Sunday, 9 July 2023

WADAU WAKARIBISHWA KUPATA TAARIFA NAMNA YA KUSHIRIKI JUKWAA LA KIMATAIFA SEKTA YA MADINI MWEZI OKTOBA 2023

...

Wananchi na wadau wanaotembelea maonesho ya Sabasaba wamekaribishwa kupata taarifa kuhusu namna ya kushiriki katika Jukwaa la Kimataifa la Sekta ya Madini kwa kujisajili katika tovuti maalum ya mkutano.

Mratibu wa Jukwaa la Mkutano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Madini Bi. Jacqueline Aloyce  amesema kuwa , jukwaa hilo linatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi Oktoba 25 na 26 jijini Dar es salaam.

Amezungumza hayo leo Julai 9, 2023 na kuongeza jukwa hilo litakuwa fursa kwa wenye nia ya kushiriki katika uchumi wa madini, kujifunza, kusikia na kukutana na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini wanaotembelea banda la Wizara ya Madini katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Dar es salaam.

Ameongeza kuwa, jukwaa hilo ni fursa kwa wote walio katika mnyororo  mzima wa shughuli za madini kuanzia wachimbaji wadogo, wa Kati na Wakubwa wa Sekta ya Madini ili kuzungumza kwa pamoja fursa mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Madini.

Ameongeza kuwa, ili kushiriki katika jukwaa hilo muhimu wadau wote wajisajili katika tovuti ya mkutano huo https://www.tanzaniamininginvestmentforum.com

Kwa nwaka 2023, Jukwaa la Kimataifa Sekta ya Madini inashirikiana na Kampuni ya DMG events na Ocean Business Partners (OBP) katika kuandaa jukwaa  la Kimataifa kwenye Sekta ya Madini hapa nchini.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger