Familia moja kutoka kijiji cha Bomeroka huko Kitutu Chache kaunti ya Kisii nchini Kenya inaomboleza ajuza aliyeuawa na mwanawe.
Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 34, anayesemekana kuwa mraibu wa dawa za kulevya, aliripotiwa kupandwa na mori baada ya kuhisi kuwa kiasi cha chakula alichotengwa kilikuwa kidogo.
Kulingana na mfanyakazi wa shambani wa nyumba hiyo, mshukiwa alitaka kula chakula chote cha mchana ambacho kilikuwa kimetayarishwa kwa ajili ya familia nzima.
Marehemu alipomsihi asichukue chakula chote, alinyakua panga na kumrukia mara moja akamkata mkono.
“Alitaka kuchukua chakula chote mamake alipomtaka awafikirie ndugu zake ambao walikuwa bado hawajala, alipandwa na mori na hapo mara moja akamjeruhi vibaya kwa panga,” alisema mfanyakazi huyo.
Mwanamke huyo alikata roho kutokana na kuvuja damu nyingi akikimbizwa hospitalini.
Chanzo: TUKO.co.ke
0 comments:
Post a Comment