Wednesday 26 October 2022

WATANZANIA MISS NA MISTER DEAF WAPO TAYARI KWA SHINDANO LA DUNIA LA UTANASHATI NA UREMBO

...

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mchakato wa kumpata Mshindi wa Mashindano ya Wanamitindo na walimbwende wa Dunia umeanza ambao Watanzania wametoa ahadi ya kubakiza ushindi Nyumbani.

Akizungumza kuelekea Shindano hilo ambalo linatarajia kufanyika Oktoba 29,2022 Jijini Dar es Salaam, Mlimbwende Khadija Rajabu amesema wamejipanga ipasavyo licha ya kuwepo kwa changamoto ndogondogo lakini imani yao ni kushinda na kubakisha taji nchini.

Aidha amesema amejipanga vizuri na anaamini ataipeperusha vizuri bendera ya Tanzania katika Mashindano hayo ya dunia.

Kwa upande wa washiriki wengine kutoka mataifa mengine wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa mashindano hayo kuwa huru.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger