Wednesday 30 April 2014

POLISI MKOANI MANYARA YAKAMATA MISOKOTO 6,000

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, (SACP) Deusdedit Nsimeki, (kulia) akiwa na polisi wengine wa mjini Babati, wakati akiwaonyesha waandishi wa habari baadhi ya misokoto 6,000 ya Bangi waliyoikamata kwenye mabasi mawili hivi karibuni ambayo ilikuwa imewekwa kwenye mikate iliyokuwa imesafirishwa na watu wawili,ambao wamewekwa ndani.
Share:

JE WAJUA UNA KILA SABABU YA KUOGA NA MPENZI WAKO KAMA UJUI SOMA HAPA

 

Unapo kuwa nyumbani , tena ni vizuri ikiwa weekend mkiwa wote mko nyumbani, hakikisha unapata nafasi ya kuoga pamoja na mpenzi wako, hivi ni vitu vidogo dogo sana vinavyoweza kufanya mapenzi yenu yawe mapya kila siku.

Wakati wa kuoga fanya mbwe mbwe kidogo msugue mwenzako, mgongoni hata sehemu nyingine hii sio kwa wanawake tu hii ni kwa wapenzi wote wawili tena hususani zaidi kwa wanaume hili ndio zoezi lao, mkimaliza kuoga chukua taulo na mfute mke wako vizuri kisha, chagua yale mafuta anayoyapenda zaidi mpake huku mkipiga story mbili tatu.

Inabidi tufahamu kuwa kunavitu unaweza kuviona ni vya kipuuzi sana kwenye mapenzi lakini, ndio vinavyokukosesha maksi kila siku. Usipomfanyia hivyo kuta watu wengine watafanya halafu utaonekana huna maaana..!! 

Kantagaze Nimekwambia
Share:

Picha mbili za maamuzi ya Samuel Eto’o kuhusu ile ishu ya Dani Alves

Screen Shot 2014-04-30 at 10.44.39 AMUnaambiwa club ya Villareal imemfungia maisha yule shabiki ambae alionyesha kitendo cha kibaguzi kwa kumrushia ndizi Dani Alves, kitendo ambacho kilitafsiriwa kwa Alves kufananishwa na nyani.
Wachezaji kadhaa wamemsupport kwa ujasiri wake wa haraka na kula ndizi hiyo aliyotupiwa uwanjani alafu akaendelea na game kama kawaida ambapo miongoni mwa waliomsupport ni Neymar.
Mwingine alieonyesha support ni Samuel Eto’o ambae baada ya kuweka picha zake mbili akiwa kwenye magari yake ya kifahari na kuandika ‘samahani nilisahau kuuliza, kuna yeyote anataka kuwa nyani kama mimi?’
Screen Shot 2014-04-30 at 9.59.38 AM
Screen Shot 2014-04-30 at 10.00.49 AM
Screen Shot 2014-04-30 at 10.01.36 AM
Screen Shot 2014-04-30 at 10.08.23 AM
Share:

MTIHANI MPYA KIDATO CHA NNE HUU HAPA, KUSAMBAZWA MEI 10


Wanafunzi wa Kidato cha Nne, watafanya mitihani miwili ya Taifa mwaka huu, baada ya kuongezwa mtihani wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), ambao utatumika kuwapima walivyojiandaa na Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Sekondari.
Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari, Paulina Mkonongo, alitangaza utaratibu huo jana na kufafanua kwamba lengo ni   kubaini wanaohitaji msaada kabla ya mtihani wa mwisho, ili kuboresha taaluma darasani. 
Kwa mujibu wa Paulina, mtihani huo wa BRN, utafanyika kwa masomo machache lakini yanayosomwa na wanafunzi wote ambayo ni Baiolojia, Hisabati, Kiswahili na Kiingereza.
Paulina alisema mtihani huo wa majaribio, tayari umeanza kuandaliwa na utasambazwa kwa maofisa Elimu nchini ifikapo Mei 10 mwaka huu, na barua kuhusu kufanyika kwa mtihani huo imeshatumwa kwa makatibu tawala wote, ili kuanza maandalizi.
Matokeo ya mtihani huo, yanatarajiwa kutumika kubaini mada ngumu kwa wanafunzi,  wanaohitaji msaada na kuwapa walimu mwanga kuhusu wapi wanafunzi hao wanahitaji msaada na lengo ni kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Tayari  tangu mwaka jana mikoa 12 ilianza kushiriki katika programu iliyohusisha mafunzo kwa walimu 4,064 wa masomo husika, na mikoa 13 iliyosalia itashiriki programu hiyo mwaka huu. 
Mafunzo ya walimu wa mikoa hiyo 13 kwa mujibu wa Paulina, yatafanyika Juni 2014 na programu ya mafunzo rekebishi kwa wanafunzi wenye upungufu, itaanza Julai mwaka huu kulingana na matokeo ya mtihani watakaofanya.
“Tutatoa mtihani wa majaribio kwa wanafunzi wa kidato cha nne, ili kubaini maeneo yenye wanafunzi wanaohitaji msaada zaidi na kutoa utaratibu wa mafunzo rekebishi na mafunzo kazini,  ili kuwajengea uwezo walimu wa kuwasaidia wanafunzi walioko kwenye hatari ya kutofanya vema,” alisema Paulina.
Hata hivyo, Paulina alisema katika utekelezaji utoaji wa mtihani huo, wanakabiliwa na changamoto ya kuwapatia mafunzo wakuu wa shule zisizo za serikali, kuchapisha kitabu cha mwongozo na ziara za wasimamizi wa elimu katika ngazi mbalimbali kutoa ushauri.
Tayari walimu wakuu 3,001 wa shule za Serikali wamepatiwa mafunzo na Taasisi ya Uongozi wa Elimu Bagamoyo (ADEM) katika maeneo yaliyoainishwa, huku kitabu hicho cha mwongozo kikiwekwa kwenye tovuti ya Wizara.
Paulina alisema mikakati endelevu iliyopo, inalenga kuendeleza mafunzo ya walimu kazini, ili kuwajengea uwezo kulingana na wakati na mahitaji ya mitaala.
Mbali na mafunzo hayo, pia wanalenga kuwajengea walimu tabia ya kutunga mitihani bora ya kupima mchakato wa ufundishaji, kubaini wanafunzi wanaohitaji kusaidiwa zaidi, kubaini mada ngumu na kutoa mafunzo rekebishi kwa wanafunzi.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk Charles Msonde, alisema vitabu rekebishi vitaonesha wanafunzi waliofanya vizuri katika kila swali, waliojibu vibaya na swali lilikuwa likitaka nini.
Vitabu hivyo vitasaidia walimu na wanafunzi kubaini makosa mbalimbali yanayofanywa na watahiniwa wakati wa kujibu maswali na kutumia mbinu bora za kujibu maswali.
“Mwisho wa vitabu hivyo, kuna mada zilizofanywa vizuri na vibaya na jinsi ya kusaidia walimu wahakikishe wanafunzi wanafaulu mada hizo,” alisema.
Vitabu hivyo kwa shule za msingi vimetolewa vya masomo ya Kiswahili, Hisabati, Kiingereza, Sayansi na Maarifa ya Jamii kwa ajili ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2012 na 2013.
Kwa sekondari, vimetolewa kwa masomo ya Hisabati, Uraia, Historia, Jiografia, Kiswahili, Kiingereza, Baiolojia, Kemia na Fizikia kwa mwaka huo.
Dk Msonde alisema Baraza pia limepewa jukumu la kupanga shule katika makundi ya ubora wa ufaulu, ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule za msingi na sekondari, na kuwajengea walimu na wanafunzi hali ya ushindani na kujitambua kama shule imepanda au imeshuka.
Makundi ya ufaulu yatapangwa kwa kutumia rangi za kijani kwa shule zenye ufaulu wa juu, njano kwa zenye ufaulu wa kati na nyekundu kwa shule zenye ufaulu wa chini kwa shule za msingi na sekondari.
Share:

BUS LA AM COACH LAPATA AJALI

Basi la Am coach limepata ajali eneo la ipuli na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja,chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi...........

Basi
la Am coach limepata ajali eneo la ipuli na kusababisha kifo cha
mwanafunzi mmoja,chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi
hilo,abiria wengine wamenusurika isipokuwa wapo ambao wamepata mshtuko
mkubwa.Endelea kuwa nasi taarifa kamili inakujia.
 
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATANO

Share:

Warioba awataja wasaliti wa Nyerere



Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema wanasiasa wanaomtuhumu kwa kumsaliti Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuhusu Muungano, ndiyo wasaliti kwa kuwa waliingiza kwenye Katiba, mambo yanayokinzana na makubaliano ya Muungano huo.
Jaji Warioba amesema usaliti huo ni pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuondoa mamlaka ya Bunge la Muungano katika utungaji wa sheria, kuitambua Zanzibar kuwa nchi inayojitegemea na kuongeza mambo ya Muungano bila kufuata Katiba.
Ametoa kauli hiyo kujibu mwendelezo wa lugha za kejeli na matusi anazorushiwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wengi kutoka CCM na baadhi ya viongozi wa Serikali baada ya Tume aliyoiongoza kupendekeza muundo wa serikali tatu.
Akizungumza juzi usiku katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, Jaji Warioba alisema viongozi wa pande mbili za Muungano wanaomtuhumu, ndiyo waliouvuruga Muungano huo
“Mwalimu aliacha Bunge likiwa na mamlaka kamili, aliacha nchi ni moja, aliacha mambo ya Muungano 11 sasa yamekuwa ni 22, kwa bahati nzuri Rais Jakaya Kikwete alieleza bungeni hilo kwamba mambo hayo yaliongezekaje,” alisema na kuongeza:
“Katika kubaini kuongezeka kwa mambo ya Muungano ndivyo ilikuwa inapunguza mamlaka kwa Zanzibar, mambo 11 yaliyoachwa na mwalimu yaliingizwa kikatiba lakini haya yaliyoongezeka yalipatikana kienyeji.”
Jaji Warioba alisema enzi za uhai wake, Mwalimu Nyerere aliheshimu na kuilinda Katiba hivyo, walioivunja ndiyo wasaliti wa Muungano.
“Sasa kati ya mimi na wao ni nani msaliti kwa Mwalimu, angekuwapo (Mwalimu) ni yupi angeonekana msaliti wa Serikali ya Muungano? Wao ndiyo wameuvuruga, alichokiacha Mwalimu ni tofauti na kinachoonekana kwa sasa,” alisema Jaji Warioba.
Kuhusu Bunge
Jaji Warioba alisema mipango mingi ya maendeleo inayopangwa ndani ya Bunge la Muungano inatekelezwa upande wa Bara pekee.
“Si hivyo tu, Bunge hilo linajadili mambo ya Bara tu na halihusishi upande wa Zanzibar. Zanzibar nayo inajadili mambo yake na kujiamulia lakini jina la Bunge hilo ni Muungano,” alisema Jaji Warioba.
Kutokana na mazingira hayo, Jaji Warioba alisema Zanzibar iliamua kuondoa mamlaka ya Bunge hilo katika utungaji wa sheria kupitia Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
“Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema sheria zinazotungwa katika Bunge hilo zitatumika ndani ya pande zote za Muungano, lakini Zanzibar wakabadilisha hilo kupitia Katiba yao wakasema sheria zote zitakazotungwa ndani ya Bunge hilo, lazima zipitiwe tena na Baraza la Wawakilishi,” na kuongeza: “(Zanzibar) Hawakuishia hapo, wakafanya mabadiliko ya Katiba mwaka 2010 iliyovunja Katiba ikiitambua Zanzibar kama nchi kamili, ikaondoa mamlaka ya Rais wa Jamhuri kugawa wilaya na mikoa kwa Zanzibar tofauti na Katiba ya Muungano, kwa maana hiyo Zanzibar ikavunja nguvu ya Bunge la Muungano.”
Aidha, alisema hatua hiyo ilionekana kuuvunja Muungano kwa vitendo baada ya kuvunja mamlaka ya Rais na kutambua marais kamili katika nchi mbili tofauti.
“Kwa kawaida nchi inakuwa na amri jeshi mkuu mmoja ambaye anapigiwa mizinga 21, Jeshi la Muungano linapiga mizinga kwa marais wawili kitu ambacho hakiwezekani,” alisema.
Malalamiko ya Watanganyika
Jaji Warioba alisema Kwa upande wa Tanzania Bara, walibaini malalamiko ya Watanganyika kuwa ni pamoja na kukosa fursa mbalimbali ndani ya Zanzibar. “Watu wa bara nao wanasema Zanzibar inashiriki Bunge la Muungano, inakagua miradi ya bara na kuihoji lakini wao hawana nguvu ya kushiriki mambo hayo kwa upande wa Zanzibar,” alisema.
Aliongeza: “Mbaya zaidi wanasema Wazanzibari wanaweza kumiliki ardhi na kupata uraia kwa upande wa bara lakini haki hizo haziwezi kupatikana kwa Mtanganyika, njia pekee tukaona ni vyema Zanzibar nayo ilete mambo yake ndani ya Muungano lakini ikashindikana.”
Hoja ya takwimu
Jaji Warioba aliwataka wajumbe wa Bunge wasihangaike na takwimu badala yake wajibu maswali yaliyojitokeza kutoka kwa washirika wa Muungano.
“Takwimu siyo tatizo, sisi hatukufanya jambo jipya, ila ilikuwa ni kama marudio tu ya Tume ya Nyalali, wanahoji takwimu hizo je, hawakuona dosari kwa takwimu za maoni ya asilimia 20 kwa jaji Nyalali?
Alisema Tume yake ilizunguka nchi nzima ikiwa na waandishi waliorekodi kwa tepu, video na maandishi kwa ajili ya kuweka kumbukumbu katika mtandao wa Tume. (CHANZO: MWANANCHI) (FS
Share:

Chipukizi Mtanzania kwenda Barcelona


Nick Van Lawick (13 , ambaye ni chotara anayetokana na mzazi wa Kijerumani na Kitanzania, anasema akikua na kuwa mchezaji mkubwa kama anavyoota.
Siku zote katika maisha ni muhimu kuwa na utamaduni wa kuheshimu ndoto zetu hata kama tunadhani ni ndoto ndogo. Kuziheshimu ndoto zetu na kuzitimiza, kunahitaji nidhamu ya ziada, ingawa wapo wanaozifikia andoto zao kwa bahati.
Wengi husema wanataka kutimiza ndoto zao, lakini ni wachache hufanikiwa kutimiza ndoto zao. Hata hivyo kwa kuwa binadamu tuna ndoto tofauti tofauti ni ngumu kuwa na kanuni moja ya jinsi ya kufikia ndoto zetu.
Mtoto Nick Van Lawick (13), anayesoma shule ya kimataifa ya Dar es Salaam Independence School, ana ndoto ya kuichezea klabu ya Barcelona ya Hispania na anatarajia atatimiza ndoto hiyo.
Hiyo inatokana na kipaji alichonacho cha soka na mipango iliyofanywa na wazazi wake, ambao watamkutanisha Nick na mtaalamu wa viungo wa klabu ya Barcelona, Juanjo Brau.
Baba mzazi wa Nick anayeitwa Hugo van Lawick anasema: “Nick amepata nafasi ya kwenda kupewa mafunzo na Brau.
“Mama yangu Jane Goodall ni rafiki wa karibu wa Brau na mama yangu anafahamu kipaji cha mpira cha mjukuu wake, ndio maana aliona awasiliane na rafiki yake kuangalia nafasi ambayo Nick anaweza kujiendeleza zaidi kisoka.
“Brau alishauri kuwa Nick aanze kwa kumpa mafunzo ndipo mchakato wa kumtafutia nafasi katika timu ya vijana ya Barcelona ufanyike.”
Kwa upande wake Nick, anayesoma kidato cha pili, anasema anapenda sana mpira na muda wake mwingi huutumia katika mambo yahusuyo mpira huku akiipenda zaidi klabu ya Barcelona kwa sababu ya staili yao ya uchezaji.
Aota kuisaidia Tanzania
Nick (pichani), ambaye ni chotara anayetokana na mzazi wa Kijerumani na Kitanzania, anasema akikua na kuwa mchezaji mkubwa kama anavyoota, atatumia sehemu ya fedha atakazopata kusaidia mambo mbalimbali nchini, hasa hasa tatizo la umeme na kusaidia watoto walio kwenye mazingira magumu. (CHANZO: MWANANCHI) (FS)

Share:

BASI LAUA WATU 18 WAKIMSITIRI MAREHEMU

    Sumry4_ee1c9.jpg
WATU 18 wamekufa papo hapo wakiwemo askari Polisi wanne katika ajali ya barabarani, wakati basi linalomilikiwa na Kampuni ya Sumry, lilipopamia watu hao wakati wakimsitiri mtembea kwa miguu, aliyekufa kwa kugongwa na gari lisilofahamika.
Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Utaho, kilometa 20 nje ya Mji wa Singida katika Barabara Kuu ya Singida Dodoma.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Geofrey Kamwela, alisema jana kuwa mbali na askari hao, wengine waliokufa papo hapo ni viongozi watatu wa kijiji hicho na wananchi wanaowaongoza na wengine wanne ambao hawajatambulika.
Kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, askari waliokufa katika ajali hiyo ni Koplo Boniface Magubika, PC Jumanne Mwakihaba, PC Novatus Tarimo na PC Michael Mwakihaba na wote wanatoka katika kituo kimoja cha kazi.
Viongozi wa Kitongoji na Kijiji cha Utaho waliokufa ni Ramadhan Mjengi, ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji, Paul Hamis, ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji na Ernest Salanga ambaye ni Mwenyekiti Kitongoji.
Wananchi wanaowaongoza katika kijiji hicho waliokufa ni Saidi Rajabu, Ushirika Itambu, Chima Mughenyi, Salim Juma, Abeid Ramadhan, Mwinyi Hamis na Issaha Hussein.
Kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, miili ya watu wengine wanne haikuwa rahisi kutambulika mara moja na wote wamehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa mjini Singida.
Kamanda Kamwela alisema ajali hiyo ilisababishwa na basi la abiria lenye usajili namba T.799 BET aina ya Nissan, mali ya Kampuni hiyo ya Sumry, inayomilikiwa na Mohamed Abdallah wa Sumbawanga, lililokuwa likienda jijini Dar es Salaam likitokea Kigoma.
Alisema kuwa basi hilo lililokuwa likiendeshwa na Paul Njilo, mkazi wa Dar es Salaam, liliwagonga waenda kwa miguu hao waliokuwa wamekusanyika kando ya barabara wakisaidiana na askari Polisi kuondoa mwili wa marehemu Gerald Zephania, aliyekuwa amegongwa na lori lisilofahamika juzi saa moja usiku.
Katika ajali hiyo kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, watu wengine wanane walijeruhiwa na wamelazwa katika Hospitali ya Misheni Puma ya mjini Singida.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kilichosababisha ajali hiyo huenda ni kuegeshwa vibaya kwa gari la Polisi, wakati likipakia mwili wa marehemu Gerald, aliyekuwa amegongwa na lori mapema kabla ya basi hilo kufika hapo. Inadaiwa gari la Polisi liliziba barabara.
Akizungumzia ajali hiyo katika Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam jana, Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, alitoa pole kwa wananchi wote waliofiwa na ndugu zao na kuwaombea majeruhi kupona haraka.
Alisema Askari wa Usalama Barabarani hawatakuwa na muhali na dereva yeyote atakayekwenda kinyume na Sheria ya Usalama Barabarani. Kutokana na hilo, ametoa mwito kwa madereva kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarni, ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.
“Polisi iko imara kuchukua hatua zozote za kisheria, kwani kuna baadhi ya watoa huduma wa usafiri hugoma pale wanapotaka kuchukuliwa hatua kwa sababu mbalimbali matokeo yake ni uvunjaji wa sheria kwa makusudi,” alisema.
Alisema Jeshi la Polisi limeanzisha msako mkali wa dereva wa basi hilo ambaye alitoroka ili kufikishwa mahakamani, na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu wa aina yeyote ile, ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani. Imeandikwa na Abby Nkungu, Singida na Theopista Nsanzugwanko, Dar (CHANZO: HABARILEO) (FS)
Share:

Tuesday 29 April 2014

ARSENAL WAZIDI KUJIKITA TOP 4, WAIZAMISHA NEWCASTLE 3-0


Arsenal wakishangilia ushindi wao usiku huu.
Bao la kwanza la Arsenal likifungwa na Laurent Koscielny dakika ya 26.
Mesut Ozil akiifungia Arsenal bao la pili dakika ya 42.
Olivier Giroud akihitimisha kwa bao la nne dakika ya 66.
Newcastle baada ya kipigo cha 3-0.
Mashabiki wa Newcastle wakiwa na bango la kumkataa kocha wao, Alan Scott Pardew.
WASHIKA bunduki wa London, Arsenal FC wamezidi kujihakikishia kubaki Nne Bora kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuibamiza bao 3-0 Newcastle usiku huu kwenye Uwanja wa Emirates jijini London.
Mabao ya Arsenal yamewekwa kimiani na Laurent Koscielny, Mesut Ozil and Olivier Giroud.
Kwa matokeo ya leo, Arsenal wamefikisha pointi 73 baada ya kucheza mechi 36 wakiwa nafasi ya nne huku anayewafuatia kwa nyuma Everton akiwa na pointi 69 baada ya mechi 36 wote wakibakiwa na mechi mbili mkononi.
Share:

UKAWA KUSIMAMISHA MGOMBEA URAIS 2015


Viongozi wanaounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKawa). Kutoka kushoto, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu. Viongozi hao wapo katika mkakati wa kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. 
Dar es Salaam.
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimeanza maandalizi ya kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais, gazeti hili limebaini.
Kadhalika, vyama hivyo ambavyo ni Chadema, NCCR Mageuzi na CUF vinakusudia kuwa na mgombea mmoja wa nafasi za wabunge na madiwani, ikiwa ni hatua ya kuzikabili nguvu za chama tawala, CCM.
Habari zilizolifikia gazeti hili zinasema tayari viongozi wakuu wa vyama hivyo wamekubaliana kuanza mchakato huo na wameandika mapendekezo na kuyapeleka katika sekretarieti za vyama vyao kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi.
Chanzo chetu kilidokeza kuwa kamati ya wataalamu kutoka vyama hivyo tayari imeundwa ili kuandaa taratibu zitakazotumika katika kufanikisha mkakati huo.
Wenyeviti wa vyama hivyo walipoulizwa kwa nyakati tofauti kuhusu mpango huo hawakukubali moja kwa moja, badala yake walisema ni mapema mno kuzungumzia suala hilo katika vyombo vya habari.
Ukawa ni umoja ambao uliviunganisha vyama vyenye malengo yanayofanana katika Bunge Maalumu la Katiba na vimekuwa vikishinikiza kuzingatiwa kwa mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba hususan muundo wa Muungano wenye serikali tatu, tofauti na serikali mbili za sasa.
Umoja huo pia uliwaongoza wajumbe wa Bunge Maalumu ambao ni wanachama wake kutoka nje kususia mchakato wa Katiba Mpya kutokana na kile walichodai kuwa ni kutokuridhishwa na jinsi mambo yanavyokwenda.

Taarifa za kuwapo kwa mpango wa kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu ujao, zimekuja siku chache tangu kufichuliwa kwa mpango mwingine wa kuundwa upya kwa Baraza la Mawaziri kivuli ambalo litawajumuisha wabunge wa vyama hivyo katika Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Baraza la kivuli la sasa linawajumuisha wabunge kutoka Chadema pekee, ambacho kinaunda Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni tangu kuanza kwa Bunge la 10, Novemba 2010.

Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema atapanga upya baraza lake katika siku za mwanzo za Bunge la Bajeti, linalotarajiwa kuanza Mei 6, mwaka huu mpango ambao umeungwa mkono na wenyeviti wa CUF na NCCR Mageuzi.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema uamuzi huo ni hatua kubwa katika ushirikiano na kwamba tayari alikwishawaarifu wabunge wa chama chake wawe tayari kushiriki katika baraza hilo.

Wenyeviti wa vyama

Mbowe alisema: “Hivi sasa suala la sisi kuungana kwa maana ya kuwa na nguvu ya pamoja halikwepeki. Siasa ni dynamic (zinabadilika), fikra za jana ni tofauti na fikra za leo kwa hiyo ni ukweli usiopingika kwamba sisi wapinzani tunahitajiana kwa manufaa ya watu wetu na nchi yetu.”

Hata hivyo, alisema ni mapema kuzungumzia uwezekano wa ushirikiano wao katika vyombo vya habari na kwamba wakati ukifika kila kitu kitawekwa wazi.

Kwa upande wake Profesa Lipumba alisema: “Ningefurahi kama tungeweza kufikia kiwango hicho cha ushirikiano maana kama unavyoona hatuwezi kusonga tusiposhikamana na kuwa wamoja, lakini hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa maana muda mwafaka bado.”

Aliongeza: “Ni kweli Katiba imetuunganisha na huu ni mwanzo mzuri ambao unaweza kutoa mwanga kwamba huko mbele tutakwenda vipi, tumeona kwamba Serikali haina nia njema kwenye suala hili la Katiba, hivyo tukiendelea kutengana hatutaweza kuukabili udhalimu huu.”

Alipoulizwa wataweza kushirikiana vipi na Chadema hali CUF wakiwa washirika wa CCM katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar, Profesa Lipumba alisema mazingira yaliyowafanya kuingia katika ubia huo yanafahamika kwani ulikuwa ni uamuzi wa Wazanzibari kupitia kura ya maoni.

“Kuwamo katika SUK siyo tatizo kwa sasa, siku zilizopita wenzetu walikuwa hawajatuelewa lakini sasa nadhani tunakubaliana kwamba kuwamo kwenye Serikali huko Visiwani siyo kikwazo tena cha kushirikiana na wenzetu,” alisema.

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alisema muungano wa vyama hivyo kupitia Ukawa limekuwa darasa kwa viongozi wakuu wa vyama husika kutafakari walikotoka, walipo na wanakokwenda. Hata hivyo, alisema ni mapema sana kuzungumzia suala la kuungana kwao hadharani.

“Tunapata nafasi ya kutafakari na kujifunza kwa kurejea tulikotoka kwa mfano hebu tuifikirie NCCR Mageuzi ya 1995 na ya sasa, CUF ya 2000 na 2005 na CUF ya leo na Chadema ya miaka iliyopita na Chadema ya sasa, haya yote yanatupa fursa ya kutafakari kwa kina tunakotaka kuupeleka upinzani katika nchi yetu,” alisema Mbatia na kuongeza:

“Kwa hiyo suala la kuungana siyo la kujadili kwa sababu ndiyo mahitaji ya sasa, mjadala pengine ni kwamba tunaungana vipi, katika maeneo gani na kwa madhumuni gani?”

Alisema katika siasa, chochote kinaweza kutokea na kwamba mfano mzuri ni Kenya... “Hakuna aliyekuwa akiwaza kwamba leo Rutto (William) angekuwa Makamu wa Kenyatta (Uhuru) kwenye Serikali ya Kenya,” alisema.
Share:

KANGA MOKO KUCHEZA SHOW WAKIWA WATUPU NI KITU CHA KAWAIDA,CHEKI HAPA


Toka umeingia huu mtindo wa lile kundi la khanga moko siku hizi kamezuka kamtindo ka wacheza show za jukwaani nao kuvaa khanga na kuonesha sehemu kubwa
za maongo yao ikiwemo kufuli walizo vaaa...Hii ni laana ya khanga moko inazidi kutafuna tasnia ya sanaaaaa ...
Share:

UKAWA MOTO MKALI RATIBA YA MIKUTANO NA MAANDAMANO HII HAPA



Wana jamvi kuna mdau amenirushia ratiba ya ukawa mikutano na maandano nchi nzima kuanzia tarehe april 30-mei 4 kama ifuatavyo; dr slaa,mtatiro na prof safari watakua dodoma na pwani;maalim seif shariff hamad na mabere marando watakua mbeya;kabwe zitto na chiku abwao kilimanjaro,tindu lissu na lipumba mwanza,kagera.simiyu;pemba na unguja mbowe,anna komu na habibu mnyaa;tabora- kigoma;jussa na wenje;dar sugu na lema;tanga mdee na machemli;shinyanga;mnyika,shib uda na nassari;singida v-nyerere na opolukwa; taarifa zaidi zitatolewa kadri zitakavyo patikana kupitia njia zote
Share:

PICHA ZINATISHA TAFADHALI: MWIZI AUAWA NA KUCHOMWA MOTO MBAGALA KWA TUHUMA ZA WIZI



Kijana Mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja Ameuawa kwa Tuhuma za Wizi Huko mbagala mtaa wa kwa Mwarabu.
Wananchi wameendelea Kujichukulia sheria Mkononi .
Wananchi wa eneo la mbagala kwa mwarabu wamefanikiwa kumuuua mwizi kwa kumchoma moto kwa tuhuma za wizi...Taarifa zaidi itawajia
Share:

POLISI WA KIKE ANAYEDAIWA KUIBA MTOTO, HUYU HAPA!



SIKU chache baada ya kukamatwa kwa askari wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 na picha yake kudaiwa ‘kuminyiwa’ na askari wenzake ili isionekane, hatimaye Ijumaa Wikienda limeinasa.
Mwanamama ambaye ni askari wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 anayedaiwa kuiba mtoto wa jinsia ya kiume aliyefahamika kwa jina la Goodluck Salehe (siku 7).
Askari huyo ambaye kituo chake ni Ilala jijini Dar, alikamatwa kwa tuhuma za wizi wa mtoto jinsi ya kiume aliyefahamika kwa jina la Goodluck Salehe (siku 7) aliyeibwa April 6, mwaka huu huko Kasumulu Kata ya Itope Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.
Ilielezwa kuwa, mtuhumiwa alishirikiana na baba mzazi aliyefahamika kwa jina la Salehe Issah Mwangosi(31) mkazi wa Matankini Kyela aliyemtambulisha kwa mama mzazi (Mboka Mwakikagile umri miaka 20) kuwa Prisca ni shangazi yake hivyo amekwenda kumwona mtoto aliyezaliwa ndipo akatoroka naye.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ahmed Msangi.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa Aprili 17, mwaka huu huko eneo la Meta Jijini Mbeya majira ya saa nne asubuhi akiwa na mtoto huyo mkononi ambapo alitiwa nguvuni na kufikishwa Makao Makuu ya Polisi Mkoa Forest ya Zamani kwa mahojiano zaidi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, siku hiyo mama huyo alikuwa katika harakati za kutokomea kusikojulikana lakini bahati nzuri polisi waliimarisha ulinzi.
“Alikuwa ndiyo yupo katika mikakati ya kutoroka na haikujulikana alikuwa anataka kwenda wapi maana tayari alishajua kuwa anatafutwa hivyo kutapatapa na kuingia kirahisi katika mkono wa sheria,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuhojiwa na polisi kujiridhisha na tuhuma hizo za wizi, mstakiwa huyo alipandishwa katika mahakama ya…na kusomewa mashtaka yanayomkabili.
Baada ya kusomewa mashtaka siku hiyo, kesi iliahirishwa hadi Mei 6, mwaka huu ambapo mshtakiwa aliruhusiwa kupata dhamana lakini akashindwa kutimiza masharti (wadhamini wawili na hati) hivyo kurudishwa sero hadi kesi hiyo itakapotajwa tena.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kabla ya kunaswa katika tukio hilo, askari huyo anayedaiwa kuwa ni mama wa watoto, aliolewa na kuachika miaka kadhaa iliyopita.
Share:

MWANAFUNZI WA KIKE AMEKUTWA AMEKUFA CHUMBANI KWA HAWARA YAKE


MSICHANA Atu Gabriel mwenye umri wa miaka 20,  mwanafunzi wa Chuo cha Eden Hill kilichopo Kwamfipa wilayani Kibaha mkoani Pwani, amekutwa amekufa chumbani kwa mtu anayetajwa kuwa ni hawara yake, Hafidh Mohammed.
Mwili wa Atu ukiwa chumbani kwa mtu anayesadikika kuwa ni mpenzi wake, Hafidh Mohammed.
Tukio hilo lilitokea April 26, mwaka huu na kukusanya umati huku mwanaume aliyelala na binti huyo akitokomea kusikojulikana.Marehemu anadaiwa kuwa mwenyeji wa Makambako mkoani Njombe.
Akizungumza na waandishi wetu juzi Kibaha, mama wa Hafidh ambaye pia ni mjumbe wa eneo hilo, Zainabu Saidi alisema mwanaye alimweleza kutokea kwa tukio hilo asubuhi kulipokucha na kabla ya hapo, hakuwa akifahamu kama alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana huyo kwa vile aliyekuwa akimfahamu ni mwanamke mwingine ambaye alizaa naye.
“Mimi kwa kweli sikuwa na taarifa yoyote juu ya uhusiano wao na huyu  mwanafunzi, nimeletewa taarifa asubuhi na kijana wangu huku akionekana kuchanganyikiwa, nimejaribu kumsihi asikimbie lakini imeshindikana,” alisema mama huyo.
Mwili wa Atu ukiingizwa kwenye gari la polisi.
ALIVYOAGA CHUONI
Wanafunzi wa chuo hicho kinachofundisha masomo ya biashara na habari ambao walikataa kutaja majina yao waliliambia gazeti hili kuwa, marehemu Atu aliwaaga anakwenda jijini Dar es Salaam kumuuguza wifi yake aliyelazwa katika Hospitali ya Amana, Aprili 23, mwaka huu.
Hata hivyo, walisema uondokaji wake uliwapa maswali mengi kwani tofauti na walivyotegemea kuwa angebeba mfuko mkubwa wenye nguo za kubadili, yeye aliondoka akiwa na mkoba wake wa mkononi pekee hali iliyoonesha hakuwa akienda mbali.
Walisema siku tatu baadaye walipatwa na mshtuko mkubwa baada ya mlinzi wa hosteli yao kuwaletea taarifa za kifo cha mwenzao kilichotokea katika chumba cha mvulana huyo anayeishi jirani.
MAJIRANI NAO WANENA
Majirani waliozungumza na gazeti hili walisema kwao haikuwa mara ya kwanza kumuona msichana huyo, kwani mara kwa mara alikuwa akifika pale ingawa akishaingia ndani hakuwa akitoka nje.
Walisema mara zote hizo, mwanaume huyo mwenyeji ndiye alikuwa akitoka nje na kwenda kumnunulia chakula.
Wananchi na wanausalama wakiwa eneo la tukio.
POLISI WAUPELEKA MWILI HOSPITALI YA TUMBI
Jeshi la polisi liliwasili eneo la tukio na kuukuta mwili huo ukiwa umelala kitandani ukiwa hauna jeraha, lakini pembeni yake kulikutwa vidonge ambavyo havikufahamika ni vya aina gani ambavyo pia vilichukuliwa pamoja na mkoba wake hadi kituonis.
Minong’ono kutoka kwa majirani kuhusiana na vidonge hivyo ilitofautiana,  baadhi yao walisema huenda vilitumika katika jaribio la kutoa mimba, wengine walisema inawezekana msichana huyo alipata ugonjwa wa ghafla usiku na mwanaume huyo alikwenda kumchukulia vidonge hivyo ambavyo havikuweza kumsaidia marehemu kupata nafuu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,  SACP Ulrrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema juhudi za kumtafuta mwanaume huyo zinaendelea huku madaktari nao wakiendelea na uchunguzi wao ili kubaini chanzo cha kifo hicho.
Share:

UNGA WAZIDI KUMTESA RAY C


Rehema Chalamila ‘Ray C’ katika pozi.
MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye aliwahi kuathirika na utumiaji wa ‘unga’, hivi karibuni alitinga ofisi ya kitengo cha kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya na kuomba kupatiwa majina, idadi na sehemu walipo watumiaji wa mihadarati hiyo ili aweze kuwasaidia kwa kuwapa somo, kitu kinachotafsiriwa kama bado unamtesa.
Ray C katika harakati zake akifanya mahojiano na msanii wa Hip hop, ambaye yupo mbioni kuachana na madawa ya kulevya, Ibra the Hustler.
Ray C anadaiwa kufika katika ofisi hizo, Aprili Mosi, mwaka huu, saa nne asubuhi hali iliyozua gumzo kwa askari waliomuona ambao walijiuliza kitu alichokifuata.
Akizungumza na Uwazi, kamanda wa kitengo hicho cha madawa ya kulevya, Godfrey Nzowa alikiri kufika kwa msanii huyo ofisini kwake na kutoa madai hayo lakini alimwelekeza kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwani huko kuna kitengo kinachoshughulika na watu wenye matatizo ya akili wakiwemo watumiaji wa madawa ya kulevya.
Ray C.
Kamanda huyo alionesha kufurahishwa na kitendo cha msanii huyo ambaye pia anamiliki taasisi yake yenye lengo la kuwasaidia waathirika wa matumizi ya madawa hayo kwa kuwapa elimu, akisema atatoa msaada mkubwa kwa wenzake.
Aliwataka watumiaji wa madawa hayo ambao wameshindwa kuacha, wamfuate msanii huyo ili awape elimu na amewaonya wote wanaotumia na kusafirisha madawa hayo.
“Wote wanaotumia na kuuza madawa hayo waache mara moja kwani kikosi kazi kinachopambana na biashara hiyo kimejipanga kila kona ili kukomesha biashara hiyo haramu,” alisema Kamanda Nzowa
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger