Saturday, 22 April 2023

USHOGA,USAGAJI NA ULAWITI VYAPINGWA KILA KONA

...
 
sheikhe wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajab.

Na Dotto Kwilasa,DODOMA.

SHEKHE wa mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu amewataka watanzania kukemea na kupinga vitendo vya ushoga, ndoa za jinsia moja, ulawiti pamoja na usagaji.

Amesema ni  jukumu la kila Mtanzania kukemea mambo mabaya na kuhamasisha matendo mema na kwamba jamii inapaswa kusimama pamoja kama taifa kuhakikisha kuwa mambo haya ya hovyo yanatoweka.

Ameyasema hayo mapema leo jijini hapa kwenye ibada ya swala ya Eid el Fitri, iliyofanyika katika msikiti wa Gadafi ambapo amesema vita hiyo ni ya wote na si viongozi wa dini na Serikali pekee.

Shekhe Mustapha pia amesema "Jamii iachane na woga wa kutokemea mambo haya ya hovyo ambayo mataiafa ya nje wanataka kutuletea tunayapinga kwakuwa ni kinyume na mila na desturi zetu”amesema 

Amesisitiza kuwa pamoja na kuwa mambo hayo ni kunyume na mila za kitanzania pia ni kinyume na maagizo ya Mungu kwa mwanaume kumuoa mwanaume mwenzake au mwanamke kuwa na mahusiano hayo na mwanamke mwingine.

Ametumia nafasi hiyo pia kuwataka Watanzania kuacha tabia ya kupokea kila kitu kinachoingizwa nchini na mataifa mengine kwakuwa hali hiyo inaweza kusababisha kuongozeka kwa vitendo vya mmomonyoko wa maadili.

“Mmomonyoko wa maadili hivi sasa umekithiri nchini kutokana na kuiga mambo ambayo siyo mila zetu hali hiyo inasababisha kuongezeka kwa vitendo vya maasi ikiwemo baba kurawiti watoto wao wa kuwazaa,wanandoa kuuana pamoja na mauaji katika jamii zetu”amesema

Sheikh huyo pia amepongeza hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan, makamu wa Rais Dk. Philp Mpango na waziri mkuu Kassim Majaliwa kwa kusimama imara kueleza hisia zao waziwazi za kupinga vitendo hivyo vya ushoga na ndoa za jinsia moja nchini.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger