Mjumbe wa Marekani kwenye baraza la usalama la umoja wa Mataifa Samantha Power.
Marekani
imependekeza azimio kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kutaka
Sudan Kusini kuwekewa vikwazo vya kununua na kuingiza silaha.
Aidha, azimio
hilo linapendekeza watu binafsi kutoka upande wa serikali inayoongozwa
na rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar kuwekewa vikwazo.
Marekani
inasema kwamba kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar, mkuu
wake wa majeshi na waziri wa habari wawekewe vikwazo na Umoja wa Mataifa
kwa kuchochea vita nchini humo.
Kwa
mujibu wa ujumbe uliopatikana na AFP Machar, mkuu wa majeshi ya rais
Salva Kiir, Paul Malong na waziri wake wa habari Michael Makuei wako
kwenye orodha nyeusi ya vikwazo.
Chini ya
hatua iliyopendekezwa, Macha ambaye anapatiwa matibabu nchini Afrika
Kusini na maafisa hao wawili watakabiliwa na vikwazo vya kusafiri na
mali zao kuzuiwa.
Hatua hii
imekuja baada ya watalaam na Umoja wa Mataifa kuonya kuwa huenda
kukatokea kwa mapigano na mauaji ya halaiki nchini humo katika siku
zijazo ikiwa hatua haitachukuliwa.
Azimio
hilo sasa linasubiri kura kutoka kwa wanachama wa Baraza hilo, licha ya
kuwepo kwa wasiwasi huenda Urusi ikatumia kura yake ya Veti na kuzuia
kupitishwa kwa azimio hilo
Mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na Vijana walioathirika
na madawa ya kulevya (hawapo pichani) alipotembelea kituo cha Sober House cha
kurekebisha waathirika wa dawa za kulevya kilichopo Vijibweni Kigamboni
wakati wa ziara yake ya siku 10 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwaajili
yakusikilza kero za wananchi. PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
Kulia ni Kijana mmoja aliyeko kwenye kituo Sober House cha
kurekebisha waathirika wa dawa za kulevya, kilichpo Vujibweni
Kigamboni, akimuonyesha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
tumbo lake lilivyobaki na makovu ya kutisha kutokana na operesheni
aliyofanyiwa kutolewa dawa za kulenya tumboni
Baadhi ya
Vijana walioathirika na madawa ya kulevyo wakipiga makofi kumpongeza
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akipokea zawadi kutoka kwa Mmiliki wa Kituo cha vijana wa Sober House,Nuru Saleh jana jijini Dar es Salaam
Katibu
Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akiongoza
Wachezaji wa timu ya Taifa ya mchezo wa kabadi walipowasili jijini Dar
es salaam wakitokea nchini India kwenye mashindano ya mchezo huo
uliofanyika hivi karibu nchini humo .
Wachezaji
wa timu ya Taifa ya mchezo wa kabadi wakiwasili jijini Dar es salaam
wakitokea India kwenye mashindano ya mchezo huo uliofanyika hivi karibu
nchini humo ambapo Tanzania imetolewa kwenye mashindano hayo .
Katibu
Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akiongea na
waandishi wa habari mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu
Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea nchini India kwenye mashindano ya
mchezo wa kabadi uliofanyika hivi karibu nchini humo .
Na Ally Daud-Maelezo.
SERIKALI
imekusudia kuboresha mazingira rafiki ya biashara nchini ili kuwezesha
utashi wa Serikali ya Awamu ya Tano katika kuifanya Tanzania kuwa nc hi
ya uchumi unaoongozwa na viwanda kama inavyoelekeza Dira ya Maendeleo ya
Taifa ya Mwaka 2025.
Akizungumza
hayo wakati wa uzinduzi wa kamati ya kuboresha mazingira ya biashara
Tanzania jijini Dar es salaam Waziri wa Viwanda ,Biashara na uwekezaji
Charles Mwijge amesema kuwa Serikali imejidhatiti kuweka mazingira
rafiki kwa maendeleo ya biashara nchini.
“Ili
kuweza kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya uchumi unaoongozwa na viwanda kama inavyoelekeza
Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025 ni lazima kuboresha mazingira
ya biashara ambayo ni rafiki kwa wawekezaji” alisema Mwijage.
Aidha
Waziri Mwijage amesema kuwa maboresho ni kusaidia kupata mikopo kwenye
mabenki na taasisi za kifedha zitakazosaidia uwekezaji na uzalishaji
wenye tija kwa maendeleo ya uchumi wa taifa letu.
Waziri
Mwijage amesema kuwa Serikali itahakikisha inaboresha mazingira rafiki
ya biashara ili kufikia lengo kwa kurahisisha utoaji wa vibali vya
ujenzi wa viwanda kwa wawekezaji wa nje na wa ndani ili kufanya sekta ya
viwanda kua endelevu Zaidi.
Mbali na
hayo Waziri Mwijage amesema kwamba kwa kuwa Serikali imeamua kujenga
uchumi wa viwanda basi itahakikisha inarahisisha suala la uboreshaji wa
mazingira rafiki ya biashara nchini .
Kamati
hiyo iliyozinduliwa rasmi na Waziri Mwijage ina kazi ya kufanya
uchambuzi wa kina katika mazingira ya kufanya biashara nchini na kutoa
mapendekezo kwa Serikali juu ya kuboresha mazingira rafiki ya biashara
nchini
Wanafunzi walilipa maelfu ya madola kwa masomo baada ya kuhadaiwa kwamba watafunzwa siri juu ya uwekezaji.
Wakili wa
rais mteule wa Marekani Donald Trump ametatua kesi ya mamilioni ya
madola iliyokuwa inamkabili mteja wake ili apate nafasi ya kutekeleza
majukumu yake mapya na kuangazia changamoto zinazoikabili Marekani.
Trump
alikuwa ameshtakiwa na wanafunzi wa zamani kwa ubadhirifu wa pesa katika
chuo kikuu cha Trump,ambapo wanafunzi walilipa maelfu ya madola kwa
masomo baada ya kuhadaiwa kwamba watafunzwa siri juu ya uwekezaji
Rais huyo
mteule amekuwa akikanusha madai hayo lakini hatimaye ameamua kulipa
dola milioni ishirini na tano ili kumaliza kesi hiyo. Mpango huo hata
hivyo haumuhitaji kukiri kwamba alifanya makosa
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua
jambo kwa wananchi wa kijiji cha Mang’oto Wilayani Makete ambapo
aliwataka walioko kwenye hifadhi ya barabara wabomoe nyumba zao na
kutafuta nyumba mbadala ili kuwezesha zoezi la ujenzi wa barabara kuanza
na zoezi la fidia lifuate baadaye.
Mbunge wa
Makete Profesa, Norman Sigala akifafanua jambo kwa wananchi wa Jimbo
hilo kuhusu umuhimu wa kutafuta nyumba mbadala ili kupisha ujenzi wa
barabara ya Njombe –Makete KM 109 utakaoanza hivi karibuni.
Mkuu wa
Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi (kulia), akimshukuru Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kufuatia hatua ya
ujenzi wa daraja la Ruhuhu linalounganisha mkoa wa Njombe na Ruvuma.
Wanananchi
wa kijiji cha Mang’oto Wilayani Makete wakimsikiliza Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Hayupo pichani).
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amewataka
wananchi waliowekewa alama za kubomoa nyumba zao zilizopo pembezoni mwa
barabara ya Njombe-Makete hadi Mbeya KM 205 waanze kuhama kwenye nyumba
hizo ili kupisha zoezi la ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Akizungumza
mara baada ya kukagua barabara hiyo Eng. Ngonyani amesema awamu ya
kwanza ya ujenzi wake itaanza wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya
kupatikana mkandarasi na mkandarasi mshauri ambayo itahusisha sehemu ya
Njombe hadi Makete KM 109.4.
“Kuweni
waadilifu waliowekewa alama za kijani kwenye nyumba zao watalipwa fidia
lakini wenye alama nyekundu hawatalipwa hivyo ni vizuri wote kutafuta
maeneo mengine ya makazi ili kuepuka usumbufu mara zoezi la ujenzi
litakapoanza”. Amesema Eng. Ngonyani.
Eng.
Ngonyani amesema kwa kuwa kazi ya ujenzi na ulipaji fidia zinagharamiwa
na Serikali ni vema zoezi la ujenzi wa barabara likaanza wakati Serikali
ikitafuta fedha kwa ajili ya fidia.
“Ili
tuweze kufanikiwa katika mambo yote tumeona tuanze na zoezi lenye
gharama kubwa ambalo ni ujenzi wa barabara kisha zoezi la fidia
litaendelea wakati ujenzi wa barabara unaendelea”. amesisitiza Eng.
Ngonyani.
Naye Mkuu
wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi ameishukuru Serikali kwa jitihada
za ujenzi wa daraja la Ruhuhu linalounganisha Mkoa wa Njombe na Ruvuma
na ameiomba Serikali kuangalia namna ya kuweka lami barabara inayokwenda
kwenye hospitali ya Mkoa wa Njombe na ile inayoenda hospitali ya
misheni ya Ikonda wilayani Makete ili kuwezesha barabara hizo kupitika
kwa urahisi wakati wote wa mwaka.
Katika
hatua nyingine Mbunge wa Makete Profesa, Norman Sigara amemuomba Naibu
Waziri Eng. Ngonyani kuhakikisha Mkandarasi anayejenga barabara ya
Njombe –Makete na Makete –Mbeya kupitia Kitulo anaanza kazi iyo kwa
wakati ili kuongeza kasi ya wananchi kubomoa nyumba zao katika maeneo ya
hifadhi ya barabara na hivyo kuunganisha kirahisi mkoa wa Njombe na
Mbeya kwa barabara ya lami.
Naibu
Waziri Ngonyani yupo katika ziara ya kukagua Miundombinu ya Barabara,
Bandari na Mawasiliano katika mikoa ya Nyanda za juu Kusini ambapo
tayari amekamilisha ziara yake katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Ruvuma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli nchini TRL, Masanja Kadogosa (kulia) kuhusu ujenzi wa
reli inayounganisha reli ya kati na kiwanda cha Kiluwa Still Group
cha Mlandizi Pwani Novemba 19, 2016 . Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WAZIRI
mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali imefanikiwa kuondoa urasimu
katika baadhi ya halmashauri nchini na idara husika katika kutoa hati
miliki kwenye maeneo ya uwekezaji ili kukuza sekta ya uwekezaji.
Aidha
Majaliwa amefarijika kukuta njia ya reli yenye urefu wa km 4.3 kutoka
reli ya kati kuelekea kiwanda cha kutengeneza nondo cha kilua kilichopo
Kibaha Vijijini mkoani Pwani imekamilika kwa asilimia 100.
Sambamba
na hayo amezisihi halmashauri nchini kutoa Ushirikiano kwa wawekezaji
ili kuongeza ari ya kushawishika kuongeza viwanda.
Majaliwa
aliyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea maendeleo ya kiwanda cha
Kilua cha Mlandizi na kiwanda cha kuunganisha magari na zimamoto cha
Equator suma jkt Ruvu.
Alisema ameridhishwa na hatua zinazoendelea katika kukamilisha ujenzi wa viwanda hivyo.
Majaliwa
alitoa wiki mbili kwa mkandarasi wa umeme katika kiwanda cha kilua
kuhakikisha anakamilisha kufikisha umeme wa uhakika kiwandani humo.
Alieleza
kuwa viwanda hivyo vimefikia kwenye hatua nzuri kwani vimekamilika kwa
asilimia 80 na vyote vinatarajiwa kuanza kazi mapema mwaka 2017.
Hata
hivyo alisema licha ya serikali kuondoa urasimu ulipokuwa ukilalamikiwa
sasa halmashauri ziendelee kutenga maeneo, kupima maeneo ili kufungua
milango ya uwekezaji.
Majaliwa alisema serikali imedhamiria kujenga viwanda na kufufua ambavyo vilikufa .
Aliiupongeza
uongozi wa mkoa wa Pwani kwa kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu
ya tano chini ya rais John Magufuli kujenga viwanda na kuvuta
wawekezaji.
“Kiwanda
hicho ni mradi mkubwa wenye thamani ya zaidi ya bil 200 mara utakapo
kamilika utazalisha tani 2,000 na kuajili ya watu 300-800’
“Awamu
ya kwanza ya kiwanda hiki kimegharimu dola za kimarekani mil. 45 sawa
na sh. bil. 90 za kitanzania, na awamu ya pili kitagharimu zaidi ya dola
milioni 100 sawa na zaidi ya bil 200, mitambo imefungwa na kipo
vizuri,hivyo alimpongeza mwekezaji mzawa Mohammed Kilua”alielezea.
Waziri
mkuu alisema mradi huo utakapoanza kazi utaliingizia mapato taifa kwa
kiasi kikubwa ,kuwezesha ajira kwa wazawa na kuwaingizia kipato
wajasiliamali.
Alisema mkoa wa Pwani unaangaliwa kupeleka viwanda na anashukuru uongozi wa mkoa na kupokea wawekezaji.
Kuhusu kiwanda cha kuunganisha magari na zimamoto Majaliwa alisema ni kiwanda mkombozi nchini.
Majaliwa alisema kwa kuunganisha matrekta na zimamoto kutarahisisha kupata kwa gharama nafuu vyombo hivyo vya moto nchini.
Nae waziri wa uchukuzi, pro. Makame Mbalawa aliomba reli hiyo itumike kwa matumizi lengwa.
Pro.
Mbalawa alielezea viwanda vinavyohitajika njia za reli zinaboreshwa na
kujengwa lakini pia ni jukumu la wawekezaji hao kuzitunza na kuzitumia
vyema.
Mkuu
wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,alisema serikali mkoani
hapo imedhamiria kuongeza wawekezaji na ongezeko la viwanda ili kuongeza
ajira hususan kwa kundi la vijana.
Alisema
wapo baadhi ya wananchi waliotakiwa kupisha reli hiyo ambao wanadai
fidia ya sh. mil 95.726 na halmashauri inadai sh. mil 307.206.
Mhandisi Ndikilo alisema mkoa wanayotaarifa na wanaendelea na mazungumzo ili haki yao walipwe kwa wakati.
Alisema wananafasi kubwa ya kufanikisha nchi kuwa ya viwanda kwa kushirikiana na wamiliki wa viwanda.
Mhandisi
Ndikilo alisema kuwa kwa sasa mkoa wa Pwani ajenda yake ni kuhakikisha
unakuwa mkoa wa viwanda na hilo linawezekana kwa kuwa na viwanda vingi
vya kuzalisha bidhaa mbalimbali.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa,
alisema waziri mkuu alitoa agizo wakamilishe reli hiyo na sasa
wamemalizia.
Alisema ujenzi huo umetumia sh. Mil 863 kwa kutumia mafundi wa ndani gharama ambayo ni ndogo.
Kadogosa alielezea kwamba wangetumia mafundi wa nje gharama ingekuwa kubwa.
Alisema licha ya kumaliza reli hiyo lakini kiwanda hicho cha kilua kimeomba tena kuongezewa reli nne za ziada.
Mkurugenzi wa kiwanda hicho Mohamed Kilua alisema wanatarajia kujenga kwenye eneo hilo viwanda vingine vinne.
Alitaja viwanda vinavyotarajiwa kujengwa kuwa ni kiwanda cha kutengeneza pikipiki, gemsum, tissues na nguzo za umeme.
Kilua alisema kukamilika kwa kiwanda hicho kinaliingizia pato taifa bil.25 kwa mwaka na kuzalisha nondo tani 2,000 kwa siku
MTU MMOJA AMEUAWA NA WATU WANAOZANIWA KUWA NI MAJAMBAZI KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA WILAYANI NYAMAGANA.
MWANAMKE MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMFANYIA VITENDO VYA UKATILI MJUKUU WAKE WILAYANI NYAMAGANA.
MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLSI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MTOTO WA DARASA LA TATU WILAYANI NYAMAGANA.
KWAMBA
TAREHE 17.11.2016 MAJIRA YA SAA 20:30HRS KATIKA MTAA WA NKURUMA KATA NA
WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA MWANAMKE MWENYE
ASILI YA KIASIA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA VASANTBEN RAMANBHAI, MIAKA 48,
MUHINDI, MAMA WA NYUMBANI NA MKAZI WA MTAA WA RUFIJI, ALIUAWA KWA
KUPIGWA RISASI MOJA SEHEMU YA MGONGONI NA WATU WANAOZANIWA KUWA NI
MAJAMBAZI WALIVAMIA DUKA LA MIAMALA YA FEDHA YA M –PESA, TIGO PESA NA
AIRTEL MONEY NA BIDHAA NYINGINE MBALIMBALI MALI YA LAURENT PETER NA
KUFANIKIWA KUPORA FEDHA NA SIMU TANO.
INADAIWA
KUWA MAREHEMU ALIKWENDA DUKANI HAPO KUPATIWA HUDUMA, NDIPO GHAFLA
WALITOKEA MAJAMBAZI WATATU WAKIWA NA PIKIPIKI MMOJA KATI YAO AKIWA
SILAHA NA KUFYATUA RISASI KADHAA HEWANI, NDIPO RISASI MOJA ILIMPATA
MAREHEMU SEHEMU YA MGONGONI NA KUFARIKI DUNIA . AIDHA KATIKA TUKIO HILO
MAJAMBAZI HAO WALIFANIKIWA KUPORA FEDHA AMBAZO HAIJAFAHAMIKA NI KIASI
GANI HADI SASA NA SIMU TAN0, SIMU TATU KATI YA HIZO ZILIKUWA ZIKITUMIKA
KUFANYA KAZI YA KUTUMA MIAMALA YA FEDHA NA NYINGINE MBILI ZIKITUMIKA
KATIKA MAWASILIANO YA KAWAIDA, ZOTE MALI ZA MWENYE DUKA.
JESHI LA
POLISI LIPO KATIKA UPELELZI NA MSAKO WA KUHAKIKISHA WATU HAO
WANAKAMTWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA, MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA
UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA
MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO
SENGA ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUTULIA
NA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KATIKA KUFANIKISHA
KUWAKAMATA WATU HAWA WENYE NIA OVU DHIDI YA USALAMA WA WANANCHI NA MALI
ZAO. TUNAENDELEA KUWASIHI WANANCHI WATULIE WASIWE NA MASHAKA JESHI LAO
LA POLISI LIPO VIZURI KUHAKIKISHA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO
UNAIMARISHWA.
KATIKA TUKIO LA PILI
MNAMO
TAREHE 11.11.2016 MAJIRA YA 20:00HRS KATIKA MTAA WA MAHINA KATA YA
BUTIMBA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA
ALIYEJULIKANA KWA JINA LA AMINA HAMISI MIAKA 56 MKAZI WA MAHINA
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUMLAZIMISHA KULA KINYESI
MJUKUU WAKE AITWAYE REHEMA SADIKI MIAKA 07, KITENDO AMBACHO NI UKATILI
DHIDI YA MTOTO NA NI KOSA KISHERIA.
INADAIWA
KUWA SIKU TAJWA HAPO JUU MTOTO HUYO ALIKWENDA CHOONI KUJISADIA NA
KUSHINDWA KUMWAGIA MAJI ILI KUONDOA KINYESI CHAKE , NDIPO BIBI YAKE ILI
KUMUADHIBU ALIMUAMURU KULA KINYESI HICHO, KITENDO AMBACHO MTOTO HUYO
ALIKITEKELEZA.
AIDHA
BAADA MTUHUMIWA KUFANYA UKATILI HUO KWA MTOTO. RAIA WEMA WALITOA
TAARIFA POLISI AMBAO WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA
MTUHUMIWA HUYO. UPELELEZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI
MARA MOJA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO
SENGA ANATO WITO KWA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA AKIWATAKA KUSHIRIKIANA KWA
PAMOJA NA JESHI LA POLISI KATIKA KUDHIBITI VITENDO VYA UKATILI HASA KWA
WATOTO KATIKA MKOA WETU. ALIONGEZA KUWA UKATILI NI KOSA KISHERIA HIVYO
WANANCHI WAACHE KUFANYA VITENDO HIVYO NA WATAKAO BAINIKA SHERIA
ITACHUKUA MKONDO WAKE.
KATIKA TUKIO LA TATU.
KWAMBA
TAREHE 16.11.2016 MAJIRA YA SAA 19:00HRS KATIKA MTAA WA NYABUROGOYA KATA
YA NYEGEZI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTOTO JINA
TUNALIHIFADHI MWENYE UMRI WA MIAKA 11, MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU
SHULE YA MSINGI NYABUROGOYA ALIBAKWA NA MTU ALIYEJULIKANA KWA JINA LA
JAMES CHIRAGWIRE MIAKA 42, AFISA MTENDAJI KATA YA MKUYUNI NA
KUMSABABISHIA MAUMIVU MAKALI KATIKA SEHEMU ZAKE ZA SIRI, KITENDO AMBACHO
NI KOSA LA JINAI.
INADAIWA
KUWA MTUHUMIWA ANAISHI JIRANI NA NYUMBANI KWA MTOTO HUYO ANAYEISHI NA
MAMA YAKE MZAZI, AIDHA INASEMEKANA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA NA MAZOEA YA
KUMCHUKUA MTOTO HUYO NA KUINGIA NAE NDANI KWAKE NA KUMPATIA FEDHA NA
ZAWADI NDOGONDOGO NDIPO SIKU HIYO ALIPOFIKA NYUMBANI KWAO, MTOTO
ALIMKUTA PEKE YAKE NDIPO ALIMCHUKUA MTOTO HUYO NA KUMFUNGA KITAMBAA
USONI KISHA AKAINGIA NAE NDANI KWAKE NA KUMFANYIA UKATILI HUO.
AIDHA
MTOTO AMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUBAINIKA KWAMBA KWELI
AMEINGILIWA KIMWILI, MTOTO YUPO HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE
AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, MTUHUMIWA WA UHALIFU HUO AMEKAMATWA, AIDHA
JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, PINDI
UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO
SENGA ANATOA WITO KWA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA, AKIWATAKA KUWA MAKINI
WAKATI WOTE NA WATOTO WADOGO WASIACHWE PEKE YAO ILI KUEPUSHA VITENDO
KAMA HIVI, LAKINI PIA ANAWASIHI WANANCHI KUTOA TAARIFA POLISI ZA WATU
WENYE TABIA KAMA HIZI ILI HATUA STAHIKI ZIWEZE KUCHUKULIWA.
Mtuhumiwa wa mauaji ya Rwanda, Jean Claude Seyoboka, wakati alipowasili KIgali.
Afisa wa
zamani kwenye jeshi la Rwanda, amewasili jijini Kigali baada ya
kusafirishwa kutokea nchini Canada, akituhumiwa kuwa alihusika kwenye
mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, ambayo watu laki 8 waliuawa.
Mwendesha
mashtaka wa Rwanda, Jean-Bosco Mutangana, amethibitishwa kurejeshwa
nchini humo kwa mtuhumiwa Jean Claude Seyoboka, usiku wa kuamkia leo,
ambapo sasa atajibu tuhuma za mashataka ya mauaji yanayomkabili.
Seyoboka,
ambaye alikuwa ni Luteni wa pili kwenye jeshi la Rwanda, anatuhumiwa
kuhusika na mauajiya watusi zaidi ya 72 jijini Kigali na pia anadaiwa
kuwa alihudhuria vikao vilivyoidhinisha mauaji hao.Machafuko hayo
yaliyodumu kwa miezi minne, ambapo watu zaidi ya laki 8 waliuawa wengi
wakiwa watusi, yalichangiwa baada ya kudunguliwa kwa ndege iliyokuwa
imembeba rais wa nchi hiyo Juvenal Habyarimana ambaye alikuwa Muhutu,
mwezi April mwaka 94.
Seyoboka
aliwasili nchini Canada mwaka 1995, ambako alipatiwa hifadhi ya kudumu
nchini humo mwaka mmoja baadae.Hata hivyo kibali cha hifadhi yake
kilitenguliwa miaka kumi baadae, baada ya kutolewa ushahudi kwenye
mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda iliyokuwa jijini
Arusha, Tanzania na kumuhusisha na mauaji hayo.
Mamlaka
nchini Rwanda zilitoa waranti ya kukamatwa kwa Seyoboka mwaka huu,
lakini alipigana kupinga kurejeshwa nchini mwake kwa kile alichosema
anahofia usalama wake na mateso.
Seyoboka
anakuwa mtuhumiwa wa pili wa mauaji ya kimbari kusafirishwa kutoka
nchini Canada, baada ya mwanasiasa wa zamani wa nchi hiyo Leon Mugesera
kurudishwa nchini Rwanda mwaka 2012.
Mugesera
alihukumiwa kifungo cha maisha jela, mwezi April mwaka 1994 kwa madai
ya kuhusika kwenye mauaji ya maelfu ya raia.Juma lililopita pia,
mwendesha mashtaka wa Uholanzi, alithibitisha kuwa raia wawili wa Rwanda
ambao ni watuhumiwa wa mauaji hayo, nao watarejeshwa nchini mwao.
Nchi
ya Rwanda iliomba kurejeshwa nchini humo kwa raia wake Jean-Claude
Lyamuremye na Jean-Baptiste Mugimba, mwaka 2012 na 2013, ili warudi
kukabiliana na tuhuma za kesi za mauaji na uhalifu dhidi ya binadamu
Viongozi
wa Ulaya wako Berlin kutaka kuhakikishiwa na Rais Barack Obama wa
Marekani juu ya mkondo ambao yumkini ukafuatwa na rais mteule wa
Marekani Donald Trump kutokana na ahadi zake kuweza kutibua mfumo wa
dunia,
Rais
Obama amekaririwa akisema "Kujitolea kwetu kwa Ulaya ni kwa kudumu na
misingi yake iko katika maadili tunayoshirikiana maadili ambayo Angela
ameyataja,kujitolea kwetu kwa demokrasia,kujitolea kwetu kwa utawala wa
sheria,kujitolea kwa utu wa watu katika nchi zetu na katika dunia.
Muungano wetu wa washirika wetu wa NATO umekuwa msingi wa sera ya kigeni
ya Marekani kwa takriban miaka sabini katika nyakati mbaya na nzuri na
kwa kupitia marais wa vyama vyote viwili na kwa sababu Marekani ina
utashi wa msingi kwa utulivu na usalama wa Ulaya."
Rais
Barack Obama wa Marekani alitowa kauli hiyo katika mkutano wa pamoja na
waandishi wa habari mjini Berlin hapo Alhamisi (17.11.2016) ambao pia
ilihudhuriwa na mwenyeji wake Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.
Fadhaa ya
kuchaguliwa kwa Trump imewatia wasi wasi viongozi wa Ulaya kutokana na
kiongozi huyo kuhoji mkataba wa usalama uliodumu kwa takriban miaka
sabini wa washirika wa Marekani chini ya kivuli cha Jumuiya ya Kujihami
ya NATO pamoja na kuahidi kujitowa katika mikataba iliopatikana kwa
tabu ya mabadiliko ya tabia ya nchi na kudhibiti mpango wa nyuklia wa
Iran.
Kujipendekeza kwa Putin
Kujipendekeza
kwake kwa Rais Vladimir Putin wa Russia pia kumezusha masuali juu ya
msimamo wake juu ya hatua ya Russia kumuunga mkono Rais Bashar al Assad
katika vita vya Syria na halikadhalika dhima ya Russia katika mzozo
mashariki mwa Ukraine.
Kabla ya
kufanyika kwa mazungumzo hayo Obama alikuwa na matumaini ya hadhari
kwamba Trump anaweza kubadili msimamo wake mara ataposhika wadhifa huo
wa urais.Amesema mtu inabidi awe makini akiwa katika wadhifa huo
venginevyo hutoweza kudumu kwa muda mrefu kwani matatizo yatakuja
kukuumbuwa.
Obama
amesema anatumai kwamba rais mteule atakuwa na mtizamo ule ule wa tija
kutafuta nyanja ambapo wanaweza kushirikiana na Russia pale maadili
yao, utashi wao vinakwenda sambamba lakini rais mteule atakuwa tayari
kusimamama dhidi ya Russia pale inapokiuka maadili yao na kanuni za
kimataifa.
Kubadilishana mawazo
Mkutano
wa leo kati ya Obama na viongozi wa Uingereza, Ufaransa,
Ujerumani,Italia na Uhispania ni wa kwanza kufanyika tokea kuchaguliwa
kwa Trump.
Mkutano
huo utatowa nafasi ya kubadilishana mawazo hadharani kwa njia isio rasmi
juu ya masuala muhimu ya kimataifa mathlan mada nzito ya mapambano
yanayongozwa na Marekani dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu
nchini Syria na Iraq halikadhalika suala la mzozo wa wahamiaji barani
Ulaya.
Obama
amesema Umoja wa Ulaya unaendelea kuwa mojawapo ya mafanikio makubwa ya
kisiasa na kiuchumi duniani mafanikio ambayo hayapaswi kuchukuliwa
kijujuu