANGU NAAMINI MAZURI MENGI YAPO MBELE NINGEOMBA MUENDELEE NA MOYO HUWO HUWO WA UPENDO NA IMANI KUNIVUMILIA NINAPOKOSEA KWANI MIMI SIJAKAMILIKA HASA UKICHANGANYA NA UJANA…!!!! LAKINI PIA NIWATAKIE HERI YA MWAKA MPYA SHABIKI ZANGU AMBAO MUPO BEGA KWA BEGA NAMI KUHAKIKISHA TUNALIKAMILISHA KILA TULIPANGALO KWA UWEZO WA MUNGU….!!!!! HAKIKA NYINYI NDIO HARMONIZE MWENYEWE….!!! LAMWISHO NIOMBE KUWASILISHA HILI DOGO KWA WAMILIKI WA MEDIA WATANGAZAJI PAMOJA NA DJ’S WOTE….!!! KAMA UNGEPENDA MIMI NIKUPIGIE JINGLE AU TANGAZO LA REDIO YAKO BASI UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUCHUKUA NUMBER HI..! 👉 +255658135762 KISHA TUMA MAELEKEZO YAKO MFANO MIMI NI DJ FULANI KIPINDI FULANI YANI TUMA MAELEKEZO YAKO YOTE KUPITIA WHTSP NADHANI WATU WA MEDIA WASHANIELEWA NINACHO MAANISHA KISHA MWISHO WEKA EMAIL YAKO NAMI NITARECORD NA NITAKUTUMI KATIKA EMAIL YAKO HI NI KWA MEDIA WATANGAZAJI DJ’S WOTE DUNIANI……!!! LET’S GO…….!!!!!!!!!!”
Msanii huyo amekuwa sio mara ya kwanza kwenda kutoa msaada Kariakoo sehemu ambayo inaaminika ndio yalikuwa makzi ya msanii huyo kwani alishawahi kufanya kazi hapo ya kuuza maji kabla ya kuwa msanii.
WADAU WA SOKA SHINYANGA WALIA NA TFF UKATA VILABUNI
Wadau wa soka Mkoani Shinyanga wameliomba Shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF) kuvinusuru vilabu vinavyoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara,kwa kutafuta mdhamini mkuu atakayeondoa hali ya ukata kwa vilabu shiriki katika mzunguko wa pili msimu huu wa 2018/19.
Wakati baadhi ya timu zinazoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara zikiwa zimemaliza mzunguko wa kwanza wadau wa michezo hasa soka mkoa wa Shinyanga wamezungumza na Malunde 1 blog katika maeneo tofauti mkoani hapa na kutoa tathmini ya mwenendo wa ligi hiyo hasa hali ya kiuchumi kutokana na timu nyingi kumaliza mzunguko huo zikiwa hohe hahe.
Alfred Peter ni miongoni mwa wadau wa soka mkoani hapa ambaye pia ni mwanachama wa timu ya stand united amesema pamoja na ligi kwenda vizuri kutokana na mpangilio wa shirikisho la soka nchini kuongeza timu nne,lakini ukosefu wa mdhamini mkuu wa ligi kumesababisha vilabu vingi kusindwa kujiendesha ikiwa ni pamoja na kukimbiwa na wachezaji.
“Wachezaji wengi wamekimbilia timu zenye ahueni kiuchumi kutokana na ukata unaozikabili timu nyingi shiriki za ligi kuu nahii imesababishwa na ukosefu wa mdhamini mkuu kwenye ligi hii” Alisema Peter.
Wadau hao wamesema endapo hali ya kukosa mdhamini mkuu wa ligi kuu soka tanzania bara msimu huu ikiendelea katika mzunguko wa pili wanahofia kuibuka kwa upatikanaji wa matokeo ya mezani kutokana na ukosefu wa fedha na kuliomba shirikisho la mpira wa miguu nchini tff kufanya jambo kuzinusuru timu hizo na kadhia hiyo.
Ligi kuu soka Tanania bara msimu huu wa 2018/19 imeendeshwa bila mdhamini mkuu huku vilabu shiriki vikiwa na hali mbaya kiuchumi ambapo ligi hiyo awali ilikuwa ikidhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom ambayo ilikuwa ikitoa fedha taslimu zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 100 kwa timu shiriki jambo ambalo limekosekana msimu huu.
Ligi kuu soka Tanania bara msimu huu wa 2018/19 imeendeshwa bila mdhamini mkuu huku vilabu shiriki vikiwa na hali mbaya kiuchumi ambapo ligi hiyo awali ilikuwa ikidhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom ambayo ilikuwa ikitoa fedha taslimu zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 100 kwa timu shiriki jambo ambalo limekosekana msimu huu.
Na Malaki Philipo, Malunde 1 blog.
CCM NJOMBE YAAHIDI KUNYAKUA VIJIJI NA MITAA YOTE KATIKA UCHAGUZI MDOGO 2019
Na Amiri kilagalila Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM mkoa wa Njombe umeahidi chama hicho kuibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2019 kutokana na kukubalika kwa chama hicho mkoani humo. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake wakati akitoa salamu za mwaka mpya katibu wa hamasa na chipukizi UVCCM mkoa wa Njombe Jonson Elly Mgimba anasema kuwa zawadi pekee wanayohitaji kumkabidhi Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ni kuhakikisha chaguzi za serikali za mitaa wanaibuka kidedea…
WATOTO WAWILI WAFARIKI WAKIOGELEA BAHARINI KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA
Watu wawili ambao ni wanafunzi wa shule ya Msingi Mgao Mkoa wa Mtwara wameokotwa wakiwa wamefariki dunia pembezoni mwa mwambao wa Bahari ya Hindi.
Uchunguzi wa Daktari imebainisha kuwa vifo hivyo vimetokana na kukosa hewa baada ya kuzama kwenye maji.
Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Blasius Chatanda amesema tukio la wanafunzi hao kuzama majini limetokea Januari Mosi katika kijiji cha Mgao ambapo uchunguzi wa awali unaonyesha watoto hao hawakuwa na wasimamizi walipokwenda kuogelea.
"Watoto hao tumeweza kuwatambua, wa kwanza alikuwa anaitwa Rajab Athman mwenye umri wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne, wa pili alikuwa anaitwa Salum Hamza ambaye alikuwa na miaka 8. Walikwenda kuogelea kwenye fukwe na bahati mbaya maji yaliwazidi na wakapoteza maisha," amesema Kamanda Chatanda.
Katika hatua nyingine siku hiyo ya Januari Mosi Amri Nayope ambae ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitari ya Wilaya ya Newala akidaiwa kushambuliwa kwa kupigwa na watu ambao hawakufahamika kisha kutelekezwa jirani na nyumbani kwao.
Kufuatia taarifa hiyo baadhi ya wakazi mkoani hapa wameitaka jamii hususani wazazi na walezi kuongeza umakini katika kuwasimamia watoto wao.
Kamanda Chatanda amesema msako mkali unaendelea kuwabaini waliohusika katika shambulio lililopelekea kifo cha mwanafunzi huyo wa sekondari huku miili ya wanafunzi wa shule za msingi tayari imesha kabidhiwa kwa ndugu baada ya uchunguzi wa Daktari ili kuendelea na taratibu za mazishi.
MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU INATARAJIA KUSIKILIZA KESI YA MALINZI NA WENZAKE KWA SIKU TATU MFULULIZO.
DAR ES SALAAM Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kusikiliza ushahidi wa kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa (TFF) Jamal Malinzi na wenzake kwa siku tatu mfululizo. Hayo yameelezwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya kesi hiyo kuitishwa leo kwa ajili ya kutajwa. Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi January 16, 17 na 21, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi, ikiwa imefikia shahidi wa 10. Washitakiwa wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga ambao wanakabiliwa na mashitaka 28,…
VYAMA 10 VYA UPINZANI VYAFUNGUA KESI KUPINGA MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA TANZANIA
Vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania kupitia muungano wao vimefungua kesi Mahakamani Kuu ya Tanzania kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa na Bunge kwa ajili ya kuupitishwa kuwa sheria.
Kesi hiyo imefunguliwa Desemba 20,2018 ikitarajiwa kuanza kusikilizwa kesho Ijumaa Januari 4,2019 huku mlalamikiwa akiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Akisoma tamko la umoja huo leo Alhamisi Januari 03, 2019, Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema muswada huo unakinzana na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 hivyo ni muhimu kwao kuupinga.
“Serikali imepeleka bungeni muswada wa sheria ya vyama vya siasa unaohalalisha agizo la Rais Magufuli alilolitoa mkoani Singida mwaka 2016 kuzuia mikutano ya vyama vya siasa. Muswada huu unafanya shughuli za kisiasa kuwa suala la jinai.
“Tumefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar chini ya hati ya dharura kupinga Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa kujadiliwa na Bunge kwa minajiri ya kuupitisha kuwa sheria kwa sababu unakinzana na katiba ya nchi.
"Hatuwezi kwenda kuujadili Bungeni, mnajua kuna wabunge wengi wa CCM, baadhi yao ni wazuri na tumekuwa tukijadiliana nao, lakini wengine ni makasuku. Kuna wabunge wengine wa CCM wanapenda sifa, siyo kwamba utakuwa mbaya tu lakini utatoka mbaya zaidi.
“Muswada huo unalenga kumfanya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa na Mamlaka ya Usimamizi (Regulatory Authority), kuwa na mamlaka ya kuingilia shughuli za kiutawala na maamuzi ya ndani ya vyama vya siasa ikiwemo kusimamisha/ kumfukuza mtu uanachama,” amesema Zitto Kabwe.
MBOWE,MATIKO KUENDELEA KUSOTA MAHABUSU HADI JANUARI 17..MAWAKILI WAHOJI KWA NINI?
Wakati Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wakiendelea kusota mahabusu, Wakili anayewatetea Profesa Abdallah Safari amehoji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu rufaa iliyokatwa na upande wa mashtaka katika Mahakama ya Rufani.
Mbowe na Matiko wanasota mahabusu baada ya Mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana yao Novemba 26,2018 kwa kukiuka masharti ya dhamana, ambapo waliamua kukata rufaa Mahakama Kuu lakini iliwekewa pingamizi baada ya upande wa mashtaka kukata rufaa Mahakama ya Rufani.
Profesa Safari alihoji swali moja kuhusu rufaa hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi kueleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa.
Profesa Safari alimuuliza Wakili Kadushi kama rufaa waliyoikata ilikuwa chini ya hati ya dharura na kama hawakufanya hivyo ni kwa nini...?
Katika majibu yake Wakili Kadushi ameeleza kuwa hakuna uhalali wa kisheria kuhusu swali hilo mahakamani hapo, labda lingeulizwa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa.
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi January 17, 2019 huku akisema swali hilo la rufaa wakalihoji Mahakama Kuu.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai namba 112/ 2018 ni wabunge wa Chadema, Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), John Mnyika (Kibamba), John Heche (Tarime Vijijini), Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini).
Pia wamo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu.
Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018 maeneo ya Dar es Salaam.
ZITTO KABWE : WABUNGE WAPENDA SIFA ,MAKASUKU WANATUKWAMISHA BUNGENI
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ameeleza kuwa wingi wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bungeni kuna kwamisha maslahi ya wananchi kutokana kutumia wingi wao kupitisha yanayowapendeza watawala.
Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye Ofisi za Chama cha CHAUMA akiambatana na viongozi wa vyama kumi vya upinzani vilivyoungana kutetea demokrasia na kupinga muswada wa sharia ya vyama vya siasa.
Vyama hivyo ni pamoja na ACT-Wazalendo, Chama cha Wananchi (CUF) Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR-Mageuzi, NRD, CCK, CHAUMA.
Zitto amesema kuwa muswada wa sheria ya vyombo vya habari utapelekwa bungeni ambapo wabunge wa CCM ambao ndiyo wengi bunge watawashinda wabunge wachache wa upinzani na kupelekea kupita kwa sheria hiyo ya vyama vya siasa ambayo wanaiona ni sheria shetani na ovu kwa demokrasia.
“Bunge limejaa wabunge wa CCM, kuna wabunge wazuri wa chama cha mapinduzi lakini kuna wabunge ‘makasuku’ kiasi kwamba muswada huu ukienda utatoka mbaya zaidi,” amesema Zitto na kuongeza.
“Kuna wabunge wapenda sifa wataufanya muswada huu kuwa mbaya zaidi na tayari tuansikia wapo wabunge watakaopendekeza kwenye sharia hiyo kwamba hakuna kufanya mikutano mpaka uchaguzi hadi uchaguzi.”
Zitto ameeleza kuwa muswada huo uliolenga kuua demokrasia ya kweli ambapo Msajili wa vyama vya siasa atakuwa na mamlaka kamili juu kuingilia mambo ya ndani ya vyama vya siasa.
Via Mwanahalisionline
ZAHERA : LIVERPOOL WANA NAFASI YA KUICHAPA MAN CITY LEO
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera
Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera ametoa mtazamo wake kuelekea mchezo mkali wa EPL leo kati ya vigogo Manchester City na Liverpool.
Akizungumza katika mahojiano na Kipenga Extra ya East Afrika Radio inayoruka Jumatatu mpaka Ijumaa, kuanzia saa 6:00 mpaka saa 7:00 mchana, Zahera amesema kuwa anaamini Liverpool wana nafasi ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
"Mechi ya Man City na Liverpool leo, mimi mtazamo wangu naona kwamba City anaweza kupigwa leo, kutokana na mbio za wachezaji wa Liverpool na ile 'Counter Attack' yao, lakini mpira ni kitu cha ajabu, naweza kusema hivi lakini kesho tukakuta kimetokea kingine," amesema Mwinyi Zahera.
"Man City imefungwa mechi mbili hapa karibuni kabla ya kushinda dhidi ya Southampton, Liverpool yenyewe ikishinda michezo mitatu ya nyuma ukiwemo ushindi dhidi ya Arsenal. Naogopa sana kwamba City anaweza kuteseka na mbinu za Jurgen Klopp," ameongeza Zahera.
Liverpool inakwenda katika mchezo huo ikiwa haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa katika EPL, wadau wengi wa soka wakiipa nafasi kubwa kuibuka na ushindi kutokana na rekodi za hivi karibuni za timu hizo kuibeba Liverpool.
Katika mechi 11 za mwisho baina ya timu hizo katika mshindano yote, Manchester City imefungwa mechi 7 na kutoa sare mechi 3 huku ikishinda mara moja pekee ambayo ni msimu uliopita ilipoifunga Liverpool mabao 5-0.
Mechi hii inaweza kutoa picha halisi kwa Liverpool katika kuwania ubingwa, kwani endapo itaibuka na ushindi itamuacha Man City kwa tofauti ya pointi 10, lakini pia Man City endapo itaibuka na ushindi, itaibua matumaini zaidi ya kuikamata Liverpool, kwani itapunguza pengo la alama na kufikia 4.
Chanzo - Eatv
RAIS MSTAAFU JACOB ZUMA KUINGIA STUDIO KUREKODI NGOMA
Rais mstaafu wa Afrika Kusini Jacob Zuma, anakusudia kuingia studio hivi karibuni, kurekodi albam ambayo itakuwa na nyimbo za mapambano.
Taarifa hiyo imetolewa na Thembinkosi Ngcobo ambaye ni Mkuu wa Hifadhi ya Utamaduni na Burudani, na kusema kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya kuona hakuna msanii wa sasa anayeimba nyimbo za mapambano, kama zamani.
“Tulikuwa tunatafuta wasanii wa nyimbo za aiana hii, ilikuwa ngumu , tulijaribu kutafuta hata video fupi fupi, lakini hatukupata kitu katika jumba la makumbusho, hapo ndipo kama Idara tukamkumbuka Zuma kwenye sula la kuimba”, ameeleza Ngcobo.
Akiendelea kuelezea hilo Ngcobo alisema kwamba, "Hivi karibuni tulikuwa na Mazungumzo na Zuma, tulienda nyumbani kwake, tukajadili, alianza kuongelea mengine lakini kabla hatujaondoka, alisema amefurahi kuwa sehemu ya 'ptoject' hiyo, hivyo tutaangalia namna ya yeye kufanya mazoezi na kwaya hivi karibuni".
Iwapo Rais Jacob Zuma ataingia studio na kurekodi album hiyo, atakuwa Rais wa Pili afrika kuweka wazi uwezo wake wa kufanya muziki, baada ya Rais Yoweri Musevi wa Uganda, ambaye ameshawahi kusikika akirap.
HIKI NDICHO KINACHOMUUMIZA KICHWA WAZIRI LUGOLA KATIKA WIZARA YAKE.
Na Allawi Kaboyo Bukoba. WAZIRI wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola,amesema kitu kinachomuumiza kichwa katika wizara yake ni Idara ya huduma za uangalizi na probesheni licha ya kuwa na watumshi wengi katika wizara hiyo. Alitoa kauli hiyo Jana wakati akipokea taarifa za idara hiyo Mkoani Kagera ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake mkoani humo kwa muda wa siku saba atakaoumaliza. Waziri Lugola,alisema watumishi wa wizara hiyo wizarani ni 160 lakini shughuli zake hazifahamiki kwa jamii. Alisema kwa hali ilivyo Wizara inamzigo wa kuibeba idara hiyo…
AMUACHA MUMEWE KITANDANI KISHA KUTOKA NJE NA KUJIUA KWA MTANDIO
Mkazi wa mtaa wa Nakayaya wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, Awetu Makunula (44) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia mtandio jirani na nyumbani kwa wazazi wake.
Mume wa marehemu Awetu, Salum Namtikwe, amesema usiku walilala wote na kabla ya tukio hilo mkewe aliamka saa 11 alfajiri na kumuaga kuwa anatoka nje kwa ajili ya kufagia nje ya nyumba yao.
Amesema baada ya kupewa maelezo hayo yeye aliendelea kulala lakini baadaye alishangaa kupata taarifa za mkewe kukutwa akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kujining’iniza katika mti uliopo jirani na nyumbani kwa wazazi wake.
“Baada ya kupatiwa taarifa hizo niliamka na kwenda eneo la tukio na kumtambua marehemu mke wangu, baadaye tulitoa taarifa kwa viongozi wa serikali kwa ajili ya taratibu za kuuondoa mwili huo katika eneo hilo,” amesema mume wa marehemu.
Akisimulia maisha ya mkewe, Namtikwe amefunguka kuwa hajawahi kugombana naye lakini alikuwa mgonjwa wa homa za mara kwa mara licha ya kwamba siku aliyojinyonga hakulalamika kuumwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, ASCP Gemin Mushy amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema polisi inaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo chake.
Chanzo- Eatv
AKAMATWA AKISAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU KWA GARI LA LAKE OIL
Dereva wa lori la mafuta mali ya Kampuni ya Lake Oil, Christopher Kikwete (42) mkazi wa Kibamba Jijini Dar es Salaam anashikiliwa na polisi mkoani Songwe kwa tuhuma za kusafirisha wahamiaji haramu 10 raia wa Ethiopia kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi mkoani huo, Mathias Nyange amesema hayo jana Jumatano Januari 02, 2019 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Amesema dereva huyo alikamatwa Desemba 31, 2018 katika stendi ya mabasi ya Makaburini mjini Vwawa wilayani Mbozi saa 4 asubuhi wakati polisi kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji wakiwa katika doria walilisimamisha lori hilo na kukuta limejaza wahamiaji hao katika kitanda kilichopo nyuma ya kiti cha dereva.
Kamanda huyo amesema lori hilo lenye namba T 500 DFJ na tera lenye namba T 833 CMN aina ya Scania ni tanki lililokuwa limebeba mafuta ya petroli kutoka Dar es Salaam kwenda nchini Zambia nalo linashikiliwa na jeshi hilo.
MAWAKILI WA 'MPEMBA WA MAGUFULI' WAIANGUKIA MAHAKAMA
Upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Yusuf Ali maarufu kama ‘Mpemba wa Magufuli' na wenzake, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Da es Salaam kuchoshwa na maelezo ya upande wa mashtaka kuwa jalada la kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Wakili wa utetezi, Hassan Kiangio, ameieleza mahakama hiyo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Wanjah Hamza, baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa jalada la kesi hiyo lipo kwa DPP kwa ajili ya kutolewa maamuzi.
Yusuf na wenzake watano, wanakabiliwa na mashtaka manne, likiwamo la kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh. milioni 785.6.
Washtakiwa hao wamekaa rumande kwa zaidi ya miaka miwili kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokukamilika.
Washtakiwa hao walifikishwa Kisutu kwa mara ya kwanza, Novemba 17, 2016 kujibu mashtaka yanayowakabili.
“Kesi hii ni ya muda mrefu, wateja wangu wanaendelea kusota rumande bila kujua hatima yao, tumechoshwa na hizi kauli za upande wa mashtaka kuwa jalada lipo kwa DPP linafanyiwa kazi, tunataka wenzetu wa upande wa mashtaka watuambie wamefikia wapi juu ya upelelezi wa kesi hii,” Kiangio aliiambia mahakama hiyo.
Akitolea ufafanuzi wa hoja hizo, Wakili wa Serikali, Elia Athanas, alidai kuwa kesi hiyo iliitishwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba jalada halisi la kesi hiyo lipo kwa DPP, hivyo wanasubiri uamuzi wake.
Novemba 15, mwaka jana, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, aliieleza mahakama kuwa wapo katika hatua za mwisho za uandaaji wa nyaraka ili kuipeleka kesi hiyo katika hatua nyingine.
Hakimu Mkazi, Hamza baada ya kusikiliza hoja za pande zote, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 15, 2019 itakapotajwa na kusema kuwa hoja za upande wa utetezi zitafanyiwa kazi na Hakimu anayesikiliza shauri hilo, Thomas Simba, atakaporejea kutoka likizo.