Wednesday 22 March 2023

UGANDA YAONESHA NIA UWEKEZAJI MIRADI YA UMEME NCHINI

...

 



Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba (nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Col Mwesigye Fred (wa tatu kulia), Katibu Mkuu Wizaya ya Nishati, Athumani Mbuttuka( wa tatu kushoto), Kamishna Msaidizi Maendeleo ya umeme, Mhandisi Styden Rwebangila(kushoto) na wawekezaji kutoka Uganda kuhusu kuwekeza katika mradi wa umeme, Machi 21, 2023.u
 

 Na Zuena Msuya, Dodoma

Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Tanzania pamoja na wawekezaji kutoka nchini humo kuhusu kuwekeza katika mradi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Lindi, Masasi, Tunduru na Songea.

Mazungumzo hayo yamefanyika Machi 21, 2023 katika ofisi za Wizara ya Nishati mkoani Dodoma na kuwashirikisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka, Kamishna Msaidizi Maendeleo ya umeme, Mhandisi Styden Rwebangila na wawekezaji kutoka Uganda.

Wawekezaji hao wamemueleza Makamba kuwa wanataka kuwekeza katika mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa Msongo mkubwa wa Kilovolti 400 wenye urefu wa Kilometa 222.3 kutoka Lindi, Masasi hadi Songea.

Wawekezaji hao watawekeza kwa kusanifu, kutafuta fedha, kujenga na kuendesha njia hiyo na kuikabidhi baada ya muda uliopangwa.

Hata hivyo Makamba ameridhia wawekezaji hao kuwekeza katika mradi huo na kusema kuwa huo ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele kwa taifa.

Vilevile amewaagiza wawekezaji hao kutana na Shirika la Umeme nchini Tanzania na maafisa wa Wizara ya Nishati ili kujadiliana na kuona njia bora ya kutekeleza katika mradi huo kwa kuangalia sheria, taratibu na kanuni za uwekezaji katika miradi ya umeme.

Aidha Wawekezaji hao pia wameonyesha nia ya kutaka kuwekeza katika mradi wa umeme wa jua katika Kisiwa cha Mafia wenye megawati 5 kwa gharama ya Dola za Kimarekani 11.64.

Hata hivyo Waziri aliwaeleza wawekazaji hao kuwa serikali imeshapa kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 5 kutoka Wakala wa Maendeleo wa Ufaransa (AFD) na kwamba iko katika mazungumzo ya AFD kuongeza fedha Zaidi.

Kwa upande wake Balozi wa Uganda nchini Tanzani, Col. Mwesigye Fred ameishukuru Serikali ya Tanzania, kwa kukubali wawekezaji kutoka nchi Uganda kuwekeza katika miradi ya umeme.

Amesema hayo ni matokeo ya ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo mbili ulioasisi na viongozi wakuu.

 




Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba(kulia) akiwa mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Col Mwesigye fred (kushoto) na wawekezaji kutoka Uganda 
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger