
Dar es
Salaam. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema haitambui kuondolewa
kwa kipengele cha ukomo wa uongozi uliofanywa na Chadema bila kufuata
idhini ya mkutano mkuu wa chama hicho.
Mwaka 2006, Katiba ya Chadema ilifanya
marekebisho yaliyoruhusu wanachama kugombea uongozi bila ukomo wakati
awali, waliruhusiwa kugombea kwa vipindi viwili vya miaka mitano.





