Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Muleba, Bw. Muhaji Bushako
****
Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera wametakiwa kuepuka kutumiwa na wanasiasa kwenye maeneo yao ili kuepusha kuwepo kwa matabaka kwenye jumuiya hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Muleba, Bw. Muhaji Bushako amesema hayo kwenye kikao cha baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi cha Wilaya cha kikanuni kwa mwezi wa sita ambapo amesema kuwa vijana wanao wajibu wa kuhakikisha wanajisimamia wenyewe.
Bushako amesema wapo baadhi ya vijana wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa kwenye maeneo yao na kusababisha kuwepo kwa matabaka hivyo wanalo jukumu la kuhakikisha wanajisimamia na kuwa kitu kimoja kwani jumuiya hiyo ni tanuru ya uongozi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Muleba Bwana Geofrey Kamili amewataka vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwenye maeneo yao ambao unatarajia kufanyika hapo mwakani kwani jukumu la kuwa kiongozi sio la watu wazima pekee.
Nao baadhi ya wajumbe wa balaza hilo la Vijana ambao ni Minath Mickdard na Muksini Mohamed wamesema kuwa kitendo cha kutumika ki siasa kina athiri maendeleo ya jumuiya hiyo ambapo watahakikisha wanakuwa wamoja na kuondoa matabaka kwenye jumuiya hiyo.
Aidha katika kikao hicho wajumbe walimpitisha katibu hamasa wa Jumuiya ya vijana CCM wilaya ya Muleba Mohamed Isumail Rwabakoba.
Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Muleba, Bw. Muhaji Bushako
0 comments:
Post a Comment