Monday, 4 July 2016
PICHA: Watu 29 wapoteza maisha katika ajali ya mabasi ya City Boy, Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi
Ajali
mbaya imeyohusisha mabasi mawili ya kampuni ya City Boy imetokea katika
kijiji cha Maweni wilaya ya Manyoni, Singida na kusababisha watu 29
kupoteza maisha papo hapo huku chanzo cha ajali kikitajwa kuwa ni mwendo
kasi.
Mabasi hayo yenye namba za usajili T531 DCE na T247 DCD, moja lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Kahama na lingine likitokea Kahama kuelekea Dar es Salaam.
Moja
ya mashuhuda wa ajali hiyo amesema kuwa madereva wa mabasi yote
walikuwa katika mwendo kasi na wakati ajali inatokea walikuwa
wakisalimiana kwa kunyosheana mikono kisha basi moja kupoteza mwelekeo
na kuingia upande wa basi lingine na ndipo yakakutana uso kwa uso na
kusababisha ajali hiyo.
Kamanda wa Polisi Singida, Thobias Sedoyeka tayari amethibittisha kutokea ajali hiyo na uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika.
Kesi za Mafisadi Kutozidi miezi 9
JAJI
Mkuu, Mohammed Chande Othman, amesema Mahakama Maalumu ya Uhujumu
Uchumi na Ufisadi itaamua kesi kwa muda usiozidi miezi tisa na kwamba
itaanza na majaji 14.
Aidha,
wameandaa kozi maalumu kwa majaji 14 watakaofanya kazi katika mahakama
hiyo itakayoanza Julai 11 hadi 15, mwaka huu, kwenye Chuo cha Mahakama
Lushoto mkoani Tanga, ili kupeana mwongozo juu ya uendeshaji wa mahakama
hiyo.
Jaji
Mkuu alisema, kesi zitakazoendeshwa katika mahakama hiyo ni zile ambazo
upelelezi wake umekamilika ili uamuzi utolewe mapema. Kwa mujibu wa
Jaji Mkuu, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kupambana na uhalifu
huo.
Aliyasema
hayo jana wakati alipotembelea Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara
ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere
vilivyopo katika Barabara ya Kilwa, ambayo alisema yamezidi kuwa bora
kuliko miaka mingine.
Alisema
baada ya sheria hiyo ya uhujumu uchumi kupitishwa na Bunge, imekuwa na
marekebisho mengi na kuboreshwa kwa kiasi kikubwa.
Jaji
Mkuu alisema pia, hatua inayofuata ni Rais kutoa idhini ya sheria hiyo
na baadaye kupitishwa kwa kutangazwa katika Gazeti la Serikali ili ianze
kutumika.
Alieleza
kuwa baada ya kutangazwa katika Gazeti hilo la Serikali, Jaji anatakiwa
kutunga kanuni mbalimbali, mojawapo ikiwa ya kulinda mashahidi kutokana
na kuwa sheria hiyo inahusu makosa makubwa na hatari ya ugaidi, rushwa
na uhujumu uchumi.
“Tuko
mbioni kutunga kanuni hizo na kuhakikisha mashahidi wanalindwa. Jengo
la mahakama hii litakuwa katika Chuo cha Sheria karibu na Mlimani City
na tayari tumepeleka wasajili watendaji,” alisema.
Mwishoni
mwa wiki, Jaji Mkuu huyo alisema kuwa majengo ya mahakama hiyo
yatakabidhiwa leo. Kutokana na maelezo yake, Mahakama iko tayari
kuendesha divisheni hiyo, baada ya kukabidhiwa majengo hayo.
Alisema
wataanza kutoa semina kwa majaji na watumishi wengine wa mahakama hiyo
juu ya namna divisheni hiyo itakavyoendesha shughuli zake.
Aidha, aliweka wazi kuwa hadi sasa hakuna kesi hata moja iliyokwishatambuliwa kwamba itashughulikiwa na mahakama hiyo.
Bwawa Nyumba ya Mungu Lafungwa kwa Miezi 12
SERIKALI
za mikoa ya Kilimanjaro na Manyara zimelifunga Bwawa la Nyumba ya Mungu
kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuepusha kutoweka kwa viumbe hai
wakiwamo samaki kutokana na kushamiri kwa uvuvi haramu.
Aidha,
wakuu wa wilaya za Moshi, Mwanga na Simanjiro wametakiwa kusimamia
maamuzi hayo na kuchukua hatua kali za kisheria kwa watakaokaidi agizo
hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadiki alisema hayo wakati wa hafla
maalumu ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya mkoani Kilimanjaro
iliyofanyika mjini Moshi, juzi.
Alisema
uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha ujirani mwema baina ya mikoa hiyo
kupitia wilaya tatu zinazolizunguka bwawa hilo na kwamba utekelezaji wa
agizo hilo umeanza rasmi Julai Mosi mwaka huu.
“Hali
ya uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu ni mbaya sana,
mazingira yameharibiwa, kuna athari nyingi zinajitokeza ikiwamo ya
kupungua kwa maji katika bwawa hilo na hii huenda ikaathiri uzalishaji
umeme na kutoweka kwa viumbe hai....kama serikali hatuwezi kuvumilia
tena,” alisema Sadiki.
Pamoja
na bwawa hilo, Sadiki alitaka wakuu wa wilaya kusimamia agizo la Kamati
ya Ushauri ya Mkoa (RCC), kupiga marufuku misumeno ya mnyororo, kwani
imebaini ni adui mkubwa wa misitu.
Katika
hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa aliwakabidhi wakuu hao wa wilaya
migogoro mikubwa mitano iliyopo katika hatua mbalimbali za utatuzi wake
kupitia viongozi waliowatangulia na kutaka kufuata sheria katika
kuishughulikia.
Miongoni
mwa migogoro aliyoitaja ni unaohusisha jamii ya wafugaji wanaozunguka
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kampuni
inayohudumia uwanja huo ya KADCO kuhusu umiliki wa eneo la ardhi.
Mgogoro
mwingine ni wananchi wa wilaya ya Longido mkoani Arusha na mwekezaji wa
eneo la utalii la Ndarakwai uliowahi kusababisha kuchomwa moto kwa eneo
hilo.
Siku 72 za Vita ya UKAWA na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson
Kukamilika kwa siku 72 za mkutano wa Bunge la Bajeti kumeacha rekodi
mpya ya wabunge wa upinzani kususia vikao vya Bunge kwa muda mrefu zaidi
kutokana na madai ya kutoridhishwa na utendaji wa Naibu Spika, Dk Tulia
Ackson katika chombo hicho cha uwakilishi nchini.
Wapinzani chini ya mwavuli wao wa Ukawa, wamejikuta kwa mara ya kwanza, 12 kati yao wakisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa nyakati tofauti baada ya kutiwa hatiani na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Newala (CCM), George Mkuchika kwa kukiuka maadili. Wachambuzi wa siasa wameeleza kuwa hali hiyo imefanya Bunge kuongozwa kwa mgogoro ulioathiri mijadala na mikakati ya ndani na nje ya bajeti hiyo.
Hata hivyo, uamuzi wa Ukawa kususia vikao
vinavyoongozwa na Dk Tulia kuliwafanya wabunge wa CCM kupoteza wastani
wa dakika tatu kati ya 10 ambazo hupatiwa kujadili hoja, kwani walikuta
wakitumia dakika za mwanzo kwenye mizaha, kebehi na vioja dhidi ya
wapinzani badala ya mijadala.
Baadhi ya wabunge ambao
walioongoza kumwaga vijembe ni Livingstone Lusinde (Mtera), Goodluck
Mlinga (Ulanga Mashariki), Juliana Shonza (Viti Maalumu) na Abdallah
Ulega (Mkuranga).
Ulega katika moja ya michango yake alifikia
uamuzi wa kumpatia mtoto wake mchanga jina la Tulia kama ishara ya
“kumuenzi Dk Tulia kwa uendeshaji wa Bunge unaofuata kanuni.”
“Dk
Tulia umekuwa mvumilivu licha ya wabunge wa upinzani kususia vikao
vinavyoendeshwa na wewe. Mke wangu naye amekuwa mvumilivu kama wewe na
nitampatia mtoto wangu jina la Tulia,”alisema Ulega kabla ya siku chache Dk Tulia kutembela Hospitali ya Taifa Muhimbili kumuona mtoto huyo.
Mlinga
alijikuta akiingia kwenye orodha ya wabunge waliotoa vioja bungeni
wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria aliposema
wanawake wa vyama vya upinzani ni lazima waitwe ‘baby’ ili wapate ubunge
wa viti maalumu.
Kauli nyingine iliyoibua mjadala ni ile
aliyoitoa kwenye mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo kwa kutaka Sanamu ya Askari iliyopo Mtaa wa Samora Jijini
Dar es Salaam ibadilishwe na kuwekwa ya mwanamuziki wa kizazi kipya,
Diamond Platinumz kutokana na kuipaisha nchi kimataifa.
Wabunge 12 wasimamishwa
Katika adhabu za awali, kambi ya upinzani ilishuhudia wabunge saba wakisimamishwa kushiriki vikao vya Bunge baada ya kutiwa hatiani na Kamati ya Maadili kuhusika na vurugu zilizotokea bungeni Januari 27, mwaka huu wakati wakipinga kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.
Katika adhabu za awali, kambi ya upinzani ilishuhudia wabunge saba wakisimamishwa kushiriki vikao vya Bunge baada ya kutiwa hatiani na Kamati ya Maadili kuhusika na vurugu zilizotokea bungeni Januari 27, mwaka huu wakati wakipinga kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.
Wabunge wawili wa Chadema
Esther Bulaya (Bunda Mjini) na Tundu Lissu wa Singida Mashariki,
walisimamishwa kuhudhuria vikao vyote vya Bunge la Bajeti lililomalizika
wiki iliyopita na mkutano utakaoanza Septemba.
Wengine wa
Chadema Pauline Gekul (Babati Mjini), Godbless Lema (Arusha Mjini),
Halima Mdee (Kawe) na Kabwe Zitto, Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia
ACT–Wazalendo walisimamishwa kuhudhuria vikao vyote vya bajeti.
Mbunge
wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema) alipigwa marufuku kuhudhuria
vikao 10 mfululizo. Juni 17 mwaka huu wabunge wawili wa viti maalumu pia
kutoka Chadema, Suzan Lyimo na Anatropia Theonest walisimamishwa kwa
kudaiwa kusema uongo bungeni.
Suzan alisimamishwa vikao vitano wakati Anatropia alisimamishwa vikao vitatu na kukatwa nusu mshahara na posho.
Kama
hiyo haitoshi, wabunge wengine watatu, Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini),
James Ole Millya (Simanjiro) na Saed Kubenea wa Ubungo walisimamishwa
vikao vya Bunge kuanzia siku hiyo na kumalizia adhabu vikao vya
Septemba.
Mbilinyi alisimamishwa vikao 10 kwa kudharau mamlaka
ya spika kwa kuonyesha kidole cha kati juu cha mkono wa kulia, ishara
ambayo inatafsiriwa ni matusi.
Kubenea na Ole Millya
walisimamishwa vikao vitano kwa kudaiwa kusema uongo baada ya kushindwa
kuthibitisha madai yao.
Upinzani wasusa
Ukilinganisha na mabunge yaliyopita, ukiacha Bunge la Katiba, wabunge wa upinzani walikuwa wakipinga jambo bungeni bila kutoka katika mkutano, lakini safari hii walikuja na staili mpya ya kususia vikao vyote vinavyoendeshwa na Dk Tulia na kusababisha kutochangia bajeti kuu.
Upinzani wasusa
Ukilinganisha na mabunge yaliyopita, ukiacha Bunge la Katiba, wabunge wa upinzani walikuwa wakipinga jambo bungeni bila kutoka katika mkutano, lakini safari hii walikuja na staili mpya ya kususia vikao vyote vinavyoendeshwa na Dk Tulia na kusababisha kutochangia bajeti kuu.
Wabunge hao
walisusa pia kushirikiana na wabunge wa CCM katika kutumia kantini ya
Bunge, michezo na mitandao ya kijamii, mbaya zaidi wamekuwa
hawawasalimu.
“Wao wameamua kuanza kututenga wenyewe, Dk Tulia
anaona kiongozi wa upinzani anatukanwa, anacheza tu, lakini mbunge wa
upinzani anapelekwa kwenye Kamati ya Maadili. Ngoja na sisi tujitenge,”
alisema Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia.
Ingawa kuna
wenyeviti wanne ambao kwa kawaida Spika hupokezana nao, katika mikutano
yote iliyotangulia kiongozi huyo aliacha kiti mara moja tu kwa Andrew
Chenge, lakini siku nyingine alikaa mwenyewe na kufanya wabunge wa Ukawa
kuondoka ukumbini kila anapoongoza.
Mbunge CCM akerwa
Hata hivyo, Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwako (CCM), ingawa alipingwa na wabunge wengi wa CCM, alisema bado anaamini katika kukaa kwa pamoja kati ya wabunge wa upinzani na Dk Tulia ili kumaliza tofauti zao.
Mbunge CCM akerwa
Hata hivyo, Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwako (CCM), ingawa alipingwa na wabunge wengi wa CCM, alisema bado anaamini katika kukaa kwa pamoja kati ya wabunge wa upinzani na Dk Tulia ili kumaliza tofauti zao.
Dk
Tulia aliwataka wabunge hao kufuata utaratibu wa kikanuni wa kufikisha
malalamiko yao kuhusu kiti cha Spika, licha ya kwamba hata yale
yaliyofikishwa dhidi yake hayakutolewa maamuzi yoyote.
Hoja zilizosisimua
Unapozungumza hoja zilizosisimua katika mkutano huo wa tatu, huwezi kuacha suala la kiinua mgongo cha wabunge kukatwa kodi kwani wabunge karibu wote waliopata nafasi ya kuchangia bajeti kuu waliibuka na hoja hiyo kuipinga, lakini waliambulia patupu.
Unapozungumza hoja zilizosisimua katika mkutano huo wa tatu, huwezi kuacha suala la kiinua mgongo cha wabunge kukatwa kodi kwani wabunge karibu wote waliopata nafasi ya kuchangia bajeti kuu waliibuka na hoja hiyo kuipinga, lakini waliambulia patupu.
Hoja hiyo ilihitimishwa baada ya Rais Dk
John Magufuli kukubali kukatwa kodi katika kiinua mgongo chake pamoja na
Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya.
Wabunge
wa CCM walimshukia Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wakidai
kuwa kitendo cha kukata kodi za kiinua mgongo cha wabunge ni mtego wa
kuwachonganisha na wananchi.
“Kwanini muwaache Rais, mawaziri,
wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na majaji?” alihoji mbunge wa Nzega
Mjini, Hussein Bashe wakati akichangia mjadala huo kabla ya viongozi hao
kujumuishwa.
Mbunge wa viti maalumu (CCM), Jacqueline Msongozi
alisema Dk Mpango amegusa pabaya kwa kukata kiinua mgongo kwa kuwa
tayari kila mwezi hukatwa Sh1.3 milioni ya kodi na kwa miaka mitano
watakayokaa bungeni watakuwa wamekatwa Sh50 milioni.
Hoja
nyingine iliyojadiliwa kwa kila wizara ni bajeti iliyopitishwa na Bunge
kutopelekwa yote ambapo Mbunge wa Tarime Mjini, Easter Matiko (Chadema),
alisema katika miaka yote aliyokuwa bungeni hajawahi kuona Serikali
ikileta bajeti bungeni inayotekelezeka.
Hata hivyo, Mbunge wa
Lulindi Jerome Bwanausi (CCM) alisema usimamizi wa karibu wa Bunge
katika kuhakikisha wanachopanga Serikali inatekeleza unaanza mwaka huu
kwa kamati ya Bajeti kukutana kila baada ya miezi mitatu ili kujadili
utekelezaji wa bajeti na kutoa ushauri.
Kubana matumizi
Miongoni mwa mambo yalitajwa sana ni kubana matumizi kukidhi sera ya Rais Magufuli, ambapo Mbunge wa Sengerema-CCM, William Ngeleja alisema ni moja ya mambo mema yaliyo kwenye mkutano huo.
Miongoni mwa mambo yalitajwa sana ni kubana matumizi kukidhi sera ya Rais Magufuli, ambapo Mbunge wa Sengerema-CCM, William Ngeleja alisema ni moja ya mambo mema yaliyo kwenye mkutano huo.
“Uchungu wa bajeti
hii ni mafisadi na wala rushwa. Walizoea kufanya kazi kwa mazoea
wataumia sana. Fedha za matumizi ya kawaida zimepunguzwa kwa kiasi
kikubwa, uadilifu ndio utatawala matendo ya watumishi,” alisema Ngeleja.
Katika wizara mbalimbali matumizi ya kawaida ikiwemo bajeti
zilizokuwa zikitolewa kwa ajili ya viburudisho imepunguzwa kwa kiasi
kikubwa huku ofisi na wizara zikiagizwa kutumia kumbi za Serikali wakati
wanapofanya mikutano, makongamano na warsha.
Chadema: Maandalizi ya Kuuzuia Mkutano wa CCM Yameanza
KATIKA
kutekeleza tamko la Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) la kufika
Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Bavicha Dodoma wameanza maandalizi ya kupokea vijana
zaidi ya 2000.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Dodoma jana Malambaya Manyanya, Mwenyekiti
wa Bavicha Mkoa wa Dodoma alisema, kwa sasa viongozi wa mkoa wameanza
maadalizi ya kuwapokea wageni wao ambao wanatarajiwa kuanza kuwasili
tarehe 21 na 22 Julai mwaka huu.
Alisema,
maadalizi hayo ni ya kuwapokea vijana ambao watatoka katika mikoa yote
ya Tanzania kwa lengo la kutimiza tamko la Bavicha taifa la kushirikiana
na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuzuia mikutano na vikao vya CCM.
Alisema,
kwa sasa mkoa tayari umeunda kikosi cha kufanya kazi ya maadalizi ya
ugeni huo ambapo kwa nia njema utafika mjini Dodoma kutekeleza kauli ya
Rais John Magufuli ya kuzuia vikao vyote na mikutano ya vyama vya siasa.
Alisema,
maadalizi hayo ya kuwapokea vijana hao ni pamoja na viongozi wa kitaifa
wa Bavicha kwa maana ya kutafuta mahali pa kulala na maandalizi ya
chakula.
“Wapo
watu ambao wanadhani Bavicha wana mpango wa kufanya fujo, sisi tunataka
kurejesha Demokrasia nchini na kutekeleza kauli ya mkuu wa nchi.
“Tumekuwa
tukiona jinsi mikutano ya Chadema inavyozuiliwa, na sasa msimamo wa
Bavicha ni kuzuia mkutano ya CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23 kwa
lengo la kubadilishana uongozi kati ya mwenyekiti wa sasa wa CCM na rais
msitaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete na Rais John Magufuli.
“Tumeandaa
vijana takribani 2000 kutoka mikoa yote nchini watakaokuja Dodoma
kusaidiana na Jeshi la Polisi kutawanya mkutano usio halali wa CCM.
“Kwa
sababau mkuu wa nchi ametoa tamko la kuzuia mikutano yote ya siasa
ikiwa ni pamoja na vikao vya ndani na mikutano ya hadhara hadi 2020.” Alisema Malambaya.
Alisema,
Jeshi la Polisi lilizuia mikutano ya vyama vya siasa vya upinzani na
mahafali ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Chadema (CHASO) na kuwa,
sasa wanashirikiana na polisi kuhakikisha mikutano ya CCM haitafanyika.