Friday, 30 October 2015

Picha 10 kutoka ndani ya Ikulu Rais JK alivyomkaribisha Dk. Magufuli.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Ni siku ambayo tayari historia imeandikwa kwenye vichwa vya Habari za Siasa Tanzania ambapo Dk. John Pombe Joseph Magufuli ametangazwa kuywa mshindi wa kiti cha Urais kwenye Uchaguzi mkuu uliofanyika October 25 2015.
unnamed ii
Rais JK na Dk. Magufuli ndani ya Ikulu baada ya matokeo ya Urais kutangazwa October 29 2015
Kwa maana hiyo Dk. Magufuli anakuwa Rais anayekuja kubadili nafasi ya Rais Jakaya Kikwete na kuwa Rais wa awamu ya tano Tanzania.
Dk. Magufuli amealikwa ndani ya Ikulu Dar es Salaam Tanzania na Rais Kikwete na kupongezwa kwa ushindi huo… hapa ninazo picha kutoka ndani ya Ikulu hiyo.
unnamed iii
Dk. John Magufuli.
unnamed iv
Rais JK, Mama Salma Kikwete kwa pamoja wakimpongeza Dk. John Magufuli.
unnamed ix unnamed v unnamed vi unnamed VII unnamed viii unnamed x unnamed XII
Share:

MAGAZETI YA LEO IJUMAA OCTOBER 30 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Thursday, 29 October 2015

ANGALIA HAPA ADA ZA CHUO KIKUU ST.FRANCIS IFAKARA MWAKA WA MASOMO 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

FEE STRUCTURE FOR VARIOUS PROGRAMMES IN ACADEMIC YEAR 2015 - 2016

Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU TIA DAR NA MBEYA CAMPUS 2ND BATCH 2015/2016

Share:

DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ATANGAZWA RAIS MTEULE AWAMU YA TANO 2015-2020

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
post-feature-image

RAIS NI MAGUFULI: TUME

Share:

DOWNLOAD HAPA JOINING INSTRUCTIONS ZA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA AFYA CHETI NA DIPLOMA-NACTE 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Habari yenu wadau wa blog hii pendwa ya MAASWAYETU BLOG Leo tena tunaweletea Joining instructions za kozi mbalimbali certificates na diploma kwa mwaka wa masomo 2015/16

Tunajua wengi mnazisubiria hizi form kwa hamu sana na mnataka mjue gharama za mafunzo kwa chuo ulichochaguliwa.

Share:

TAARIFA MUHIMU KWA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) KUBADILISHWA KWA TAREHE YA KURIPOTI CHUONI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
slide2
Chuo Kikuu cha Dodoma kinasikitika kuwatangazia Wanafunzi wote kuwa, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Chuo tarehe za kufungua Chuo zimebadilishwa.
·        Kwa wanafuzi wapya, Chuo kitafunguliwa tarehe 14 Novemba 2015 badala ya tarehe 31 Oktoba 2015
·     Kwa Wanafunzi wanaondelea, Chuo kitafunguliwa tarehe 21 Novemba 2015 badala ya tarehe 7 Novemba 2015 iliyokuwa imetangazwa awali. 
·        Mitihani ya marudio (Suplimentary Examinations) itafanyika kuanzia tarehe 16 hadi 20 Novemba 2015.
Wanafunzi wote mnatakiwa kukamilisha malipo ya ada na malipo mengine kabla ya kuripoti Chuoni. Wanafunzi watakaoshindwa kukamilisha malipo hayo hawatapokelewa Chuoni.
Tunasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Imetolewa na Ofisi ya Mahusiano
29 Oktoba 2015

Share:

Wednesday, 28 October 2015

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO CHUO KIKUU SEKOMU 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Loans Allocations Of Continuing Students
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO CHA ST.JOHN UNIVERSITY 4TH BATCH 2015/2016

Share:

ANGALIA HAPA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO MBALIMBALI VYA AFYA 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Habari yenu,
Kama kawaida yetu MASWAYETU blog tunanendelea kukuletea huduma karibu zaidi,Kutokana na NACTE kutangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya afya 2015/2016 pia unatakiwa kufanya confirmation ya uchaguzi ulipochaguliwa usipofanya hivyo nafasi yako itapotea.

Kwa hiyo MASWAYETU BLOG INATOA HUDUMA IFUATAYO,

1.TUMA JINA ALKO KAMILI KWENDA NAMBA 0768260834 mfano:PAUL  LUGANDA(AFYA SELECTION OCTOBER 2015/2016)

2.HUDUMA HII UTASAIDIA KUFANYIWA CONFIRMATION YA CHUO
   ULICHOCHAGULIWA.


3.HUDUMA HII UTATOZWA TSHS 1000 TU AMBAYO UTAITUMA KWA MPESA KWENDA NAMBA 0768260834 AU TIGO PESA 0652740927
4.UTAJIBIWA NDANI YA DK MOJA TU.
Share:

Mambo 20 yaliyotamkwa na Edward Lowassa (UKAWA) na January Makamba ( CCM) leo Oct 28.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
MALALAMIKO YA CCM KUHUSU MATOKEO KWENYE BAADHI YA MAJIMBO
1: Chama cha Mapinduzi hakijaridhishwa na utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo kwenye baadhi ya majimbo, katika majimbo manne kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi, hasa katika kujumlisha matokeo uliopelekea wabunge wa upinzani kutangazwa washindi, majimbo hayo ni Iringa Mjini, Mikumi, Ndanda na Kawe.
———-
2: Wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo haya wamevuruga uchaguzi, kutokana na utata uliokuwa umejitokeza wakati wa zoezi la kujumlisha kura, CCM iliomba kura zihesabiwe upya lakini ikanyimwa haki hiyo ya msingi ambayo iko kwenye sheria. Kwenye baadhi ya majimbo, ikiwemo Nyamagana, wapinzani walipewa haki ya kura kuhesabiwa upya. Kwa msingi huo, CCM imeamua kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo haya.
———-
3: Tunataka sote tujiridhishe kwamba utashi wa wananchi umeheshimiwa, bado tunaendelea kukusanya taarifa za maeneo mengine kama kulikuwa na ukiukwaji mkubwa uliobadilisha matakwa ya wapiga kura, hata hivyo tunakiri kwamba kwenye maeneo mengi tulikopoteza viti vya Ubunge, tumepoteza kihalali, hatuna malalamiko, tunaheshimu maamuzi ya wananchi na tutafanya tathmini baada ya uchaguzi ili tubaini makosa na kuyarekebisha.

MAONI YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI
4: CCM imepokea maoni ya awali ya waangalizi wa uchaguzi, tumefarijika kwamba karibu wote wametoa kauli ya pamoja kwamba uchaguzi huu ulikuwa wa haki na huru uliofanyika kwa uwazi na kwa amani na kwamba changamoto zilizojitokeza ni ndogo na zimetokea katika maeneo machache kiasi zisingeweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa sasa.
———-
5: Tumepokea mapendekezo waliyoyatoa kwa wadau mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha mchakato wa uchaguzi kwa miaka ijayo, na hivyo kuimarisha demokrasia nchini mwetu. Kwa kauli za waangalizi hawa, kwamba, kwa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa, matokeo yanayotangazwa sasa ni kielelezo sahihi cha utashi wa Watanzania kuhusu viongozi wanaowataka.
———-
MALALAMIKO YA UKAWA
6: Tumesikia malalamiko ya viongozi wa UKAWA kupitia mkutano wao na waandishi wa habari jana, tumeshangazwa na kauli kwamba hawakubali matokeo ya Urais yanayotangazwa na Tume, hata hivyo matokeo ya Ubunge wanayakubali na kule wanakoshinda, wanayasheherekea.
———-
7: Tunashangazwa kwasababu Tume iliyoandaa uchaguzi wa Rais ni hiyo hiyo iliyoandaa uchaguzi wa Wabunge, wasimamizi ni walewale, vituo ni vilevile, na sheria na taratibu zilizotumika ni zilezile, hata fomu ya matokeo walizosaini wakala wao kwenye vituo vya kupiga kura, zimegawanywa katika sehemu (columns) tatu: urais, ubunge na udiwani.
———–
8: Mawakala wao walisaini fomu hizo kwenye vituo vya kupiga kura. Wameanza kuwa na matatizo na matokeo haya baada ya kuona mwelekeo wa kushindwa. Kama mwelekeo ungekuwa tofauti, wangekuwa na imani na Tume, wasimamizi na taratibu zote.
————
9: Tunaomba ifike pahala sasa kwamba, katika kuijenga demokrasia yetu na kuliimarisha taifa letu, tuanze utamaduni mpya wa anayeshindwa kunyanyua simu kumpigia anayeshinda na kumpongeza. Nafasi ya mwisho aliyonayo mgombea wa UKAWA kuendelea kujijengea heshima katika jamii yetu, na kuwa mwanademokrasia, ni kwa kufanya hivyo siku Dkt. Magufuli atakapotangazwa mshindi.
————-
10: Kwetu sisi CCM, kuchagua wagombea bora na kuwanadi na kutengeneza sera bora na kuzinadi, pamoja na rekodi yetu katika uongozi wa nchi, ndio njia zetu pekee za ushawishi. Katika uchaguzi huu, wananchi wamefanya maamuzi yao kwa uhuru na utashi, ikiwemo kuwaangusha mawaziri sita ambao tuliwasimamisha kama wagombea wetu katika majimbo mbalimbali nguvu na utashi wa wananchi umejidhihirisha katika uchaguzi huu.
————–
11: Mchakato wa uchaguzi sasa unakaribia kufikia ukingoni, tutawapata madiwani, wabunge na Rais, tunapaswa kuendelea na maisha na tuwape nafasi watutumikie. Jitihada tunazoziona sasa za viongozi wa UKAWA za kuendeleza siasa za uchaguzi kwenye mitaa ya miji yetu kwa njia za vurugu na maandamano hazikubaliki hata kidogo.
————–
12: Tunalaani kitendo cha wafuasi wa UKAWA kuchoma ofisi za CCM katika Wilaya ya Mbozi. Amani ya nchi hii ina thamani kuliko hitaji la madaraka la mtu yoyote. Wenzetu wa UKAWA wana haki ya kulalamika lakini hawana haki ya kuiingiza nchi yetu machafukoni kwa kuwakusanya vijana na kuwaingiza mitaani wafanye vurugu na kuhatarisha maisha, kuharibu mali na kusimamisha shughuli za watu wengine. tunawaomba Watanzania waendelee na shughuli zao kama kawaida huku kila mmoja akitambua wajibu wake wa kuilinda amani ya nchi yetu.


MAMBO 8 YALIYOSEMWA NA EDWARD LOWASSA

1: ‘Hatukubaliani na matokeo ya uchaguzi mkuu ya Rais, Wabunge na Madiwani yanayoendelea kutangazwa nchini na tume ya taifa ya uchaguzi, hii ni sababu upo ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba utangazaji wa matokeo haya umevurugwa kwa makusudi na Watendaji ndani ya NEC kwa kusaidiana na wa chama cha Mapinduzi’

2: ‘Katika maeneo mengi matokeo yalikotangazwa, kilichoripotiwa kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais hakifanani wala kwendana na matakwa halisi ya Wananchi, matokeo mengi yamesheheni udanganyifu, ulaghai na yameandaliwa kwa lengo maalum la kumbeba mgombea wa CCM John Pombe Magufuli’

3: ‘Katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi kura zetu zimepunguzwa na kuongezwa kwa mgombea wa CCM… kwa aibu sana, maeneo mengine kura zilizotangazwa zimetofautiana na idadi halisi ya kura zilizopigwa, mfano Jimbo la Mkoani na Mtambile Pemba, Makunduchi, Chambani, Kilindi na kwengineko ni miongoni mwa matokeo yanayothibitisha kuwa sio kura za uchaguzi mkuu wa Rais bali mzimu wa uchaguzi’

4: ‘Katika maeneo mengine likiwemo jimbo la Ubungo, matokeo yaliyopo mikononi mwa msimamizi wa uchaguzi yanatofautiana na yale yaliyokusanywa kutoka katika vituo vyote vya jimbo hilo, hali kama hii ipo kwenye majimbo yote ambayo wagombea wa CHADEMA, NCCR na C.U.F ama wamekua na nguvu kubwa au wameibuka Washindi’

5: ‘Uko ushahidi wa wazi katika majimbo yote Wagombea wa UKAWA wameshinda, tume imechelewa kutangaza matokeo ya Urais kwa sababu zinazothibitishwa kuwepo mikakati ya hila, matukio yote haya ya NEC kutangaza matokeo yaliyochakachuliwa yamekuja baada ya jeshi la Polisi kuvamia vituo vyetu vitatu vya kuhesabu kura na kuwakamata Wataalamu wetu waliokua wakipokea matokeo ya nchi nzima ambako tulikua tukiongoza kwa maeneo mbalimbali’

6: ‘Tunaamini kwa dhati kwamba uvamizi huo ulifanyika kwa makusudi kwa malengo ya kufanikisha uchakachuaji ambao sasa tunauona ukiendelea kufanyika kupitia matangazo yanayoendelea kutolewa na NEC, tunapenda kuwataarifu na Jumuiya ya kimataifa kwamba hadi wakati huo uvamizi umefanyika kura zetu za Urais zilionyesha tukiongoza kwa asilimia zaidi ya 60 kabla hawajatunyang’anya documents zetu, computer zetu’

7: ‘Kutokana na makosa hayo makubwa na ya makusudi yanayofanywa na Watendaji wa NEC, mimi Edward Lowassa na mgombea mwenza, tunautangazia Umma wa Watanzania na Jumuiya ya kimataifa kwamba hatukubaliani na matokeo yanayotangazwa na NEC, tunataka wasitishe mara moja na kuanza upya kuhakiki, kinachofanywa na NEC hapa ndicho kinachofanywa Zanzibar, zinafanyika juhudi za kupora kwa hila na kwa mabavu mwelekeo wa ushindi wa Maalim Seif’

8: ‘Tunaomba Watanzania waendelee kuwa watulivu na amani na mshikamano, tunachosema sisi utaratibu umekosewa wasitishe na wasipositisha tutachukua hatua ambazo tutazitangaza baada ya kamati kuu ya chama chetu kukutana leo’
Share:

TANGAZO LA KUHAMA CHUO KWA WANAFUNZI MLIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO MBALIMBALI 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Habari yako,
Endapo wewe ni mmoja ya wanafunzi uliechaguliwa kujiunga na chuo chochote TANZANIA kupitia NACTE tafadhali ,endapo utahitaji kuhama  chuo omba uhamisho MAPEMA.


TANGAZO KWA UMMA
WAOMBAJI WA UHAMISHO KWA PROGRAMU ZA AFYA: STASHAHADA NA ASTASHAHADA
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote waliochaguliwa kwenye kozi za afya katika ngazi za Astashahada na Stashahada kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kwamba kutakuwa na utaratibu wa kuhama kupitia kwenye mfumo (CAS). Tunapenda pia kuwaarifu kwamba wale wote ambao wanataka kuhama kutoka kwenye vyuo walivyopangiwa kwenda vyuo vingine itawapasa kutumia utaratibu ule ule kama walioutumia wakati wa kuomba nafasi kwa gharama  ya Tshs. 30,000/=.
Kwa utaratibu huu tunapenda ifahamike kwamba waombaji watashindanishwa kwa kutegemea nafasi zilizopo na sifa za muombaji.
Utaratibu wa uhamisho utaanza  rasmi Jumatano tarehe 28 Oktoba 2015.

Imetolewa na:
Katibu Mtendaji 
Baraza la Taifa la ElimuyaUfundi (NACTE)
28 Oktoba 2015
Share:

MATOKEO YA AWALI KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KOZI YA MUHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII


INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 
MATOKEO YA AWALI KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KOZI YA
MUHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kujiunga na kozi ya Muhudumu wa afya ngazi ya jamii (Community Health) kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kuwa, Uteuzi wa awali umefanyika na waombaji 3985 kati ya 9797 wameteuliwa kujiunga na vyuo mbalimbali. Matokeo ya uteuzi huo yanapatikana katika kurasa binafsi (Profiles) za waombaji
Share:

Tuesday, 27 October 2015

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU SAUT 3rd BATCH 2015/2016-KUPITIA NACTE

Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA SAUT 2015/2016-KUPITIA TCU 3RD BATCH

Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU SAUT MWANZA-DIPLOMA IN PRIMARY EDUCATION 2015/2016

Share:

HAYA HAPA MATOKEO MBALIMBALI YA UBUNGE NCHINI TANZANIA HADI MDA HUU

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Tunawaletea matokeo rasmi kwa nafasi ya Ubunge kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC kama yanavyotangazwa  na  Wakurugenzi  wenye  dhamana  hiyo

Tembelea  ukurasa huu mara kwa mara  kwa updates zaidi

==============================================


Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki: Omary Mgumba wa CCM ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 27940, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Salama Awadh wa CUF, aliyepata kura 13823
 
Jimbo la Wanging'ombe mkoani Njombe mgombea wa CCM Gerson Hosea Lwenge ameibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake wa karibu Disman Andrea Luhwago wa CHADEMA
 
Jimbo la Muhambwe – Kigoma Atashasta Justus Nditiye ameshinda Ubunge kwa tiketi ya CCM, na kumbwaga mpinzani wake wa NCCR Felix Francis Mkosamali katika kinyang’anyiro hicho
 
Updates: Lazaro Nyalandu ameibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha ubunge jimbo la Singida Kaskizini kwa tiketi ya CCM kwa kupata kura 42,191, Huku Mpinzani wake wa CHADEMA David Joseph Mghanja akipata kura 20,264
 
Updates:Jimbo la Rungwe mgombea wa CCM Saul Henry Amon ameshinda ubunge kwa kura 44,745, huku mpinzani wake wa CHADEMA kapata kura 43,613 John David Mwambigija. hivyo CCM kuibuka mshindi katika kiti hicho
 
Updates:Mgombea ubunge wa jimbo la Ileje kwa tiketi ya CCM Janet Zebebayo Mbene ameibuka mshindi kwa kujinyakulia kura 27582 dhidi ya kura 14578 za mpinzani wake wa karibu Emmanuel Amanyisye Mbuba wa NCCR
 
Updates:Mgombea wa kiti cha ubunge kupitia tiketi ya CCM kwenye Jimbo la Busokelo – Mbeya Atupele Fredy Mwakibete aibuka kidedea na kuwa Mbunge mtarajiwa kwa kupata jumla ya kura 20,206. Huku mpinzani wake wa CHADEMA Boniface Anyisile Mwabukusi kushindwa kwa kupata jumla ya kura 12,807
Updates:Mgombea ubunge wa jimbo la Mbozi mkoani Mbeya kwa tiketi ya CHADEMA Pascal Yohana Haonga ametangazwa mshindi wa kiti hicho kwa kujinyakulia kura 32442 dhidi ya kura 17220 za mpinzani wake wa karibu Godfrey Weston Zambi wa CCM
 
Updates:Harrison George Mwakyembe ameibuka Mshindi wa ubunge katika Jimbo la Kyela kupitia tiketi ya CCM kwa kupata kura 44,269 dhidi ya mpinzani wake Hebel Abraham kwa kura 39,379
 
Updates:Mgombea ubunge wa jimbo la Mbarali kupitia tiketi ya CCM Haroon Mulla Pirmohamed ameibuka mshindi wa kiti hicho kwa kura 45352 dhidi ya kura 36603 za mpinzani wake wa karibu Liberatus Laurent wa CHADEMA
 
Updates:Mgombea ubunge jimbo la Momba kwa tiketi ya CHADEMA David Ernest Silinde ameibuka mshindi kwa idadi ya kura 26468 huku mpinzani wake wa karibu Luka Jelas Siyame wa CCM akiambulia kura 26260
 
Updates:Mgombea ubunge wa jimbo la Mbeya Vijijini kupitia CCM Oran Manase Mteza ameibuka mshindi kwa kujinyakulia kura 56307 wakati mpinzani wake wa karibu Adam Abraham Zella wa CHADEMA akijinyakulia kura 52298
 
Updates:Jimbo la Ubungo- Dar es Salaam Mgombea wa CHADEMA Kubenea Saed Ahmed ameibuka kidedea kwa kujinyakulia kura za Ubunge 87,606 dhidi ya mpinzani wake Massaburi Didas John wa CCM aliyepata kura 59,514
 
Updates:Peter Lijuakali (Chadema) ametangazwa kuwa Mbunge Mteule wa jimbo la Kilombero.
 
Updates: Suzan Limbweni Kiwanga (Chadema) ametangazwa kuwa Mbunge Mteule wa jimbo la Mlimba
  
Updates: Majira ya Saa kumi na nusu alfajiri. Waitara Mwita wa CHADEMA ametangazwa kunyakua kiti cha Ubunge Ukonga, kwa kumbwaga Jerry Slaa wa CCM ambaye alikuwa mpinzani wake mkubwa.
 
Jimbo la Bagamoyo: Dk Shukuru Kawambwa (CCM) 26,434, Andrew Kasambala (CUF) 16,330, Mwamini Saidi (UMD) 418 na Saidi Athman (ACT Wazalendo) 418.

Jimbo la Ngara: Alex Gashaza (CCM) 53,387, Dk Bujari Simon (Chadema) 35,254, Helen Gozi (NCCR-Mageuzi) 997 na Dotto Jasson Bahemu (ACT Wazalendo) 440.
 
Jimbo la Msalala: Ezekiel Maige (CCM) 36,010, Paulo Malaika(Chadema) 20, 124, Marco Suwa (ACT Wazalendo) 672 na Abeid Ibeshi (UDP) 251.
 
Jimbo la Busega: Dk Raphael Chegeni (CCM) 40,977, David William (Chadema) 26,995 na Zangi Robart (UDP) 802.
 
Jimbo la Mbogwe: Augustino Masele (CCM) 32,921, Nicodemus Maganga (Chadema) 13,975 na Andrew Mnuke (ACT Wazalendo) 5,464.
 
Jimbo la Bukombe: Dotto Biteko (CCM) 47,147, Profesa Kulikoyela Kahigi (Chadema) 29,929 na Dick Bagamba (ACT Wazalendo) 1,673.
 
Jimbo la Babati Mjini: Pauline Gekul (Chadema) 21,970 na Kisyeri Chambiri (CCM) 16,434.
 
Jimbo la Kahama Mjini: Jumanne Kishimba (CCM) 47,553, James Lembeli (Chadema) 30,122 na Bobson Wambura (ACT Wazalendo) 605.
 
Jimbo la Kibaha Mjini: Silvestry Koka (CCM) 31,462, Paul Mtally (Chadema) 24,860, Habibu Mchange (ACT Wazalendo) 3,438, Gombati Waziri (CCK) 259, Betha Mpata (APPT), 120 na Kibona Ally (AFP) 108.
 
Jimbo la Geita Mjini: Kanyasu John (CCM) 34, 953, Rogers Ruhega (Chadema) 26, 303 na Malebo Michael (CUF) 625.
 
Jimbo la Mkinga: Dustan Kitandula (CCM) 21,623, Bakari Kassimu (CUF) 13, 547, Rachel Sadick (Chadema) 3,789 na Ali Mwita (ACT Wazalendo) 402.
 
Jimbo la Lindi Mjini:Selemani Kaunje (CCM) 20,733 na Salum Barwany (CUF) 18, 843
 
 Jimbo la Same Mashariki: Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amemshinda Anne Kilango Malecela kwa jumla ya kura 18836, dhidi ya kura 15539.
 
Updates: Mgombea Ubunge Jimbo la Mwanga Prof. Jumanne Maghembe wa CCM ameibuka kidedea na kutetea kiti chake cha Ubunge
-Amembwaga Henry Kileo wa CHADEMA
 
Updates: Wilfred Lwakatare (Chadema) kapata kura 28, 112 na kumshinda Balozi Khamis Kagasheki (CCM) aliyepata kura 25, 565
Updates:Jimbo la Vunjo, Kilimanjaro; Mgombea wa NCCR Ndg. James Mbatia, ameshinda kiti cha Ubunge kwa kuzoa kura 60,187 akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa CCM Innocent Melleck Shirima aliyeambulia kura 16,097.

Updates:Jimbo la Moshi Vijijini, Kilimanjaro; Mgombea wa CHADEMA Anthony Calist Komu ameshinda kiti cha Ubunge kwa kuzoa jumla ya kura 55,813, akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa CCM Dr. Cyril Chami ambaye pia alishawahi kuwa Waziri Viwanda na Biashara aliyepata kura 24,415.
 
Updates:Jimbo la Nyamagana, Mwanza: Mgombea wa CCM, Mabula Stanslaus Shing'oma ameshinda kwa kuzoa kura 81,017, akifuatiwa kwa karibu na Ezekiel Wenjewa CHADEMA aliyeambulia kura 79,280.

==>CCM pia imeshinda Kata 14 kati ya 18 za udiwani katika Jimbo la Nyamagana huku Chadema kikiambulia Kata Nne, hivyo CCM itaunda Halmashauri ya Nyamagana.

Updates:Jimbo la Tarime vijijini, mkoani Mara: Mgombea wa CHADEMA, Heche John Wegesa ameibuka kidedea kwa kupata kura 47,249, huku akifuatiwa kwa karibu na Kangoye Christopher Ryoba wa CCM aliyepata kura 42325.

Updates:Jimbo la Chato, mkoani Geita: Mgombea wa CCM, Dr. Kalemani Matogolo Medard ameibuka mshindi kwa kupata kura 78,817 akifuatiwa na Lukanima Benedicto Kulwizira wa CHADEMA aliyepata kura 32,513.

Updates:Mgombea wa CCM katika jimbo la Ilala, jijini Dar es salaam, Azzan Mussa Zungu ameibuka kidedea kwa kupata kura 35,818 dhidi ya kura 32,533 za Muslim Haiderali Hassanali wa CHADEMA
 
Update: Mgombea ubunge jimbo la Kasulu mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo, Moses Machali amepoteza jimbo hilo, ameshindwa na Mgombea wa CCM Daniel Sanze.
-Amepata kura 22,512 na mshindi Daniel wa CCM amepata kura 25,336
  
Updates:Matokeo ya ubunge Iringa Mjini kutangazwa kesho baada ya kuchelewa kupatikana kwa matokeo ya kituo cha Kata ya Ruaha.

Updates:Jimbo la Sumbawanga Mjini: Aeshi Hilaly wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 41763, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Ikuwo Malila wa Chadema, aliyepata kura 36183.

Updates:Joram Hongoli wa Chama cha Mapinduzi (CCM) atangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Lupembe kwa kupata jumla ya kura 20,430 na kumwangusha mpinzani wake toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Edwin Swalle aliyepata jumla ya kura 10407
 
Updates: Jimbo la Mchinga: Hassan Bobali wa CUF, ameshinda kwa jumla ya kura 14776, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Saidi Mtanda wa CCM, aliyepata kura 13665

Updates:Jimbo la Singida Magharibi: Kingwi Immanuel wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 25102, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Allute Mdinka wa Chadema, aliyepata kura 13480
 
Updates:Jimbo la Singida Mashariki: Tundu Lissu wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 25010, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jonathan Njau wa CCM, aliyepata kura 18614.
 
Updates: Jimbo la Singida Mjini: Mussa Sima wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 36690, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mgana Msindai wa Chadema, aliyepata kura 16702
 
Updates:Wiliiam Lukuvi ametangazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge toka tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Ismani, mkoani Iringa kwa kuwa na jumla ya kura 26,119 na mpinzani wake Patrick Sosopi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa kwa kupata jumla ya kura 15,534
 
Updates:Jimbo la Mtama: Nape Nnauye wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 28110, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Suleiman Luwongo wa Chadema, aliyepata kura 13918
  
Updates: Cecil Mwambe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) apata kiti cha Ubunge katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa kuwa na kura 26,247, huku Mariam Kasembe wa Chama cha Mapinduzi kukikosa kiti hiko kwa kupata kura 26,215

Updates:Jimbo la Same Magharibi: Dkt. David Mathayo wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 21418, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Christopher Sangweli wa Chadema, aliyepata kura 15347

Updates: Jimbo la Same Mashariki:Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amembwaga Anne Kilango Malecela kwa jumla ya kura 18836, dhidi ya kura 15539

 
Updates:Jimbo la Ilemela jijini Mwanza Angelina Mabula  wa  chama  cha Mapinduzi CCM ameshinda kwa kura za Ubunge, huku Hainess Kiwia kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameshindwa kukitetea kiti chake

Updates:Mtwara mjini Maftah Nachuma wa Chama cha CUF ameshinda kwa kura za Ubunge, huku Asnain Murji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ameshindwa kukitetea kiti chake
 
Updates:Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) atangazwa kuwa Mbunge kwa kupata jumla ya kura 51,124, huku mgombea kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Danstan Mallya apata jumla ya kura 26,966. 

Updates:Jimbo la Mbeya Mjini: Joseph Mbilinyi wa Chadema, ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 97675, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mwalyengo Shitambala wa CCM, aliyepata kura 46894

Updates:Jimbo la Kigoma Mjini: Zitto Kabwe wa ACT-Wazalendo, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 31546, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Amani Kaburou wa CCM, aliyepata kura 16344
 
Updates:Jimbo la Iramba Magharibi: Mwigulu Nchemba wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 54660, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jesca Kishoa wa Chadema aliyepata kura 12580
 
Updates:Jimbo la Ileje: Janet Mbene wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 27582, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Emmanuel Mbuba wa NCCR-Mageuzi, aliyepata kura 14578
 
Updates:Jimbo la Mpanda Mjini: Sebastian Kapufi wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 29193, dhidi ya mpinzani wake wa karibu wa Chadema Jonas Kalinde, aliyepata kura 18649
 
Update: Anthony Mavunde (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Joram Hongoli (CCM) akishinda Jimbo la Njombe Kaskazini.

Upadate: Jumanne Kishimba (CCM) ameshinda Jimbo la Kahama Mjini, Steven Masele ameshinda Jimbo la Shinyanga Mjini.

Update:  Hussein Bashe ameshinda Jimbo la Nzega Mjini na Silvestry Koka ameshinda Jimbo la Kibaha Mjini

Jimbo la Serengeti
Marwa Ryoba (Chadema) amengazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge kupitia tiketi ya Chadema katika jimbo la Serengeti.Jimbo  hilo  lilikuwa  chini  ya  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe
  
Jimbo la Chalinze
Ridhiwani Kikwete wa CCM, aibuka mshindi katika Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani kwa jumla ya kura 52695, dhidi ya Mang’unda Torongei wa Chadema aliyepata kura 23470
 
Jimbo la Moshi Mjini
Japhary Michael wa Chadema ameshinda kwa kura-51647, huku mpinzani wake Davies Mosha wa CCM akipata kura-26920
 
Jimbo  la  Bunda
Wassira aangushwa!
Ni baada ya Esther Bulaya wa Chadema kuchukua Jimbo la Bunda KWA KURA 26207, huku Wassira kupata kura 17573.

Steven Wassira

Jimbo la Peramiho 
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Peremiho kwa tiketi ya CCM , Jenister Mhagama ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo

Jimbo  La  Arumeru Mashariki
Mgombea Ubunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chadema , Joshua Nassari ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo

Nassari ameshinda kwa kura 86694, na mpinzani wake wa karibu John Pallangyo wa CCM amepata kura-31847 
 
Jimbo la  Shinyanga
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo Shinyanga Patrobas Katambi amegoma kuendelea kusikiliza kutangazwa kwa matokeo na msimamizi wa uchaguzi Kalinjuna Lewis, kwa madai kuwa hana imani na matokeo hayo na kuamua kutoka ukumbini na wapambe wake wakati matokeo ya kila kituo yakiendelea kusomwa. Hadi sasa bado hajatangazwa mshindi

Jimbo la Tandahimba
Katika jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara, Katani Ahmed Katani wa CUF ameshinda kiti cha ubunge kwa kura-55156, huku mpinzani wake mkubwa wa CCM, Shaibu Salimu Likumbo akipata kura-41088
 

Jimbo la Mbinga Mjini
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mbinga Mjini Sixtus Mapunda ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
 
Jimbo la Musoma Mjini
Ubunge: Vicent Nyerere(Chadema)  25,549  na Vedastus Mathayo(CCM) 32,836.

Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Musoma Mjini Vedastus Mathayo ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo

Jimbo la Mbinga Vijijini
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mbinga Vijijini Martin Msuha ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
 
Jimbo la Monduli
Ubunge: Julius Kalanga (Chadema) 35,024 na Namelock Sokoine (CCM) 25,925.

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Monduli, Ndugu Julius Kalanga ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo  
 
Aggrey Mwanry

Jimbo la Siha
Ubunge: Dk Godwin Mollel (Chadema) 22,746 na Aggrey Mwanry (CCM) 18,584.
 
Msimamizi wa Uchaguzi, Rashid Kitambulio amemtangaza Dk Mollel kuwa mshindi wa jimbo hilo ambalo mbunge wake alikuwa ni Aggrey Mwanry (CCM).
 
Jimbo la Tunduma
Ubunge: Mwakajoka Frank (Chadema) 32,442, Frank Sichalwe (CCM) 17,220, James Mwakalonge(TLP) 85, Reddy Makuba (ACT Wazalendo) , 319.
 
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Tunduma, Halima Mpita ametangaza matokeo hayo.

Jimbo Buyungu
Ubunge: Bilago Samson Chadema), 23,041 na Christopher Chiza(CCM) 22,934
  
Mgombea ubunge wa Chadema Bilago Samson amefanikiwa kunyakua Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa kura 23041. 
Christopher Chiza
Jimbo hilo lilikuwa chini ya CCM kupitia Waziri Christopher Chiza aliyepata kura 22934.
  
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kakonko, Jaina Msangi ametangaza matokeo hayo

Jimbo la Tarime Mjini
Ubunge: Ester Matiko(Chadema) 20,017, Michael Kembaki(CCM), 14, 025, Deogratias Meck(ACT-Wazalendo) 356.
 
Msimamizi mkuu wa Uchaguzi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Juma Mwajombe amemtangaza Matiko kuwa mshindi katika Jimbo hilo

Jimbo la Lindi Mjini 
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Lindi Mjini, Ndugu Hassan Suleiman Kaunje ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger