Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia kwa kipindi kisichojulikana
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la
Nay wa Mitego hadi hapo litakapojiridhisha kwamba ametekeleza maagizo
yote aliyopewa na Baraza sambamba na yeye kubadilika katika kubuni kazi
zenye maadili na zisizo dhalilisha watu wa kada mbalimbali.
Maagizo
aliyopewa Msanii Nay ni pamoja na kulipa faini (adhabu) ya kiasi cha
Shilingi milioni 1, kufanya marekebisho ya mashairi ya wimbo wake wa
‘Pale Kati’, kufuata sheria, kanuni na taratibu za urasmishaji sekta ya
Sanaa kwa maana ya kusajiliwa na BASATA na kuhakikisha wimbo wake
umefuata taratibu zote.
Aidha,
Msanii Nay ameagizwa kuwaomba radhi watanzania kwa kutoa kazi ya muziki
yenye kuvunja maadili na kudhalilisha watu wa kada mbalimbali hususan
wanawake.
Maamuzi
haya yamefanyika kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) cha sheria nambari 23
ya mwaka 1984, ikisomwa pamoja na kifungu cha 30(1)(2) na waraka wa
Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wa tarehe 16/7/2009 ambayo kwa
sasa inafahamika kama Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Adhabu
hizi zimetolewa kufuatia BASATA kufanya kikao cha pamoja na Msanii huyu
jana siku ya Jumanne tarehe 26/07/2016 kwenye Ukumbi wa Baraza na yeye
kukiri makosa na kuahidi kubadilika.
Makosa aliyosomewa na yeye kuyakiri kwa maandishi ni pamoja na;
1. Kujihusisha na shughuli za Sanaa pasipo kusajiliwa na BASATA.
2. Kutoa wimbo wa “Pale Kati” na kuupakia katika mitandao ya kijamii bila kuuleta kufanyiwa uhakiki wa maudhui yake.
3.
Maudhui ya wimbo wa ‘Pale Kati’ kwa sehemu kubwa hayafai kwa matumizi
ya wazi na ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya mtanzania.
Ikumbukwe
kwamba mnamo tarehe 16/07/2016 BASATA lilitoa taarifa kwa umma ya
kuufungia wimbo wa Pale Kati kufuatia kubeba maudhui yenye uvunjifu
mkubwa wa maadili na kupambwa na picha dhalilishi kwa wanawake.
Aidha,
tarehe 12/02/2016 BASATA liliufungia wimbo wa Shika Adabu Yako wa
Msanii huyuhuyu kwa makosa yanayofanana na haya. Hivyo adhabu hii
imetolewa ili kumpa muda wa kujifunza, kujitathimi na kujirekebisha kama
kweli ana nia ya kuendelea kufanya kazi ya muziki
The Higher Education Students’ Loans
Board (HESLB), hereby notifies all loan beneficiaries who are not
servicing their loans and whose names appear herein that they have
breached a contract as per the HESLB Act. No. 9 of 2004 (as amended)
Section 19 (1).
These Loan Defaulters are further
notified that according to HESLB Act No. 9 0f 2004 the Board, intends to
take the following steps: -
(i) Shall be liable to legal action as per Section 19 (a) (1) of the HESLB Act.
(ii) Shall be subjected to additional
monthly Penalty of 5% p.a. on the outstanding loans, over and above the
5% that was levied earlier.
(iii) Shall have his/her outstanding loan loaded with the cost of tracing that will be charged after being traced by the Board.
(iv) Shall be blacklisted and his/her
information shall be submitted to the Credit Reference Bureaux,
following which they shall be barred from access to credit facilities
from all Financial Institutions.
(v) Shall be barred from securing
Government scholarships or admission for Postgraduate studies in any
Higher Learning Institution within and outside the country.
(vi) Their details shall be submitted to
the Ministry of Home Affairs, Department of Immigration and all
Embassies where they will be denied approval for travelling abroad.
All Loan Beneficiaries whose names have
been published in the newspapers and on this website of the Board
through http://olas.heslb.go.tz are required to repay their due loans
immediately to avoid facing the above listed measures. Loans statements
and other details of their due loans can be accessed by visiting HESLB
Offices or writing to:
Acting Executive Director, Higher Education Students’ Loans Board, P.O. Box 76068 Dar es Salaam Email: info@heslb.go.tz
TCU YAFUNGIA VYUO VINGINE KUDAHILI.
BAADA ya wiki jana kutangaza orodha ya vyuo ambavyo havitaruhusiwa
kudahili Wanafunzi Kwa Mwaka wa Masomo 2016/17 katika vyuo vya;
(IMTU,KAMPALA,UDOM,SUZA,SFCHAS)-MEDICINE ,BAGAMOYO UNIVERSITY NA ST.JOSEPH
KUNA TETESI KWAMBA KUNA VYUO VINGINE VIMEFUNGIWA....... (ninafuatilia kuhusu vyuo vingine kufungiwa ni kweli au la)
Ni
siku ya jumamosi kama kawaida wanafunzi wote wa shule tunayosoma
tunakwenda viwanjani kucheza michezo mbali mbali kama mpira wa miguu na
michezo mingine ambayo wanacheza wasichana waliopo katika shule yetu
ambayo niya bweni yenye mchanganyiko wa wasichana na wavulana kuanzia
kidato cha kwanza hadi cha sita na nishule ya mtu binafsi(PRIVET SCHOOL)
iliyopo katoka mkoni Arusha.
Kama
kawaida yangu ya kuwa shabiki wa timu ya darasa langu la kidato cha
tano ninachosoma ninaendelea kutazama mechi tunayocheza na kidato cha
tatu hadi wakati huu tumeshafungwa goli mbili kwa moja huku dakika
zikiwa zinakimbia kuelekea ukingoni huku mashabiki wa kike wa kidato cha
tano wakiendelea kuwapa moyo wachezaji wetu waliopo uwanjani
“Ndio maana angekuwa huku tulipo sisi wala asingekuwa mzuri”
“Hembu acha pumba zako Eddy”
“Kweli
John unadhani angekuwa science unadhani angekuwa hivi wewe si unawaona
wakina Matha walivyo kauzu class hadi kuwatongoza mtu unashindwa”
Tukajikuta
tukikatisha mazungumzo baada ya mchezaji wetu mmoja kufunga bao la
kukomboa jambo lililoturudishia furaha hata ya kuwepo uwanjani.
Kabla hata ya dakika mbili mbele mchezaji wetu yule yule akafunga bao jingine
kupitia mpira wa kona uliopigwa na akaudumbukiza nyavuni kwa kichwa na
kuamsha shangwe za wanafunzi wote wa kidato cha tano na kuwafanya
mashabiki baadhi kuingia uwanjani huku wakishangilia kwa furaha kwani
tayari dakika zilisha kwisha.
Mimi na rafiki yangu John tukabaki nje ya uwanja huku sura zetu zikiwa na furaha kupita maelezo
“Wee dada jamaa anakuita hapa”.John alimuita yule msichana tuliyekuwa tunamjadili dakika kadhaa zilizopita.
Akatuangalia
kwa dharau yeye na rafiki zake kisha wakaongea maneno ya kunong’onezana
na kuanza kucheka kicheko kilichotufanya tuwe kimya kama tumemwagiwa
maji ya baridi.
Safari
ya kurudi shuleni ikaanza kwani kiwanja chetu cha mpira kipo eneo la
nje ya eneo la shule.Tukiwa tumeongozana na kundi la wasichana wa kidato
chetu wakiimba nyimbo za ushindi mimi na John tukawa na kazi ya
kumfwatilia yule msichana ambaye kusema la ukweli amejaliwa uzuri
unaweza kusema alipewa siku yake ya pekee katika uumbwaji wake
Tukafika
hadi kwenye duka la shule ambapo yule msichana alikwenda na rafiki yake
ambaye kidogo naye anavutia japo si sana.Kutokana hatukuwa na lengo la
kufika katika duka hilo kwa aibu tukajikuta tukinunua mifuko miwili ya
pipi za Big boom
“Claudia ile hela siioni”Yule
msichana alizungumza huku akiwa anajipapasa papasa kwenye mifuko ya
sketi yake huku akionekana kuwa na wasiwasi wa hali ya juu kwani tayari
walishakunywa soda pamoja na kula keki za watu
“Hebu tazama vizuri”
“Kweli si unaona mifuko yote haina hela jamani sijui imeangukia wapi”
Nikawatazama
kwa huruma kisha nikatoa waleet yangu mfukoni iliyotuna kwa wingi wa
pesa nikamuuliza muuza duka ni kiasi gani cha pesa anachowadai
akaniambia nikawalipia na chenchi iliyobaki nikamwambia muuza duka
awapatie.
Tukaanza
kuondoka kabla hatujafika mbali Claudia akatuita na tukasimama wakaja
katika lile eneo tulilosimama huku rafiki yake ambaye ndio aliyetufanya
twende pale dukani kwa kumfatilia akaawa analia
“Samahani kaka zangu tunawashukuru”
“Haina shida vitu vya kawaida,Eddy twende zetu”
“Ngojeni kwanza”
Claudia alizungumza huku akimshika John beda aliyeanza kugeuka na kutaka kuanza kuondoka katika eneo tulilo kuwepo
“Mbona huyo mwenzako analia”
“Amepoteza pokety money yake ndio kwanza ametoka kuipokea leo mchana kwenye basi”
“Mmmm poleni”
John
alizungumza kwa maringo na kuanza kuondoka ikanilazimu mimi kubaki
kwani roho ya huruma ilianza kunitawala huku wakati wote nikimtazama
yule msichna ambaye bado sikulitambua jina lake
“Amepoteza sh ngapi?”
“Eti Salome umepoteza shii ngapi?”
“Elfu themanini na tano”
Nikakaa
kimya kama dakika mbili nikifikiria nini nifanye,nikajikuta nikiitoa
wallet yangu mfukoni na kuesabu noti tisa za elfu kumi kumi kisha na
kuzitoa na kumpa Salome taratibu akazipokea huku akiwa haamini tukio
linalo tendeka kwa wakati huo.
“Zitakusaidia saidia siku mbili tatu”
“Asante sana kaka yangu”
“Powa ukiwa na shida utakuja darasa la PCB ndio ninaposoma”
Nikawapa
na mfuko wa pipi nilio nunua kisha nikaondoka huku moyoni mwangu
nikijifariji kuwa tayari nimesha fanikiwa katika hatua ya kwanza ya
kumpata mtoto mzuri.
Tukafika
bwenini tukaoga kujiandaa na sikukuu ya wanafunzi ambayo hufanyika kila
mwisho wa mwenzi wakati wa usiku katika ukumbi wa shule.
Sikukuu
hii hutoa fursa ya wanafunzi kuonyesha vipaji vyao mbali
mbali.Tukapitia katika cantin ya shule na tukanunua chakula kisha
tukaelekea kwenye ukumbi uliojaa wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza
ahadi cha sita
Shughuli
zikaanza huku wanafunzi mbali mbali wakionyesha vipaji vyao huku
wakishangiliwa na wanaofanya vibaya huzomewa.Ukumbi ukakaa kimya huku
tukiwasubiria washiriki wa shindano la umiss wa shule kupita mbele yetu
huku majaji wakiwa ni waalimu wetu wa michezo pamoja na wanafunzi
baadhi.
Wakaanza
kuingia mmoja mmoja huku wakiwa wamependeza,nikajikuta ninanyanyuka kwa
furaha huku nikipiga makofi hii ni baada ya kumuona Salome akiwa katika
msururu huo wa mamisi waliochanganyika vidato mbali mbali.
Wakajipanga mbele ya majaji na kuanza kuulizwa maswali mmoja baada ya mwingine kwa lugha ya kingereza.Ikafika zamu ya Salome kuulizwa swali wanafunzi wote wakakaa kimya kumsikiliza atakacho kijibu
“SALOME CAN YOU TELL US WHAT IS LOVE?”(Salome unaweza kutuambia upendo ni nini?)
“Love
is force of nature however much we may want to,we can not
command,demand or disapper love,any more than we can and in adition love
cannot be bought,sold or trade.You cannot make some one to love
you.Thanks”(Upendo ni hali ya msukumo wa kihalisia kwa jinsi tunavyo
hitaji.Hatuwezi kulazimisha,kukomalia au kutawanya upendo kwa kadri
tunavyoweza na kwa kuongezea Upendo hauwezi kununuliwa kuuzwa au
kubadilishana.Hauwezi kumfaya mtu kukupenda wewe.Asante”)
Ukumbi
mzima ukapiga makofi kasoro mimi kwani nikajikuta sentensi ya mwisho ya
Salome ikijirudia rudia akilini mwangu “YOU CAN CANNOT MAKE SOMEONE TO
LOVE YOU”(Huwezi kumfanya mtu kukupenda).Wakatoka ukumbini kwa wimbo
walio ingilia kupisha mambo mengine kuendelea huku tukisubiri matokeo
kutoka kwa majaji wetu.
Muda
wa matokea ukawadia huku washiriki waote wakisimama mbele yatu.Jaji
mmoja akaanza kutangaza nafasi kuanzia ya tatu na ya pili huku nafasi ya
kwanza akimkabidhi
mgeni rasmi ambaye ni mmiliki wa shule kuitangaza huku wakiwa wamebakia
washiriki wanne.Tukakaa kimya kusubiria ni nani atakaye nyakua taji kwa
mwaka huo
“NA MSHINDI WETU NI……………………..SALOME ALEX EDWARD”
Ukumbi
mzima ukanyanyuka na kuanza kupiga makofi ikiwemo mimi huku John
akinisukuma sukuma kila wakati huku akinionyeshe jinsi Salome
alivyopendeza na kuzidi kuvutia kwenye macho ya wengi.Akaanza kuvalishwa
vitu wanavyo valishwa mamisi pale wanapashinda huku akikabithiwa uwa
kubwa na mgaeni rasmi.
Muongoza
shindano MC akamuomba Salome amchague mtu wa kwenda kucheza naye mziki
kwa dakika tano.Salome akachukua kipaza sauti na sote tukakaa kimya
kumsikiliza ni nani atapata bahati hiyo ya kuitwa mbele ya ukumbi
huo.Salome akatizama tizama na macho yake akaelekea sehemu tuliyokaa
sisi.Akanyoosha kidole chake watu wote wakaangalia tulipo sisi
“Eddy hichi kidole ni chako”.John
alizungumza huku akinisukuma sukuma kwa kutumia bega lake.Nikanyanyuka
kidogo ila Salome akatingisha kidole chake kwamba si mimi ni jamaa
aliyekaa kiti cha nyuma yetu ambaye ni kaka mkuu wetu.
Jamaa
akanyanyuka kwa furaha huku wezake nyuma wakimtuma akamchezee Salome
hadi alainike.Mimi na John tukabaki kama watu wasio amini huku mimi roho
ikianza kuniuma kupita maelezo na kumfanya John kuachia msunyo mkali
adi watu wa pembeni yetu wakamtazama na kuanza kucheka
“Mademu wengine bwana was**e kama nini”John
alizungumza huku akiendelea kutoa misunyo.Jamaa kama alivyoagizwa na
wezake akawa anazidi kumshika shika Salome mwili wake huku wanafunzi
wakishangilia kwa furaha na kuzidi kunifanya niichukie sikukuu hiyo
“John twende zetu tukalale”Tukanyanyuka
kwenye viti vyetu kutokana na mlango wa kutokea upo mbele tukalazimika
kupita mbele ya ukumbi huku macho yangu yaliyojaa hasira yakimtazama
Salome ambaye naye alinitazama kwa sekunde kadhaa kisha akayapeleka
macho yake sehemu nyingine.Tukashuka kwenye ngazi za ghorofa lenye
ukumbi wa shule.Kabla hatujafika chini mwanafunzi mmoja akatuita.