Sunday, 29 May 2016

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MAY 29 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:

Saturday, 28 May 2016

Breaking news:WANAFUNZI WOTE WA SPECIAL DIPLOMA UDOM WARUDISHWA NYUMBANI,HADI HAPO WATAKAPO TAARIFIWA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 
Kutokana na tatizo la ufundishaji wa stashahada ya elimu(hisabati,sayansi na teknolojia)chuo kikuu cha udom .serikali kupitia wizara ya elimu sayansi na teknolojia imewarudishwa wanafunzi wote nyumbani.


Soma hapo chini BARUA HIYO

Share:

BREAKING NEWS:WATU WANNE 4 WAMEFARIKI BAADA YA BOTI KUZAMA MDA HUU

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Image result for BREAKING NEWS
Watu 4 wamefariki baada ya boti waliyokuwa wakisafiria ikitokea kigamboni kuzama.

TAARIFA KAMILI ZINAKUJA
Share:

Mkuu wa Mkoa Afumaniwa Akifanya Mapenzi na Mwanae

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mkuu wa zamani wa Mkoa wa Kaskazini Pemba na mshauri wa Rais wa Zanzibar kisiwani humo, Dadi Faki Dadi amekamatwa akituhumiwa kufanya mapenzi na mtoto wake wa kambo.

Dadi alikamatwa juzi akidaiwa kukutwa na mtoto huyo wa mkewe wa ndoa mwenye umri wa miaka 21 katika nyumba ya kulala wageni inayoitwa Executive, jirani na makao makuu ya Uhamiaji Zanzibar katika eneo la Kilimani chini na Maisara, mjini Unguja.

Mwanasiasa huyo alijikuta akipigwa pingu na polisi akiwa kifua wazi mbele ya mkewe na wanafamilia na kisha kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Mwembemadema.
Picha za video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zilimwonyesha Dadi akikabiliwa na mashambulizi makali ya maneno kutoka kwa watu waliomkamata, akiwamo mkewe.
“Mwacheni avae nguo kwanza, mpeleke bwana, twende bwana..." ni baadhi ya maneno yanayosikika katika video iliyorekodiwa wakati wa kumtia mbaroni.

Taarifa zilizopatikana miongoni mwa wanafamilia ya kiongozi huyo, zilidai kwamba alikamatwa baada ya kumtilia shaka binti huyo kutokana na mienendo yake ya hivi karibuni na kuamua kumfuatilia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha kumshikilia Dadi kwa muda kabla ya kumwachia kwa dhamana.

“Kijamii alitenda kosa, lakini sisi tunaendelea kufanya uchunguzi, iwapo tutabaini ametenda kosa la kisheria na anaweza kuwa mashtaka tutamkamata ili kumpeleka katika vyombo vya sheria,” alisema Mkadam.

Mmoja wa wanafamilia ambaye aliomba jina lake lisitajwe alisema: “Mwizi siku zake ni arobaini, tulimtega na hatimaye tumemnasa sasa tuone mwisho wake utakuwa nini na kipi kitajiri baadaye.” 

Share:

HAPPY BIRTHDAY DADA ANGU AURELIA (mama kasiga)

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Habari yenu wadau wa blog hii ,
leo nina furaha sana kwani dada angu wa pekee Aurelia (dada ake blogger boy)katimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa hapa duniani.

Dada angu Mungu akupe miaka buku,NAKUPENDA SANA.

"NISAIDIENI KUMWISHI HAPPY BIRTHDAY DADA ANGU.
NAMPENDA SANA. "

Share:

MECHI YA FAINALI UEFA LEO MAY 28 2016 REAL MADRID VS ATLETICO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
  • Real Madrid and Atlético to meet in second Champions League final in three seasons
  • Repeat of 2014 final, when Real Madrid came back to beat Atlético in extra time
  • Madrid also triumphed 1-0 over two legs in last season's quarter-finals
  • Diego Simeone: "Only winning will satisfy me now"
  • Zinédine Zidane says above all Real Madrid must "run: run, run run"
Possible lineupsReal Madrid: Navas; Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo; Casemiro, Kroos, Modrić; Bale, Benzema, Ronaldo.
Out: Varane (hamstring)
Doubtful: none
Atlético: Oblak; Juanfran, Godín, Savić, Filipe Luís; Koke, Gabi, Fernández, Ñíguez; Griezmann, Torres.
Out: none
Doubtful: none
Sergio Ramos: My Magic Moment
Zinédine Zidane, Madrid coach
Ronaldo has been feeling a bit of pain but he's OK. He'll be there 100%. He has a little niggle, but that disappears when you're going to play in a Champions League final.
It's going to be a difficult game for sure, extremely difficult, but we already know this and we're prepared for it. We've had two weeks to prepare and now the players want the ball to start rolling.
I see the players the same as in Lisbon. We're one game away. We're all very happy to be in this final. We're ready for this, and that's the big word: we're ready to play. We've worked hard to achieve this. I'm happy with the work we've carried out. We've suffered a lot, but reaching a final without suffering is impossible. We know how to do that and that's what we'll have to do again, no doubt. In a final it's perfectly normal to have difficulties. If you want to win it, you have to suffer.
©Getty Images
Zinédine Zidane takes training at San Siro
Losing will not be a failure. Failure is in your attitude, or if you don't give your all. It's just a football game. You never know what will happen but I can tell you we're very prepared. [Since 2014] some players have left but the idea of this club is always the same. It's the great story: unity, effort, companionship and, when the time comes to play, quality and leaving everything on the field. We want to repeat that.
When the match begins I'll be a bit more tense [than as a player] but that's usual too – it's part of the coaching job. I like it, I like this kind of pressure. I've experienced it as a player but as a coach it's completely different. Carlo Ancelotti used to tell me that often. He told me before the final in Lisbon: "I hope you experience this some day as head coach." Here we are, so I keep thinking of Carlo.
Above all you have to defend well, first and foremost, especially when you don't have the ball. On top of that, we have our weapons to work well when we're attacking. What we really have to do is run: run, run, run.
Diego Simeone, Atlético coach
The game will be very tense, very even, especially at the beginning. Casemiro enables them to regroup better if they lose the ball. Whoever wins the early battles in midfield will have an advantage – Madrid, with their technical qualities, might try to play more.
The club, the players, the group we've created, is reinventing itself continuously. That's what is most valuable at this club. Everyone works with the idea of improving, growing, and that's life – if you work, work, work, eventually you get what you want.
©Getty Images
Diego Simeone overseeing training
To play a final is absolutely fantastic, to win it is even better. That experience makes you want to continue living these moments. It's not easy; you have to pick yourself up, keep inventing yourself, change the players but not change the commitment, the values, the work. If you keep working, you're insistent, you can achieve things.
We're not really going to change much for this game – neither team will. Madrid haven't changed much [since 2014]; we've changed more but we have the same structure. Casemiro makes Madrid a lot more dangerous on the counterattack – that's how they played in both [semi-final] legs against Manchester City. Many people think that's bad – not me. There could be different situations during the game but it's clear that, if you give Madrid space, they're very dangerous.
I like to have 113 years of history on my back – I like that, I love the pressure. Only winning would satisfy me.
Highlights: See how Real Madrid reached the final
Most recent results
Deportivo La Coruña 0-2 Real Madrid (Ronaldo 7 25)
The Merengues' slim hopes of snatching the title from Barcelona on the last day ultimately came to naught as Luis Suárez led the Catalans to a comfortable win at Granada. Madrid did what they could, and Cristiano Ronaldo's early goal meant that for 15 minutes Zidane's men even topped the provisional table. Ronaldo hit a second soon after – his 35th in the league this term – but Madrid were destined to finish runners-up by a point.
Highlights: See how Atlético reached the final
Atlético Madrid 2-0 Celta Vigo (Torres 51, Griezmann 54)
Atlético, already fated to come third, ended their domestic campaign with a routine victory. Fernando Torres opened the scoring following a fiery, if goalless, opening 45 minutes at the Estadio Vicente Calderón. Antoine Griezmann then overtook Radamel Falcao as the club's top marksman of the Simeone era, with his 44th strike in that frame. The clean sheet meant ever-present Jan Oblak conceded just 18 in the Liga season, equalling Francisco Liaño's Spanish top-flight record.
Form guide (all competitions, most recent first)
Real Madrid: WWWWDW
Atlético Madrid: WLLWWW
Highlights: The sides' 2014 meeting
Reporter's view: Andrew Haslam (@UEFAcomAndrewH)
This is the fourth European Cup final in Milan, and the first in 15 years, but none of the others had such a local flavour. Real Madrid's dramatic defeat of Atlético in Lisbon two years ago was the first European final between teams from the same city and Atlético will not lack for motivation as they seek a first European Cup, while Madrid have the pedigree.
Simeone's side are unbeaten in domestic fixtures against their opponents since that galling 2014 reversal (W5 D3) and, if they can finally translate that form to the continental stage, they could become the 23rd club to lift the trophy.
View from Madrid: Joseph Walker (@UEFAcomJoeW)Simeone and Atlético will attempt to avenge their heartbreak of two years ago as they take on their great city rivals. Atlético will be full of confidence, having lost just once in the last ten meetings between the teams, and knocked out both Barcelona and Bayern München on their way to this final.
Real Madrid, on the other hand, will feel they have the psychological advantage following what happened in Lisbon – and the fact their one victory in the last ten derbies came in last season's UEFA Champions League.
Did you know?
This is the sides' fourth European Cup tie, and Real Madrid have won the previous three: the 1958/59 semi-final, the 2014 final and last term's quarter-final. Find out more in our extensive match background.
Share:

Audio | Songa, Chidy Benz & Nikki Mbishi - Wacha Mchecheto | Mp3 Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Audio | Songa, Chidy Benz & Nikki Mbishi - Wacha Mchecheto | Mp3 Download

- See more at: http://www.johventuretz.com/2016/05/audio-songa-chidy-benz-nikki-mbishi.html#sthash.5mHzZYWE.dpuf

Share:

Serikali YASITISHA Mchakato wa Ada Elekezi Kwa Shule Binafsi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
SERIKALI imefuta mchakato wa kutangaza ada elekezi tangu katikati ya Mei mwaka huu, ambapo udhibiti wa ada hizo sasa utafanywa na Kamishna wa Elimu na Idara ya Ukaguzi.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema hayo jana jioni alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara hiyo na kuongeza kuwa mchakato huo umefungwa baada ya kujadiliana na wamiliki na Kamati ya Bunge.

Kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, usimamizi wa utoaji wa michango na ada holela katika shule hizo utashughulikiwa kwa mujibu wa sera, ambapo kutatakiwa kuwepo kwa kibali kwanza.

Alisema kutokana na hatua hiyo ya Serikali, ambayo inalenga kupata muda wa kutafakari suala hilo na kutafuta namna bora ya udhibiti, sasa hakutakuwa na ada elekezi ila michango itadhibitiwa.

Awali katika mjadala, baadhi ya wabunge walipinga mchakato huo na kutaka Serikali kujikita katika kuboresha shule zake na kuachana na utoaji wa ada elekezi. 
Akizungumza katika mjadala huo, Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM) alisema hakuna sababu ya kuwa na ada elekezi kwa shule binafsi.

Lugola alisema kama Serikali ikitaka shule binafsi zife, ni kuwalipa vizuri walimu wake, kuwajengea nyumba zao, kuwa na madarasa na kuweka chakula na hayo yakikamilika, hakuna mtu binafsi atakayepandisha ada. 
Kwa mujibu wa Lugola, kama hayo hayatafanyika, kila mtu ana uamuzi wa kumpeleka mtoto katika shule anayotaka hata Ulaya.

“Kuna tatizo gani na hizi shule za binafsi? Kwanza wamerundikiwa kodi nyingi mara kupaka rangi magari na mengineyo, sasa watarudishaje hizo fedha? Ndiyo maana wanatoza ada kubwa,” alitetea.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Zubeda Hassan (Chadema), alielezea kushangaa ni kwa jinsi gani ada elekezi itawekwa, wakati hakuna viwango vya utoaji elimu kwa watoto. 
Mbunge wa Maswa, Mashimba Ndaki (CCM), alisema suala hilo la ada elekezi watakaonufaika ni watu wenye fedha kwani ndiyo wanaowapeleka watoto katika shule binafsi na kusahau kuboresha shule za Serikali ambazo ni kwa watu wenye vipato vya kawaida.

Ndaki alisema iwapo shule za Serikali zingekuwa bora, zingechukua wanafunzi wote na zile za binafsi zingekosa wateja kwa gharama zao hizo kubwa, hivyo hakuna sababu ya kuwawekea ada elekezi.

“Shule binafsi wanapata wateja kutokana na miundombinu mibovu, matatizo ya walimu yanayotokana na kutotendewa haki katika shule za Serikali tofauti na shule binafsi ambazo wanawathamini walimu na kufanya watoe elimu bora,” alisisitiza.

Alitaka waziri, badala ya ada elekezi angekuja na mkakati madhubuti wa kuboresha shule za Serikali kwa kuwapa mahitaji yao walimu, kununua vitabu mashuleni na kuboresha miundombinu na shule hizo na hilo lingesababisha wapunguze wenyewe ada zao.

Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Mahawe (CCM) alisema Sheria ya Elimu ya 1978, inasema elimu siyo biashara bali huduma, lakini sasa wanaotoa elimu hiyo binafsi wanaonekana kama wao ni maadui.

Alisema shule binafsi, zinasaidia kusomesha Watanzania lakini bila kuthaminiwa wakati nchi nyingine watu binafsi wanasaidiwa kuwalipa mishahara, hapa nchini wanawapiga chini licha ya kuwa wanasaidia kusomesha hata watoto yatima, ili kuondoa watoto wa mitaani huku akieleza yeye katika shule yake anasomesha watoto 67.

Mahawe alisema shule binafsi wanalipa kodi zaidi ya 10, licha ya kuwa wameokoa kupeleka watoto kusomeshwa katika nchi za Kenya na Uganda huku akiomba wizara kuwapatia dawati wizarani ili wawape ushauri hususan katika mitaala.

Mbunge huyo alilalamikia shule binafsi kutengwa na wizara kwani hivi karibuni walitoa mafunzo kwa walimu wa watoto wa darasa la kwanza mkoani Dodoma bila kuwashirikisha
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MAY TAREHE 28.5.2016

Share:

Friday, 27 May 2016

Wanafunzi Wamkataa Mwalimu Wao Wakimtuhumu Kulawiti Wanafunzi Wa Kiume Huko Katavi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Katika hali isiyo ya kawaida wanafunzi wa kiume wanaosoma  kidato cha tano katika shule ya Sekondari Usevya Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wamemkataa Mwalimu wao (jina tunalo) wakimtuhumu kuwafanyia vitendo vya ulawiti. 


Wakizungumza kwa masikitiko na waandishi wa habari shuleni juzi jioni Mbele ya Afsa Elimu Mkoa wa Katavi Everest Hunji,baadhi ya manafunzi ambao ni mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi wa Sekondari ya Usevya Moshi Ramadhani na Katibu Joniour Mgallah,walisema vitendo anavyofanya mwalimu huyo vimewaathiri kisaikolojia na kudhorotesha ufaulu wao kimasomo.
 
 

''Kwa kweli sisi wanafunzi tunakiri mwalimu ambae jina lake tunalo amekuwa akitumia Madaraka yake ya umakamo mkuu wa shule vibaya,Hususani anapokukamata na kosa hapa shuleni badala ya kukupa adhabu ya kulingana na kosa ulilofanya anakuomba kujamiiana naye huku akijua kuwa anayetaka kufanya naye mambo hayo ni mwanaume na utakapokataa anatishia kukufukuza shule'' ,walisema.
 

Hata hivyo Wanafunzi hao waliendelea kufafanua kuwa mwalimu huyo tayari ameshatekeleza vitendo hivyo vya ulawiti kwa baadhi ya wanafunzi na kuongeza kuwa wapo tayari kutoa ushahidi mahakamani kama kutahitajika kufanya hivyo.

Sambamba na hayo,walisema kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwatumikisha wanafunzi katika shughuli zake binafsi za uzalishaji kwa kuwapeleka kufanya kazi kwenye mashamba yake.
 
 

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe Erasto Kiwale ambaye aliambatana na Afsa Elimu Mkoa wa Katavi Everest Hunji alisema Kitendo hicho hakikubaliki na tayari hatua sitahiki zimeshachukuliwa za kumpeleka katika vyombo vya kisheria.Hivyo Wanapomuona mwalimu huyo mitaani wasidhani hajachukuliwa hatua.
 
 

Kwa upande wa Afsa Elimu Mkoa wa Katavi Everest Hunji.Aliwaambia Wanafunzi kuwa watulivu na kuziacha mamlaka husika kulishughulikia suala hilo huku akiwaahidi malalamiko yao yatashughulikiwa ipasavyo.
Share:

Picha!! Rais Dkt Magufuli Afanya Mazungumzo Ikulu Na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam


Share:

Majanga ya Mwanza!! Jamaa Apanda kwenye Mnara wa Simu Na Kutaka Kujirusha ili Afe..Aangalia Picha Hapa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Kijana Mmoja Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.


Tukio hilo limetokea leo asubuhi na kuvuta hisia za watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambaye alipanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana. 




Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia. 




Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, ametoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema. 




Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa, ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati ya mnara huo. 




Baada ya kijana huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa ajili ya huduma ya kwanza.

Zoezi la uokoaji lilichukua zaidi ya masaa sita bila mafanikio

Kijana huyo akiwa katika kilele cha mnara huo uliopo barabara ya makongoro-Airpot jijini Mwanza

Kijana akiwa hoi baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara

Kijana akiwahishwa hospitalini huku akiwa hoi baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara


Ghafla kuna jamaa mmoja akatuhumiwa kwa wizi na hapo shughuli nyingine ya kumuokoa na yeye ikaanza upya.
Share:

Watu Watatu Wakamatwa Na Kadi 19 Za ATM za Watu Tofauti Wakitoa Fedha Benki ya NMB

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa wanatoa fedha benki ya NMB tawi la Mpanda kiasi cha shilingi milioni 3,680,000 wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi hizo. .

Kaimu Kamanda wa Polisi  wa mkoa wa Katavi Damasi Nyanda amesema watuhumiwa hao watatu walikamatwa jana majira ya saa tatu usiku katika Tawi la NMB Mpanda .

Watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa kuwa upelelezi bado unaendelea , wamekamatwa na askari wa jeshi la polisi waliokuwa wakilinda Benki hiyo.

Nyanda ameeleza kuwa watumiwa walikamatwa baada ya askari polisi kuwatilia mashaka kutokana na kuwaona wakiwa wamekaa muda mrefu kwenye chumba cha mashine ya kutolea feda .

Amesema baada ya kuwatilia mashaka polisi waliingia ndani ya chumba hicho na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa wanaendelea kutoa fedha katika mashine tatu zilizomo kwenye mashine za kutolea fedha .

Kaimu Kamanda alieleza ndipo askari polisi walipoamua kuwapekua watuhumiwa na waliwakuta wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi h izo na walikuwa tayari wameishatoa kiasi cha fedha taslimu silingi milioni 3,680,000.

Amezitaja Namba za Kadi za ATM walizokamatwa nazo watuhumiwa kuwa ni AC 61908000058,AC 61902403196,AC61902400417,AC61908000427,AC 61902240100,AC 61908000237,AC 61902400518 AC 61910000645, AC 61910004240,AC 61908000609 AC 61902403168.

Kaimu kamanda Nyanda amezitaja kadi za ATM zingine zilizokamatwa kuwa ni zenye namba AC 61910000537,AC 61902402653, AC 61910000250, Ac 61902400818, AC 61908000449,AC1902403219 AC 61910002329 na AC , 70408100131.

Amesema watuhumiwa wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa tukio hilo utakapokamilika na bado watuhumiwa wote watatu wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi .

Kaimu kamanda ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa siri kwa watu za namba zao za siri za kadi wanazozitumia za ATM za kwenye benki .
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger