Saturday, 27 August 2016

Angalia Picha 30: ASKARI WA JESHI LA POLISI SHINYANGA WAKIFANYA MAZOEZI KUJIANDAA KUKABILIANA NA UHALIFU



Leo Jumamosi,Agosti 27,2016 Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limeendelea kufanya ya mazoezi ya utayari wa kukabiliana na vitendo vya kihalifu.
Akiongoza mazoezi hayo,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amesema mazoezi hayo aliyoyataja kwa jina la Kiingereza ““Route Match” ni ya kawaida kwa ajili ya kujiweka tayari kukabiliana na uhalifu unaoweza kujitokeza. 
Kamanda Muliro amesema wamekuwa wakifanya mazoezi mara kwa mara lakini kilichofanyikani kubadilisha muda wa kufanya mazoezi na wataendelea kufanya kila siku za Jumamosi. 
“Huu ni mfumo huu ni wa kawaida kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazolisimamia jeshi la polisi..tumefanya matembezi yanayohusiana na ukakamavu,yanayojenga ujasiri kwa askari kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake,kwa hiyo kwa wananchi wanaoishi karibu na kambi ya jeshi siyo wageni wa mambo haya ambayo huwa tunayafanya siku za Jumamosi ”,alieleza Muliro. 
“Kilichofanyika leo tumepita mtaani asubuhi/mchana badala ya usiku/alfajiri (saa 11 hadi saa 1.30) kama vile tumekuwa tukifanya lakini lengo ni moja tu,watambue kuwa jeshi lao la polisi liko imara katika kuwalinda raia na mali zao,kusimamia sheria za nchi na askari mzuri ni yule mkakamavu,mwepesi ana uwezo wa kufikiri haraka kujua kile anachokitekeleza kimesimamia sheria gani”,aliongeza Muliro. 
Alisema mazoezi hayo ni ya kawaida na kusisitiza kuwa kwa wananchi ambao siyo wahalifu na walio wema wamefurahia mazoezi hayo. 
Askari polisi wakiongozwa na kamanda Muliro walipita katika maeneo mbalimbali mjini Shinyanga na maeneo huku wakiwa na vifaa mbalimbali vya jeshi hilo ikiwemo magari,silaha na magari ya maji ya kuwasha. 
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo maeneo mbalimbali walikopita askari polisi mjini Shinyanga,ametuletea picha 31…Shuhudia hapa chini 
Hapa ni katika kambi ya jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga-Kulia ni Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akitoa maelekezo kwa askari wa jeshi hilo kabla ya kuanza mazoezi mtaani leo majira ya saa tatu asubuhi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akieleza kuhusu mazoezi ya "Route Match"
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akisisitiza jambo kabla ya kuanza kufanya mazoezi
Askari polisi wakiwa kambini kabla ya kuanza kufanya mazoezi mtaani
Askari polisi wakijiandaa kuanza kufanya mazoezi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akifanya mazoezi na askari polisi wa jeshi hilo mjini Shinyanga
Askari polisi wakiendelea na mazoezi mtaani
Askari polisi wakiwa katika gari la maji ya kuwasha
Mazoezi yanaendelea katika eneo la Phatom mjini Shinyanga
Gari la maji ya kuwasha likiwa barabarani
Magari ya polisi yakiwa barabarani
Mazoezi yanaendelea
Askari polisi wakiwa ndani ya gari 
Wananchi wakiendelea na shughuli zao huku askari polisi wakiendelea na mazoezi yao
Wananchi wakiendelea na safari zao
Askari polisi wakiendelea na mazoezi yao
Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa kambini baada ya kumaliza kufanya mazoezi 
Askari polisi wakiwa kambini baada ya kumaliza kufanya mazoezi mtaani
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza kambini ambapo aliwaambia askari polisi kuwa watakuwa wanafanya mazoezi ya namna hiyo kila siku za Jumamosi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akisisitiza jambo
Maafisa wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa kambini baada ya kumaliza kufanya mazoezi
Askari polisi wakiwa kambini
Askari polisi wakimsikiliza kamanda Muliro
Kamanda Muliro akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kufanya mazoezi
Waandishi wa habari wakiwa kambini
Askari polisi wakijiandaa kutawanyika baada ya kumaliza kufanya mazoezi.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Share:

Picha: JESHI LA POLISI LAONGEZA ASKARI WENGINE 80 KUSAKA MAJAMBAZI VIKINDU MKOANI PWANI


  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeongeza nguvu kwa kutuma askari wengine 80 katika oparesheni ya kusaka majambazi inayoendelea katika maeneo ya Vikindu, wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
 Akizungumza na vyombo vya habari leo katika kituo kikuu cha  Polisi Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo Kamishna Simon Sirro, amesema Jeshi hilo limeanza rasmi oparesheni hiyo usiku wa kuamkia jana, ikiwa na lengo la kusaka watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wanaodaiwa kufanya matukio kadhaa ya ujambazi likiwemo lile la kuuawa kwa askari wanne waliokuwa wakienda lindoni, katika benk ya CRDB, Mbade jiji Dar es Salaam. 
 Amesema kuwa katika oparesheni hiyo kuna watu waliouawa na wengine wanashikiliwa na jeshi hilo, lakini amekataa kutaja idadi yoyote ile ya waliouawa au waliokamatwa kwa sababu za kiusalama kwa kuwa oparesheni hiyo bado inaendelea.
“Itakuwa ni kinyume cha utaratibu nikieleza kinachoendelea kwenye operesheni, niwahakikishie silaha zilizochukuliwa zinarudi,kinachoendelea nitawajulisha jumanne ili wananchi wajue kitu gani kinaendelea,” amesema.
Ameongeza kuwa; “Mapambano ni ya kawaida sana, na ndio maana askari polisi akifa kwa silaha ni jambo la kawaida sana. Operesheni tutaifanya maeneo ya Vikindu, Pwani Dar es Salaam, sababu hii network (mtandao) ipo na lazima tutaisafisha.Kama walidhani wataitawala DSM wamejidanyanya lazima tutarudisha heshima ya jiji.”
Katika hatua nyingine, Sirro amesema amepata taarifa kuwa wapo baadhi ya watu wanapewa fedha kwa ajili ya kufanya maandamano Septemba Mosi mwaka huu ambapo ametoa onyo kwa watakaoshiriki kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kuwa maandamano hayo hayajaruhusiwa.
“Wote tunajua madhara ya fujo, wazalendo naomba msishiriki, Wanaotaka kujionesha wanapambana na polisi waje barabarani, ” amesema.
Usiku wa kuamkia jana, hali ya taharuki iliwakumba wakazi wa Vikindu baada ya kikosi maalum cha askari kuvamia nyumba moja iliyoko eneo hilo, na kisha kuzuka kwa majibizano ya risasi kati ya polisi na wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa katika nyumba hiyo.
Baadhi ya askari wakiwa tayari kwenye magari yao wakati wa kujiandaa kuelekea Vikindu kwenye mapambano 
Vikosi hivyo vikitoka makao makuu ya kanda maalum ya Dar kuelekea kwenye mapamban 
Share:

LOWASSA AKUTANA USO KWA USO NA RAIS MAGUFULI KANISA LA MTAKATIFU PETRO JIJINI DAR ES SALAAM


Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa leo tarehe 27 Agosti, 2016 ameadhimisha Jubilei ya Dhahabu ya Miaka 50 ya Ndoa yake na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Hafla ya Jubilei hiyo imefanyika nyakati za mchana katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa uliopo kando ya kanisa la Mtakatifu Petro-Oysterbay na imetanguliwa na Misa ya shukrani iliyofanyika katika kanisa hilo majira ya asubuhi.
Jubilei hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume, Mke wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere, Mawaziri Wakuu Wastaafu Mhe. Cleopa Msuya, Dkt. Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Warioba na Mhe. Edward Lowassa.
Misa Takatifu ya Shukrani imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Mhashamu Askofu Josephat Lebulu na kuhudhuriwa na Maaskofu na Maaskofu Wakuu saba akiwemo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa Misa Takatifu Rais Magufuli amempongeza Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa kwa kutimiza miaka 50 ya ndoa na ameeleza kuwa ndoa hiyo iliyowaunganisha wanandoa wanaotoka katika madhehebu tofauti ya Kikristo imetoa fundisho kubwa kuwa binadamu wanapaswa kuwa wamoja hata kama wana tofauti mbalimbali zikiwemo za kimadhehebu ya dini, siasa na kanda.
Rais Magufuli amesema miaka 50 ya ndoa ya Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa Katoliki na Mkewe Mama Anna Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa la Kilutheri inawafundisha watanzania wote hususani wanasiasa kuishi kwa upendo na kuilinda amani waliyonayo na ametoa wito kwa viongozi dini kuendeleza juhudi zao za kuliombea taifa na kuwaunganisha wananchi licha ya tofauti walizo nazo.
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa pamoja na kuwashukuru Viongozi wote, ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria Misa ya Shukrani na Jubilei hiyo ya miaka 50 ya ndoa yake amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijaalia ndoa yake umri mrefu.
Rais Mstaafu Mkapa pia ametoa wito kwa watanzania kupenda na kushirikiana huku akibainisha mafunzo aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa dini kuwa "Kila mmoja ni zawadi kwa mwenzake"
Nae Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amempongeza Rais Mstaafu Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa kwa kuadhimisha miaka 50 ya ndoa na amewasihi watanzania kuiga mfano mwema uliooneshwa na wana ndoa hao ambao wamedumu katika imani bila kuyumba.
Kardinali Pengo amesema ndoa ya Rais Mstaafu Mkapa anaifundisha jamii kuwa tunaweza kuishi kwa imani zetu bila kubadili dini
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
27 Agosti, 2016
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SAUT-ARUSHA 2016/2017

Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA DIPLOMA NA CHETI CHUO KIKUU BUGANDO 2016/2017

 CUHAS - Bugando


New selected candidates for Diploma Pharmacy (DPS) Morning & Evening sessions for 2016-2017>Click to View/download 


New selected candidates for Diploma Radiography (DDR) Morning & Evening sessions for 2016-2017>Click here to download

New selected candidates for Diploma Medical Laboratory Sciences (DMLS) Morning & Evening sessions for 2016-2017>Click to View/download 
Share:

NACTE:TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA PILI NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na umma kwa ujumla kuwa lilifunga dirisha la maombi mnamo tarehe 15 Agosti 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo. Uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa cheti na diploma unatarajiwa kutangazwa tarehe 31 Agosti 2016.


Baraza pia linapenda kutoa taarifa  kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) utafunguliwa tena tarehe 1 Septemba 2016 hadi tarehe 15 Septemba 2016 ili kujaza nafasi za udahili zitakazokuwa wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na  kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuomba udahili hapo awali.


Baraza pia linapenda kuwaarifu waombaji waliofanya maombi kwenye vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa uteuzi kwenye vyuo hivyo bado unasubiri mwongozo wa Serikali na hivyo watafahamishwa punde Baraza litakapopata mwongozo kutoka Wizara yenye dhamana ya Elimu juu ya uchaguzi huo. Waombaji wa vyuo hivi wanashauriwa kusubiri na kutokubadili machaguo yao hadi kutangazwa kwa uteuzi kwa vyuo vya Ualimu vya Serikali.


Aidha, Baraza linapenda kuwafahamisha waombaji wa Shahada ya Kwanza waliofanya maombi kupitia Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) wa Baraza kabla ya tarehe 16 Julai 2016 ambapo Tume ya Vyuo Vikuu ilitoa tangazo juu ya sifa za udahili na hawajafikisha sifa hizo kwamba unafanyika utaratibu wa kuwarudishia fedha zao. Utaratibu huu utamalizika baada ya kukamilisha tathmini ya idadi ya waombaji wa aina hiyo. Hivyo wahusika wanaombwa kuwa na subira  mpaka tathmimi itakapokamilika.

Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 26 Agosti, 2016

Share:

Waziri Nape Atengua Uteuzi wa Mjumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA


Share:

Magazeti ya Leo Jumamosi ya Agosti 27, 2016



Share:

Friday, 26 August 2016

Makundi ya klabu Bingwa Ulaya 2016/2017

Droo ya kupanga Makundi ya klabu Bingwa Ulaya 2016/2017 ratiba kamaili ya hatua ya makundi ya Uefa champions League imetoka angalia hapa makundi yalivyo pangwa.
CquFfxEWAAAzLWR
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU CHA RUAHA 2016/2017

  •  

    Candidates selected to join Diploma in Pharmaceutical Sciences

  • Admission letters for candidates joining academic year 2016/2017

    Read more...  
  • Selected candidates to join various Certificate and Diploma Programs 

    Read more...

Share:

haya hapa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga cheti na diploma chuo cha st.john university 2016/2017 -BATCH 1

Share:

Mabasi Yaliyofungiwa Yaanza Kuachiwa ,CITY BOY NA KISBO ZAACHIWA PIA


MABASI yanayosafirisha abiria wanaokwenda mikoani yaliyofungiwa na Serikali kwa kusababisha ajali yameanza kuruhusiwa kutoa huduma hiyo.

Mabasi hayo yameruhusiwa baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu na Majini (SUMATRA) na Wamiliki wa Mabasi ya Abiria (TABOA) kufikia muafaka.

Makubaliano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita yalilenga kuleta suluhu kwa kuwataka TABOA kusimamisha mgomo wa mabasi uliopangwa kufanyika nchi nzima Agosti 22 mwaka huu.

Zaidi ya mabasi 60 ya kampuni tofauti yalifungiwa na Serikali baada ya kile kilichodaiwa na serikali kwamba yalisababisha ajali kwa uzembe wao.

Wamiliki wa mabasi hayo walikuwa wanahoji sababu ya SUMATRA kufungiwa leseni ya usafirishaji  kwa kampuni badala ya kupewa adhabu basi moja lililopata ajali badala ya kufungiwa kampuni nzima.

Katibu Mkuu wa TABOA, Enea Mrutu jana alisema wamekubaliana mabasi ambayo ni mazima yaliyofungiwa yaachiwe kutegemeana na utaratibu wa ukaguzi yaweze kuingia barabarani kutoa huduma ya usafirishaji.

“Tulikubaliana na serikali ndani ya siku saba iwe imeyafungulia mabasi yetu mazima kutegemeana na utaratibu wa ukaguzi yaendelee kutoa huduma kwa wananchi na tayari serikali imeanza kuyaachia baadhi ya mabasi hayo,

“Baadhi ya mabasi yaliyofungiwa ambayo  yameachiwa kutoa huduma ni ya Mohammed Trans, Mbazi, Kisbo Safari, City Boy, KVC, Wibonera na Kandahari”, alisema Mrutu.

Alisema walikubaliana serikali iyakamate mabasi yote madogo nchini yanayofanya safari za usafirishaji abiria mikoani bila ya kuwa na leseni ya biashara hiyo.

Alisema mabasi hayo yamekuwa kero kubwa kwa kugombania abiria na yanapokuwa barabarani yanawachomekea madereva wa mabasi makubwa.

Pia aliomba idadi ya vituo vya polisi vya ukaguzi barabarani vipungue.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger