Tuesday, 24 May 2016

Mjamzito apigwa chumbani afa!

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

YOHANA (5)Marehemu Yohana Albogasti.
Issa Mnally na Richard Bukos, UWAZI
DAR ES SALAAM: Yohana Albogasti, 21, (pichani)mkazi wa Majohe Viwege Kwampemba jijini Dar ameuawa kwa kupigwa risasi chumbani akiwa mtupu, Uwazi limeipata.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilijiri usiku wa Mei 13, mwaka huu huko Majohe ambapo marehemu alikuwa ametoka kuoga.
“Mimi nilisikia mlio wa risasi mara moja tu. Nilikuwa na wenzangu, wote tulikaa kimya kila mmoja akihofia kusogelea eneo hilo kwani hatukujua kilichokuwa kikiendelea,” alisema shuhuda mmoja.
Akaendelea: “Kwa kuwa jirani na eneo hilo kuna jumba la kifahari  linalomilikiwa na mfanyakazi wa Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania) tulijua majambazi wamevamia kwake.
“Baada ya dakika kadhaa, watu tulianza kwenda eneo la tukio. Ndipo tulipoukuta mwili wa marehemu ukiwa chini hatua chache kutoka nyumba aliyokuwa akiishi.
“Alipigwa risasi chini ya titi la kushoto. Inaonekana alitoka ndani ili kujiokoa lakini alianguka sehemu hiyo akiwa mtupu.”
YOHANA (1)Jirani mwingine aliyedai kushuhudia tukio hilo alisema akiwa eneo hilo alisikia sauti ya mwanamke ikipiga kelele kuomba msaada kisha alimuona mwanaume mmoja akitoweka baada ya mlio wa risasi.
Uwazi pia lilizungumza na mume wa marehemu, Pazi Hamis (23) ambaye alisema:
“Kwa kweli hata mimi nashangaa sana, sijui hawa wauaji walikuwa na kisa gani na mke wangu kwani marehemu hajawahi kuniambia jambo lolote ambalo ningelihusisha na tukio hilo.
YOHANA (2)“Siku ya tukio, saa mbili usiku nikiwa kwenye mihangaiko nilipigiwa simu na jirani na kupewa taarifa. Sikuwa na jinsi, niliwahi eneo la tukio.
“Nilimkuta mke wangu amelala kifudifudi akitoka damu nyingi chini ya ziwa. Polisi nao walifika, wakauchukua mwili hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuuhifadhi.
YOHANA (3)“Kwangu kifo hiki ni pigo kubwa, kaniachia mtoto Halima ana miaka miwili. Yeye pia alikuwa na ujauzito wa miezi sita.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, SACP Lucas Mkondya alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa mmoja ameshakamatwa, wengine wanasakwa.
 “Mtuhumiwa huyo jina tunalihifadhi kwa ajili ya uchunguzi, mwingine ametoroka.
YOHANA (4)“Tukio lenyewe linaonekana kuwa na utata kwa kuwa marehemu alikuwa akiishi maisha ya hali ya chini, yaani hakuwa na pesa za kuweza kuvamiwa.
“Yawezekana kuna visasi! Hilo ndilo jambo tunaloendelea kulifanyia uchunguzi wakati tukiendelea kumsaka mtuhumiwa aliyetoroka,” alisema Mkondya.
Marehemu amezikwa Jumanne iliyopita kwenye Kijiji cha Kisaki Kata ya Singisa, Matombo mkoani Morogoro.
Share:

Wakili Hashim Rungwe Aishauri Serikali Mambo Mazito

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

rungwe
Wakili Hashim Spunda.
*Azungumzia mbinu ya kupunguza bei ya sukari, asema watu wana njaa!
MMOJA wa wagombea Urais na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Umma (Chauma), Wakili Hashim Spunda Rungwe amefanya mahojiano maalum na wahariri wetu ili kutoa tathmini yake ya utawala wa miezi sita wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli tangu ashike madaraka ya kuongoza nchi. Wakili Rungwe ameshauri mambo mazito ya nini cha kufanya ili nchi iweze kusonga mbele kimaendeleo. Hata hivyo, ametoa maoni juu ya mjadala wa Bunge kutooneshwa laivu na sakata la sukari, fuatana nasi katika makala haya ujue kile alichokisema:
Tupe maoni yako kuhusu utawala wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ambaye amefikisha miezi sita akiwa madarakani, je, anakwenda vizuri?
Rungwe: Miezi sita ya Serikali ya Awamu ya Tano sijasikia mpango wowote wa kuondoa njaa kwa wananchi. Lazima rais ajue kwamba watu wana njaa na zifanyike juhudi kuhakikisha kipato kwa mwananchi mmojammoja kinaongezeka badala ya kupungua na bei ya vyakula inapungua. Maana yake ni kwamba vyakula vipungue bei badala ya kuongezeka. Kwa mfano, sukari ilikuwa Sh. 1,800 sasa ni zaidi ya Sh. 3,000 kwa kilo. Hili ni tatizo. Nitoe ushauri wa bure kwa Rais Magufuli, asihubiri ubaya wa baadhi ya watu hadharani kwa sababu kunaweza kuwafanya wawekezaji kuogopa kuja kuwekeza nchini.
Yapo mambo ambayo anapaswa kuongea na watendaji wake tu na mambo yakaenda bila kuwafanya watu wa nje kujua kuwa Tanzania ni nchi ambayo unaweza kunyang’anywa mali yako bila kufuata utaratibu wa kisheria. Huu ni ushauri tu, nimeutoa kwa faida ya nchi.
Nini maoni yako kuhusu Bunge kutorushwa laivu?
Rungwe: Kwanza ieleweke kuwa kuzuia Bunge kuoneshwa laivu ni ukandamizaji mkubwa wa vyombo vya habari lakini pia ni kuwanyima wananchi kuwaona wabunge wao wanavyojadiliana juu ya maisha yao. Tusifuatishe nchi nyingine, kama sisi tuliamua kufanya hivyo na wananchi wakaona inafaa, kuna ubaya gani nchi za nje zikituiga sisi? Kwa maneno mengine kutoonesha bunge laivu tunaweza kusema huu ni utemi wa wazi. Hakuna sababu yoyote ya msingi ya kuwanyima wananchi haki yao ya kumuona mbunge wao akitoa hoja zao kwani ndivyo katiba ya nchi yetu inavyosema tofauti na katiba nyingine.
Katika miezi sita hii tumeshuhudia watumishi wa sekta za umma wakitumbuliwa majibu, je, una maoni gani kuhusiana na zoezi hilo?
Rungwe: Mimi kama wakili nashauri viongozi wa serikali wa ngazi zote wasifukuze wafanyakazi hovyohovyo bila kuwasikiliza. Kufanya hivyo ni ukiukaji wa sheria, kwani katika sheria tunaambiwa usihukumu kwa kusikiliza hoja za upande mmoja. Usimhukumu unayemuona muovu kwa kufanya uovu. Ushauri wangu ni kwamba wanaosimamishwa wote, wasikilizwe, huo ndiyo utawala wa kisheria.
Ndani ya miezi sita kuna changamoto nyingi katika serikali, kuhusu sekta ya elimu kuna uhaba wa madarasa na madawati, unasemaje kuhusu hilo?
Rungwe: Ili kumaliza changamoto hiyo niseme tu kwamba serikali iache matumizi makubwa kama vile viongozi kujinunulia magari ya kifahari, fenicha mpya, kujilipa posho nono na kuwasaidia watu kukwepa kodi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, badala yake wajenge nchi kwa kufanya kazi kwa bidiii na kwa kusaidiana na wananchi wenye nia njema kuchangia maendeleo, matatizo hayo yatakwisha.
Hivi sasa kuna tatizo kubwa la mfumuko wa bei ya vyakula, unadhani serikali ifanye nini kuondoa kabisa tatizo hilo?
Rungwe: Serikali isitafute mchawi, mchawi ni yenyewe kutokana na mfumo uliokuwepo tangu zamani. Marais waliopita ni watu wa timu yake Rais Magufuli na nisiwatetee, hao wamesababisha haya. Tulikuwa na mashirika ya umma mengi kama vile Bhesco, RTC, Hosco, NBC na kadhalika lakini mengi yamekufa kutokana na kuwekwa watu kuongoza wasio na uzoefu.
Mfumuko wa bei upo, kwa mfano, hili la sukari ni tatizo kubwa kwa sababu hivi sasa kikombe cha chai ya rangi kwa mama ntilie ni shilingi 500 badala ya shilingi 200. Hii utaona kuwa haijamsaidia mlalahoi, watu wana njaa, serikali itafute mbinu ya kuondoa adha kama hii. Bei ya Dizel, ipungue kila kitu kitapungua bei kwa sababu vyakula vinasafirishwa kutoka shambani kwa gharama kubwa.
Sukari ya nje imezuiliwa kuingia nchini nini ushauri wako?
Rungwe: Mimi ningekuwa mshauri wa rais, ningemshauri asizuie kuagizwa sukari kutoka nje badala yake ningeshauri waitoze ushuru mkubwa na hii inayozalishwa nchini ikaondolewa ushuru. Kwani kuna hasara gani kuondoa ushuru kwa commodity (bidhaa) moja? Ni wazi watu wangekimbilia sukari ya bei nafuu.
Share:

Buriani Makongoro Oging’

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

makongoroMwandishi Makongoro Oging’ enzi za uhai wake.
“Makongoro Oging’ amefariki dunia,” yalikuwa ni maneno yaliyopenya masikioni mwangu kutoka kwa Oscar Ndauka, Mhariri Kiongozi wa Global Puplishers alipofika nyumbani kwangu Jumamosi usiku wa Mei 21, mwaka huu akiwa na Sifael Paul, Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda.
Nilipigwa na butwaa kusikia habari hiyo ambayo kama ningekuwa na matatizo ya kiafya ningeweza kupata presha, huku mke wangu akishikwa na mshangao na akihoji kama vile hakusikia: “Makongoro kafariki duni?”
tar 14.8.2015 Makongoro akimuhoji mke wa aliyekuwa askari wa gereza la Dondwe Pwani ambaye aliuawa katika uvamizi wa kituo cha Stakishari, Picha na Richard Bukos (1)Tar 14.8.2015 Makongoro akimuhoji mke wa aliyekuwa askari wa gereza la Dondwe Pwani ambaye aliuawa katika uvamizi wa kituo cha Stakishari, Picha na Richard Bukos.
Nilimuona akifuta machozi kwa khanga, kisha nami nikachukua kitambaa na kufuta machozi. Tulizungumza mengi hadi saa nane usiku kupanga tufanyeje kesho kukicha baada ya kuzungumza na mke wa Makongoro usiku huo huo na kututhibitishia habari hiyo.
Jina la Makongoro Oging’ siyo geni kwa watu wanaofuatilia habari hasa wasomaji wa magazeti ya Global Publishers hususan Gazeti la Uwazi.
Ni juzi tu aliniletea fomu zake za kutaka press card na alipoijaza ikaonesha kuwa yumo ndani ya tasnia ya habari kwa miaka 21 sasa, hivyo kutosha kusema kwamba ni mkongwe katika fani hii.
Makongoro alikuwa mahiri wa kuandika habari za uchunguzi kwani  mwaka 2004 alipewa tuzo ya mwandishi bora wa habari hizo, iliyotolewa na Chuo cha Uandishi wa Habari cha Royal Tanzania kilichopo Ubungo, Dar es Salaam.
Miongoni mwa watu waliotunukiwa tuzo siku hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa pamoja na waandishi wa habari wengine ambao majina yao siwezi kuyakumbukwa kwa sasa.
Alistahili kwa sababu Makongoro alipokuwa kazini hakuwa na mchezo. Alikuwa akifuatilia habari za uchunguzi kwa kina. Nakumbuka siku moja aliandika habari moja ya udhalilishaji uliofanywa na vijana fulani baada ya kumteka msichana mmoja na kumpiga sana kisha kumvua nguo.
Sakata hilo lilifika jeshi la polisi wakati huo Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Kamishna Mstaafu Alfred Tibaigana akiwa madarakani alinipigia simu na kunitaka niende na Makongoro ofisini kwake ‘ sentro’.
Tulipofika tu akatuona tupo kwenye korido akasema kwa sauti, “Kamanda Zombe ( Abdallah), watu wa Uwazi wamefika, Makongoro uliyekuwa ukimtafuta huyu hapa, kaja na bosi wake.”
Zombe aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam wakati ule, alikuwa kwenye chumba kimoja na aliposikia sauti ya bosi wake alitoka na kutulaki huku akitukaribisha.
“Karibuni sana.”
“Ahsante.”
“Tumekuwa tukifuatilia gazeti lenu la Uwazi na habari ya wiki hii ipo mezani kwangu naomba mtusaidie mawili matatu,” alisema Zombe.
Baadaye alitukabidhi kwa askari mmoja wa upelelezi ambaye namkumbuka kwa jina moja tu la Judi ili tufanye naye mahojiano.
Judi alituchukua hadi ofisini kwake na kuanza kunihoji mimi kwa dakika chache kama mhariri wa habari ile na baadaye akaanza kumhoji Makongoro ambaye alichukua muda mrefu kutokana na mambo mengi ambayo alikuwa anayajua kuhusiana na habari ile.
Baada ya mahojiano yale Kamanda Tibaigana alituita ofisini kwake na kusifia umahiri wa Makongoro katika kuandika habari za uchunguzi na akasema huwa zinamsaidia sana katika uchunguzi wa tuhuma mbalimbali ambazo zinawafikia.
Tangu siku hiyo Makongoro Oging akawa rafiki wa Tibaigana na Zombe pamoja na askari wengine wengi pamoja na mawakili akiwemo Mabere Marando hali iliyofanya awe mahiri wa kuandika habari zinazohusu watuhumiwa mbalimbali.
Ilikuwa siyo rahisi kwa Makongoro kwenda kwenye kituo fulani cha polisi na kukosa ushirikiano anapofuatilia jambo kutokana na uhusiano mzuri alioujenga na askari hao hata wale wa Magereza na Kikosi cha Zima Moto.
Kwa upande wa wagonjwa katika hospitali mbalimbali, Makongoro alikuwa akiwaandika sana na kuwaombea misaada kwa wasomaji wa Gazeti la Uwazi na alifanikiwa kuwawezesha baadhi yao kupelekwa nje ya nchi kutibiwa kwa kuchangiwa na wasomaji.
Wengine walipelekwa India, wengine hospitali za humu ndani na kubadili maisha yao baada ya kutibiwa na kupona kutokana na kalamu yake aliyoitumia kwa manufaa ya jamii.
Wapo watu ambao walikuwa na maisha duni lakini Makongoro kwa kutumia kalamu yake aliandika habari zao na baadhi yao kufanikiwa kujengewa nyumba za kisasa.
Kwa upande wa wanafunzi, Makongoro hakuwaacha nyuma, nao alikuwa akiwafuata na kuandika matatizo yao. Wapo waliokuwa wakikwama kimasomo kutokana na wazazi wao au walezi wao kushindwa kuwalipia ada, mwandishi huyu aliandika habari zao na baadhi yao wakafadhiliwa na kusoma hadi chuo kikuu.
Makongoro hakuwa mchoyo wa fani yake, nimemshuhudia zaidi ya miaka 15 akiwafundisha waandishi chipukizi habari za uchunguzi na kuwa wa kutumainiwa katika chumba cha habari.
Alikuwa akipenda kuwafundisha uandishi wa uchunguzi waandishi chipukizi kivitendo kwani baadhi yao alikuwa akiongozana nao kwenye matukio na kuwafundisha kivitendo jinsi ya kufuatilia habari za uchunguzi alizokuwa akiziandika enzi za uhai wake.
Kazi yake ilimfanya ajulikane sehemu nyingi, kama vile ndani ya majeshi yetu yote, katika hospitali kubwa, mitaani na hata kwenye mashirika na taasisi za umma na zile binafsi.
Alikuwa jasiri kwa kufuatilia jambo bila woga na ndiyo maana mpaka anaaga dunia Jumamosi saa moja jioni hatukuwahi kuwa na kesi kwenye gazeti iliyosababishwa naye.
Makongoro ameacha mjane na watoto watatu. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.
Share:

Ulevi huu ni mbaya kuliko ule wa Kitwanga

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

kitwangaAliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.
LIMETOKEA jambo baya katika nchi yetu linaloweka historia kwa kiongozi wa serikali, ngazi ya uwaziri kupoteza kazi kwa sababu ya ulevi. Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga amefukuzwa kazi na Rais Dk. John Magufuli kwa sababu ya mteule wake huyo kuzidisha kilevi kilichomfanya kushindwa kutimiza majukumu yake sawasawa.
Kuna mambo mengi yanazungumzwa juu ya hatua iliyochukuliwa, wengi wakimpongeza rais kwa nia yake ya dhati ya kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa maadili, uwajibikaji na nidhamu.
Ni kweli kwamba kuna kundi kubwa la watu wanaokunywa pombe, baadhi yao wakipitiliza na kujikuta wakishindwa kufanya kazi au kufanya vyema katika majukumu yaliyo mbele yao, lakini pia wakishindwa kuweka sawa mambo yao.
Lakini ulevi wa pombe una madhara kidogo sana kwa jamii yetu kuliko ulevi wa madaraka walionao viongozi wengi katika serikali yetu. Hapa ninazungumzia watu kama wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa idara, wakuu wa mikoa, maofisa wakubwa mikoani, wakurugenzi walio wizarani, manaibu mawaziri na hata mawaziri wengine.
Ulevi huu wa madaraka upo pia hadi kwa maofisa watendaji wa ngazi za vijiji na kata, achilia mbali watu waliopewa dhamana ya kulinda uhai wa watu kama madaktari na polisi.
Kabla ya kuingia madarakani kwa serikali hii ya Magufuli, wananchi walikuwa wakiteswa sana na kauli kama ‘unajua mimi ni nani?’.
Kauli hizi zilitolewa na viongozi hao wakati wananchi wakiwa wanahitaji huduma zao, lakini wanacheleweshewa au kunyimwa. Mbaya zaidi, wakati mwingine zinatolewa hata na watoto wao, vimada wao, wake zao, wajomba zao au wategemezi wengine kwa sababu tu waziri, mkuu wa mkoa au bosi wa mamlaka ni baba, mjomba, shangazi au unasaba mwingine.
Ulevi huu upo sana kwa viongozi wa serikali, wanataka wananchi wawaogope, wakienda kutaka huduma, wanyenyekewe, wakati ukweli ni kwamba wanaopaswa kunyenyekewa ni wananchi kwa sababu ndiyo waajiri.
Ni vyema, Rais Magufuli akamulika eneo hili na wananchi wapo tayari kumsaidia. Kuna mabosi wanafika kazini muda wanaotaka, wanafanya kazi pale wanapojisikia na wanatoa lugha za kejeli na masimango bila kujali kana kwamba ni shughuli zao binafsi.
Tunajua jeshi la polisi kwa mfano, linaendeshwa kwa fedha za walipa kodi, lakini siyo jambo la ajabu kwamba wananchi wanapokwenda kupeleka matatizo yao, baadhi ya askari waliolewa madaraka wanawalazimisha kutoa hela ya mafuta ili waende kufuatilia tatizo lake.
Shida kama hizi wanazipata karibu katika ofisi zote za umma ambazo zimewekwa kwa ajili ya kuwahudumia.
Ni afadhali ya ulevi wa pombe kwa sababu wanakunywa kwa pesa zao, lakini ulevi huu unawaumiza watu wasiostahili, tena katika ofisi za umma.
Vyema Rais Magufuli akautazama ulevi huu. Wananchi wanawajua watumishi wa umma waliolewa kilevi hiki na wako tayari kuwataja ili nao wawajibishwe kama ilivyotokea kwa Charles Kitwanga.
Nachochea tu!
Share:

Maalim Seif Sharif Hamad Aitwa Polisi Kuhojiwa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Jeshi la Polisi Zanzibar litamhoji Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad Ijumaa ya wiki hii kuhusu masuala mbalimbali ambayo hata hivyo, hayakuwekwa wazi.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Makame alisema jana: “Natambua kuwa wasaidizi wangu watazungumza naye Ijumaa. Wao ndiyo wanajua watamhoji nini.”

Alipoulizwa kuhusu mahojiano hayo, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi naye hakuweka wazi badala yake alisema kuna masuala mengi ambayo ofisi yake inahitaji kuyafahamu kutoka kwa Maalim Seif.

Hii ni mara ya kwanza kwa Maalim Seif kuhojiwa na polisi tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu ambao kwa Zanzibar ulirejewa Machi 20, baada ya ule wa Oktoba 25 mwaka jana kufutwa.

Maalim Seif ambaye kabla ya uchaguzi huo alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alipinga kurudiwa kwa uchaguzi huo msimamo ambao pia ulichukuliwa na chama chake.

Kiongozi huyo amekuwa akitoa matamko kadhaa ya kuwashawishi wananchi kupinga utawala wa Serikali iliyopo madarakani.

Akiwahutubia wafuasi wake huko Pemba hivi karibuni, Maalim Seif alisema Serikali ya CCM imeanza kutikisika kutokana na vikwazo vinavyoendelea kuwekwa na wahisani pamoja na hatua ya chama chake CUF kutowatambua viongozi wake pamoja na Serikali. 
“CCM wajue wamekalia kuti kavu, siku yoyote wataanguka... tufanye kazi mpaka haki yetu tuhakikishe imerudi na wenzetu hawana safari ya kudumu,” alisema.

Aliwataka wanachama wake kuonyesha kwa vitendo kutoitambua Serikali ikiwamo kukataa kulipishwa kodi za ovyovyo pamoja na kujitenga na viongozi wa Serikali katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Mfano tunaweza kuamua siku fulani kuanzia saa sita, tunasimamisha vyombo vyote vya usafiri na siku nyingine tunaamua kupiga honi Zanzibar nzima kuonyesha hatuitaki Serikali ya CCM,” alisema huku akishangiliwa na umati uliofurika katika ofisi za chama hicho.

Mapema jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo alisema kuwa amesikia juu ya wito huo lakini hakuwa amepata taarifa rasmi kutoka kwa mkuu wake.

“Nimesikia kama mlivyosikia ninyi,” alisema na kuongeza: “Nimeelezwa pia hata leo Kamishna wa Polisi Zanzibar alikuwa na mahojiano naye.”

Kuhusu hilo Kamishna Makame alisema: “Sijaonana wala kuzungumza naye leo. Hiyo si kweli.”

Juzi, wakati akizindua ripoti ya Uvunjifu wa Haki za Binadamu uliofanyika visiwani humo kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema wanazo taarifa za Serikali kutaka kuwakamata viongozi waandamizi wa chama hicho na kuwashikilia.
Alisema wamebaini mpango wa kukamatwa kwao na kuwekwa kwenye Mahakama za bara ili kuwanyamazisha Wazanzibari.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MAY TAREHE 24.5.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:

Alikiba Amuombea Kura Diamond Platnumz

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Alikiba alisema haya kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kusisitiza kuwa yeye kusaini mkataba na kampuni ya ‘Sony Music’ jambo kubwa sana katika maisha yake ya muziki.

“Kiukweli toka nimerudi rasmi kwenye game na kutoa wimbo wa Mwana mashabiki walipokea vizuri sana Africa Mashariki, na kadili nilivyokuja kutoa wimbo mwingine wa Chekecha walizidi kuongezeka mashabiki na kujiona nina mashabiki wengi, hivyo kuja kusaini mkataba na ‘Sony Music’ ndani ya muda mfupi hivi kwangu mimi najiona ni kama nimepiga msamba maana siyo hatua za kawaida” alisema Alikiba.

Mbali na hilo Alikiba alimuombea msanii Diamond Platnum kwa watanzania ili wampigie kura kwenye tuzo anazoshiriki sasa na kusema kuwa yeye ndiye msanii pekee anayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo hivyo watanzania wampigie kura ili aweze kushinda.
Share:

Mh. Zitto Kabwe amvisha pete mchumba wake

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mwanasiasa Zitto Kabwe Ameamua kuacha ukapela, kwenye picha akionekana kumvisha pete ya ya uchumba mchumba wake anayetarajia kumuoa
Share:

Monday, 23 May 2016

Official VIDEO | Promise Ft. chege & Mucky - Nipe penzi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

https://youtu.be/BeEDuKL8lNw
Share:

2 PhD Scholarships Available – Call for applications.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Agricultural Investors as Development Actors (AIDA)?
Examining the development outcomes of foreign agricultural investments with respect to employment, land tenure security and water security.
Share:

BREAKING NEWS:CHUO KIKUU CHA SUA WATUMBUA JIPU,RAIS WA CHUO APIGWA CHINI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Image result for SUANET
Rais wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha sua FRANCIS NDUNGURU anaesoma Kozi ya AGRIBUSSINES (AEA) 3rd year, amepigwa chini kutokana na kashfa za rushwa,uamuzi huo umefanywa na wabunge wa chuo hicho likiongozwa na spika mahiri amabae alisimama kidete,kura zilipigwa na ndipo matokeo yakatoka na kuonesha kwamba robo tatu hawana imani nae.
MASWAYETU BLOG ikiongea moja kwa moja na baadhi ya wabunge walikuwapo bungeni wamesema kwamba wameamua kumpiga chini kutokana na kuendesha serikali bila kufata sheria.
SOMA BARUA HAPO CHINI YENYE KASHFA ZAKE ZOTE.
Share:

BREAKING NEWS:BASI LA HAPPY NATION LAPATA AJALI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Ajali basi la happy nation leo

Basi la kampuni ya HAPPY nation ikiwa inatoka arusha kwenda Handeni imepata hajali katika  wilaya ya handeni kijiji cha mkata mkoani tanga.
MASWAYETU BLOG ikiongea na mmoja wa abiria ambao walikuwapo kwenye ajali hiyo amesema kwamba.
Ajali hiyo imesababishwa na dereva wa boda boda aliingia vibaya njiani,kusababishwa kugongwa.
Boda boda huyo alikuwa amebeba mtu ambao wote wamefariki dunia.
MASWAYETU BLOG inawapa pole waliofiwa na walionusurika na ajali.

TAFADHALI DOWNLOAD APPLICATION YETU YA MASWAYETU BLOG KWENYE SIMU YAKO KWA HABARI MPYA

Share:

BREAKING NEWS:AJALI YA MELI KUZAMA ZIWA NYASA WATU 10 WAHOFIWA KUFA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Taarifa ya awali iliyoripotiwa na kituo cha television cha ITV muda mfupi uliopita imeeleza kuwa watu zaidi ya 10 wanahofiwa kufariki dunia katika ziwa nyasa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kutoonekana kwa siku mbili huko Mbamba Bay mkoani Ruvuma. 
Share:

Linex - KWA NEEMA | Mp3 Download [New Song]

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Linex - KWA NEEMA | Mp3 Download [New Song]

- See more at: http://www.johventuretz.com/2016/05/linex-kwa-neema-download.html#sthash.sL4e4IXt.dpuf
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger