APPLICANTS SELECTED FOR ADMISSION INTO PhD DEGREE PROGRAMMES
APPLICANTS SELECTED FOR ADMISSION INTO PhD DEGREE PROGRAMMES
The University of Dodoma (UDOM) wishes to announce the names of
candidates selected for admission into various PhD programmes for the
academic year 2016/17.
Admission letters for successful candidates are available in UDOM
Graduate studies offices at the main administration building, Office No.
124, Third Floor.
For enquiries please visit UDOM Graduate studies offices at the main
administration building, Office No. 131,Third Floor
or send email through udomgsce@yahoo.com List of Successful PhD Applicants 2016-2017 BATCH II
WATU
13 wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la Super Shem lenye
namba za usajili T 874 CWE lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Mwanza na
Hiace yenye namba T 368 CWQ iliyokuwa ikitoka Jijini Mwanza kuelekea
Wilaya ya Kwimba.
Katika
ajali hiyo mfanyabaishara ndogo ndogo maarufu machinga, Peter Tobari,
aliokoa maisha ya abiria zaidi ya 30 na kumsaidia dereva wa basi la
Super Shem ambaye alikuwa amekandamizwa miguu na basi hilo baada ya
kugongana na Hiace.
Ajali
hiyo imetokea siku mbili baada ya ile ya basi la Kampuni ya New force
iliyotokea mkoani Njombe ikihusisha basi lenye namba T 429 DEU
lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Songea mkoani Ruvuma, ambapo
watu 12 walifariki dunia na wengine 28 kujeruhiwa vibaya. Katika ajali
ya Mwanza, gari dogo aina ya Hiace liligongana uso kwa uso na basi la
Super Shem na kusababisha vifo hivyo na wengine 10 kujeruhi.
Ajali
hiyo imetokea umbali wa mita 200 kutoka kituo kidogo cha mabasi cha
Hungumalwa njia panda ya Shelui na Mwamashimba katika Kijiji cha Mwamaya
wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Ilielezwa katika tukio hilo, dereva wa
Hiace aliingia barabara kuu ya Mwanza-Shinyanga bila kuchukua hadhari na
hivyo kukutana na basi hilo.
Akithibitisha
kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi
alisema baada ya ajali hiyo watu 10 walikufa papo hapo na wengine 11
kujeruhiwa, ambapo mmoja alifariki dunia akiwa njiani akipelekwa
Hospitali ya Wilaya ya Kwimba na wawili walifariki dunia wakati
wakipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kwa matibabu zaidi.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kwimba, Dk. Bethod Nchemba,
akizungumzia ajali hiyo alisema walipokea majeruhi 10 wakiwemo wanaume
na wanawake watano ambapo mmmoja alikuwa na hali mbaya na alifariki
akiwa mapokezi wakati akiendelea kupewa huduma.
Aliwataja
waliofariki dunia kuwa ni Monica Shija, Christina Costantine, Theresia
Majenga wote wakiwa wakazi wa Kijiji cha Gulumwa wilayani Kwimba, Lwinzi
Kope mkazi wa Kijiji cha Chaselwe, Mabula Magi wa Rukwa, Isaya
Deogratius mkazi wa Mbande, Moses Kamel wa Kijiji cha Bupamwadomu,
George Ndila mkazi wa Sangu, Kondakta wa hiace aliyefahamika kwa jina
moja la Poni pamoja na mtu mmoja mwanaume, mama mmoja na mtoto ambao
hawajafahamika wote wakiwa ni abira wa Hiace.
Alisema
majeruhi watatu wanaendelea vizuri na matibabu katika hospitali hiyo na
miili tisa kati ya 11 imeshatambuliwa isipokuwa mwili wa mama mmoja na
mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 5 na majeruhi sita
wamelazimika kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu
zaidi.
The University of Dodoma (UDOM) wishes to announce the names of candidates selected for admission into various graduate programmes for the academic year 2016/17 which starts on October, 2016.
Mkazi wa Mbezi Africana Dar es Salaam, Amani Elikana (32), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akituhumiwa kumuua Askari wa Usalama Barabarani, Sajenti Mensali wa Kituo cha Polisi Mabatini – Kijitonyama.
Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu, Caroline Kiliwa, Wakili wa Serikali, Amani Mghamba alidai mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 22 mwaka huu eneo la Kijitonyama.
“Mtuhumiwa inadaiwa kwamba siku hiyo kwa makusudi ulimuua askari mwenye namba D. 8254 Sajenti Mensali kinyume cha sheria ya Jamhuri ya Muungano,” alidai Mghamba.
Hakimu Kiliwa alisema mtuhumiwa hapaswi kujibu kitu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hivyo shtaka hilo liliahirishwa hadi Oktoba 4 mwaka huu litakapotajwa tena.