Thursday, 27 April 2023

WADAU MBALIMBALI WATEMBELEA BANDA LA NACTVET KWENYE MAONESHO YA WIKI YA UBUNIFU

...
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), linashiriki katika maonesho ya wiki ya ubunifu yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.

 Maonesho hayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na yanatarajiwa kudumu kwa siku tano, kuanzia tarehe 24 hadi 28 Aprili 2023.

Lengo la ushiriki wa NACTVET katika maonesho hayo ni kukutana na wadau mbalimbali ili kutoa elimu kuhusu majukumu ya Baraza na kutoa ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali yanayosimamiwa na kutekelezwa na Baraza.

Akizungumza katika maonesho hayo, Afisa Habari na Uhusiano wa Baraza , Bi. Casiana Mwanyika, amesema kuwa ushiriki wa NACTVET katika maonesho hayo ni muhimu ili kuwawezesha wadau kufahamu shughuli za Baraza na kujenga uelewa kwa wananchi.

 Hivyo basi, amewakaribisha wadau na wananchi kwa ujumla kutembelea banda la NACTVET ili kupata taarifa mbalimbali zinazofanywa na Baraza, ikiwemo kusimamia ubora wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu akiweka saini alipotembelea banda la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), katika Maonesho ya Wiki ya Ubunifu yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.
Afisa Uhusiano wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Casiana Mwanyika akiwa na mdau katika Maonesho ya Wiki ya Ubunifu yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.
Wadau mbalimbali wakipata maelezo mara baada ya kutembelea banda la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), katika Maonesho ya Wiki ya Ubunifu yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi walipotembelea banda la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), katika Maonesho ya Wiki ya Ubunifu yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger