Wednesday, 26 December 2018

Makubwa Haya : KIJANA AFARIKI KWENYE SHINDANO LA KUFANYA MAPENZI..ROUND 7 TU KWISHA HABARI YAKE



Makubwa Haya!! ndivyo unaweza kusema... Ama kweli hili ni tukio la kufungia mwaka 2018. Katika hali isiyokuwa ya kawaida Kijana aliyejulikana kwa jina la Davy amefariki dunia baada ya kufanya mapenzi na kwenda round saba mfululizo na mwanamke aliyejulikana kwa jina la Loveth nchini Nigeria.

Watu hawa walibeti juu ya nani anatisha zaidi kwa kufanya mapenzi muda mrefu zaidi ,basi Davy akaweka dau la Naira 50,000 ambazo ni shilingi elfu 14 za Kenya ama laki 3 za Tanzania kwa atakayeshinda.

Isome zaidi hapa chini

A middle-aged man, simply known as Davy, has died in a popular hotel in Ikotun area of Lagos State during a sex competition with a lady identified as Loveth.

It was gathered that the late Davy had argued with Loveth on who can last longer in a sex bout.

Both claimed they were stronger and refused to admit defeat.

During the argument, Davy staked N50,000 on the condition that if Loveth defeats him during the romp, she will take the money.

Loveth agreed, moved into the hotel and booked for a chalet.

It was gathered that while the marathon sex lasted, Davy pulled through to the sixth round but Loveth was unshaken till the seventh round when he collapsed and died on top of her.

She then raised the alarm and contacted the hotel management, who handed her over to the Ikotun Police Division while the body of the deceased was deposited at an undisclosed hospital for autopsy.

Loveth was later transferred to the SCIID Panti, Yaba, where she told investigators what transpired between her and the late Davy. The fate of Loveth will depend on the outcome of the autopsy.

Source - Guardian.ng
Share:

MHE MABULA AFADHIRI MICHUANO YA KOMBE LA KISHIRI 2018/2019

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula amefadhiri Vifaa Vya michezo vikiwemo Jezi, Mipira na Vitini Vya waamuzi vyenye thamani ya shilingi 5,000,000 kwa vikosi 10 vishiriki michuano ya Kombe la Kishiri lililoandaliwa na Diwani Kata hiyo Mhe. Sospeter Ndyumi kwa ushirikiano wa Chama Cha Mapinduzi litakalo anza tarehe 28.12.2018 hadi tarehe 20.01.2019. Mhe. Mabula akikabidhi Vifaa hivyo amesema, amedhamiria kuhakikisha Nyamagana inakuwa tanuru la kuibua na kuendeleza Vipaji kupitia michuano mbali mbali katika ngazi ya Mitaa, Kata, Wilaya hadi Mkoa na Taifa. Vikosi vinavyotadhamiwa kushiriki ni pamoja na Kishili…

Source

Share:

IMANI YA USHIRIKINA YATANDA KIJIJI CHA IDUNDA MKOANI NJOMBE.

Na Amiri kilagalila Wakati waumini wa dini ya kikristu nchini wakiungana na mataifa mengine Duniani wakiendelea kusheherekea sikuku ya kuzaliwa kwa Yesu kristu ambayo imekuwa ikifanyika desemba 25 kila mwaka. Taharuki kubwa imetokea kwa wananchi wa kijiji cha Idunda kilichopo katika halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo mapema asubuhi siku ya tarehe 25 wakati wakiwa katika maandalizi ya kuelekea katika shughuli za ibada na kukutana na kifaa kikubwa kilichoanguka pembezoni mwa nyumba ya mmoja wa wanakijiji kikiwa kimefungwa pembe za Ng’ombe mbele na nyuma. Hali iliyowafanya wakazi wa kijiji…

Source

Share:

MAALIM SEIF KUHAMIA ACT WAZALENDO?


Chama cha Wananchi (CUF) upande wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba umedai Maalim Seif Sharif Hamad anajiandaa kuhamia ACT-Wazalendo.

Amesema Maalim Seif ambaye ni katibu mkuu wa chama hicho kwa sasa yuko mbioni kutimkia ACT.

Akizungumza leo Jumatano katika mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa CUF, Khalifa Suleiman Khalifa amedai vyama sita vya upinzani vilivyokutaka Zanzibar wiki iliyopita moja ya ajenda yao ilikuwa namna gani Maalim Seif atakubaliana na ACT-Wazalendo.

Amesema miongoni mwa makubaliano hayo ni kuwa upande wa Maalim Seif uachiwe nafasi zote za uongozi upande wa Zanzibar na Zitto Kabwe ambaye ni kiongozi wa ACT, wachukue uongozi wa Tanzania Bara.

Amedai kuwa hata kama Maalim Seif ataondoka CUF, wataendelea kuwa imara huku akiwataka wote watakaoambatana na katibu mkuu huyo kwenda ACT kutosita kwa sababu uamuzi wao utaheshimiwa.

Mgogoro ndani ya CUF ulianza baada ya Lipumba kurejea katika uongozi mwaka 2016, ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu alipojiuzulu. Jambo hilo liliibua mgogoro wa uongozi baada ya ofisi ya msajili kutangaza kumtambua Lipumba kama mwenyekiti na kusababisha pande hizo mbili kukimbilia mahakamani na kufungua kesi kadhaa ambazo zinaendelea.
Share:

MASHUJAA FC WAICHAPA SIMBA 3 - 2...WAING'OA KOMBE LA SHIRIKISHO


Klabu ya soka ya Simba imeng'olewa katika michuano ya shirikisho (Azam Sports Federation Cup) baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Mashujaa FC .

Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa taifa, Simba imefungwa mabao 3-2 na kuwaondoa kabisa katika mshindano hayo. 

Mabao ya Mashujaa FC yamefungwa na Shaaban Hamis katika dakika ya 47, Jaremiah Josephat katika dakika ya 57 na Rajabu Athuman huku mabao ya Simba yakifungwa na Paul Bukaba katika dakika ya 19 na 79.

Simba imeondolewa katika michuano hiyo kwa msimu wa pili mfululizo, ambapo msimu uliopita iliondolea katika hatua hii kwa kufungwa na Green Warriors kwa mikwaju ya penati 4-3.

Inabakiza nafasi mbili pekee za kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao, ambazo ni Ligi Kuu Tanzania Bara endapo itaibuka bingwa pamoja na michuano ya Klabu Bingwa Afrika endapo itashinda ubingwa huo.

Matokeo ya mchezo mwingine ni ya Mtibwa Sugar na Kiluvya United, ambapo Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kuungana na vigogo wengine wakiwemo Yanga na Azam FC ambao wanafuzu hatua inayofuata ya 32 bora.
Share:

TAZAMA JINSI DIAMOND ALIVYOPOKELEWA KWA SHANGWE KENYA

Wasanii watakaofanya show leo Jumatano  katika Tamasha la Wasafi Festival nchini Kenya kutoka Tanzania wamepokewa kwa shangwe kubwa na Wakenya hapo jana.

Awali show hiyo iliingiwa na sitofahamu baada ya msanii Diamond na Rayvanny kutoruhusiwa kufanya onesho nje ya nchi baada ya kufungiwa na BASATA kwa kosa la kuimba wimbo Mwanza ambao ulifungiwa na baraza hilo.

Lakini juzi baraza hilo lilitoa ruhusa kwa waimbaji hao ya kufanya enesho kwa madai adhabu ya kufungiwa ilikuja kwa wawili hao wakati tayari wameshaingia makubaliano ya enesho la Kenya.

Baada ya team hiyo kuwasili nchini Kenya, Rais wa WCB Diamond Platnumz aliwataka mashabiki kukaa mkao wa kula kwaajili ya enesho hilo la aina yake.
Share:

HII HAPA ORODHA YA WASANII WATAKAO PERFORM SHOW YA FUNGA MWAKA NA KING KIBA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Salehe Kiba alimaarufu Alikiba ameweka wazi orodha ya wasanii watakaoperform katika show yake ya funga mwaka na King Kiba.

Katika Orodha hiyo wamo Mr Blue, Mwana Fa,Barnaba classic, Nuh Mziwanda, The Mafikh, Billnas, na kundi lake la The Kings music, na wengineo wengi ambapo show hii itafanyika katika ukumbi wa Next door Arena Masaki jijini Dar Es Salaam.

Kiba amewasisitiza watu kuwahi kwa ajili ya kwenda kupata burudani nyingi hasa kutoka kwa mkongwe wa Bongo fleva Mwana Fa. Alikiba aliandika hivi kuhusu Mwana Fa:-

“Labda siku nyingi hujamuona @mwanafa kwenye jukwaa. Unahitaji kusikia mashairi yake ya kitambo na ngoma kali za hapo juzi kati kama #AsanteniKwaKuja#Sielewi#DumeSurualina nyingine.

Kiu ya burudani za Falsafa itakatwa Jumamosi hii pale Next Door Arena kwenye #FungaMwakaNaKingKiba. Hakikisha unanunua tiketi yako mapema.

Bila shaka unyunyu wa @fynbyfalsafautapatikana pale pia.
#mofayabyalikiba
#FungaMwakaNaKingKiba
#KingKiba”
Advertisement
Share:

HAWA NDIYO WANASIASA WALIOTIA FORA MWAKA 2018..YUMO MEMBE,BASHIRU NA MZEE WA FYEKELEA MBALI...JIFANYE UNAJIKUNA


Mwaka 2018 unakwisha ukiacha alama katika ulingo wa kisiasa ambapo baadhi ya viongozi wa siasa wameng’ara kwa utendaji mzuri wakipata sifa serikalini na mbele ya wananchi.

Miongoni mwa viongozi waliong’ara ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ambaye Septemba 8, Rais John Magufuli alimtangaza kuwa Mkuu wa Mkoa anayeongoza wa kufanya kazi vizuri.

Pia, CCM imeingia katika vita mpya dhidi ya wagombea urais wa mwaka 2015, baada ya katibu wake mkuu, Dk Bashiru Ally kumtuhumu hadharani Bernard Membe kuwa anakwamisha mikakati ya urais 2020.

Mwanri

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri naye ametoa fora kutokana na utendaji wake, lakini kubwa zaidi ni kauli zake za kusisitiza jambo zilizoonekana kama vichekesho lakini akiwa akionyesha umakini wa kufuatilia mambo.

Miongoni mwa kauli zake zilizotia fora ni ile ya ‘nyoosha mkono jifanye kama unajikuna’ ambayo aliitoa wakati akitaka kujua nani anaona maagizo yake ni ya kipuuzi.

Kauli nyingine ni ile ya ‘Fyekelea mbali’ ambayo pia alikuwa akiwaonya watendaji mkoani humo, ikifuatiwa na kauli ya sasa ya ‘Injia soma ramani’.

Kauli zote hizo zimemfanya Mwanri kuwa maarufu kwenye mitandao ya jamii huku pia akionekana kusimamia vyema maendeleo ya Mkoa wa Tabora.

Biteko

Mwanasiasa mwingine anayechipukia ni Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko aliyeteuliwa Januari mwaka huu baada ya kuongoza kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite.

Biteko aliteuliwa kumsaidia Waziri Angela Kairuki baada ya Wizara hiyo kuundwa ikinyofolewa kutoka kwa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini.

Kamati aliyokuwa akiiongoza Biteko iliundwa na Spika wa Bunge Job Ndugai Juni 2017, akiipa kazi ya kuchunguza Sekta nzima ya Madini ya Tanzanite.

Mbali na Doto Biteko ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wajumbe walikuwa ni pamoja na Mohammed Mchengerwa, Ezekiel Maige, Balozi Adadi Rajabu, Dk Merry Mwanjelwa, Subira Mgalu, Juma Omari, Abdalla Mtolea na Joseph Ole Millya.

Ripoti ya kamati hiyo ilikabidhiwa kwa Rais John Magufuli Septemba 2017 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa kazi alizofanya Biteko ni pamoja na kukamata madini ya vito aina ya Rhodilite yenye uzito wa takribani tani saba yaliyokuwa yamefichwa nyumbani kwa mchimbaji wa madini hayo, Juvenal Mnene ambaye ni mmiliki wa kampuni ya J. J. Mnene & Partners Julai 2018 wilayani Gairo Morogoro.

Zitto

Licha ya umaarufu wake wa muda mrefu, Zitto aliibuka upya mwaka huu pale alipoibua hoja ya Sh1.5 trilioni alizodai kuwa hazijulikani zilipo kutoka na ripoti Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2016/17 iliyotolewa Aprili mwaka huu.

Baada ya Zitto kulipua bomu la Sh1.5 trilioni, Chama cha Mapinduzi kupitia Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole kilijibu ambapo kiongozi huyo alitumia ‘flip chart’ kufanya hesabu kufafanua kuwa hakukuwa na upotevu wa fedha hizo.

Hoja ya Zitto ilimkera Rais Magufuli ambaye katika hotuba yake ya Aprili 20 Ikulu ya Dar es Salaam alikanusha madai hayo. Pia, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alitoa taarifa bungeni Dodoma kufafanua fedha hizo.

Licha ya ufafanuzi wote huo, hoja ya Sh1.5 trilioni iliendelea kushika kasi kwenye mitandao ya jamii kama moto kichakani, jambo lililompa umaarufu Zitto ambaye ni Mbunge pekee katika chama cha ACT Wazalendo.

Nape

Nape aliyetimuliwa uwaziri mapema mwaka 2017 ameendelea kung’ara, mwaka huu akijikita zaidi kutetea wakulima wa korosho.

Nape aliuanzisha mtiti mapema Mei mwaka huu akishikilia shilingi ya aliyekuwa waziri wa kilimo, Dk Charles Tizeba kwa kutoridhishwa na majibu ya Serikali kuhusu fedha za ushuru wa mauzo ya nje ya korosho (export levy).

Wiki moja baadaye Mei 24, Nape aliibua tena hoja hiyo na kumfanya Spika Job Ndugai kutoboa siri ya Waziri Tizeba kulia kama mtoto mbele ya kamati ya bajeti.


Via >>Mwananchi
Share:

WATU WANNE WA FAMILIA MOJA WAPIGWA RISASI NA ASKARI KATAVI

Ndugu wanne wa familia moja katika Kijiji cha Ikongwe, Kata ya Sitalike wilayani Mpanda, wamelazwa Hospitali ya Mkoa wa Katavi, baada ya kudaiwa kupigwa risasi sehemu mbalimbali za miili yao na askari wa Wakala wa Hifadhi wa Misitu (TFS) wa Halmashauri ya Nsimbo.

Diwani wa Kata ya Sitalike, Adamu Cherehani jana alisema tukio hilo lilitokea juzi saa sita mchana na kuzua hataruki kubwa kutoka kwa wananchi.

Aliwataja wanakijiji waliopigwa risasi kuwa ni Josephat Patrick (27) aliyepigwa risasi mbili kifuani, Jofrey Patrick (39),aliyejuruhiwa mkono wa kushoto,Fiberiti Patrick (40), alijeruhiwa mguu wa kushoto, Januari Patrick (22), alipigwa risasi ya bega la kulia na mwingine aliyetambulika kwa jina la Nkuba Sai aliyepigwa risasi mkono wa kushoto .

Diwani Cherehani, alidai chanzo cha wanakijiji hao kushambuliwa kwa risasi ni askari wa TFS waliofika kijijini na kuanza kufyeka mahindi yao kwenye mashamba kwa kile walichodai yamelimwa ndani ya eneo la hifadhi ya Msitu wa Msaginya .

Baada ya kupata taarifa mahindi yao yanafyekwa, wanakijiji hao waliokuwa zaidi ya kumi walifika mashambani na kuwasihi askari hao waache kufyeka mazao yao kwa sababu ndiyo wanategemea kwa chakula na familia zao, lakini waliwagomea.

Alisema askari waliendelea kufyeka mahindi hayo, hali ambayo iliwafanya wanakijiji waanze kuwazomea.

“Haya mahindi yalikuwa yamebakiza mwezi mmoja tu yaive, lakini askari wamefyeka yote, jambo hili linatia uchungu,”alisema.

Kutokana na hali hiyo, wananchi walianza kuwazomea askari hao wakati wanaingia kwenye gari lao aina ya Toyota LandCruser, ghafla wakaanza kurusha risasi ovyo.

Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo (CCM) alisema amesikitishwa na kitendo hicho kwani hawakuwa na sababu ya kutumia nguvu kubwa kiasi hicho kuwakabili wananchi ambao hawakuwa na silaha.

Alisema eneo hilo linalodaiwa mali ya TFS, lilipimwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2002 na kutenganisha maeneo ya hifadhi na shughuli za binadamu

Alisema eneo hilo lilipimwa tena mwaka huu chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kabla ya kuanzishwa Halmashauri ya Nsimbo .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema hatua zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya wahusika.

Alisema alikwenda eneo hilo la tukio kuokota ganda moja la risasi ambayo inaonekana kuwa ni gobore.

Alisema ameagiza kukamatwa mara moja kwa askari wa TFS waliohusika kufanya kitendo hicho ili waweze kuhojiwa na sheria kuchukua mkondo wake wake.
Share:

WABUNGE WA CCM WANAOTAFUTA KIKI KWA MGONGO WA JPM WAONYWA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole amewataka wabunge wa CCM nchini, kuacha kulala usingizi au kutafuta kiki ya kisiasa kwa mgongo wa Rais John Magufuli.


Badala yake, amewataka kuwatumikia wananchi katika majimbo yao na kuiga mfano uliofanywa na mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama wa kujikita katika kusaidia ujenzi wa ofisi za matawi ya chama jimboni humo.

Polepole alitoa kauli hiyo juzi katika mkutano mkuu wa jimbo la Peramiho ambapo pia alikabidhi pikipiki 16 zenye thamani zaidi ya Sh milioni 45 kwa ajili ya makatibu kata wa chama hicho. 

Pia alikabidhi baiskeli 132 kwa ajili ya makatibu wa matawi, bati 835 kwa ajili ya ofisi za matawi na saruji mifuko 1,230 kwa ajili ya matawi hayo na ambavyo vilitolewa na Jenista alisema vifaa hivyo vitakuwa msaada mkubwa kwa viongozi wa kata na matawi katika kutekeleza majukumu yao.


Polepole alisema kuwa jukumu la viongozi wa kata na matawi ni kuhakikisha wanavitunza vifaa hivyo ambavyo ni mali ya chama na kwamba pasitokee kiongozi au mtendaji kutumia vibaya vifaa hivyo ambavyo vimetolewa na mbunge huyo wa jimbo la Peramiho. 

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama alisema katika jimbo hilo kulikuwa na matawi ambayo ofisi zake hazifanani na Chama Cha Mapinduzi ambacho ni kikongwe hapa nchini na duniani hivyo ameamua kwa dhati kusaidiana na wanachama kurekebisha hali hiyo.
Share:

WAZIRI LUHAGA AKOMALIA 'OPERESHENI NZAGAMBA'..KAFICHUA NYAMA MBOVU

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema Serikali haitakubali Tanzania kugeuzwa kuwa dampo la bidhaa za mifugo zilizokwisha muda wa matumizi na kuua uwekezaji kwa manufaa ya watu wachache.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Saalam juzi, wakati wa kutoa matokeo ya ‘Operesheni Nzagamba’ iliyoendeshwa kwa vipindi viwili tofauti, Waziri Mpina alisema kilo 26,295 za bidhaa za nyama na maziwa zimekamatwa,baada ya kuingizwa nchini kutoka nje bila vibali, kulipiwa ushuru wala kuhakikiwa ubora wake.

Pia kilo 2,376 za bidhaa za nyama na maziwa yaliyokwisha muda wa matumizi nazo zikikamatwa zikiuzwa maeneo mbalimbali na kuhatarisha afya za walaji na kuingia katika hatari ya kupata magonjwa makubwa ikiwemo saratani.

“Hatutakubali kuua uwekezaji, viwanda na ajira za Watanzania kwa manufaa ya watu wachache, hatutakubali kuziweka rehani afya za watanzania eti kwa sababu ya uwekezaji operesheni hizi zitaendelea hadi pale wahalifu hao watakapoacha mchezo huu mchafu,” alisema Mpina.

Alisema hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii kuliibuka taharuki juu ya hatua zinazochukuliwa na Serikali dhidi ya wahalifu katika operesheni inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema operesheni hiyo, inayoendeshwa kwa mujibu wa sheria ina lengo la kudhibiti uingizaji holela wa mazao ya mifugo nchini, kudhibiti uuzaji wa mazao ya mifugo, pembejeo na chakula cha mifugo kilichokwisha muda wa matumizi na utoroshaji wa mifugo na mazao yake nje ya nchi. 


Alisema kilo 17,712 za pembejeo za mifugo zilizokwisha muda wa matumizi zilikamatwa, huku kilo 880 za nyama na maziwa ambazo hazina lebo wala taarifa yoyote katika vifungashio pamoja na usajili kutoka mamlaka husika nazo zikikamatwa.

Alisema tani 25,423 za chakula cha mifugo zilikamatwa zikisafirishwa kwenda nje ya nchi bila vibali ambapo katika uhakiki wa hesabu za ulipaji ushuru kwa kampuni chache zilizofanyiwa uhakiki katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/18, ilibainika Sh bilioni 4.25 zilikwepwa kulipwa


Alisema ng’ombe 40,954, mbuzi na kondoo 165,115 nazo
zilikamatwa zikiwa zinatoroshwa kwenda nje ya nchi bila vibali na bila kulipa ushuru wa aina yoyote huku zaidi ya ng’ombe 50,000 zilikamatwa zikiwa zimeingia nchini bila vibali

Katika operesheni hiyo,vifaranga 21,100 na mayai 21,480 yalikamatwa yakiingia nchini bila vibali ambapo yalitaifi shwa na Serikali kisha kuketetezwa.

Alisema licha ya bidhaa zinazoingizwa nchini bila vibali na huku Tanzania ikiwa na mifugo mingi, uagizaji wa bidha za mifugo kutoka nje ya nchi ni mkubwa nchini ambapo uagizaji wa bidhaa za nyama nchini umefi kia thamani ya wastani wa sh. bilioni 10 huku maziwa ikiwa ni wastani wa sh bilioni 30 kwa mwaka.

Waziri Mpina ametaja baadhi ya madhara ya uingizaji holela wa bidhaa hizo nchini ikiwemo kuathiri afya za wananchi kunakoweza kusababisha maradhi sugu ikiwemo saratani.
Share:

KRISMASI YAWA CHUNGU KWA MACHANGUDOA ZANZIBAR

Wamikili wa nyumba saba Zanzibar ambazo ni maarufu kwa kufanyiwa biashara ya ukahaba ‘machangudoa’ wametakiwa kuripoti kwa Kamanda wa Polisi, Mjini Magharibi, Zanzibar ifikapo kesho.

Hatua hiyo kwa wamiliki wa nyumba hizo visiwani humo kunatokana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo kufanya operesheni ya kudhibiti biashara hiyo ambapo watu 22 wanaofanya biashara hiyo walikamatwa katika nyumba hizo zilizoko katika maeneo ya mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud, alitoa agizo hilo baada ya operesheni hiyo.

Akizungumza baada ya operesheni hiyo, Mkuu wa mkoa huyo, alisema wamiliki wa nyumba hizo wanatakiwa kuripoti ifikapo saa nne asubuhi na atakayekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua.

Alizitaja nyumba hizo ni zilizoko katika maeneo ya Raha Leo, Mwembe Shauri, Miembeni, Kikwajuni Juu na Kilimani na kwamba kamati ya ulinzi na usalama imejiridhisha kwenye nyumba hizo zinafanywa biashara za ukahaba.

Alisema biashara hiyo si halali, hivyo aliwataka wanaofanya biashara hiyo kuacha na watafute shughuli nyingine ya kujipatia kipato halali.

Wakati wamiliki wa nyumba hizo Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar wakitakiwa kuripoti polisi kesho, Polisi mkoani Singida imefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 11 wakiwemo wanawake 10 na mwanaume kwa tuhuma za kujihusisha na kufanya biashara ya ukahaba mjini Singida.


Kamanda wa Polisi, Mkoa wa huo , Sweetbert Njewike, alisema watuhumiwa hao walikamatwa kutokana na misako wa kubaini vitendo vya uhalifu na wahalifu wa makosa mbalimbali katika Mji wa Singida na viunga vyake.

Alisema msako huo ulifanyika Desemba 18 na 19, mwaka huu, katika maeneo ya Serengeti, kata ya Majengo na kufanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa hao.
Share:

Tuesday, 25 December 2018

CCM YATUMIA UJANJA KUFANYA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO MWAKANI

  Ikiwa leo December 25 Waumini wa Dini ya Kikristo Nchini wanaungana na Wakristo Wengine Duniani Kote Kusherehekea Sikuku ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo Ambapo Wananchi Mjini Njombe wametoa Wito kwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Humo Kuhakikisha Kuwa wanaendelea Kuisimamia na Kuitetea Serikali ya Awamu ya Tano. Wananchi hao waliokuwa Wakizungumza na Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Ndg. Erasto Ngole (Shikamoo Parachichi) Kwa nyakati Tofauti katika Maeneo ya Stendi kuu, Ramadhani, Mjimwema, Na maeneo Mengine Mjini Njombe, Walimweleza Kuwa Wanaimani…

Source

Share:

BERNARD MEMBE AIBUKIA KANISANI MISA YA KRISMASI

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya awamu ya nne, Bernard Membe amekuwa miongoni mwa waumini wa dini ya kikristo walioshiriki ibada ya Krismasi katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.

Membe ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Mtama, ameshiriki misa hiyo leo Jummane Desemba 25, 2018 iliyoongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa.

Katika ibada hiyo, Membe ambaye hivi karibuni alizua gumzo kati yake na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally, alionekana kwenye safu ya mbele akiwa amevaali suti ya rangi nyeusi.

Membe alikuwa gumzo hivi karibuni baada ya Dk Bashiru kutamka hadharani kuwa waziri huyo wa zamani anakwamisha mikakati ya urais ya 2020.

Ibada hiyo ilikuwa ya pili na ilianza saa nne, baada ya ile asubuhi kuhudhuriwa na mke wa Rais Janeth Magufuli.

Akitoa mahubiri katika ibada hiyo, Askofu Nzigilwa amesema Sikukuu ya Krismasi ina neema ya matunda manne na ni vyema waumini wa dini wakayazingatia.

Amesema matunda hayo kuwa ni upatanisho, furaha, umoja na amani na kusema ni vyema waumini wa dini wakayatilia mkazo wakati wakisherehekea Krismasi.

“Tunaishi dunia yenye misuguano, kuna watu hawaongei katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya kazi tena wengine pia wanaishi nyumba moja halafu tunasema tunasheherekea Krismasi, sikukuu gani hiyo wakati hakuna upatanisho?” Alihoji Askofu Nzigilwa.

Na Bakari Kiango, Mwananchi
Share:

ASKOFU MALASUSA APATA HOFU ONGEZEKO LA UTITIRI WA TALAKA

Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa amedai kuwa kwa sasa jamii imekosa hali ya upendo hali inayosababisha kuongezeka kwa matukio ya mahusiano mengi kuvunjika.

Askofu Malasusa amesema kauli hiyo Desemba 25, 2018 katika ibada ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam ambapo amesema wana ndoa wengi wanahofu na mahusiano.

“Siku hizi talaka zimezidi jamii haina upendo wala hofu ya Mungu, hofu imejaa katika ulimwengu, wengi waliopo katika ndoa hawana hakika kama wataendelea,’’ amesema.

Aidha ameongeza kuwa “malaika anasema usiogope nitawaletea habari njema, tena katika aya yetu ya siku ya leo tunasema tumepewa mtoto mwanamume, yeye yupo tayari kubadilisha mitazamo yetu kutuondoa katika hofu na kuwa wajasiri katika maisha yetu.”

Mamilioni ya waumini wa dini ya kikristo Duniani leo Desemba 25 wanaadhimisha sikukuu ya Krismasi ikiwa kukumbuka ya siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Share:

ALIKIBA ATOA OFA KWA MWANADADA ALIYEMLILIA

Msanii Alikiba ameamua kutoa ofa kwa mwanadada Emiliana Mgema aliyemlilia juzi kwenye tamasha la Tigo Fiesta

Katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Ali Kiba ametangaza ofa hiyo huku akiwa ameweka video ya dada huyo akiwa anahojiwa huku analia na kueleza hisia zake jinsi anavyompenda msanii huyo.

Ali Kiba ameandika “Asante sana dada anayemjua huyu dada amwambie nina tiketi yake ya bure na mofaya zake za kutosha tarehe 29 /12 Next Door Arena,” aliandika Kiba wakati anatangaza ofa hiyo kwa Emilina ambapo anatarajia kufanya shoo yake aliyoipa jina la ‘Funga mwaka na KingKiba.’

Emy amesema ameanza kumpenda Ali Kiba tangu alipotoa kibao chake cha Macmuga ambapo kipindi hicho alikuwa akisoma darasa la saba Shule ya Msingi Nata mkoani Tabora na kuanzia hapo amekuwa akimfuatilia hadi leo na hakuna ngoma yake hata moja aliyowahi kuiona mbaya.
Share:

NYOTA YA MCHEZAJI CHAMA YAZIDI KUNG’AA AINGIA KWENYE ORODHA HII YA AFRIKA

Na karoli Vinsent NYOTA ya Mchezaji wa Mbingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara,Timu ya Simba,Clatous Chama, inazidi kung’aa kwenye kimataifa ndivyo naweza kusema baada ya kushika nafasi ya pili ya kwenye orodha ya wachezaji waliofunga matatu na kuendelea katika michuano ya ligi ya Mabindwa Afrika. Mchezaji huyo mwenye “Udambwe Udambwe” wa hatari anapokuwa uwanjani ameshika nafasi ya pili kwenye orodha ambayo yupo nyuma na Moataz Al-Mehdi anayekipigia kwenye timu la Al nasr. Katika Orodha hiyo nafasi ya tatu inashikwa na Mshambuliaji hatari ambaye hana huruma anapokuwa kwenye gori la timu pinzani,Meddei…

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger