Monday, 5 May 2014
Kigwangala Atafakari Urais 2015
Na John Dotto
Mbunge
wa jimbo la Nzega Mkoani Tabora kupitia CCM, Hamis Kigwangala,
ametanabaisha kuwa anatafakari kama anaweza kugombea Urais kwenye
uchaguzi mkuu ujao kupitia chama cha mapinduzi CCM.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua fununu zilizo enea kwenye
baadhi ya mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikiibua mijadala mara kwa
mara inayomshawishi kugombea Urais mwaka 2015, Dk. Kigwangala amesema
anatafakari jambo hilo zito na kuongeza kuwa muda utakapofika
atayazingatia maoni ya wananchi.
Akizungumzia
maelezo kwamba haoni kama ni hatari kwake kutangazwa mapema kwamba
anataka kuwa kugombea Urais ni kujipunguzia sifa katika chama chake, Dk.
Kigwangala alisema yeye hajatangaza kama anataka Urais na wala
hajamtuma mtu kuanza kumfanyia kampeni, kwani watanzania wanaongozwa na
katiba yenye Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, hivyo hayo ni mawazo yao
na wana haki ya kufanya hivyo na yeye binafsi hawezi kuwapinga.
Hivi
karibuni kumeibuka mijadala mizito kwenye mitandao ya kijamii na baadhi
ya wanaharakati kutengeneza vuguvugu la kumshawishi Dk. Kigwangala
kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
ifikapo mwaka 2015.
Mijadala
hiyo mizito imeanzishwa katika mitandao ya Internet na simu za mkononi
walio ipachika jina "Citizens for Kigwangala" ambapo katika mijadala
hiyo wamekuwa wakishawishiana na kumwagia sifa Dk Kigwangala kwamba
ndiye kiongozi pekee anayefaa kuwakilisha chama cha Mapinduzi katika
uchaguzi mkuu ujao.
Baadhi ya
vijana wamekuwa wakijadili kuwa Dk Kigwangala ndiye anayeweza kuleta
upinzani wa kweli kwa vyama vya upinzani, wakijenga hoja kuwa amekuwa na
misimamo na uwezo wa kujieleza kwa ufasaha ndani ya vikao vya bunge.
Dk
Kigwangala ni mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora, mwenye taaluma ya
udaktari wa tiba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge
ya tawala za mikoa na serikali za mitaa.
MVUA YAMUWEKA KINANA DAKIKA 20 ANGANI
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kutoka kwenye ndege ya
kampuni ya Flightlink kwenye uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya kukaa
angani kwa dakika 20 zaidi ya muda uliopangwa kutokana na hali ya hewa
kuwa mbaya na mvua kubwa kunyesha.Katibu Mkuu amewasili Zanzibar kwa
ajili ya mkutano wa hadhara utakaofanika kwenye viwanja vya mikutano vya
Kibanda Maiti.
Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akishuka kutoka kwenye ndege ya
kampuni ya Flightlink kwenye uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya kukaa
angani kwa dakika 20 zaidi ya muda uliopangwa kutokana na hali ya hewa
kuwa mbaya na mvua kubwa kunyesha. Katibu Wa NEC ameongozana na Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mvua kubwa ikinyesha Zanzibar ambapo CCM inatazamiwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara.
Bajeti ya 2014/15 itambue sekta ya michezo
Bunge la
bajeti linaanza kesho huku Serikali ikiwa imetoa mwelekeo wa bajeti ya
mwaka wa fedha wa 2014/15 kuwa ni Sh19.6 trilioni, ikilinganishwa na
Sh18.2 za Bajeti iliyopita.
Vipaumbele
vya bajeti hiyo ni kuendeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano
ulioanza mwaka 2011 na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao
unajumuisha maeneo sita ya kitaifa ya kilimo, elimu, maji, utafutaji wa
rasilimali fedha, nishati, uchukuzi na uboreshaji wa mazingira ya
kufanyia biashara.
Kwa
mujibu wa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, matumizi ya kawaida kwa mwaka
ujao wa fedha yanalenga kufanikisha mambo 20 muhimu, yakiwamo Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa mwaka 2014, Uchaguzi Mkuu 2015, kukamilisha
mchakato wa Katiba na nyongeza ya mishahara na kulipa kwa wakati.
Waziri
huyo alisema makadirio ya matumizi ya maendeleo ni Sh7.7 trilioni sawa
na asilimia 39 ya matumizi yote ya Serikali na kati ya fedha hizo miradi
ya maendeleo imetengewa Sh5.4 trilioni sawa na asilimia 27 na matumizi
mengine ya maendeleo ni Sh2.2 trilioni.
Pia
alisema katika mwaka wa fedha 2014/2015, Serikali imekusudia kukopa
Sh4.2 trilioni kutoka vyanzo vya mapato vya ndani na nje ili kuziba
pengo la mapato.
Serikali
imetenga Sh5.4 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na imeonyesha
vipaumbele vyake vikuu katika miradi hiyo ya maendeleo ni kilimo, elimu,
maji, utafutaji wa rasilimali fedha, nishati, uchukuzi na uboreshaji wa
mazingira ya kufanyia biashara huku michezo ikikosekana katika
vipaumbele hivyo.
Sisi
tunaamini sekta ya michezo ilistahili kuingizwa katika vipaumbele vya
Serikali katika bajeti yake ya 2014/15 kwani sekta hii ikitengewa fedha
nyingi na kuwekewa misingi imara ni chanzo kikubwa cha mapato.
Tumeshuhudia
katika nchi mbalimbali duniani ambazo Serikali zao zinaithamini sekta
ya michezo kwa kuitengea bajeti kubwa ya miradi ya maendeleo,
wanamichezo wa nchi hizo wamekuwa wakinufaika na kupata mapato makubwa
na hivyo kulipa kodi kubwa ambazo zimekuwa ni chanzo kikubwa cha mapato.
Ni wazi
ukiangalia kwa undani nchi zote zilizoendelea katika michezo utaona kwa
nanma moja au nyingine kuna nguvu nyingi za Serikali za nchi hizo hasa
utagundua Serikali za nchi zao hutoa fedha na kuboresha miundombinu ya
michezo ili kuweza kuwa na programu nzuri za kuendeleza michezo na
husaidia timu zao za taifa.
Tunaamini
kwamba hata kama mapato ya nchi ni madogo, Serikali ikiwa na dhamira ya
dhati ya kupenda michezo na kuipa kipaumbele, haitashindwa kupata
vyanzo mbalimbali vya mapato kwa ajili ya kuhakikisha sekta ya michezo
inakuwa katika vipaumbele vya bajeti na kutengewa fedha za kutosha kwa
ajili ya miradi ya maendeleo.
Inaeleweka
kuwa Tanzania tuna bahati ya pekee duniani kwani tuna utajiri mkubwa wa
rasilimali ambazo kama kama zitatumika ipasavyo zitanufaisha sana taifa
letu na wanamichezo wetu watapata vifaa vya michezo kwa bei nafuu,
viwanja vya michezo na walimu bora wa michezo.
Hata
hivyo katika hali ya kushangaza utajiri huo wa rasilimali umekuwa
ukionekana kunufaisha wachache huku hali hiyo ikionekana kama ni jambo
la kawaida. Tunatarajia wabunge watatuunga mkono na kuisimamia Serikali
ipasavyo katika kuhakikisha kuanzia Bunge hili la bajeti sekta ya
michezo inatambuliwa na kutengewa fedha nyingi katika miradi ya
maendeleo.(CHANZO: MWANANCHI) (FS)
JINI SIZAI TENA NJE YA NDOA
MSANII wa filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kuwa hayupo tayari kuzaa tena nje ya ndoa mpaka atakapoolewa.
Akistorisha na paparazi wetu, Jini Kabula alisema hawezi kurudia tena jambo hilo kwani anaogopa kuchanganya damu kwa vile baadaye watoto wanaweza kuja kugombana na kukosa maelewano hivyo anamuomba Mungu atimize ahadi ya kuolewa ndipo azae.
“Nilizaa na Chuz kwa sababu tulikubaliana kuzaa tu na siyo kuoana hivyo kwa sasa nasubiri niingie kwenye ndoa ndipo nizae, sitaki kuwachanganya watoto wangu,”alisema Jini Kabula.
Akistorisha na paparazi wetu, Jini Kabula alisema hawezi kurudia tena jambo hilo kwani anaogopa kuchanganya damu kwa vile baadaye watoto wanaweza kuja kugombana na kukosa maelewano hivyo anamuomba Mungu atimize ahadi ya kuolewa ndipo azae.
“Nilizaa na Chuz kwa sababu tulikubaliana kuzaa tu na siyo kuoana hivyo kwa sasa nasubiri niingie kwenye ndoa ndipo nizae, sitaki kuwachanganya watoto wangu,”alisema Jini Kabula.
SHILOLE ABADILI JINA LA HOTEL YAKE AMBAYO ILIKUA INAITWA "CHUNA BUZI"
Mwanamuziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amebadilisha jina la Hoteli yake mpya anayotarajia kuifungua maeneo ya Mwananyamala, awali jina la Hoteli hiyo aliiita Chuna Buzi Hotel lakini baada ya ushauri sasa anaipa jina la Igunga One Restaurant.
“Nimeamua kubadili jina baada ya kushauriwa na rafiki zangu, maana jina la kwanza lilikuwa na utata, na hata lilikuwa na maswali mengi kwa wapita njia, lakini jina la sasa lipo poa kila mtu kalifurahia,”anasema
Moja ya sababu nyingine iliyopelekea kubadili jina na kuipa jina la Igunga One Restraurant, ni kutokana na huduma itakayopatikana katika Hotel hiyo kutauzwa
MASKINI MTOTO HUYU, ANASUMBULIWA NA GONJWA LA AJABU..SOMA ZAIDI HAPA
Mtoto AMISA MALEBHI(miaka 2 na miezi sita)ambaye ana matatizo ya jicho la
kushoto anahitaji msaada wa kupelekwa hospitali ya KCMC Moshi kwa ajili
ya matibabu kwa atakayeguswa anaweza kuwasiliana na mama yake mzazi
TAUSI HAMISI mkazi wa Ufuluma wilaya ya Uyui mkoani Tabora....Mtoto huyu
imeelezwa kuwa endapo atacheleweshwa kupatiwa msaada anaweza kupata
Saratani ya Jicho,...KWA HALI NA MALI FANIKISHA MATIBABU YA MTOTO HUYU
AMBAYE ANAHITAJI FURAHA KAMA WALIVYO WATOTO WENGINE.
Mama
wa mtoto huyo Bi.TAUSI HAMISI akiwa barabarani katika kutafuta msaada
wa matibabu ya mtoto wake huku baba wa mtoto huyo AMISA alifariki dunia
miezi michache iliyopita baada ya kupata ajali ya pikipiki.
Mtoto AMISA MALEBHI(miaka 2 na miezi sita)ambaye ana matatizo ya jicho la kushoto anahitaji msaada wa kupelekwa hospitali ya KCMC Moshi kwa ajili ya matibabu kwa atakayeguswa anaweza kuwasiliana na mama yake mzazi TAUSI HAMISI mkazi wa Ufuluma wilaya ya Uyui mkoani Tabora....Mtoto huyu imeelezwa kuwa endapo atacheleweshwa kupatiwa msaada anaweza kupata Saratani ya Jicho,...KWA HALI NA MALI FANIKISHA MATIBABU YA MTOTO HUYU AMBAYE ANAHITAJI FURAHA KAMA WALIVYO WATOTO WENGINE.
Mama wa mtoto huyo Bi.TAUSI HAMISI akiwa barabarani katika kutafuta msaada wa matibabu ya mtoto wake huku baba wa mtoto huyo AMISA alifariki dunia miezi michache iliyopita baada ya kupata ajali ya pikipiki.
NI ZAIDI YA LAANA HII 18+ AIBU KWA WATANZANIA:VIDEO YA WANAWAKE WACHEZA KAMA WALIVYOZALIWA (UCHI WA MNYAMA) MCHANA KWEUPEEEEE!!
maadili ya kitanzania yanapotea au ndo yanajengeka ,hebu cheki video hii kwanza
Kutokana na maadili tumeshidwa kuiweka video hii ;;;
Sitasahau siku nilipomfumania mpenzi wangu akiwa hotelini na rafiki yangu ambaye ni zaidi ya ndugu
Sikutaka tena mtu akae na kuniambia kuhusu eti nitulie au niwe na mtu nimwitaye mpenzi wangu au mke mtarajiwa.
Hebu fikiri mtu unapigiwa simu na kuambiwa kuwa binti uliyempenda na kukaa naye kwa zaidi ya miaka mitatu na mkitarajia kuanza mipango ya kukaa wawili na mahaba tele, eti yuko hotel moja katika chumba fulani akila raha na rafiki yako wa karibu zaidi ambaye ni zaidi ya ndugu?
Na kama haitoshi umeenda na kumfumania na kwa kuwa bado unampenda unafamua umsamehe kwa kuzingatia muda ambao umekaa nae na mkijiandaa kuwa mtu na mke kuwa ungepotea bure.
Lakini pamoja na kumsamehe huko bado ndani ya wiki unakuja kugundua kuwa mpenzi wako ana mimba na yeye mwenyewe baada ya kumbana sana anakuja kuthibitisha kuwa ni mimba ya rafiki yako?????????
oooh no thanks!!! it was more than hell.........
Niliachana nae na kwa kuwa kuna vitu tulishavinunua na kuviweka kama mali zetu za kuanzia maisha na baadhi ya miradi ya pamoja nikaamua kumgawia alichostahili ili kutoa maneno kwa baadhi ya ndugu nna rafiki zake wa karibu waliojua mahusiano yetu na mali hizo.
Na kuanzia hapo nilianza kuishi maisha ya mtu mwenye stress yaani maisha ya kuwa mlevi, wanawake kwa sana yaani leo huyu kesho yule hata kama waengi walionyesha kuwa wangekuwa na mapenzi ya dhati ila nikasema NO WAY ........sitaweza amini tena mwanamke.
Nilifurahia sana kuona mwanamke akilia juu ya mimi baada ya kuachwa au kuona nimemsaliti kwani ndio ilikuwa tiba ya stress zangu na niliona kuwa kila mwanamke alihitaji kupata adhabu sawa na ile ambayo ningempa Jane ambaye alinifanyia umafia wa aina yake kwa karne hii.
Kila nilipoiona sura ya ya jane iwe mtaani au kwenye mitandao ya kijamii na pia kuona baadhi ya wanawake ambao ni mastaa wa kibongo au nje wakiruka leo na mwanaume huyu kesho na yule hasira zilizidi na nikaona hizi ndio tabia za kila mwanamke hivyo nami nikazidisha bidii ya kuchukua na kuwaacha wanawake pamoja na ushauri mzuri niliopata toka kwa marafiki lakini bado moyo uligoma kubadili msimamo na kusema lazima fuledi anyooshe adabu za hawa mabinti.
Ijumaa mmoja nikajivuta mpaka hotel moja marufu sana hapa jijini mbeya na kisha nikakaa na kuagiza pombe yangu na kuendelea kuburudika huku nikiperuzi mitandao mbalimbali ya kijamii na kujisomea baadhi ya comment za wadau wa ukurasa huu na kama ujuavyo kuna mabingwa wa kukomenti facts na wengine wanajijua wenyewe matusi kama walizaliwa hukoooo..... lakini ndio marafiki unakuwa huna jinsi tena.
Pale nilipokaa pembeni yangu alikaa dada mmoja ambaye kiukweli alionekana kuwa busy na kazi zake huku akiendelea kupata vinywaji na inaonekana kama sio kaaririwa sehemu basi alikuwa na kazi zake binafsi kwani alionekana kuwa smart na mwenye kujitambua..
Ni ule uzuri wake ndio ulio nifanya niwe nikimkodolea macho kila dakika na dakika chache ikanibidi nitulie baaada ya kuingia kundi la marafiki zake na kunifanya niwe napata taabu kumkodolea macho kutokana na kuzungukwa na wale warembo bomba lakini kila dakika niliona nazidiwa hivyo nikawa na kiburi cha kumwangaliac tu bila kujali.
Nikasema moyoni huyu leo simwachi naka haitoshi nae lazima alizwe tu kama wengine maana ule uziri wake ulikuwa wa viwango vya kuridhisha na alifaa kwa matumizi yote kama vile kwenda naye outing, kujirusha naye na hata kutambulisha kwa marafiki, wafanyakazi na bado akakodolewa mimacho na watu wenye nia mbaya na viumbe hawa kama mimi.
Uzalendo ukanishida kwani kuna mwanya ulijitokeza nikasema hapa sikosei yaani nafanya kweli kwani kuna simu iliita na akatokanje ili kuipokea kwa utulivu.
Alipotoka nje tuu kuongea na simu nami nikamfuata nikijifanya naelekea nje pia kupokea simu na kisha kumdaka na kuanza kuongea nae mambo mawili matatu lakini jambo la msingi lilikuwa ni kubadilishana mawasiliano.
Siku zikaanza kusonga mbele na tukaanza kuwa na ukaribu wa kutoana out mara kukaribishana nyumbani na nilichomshangaa ni kuwa katika kaa yangu hakuwa na tabia ya kuingilia ratiba zangu, kunishtukiza kuja home kwani kila alipotaka kuja aliniuliza kama nina muda wa kuonana nae na kama nilimwambia nipo busy alielewa hata kama nilimdanganya.
Lakini jambo la kuvutia zaidi ni kuwa hata tukitoka out naye alitamani alipe bill, akitaka kuja na marafiki aliniuliza na hakuwa mtu wa kunipekuwa wala kutaka kuongelea issue yoyote ya masuala ya ndoa mimi na hakuwa na tamaa bali alikuwa mwelewa kwa kila jambo.
Kuna mara nilimuudhi hata kwa makusudi lakini alinishangaza kwani uso wake ulikuwa na furaha na kama mabishano yangezidi angeniacha na kuondoka bila neno na kesho yake angenifuata na kuja kuyadadili au kuna wakati alinishika na kunikiss na kusema MABISHANO HAYAJENGI TUKAE NA KUTATUA NA TUWE NA MUDA WA FURAHA ZAIDI KULIKO UGOMVI..
Uuuuh!!! kidume nakuja kuzinduka tuna mahusiano ya zaidi ya mwaka na nusu na jambo zuri kuliko yote sijawahi kufikiri kumwacha na kila siku namwona mzuri na wakunivutia mwenye mapenzi moto moto zaidi ya jana.
Na ile tabia yake ya kuwa wa kwanza kuomba msamaha hata kama ningemkosea na kunisihi tuwe na maelewano pamoja na ule wepesi wake wa kunisikiliza kwa kila jambo na kunipa ushauri mzuri, vikaanza kunipa nami ujasiri wa kuomba msamaha pale nilipokosea na kupenda kuepuka kumkwaza..
Kwa kweli nikaanza kufurahia kuwa naye nikaanza kumiss uwepo wake kila mara hasa siku za weekend na nikwa na tabia ya kutoka nae, kumshirikisha mambo yangu na matatizo yangu na kwa mbaaali nikajiona napunguza unywaji taratibu na baadae kuwa natumia muda mwingi kufanya mambo ya msingi na kuwa naye na kusahau habari za kubadilisha wanawake na ule ukatili na jane akapotea akilini..
Miaka miwili ilipotimia tu nikaomba tuanze taratibu za kuishi pamoja na akanikubalia ingawa akaomba tukae chini na kufikiri tutahitaji kuja kuishi maisha ya namna gani tukiwa kama mme na mke.
Nikamwambia natamani maisha haya ya urafiki yaendelee mika yetu yote naye akaonyesha kufurahia sana tamko hilo.
Leo hii ni mwaka wa saba tangu tuoane naye na tunaishi kama tupo siku ya kwanza ya uhusiano wetu na tumekuwa tunaitana marafiki hata watoto wetu wanatufurahia kuwaa na wazazi kama sie.
Kila nikikumbuka visa vilivyopita nakaa na kusema sio wanawake wote wabaya ila wanawake wana nafasi ya kutufanya sisi tuishi vyema au vibaya.
Hadithi hii ni ya uongo ila kama unaona iko poa fuata nyayo hizo kwa kuyajenga mahusiano yako na umpendaye kuwa yenye furaha na kuepuka tabia za usaliti na pia kwa kujifunza kumpenda atakavyo na kuja kuishi mtakavyo.
MTOTO WA MIAKA 8,ABAKWA,AZIBWA MDOMO NA SEHEMU ZA SIRI KWA NGUO,KISHA KUNYONGWA
Katika hali ya kusikitisha na kutia
simanzi, mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Kalangalala
mjini Geita aitwaye Magreth Kervini(8) amebakwa na kufungwa nguo
mdomoni na sehemu za siri kisha kunyongwa shingo hadi kufa na kutupiwa
uvunguni mwa kitanda usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Nyerere mjini
Geita.
Tukio hilo lililoshangaza watu wengi mjini Geita
limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 8 usiku ambapo mmoja kati ya walioshuhudia tukio hilo amesema usiku huo kulikuwa na ugomvi kati ya mpangaji mwenzake aitwaye Shida ambaye alikuwa analazimishwa kufanya mapenzi kwa lazima na shemeji zake wawili ambao ni Kurwa Juma na Dotto Juma(30-35) ambaye ni mke wa mdogo wao Shija Juma.
Shuhuda huyo aliendelea kusimulia kuwa mpangaji huyo (mme wa Shida) Shija siku hiyo alikuwa ameenda kulala kwa mke mwingine katika maeneo ya Bomani lakini kufuatia ugomvi uliokuwa ukiendelea nyumbani kwake, alipigiwa simu na mdogo wa mke wake anayekaa naye huko mtaa wa Nyerere na kuambiwa kuwa wadogo zake wamekuja nyumbani na wamo ndani wanafanya fujo wanataka kumbaka yake dada yake(Shida).
Mara baada ya kupata taarifa hizo Shija aliondoka alikokuwa amelala akapanda pikipiki hadi kwa mke wake Shida na alipofika aliwakuta ndugu zake (Kurwa na na Dotto) wamo ndani wakigombana na shemeji yao.
Kufuatia kitendo hicho Shija alianza kuwapiga Kurwa na Dotto hali iliyomfanya Dotto kutoka nje na kujificha nje ya geti wakati huo huo ndani Kurwa na Shija wakiendelea kugombana.....
Kufuatia kipigo alichokipata,Kurwa naye alitoka nje na Shija baada ya kuona ndugu zake wametoka,mke wa Shija(Shida) alifunga mlango na akalala huku Shija akirudi kulala Bomani alikokuwa amelala awali.
Shuhuda huyo anasimulia kuwa....
“Baada ya muda mfupi Dotto alirudi baada ya kuona Kurwa na Shija wameondoka,
na ndipo akaenda kwenye mlango wa shemeji yake akakuta umefungwa na kuamua kuhamia kwenye mlango mwingine na ndipo alipogonga mlango huo akatoka mtoto Magreth Kervini (8) kumfungulia kwani alijua kuwa atakuwa mama yake aliyekuwa ameenda kazini huenda amerudi kwani mama yake na mtoto Magreth anafanya kazi Makongoro bar.
Inadaiwa kuwa Dotto baada ya kufunguliwa mlango na Magreth Kervini,aliingia na kuanza kumbaka mtoto huyo na baada ya kutekeleza adhima yake alimnyonga hadi kufa na akamfunga nguo mdomoni na sehemu za siri akatoka nje na alipotoka nje alienda tena kwenye mlango wa nyumba nyingine ya mama Mulugu Nyamuhanga ili akafanye unyama mwingine.
Baada ya muda mfupi mama huyo Mulugu Nyamuhanga alisikika akipiga kelele za kuomba msaada kwamba amevamiwa na majambazi majirani walitoka nje wakakuta mlango wa binti huyo ukiwa umefunguliwa na walipoangalia walikuta binti huyo akiwa amefungwa kanga na damu zikitoka sehemu za siri akiwa amekufa.
Hata hivyo kuna na tetesi kuwa mama mzazi wa mtoto aliyeuawa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Dotto.
Kwa upande wa mama yake mzazi Peki Makoye (29) hakuwepo nyumbani na hakuwa na mawasiliano ya simu, alikuwa kazini.
Alisema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Dotto bali ana uhusiano na Kurwa na kuongeza kuwa huenda Dotto ndiye amefanya unyama huo kwani alishawahi kumtaka kimapenzi na akakataa.
Mpasa sasa hivi Shija,Kurwa na Shida wanashikiliwa na jeshi la polisi.
Kamanda wa polisi mkoani Geita kamishina msaidizi Joseph konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi bado unaendelea ili hatua zaidi zichukuliwe
Tukio hilo lililoshangaza watu wengi mjini Geita
limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 8 usiku ambapo mmoja kati ya walioshuhudia tukio hilo amesema usiku huo kulikuwa na ugomvi kati ya mpangaji mwenzake aitwaye Shida ambaye alikuwa analazimishwa kufanya mapenzi kwa lazima na shemeji zake wawili ambao ni Kurwa Juma na Dotto Juma(30-35) ambaye ni mke wa mdogo wao Shija Juma.
Shuhuda huyo aliendelea kusimulia kuwa mpangaji huyo (mme wa Shida) Shija siku hiyo alikuwa ameenda kulala kwa mke mwingine katika maeneo ya Bomani lakini kufuatia ugomvi uliokuwa ukiendelea nyumbani kwake, alipigiwa simu na mdogo wa mke wake anayekaa naye huko mtaa wa Nyerere na kuambiwa kuwa wadogo zake wamekuja nyumbani na wamo ndani wanafanya fujo wanataka kumbaka yake dada yake(Shida).
Mara baada ya kupata taarifa hizo Shija aliondoka alikokuwa amelala akapanda pikipiki hadi kwa mke wake Shida na alipofika aliwakuta ndugu zake (Kurwa na na Dotto) wamo ndani wakigombana na shemeji yao.
Kufuatia kitendo hicho Shija alianza kuwapiga Kurwa na Dotto hali iliyomfanya Dotto kutoka nje na kujificha nje ya geti wakati huo huo ndani Kurwa na Shija wakiendelea kugombana.....
Kufuatia kipigo alichokipata,Kurwa naye alitoka nje na Shija baada ya kuona ndugu zake wametoka,mke wa Shija(Shida) alifunga mlango na akalala huku Shija akirudi kulala Bomani alikokuwa amelala awali.
Shuhuda huyo anasimulia kuwa....
“Baada ya muda mfupi Dotto alirudi baada ya kuona Kurwa na Shija wameondoka,
na ndipo akaenda kwenye mlango wa shemeji yake akakuta umefungwa na kuamua kuhamia kwenye mlango mwingine na ndipo alipogonga mlango huo akatoka mtoto Magreth Kervini (8) kumfungulia kwani alijua kuwa atakuwa mama yake aliyekuwa ameenda kazini huenda amerudi kwani mama yake na mtoto Magreth anafanya kazi Makongoro bar.
Inadaiwa kuwa Dotto baada ya kufunguliwa mlango na Magreth Kervini,aliingia na kuanza kumbaka mtoto huyo na baada ya kutekeleza adhima yake alimnyonga hadi kufa na akamfunga nguo mdomoni na sehemu za siri akatoka nje na alipotoka nje alienda tena kwenye mlango wa nyumba nyingine ya mama Mulugu Nyamuhanga ili akafanye unyama mwingine.
Baada ya muda mfupi mama huyo Mulugu Nyamuhanga alisikika akipiga kelele za kuomba msaada kwamba amevamiwa na majambazi majirani walitoka nje wakakuta mlango wa binti huyo ukiwa umefunguliwa na walipoangalia walikuta binti huyo akiwa amefungwa kanga na damu zikitoka sehemu za siri akiwa amekufa.
Hata hivyo kuna na tetesi kuwa mama mzazi wa mtoto aliyeuawa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Dotto.
Kwa upande wa mama yake mzazi Peki Makoye (29) hakuwepo nyumbani na hakuwa na mawasiliano ya simu, alikuwa kazini.
Alisema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Dotto bali ana uhusiano na Kurwa na kuongeza kuwa huenda Dotto ndiye amefanya unyama huo kwani alishawahi kumtaka kimapenzi na akakataa.
Mpasa sasa hivi Shija,Kurwa na Shida wanashikiliwa na jeshi la polisi.
Kamanda wa polisi mkoani Geita kamishina msaidizi Joseph konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi bado unaendelea ili hatua zaidi zichukuliwe
RIDHIWANI AMPONGEZA DIAMOND PLATINUMZ KUPITIA UKURASA WAKE WA FACEBOOK, SOMA UJUMBE HAPA
Kwanza
Hongera sana kwa kushinda Kili Awards.Hii ni zawadi nzuri unayoweza
kupata baada ya Jitihada,Kujituma, na Burudani nzuri kwa washabiki
wako.Mungu akujalie mema zaidi ya hapo.Hongera sana Platnumz.
WASHINDI WA KILLI MUSIC AWARDS-2014 HAWA HAPA
Fid Q akiwa katika pozi
la picha na tabasamu la ukweli baada ya mwana Hip hop bora Tanzania.
Diamond akitoa machache
baada ya kupata Tuzo
Kikundi cha Weusi
wanaotamba na wimbo wa Gere nao hawakuziachia tuzo hivi hivi.
Background
Kilimanjaro Music Awards ni tuzo zinazotolewa kila mwaka kwa wasanii wote nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Hujulikana kama “Kili Music Awards” kutokana na mdhmini wake mkuu ambaye ni Kilimanjaro Premium Lager.
Tuzo huwa zinatolewa kila mwaka kwa dhumuni la kuwapa uwamko wasanii wa Afrika Mashariki, kundeleza vipaji na usia kwa jamii ya kiafrika kwa ujumla, hivyo hupewa kama pongezi kwa kazi walioifanya kwa uelimisha jamii katika kipindi cha mwaka mzima.
Hizi ni tuzo pekee zinazowaenzi wasanii wa aina zote za muziki, zilianzishwa toka mwaka 1999 na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA). Toka wakati huo, tuzo hizi zimekua maradufu na zimedhaminiwa kwa ushirikiano na bia ya Kilimanjaro Premium Lager toka 2003.
Washindi hawapati kutambulika na nafasi ya kuonekana katika vyombo vya habari tu, bali hushinda zawadi za fedha taslimu zinazowasaidia kuendeleza muziki wao. Lengo la Kilimanjaro Tanzania Music Awards ni kuwahamasisha wasanii kutoka sehemu mbalimbali nchini kufikia kilele cha mafanikio ya kimuziki, kwa kutambua kwamba ndoto zao hazishii ngazi ya kitaifa, bali kimataifa pia.
WASHINDI WA KILLI MUSIC AWARDS 2014
1. WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA TANZANIA - Bora Mchawi, Dar Bongo Massive
2. MSANII BORA CHIPUKIZI ANAYEIBUKA - Young Killer
3. WIMBO BORA WA ZOUK - Yahaya, Lady Jaydee
4. WIMBO BORA WA AFRO POP - Number One, Diamond Platnumz
5. WIMBO BORA WA RAGGA / DANCEHALL - Nishai Chibwa Ft Juru
6. WIMBO BORA WA RAGGAE - Niwe na wewe, Dabo
7. WIMBO BORA WA TAARAB - Wasiwasi wako, Mzee Yusuf
8. KIKUNDI CHA MWAKA CHA TAARAB - Jahazi Modern Taarab
9. MWIMBAJI BORA WA KIKE TAARAB - Isha Ramadhani
10. MWIMBAJI BORA WA KIUME TAARAB - Mzee Yusuf
11. WIMBO BORA WA KISWAHILI BENDI - Ushamba mzigo, Mashujaa Band
12. MWIMBAJI BORA WA KIKE BENDI - Luiza Mbutu
13. MWIMBAJI BORA WA KIUME BENDI - Jose Mara
14. RAPA BORA WA MWAKA BENDI – Furguson
15. BENDI YA MWAKA - Mashujaa Band
16. MWIMBAJI BORA WA KIKE, KIZAZI KIPYA - Lady Jaydee
17. MWIMBAJI BORA WA KIUME, KIZAZI KIPYA – Diamond
18. KIKUNDI CHA MWAKA CHA KIZAZI KIPYA – Weusi
19. WIMBO BORA WA RNB - Closer, Vanessa Mdee
20. WIMBO BORA WA HIP HOP - Nje ya Box, Nick wa Pili Ft Joh Makini & Gnako
21. MSANII BORA WA HIP HOP - Fid Q
22. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHA / KUSHIRIKIANA - Muziki Gani, Nay wa Mitego ft Diamond
23. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI - Tubonge, Jose Chameleone
24. MTUNZI BORA WA MWAKA TAARAB - Mzee Yusuf
25. MTUNZI BORA WA MWAKA BENDI - Christian Bella
26. MTUNZI BORA WA MWAKA KIZAZI KIPYA – Diamond
28. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA, TAARAB – Enrico
29. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA, BENDI – Amoroso
30. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA, KIZAZI KIPYA - Man Water, Combination Sound
31. HALL OF FAME, INDIVIDUAL - Hassan BItchuka
32. HALL OF FAME, INSTITUTION - Masoud Masoud
33. VIDEO BORA YA MUZIKI YA MWAKA - Number One, Diamond
34. WIMBO WA MWAKA - Number One. Diamond
35. MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE WA MUZIKI - Isha Ramadhani
36. MTUMBUIZAJI BORA WA KIUME WA MUZIKI - Diamond
CHANZO: www.bongosound.com
Sunday, 4 May 2014
MVUA YATIBUA SHOO YA LADY JAY DEE
MVUA kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia
leo imetibua shoo ya mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee
nakusababisha shoo hiyo kusogezwa mbele mpaka itakapotangazwa.
Shoo hiyo iliyopangwa kufanyika katika
ukumbi wa Nyumbani Lounge ambapo mbali na Lady Jay Dee walikuwa
wamealikwa wasanii wengine wakiwemo, Prof. Jay, Patricia Hillary, Roma
mkatoliki, Baghdady na wengine kibao.
Mvua hiyo ambayo ilianza kunyesha toka
majira ya jioni na kuzua hofu ya kuendelea kwa shoo mpaka kufikia saa
saba za usiku mwanadada Jide alipanda jukwaani na kuomba radhi kwa
mashabiki waliokuwa wamehudhuria ukumbini hapo kutokana na hali hiyo
nakuwahaidi kuwa shoo hiyo itarudiwa tena ila kwa wale waliojitokeza
watapatiwa tiketi ya shoo ijayo (Hawatalipa kiingilio tena). Baada ya
kuomba radhi alipiga nyimbo zake kadhaa akifuatiwa na wasanii wengine.